Luka 24:49 “Na tazama nawaletea juu
yenu ahadi ya Baba yangu lakini kaeni humu mjini, Hata MVIKWE uwezo utokao juu”
Leo nataka
kuzungumzia Jambo la Muhimu sana kuhusu Ujazo wa Roho Mtakatifu ambalo kwa kawaiada wahubiri wengi pamoja na
kanisa huwa hawalizungumzii, wanapofundisha kuhusu Roho mtakatifu au alama
zinazotumika kumuelezea au kuelezea kazi za Roho mtakatifu, na alama hii au kielelezo hini kinatokana na neon “MVIKWE” Neno hilo ukilichunguza kwa
makini lina uhusiano na tendo la kuvaa au kuvikwa ambapo ndani yake kuna neon
vazi
Ni muhimu kama
wanafunzi wa Biblia kujiuliza kwa nini Yesu anaunganisha tendo la kumpokea au
kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu na neon kuvikwa au vazi? Hii ni Lugha ya
kinabii, kwa Kawaida Biblia inapozungumzia kuhusu Vazi, inazungumzia kuhusu
Heshima au Mamlaka ni hesima gani na mamlaka gani ni muhimu kuelewa!
Mara baada ya
Adam na Hawa kufanya dhambi, utakumbuka mara moja walipoteza heshima na mamlaka
na kupungukiwa na utukufu wa Mungu na hivyo walijitambua na kujiona kuwa wako UCHI
Mwanzo 3:10,21.
Lugha za
kinabii katika maandiko zinatufundisha kuwa Vazi lina uhusiano mkubwa sana HESHIMA ama kuipata au Kuipoteza:
Biblia imejaa
mifano kadhaa inayoonyesha Lugha ya KInabii kuhusu Vazi
Mfano
1.
Yusufu alitengenezewa Vazi maalumu na Baba yake
kama alama ya heshima na kibali kutoka kwa baba yake Mwanzo
37:1-3
2.
Vazi hilo
lilipata mashambulizi na kuonyesha kuwa ametoweka Mwanzo 37:31-33
3.
Baadaye alipata heshima nyingine kutoka kwa
Potifa Mwanzo 37:1-5
4.
Heshima hiyo iliharibiwa kwa Mke wa Potifa na
akakimbia na kuacha vazi Mwanzo 39:11-15
5.
Mungu aliirudisha Heshima ya Yusuphu na akavikwa
mavazi tena Mwanzo 41:41-43
Mavazi pia
yanazungumzia Heshima ya Kifalme katika Ufalme wa Mungu 1Samuel 15:27-29 Vazi linaporaruliwa maana yake ufalme umeondolewa!
Vazi
linawakilisha Heshima, mamlaka, Ufalme na ndio maana wanafunzi wanapohitimu
huvaa mavazi maalumu ya kuonyesha kuwa wanastahili heshima hiyo Vazi lina
ashiria Upako 1Wafalme 19:19-21, 2Wafalme 2:11-15
Yesu alippokari
bia kupaa mbinguni aliahidi kuwa atatuachia Roho wake mtakatifu maana yeke
Anatuachia
Heshima ambayo wanadamu waliipoteza
Anatupa
mamlaka ambayo Adamu aliipoteza
Mtu
anapompokea Roho Mtakatifu anapokea Heshima, mamlaka, utawala, ufalme, upako, uwezo
na nguvu na aibu yake inaondolewa, Ndio
maana Yesu akawaambie msitoke Humu mjini mpaka mmevikwa uwezo utokao juu Yaani
Roho Mtakatifu, anafaida nyingi katika masisha ya Ukristo analeta Heshima na
kufunika aibu!
Ubarikiwe mtumishi kwa somo zuri,
JibuFutaAmina
JibuFuta