Alhamisi, 11 Februari 2016

Mfululizo wa Masomo yahusuyo Uongozi wa Kanisa 6



******************************************************************
                                               Somo; Jinsi ya kuliongoza kanisa
Tunaendelea kujifunza Mfululizo huu wa Masomo maalumu yahusuyo uongozi na sasa tunajifunza somo hili Jinsi ya kuliongoza kanisa la Mungu tutajifunza somo hili pia kwa kuzingatia vipengele viwili

*      Hatari ya kuwa na Viongozi vipofu katika kanisa
*      Jinsi ya kuliongoza kanisa.

Hatari ya kuwa na Viongozi vipofu katika kanisa
     Ni hatari kubwa kama tutakuwa na Viongozi vipofu katika kanisa. kipofu alimuongoza kipofu mwenzake watatumbukia shimoni wote wawili Luka 6;39 kwa kukosa akili au Ufahamu wa jinsi ya kuliongoza kanisa sisi nasi tunaweza Kuhesabiwa miongoni mwa vipofu Mathayo 15;14-16 ilitupate Ufahamu wa kutosha kuhusu kuliongoza kanisa tutachukua muda mwingi katika somo hili kujifunza mambo kadhaa wakadhaa yahusuyo jinsi ya kuliongoza kanisa.
Jinsi ya kuliongoza Kanisa.
      Yako mambo kadhaa ambayo ni muhimu kuyaangalia na kuyazingatia kwa makini ili tupate mafanikio yanayokusudiwa katika kuliongoza kanisa
  1. Kujiamini.
Mungu anapokuwa ametuchagua kuliongoza kanisa tunaweza kujikuta kuwa tuna umri mdogo kuliko wale tunaowaongoza, hii sio ajabu Musa alikuwa mdogo kuliko kaka yake Haruni Lakini ni Mungu aliyemchagua Musa aliye mdogo kumuongoza kaka yake Kutoka 7;7 sio hilo tu Mungu aliwachagua Viongozi waliokuwa na umri mdogo mno  na Biblia inaonyesha kuwa wengi kati ya hao waliongoza vizuri na kwa mafanikio makubwa  Mfano ni Yoashi aliyeongoza akiwa na miaka saba 2Nyakati 24;1-2 Yosia alinza kuwa kiongozi akiwa na umri wa miaka nane 2 Nyakati 34;1-2 Uzia alikuwa na umri wa miaka 16 2Nyakati 26;3-4 Yothamu na Hezekia woote walikuwa na umri wa miaka 25, 2Nyakati 27;1-2,29;1-2. Timotheo naye alikuwa kijana mdogo tu kama Yeremia alipoanza kuongoza 1Timotheo 4;11-12,Yeremia 1;4-7 tunaweza kuwa sio tu na umri mdogo Lakini pia Elimu ndogo kuliko wale tunaowaongoza hii pia sio ajabu Viongozi wakubwa wa kanisa, Petro na Yohana  walikuwa ni watu ambao walikuwa hawana Elimu wala maarifa  Matendo 4;13 lakini waliifanya kazi ya Mungu kwa ujasiri na kuliongoza kanisa. Hatupaswi kamwe kujidharau wala kubabaika  kutokana na vigezo hivyo vya kibinadamu tunapaswa Kujiamini na Mungu atawatiisha chini yako wazee na wasomi nao watakusikiliza  kumbuka kuwa si sisi tuliojichagua wenyewe na kuwa ni Mungu ndiye aliyetuchagua hivyo yu aweza kutupa uwezo wa kuongoza na kulisimamia kanisa lake Yohana 15;16,Zekaria 4;6;Wafilipi 4;13 kwa sababu hiyo yeye aliye dhaifu na aseme mimi ni Hodari maana uhodari wetu uko katika Bwana  aliye tuwezesha maana amesema atakuwa pamoja nasikatika utumishi wetu woote Yoel 3;10, 1Nyakati 28;20, Mathayo 28;19-20.
  1. Kuwa na utii uliotimia kwa Viongozi wetu wa juu.
    Uasi wa namna yoyote kwa kiongozi wetu wa juu unamfanya Roho Mtakatifu atuache, wakati wowote ni muhimu kwa Viongozi wa kanisa kuhakikisha kuwa wanawatii Viongozi wao wa juu na wajuu wanawatii wale wa juu, utii huu ni kama ule utii wa jeshini  ni utii usio na ubishi wala majadiliano  hata kama moyoni unadhani kuwa agizo hilo lina dosari, mradi sio agizo la kufanya dhambi  ni muhimu kulitii kwanza  tukijiona kuwa tuna kitu chochote cha ziada kuliko kiongozi wetu wa juu  na kuacha kumtii basi Roho Mtakatifu anatuacha Barnaba alipoacha kumtii kiongozi wake Paulo na kushindana naye kuanzia hapo Roho wa Mungu aliacha kutupa historia yake akiwa na Marko Bali Roho anatupa ripoti ya Paulo na wale aliofuatana nao katika utumishi yaani Silla na Timotheo Matendo 15;36-41,16;1-3 kama Viongozi wa kanisa tunataka kuona Roho wa Mungu akiwa pamoja nasi na kututumia katika viwango vya kupita kawaida basi siri ni utii uliotimia 2Koritho 10;4-6.na tatizo la Viongozi wengi katika makanisa ya kiroho shida yao kuu ni kukosa utii na hasa utii uliotimia, Viongozi wengi watataka kufanya kazi kwa kusukumwa sukumwa tu na kwa msingi huo utendaji wa Mungu na karama za Roho Mtakatifu hufifia Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa mtii na kuzidi katika  Yesu
  1. Kuwaongoza watu kwa kutumia maombi
    Kiongozi wa kanisa hana budi kuwa mtu muombaji siku zote akiwaombea wale anaowaongoza kwa kuwataja  majina na kuwaombea juu ya udhaifu walio nao, tukiwa tunapenda kufoka tu bila maombi ya kutosha  pamoja na kufoka kwetu sana tutaona mambo hayatendi kama inavyokusudiwa Yeremia 31;9 kuomba ni kumhudumia bwana inatupasa kumhudumia bwana zaidi kabla ya kuwahudumia watu tunao waongoza ili tuone mafanikio maombi ni kama mafuta yanayolainisha msuguano au ugumu wa mioyo ya watu tunaowaongoza bila maombi ya kutosha kanisa letu haliwezi kukua kiidadi na pia wale tunaowaongoza hawawezi kukua kiroho na watadumaa  kadiri mtu anavyopewa majukumu makubwa ndivyo anavyopaswa kuomba zaidi maombi husaidia kunyonya kiburi cha kibinadamu tukipenda kuwahudumia watu bila maombi ya kutosha ni rahisi kujidhuru  kiroho sisi wenyewe
  1. Kuacha kuongoza pale tunapokuwa vipofu.
     Katika sheria za usalama barabarani  dereva anashauriwa kusimamia ikiwa haoni vizuri mbele kutokana na ukungu au moshi n.k vilevile dereva anashauriwa kuegesha gari pembeni  na kulala ikiwa anaona usingizi  Dereva akipuuzia ushauri huo ni rahisi kupoteza maisha  vivyo hivyo kama Viongozi wa kanisa hatupaswi kumshauri mtu kitu ambacho hatuna uhakika nacho tukiwashauri watu makosa tutapata adhabu iliyo kubwa zaidi  Yakobo 3;1,Mathayo 18;6-7 lolote lile tusilokuwa na uhakika nalo ni vema kuulizwa kwa uongozi wa juu zaidi kisha kutoa majibu yapasayo  hivyo ni muhimu kuacha kufanya jambo lolote tusilolifahamu vema.

  1. Kuongoza kwa neno la Mungu
      Tukiona lolote kwa wale tunaowaongoza lisilofaa inatupasa kutumia neno la Mungu  kulirekebisha kwa upendo na sio Maneno matupu ya kibinadamu Neno la Mungu lina uwezo mkubwa wa kumbadilisha mtu wala sio adhabu zetu au Maneno yetu ya kuumiza mwanadamu huwezwa na Mungu tu Maneno ya kibinadamu husukumia tatizo kuzidi Mithali 6;21-23; 2timotheo 3;16-17,4;2.
  1. Kutokubali kuvunjika moyo.
      Adui Ibilisi humwandama kiongozi wa kanisa na kutumia kila aina ya mbinu ili kumvunja moyo, iwe ni kwa matatizo ya kikazi, kifamilia au kibiashara, kusengenywa, kunenewa vibaya kwa kila aina ya Maneno, n.k  na wakati mwingine atatuonyesha hali za kutokufanikiwa kwa njia mbalimbali hata kukuonyesha jinsi kanisa lako lisivyokua  na atakushauri ni afadhali uache  yamekushinda  kamwe hatupaswi kusikiliza ujinga huo na kukubali kuvunjika moyo kwa lolote hata kama tuna watu waili au mmoja katika kanisa Endelea kuwalisha kwa uaminifu na tudumu katika kazi ya bwana kwa uaminifu kwani kuna majira ya kupenda na kuvuna Matendo 21;9-14 Zaburi 126;5-6 Muhubiri 3;1-2 marufuku kukata tamaa tusikubali kuvunjika moyo kwa namna yoyote.
  1. Kuongoza kwa Hekima.
     Ni vigumu kuongoza kanisa la Mungu huku hatuna Hekima Hekima inatusaidia kujua kuwa tuseme nini, tujibu nini au tufanye nini na kwa wakati gani  Hekima ya Mungu ndio ufumbuzi wa tatizo hilo na hufumbua kwa amani Hekima humfanya mtu ajue neno la kuzungumzia wakati Fulani na sio kuropoka tu na kusababisha matatizo zaidi Mithali 25;11-12 kwa Hekima tunaweza kuwapa watu Elimu ya Mungu Mithali 16;21 hekima hutupa kujua jinsi ya kuwashughulikia wazee Tofauti na vijana n.k 1Timotheo 5;1 kwa sababu hii Suleimani alipofanywa kuwa mfalme   jambo la kwanza lilikuwa ni kuomba Hekima sisi na si ni muhimu kumuomba mungu atupe Hekima  kila siku katika shughuli zetu za maongozi 2Nyakati 1;7-10,Yakobo 1;5.
  1. Kufanya kazi ya Mungu kwa bidii.
     Hatuwezi kuwa na mafanikio makubwa katika kazi yoyote ya Bwana kama sisi wenyewe ni watu wavivu au walegevu inahitajika bidii kubwa ili kufanikiwa Yeremia 48;10 Warumi 12;11 hata hivyo ni muhimu kukumbuka kuwa na vipindi vya mapumziko na kukumbuka kula chakula vizuri ili tusimpe ibilisi nafasi Marko 6;31-33.
  1. Kumbuka kuwaita moyo wale tunaowaongoza.
     Kiongozi wa kanisa hapaswi kuwa mtu wa kuchokonoa mabaya tu ya kondoo wake na kutaja mapungufu yao tu inatubidi pia kutafuta yale yaliyo meme hata madogo na kuyainua hayo na kuwaita moyo na kuwapongeza kwa kawaida pongezi humtia mtu moyo wa kufanya vizuri zaidi na husaidia kuondoa makosa makubwa ya mtu na kufanya bidii zaidi 2samuel 11;22-25,Kumbukumbu 3;28.
  1. Kutangulia mbele ya Kondoo
     Mchungaji hutangulia mbele ya kondoo wake kuongoza , hii maana yake ni kuongoza kwa mfano huku ndio kuongoza kunakoleta mafanikio makubwa kiongozi anayechelewa kufika mahali pa ibada na kuonyesha udhaifu Fulani Fulani  huyo sio kiongozi anayewatangulia kondoo Yohana 10;4 Waamuzi 5;2 Marko 10;22-25 Kumbukumbu 3;28.
  1. Kuwa na utayari wa kuwapa wengine majukumu
     Kiongozi aliye botra hafanyi kazi yeye mwenyewe bali huwa tayari kuwapa wengine majukumuhususani wale anaowaongoza na wakati mwingine hata wale wachanga Kutoka 18;13-17.
  1. Kuheshimu mipaka ya madaraka uliyo nayo.
     Mithali 22;28 ni muhimu kutakuwa na kimbelembele kwa mambo yasiyohusiana na madaraka uliyo nayo fanaya kazi ndani ya mipaka yako mfano kama wewe sio msomaji wa kanisa usipendelee kuzungumzia lolote kuhusu kanisa acha wenye mamlaka kuu zaidi wazungumzie.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni