Afrika Imelaaniwa?
Ni swali la miaka kadhaa
ambalo wengi tumejuliza kuhusu bara letu la Afrika kutokana na hali duni
iliyonayo bara letu la Afrika ni kama kwamba ndio bara lililo nyuma zaidi ya
mabara mengine umasikini uliokithiri vita vya wenyewe kwa wenyewe na matatizo
kadhaa ya magonjwa na maradhi, je Mungu ana makusudi mema na Afrika? Naam
Mungu hana upendeleo Mungu ana mpango na makusudi mema na Bara la Afrika
vumbua siri hii na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima Rev. Innocent Kamote, katika
kijitabu hiki Afrika katika Mpango wa Mungu.
SOMO: AFRIKA KATIKA
MPANGO WA MUNGU
Umasikini ni moja ya matatizo makubwa sana Afrika,
Afrika ni moja ya Bara ambalo bado liko nyuma sana kimaendeleo ukilinganisha na
Mabara mengine, hata ingawa umasikini uko dunia nzima lakini kuna umasikini
mkubwa uliokithiri katika nchi za Afrika, miji mingi ya Afrika imejawa na watu
masikini ambao mwanakosa huduma muhimu sana, miundo mbinu hafifu, mitaa
isiyopangiliwa, watoto wa mitaani, ukosefu wa maji safi ya kunywa naya kutosha,
huduma duni za afya, tatizo la wakimbizi,watu wasio na mavazi, ombaomba na
maswala kadhaa yenye kuvunja moyo. Ni nini tatizo la Afrika? Je Mungu anaijali
Afrika? Je Mungu ameiacha Afrika? Mbingu zina mpango gani na Afrika? Tutachukua
Muda kutafakari somo hili Muhimu Afrika katika Mpango wa Mungu kwa kuzingatia
vipengele kadhaa vitano vifuatavyo:-
·
Dhana potofu kuhusu sababu za Umasikini wa
Afrika
·
Mpango wa Mungu kwa Bara la Afrika
·
Kuhani mkuu kwa mfano wa Yethro.
·
Tatizo la Afrika na ufumbuzi wa matatizo yake
kibiblia
·
Mungu ataitumia Afrika wakati wa zamu yake.
Dhana potofu kuhusu sababu za Umasikini wa Afrika
Kama tulivyoona katika utangulizi
kuwa Afrika inakabiliwa na hali ya umasikini wa kupita kawaida mtafiti mmoja
nchini Kenya alifanya utafiti kati ya 1988 -1990 na kubaini kuwa moja kati ya
kila watu watatu barani afrika hawashibi, yaani wanakabiliwa na njaa kwa msingi
huo zaidi ya watu milioni 168 wa afrika hwashibi, licha ya kuwa na uhaba wa
chakula cha kutosha, makazi yasiyoridhisha na ukwasi umasikini unatawala Afrika
kwanini kwanini? Wataalamu wa maswala ya kiroho wanafikiri yafuatayo
1.
Afrika
imelaaniwa
Hii ni moja ya
dhana potofu sana ambayo imewatawala Waafrika kwa Karne nyingi hatujui ni nani
mwanzilishi wa msemo huu au dhana hii lakini imejengeka kwa miaka mingi na watu
wanafikiri ndivyo ilivyo kimaandiko pia Je Mungu aliruhusu Afrika ilaaniwe?
Maandiko yanayotumika kuhalalisha dhana hii potofu ni Mwanzo 9: 25 – 27 Maandiko haya yanasema Hivi
“Akasema na alaaniwe Kanaani,
Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake, Akasema Na atukuzwe Bwana Mungu wa Shemu na kanaani awe mtumwa wake, Mungu
akamnafsishe Yafeth na akae katika
Hema za Shemu na Kanaani awe mtumwa wake”
Dhana hii kuwa
Afrika imelaaniwa, kihistoria iliweza kutumiwa vibaya, kwa mfano Huko Afrika ya
kusini, watu weupe waliitumia dhana hii kuwakandamiza watu weusi, wakidai kuwa
kibiblia wao ni watumwa wa watumwa, kwa vile Mungu amewalaani tagu awali,
Ni muhimu
kufahamu kuwa Ahadi za Mungu “Zinategemea”
yaani ni “conditional” Laana iliyotamkwa hapo inaweza kumpata mtu yeyote
mwenye tabia kama ya Hamu na mwanae Kanaani, wao kimsingi walikuwa na tabia ya
kutokuheshimu wazazi na hivyo walipoteza heri,maswala ya ngono na picha za
ngono na simulizi zake kwao kilikuwa ni kitu cha kawaida na walifikia ngazi ya
kufikiri kuwa kila mtu angekubaliana na mawazo yao yaliyofikia ngazi za kuacha
kuheshimu wazazi wao
Ni Tabia ya Hamu
ndiyo iliyopelekea mwanae Kanaani kupoteza haki ya mzaliwa wa kwanza na
kutamkwa kama mtu atakayekuwa mtumwa, Ni dhahiri kuwa kama Kanaani na kupitia
Hamu Baba yake wangeshikamana na utii na heshima kwa Mzazi wake Nuhu, wao ndio
wangekuwa Kinara na taa ya dunia na Mungu asingeliwapokonya Ile nchi Nzuri
ijulikanayo kama Israel leo.
Laana ya Nuhu
ilikuwa inategemea, na utii au kutokutii kwa Kanaani, na pale walipojiingiza
katika utendaji wa dhambi na kuacha sheria na mapenzi walipoteza haki ya
mzaliwa wa Kwanza jambo hili si geni kimaandiko kwa vile Hata Reuben Mzaliwa wa
kwanza wa Yakobo kwa kushindwa kumuheshimu baba yake na kufanya kosa kubwa
zaidi ya lile la kanaani alipoteza haki ya mzaliwa wa Kwanza Mwanzo Mwanzo 49: 3-4 Ni wazi kuwa Biblia
inaonyesha kuwa Reuben alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Yakobo yaani Israel na
hivyo alikuwa na haki ya Mzaliwa wa Kwanza na nafasi ya kwanza ya heshima na
ukuu na uongozi na nguvu lakini badala yake nafasi yake ilichukuliwa kutokana
na kulala na mke wa Baba yake Mwanzo
35:22, Kumbukumbu 27:20 hii ni
wazi kuwa kushindwa kitabia kunakodhihiriswhwa na matendo mabaya ya dhambi na
kukosa Heshima kunaweza kumuondoa mtu katika nafasi aliyokusudiwa na Mungu
Makosa ya Reuben yalikuwa ni makubwa zaidi
kuliko ya Hamu kuuona Uchi wa Baba yake, kimsingi wote walipoteza haki ya kuwa
viongozi hiki ndicho kilichotokea kwa kanaani
na hivyo wana wa shemu walikuja na kuichukua nchi yao na wakanaani wengi
waliuawa na kutawanyika maeneo mengine.
Hivyo dhana hii ya kitheolojia kuwa AFRICA
Imelaaniwa ni dhana Potofu kibiblia na haikubaliki katika mazingira na mpango
wa Mungu Mungu si wa taifa Fulani tu Mungu ni wa mataifa yote Matendo 10: 34 - 35 “…Hakika natambua
ya kuwa Mungu hana Upendeleo Bali Katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki
hukubaliwa na Yeye”
2.
Afrika
iliwatumikisha wana wa Israel
Ziko baadhi ya
dhana kuwa huenda umasikini wa Afrika umechangiwa na historia ya kuwatumikisha
wana wa Israel kwa miaka zaidi ya 400 huko Misri mpaka Musa nabii alipowakomboa
kutoka nchi ile ya Utumwa, na kwa sababu ya kuwatumikisha watu wa Mungu huenda
ikawa sababu ya umasikini tulio nao leo kwa vile Mungu alimwambia Ibrahimu “nitawabariki wakubarikio naye akulaaniye
nitamlaani” Mwanzo 12:2-3.
Ni muhimu
kufahamu kuwa Israel kuja Misri ulikuwa ni mpango wa Mungu, Mungu alimjulisha
Abraham Mapema mpango huu Mwanzo 15 : 13
– 16, Mungu alimuahidi Ibrahimu kuwa uzao wake utakuwa mgeni katika nchi
isiyo yake na kuwa huko watatumikishwa lakini watatoka na mali nyingi na taifa
lile litahukumiwa
Ni dhahiri kuwa
Israel kuelekea Misri ulikuwa ni mpango wa Mungu na Kutoka huko Mungu
aliwabariki sana walitoka na Mali nyingi, walishuhudia Mungu akilihukumu taifa
lile na walipata Mafunuo na mafunzo kuhusu Mungu kutoka Misri na taratibu
ustaarabu na sheria za kuongoza Taifa.
·
Israel walipata nafasi ya kuwa taifa kwa kushuka
Afrika
·
Walijifunza kuhusu Mungu wa kweli kutoka afrika
·
Walijifunza sheria na taratibu za kimaongozi na
vita kutoka Afrika
Misri ilihukumiwa na hakukuwa na laana yoyote kuihusu
Afrika kwa sababu ya utumwa ule.
·
Ujerumani wakati wa Hitler waliwafanyia Wayahudi
ukatili na mauaji ya Halaiki yet Ujerumani ni moja ya mataifa makubwa
lililoendelea kiuchumi duniani natambua kuwa wajerumani waliomba radhi kwa hilo
na wanalipa fidia lakini bado wana hali Nzuri, Kama afrika ingekuwa inaadhibiwa
kwa kuwatesa wayahudi Ujerumani na ulaya ingeadhibiwa kwa kuwatesa wayahudi na
kwa kumuua Yesu
3.
Afrika
iko gizani kwa sababu ya Upagani/na Uchawi uliokithiri na ibada za mizimu
Wako wanaofikiri
kuwa Afrika iko gizani na inafunikwa na wimbi la Umasikini kwa sababu ya
kuabudu mizimu, miungu uchawi na upagani uliokithiri dhana hii pia haina ukweli
wowote wa kusababisha Mungu asiibariki Afrika
·
Historia inaonyesha kuwa nchi nyingi za Ulaya kabla ya Ukristo ziliabudu miungu
na kulikuwa na Upagani mzito na mkubwa, athari za kuabudu sanamu zilizokuwa
ulaya bado zinaonekana ndani ya Kanisa Katoliki na Anglikana, Hata hivyo nchi
hizo zimepiga hatua
·
Japan
ni moja ya nchi zilizoendelea sana lakini ilikuwa ni nchi iliyogubikwa na
kuabudu miungu kwa hali ya juu, nchi ya Japan ina dini inaitwa Shinto na wanaabudu
Mungu Jua Bendera ya taifa hilo ina picha ya jua jekundu katikati hata wafalme
wa Japan huabudiwa kama Mungu lakini Japan imeendelea sana
·
India
ni nchi iliyokuwa masikini sana lakini sasa inakua kwa kasi kuondoka katika
umasikini, India kunaongoza kwa upagani kuliko Afrika, kuna miungu inayoabudiwa
zaidi ya milioni 280 Lakini sasa
wanauzwezo hata wa kutengeneza Mabom ya atomic, wanazalisha injini za treni,
wana viwanda vya magari ni wataalamu wa maswala ya tiba na madawa, wanapiga
hatua kwa kasi sana lakini kuna upagani wa hali ya juu, dini ya Uhindu, Budha
na sikhiism ziko kule India Lakini wameendelea sasa
·
Korea Kaskazini
inapiga hatua ingawa sio kama Korea ya kusini ambao wao wameendelea zaidi,
Korea Kaskazini Rais wao KIM IL SUNG ni
Mungu anaabudiwa, Afrika haijawahi kufikia dhambi ya kuabudu Mtu, MAO TSE TUNG huko
China aliheshimika kama Mungu, Ukomonist uliitawala china na hakuna uhuru wa
kuabudu Lakini leo china ina nguvu kubwa duniani ni moja ya taifa ambalo
limeendelea na uchumi wake unakua kwa kasi sana, ni tishio kwa mataifa makubwa
lakini ni taifa la kipagani dini zao ni pamoja na dini ya Taoism.
Ni lazima tujiulize what’s wrong
with Africa? Kuna tatizo gani Afrika? Je Mungu ameilaani Afrika? Je nini sababu
ya Afrika kuwa Nyuma je Mungu anaipa kipaumbele Afrika? Je Mungu ameisahau
Afrika? Mungu hana mpango na Afrika?
Hilo sasa linatuleta kutafakari kipengele kifuatacho Mpango wa Mungu kwa bara
la Afrika
Mpango wa Mungu kwa Bara la Afrika
1.
Maana
ya jina Afrika
Ni muhimu kuwa na ufahamu kuwa kabla
hatujazungumza mpango wa Mungu kwa Afrika tuwe na ujuzi kuhusu jina Afrika na
maana yake, Asili ya jina Afrika wengi wetu tunaweza tukawa hatuifahamu lakini
neno hili Afrika kwasili linatokana na neno la kilatini afrika Africa ambalo maana yake ni JUA na neno la Kiyunani “Aphrike”
ambalo maana yake isiyo ya Baridi,
Jina hili lilitumiwa mwanzoni na Warumi wakilitumia kuwaita watu wa Libya,
Tunisia na Algeria Hivyo Neno Afrika maana
yake ni inchi ya Mwanga wa Jua, Hata hivyo wazungu waliokuja mwanzoni
kutembelea Afrika waliliita bara la Giza
the “Dark Continent” pengine kwa
sababu ya kutolijua vema bara hili.
Nyakati za Agano la Kale Afrika
ilijulikana sana kwa uwakilishi wa Mataifa mawili makubwa EGYPT na ETHIOPIA Neno Ethiopia linatokana na maneno mawili ya
Kiyunani Ethio Pian e’thi o pia” maana yake burnt Faces / au dark faced yaani
watu wenye ngozi nyeusi au uso mweusi, nchi hii ilijulikana kama nchi ya
Nubi “Nubian Kingdom”na iko kusini mwa Misri na kaskazini mwa Sudani ni
maarufu na ilijulikana kama ardhi ya malikia wa sheba, kwa ujumla Misri,
Ethiopia au Kushi na Kirene zinapotajwa katika biblia hutajwa kwaniaba ya
Afrika, huwakilisha Afrika, kwa Upande wa Jina Egypt waebrania waliita Misri, Mizraim
na Misr kwa kiarabu na hii ndio
asili ya jina Misri kwa Kiswahili, Nchi hii iliwakilisha na maeneo makuu mawili
ambayo zamani yalijulikana kama Upper
Egypt na Lower Egypt kitu
kikubwa ikiwa ni ardhi kuu za aina mbili ardhi nyekundu yaani jangwani na ardhi
nyeusi yaani ardhi yenye rutuba nyingi
na udongo mweusi, hivyo Egypt au Mizraim maana yake ni Nchi ye Udongo mweusi
wenye rutuba.Ama aina mbiliza Udongo Mizraim alikuwa moja ya wana wa Hamu mwana
wa Nuhu Mwanzo 10:6-13 1Nyakati1:8,11.
2.
Afrika
katika mpango wa Mungu
1.
Mungu anao mpango na Afrika kama alivyo na
mpango na mataifa yote duniani Matendo
10:34-35
2.
Mungu ameweka majira na nyakati kwa kila taifa
ingawa wote twatoka katika chanzo kimoja Matendo
17:26-28 sisi sote tu wazao wake. Zamu ya Afrika inakuja!
3.
Mungu alimuahidi Ibrahimu kuwa Mpango wake ni
kubariki mataifa yote ya dunia kupitia yeye Mwanzo 12:2-3
4.
Mungu atawaita watu ambao si watu wake Warumi 9:25-26
5.
Viashiria vya kinabii kuhusu mpango wa Mungu kwa
Afrika
·
Mfalme wa Kwanza kuongoza Dunia Nimrod alikuwa
mwafrika Mwanzo 10:6-12
·
Kutakuwa na Madhabahu ya Bwana Afrika (Misri) Isaya 19: 19- 25, Ashuru (Asia) na
Israel watakuwa Baraka kwa Dunia
·
Ujio wa Malkia wa kushi Mathayo 12: 42, 1Falme 10:1, 2Nyakati 9:1 ni Ishara ya Kanisa la Afrika
litakavyomjia Kristo na Litakavyobarikiwa, Malikia huyu alikuja na vito vya
thamani sana kwaajili ya mfalme Suleman na Mfalme alimrudishia mara dufu, Mungu
ataibariki Afrika kwa namna ya kushangaza Afrika itamzalia Matunda Mungu.
·
Africa ndio waliomsaidia Yesu wakati akiwa na
wakati Mgumu yaani wakati wa Mateso Mathayo
27: 32 na Marko 15:21, maandiko yanaonyesha kama mkirene alishurutishwa
kuubeba msalaba wa Yesu, lakini taarifa za kitamaduni zinaeleza kuwa mtu huyu
alimuonea Yesu Huruma hasa aliposhuhudia
akianguka na msalaba huo na alimsaidia msalaba wake hii ni ishara ya Afrika
kushiriki mateso ya Kristo, na Kristo hakukataa kusaidiwa Msalaba na Simeon
Mkirene, Kirene ni mji mkubwa uliokuwa kaskazini mwa Afrika wengi huusisha na
nchi ya Libya, ni wazi kuwa katika jamii ambazo zimewahi kuteseka na kushuhudia
dhiki na uonevu ni Afrika na Israel Uko wakati Mungu atayafutamachozi ya
Afrikana kulketa faraja kubwa duniani
·
Kati ya Manabii na walimu wa Neno la Mungu
waliokuweko Antiokia wawili wanatajwa kutoka Afrika Simeon aitwaye Niger (Niger
ni Afrika Niger au Nigeria pia hunaanisha mtu mweusi) Lukio Mkirene Libya
(Afrika) Matendo 13:1-3, Hawa
alihubiri nyakati za kanisa la kwanza, walituma wamisionary na kuwategemeza.
·
Mungu alitoa kipaumbele zaidi kwa Towashi wa
Kushi (Ethiopia) Matendo 8: 26-39 na
kinabii ina maana pana zaidi nitakayoizungumzia baadaye Ethiopia ni kinara cha
Afrika na makao makuu ya Afrika yako pale Addis Ababa Ethiopia
·
Afrika itapeleka habari njema kwa mfalme wakati
wa hali ngumu sana 2 Samuel 18: 19-33
Unabii unaonyesha kuwa tutabeba habari njema wakati ulimwengu ukiwa na hali
ngumu na uvunjifu mkubwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili na uadilifu.
3.
Kuhani
mkuu kwa mfano wa Yethro
Unapoisoma
biblia utaweza kuona Biblia ikizungumzia kuwepo kwa kuhani mkuu kwa Mfano wa
Melkizedeki Waebrania 5: 5-6
Ni wazi kuwa
Maandiko hayo ya ukuhani yanamuhusu Kristo, kwa vile katika sheria ya Musa
Ukuhani ulifuata Order/mstari wa/ ya kabila ya lawi, hivyo ni walawi peke yao
katika jamii ya Israel walipaswa kutoa kuhani na sio nje ya hapo, na hivyo Yesu
Kristo kama Kuhani mkuu hakuwa wa kabila ya lawi Yeye ni kuhani watofauti kwa
Mfano wa Melkizedeki.
Hata hivyo
Biblia inatupa taarifa za kuweko kwa Kuhani mkuu mwingine ambaye naye alikuwepo
kabla ya sheria ya Musa huyu ni Yethro, Yethro alikuwa ni kuhani wa Mungu
aliyemuabudu Mungu wa kweli Yehova na alikuwa mkwe wa Musa na ana mchango
mkubwa sana kwa Israel kumjua Mungu Hakuna kitu kinazungumzwa kuhusu kuhani
huyu muhimu na wengi hawajua anawakilisha nini
Habari njema ni
kuwa kuhani huyu mkuu ni wa muhimu sana kwa hivyo lazima tufuatilie chimbuko
lake kisha tutapata picha ya kinabii na mpango wa Mungu dhidi ya Afrika. Biblia
inasema nini kuhusu Yethro
·
Huyo
Yethro ni nani
·
Jina Yethro maana yake ni wingi au ubora (Abundantly or Excellence )
·
Alikuwa Kuhani mkuu wa Midian lakini jambo la
muhimu ni wapi wamidian wametokea na kuhani ni nani na ana asili ipi “Biblia inayo majibu”
·
Wamidian ni watoto wa Ibrahim ambao alizaa na
Ketura baada ya kifo cha Sara Mwanzo
25:1-6, 1Nyakati1:32-33 Yethro alikuwa kuhani wa wamidian maana yake ni
wana wa Ibrahimu kwa Ketura hivyo wamidian walikuwa na ujuzi kuhusu Mungu wa
kweli
·
Uthibitisho unaotutambulisha hili unapatikana
katika sifa ya Mungu kumchagua Ibrahimu Mwanzo
18: 17-18 Mungu alimchagua Ibrahimu kwa vile alijua kuwa Ibrahimu
atawafundisha wototo wake njia ya Mungu hivyo wamidian waliishika nja ya Mungu
waliyojifunza kutoka kwa baba yao, walimuabudu Mungu na walikuwa na ujuzi naye
·
Sasa tunamuona Yethro kama kuhani wa Midian
lakini mtu huyu alikuwa ni mtu wa namna gani
1.
Alimpa Musa usalama na kumtunza alipokuwa mkimbizi
na kumuoza mke yaani binti yake aliyeitwa Sipora, kuhani huyu alionyesha wema
kwa Musa alipokuwa ukimbizini
2.
Alikuwa na ujuzi kuhusu Mungu wa Kweli
YEHOVA na ndiye aliyemtambulisha Musa
kuhusu Mungu Yehova kwa vile kabla ya hapo Musa na waebrania wote walimjua
Mungu kama Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo na kwa vile walikuwa utumwani
hawakuwa na nafasi ya kumjua Mungu kwa Muda mrefu, ndio maana watu hawa
walitaabika na kuabudu miungu mara kadhaa,Kutoka
18:1-11.
3.
Alikuwa na ujuzi kuhusu Mgawanyo wa Uongozi Kutoka 18:13-23
4.
Ndiye kuhani aliyeweza kutoa dhabihu kabla ya
ukuhani wa Musa na Haruni Yeye alikuwa na Nguvu ya kusongeza sadaka za
kuteketezwa Kutoka 18: 12
5.
Yethro alijulikana kwa majina makuu mawili
katika Biblia maarufu zaidi ni Yethro na linguine ni Reuel Kutoka 2:18 na Heabu 10:29
6.
Familia
ya Yethro ilikuwa na ujuzi mkubwa kuhusu Yehova na walifahamu umuhimu wa
kushika agano la Tohara ambalo hata Musa alilipuuzia Kutoka 4: 24-26, angalia kuwa mke wa Musa aliweza kumuokoa mumewe
kwa kumtahiri mtoto wao Musa alikuwa hajatilia maanani mkewe Sipora alikumbuka
na kuokoa maisha ya Musa
7.
Swali
bado linabaki palepale Huyu Yethro mtu muhimu namna hii ni nani Hesabu 12 : 1-2 Mistari hii inaweka
wazi kuwa kumbe mke wa Musa alikuwa mkushi Yaani Mwafrika, kwa msingi huo
Yethro ambaye alikuwa kuhani mkuu wa Midian alikuwa mkushi Mwafrika, Huu ni
unabii ulio wazi kuwa Afrika ina ujuzi wake wa asili kuihusu Mungu Yehova na namna
ya kuabudu, Miriam na Haruni walimnena mke wa Musa kwa sababu gani, ilikuwa wao
kabla ya kuja mke wa Musa walikuwa ni washauri wakuu, sasa amekuja mkewe Musa
na anaujuzi kutoka kwao kuhusu Mungu Yehova sasa Musa anamsikiliza mkewe zaidi
na Miriam na haruni wanaona wivu sasa wanataka kutumia weusi wake kumkandamiza
na Mungu anaingilia kati na kuwaadhibu, kisa hiki ndicho kimeruhusiwa na Roho
Mtakatifu kutufunulia juu ya Yethro Afrika ni kuhami mkuu kwa mfano wa Yethro,
“Africa is a high priest of the most
High God in the order of Jethro”
8.
Afrika ni
jicho la Israel, katika maandiko ya Biblia inaonekana wazi kuwa Musa
alihitaji ujuzi wa njia ya kuelekea kanaani nchi iliyojaa maziwa na asali na
walitambua kuwa Mungu amekusudia kuwabariki huko lakini laihitaji uongozi na
ujuzi wa kupita jangwani nani angesaidia Hesabu
10: 29 – 34 Musa sasa anawaingiza Afrika katika safari ya kanaani na
kuahidi kuwa mema ambayo Bwana anayaandaaa kwa ajili ya Israel nao pia
watainjoy uzao wa Yethro ulikwenda na Israel hata Kanaani Waamuzi 4:11.
9.
Africa itanyoosha mkono wake kwa Mungu Zaburi 68:31,Isaya 45:14,Sefania 3: 10.
Isaya 66: 18-21, Moja ya waanzilishi wa umoja wa Afrika “OAU” alikuwa ni
Rais wa Ghana Kwame Nkuruma Rais Kwame
alikuwa ni mtu aliyesoma theology hivyo alikuwa Mchungaji na Mwalimu, Kwame
alitabiri kule Addis Ababa kupitia Zaburi 68:31 Kuwa Afrika itainua mkono wake
kwa Mungu
10.
Afrika ni kimbilio la viongozi na manabii
-
Abraham alifika afrika Misri kwaajili ya
kujikimu kwa chakula Mwanzo 12:10
-
Familia ya Yakobo Israel walishuka Misri
kwaajili ya chakula na kupewa sehemu nzuri ya nchi yenye rutuba sana ifaayo kwa
mifugo
Tatizo la Afrika na ufumbuzi wa matatizo yake kibiblia
Kwa jicho la kinabii tunaweza
kuziona sifa za Afrika na Matatizo ya Afrika kwa kumtazama Towashi wa Kushi, na
pia tukatambua mapenzi ya Mungu kwa Afrika Matendo
8: 26-40
·
Swali kubwa la kujiuliza ni kwanini Mungu anatoa
kipaumbele kikubwa kwa Towashi wa kushi, wakati mwinjilisti Philipo alikuwa
amehubiri samaria na kazi kubwa ilikuwa imefanyika kiasi ambacho kanisa la
Yerusalem Lilimtuma Petro na Yohana kumsaidia Filipo?
i.
Mungu alitoa kipaumbele kwa Bara la afrika
kufikiwa na injili kupitia towashi huyu
ii.
Malaika wa Bwana alihusika kumuelekeza Filipo kuhusu Towashi wa Kushi
kama ilivyokuwa kwa Cornelio wa kirumi kupitia Petro 26
iii.
Roho mtakatifu aliongea na Filipo kumuelekeza
kumsogelea Towashi wa kushi 29 je kwanini towashi huyu anapewa kipaumbele hivi.
a.
Mtu huyu alikuwa anapenda kuabudu, alikwenda
Israel kuabudu 27
b.
Alikuwa ni mtu mkubwa sana ni mtunza hazina za
Malkia wa Kushi Kandake
c.
Alikuwa na kiu ya kumtafuta Mungu na kulisoma
neon lake
d.
Alikuwa na utayari wa kufundishika, alijifunza
kutoka kwa Myahudi huyu Filipo
e.
Alikuwa na ujuzi wa Lugha Kiibrania na kiyunani
zilizomuwezesha kujisomea Gombo la nabii Isaya
f.
Gombo la nabii Isaya lilikuwa na mvuto kwa vile
alitabiri maswala mengi kuhusu Kushi yaani Afrika Isaya 19: 19- 25
g.
Lakini pia walikuwa wakimtazamia masihi na
walivutiwa na habari zake katika kitabu cha nabii isaya towashi huyu wa Kushi
alikuwa akisoma Isaya 53 na swali
lake lilikuwa katika Mstari wa 7-8
na kupitia mistari hii Filipo alimuhubiri injili na aliamini na kudai abatizwe
na alifurahi na kurejea kwao Histiria ya kanisa inaonyesha kuwa kanisa
liliingia Afrika mapema kupitia towashi huyu
Picha ya kinabii kuhusu Towashi huyu
1.
Alikuwa Towashi – maana yake hana uwezo wa
kuzalisha
2.
Alikuwa anasoma lakini haelewi
Kibiblia haya
ndio matatizo makuu ya Bara la Afrika, Ni bara lenye hazina kubwa sana
malighafi na utajiri uliotukuka, lakini kibiblia inaonekana suluhu yake
itapatikana kwa
1. Uongozi: bora
2. Elimu: ya kutosha lazima afrika
ijikwamue kielimu, Afrika inahitaji uongozi wa kuelewa, wanasoma lakini
wanahitaji Filipo kuwawezesha kuelewa vema
3. Uzalishaji: Afrika inahitaji
kujiimarisha katika swala zima la uzalishaji mali Picha ya towashi wa Ethiopia (Kushi) ni alama ya kinabii kuihusu Afrika, Ina uwezo wote lakini haizalishi malighafi zake yenyewe, wajanja wanaigeuza Afrika kuwa soko la bidhaa na wakazi wa kichuuzi, viongozi watakaoitwa na Mungu kuiongoza afrika ni lazima wawe na mtazamo wa kujitegemea, dhana ya kujitegemea haiwezi kuweko kama kila kitu kinafanyika katika mataifa mengine na sisi tukabakimkama wanunuzi tu! ni lazima tuzalishe kila kitu wenyewe, na kuwapa mitaji wawekezaji kutoka Afrika ni lazima tuwe na Nguvu ya maaumuzi ya wakati wetu ujao (Robert Nesta Maley Bob Maley) Aliimba "Every Human being has the right to decide for his Destination " alipokuwa akishangilia uhuru wa Zimbabwe, Uhuru wa kweli wa AFRICA Ni lazima uendane na uchapaji kazi na maamuzi ya dhadi ya kujikwamua sisi wenyewe ili tuwe na uwezo wa kuamua kesho yetu itakuwaje Mungu anatusubiri tufikie hatua hiyo ndipo aiinue Afrika, ni wakati wa Mungu nkuitumia Afrika na ni wakati wetu umefika kutoa misada kwa mataifa mengine
·
Mungu ataitumia Afrika wakati wa zamu yake.
Kuna mambo
yanabadilika duniani, miaka michache iliyopita Amerika na Canada na ulaya ndizo
nchi zilizokuwa na utajiri mkubwa sana duniani, lakini katika miaka kumi
iliyopita mambo yamebadilika, China na India nzi zilizokuwa masikini sana na
baadhi ya nchi za asia zimepanda juu sana kiuchumi, na kuanza kuwa tishio
kuliko Marekani na mataifa mengine ya Ulaya, Mexico, Brasil, china na india zinapanda kiuchumi sana duniani
Miaka 20 ijayo hali ya Afrika itabadilika
na kuwa tofauti, mexico iliyokuwa nchi ya daraja la tatu na Brazili na India na
China zimekuwa kiuchumi na baada ya miaka kadhaa itakuwa zamu ya Afrika, ni
kweli kuwa kwa sasa hali ya afrika imekuwa na matatizo mengi, vita vya wenyewe
kwa wenyewe, shida na matatizo lukuki na tunafikiri kuwa hatuwezi kuinuka
Ni muhimu kufahamu kuwa kila taifa ambalo
limeendelea kwa sasa limepitia matatizo mengi ambayo Afrika inapitia China
iliathiriwa na Ukomonisti kwa miaka wakaonekana kama wanachelewa, India ilikuwa
inaongoza kwa kuua viongozi wake kila wakati, na Brazil ilikuwa duni lakini
ndani ya kipindi kifupi kumekuwa na mabadiliko makubwa, sana uchumi wa mataifa
mengi ya Magharibi sasa unaporomoka sana, Ugiriki hali ni mbaya uturuki
inashindwakulipa hata wafanya kazi, uchumi wa ulaya unaporomoka na uchumi
wamarekani hali kadhalika hali ni mbaya
Afrika itakuja juu wakati wa zamu yake na Mungu ataitumia Afrika
Ndimi Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
Ushauri wangu kwako naomba kama uaweza andika vitabu vya historia ya biblia
JibuFutaVitabu vyako nita vipataje?
JibuFutaGood👏👏👏
JibuFutaWhere can I get this book
JibuFutaNuru ya Mungu izidi kuwa nawe kila leo yazaliwe mengi kupitia wewe kwa faida ya waafrika.
JibuFuta