Jumapili, 7 Februari 2016

KWANINI WAKRISTO TUNAZIKA NA SANDUKU?


 Waislamu wamekuwa na tabia ya kushambulia wakristo na kuwashutumu katika mambo mengi likiwemo swala la mazishi hususani swala la kuzika na Sanduku linalofanywa na wakristo,katika eneo hili tutakuwa tunajibu na kuchambua jinsi mazishi ya kiislamu yanavyotofautiana na mazishi ya kikristo  tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo;-
 
1.       Mazishi ya Kikristo yanavyokuwa.
2.       Mazishi ya Muhamad yalivyokuwa.
3.       Mazishi ya Kiislamu yanavyokuwa.

Mazishi ya Kikristo yanavyokuwa.
     Wakristo wote tunafahamu kuwa muongozo wetu ni Biblia,Hivyo kila tunalolifanya linatakiwa kuongozwa na Biblia neno la Mungu,Imani yetu imejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii naye Kristo ni jiwe kuu la Pembeni (Efeso 2;20). Hivyo tunajifunza kutoka kwao Maandiko hayatufundishi popote kuwa Walipokufa mitume walikamuliwa kama wafanyavyo waislamu mfano Ibrahimu alipokufa hatusomi kuwa alikamuliwa(Mwanzo 25;7),Isaka na yakobo pia walikufa na kuzikwa bila kukamuliwa (Mwanzo 49;32,50;1-6). Ni muhimu waislamu kutuambia kuwa maswala ya kukamuana wanajifunza kwa nani? Maana quran imeagiza wajifunze kutoka kwa Wakristo na wayahudi kama wana shaka katika jambo lolote {Surat Yunusi (Yona) 10;94)}
 Kwa nini Wakristo tunazika na Sanduku?

      Swala la kuzika na sanduku limekuwa likiwakera sana na kuwachanganya waislamu wamekuwa wakihoji kuwa wakristo wamejifunza wapi Tabia ya kuzika na sanduku?wakati mwingine wanafikiri tunaigiza utamaduni wa kizungu,kwa kawaida Wakristo hatufanyi mambo kinyume na maandiko yanavyo tufundisha soma (Mwanzo 50;24).
     “..Yusufu akawaambia nduguze,Mimi nitakufa,Mungu atawajia ninyi bila shaka atawapandisha kutoka nchi hii mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu;na Isaka na Yakobo,Yusufu akawaapisha wana wa Israel  akasema bila shaka Mungu atawajia ninyi nanyi mtapandisha huko mifupa yangu.Basi Yusufu akafa,mwenye miaka mia na kumi,WAKAMPAKA DAWA WAKAMTIA KATIKA SANDUKU HUKO MISRI.”
    Tunajifunza kutoka mfano wa Yusufu.baada ya kufariki alipakwa dawa kama wafanyavyo wengi leo na pia akawekwa katika sanduku.hatuoni pia kuwa Yesu alikamuliwa alipokufa bali aliviringishwa katika sanda akazikwa Hakukamuliwa.Vilevile tunaposoma katika (Yohana 11;40-44).Pale Yesu alipomfufua lazaro ambaye alikuwa maiti siku nne baada ya kumfufua Yesu aliamuru “Mfungueni mkamuache aende zake”Ni wazi kuwa kama Lazaro hakuwa na nguo zake ndani ya sanda ingekuwa vigumu Yesu kuamuru afunguliwe sanda aachwe aende zake? Hivi ndivyo wakristo wafanyavyo hakuna ubaya mtu kuvalishwa nguo zake kasha kufunikwa na sanda na kuagwa nk.
Mazishi ya Muhamad yalivyokuwa.
Kifo na mazishi ya Muhamad ni tofauti kabisa na waislamu wafanyavyo leo ,Habari za kifo na mazishi ya Muhamad yana patikana katika kitabu kiitwacho maisha ya nabii muhamad (SAW) kilichoandikwa na Shekh Abdullah Saleh Farsy uk 79 ambapo kuna maelezo mengi nitanukuu baadhi.
  “Baada ya kuoshwa lilichimbwa Kaburi hukohukochumbani alikofia,chumba cha Bibi Aysha.na aliyesimama kutengeneza mwandani ni Bwana Abu Tah wa Kiansar.Baada ya hapo wakamvua nguo za kuoshea,wakamkafini(Wakamvisha).kwa nguo tatu nyeupe za Pamba.
   Baada ya kufukiziwa udi.vyema na kutiliwa manukato vizuri kasha akalazwa juu ya kitanda kwenye ukingo wa kaburi akafunikwa nguo moja kwa moja,baadae wakapewa ruhusa watu kuingia kumuaga mtume wao,yakawa makundi haya yanaingia haya yanatoka,mchana kutwa wa jumatatu,na mchana kutwa wa jumanne na usiku kucha wa kuamkia jumatano.hata karibu na alfajiri ya hii jumatano,mtume alishushwa kaburini mwake akazikwa.Mtume amekufa mchana wa jumatatu mwezi wa 12 mfungo sita mwaka wa 11 A.H. yaani 8/6/632”
 Kwa msingi huo hapo juu tunajifunza kuwa ,Muhamad hakukamuliwa ,alizikwa kawaida kama wakristo wanavyozika.Muhamad aliagwa kama wakristo wafanyavyo,Inashangaza kuona wafuasi wake hawafanyi kama Mtume wao alivyofanyiwa je aina ya mazishi ya waislamu na uchafu wa kukamuana wanatoa wapi? Utaniwia radhi kwani unapaswa kuwa mvumilivu ninapoanza kuzungumzia namna mazishi ya waislamu yanavyokuwa tangu hatua za kifo hata mwisho fuatana nami katika kipengele muhimu kifuatacho

Mazishi ya Kiislamu yanavyokuwa.
      Mwislamu anapokuwa katika hatua za kufa ,Sharti aelekezwe kibla kama haiwezekani,yaani yu mahututi,basi kitageuzwa kitanda nyayo zikiwa zimeelekea katika jiwe jeusi (Hajar al aswad) huku akiwa amelazwa kichalichali,Wanasema ni lazima kumuelekeza kibla ili weze kuwasiliana  na kile kilichopo makka.Baada ya kufa anawekewa mfano wa kitu kizito katika tumbo lake kama tofali,Baada ya kuwekewa kitu kizito juu ya tumbo lake ndipo wanapoianza shughuli yenyewe ya Maandalizi ya mazishi,kuna idara tatu ambazo ni
 1.Uchimbaji wa kaburi,ambalo linakuwa na mwana ndani ukubwa wa mwana ndani hutegemea urefu wa nyayo za marehemu ambazo hupimwa kwa kamba.
2.Ushonaji wa Sanda.sanda ya mwanaume huandaliwa hivi;-
a].Shuka sita ambazo mojawapo hupimwa ridhaa tatu ambayo ndiyo sanda ya mtu mzima baada ya kukamilisha maandalizi ya sanda wahusika wataingia ndani kwa maiti watachukua shuka moja na kumvalisha kama msuli
b]. Pia kutahitajika mswaki,ambacho ni kipande cha sanda kinachopimwa usawa wa kiganja cha mtu mzima.
c]. Zinatakiwa kamba tatu ambazo hutumika kumfungia marehemu kichwani na tumboni na miguuni.
d]. Zinatakiwa groves za kuvaa mikononi ambazo atazitumia mkamuaji, hizi hupimwa upana wa kiganja cha mkono na kuchana mpaka chini, zinatakiwa tatu. Huwa zinashonwa mshazari kama vile sambusa.
e]. Marashi,udi, mkeka,na kitanda cha kamba.
     Wakamuaji wakiwea chumbani ambako ndiko shughuli yenyewe iliko,kwanza kabisa litachimbwa shimo katikati ya chumba,shimo hukadiriwa kuwa na urefu wa futi moja na nusu,baadae huchukuliwa kitanda cha kamba ambacho huwekwa katikati ya shimo,baada ya hapo huletwa vifaa vitakavyotumika  ikiwa ni pamoja na ndoo ya maji.
 Kule ndani ambako shughuli inafanyika kunakuwa na watu watatu wa kwanza anaitwa kigingi au kiguzo,kazi yake ni baada ya Marehemu kukalishwa kwakuwa atakua amelegea,basi yeye ataweka mguu wake wa kulia,goti likiwa limegusa uti wamgongo wa marehemu.Na mikono yake akiwa amemshika mabega .Wapili kazi yake ni kuleta ndoo za maji ambazo zina kuwa mbili na kazi yake ni kuyachanganya maji ya moto na baridi na kumwagilia pindi yanapohitajika.Watatu kazi yake ni mbaya zaidi yeye ndiye mwenye kushughulika zaidi naUkamuaji.
     Kwanza watamfunika marehemu shuka moja gubigubi, hili shuka ni moja kati ya yale sita,atalazwa kitandani,atapakwa sabuni huku mtu wa maji anaendelea kumwagilia,hapa ataogeshwa kwanza josho la kawaida,Baada ya kuogeshwa marehemu litatolewa hilo shuka na kutumbukizwa ndani ya shimo,litachukuliwa shuka la pili ataogeshwa tena.
   Baada ya kuogeshwa josho la kawaida, litafuata josho maalumu ambapo maiti atakalishwa kitakotako,Mkamuaji ataanza kumkamua ambapo wanasema “Zada imrara-hatta yakhuruju fibutuniha”yaani utazidi kukandamizwa mpaka utoke uchafu wote uliokuwa ndani ya tumbo lake,utaendelea kukandamizwa mpaka mavi yoote yaishe tumboni,Baada ya hapo litafuata tendo la kupima kama uchafu umekwisha au la.
    Mkamuaji atavaa gloves ya kwanza kati ya zile tatu,baada ya kuvaa atatumbukiza kidole chake katika sehemu ya kutolea haja kubwa ya marehemu,na kuangalia uchafu unaotoka ni wa rangi gani?ukitoka wa rangi ya manjano atajua bado uchafu upo,hivyo shughuli ya ukamuaji itaendelea watakandamiza mpaka waone uchafu wa rangi ya kijivukijivu,kama kijivu itakuwa imechanganyika na manjano watabadili njia ya ukamuaji ambapo kiguzo atamwacha akiwa amekaa,watamwangalia ataegemea upande gani? Lengo ni kuhakikisha anapata balance bila kuegemea upande wowote na watasema “Faidhazada ilaa yaminihi,(endapo atazidi upande wakulia) Kana najsa yaminiha faidhazada ilaa yasarihi,kana Najsa fi yasarihi”yaani kama uchafu uko upande wa kulia wataendelea na shughuli hali kadhalika upande wa kushoto,wakisha kuikalisha ile maiti ikainama wanajua shughuli ya ukamuaji imekwisha na mkamuliwaji amekwisha kuwa safi hana kitu tumboni,baada ya hapo watamlaza na kumuogesha tena na watachukua shuka moja na kumfuta maji,ndipo litafuata tendo la kumpigisha mswaki ambapo muoshaji hutumia kidole chake cha shahada  na kuviringisha kipande cha nguo kwenye kidole hicho,baada ya hapo kiguzo ata panua mdomo wa maiti ili meno yaonekane ndipo mwoshaji atakapoanza shughuli ya kumsugua meno kushoto mara tatu,kulia mara tatu,katikati mara tatu,Baadae yataletwa maji na maiti atapanuliwa mdomo,atamiminiwa maji na atatikiswa kichwa chake kama nazi na watarudia hivyo mara tatu.
    Baada ya hapo zitaletwa shuka tatu ya kwanza kwa mwanaume atavishwa msuli katikati, shuka ya pili ambayo inakuwa imeshonwa kama kanzu atavishwa, nay a tatu ataviringishwa mwili mzima, zitachukuliwa kamba tatu na zitafungwa moja kichwani, ingine katikati na ingine miguuni na utaratibu wa kuzikwa utakuwa unasubiriwa.
     Wakamuaji watatoka nje tayari kwa kupata uji,wakati wakisubiri uji watakuwa wakinukuu baadhi ya aya za quran na wataomba dua na baada ya duwa watatulia kusubiri uji na maharagwe. Uji utakapoletwa ytawekwa kwenye zilezile ndoo zilizokuwa zikitumika kwa shughuli za ukamuaji,mbaya zaidi ni kuwa wale watu watatu waliokuwa wakamuaji ndiyo hupewa kipaumbele kunawa maji kwanza kasha maji hayo hupewa wengine kunawa.
     Baada ya kunywa uji watamweka maiti kwenye jeneza tayari kwa kwenda msikitini kumswalia,wimbo huu huimbwa wanapokua njiani “La ilaa haa ilaa ilah,la ilaa haa ilaa ilah,la ilaa ilah Muhamad rasuru-ilah”yaani hapana mola ila Allah na Muhamad ni mtume wake.wakifika msikitini hujipanga mstari wanaswali na kuiswalia maiti na kuiombea dua kama hivi.
Allahuma aki daru khayri min daarith-ewe Alla mpe nyumba bora kuliko nyumba yake,
Allahuma ati ahalal……..mina ahaliha-mpe watu bora kuliko watu wake,
Allahuyma ati zawji min zawjiha-mpe wake bora kuliko wakeze.
Baada ya hapo watatoka msikitini wakiimba wimbo ule wa kwanza  na wanapofika makaburini hubadilisha na kusema Allah-u-Akbar-Allah-u-Akbar x3.
   Kwa mujibu wa dua hizo hapo juu mwanaume anapokufa huombewa apewe wanawake bora kuliko wakeze lakini anapokufa mwanamke dua hii haisemwi! Hivyo katika uislamu wanawake mtajiju.
   Ndani ya kaburi kutaingia watu wapatao watano ambao watamhifadhi marehemu wakati huo juu ya kaburi kutakuwa kumefunikwa shuka ili watu wasione mambo yatakayotendeka ndani maiti ya (kiislamu inafichwa sana). Watu waliopo ndani watampokea marehemu na atatua juu ya magoti yao akiwa chali,baadae hushikwa ubavu mmoja  na kutumbukizwa ndani ya mwandani ambapo huhakikisha uso wake umeelekea kibla (makka kwenye jiwe jeusi).endapo maiti atakuwa mwembamba kuliko mwandani atawekewa nyasi ili awe sawasawa na mwandani bila kupwaya, atawekewa mto ambao kwa kawaida huwa ni udongo. Baada ya hapo kutaagizwa kisu ambacho kazi yak e ni kukata sanda eneo la sikio moja kwani maiti huwa analazwa kiubavubavu,sikio hilo hubaki wazi ili liguse ardhi wanaamini marehemu atatumia sikio hilo kusikia maswali atakayoulizwa humo kaburini, kasha utaagizwa ubao ambao hufunikia eneo la juu la mwandani,endapo ubao
utakua mwembamba yatachukuliwa majani ili kuziba eneo lililobaki wazi kisha wataweka udongo ,shuka litatolewa na waliokuwemo kaburini watatoka na wakati huo hata ukitazama huoni kitu ndani hivi ndivyo jinsi maiti ya kiislamu inavyofichwa,kasha watu wataazna kufukia.Baada ya kumaliza kufukia litafuata swala la kumuombea dua na kumfundisha marehemu kujibu maswali.kunakuwepo kibirika  chenye maji wanamwagilia juu ya kaburi wanaamini kuwa yale maji yaliyo mwagwa juu ya kaburi yanapenya udongo na kuingia kwenye sikio la juu na kutokea kwenye sikio la chini,halafu mtu yule anafufuka ,baada ya kufufuka atakaa na kusema alhamdulillahi kumbe nimekufa1! Hapo wanaamini kuwa ataanza kusikia. Sheikh Anasoma kitabu kiitwacho Talakini l-mait yaani kitabu maalum cha kuzikia, wanamfundisha kujibu maswali kwani wanaamini wasipomfundisha kujibu maswali vitakuja viumbe kumuuliza maswali na endapo atashindwa kujibu atapigwa marungu.katika kitabu hicho uk wa 104-105 atafundishwa hivi;-
 Yaa amalallah bint hawai,udh-uru l-ahad khalajat,mindari dunia,I laa dar akhera wa huwa shahaadatan an laa ilaha Muhammad rasur-Illah,wa ana jannat hakkon,wa anna nnara hakkon,waanna l-maut hakkon, wa anna l-qabur hakkon,wa anna l-mu-nkara-nnakira hakon, wa anna suila hakkon,wa anna l-jawaba hakkon.”
Tafasiri ya maneno hayo ni kama ifuatavyo;-
   “Ewe mja wa allah motto wa mwanamke kumbuka ahdi ambayo ulitolewa katika nyumba ya dunia mpaka nyumba ya kuzimu nawe ni mwenye kushuhudia hakuna mola ila allah na Muhamad ni mtume wake,kwa hakika pepo ni haki yako,kwa hakika kufa ni haki yako,kwa hakika kaburi ni haki yako,kukujia viumbe viwili vyenye kutisha ni haki yako na hivyo viumbe viwili kukuuliza maswali ni haki yako na wewe kuwajibu ni haki yako”
“Ewe fulani bin fulan umetoka katika ulimwengu wa dunia umeingia katika ulimwengu wa kuzimu,ukiwa kuzimu sema hakuna mola ila allah na hakika Muhamad ni mtume wa allah, leo hii kupata pepo ni haki yako na leo hii kuunguzwa moto ni haki yako,viumbe vyenye kutisha ni katika viumbe wa allah. Yaa…..L 1-anna yattika,L-Karima,walaa yuvihibaka fainahumma khalaqu min – allat llah.Faidhhhsaalaka. (Sisi tutakapoondoka Watakujia viumbe vya allah sw. hivyo vitakuuliza maswali yafuatayo;-
Maaismuka…………………………...…Jina lako nani?........................................................................
Manni Rabbuka?.........................Mola ni wako nani?............................................................................
Wa man Nnabbiyyuka?...............Nabii wako nani?...............................................................................
Wa maa Imammuka?..................Kiongozi wako nani?..........................................................................
Wa maa diynuka?........................Dini yako ni nani?..............................................................................
Wa maa kibbilatuka?...................Kibla (uelekeo) chako ni kipi?..........................................................
Wa maa I khiwanuka?..................Ndugu zako akina nani?...................................................................
Fukullu………………………………………Wewe utasema kuwaambia…………………………….
Ismi…………………………………………...Jina langu ni Fulani bin Fulani………...........................
Allahu Rabbi……………………………….Allah ndiye Mola wangu……………………………......
Wa Muhamad Nabii……………………Na Muhamad ndiye nabii wangu……………………….......
Wal-qur-an Imam……………………….Na quran ndiyo kiongozi wangu…………………………...
Wal-qaaba Kibrati………………….......Alkaaba ndiyo kibla yangu………………………………....
Wal-Islama dini……………………………Na uislamu ndiyo dini yangu…………………………….
Wal-muumun wal-muuminat kulumIkhiwani…Waisalamu/kike/kiume ndio ndugu zangu.
Faajibu hadha bi kauli dhabit………Wajibu haya  pasipo kutetemeka wala kuwa na woga tena kwa lugha ya kiarabu.

     Baada ya hapo itaombwa dua maalum kwa ajili ya marehemu na baada ya dua hiyo watu wote hutawanyika.
 Na kwa ajili ya hayo yatakuwepo marungu ya chuma kila mara watakapotaka kutoka humo watarudishwa humohumo na kuambiwa ionjeni adhabu.(Quran). Hivyo kuna adhabu ya marungu huko kaburini, tena Muhammad analielezea rungu hilo kuwa ni zito sana kiasi kwamba hata kama watu wote ulimwenguni kuanzia Adamu mpaka mtu wa mwisho kuzaliwa  ulimwenguni tungejaribu kuliinua tusingeliweza.
 Hata hivyo mashehe hudanganya watu sana kwani kwa mujibu wa quran maiti haisikii. Quran 12;106.(Ufafanuzi wa 106),35;22, soma Biblia pia Mhubiri 6;4,Ebrania 9;25. Je waislamu wamejifunza kwa nani kuwa maiti inasikia? Ni vizuri kuchagua leo kudanganywa au kuiamini injili na pia mwili wako usikubali kuchezewa njoo kwa Yesu Yeye nira yake ni laini.

Maoni 1 :

  1. Wewe inaonekana huijui kabisa dini ya kiislam maneno unayoongea ni ya kizushi

    JibuFuta