Jumanne, 26 Januari 2016

KWANINI TUNAKULA NGURUWE


Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.
Neema na amani zotokazo kwa Bwana Mungu wetu na ziwe juu yenu Nyote !
Ndugu Mpenzi kama ilivyo kawaida leo Mkuu wa wajenzi nimetamani nizungumzie swala hili nyeti Duniani ili kujibu swali Kwanini tunakula Nguruwe ? watu wa imani nyingine wamakuwa wakiwashutumu wakristo na hata kuwaita makafiri kwa vile eti wanakula nyama ya nguruwe, kwa madai kuwa eti imekatazwa katika maandiko matakatifu yaani Tourati na ikiwemo Quran, leo nataka kuanika wazi ili kama unakula mdudu huyu umle kwa amani bila kuhukumiwa au kushutumiwa na mtu.
 Kiti moto mdudu mwenye mjadala mkali duniani

Biblia inasema hivi katika Wakolosai 2 : 16 ‘Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;’ Kwa tafasiri nyepesi biblia inasema usimuache mtu yeyote akuhukumu ‘do not let anyone judge you’ kwa habari ya nunakula nini unakunywa nini, au kama huandami mwezi au kushika sabato mtu asikuhukumu, maana yake ni kuwa mafundisho yoyote duniani ya imani yoyote yanayokataza ule nini usile nini ni mafundisho ya Mashetani, sisi wakristo hatuna miiko, ukienda kwa wapunga pepo wanganga watakupangia ule nini usile nini haya ni mafundisho ya mashetani ona 1Timotheo 4 1-5 Biblia inasema :-
‘1. Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2. kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3. wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. 4. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5. kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.’
Ndugu zangu unaweza kuona maandiko haya yako wazi kabisa kwamba kumzuia mtu ajiepushe na chakula fulani ni mafundisho ya roho zidanganyazo yaani mapepo na mashetani biblia iko wazi kuwa kila kiumbe kilichoumbwa na Mungu ni kizuri kama ukikipkea kwa shukurani kwa vile vimeatakaswa na neno la Mungu !
Wakati najenga Msingi huu napenda pia nikufahamishe vema somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo :-
  • Ufahamu kuhusu Nyakati saba za Maongozi ya Mungu.
  • Mafundisho ya Quran kuhusu Nyama ya Nguruwe.
  • Mafundisho ya Agano jipya kuhusu kula Nguruwe.

Ufahamu kuhusu nyakati saba za maongozi ya Mungu.
       Moja ya sababu zinazopelekeabaadhi ya watu kupinga aina Fulani ya vyakula  ikiwemo nyama ya nguruwe ni kuto kuyajua maandiko na kutofahamu juu ya nyakati saba za Maongozi ya Mungu ambapo Mungu aliongoza kwa Sheria tofauti tofauti, ikumbukwe kuwa Mungu ndie mtunga sheria na huweza kupanga au kupangua sheria  “Amendments” kulingana na nyakati Yeye mwenyewe, kama apendavyo, Kama bunge linavyoweza kupitisha sheria  na hatimaye kuibadili wakati Fulani kama wapendavyo ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, Mungu ameiongoza Dunia hii kwa nyakati tofauti tofauti zipatazo saba, maeneo sita kati yake yametimizwa na eneo la saba litakuwa ni wakati ujao
Nyakati za Maongozi ya Mungu kibiblia Zimegawanyika katika Maeneo makuu saba yafuatayo
  1. Innocence Period-Hiki ni kipindi cha uumbaji mpaka anguko la Adamu(mwanadamu)
  2. Concience Period-Hiki ni kipindi cha dhamiri mpaka gharika
  3. Human Government Period-Hiki ni kipindi cha kujitawala mpaka wakati wa Ibrahimu
  4. Promise au Patriach Period-Hiki ni kipindi cha mababa mpaka wakati wa Musa.
  5. Dispensation of Law- hiki ni kipindi cha sheria ya Musa.
  6. Dispensation of Grace-Hiki ni kipindi cha neema au wakati wa Mataifa.
  7. Escatological times-Kipindi cha mambo yajayo (Dhiki kuu, hukumu ya mataifa, utawala wa miaka 1000,vita ya gogu na magogu, ziwa la moto, Mbingu mpya na nchi mpya.)

Katika vipindi hivi vyoote Mungu aliweka sheria mbalimbali za kuongoza vipindi hivyo,Mtu asipofahamu vizuri anaweza kuchanganya  mambo katika vipindi hivyo Mungu aliweka au kubadili sheria zake kulingana na nyakati hizo na makusudi yake aliyoyakusudia kwa wakati huo.
Mfano sheria kuhusu Vyakula;-
  1. Kipindi cha uumbaji mpaka anguko la Adamu (Innocence Period).
 Sheria ilikuwa moja tu wasile tunda la ujuzi wa mema na mabaya tu wakati huu mwanadamu hakula nyama (Mwanzo 2;16-17,1;28-30) Mungu aliweka sheria hii moja kwa sababu Adamu na Eva walikuwa Peke yao na Mungu aliwapa vitu vyote hebu jaribu kuwaza kama Mungu angesema Usizini, usiibe hizo sheria pale Bustanini zingemuhusu nani wakati Adam yuko peke yake na mkewe
  1. Kipindi cha dhamiri Anguko mpaka wakati wa gharika Gharika (Concience period.)
 Wakati huu Mungu aliamuru wale vitu vyoote isipokuwa Damu tu (Mwanzo 9;1-4).Baada ya gharika Mungu alimruhusu Nabii Nuhu na wanawe kula kila kitu yaani vitu vyote isipokuwa Damu tu yaani lazima damu ya mnyama imwagike unapotaka kumla, soma biblia yako Mwanzo 9: 1-4 waliruhusiwa kula kila kitu yaani vyote akiwemo Yule mdudu Nguruwe!
  1. Wakati wa sheria ya Musa (Mungu aliamuru wale baadhi ya vitu na baadhi vilikatazwa).
  hii ilikuwa ni kwa sababu za kiafya na kutafuta utii wa Israel, baadhi ya vitu vilivyokatazwa ni pamoja na Ngamia, Sungura, Nguruwe, Kambale, Taa, Pweza, Ngisi, n.k. Mungu aliwakataza WAYAHUDI peke yao wasile baadhi ya wanyama na samaki wote wasio na Magamba na wanyama wasio na kwato zilizopasuliwa kati, au wenye kwato zilizopasuliwa kati lakini hawacheui soma (Walawi 11;1-47).
  1. Wakati wa Neema,
Wakati huu Mungu aliamuru kuliwa kwa vitu vyoote isipokuwa damu ambayo kibiblia imekatazwa milele. ( Luka 17;10,1Koritho 10;25-27,Kolosai 2;16,1Timotheo 4;1-5). Wakati wa neema ndio wakati huu wa agano jipya wakati huu tunaruhusiwa kula kila kitu bila kujali wala kuulizauliza soma maandiko yale juu.
   Tatizo kubwa la waislamu ni kutokujua nyakati hizi za maongozi ya Mungu na Sheria alizoweka,wanachanganya mambo. Aidha katika namna ya kushangaza waislamu wanaona Nguruwe tu kuwa ni haramu, huku wamesahau kuwa Mungu alikataza hata ngamia ambao mara nyingi huchinjwa na waislamu wakati wa iddi alhaji. wavuvi wengi wa pwani ni waislamu mara nyingi huvua taa, pweza na ngisi, Mtu anayeamua kuishika sheria na ashike yoote na asiyedumu katika yoote amelaaniwa (Galatia 3;10). Wanyama wengi miongoni mwa waliokatazwa wanahitilafu za kiafya kama wasipoandaliwa vema mfano Nguruwe ana tegu wengi katika nyama yake pia huharibika kwa Haraka nyama yake inapokaa zaidi ya wakati hivyo kutokana na mazingira ya jangwani walikokuwa wanasafiri Israel isingelikuwa vema kuruhusiwa kutumia aina hizi za nyama. Mungu aliwapa sheria hii Wayahudi peke yao wakiwa chini ya nabii Musa. Baada ya kuyaelewa haya sasa hebu tuangalie Mafundisho ya Quran kuhusu Nguruwe!
* Mafundisho ya Quran Kuhusu Nyama ya nguruwe;
     Pamoja na kuwa waislamu wanatushutumu sana wakristo kuwa tunakula Nguruwe Quran inajikanganya sana katika swala zima la kuliwa ama kutokuliwa kwa mnyama huyu ni muhimu kuangalia, kwa ufupi hakuna aya maalumu katika Quran inayoharimisha na kukataza kula nguruwe
Quran inasemaje kuhusu nyama ya nguruwe;-
  • Quran inaeleza wazi kuwa Mungu aliharimisha Vitu vizuri (akiwemo Nguruwe) kwa Wayahudi kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, yaani Mwenyezi Mungu aliwakataza kula nyama hii kama sehemu ya kuwahukumu wayahudi na si vinginevyo soma (Surat an-nisaa 4;160).Quran inasema hivi katika aya hiyo “Basi kwa dhulma yao hao Mayahudi tuliwaharimisha vitu vizuri walivyohalalishiwa na vilevile kwa sababu ya kuzuiliwa kwao watu wengi na njia ya mwenyezi Mungu” ni aya iliyo wazi kuwa wayahudi walizuiliwa vitu vizuri kwaajili ya dhuluma Mungu alitaka kuwahukumu kwa kuwanyima baadhi ya vitu vizuri Quran inakiri wazi kuwa Nguruwe ni kitu kizuri Umeona?
  • Quran inafundisha kuwa Yesu alikuja kuhalalisha yale yaliyo harimishwa (Surat al-Imran 3;50).Quran inasema haya katika aya hii “ Na nitakuwa Msadikishaji way ale yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati na nimekuja ili NIKUHALALISHIENI yale MLIYOHARIMISHWA na nimekujieni na hoja Kutoka kwa Mola wenu kwa hiyo mcheni mwenyezi Mungu na NITIINI” Hayo ni meneno ya Yesu Ndani ya Quran ikionyesha wazi kuwa Yesu alikuja kuhalalisha yale yaliyoharimishwa katika Tourati na anatuamuru kumtii, ni wazi kuwa Yesu ameruhusu kula Nguruwe na Quran pia
  • Quran imehalalisha kula vilivyo vizuri walavyo waliopewa kitabu (Al-maida 5;3-5).Sura hii almaida maana yake maswala ya meza inasema hivi “……..Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni Halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao…” Hii ni aya iliyo wazi inayoruhusu kila muislamu kula vyakula vya wakristo na wayahudi na sisi kula vyao umeona!
  • Quran ina kigugumizi kwa vile hakuna katazo la moja kwa moja kuhusu kutokula Nguruwe yaani inakataza kula Nguruwe na wakati huohuo inaruhusu endapo utashurutishwa na njaa (Al-baqara 2;173) au kama una dharula waweza kula hapa ndipo quran inapojikanganya ni muhimu kujiuliza imekataza au imeruhusu? Na dharula hii ni ipi? Quran inajibu kuwa dharula hii ni njaa (Al-an nam 6;145)Quran inasema kula bila kupita kiasi hili ni jema kwani biblia inafundisha kuwa hata kama una njaa kiasi gani kula kupita kiasi  hata kama si nguruwe chakula chochote ni ulafi ni dhambi (Galatia5;21)
  • Quran inafundisha kuwa Mungu hakuharimisha chochote ila wazee wa kiyahudi waliharimisha kwa mapokeo yao tu (Al-an nam 146)
  • Quran inatahadharisha kuwa makini kumzulia Mungu uongo kuwa ameharimisha kitu kumbe hakuharimisha chochote (An Nahl 16;116)
  • Qyran inaamuru uletwe Ushahidi kuwa ni wapi Mungu ameharimisha wanyama? Soma (Al an- am 6;150).
Hivyo ukisoma kwa makini Quran utaona hakuna kilicho haramu ndugu zangu waislamu kula nguruwe ni ruksa ila kiasi tu usizidishe ndivyo quran inavyofundisha kama husadiki pale uwanja wa sabsaba Tanga kwa Minchi waislamu wnzenu hujumuika kula kiti moto kila iitwapo leo kwani wameelimika na wamegundua siri hii.Mimi sikushawishi ila nina kuweka huru kama mwalimu wa kweli ya Mungu “….. Mtaifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru
 Mafundisho ya Agano jipya kuhusu vyakula (Nguruwe).
  • Biblia inasema mafundisho yoyote yanayokataza mtu kula vitu Fulani ni mafundisho ya Mashetani (1Timoth 4;1-5). Ndio maana waganga wa kienyeji mtu anapokwenda kuaguliwa hukatazwa kula baadhi ya vitu Mungu sio Mganga wa kienyeji. Na wanaomwamini hawana sheria ya kuwazuia nini cha kula au kutokula
  • Biblia inasema hakuna kitu najisi kwa mtu asiye najisi lakini kitu Fulani ni najisi kwake yeye aliye najisi (Rumi14;14)Biblia inafundisha kuwa kula au kutokula  hakuongezi utakatifu wala hakuzuii tamaa za mwili (Kolosai 2;16-23) hivyo hatupaswi kujitia katika mambo ya kutunga tu ya mtu,au akilizake na maono ya wanao abudu malaika kumuabudu Mungu hakuji kwa kula au kutokula aina fulani ya vyakula  bali katika moyo safi (Math 5;8)
  • Biblia inafundisha kuwa unajisi wa mtu hautoki nje bali ndani ya mtu pia Yesu alitakasa vyakula vyoote (Marko 7;14-16,17-19)
  • Paulo mtume alifundisha kuwa chakula ni kwa tumbo tu na si mambo ya rohoni
(1Koritho 6;13).Hoja ya Pepo waliotolewa na Yesu kuwaingia nguruwe je ina maana gani?

      Jambo lingine ambalo wanaharakati wa kiislamu Hulishikia bango kuwa nguruwe hawafai ni lile tendo la Pepo waliotolewa kwa mtu aliyeteseka kama kichaa kuomba ruhusa kuwaingia Nguruwe (Marko 5;12-13)
Kwa mujibu wa wachangiaji wa maoni ya kibiblia kama Mathew Henry commentary na wengineo hujaribu kutoa ufafanuzi huu kuhusia na na swala hili
   Nchi ya wagerasi ilikuwa inakaliwa na wayahudi wengi walioasi na kufuata mambo ya mataifa, swala la kufuga Nguruwe lisingeweza kufanywa na Wayahudi wa kawaida kwani kwao walikatazwa kula wanyama hao kwa mujibu wa sheria ya Musa, Hivyo tendo la Yesu kuruhusu pepo kuingia Nguruwe kama walivyojiombea wenyewe lilikuwa ni sehemu ya hukumu kwao kwa kuishi kinyume cha sheria ya Musa,Jambo hili linathibitishwa na maombi ya mapepo “asiwapeleke nje ya nchi ile” maana yake kutokana na uasi uliokuwepo katika nchi ile mapepo bado yalikuwa na kazi katika mji ule, na hivyo waliomba wasihukumiwe kabla ya wakati wala wasifungwe kwani Kristo alikuwa na mamlaka hiyo.
     Aidha inaonekana Tendo lile lilifanyika kwa kusudi la kuwafanya wachungaji wa nguruwe kuingia mjini na kutoa taarifa kwa haraka watu wamtukuze Mungu na kama sehemu ya kutoa Hesabu ya mifugo kupotea hivyo kutokuwa na Kesi.Jambo hili liliwafanya wagerasi waogope na kumsihi Yesu aondoke mipakani mwao.
    Katika eneo hili pia tunaona jinsi thamani ya mwanadamu ilivyo bora nguruwe walikuwa wapata 2000 kwa sasa kilo ya nyama ya nguruwe ni kati ya 6000/- kwa wastani chukua 6000 zidisha mara 100 yaani kilo za nguruwe mmoja mara 2000 idadi ya nguruwe woote utapata gharama ya 120,000,000/yaani Bilioni moja na milioniishirini. Hasara waliyoipata wagerasi hailinganishwi na roho moja ya mtu anayepokea wokovu hivyo Kristo alitaka kuonyesha ni jinsi gani Roho ya Mtu ina thamani.
   Jambo lingine ni kuonyesha wingi wa pepo ambao walijitaja kuwa ni jeshi legion kwa kawaida kikosi cha askari wa kirumi kilichoitwa legion kilibeba askari 6000 au zaidi,Pepo hao walikuwa ni wengi na isingeliwezekana watu kujua Mtu huyu anateswa na pepo wengi kiasi gani kama Masihi hangeuliza Maswali na pia kuruhusu Pepo hao kuingia Nguruwe, hii ilisaidia wanafunzi na jamii kujua ni wingi wa mapepo kiasi gani wakati mwingine hutesa watu,Kwa bahati nzuri pia nguruwe hao walikufa baharini, hii haimaanishi kuwa Nguruwe woote wana mapepo.Tendo la Masihi hapo halina uhusiano na kula au kutokula nguruwe bali thamani ya mtu na mateso yanayotokana na Mshetani ambayo waislamu ni rafiki zao.
Kwa kuhitimisha Mjenzi mwenye hekima nawaalika watu wote duniani msiwe na wasiwasi wa kula kiti moto na wanyama wengineo mnaojisikia kuwala Karibuni
“Maana msingi mwingine hakuna awezaye kuuweka isipokuwa ule uliokwisha kuwekwa yaani Yesu Kristo” makala na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima, Rev. Innocent Kamote 1Wakoritho 3:10-11

Maoni 19 :

  1. Asante sana kwa ujumbe huu, Mungu akuzizishe katika mafunuo sahihi.
    AMINA

    JibuFuta
    Majibu
    1. Kwa faham zangu ni kwamba Baba Mungu ni Mkuu sana sisi ni watto wake unapohitaji kitu kwa baba yako unapaswa kumwomba kwa nidhamu na unyenyekevu na sio kumpayukia kama unalazimisha kukipata unachoomba
      Je kwa kawaida unaweza muomba mzazi wako kitu kwa kumpayukia ndo aguswe akupatie unachotaka au upayuke ili jiran aone humpag mtto wako mahitaj yake ndo mana anakupayukia so tunapaswa kunyenyekea kwa Mungu Baba ili atupe haki zetu

      Futa
  2. Kwa kuongezea hapo kuhusu unajisi wa chakula,,bofya link hii >> https://wingulamashahidi.org/2019/09/02/biblia-inaposemavilivyotakaswa-na-mungu-usiviite-wewe-najisimdo-1015-je-kauli-hii-inatupa-uhalali-wa-kula-kila-kitu/

    JibuFuta
  3. Naomba kuuliza Yesu aliposema msipwayukepwayuke kamawatu wamataifa alikuwa namaanagani?

    JibuFuta
    Majibu
    1. Kwa faham zangu ni kwamba Baba Mungu ni Mkuu sana sisi ni watto wake unapohitaji kitu kwa baba yako unapaswa kumwomba kwa nidhamu na unyenyekevu na sio kumpayukia kama unalazimisha kukipata unachoomba
      Je kwa kawaida unaweza muomba mzazi wako kitu kwa kumpayukia ndo aguswe akupatie unachotaka au upayuke ili jiran aone humpag mtto wako mahitaj yake ndo mana anakupayukia so tunapaswa kunyenyekea kwa Mungu Baba ili atupe haki zetu

      Futa
  4. Nashukuru Sana kwa ujumbe huu Mungu azidikukubariki Amina.

    JibuFuta
  5. Ahsante umenipa mwanga ,sasa pale Bwana wetu Yesu Kristo aliposema nalikuja kuitimiliza torati,alimanisha nini tusaidianae jamani

    JibuFuta
  6. Lakini aliyesema msile nguluwe so mungu? Je,wapi tena kasema kulen nguluwe?

    JibuFuta
    Majibu
    1. Soma vizur maandiko mbona kaelezea vzur

      Futa
  7. alikua anaelekeza namna ambayo watu wa mungu tunatakiwa kuomba....tusipayukepayuke kama watu wa mataifa...soma mathayo ( ) kuna utaratibu wa kuomba

    JibuFuta
  8. Mungu akujali kwaufafanuzi wako maana siyo wasilamu tuu Bali ata wasabato wanatunganyapaa sisituokula nguruwe amina

    JibuFuta
  9. Msipayuke payuke kama watu wa mataifa alikuwa anamaanisha kwamba uombapo omba sirini means kwamba omba kwa kumaanisha siyo ilimradi watu wakuone wewe unasali sana uwasalii binadamu bali unapaswa kumtukuza Mungu aliye hai Amen 🙏

    JibuFuta
  10. Mungu akubariki kwa some zuri. Nimejifunza kitu hapa na mimi nielimishe wengine

    JibuFuta
  11. Mi naona wasabatto wako SAWA kwa sababu mandiko yaripinga vikari hasa kwenye ulaji wa vyakula na pia ukianza kufatiria vzr pia mandiko yariruhusu tuso ( inamaanisha elimu) nakama yariruhusu ivyo na pia wario soma nikimaanisha wanasanyansi wanadai ivyo vyakula ni hatari alafu uku tunaambiwa viliwe amuoni kua ni hatari pia cjaona kwenye mandiko imeluhusu kua mdudu au kitimoto iliwe ila nimeona sehem imekatazwa

    JibuFuta
    Majibu
    1. Unajisi unatoka moyoni mwako na sio kwenye vyakula alivoumba Mungu hayo n maneno ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu

      Futa
  12. Je yesu mwenyewe alikula nguruwe?

    JibuFuta
  13. Mungu akubarik mtumish

    JibuFuta