Mstari wa msingi 1Petro 2;2 “
Kama watoto waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa ili kwa
hayo mpate kuukulia wokovu”
Ni muhimu kufahamu kuwa tangu
ulipoamua kuokoka wewe sasa umekuwa mtoto wa Mungu Biblia inasema katika Yohana
3;6 “ Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho wewe
umezaliwa kwa roho ndiyo maana inatajwa pia kuwa umezaliwa mara ya pili , hapo
mwanzo ulizaliwa katika mwili na kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kamwe hakiwezi kuishinda dhambi, lakini
sasa umezaliwa mara ya pili na ufalme wa Mungu ni wako, kwa msingi huo sasa
tungependa kutafakari jambo moja la msingi sana
wokovu ni hatua
Mtoto mchanga wa kimwili
anapozaliwa yaani katika hali ya kawaida
ya kibinadamu ili aendelee kuishi
anapaswa au analazimika kupewa maziwa ili aweze kuishi jambo kama hili ni sawa
kwa mtoto wa kiroho pia vinginevyo anaweza kufa au kudumaa na hatimaye kuwa dhaifu
na kufa, kufa kiroho ni kurudi nyuma na kumtumikia shetani sasa ili mtu
aliyezaliwa mara ya pili aweze kuendelea katika wokovu ni lazima anywe maziwa
ya Kiroho 1Wakoritho 3;1-2 na Waebrania 5;13 “Kwa maana kila mtu atumiaye
maziwa hajui sana neno la haki kwa kuwa ni mtoto mchanga” Hivyo mara baada ya
kuzaliwa kiroho au kuokoka tunakuwa bado hatujui sana neno la haki tunahitaji
maziwa ili tuweze kukua katika wokovu.
Maana ya maziwa
Maziwa haya ni kinywaji cha
kiroho Kutoka kwa Yesu Kristo ni neno la Mungu au neno la Kristo soma
1Wakoritho 10;4 wote wakanywa kinywaji kile cha roho kwa maana waliunywea
mwamba wa roho uliowafuatia na mwamba ule ulikuwa ni Kristo” Mtu awaye yote
aliyeokoka kama hatapata mafundisho ya neno la Mungu atadumaa nakujiweka katika hali ya kufa
kiroho na kurudi tena katika utumwa wa dhambi, hakuna uwezekano wowote wakuendelea na wokovu bila mafundisho
ya neno la Mungu Neno la Mungu lina
sehemu kubwa sana katika maisha ya kiroho ya mtu.
1.
Ni
chakula cha kiroho.
Biblia inasema
mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu,
kwa msingi huo kusudi la kuishi kwetu halitegemei kula chakula cha kawaida tu
bali na chakula cha kiroho ambalo ni neno la Mungu Yeremia 15;16 “maneno yako
yalionekana nami nikayala…” Neno la Mungu ni chakula halisi Yesu alisema amlaye
yeye ataishi kwanini kwa sababu Yesu ni neno la Mungu Yohana 1;1 Ufunuo 1913
Yohana 6;48-58 Tukiacha kulila Neno la Mungu
baada ya kuzaliwa mara ya pili
hatutaweza kuishi milele ili kuishi milele ni lazima tumle Yesu Kristo
Yohana 6;48-49,57-58, Yeye ndiye chakula cha uzima Mathayo 4;4 Yesu alisema mtu hataishi kwa
mkate tu…” Kumbukumbu la torati 8;3 Mungu aliwafundisha Israel kuwa hawawezi
kuishi kwa mkate tu bali kwa kila litokalo katika kinywa cha Mungu ni kwa ujuzi
huu watatakatifu waliotutangulia walifahamu umuhimu wa kulishika Neno kama
chakula Ayubu 23;12, wao waliiona sheria ya Mungu yaani neno kuwa la thamani
kuliko maelfu ya dhahabu na fedha”
2.
Ni
taa na mwanga wa njia yetu ya Mbinguni
Njia ya mbinguni
ni nyembamba sana kwa maana nyingine
imesonga na mlango ni mwembamba sana
Mathayo 7;14 ili wakati wote tuweze kutembea
bila kuanguka au kuteleza na
kuingia katika njia iendayo upotevuni
inatupasa kuwa na mwanga Mathayo 7;13, tusipolizingatia Neno la Mungu tunaweza
kupotea katika wokovu Zaburi 119;105 Neno
lako ni taa ya miguu yangu, Mithali 6;21-23 sheria ya Mungu ni nuru…”
3.
Ni
silaha ya ushindi dhidi ya dhambi.
Ni vigumu kabisa kuishinda dhambi bila
kujaa neno la Mungu Yesu Kristo alimshinda shetani katika mathayo sura ya 4 kwa
kutumia neno la Mungu aliposema imeandikwa, kumbe kumshinda adui na kuishinda
dhambi kunahitaji uwe na ujuzi pia wa neno la Mungu Huwezi kuishinda dhambi na adui shetani kama
hupendi kuhudhuria mafundisho na ibada ambako tunajifunza Neno la Mungu, Zaburi
ya 119;11 Biblia inasema Moyoni mwako nimeliweka Neno lako nisije nikakutenda
dhambi kumbe kujifunza neno la Mungu na kulifanyia kazi yaani kulitii
kunatusafishia njia ya kwenda mbinguni Zaburi ya 119;9 Jinsi gani kijana
aisafishe njia yake ni kwa kutii Neno la Mungu na kulifuata daima, Neno la Mungu
pia hufanya maisha yetu kuwa safi Yohana 15;3,Yohana 17;17, kuacha kujifunza
neno la Mungu kunaweza kutufanya pia kufanya dhambi bila kujua Mambo ya walawi
5;17
4.
Ni
Afya ya miili yetu na nyundo ya kuyavunja matatizo tuliyo nayo
Ikiwa tuliponywa
kwa Neno la Mungu katika mikutano ya injili au katika maombezi yoyote ni neno
la Mungu linalotuhakikishia uzima wakati wowote, mara nyingi shetani anapotuona
kuwa tunaujuzi wa Neno la Mungu hawezi kurudi kutufuata fuata tena Luka
11;24-26, hata kama hatujapokea uponyaji wa miili yetu bado ni muhimu kufahamu
kuwa Neno la Mungu ndio ufunguo wa uponyaji wetu Mithali 4;20-22 Yohana 6;63.
Yatafute maneno ya Mungu na kuyaweka moyoni.
Unapokuwa umebanwa na matatizo ya aina yoyote dawa siyo kuacha kutafuta mafundisho ya Neno
la Mungu tumia kila inavyowezekana
kulitafuta Neno na kulitumia lenyewe ni kama nyundo ya kuvunja vunja kila aina
ya matatizo matatizo yote yanayoonekana kama mawe magumu Neno linauwezo wa
kuyavunja Yeremia 23;29 Je Neno langu si kama moto? Asema Bwana na kama nyundo
ivunjayo mawe vipande vipande?
Vizuizi vya kukuzuia kupata mafundisho au chakula cha kiroho yaani Neno
la Mungu.
Tumeona jinsi ambavyo neno la
Mungu lina faida nyingi sana katika maisha yetu ikiwa ni pamoja na kutufanya
tuishi milele na milele kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa shetani
hatapedezwa na sisi kulipata Neno la Mungu kwa msingi huo kutakuwa na vizuizi
vya kila aina kutoka kwake ili tusiwezi kulielewa na kulijifunza Yeye anajuwa
wazi kabisa kuwa hawezi kumshinda mtu aliyejaa neno kama ilivyokuwa kwa Bwana
Yesu Mathayo 4;1-11 kwa msingi huo atahakikisha kuwa kwa gharama yoyote ile
anatuzuia kulipata Neno na ndio maana
hukusudia kutuua kiroho mapema katika uchanga wetu ili tusifikie ngazi ya
kulijua Neno ambalo kwalo anajua kuwa hataweza kutushinda tena alikusudia
kumuua Yesu mapema Mathayo 2;13,16, sisi
nasi tunapookolewa ni muhimu kufahamu kuwa tunakuwa tumezaliwa kwa Roho na
hivyo ibilisi atahakikisha kuwa anatuua mapema kabla hatujalijua sana neno kwa
kuwa tunazifahamu fikra zake ni muhimu kujifunza mbinu zake mapema kabla
hajaanza kuzitumia na kutupata 2Wakorotho 2;11 tukizifahamu mbinu anazozitumia
basi hatutampa nafasi ya kukuua mpinge naye atakukimbia Waefeso 4;27.Yakobo
4;7.
Njia Tano anazozitumia shetani Kumzuia mtoto mchanga kupata Neno la
Mungu ili kumuua.
·
Kumfanya
ajione anajua na akatae kufundishwa
Biblia inasema mtu akidhani kuwa anajua neno hajui bado kama impasavyo kujua 1Koritho 8;2 Mtu awaye yote akikosa ladha ya
chakula na kukataa kula akisema kuwa anajisikia kuwa ameshiba maisha ya mtu huyo yako hatarini hiki ndicho
shetani anachokifanya kwa watu wengi waliookoka huwafanya wajione kuwa wanajua na hawahitaji
kujifunza tena na kutokukubali kujifunza
neno la Mungu na hatimaye hujikuta wanakufa kiroho mtu akitaka kujifunza siku
zote ni lazima ujifanye kuwa mjinga Zaburi 73;22,24 na ni lazima ukubali kufundishwa
na Mungu siku hadi siku Zaburi 143 ;10 Tunapokuwa katika hali ya kukubali
kufundishwa ndipo tunapata nafasi ya kumpendeza Mungu Zaburi 25;4-5,Yohana 6;45
Isaya 54;13 Kuangamizwa kwetu kunatokana na kukosa maarifa Hosea 4;6 kwa msingi
huo ni lazima tukubali kufanya sehemu yetu na kukubali kujifunza Neno la Mungu
na kamwe tusikubali kulizoea Neno kila siku kubali kujifunza kana kwamba ndio
unaanza sasa ukifanya hivyo ushindi utakuwa ni wako.
·
Kumfanya
asongwe na shughuli za dunia na udanganyifu wa mali.
Mathayo 13;22 tunajifunza mfano wa mbegu zilizoangukia
kwenye miiba kuwa ni watu wanaoshindwa kukua kiroho kwa sababu ya kushindwa
kudumu katika neno na kusongwa na shughuli za dunia na udanganyifu wa mali, kwa
msingi huo ni lazima uwe mwerevu katika mema fahamu kuwa lolote lile
linalokuzuia kujifunza Neno la Mungu wakati mwingine ni kifungo cha kukufanya
usikue kiroho na huyo ni adui 3Yohana 1;2 Mungu anapenda tufanikiwe katika
mambo yote lakini msingi wa mafanikio ya
kweli huanzia rohoni na ndio maana Yesu alisema tutafute kwanza ufalme wa Mungu
na haki yake na mengine yote tutazidishiwa
Mathayo 6;33 kumbuka kuwa haitakufaidia kitu kama utaupata ulimwengu
mzima na kupoteza nafsi yako ? Marko 8;36 ni muhimu kufanya kazi na
kujishughulisha kwani Biblia inasema asiye fanya kazi kula na asile lakini ni
muhimu kutokutawaliwa na utafutaji wa mali na kujikosesha mambo ambayo ndio
msingi wa baraka za mwili pia kwa kila jambo kuna majira yake Muda wa ibada uwe
ibada na Muda wa kazi na biashara na uwe muda wa kazi na biashara Muhubiri 3;1
kwa msingi huo wakati wa kipindi cha neno acha shughuli zako nyingine maana
neno la Mungu ndio uhai wa maisha yetu hivyo ni muhimu likapewa kipaumbele.
·
Kuwafanya
watu wawe wanatoa udhuru wakati wote wanapohitajika kwenda kwenye neno
Una weza kushangaa kuwa siku za ibada ya kujifunza
maneno ya Mungu ndio kunatokea sababu kadhaa wa kadhaa ili mradi tu kukufanya
usione umuhimu wa kuja kujifunza neno la Mungu inapotokea hali hiyo fahamu kuwa
ni hila za adui Luka 14;16-20 Yesu
alitoa mfano wa watu walioalikwa harusini lakini kila mmoja alionekana ana
sababu za msingi za kumfanya asihudhuria sherehe ile hali iliyomuudhi mwenye harusi Luka 14;33
Yesu alihitimisha kwa kuonya kuwa “basi kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha
vyote alivyo navyo hawezi kuwa
mwanafunzi wangu”
·
Kumletea
mtu dhiki au udhia kwa ajili ya wokovu.
Mathayo 13;20-21 ni mfano wa Yule aliyepandwa kwenye
miamba kwa kukosa mizizi inapotukia
dhiki huchukizwa , hiii ni mbinu nyingine ya adui ili kwamba aweze kuwakatisha
watu tamaa ya kujifunza neno la Mungu kisha wafe kiroho inakupasa kuvumilia
yanapotokea magumu na wala uusiliache
neno la Mungu heri ni wale wanaostahimili
Mathayo 5;11-12,1Petro 4;12-16 Yakobo 5;10
·
Kukufanya
utafute mafundisho yaliyo karibu na nyumbani
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati mwingine
shetani anaweza kuleta ushawishi unaoonekana kama wenye busara kwa kukushawishi
kufuata mafundiho yanayopatikana karibu na nyumbani ili kukupeperusha kwa kupenda njia ya mkato Mungu alipandisha
Israel kutoka Misri aliwapitisha katika njia iliyo ndefu na ya mbali kwenda
kanaani Kutoka 13;17-18 si vibaya kusali karibu na nyumbani kwako kama wana
mafundisho mazuri lakini ni vema kukaa na wale waliokuzaa kiroho kwani hao ndio
wana uchungu na wewe na pia endapo mafundisho ya mahali hapo ni dhaifu basi ni
afadhali kwenda mbali kwa faida ya roho yako
hekima ya Mungu wakati mwingine hutafutwa kwa gharama Mathayo 12;42
ukitaka ukue kiroho wakati mwingine uwe kama
malikia wa sheba.
Umuhimu wa kunywa maziwa Yasiyoghoshiwa Incorrupt Gospel 1Petro 2;2
Maziwa yasiyoghoshiwa ni neno la
Mungu halisi lisilochanganywa na chochote, neno la Mungu ambalo limechanganywa
na mapokeo ya wanadamu halifai katika malezi ya kiroho, baada ya kuokolewa kama
utakuweko mahali ambapo neno la Mungu linachanganywa na mapokeo ya wanadamu
mahali hapo panaandaa mauti yako ya Kiroho, ni muhimu kwako kukaa mahali ambapo
unajifunza Neno la Mungu safi lisilochanganywa na mapokeo ya kidini kwani hayo
ni sumu ya kuua watu wa kirohon kaa mahali penye mafundisho ambayo ni neno la
Mungu halisi.
Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi wagalatia 4;19-20
Neno la Mungu linatufundisha kuwa
Mzazi wa kiroho kama ilivyo kwa mzazi wa kimwili anakuwa na uchungu wa mtoto
wake kuliko Yule asiyekuzaa ili uweze kupata huduma nzuri kaa na wale
waliokuzaa kiroho wao wana uchungu wa kweli kwaajili yako, hudhuria ibada hapo
njoo na kalamu na daftari andika mafundisho yote unayojifunza ukijua ya kuwa
nawe utakuwa kiroho na kuwa mwalimu wa wengine huo ndio mpango wa Mungu kwaa
jili yako Ubarikiwe.
Barikiwa sana mafundisho no mazuri, nmeyapenda
JibuFutaUbarikiwe sana nimebarikiwa sana!
JibuFutaSomo zuri
JibuFuta