Ufunuo 5:1-5 Biblia inasema hivi “1. Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. 2. Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? 3. Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 4. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 5. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba”
Mungu ni wa ajabu sana nilipokuwa
najisomea Biblia na kufika katika Mstari wa tano nikayaona maneno hayo Simba aliye wa Kabila la Yuda! Maneno hayo yalinishangaza sana ni wazi kuwa
Simba anayetajwa hapo ni Yesu Kristo hilo halina mjadala, ni wazi kuwa Yesu ni Masihi na masihi alikuja
kupitia ukoo wa Yuda hilo pia halina mjadala, Daudi pia alitokea ukoo huu wa
kabila la Yuda hilo halikuwa na mjadala, Jambo kubwa lililovuta hisia kwangu ni
kutajwa kwa Yuda mwenyewe hapa ndipo penye mjadala
Yuda wanaotajwa katika biblia
wanaweza kuwa wengi, lakini walio maarufu ni watatu 1. Ni Yuda Iskariote
umaarufu wake umekuja kutokana na tendo lake la kumsaliti Bwana Yesu, 2 Yuda
ndugu yake Yakobo hawa ndi ndugu wa kunyonya wa Yesu Kristo na waandishi wa
nyaraka za Yakobo na ule waraka wa Yuda, hawa wako katika agano jipya, Yuda
anayetajwa akiunganishwa na Masihi ni Yuda wa agano la Kale huyu ni mtu wa
namna gani?
Yuda alikuwa miongoni mwa watoto
wa kiume wa Israel au Yakobo, alipata umaarufu sana kuliko ndugu zake, Kabla
kidogo ya kuondoka ulimwenguni Yakobo ambaye ndiye Israel alitoa unabii kuhusu
maswala ya maisha ya wanae ya baadaye, alimtabiria mema sana Yuda Mwanzo
49:8-12 moja ya maswala hayo muhimu ni kuja kwa Masihi kupitia kabila la Yuda
Yakobo alikuwa na wana 12 lakini
swali la kujiuliza kwa nini Yuda awe maarufuna wa muhimu labda zaidi kuliko
wengine? Kwa nini ni kama amebarikiwa zaidi, kwa nini aunganishwe na ubaba wa
kuja kwa Masihi kwa nini Yesu aitwe SIMBA ALIYE WA KABILA LA YUDA? Ni lazima
kuna maswala ya kujifunza kumhusu Yuda
Ni wazi kuwa tunaelewa kuwa Mungu
alinmtumia Yuda kutimiza mpango wake, Mungu katika hekima yake iliyo ya ajabu
kuliko ya wanadamu, huwatumia wanadamu kwa makusudi yake na kwa neema yake na
rehema, “1Koritho 1:26-29” si lazima uwe maalumu sana au utoke katika ukoo muhimu
sana au uwe na tabia maalumu sana ndipo Mungu akutumie Hapana ! unapomchunguza
Yuda utagundua ni kwa neema na rehema na wala si kwa matendo tunastahili Baraka
za Mungu
Matatizo ya Yuda
Mwanzo 37:26 Yuda alihusika kwa
kiwango kikubwa pia katika miakakati na mipango ya kumuuza Yusufu ndugu yake,
ilikuwa ni kama ana huruma na ujanja wa kumuokoa Yusufu asiuawe, lakini Bado
anawajibika kwa mkiwango kikubwa katika uovu wa kumuuza ndugu yake wa Damu awe
mtumwa.
Mwanzo 37:31-35 Yuda na ndugu
zake, wakiwa wamejikausha walishiriki wazi katika kusema uongo kwa baba yao
kuhusu Yusufu, kumbuka wote walikubaliana waseme ameliwa na mnyama
mkali,kumbuka zilikuwa ni habari za msiba wa kuumiza kwa Israel Baba yao, Yuda
alishiriki utayari wa kumuaminisha Israel kuwa mwanae amekufa na kunyamaza na
uongo huo kwa miaka zaidi ya 13, huku mzee akilalamika kupoteza mwana mpendwa,
Kama amri ya kuwaheshimu wazazi ili upate heri na miaka mingi duniani Yuda
alikuwa amaeharibu tayari
Mwanzo 38:1 Yuda huyuhuyu
ulipofika wakati wa kuoa, Yeye aliamua kuoa mwanamke mkanaani , hii ilikuwa
kinyume na tamaduni za Israel na Isaka na hata Ibrahimu, wote wliona umuhimu wa
kuoa kwao lakini yeye hakuona umuhimu huo kwake mwanamke ni mwanamke tu alioa
mkanaani
Mwanzo 38:7-10 Yuda kupitia
mwanamke huyu mkanaani alipata watoto, wa kiume, lakini wawili kati yao mungu
aliwaua mapema kwa sababu walikuwa waovu mbele za Bwana bila shaka unakumbuka
Eri na Onani, Unadhani nani anawajibika
na uovu wa watoto hao? Utasema ni mwanamke mkanaani sawa lakini nani aliyemuoa?
Na wanapouawa wanao unaowategemea nani anapitia uchungu?
Mwanzo 38:12-16 Yuda alikuwa ni
mtu aliyeshindwa kuutawala mwili, aliongozwa na tamaa ya mwili, alifiwa na
mkewe sawa , lakini anakwenda njiani anaona mwanamke kahaba anaingia kwake
akifikiri ni kahaba, hakuwa na muda wala hata umakini wa kuangalia mwanamke
huyo ni nani alitimiza tamaa yake na kuondoka zake
Mwanzo 38:24-30 Yuda alukuwa na
moyo wa Kuhukumu, angalia kuwa analipogundua mkwewe Tamari ana mimba, hata
pamoja na kuwa ndiye aliyemwekea mtego kwa kujifanya kahaba kwa sababu hakumpa
haki zake, Yuda anawajibika kwa matendo yake ya hukumu akiamuru apigwe kwa mawe
huku akiwa amesahau kuwa na Yeye ni mzinifu tu, ashukuriwe Mungu kuwa Tamari
alimtaja mtu aliyempa mimba na kuonyesha ushahidi, na kupitia uhusiano huu wa
kijinga na wa aibu kunazaliwa Mapacha na
mmoja anaingia katika mstari wa kutuletea Masihi Mathayo 1:3
Unamwangaliaje Yuda? Je ni kama
asiyefaa kabisa kutumiwa na Mungu? Angelikuweko leo katika makanisa yanayojiita
ya kiroho angetengwa na kufungwa kwa siku kadhaa, au anagefukuzwa kanisani na
maadiko yangetumika kuwa hizi ni nyakati za agano jipya ni tofauti na zamani za
ujinga? Na ingesahaulika kuwa mwanadamu ni yuleyule kihistoria, Ukweli kwa
Mungu unabaki palepale Mungu alikuwa ana mpango naye, Mungu alikuwa
anashughulika naye amfanye kuwa Baraka kwa wengine Mwanzo 49:8-12
Yuda alikuwa kama pande la Mti
usiofaa na Mungu alikuwa na Mpango wa kuuchonga ufae kwa kazi zake, Kama ni
mwanafunzi mzuri wa Biblia utagundua kwa haraka kuwa wako wengi waliotumiwa na
Mungu kwa namna na viwango vya kipekee, lakini maisha yao yakiwa yamepitia
katika mpango mbaya wa kusikitisha na kuumiza
Rahabu aliyekuwa kahaba wa
kutupwa katika mji wa Yeriko alimjua Mungu na akawa miongoni mwa hao waliomleta
masihi (Joshua 2:1 Mathayo 1:5)
Ruth aliyekuwa mpagani na kutokea
kabila la madui wa Israel alimjua Mungu na kuingia katika mstari wa waliomzaa
Yesu
Daudi wa ukoo huo huo wa Yuda
aliyezini na kuua kupitia Bathsheba anamzaa Sulemani ambao wote wanaingia katika
Mababa waliomleta Yesu Kristo
Mathayo aliyekuwa Mtoza ushuru,
aliyeajiriwa na serikali ya kirumi, watoza ushuru walijulikana kama wezi,
waongo, na wadhalimu, wasaliti, Mungu alumuokoa na kumtumia kwa utukuifu wake
ikiwamo kuandika injili Mathayo 10;3 akawa miongoni mwa Mitume
Paulo mtume akishuhudia yeye
mwenyewe kwamba alikuwa mwenye dhambi, mtukanaji na muongo Itimotheo 1:12-15 na
Matendo 26:9-11
Je ninani nanastahili kuwa
Muhudumu wa Agano jipya? Paulo mtume anasema Mungu ndiye atustahilihishaye
2Wakoritho 3:5
Ndugu zangu Mabadiliko ni
Mchakato, tunapompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi katika maisha yetu uhalisia
wa maisha hugawanyika katika maeneo makuu matatu, kuna mabadiliko ambayo
utayapokea mara moja Instant na mengine utaanza kukamilishwa taratibu na
hatimaye utakamilika katika kifo, Instant Sanctification, Progressive
sanctification and Perfect Sanctification !
Mwanzo 43: 1-9 Maisha ya Yuda
baada ya miaka yalikuwa yamebadilika kabisa, Yuda aliyekuwa na
Ubinafsi,Uasherati, Umimi choyo na kuhukumu sasa ameacha kabisa kujifikiri
mwenyewe
Anafikiri kuhusu Familia yake
yote anajua kuwa wanahitaji chakula ili waishi, anafikiri kuhusu Familia yao na
maisha yao ya baadaye watakuwaje
Anafikiri kuhusu Ndugu yake
Simeon ambaye amefungwa na Yusufu anafikiri namna atakavyomrudisha nyumbani
lakini sasa ni lazima waende na Benjamin
Yuda amabye alikuwa hafikiri
sawasawa sasa amekuwa na ushawishi yuko
tayari kuyatoa maisha yake kwa Usalama
wa Simeon, Benjamin, Baba yake na Familia nzima, yuko tayari kubeba lawama za
wote milele kama hatathibitisha uaminifu kwa baba yake Yuda sasa Amekuwa
amekomaa
Mungu hutumia majaribu na mapito
kadhaa katika maisha kutubadilisha kitabia Yakobo 1:12, 1Petro 6-7
Mungu wakati wote ana mpango wa
kukamilisha ndoto zetu na makusudi yake katika maisha yetu yuko tayari
kugharimika kwa namna yoyote katika kuhakikisha kuwa kusudi lake ndani yetu
linatimia uisnihukumu, nisikuhukumu, tusihukumiane kabla ya wakati Mungu ni
Mfinyanzi na sisi tu Udongo maadamu tuko mikononi mwake atatugeuza kokote
apendako Yeremia 18:1-6
Yuda yuko tayari kuwa Mtumwa kwa
aajili ya Ndugu yake na Baba yake mzazi ndugu Yakobo wasiumizwe Mwanzo 44:33,
Yuda alikuwa mwenye moyo wa toba sasa na mwenye kuamini katika hukumu za Mungu
na kisasi cha Bwana Mwanzo 44;16
Mungu atatutumia kwa kiwango cha
juu na kutufanya Baraka tutakapofikia katika badiliko kuu ambalo yeye
amelikusudia Wagalatia 4:1-5 tusikubali kubaki kama watoto wadogo tuliodumaa
Mungu anatutaka tukue na kubadilika 1Petro 2;2 2Petro 3;18 Waebrania 5:11-61
Biblia inatutaka tukue
Ukiyajua hayo heri wewe
ukiyatenda
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.
Rev. Innocent Kamote.
Hoja hapa ni kwa nini alistahili kuzivunja zile muhuri saba? Zili muhuri saba ni nini?
JibuFuta