Alhamisi, 11 Februari 2016

Mfululizo wa Masomo yahusuyo Uongozi wa Kanisa 5



*********************************************************************
                                        Somo ; Wito wa kumtumikia Mungu
      Somo tunalojifunza sasa katika Mfululizo wa Masomo maalumu ya shule ya uongozi ni Wito wa kumtumikia Mungu hili ni moja ya Masomo muhimu sana na tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitano vifuatavyo;-

*      Mafundisho ya msingi kuhusu wito wa kumtumikia Mungu
*      Aina tatu za wito wa kumtumikia Mungu
*      Njia Tofauti za kuteuliwa katika kushika nafasi za uongozi wa kanisa
*      Aina ya watu wanaoitwa na Mungu
*      Neema ya kuwekewa mikono katika Mpango wa Mungu

Mafundisho ya msingi kuhusui wito wa kumtumikia Mungu
Wako watu wengine katika kanisa la Mungu ambao kwa kukosa Ufahamu husema hawawezi kukubali kumtumikia Mungu au kukubali nafasi yoyote ya uongozi katika kanisa kwa madai kuwa eti mpaka wasikie Sauti halisi ya Mungu ikiwaita katika utumishi huo, huku ni kukosa Hekima na sio sahihi Wito wa kumtumikia Mungu sio lazima uambatane na kuisikia sauti halisi ya Mungu Elisha hakusikia sauti ya Mungu alipoitwa ni Eliya alipita karibu naye na kumtupia vazi 1Falme 19;19-21 pamoja na hayo Mungu alikuwa pamoja naye na alimtumia kwa upako maradufu kuliko Eliya, Yoshua hakusikia pia sauti ya Mungu  bali alitwaliwa na Musa na kuwekewa mikono Hesabu 27;22-23 pamoja na hayo Yoshua alikuwa mtumishi wa Mungu wa kipekee, upande mwingine pia wako watu ambao hujipachika majina makubwa kama Mwinjilisti, Mwalimu, Mchungaji n.k bila ya kuwa na wito maalumu wa kuwafanya wawe na nafasi hizo watu wa jinsi hii hufanya makosa na wanapojaribu kufanya kazi hizo kamwe hawawezi kupata matokeo mazuri mfano wa kibiblia ni kwa AHIMAASI mwana wa Sadoki na mkushi mmoja  Ahimaasi alikuwa na moto wa kijipachika cheo cha kuwa mchukuwa habari na kufikiria kuwa ni swala la kuwa na ubingwa wa kupiga mbio na ni kweli alikuwa wa kwanza kufika kwa mfalme  Lakini alipofika na kuulizwa habari alibabaika tu na hakuwa na ujumbe maalumu kama ilivyokuwa kwa mkushi aliyekuwa na wito maalumu wa mchukua habari 2Samuel 18;19-33. Awaye yote anayetaka kumtumikia Mungu ni muhimu kuwa na wito.
Aina tatu za wito wa kumtumikia Mungu
Ziko aina kuu tatu za wito kuelekea katika kumtumikia Mungu
1. Wito wa jumla katika wokovu- huu ni wito ambao mtu huitwa kutoka dhambini na kusamehewa dhambi ili apate kumuabudu Mungu  na ili kuurithi uzima wa milele hata hivyo wito huu huambatana na wito wa jumla wa kumtumikia Mungu yaani Mungu anapokuwa amekuokoa anataka pia umtumikie
2. Wito wa jumla wa kumtumikia Mungu- Mtu hawezi kuingia katika wito wa jumla wa kumtumikia Mungu kabla hajaokoka, Lakini punde mtu huyo anapokuwa ameokolewa anakuwa ameitwa katika wito wa jumla wa kumtumikia Mungu na wito wa kuyaishi maisha matakatifu Waefeso 4; 1,1Petro 1; 15-16 kila mtu aliyeokoka amepewa wito wa kuenenda ulimwenguni mwote na kuihubiri injili kwa kila kiumbe Mathayo 28;19-20 Marko 16;15 wito huu ni kwa jinsia zote, Nyakati za kanisa la kwanza watu woote waliitikia wito huu pale walipotawa nyika na kwenda huko na huko wakiwaacha mitume pale Yerusalem Matendo 8;1,4. Hivyo kila mtu aliyeokoka bila hata ya kungojea sauti ameitwa katika wito huu wa kumtumuikia Mungu
3.Wito maalumu wa kumtumikia Mungu- wito huu hutolewa na Mungu kwa Mtu maalumu  ili kufanya utumishi Fulani wa kimaongozi katika kanisa  wakati mwingine wito huu utaambatana na karama maalumu zitakazomwezesha mtu huyo kulitimiza Jukumu alilopewa kwa ufanisi .Yusufu alipewa wito maalumu wa kuhifadhi roho za watu na maisha yao wasife kwa njaa na alipewa karama maalumu za kutafasiri ndoto Mwanzo 45;5-8 wito huu ulioambatana na karama hizo maalumu  ulimuwezesha kuwa waziri mkuu katika inchi ya Misri, Esta 4;15-16 alikuwa na wito maalumu wa kuliokoa taifa la kiyahudi lisiangamizwe na aliwezeshwa kuwa tayari kuangamia  au kukutana na magumu ya aina yoyote ile hivyo ili mtu awe Mtume, Nabii, Mwinjilisti, Mchungaji au Mwalimu lazima wito wake uambatane na neema maalumu itakayomwezesha kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi wa kipekee, aidha wito maalumu pia huambatana na mtu kuwa mwaminifu katika kutekeleza wito wa jumla wa utumishi kabla ya kuingia katika wito maalumu wa kumtumikia Mungu Matendo 13;1-3 Barnaba na Sauli walikuwa waaminifu sana katika wito wa jumla wa kumtumikia Mungu kabla hawajaitwa katika wito maalumu wa kumtumikia Mungu baada ya kupewa wito maalumu huduma zao zilibadilika kabisa. 
Njia Tofauti za kuteuliwa katika kushika nafasi za uongozi wa kanisa
  1. Kujipachika mwenyewe uongozi
Hii ni sawa na ule mfano wa Ahimaasi mwana wa Sadoki 2Samuel 18;19-33 na tuliona kuwa matokeo yake haya kuwa mazuri, Uzia alijipachika kufanya ukuhani na matokeo yake alipatwa na ukoma na kufa 2Nyakati 26;16-23 kora na wenzake hawakuwa tayari kuwa chini yza Musa yeye na wenzake wakataka na ukuhani matokeo yake walipoteza hata nafasi ile waliyokuwa nayo wakafa kifomcha aibu Hesabu 16;1-35 ni hatari kubwa mtu kijipachika uongozi katika kanisa.
  1. Kuchaguliwa na wanadamu bila kufuata uongozi wa Roho mtakatifu.
Kiongozi wa kiroho kamwe hachaguliwi kwa kupigiwa kura au baada ya kufanya kampeni nyingi kama za kisiasa,tunaweza tukampigia kura mwanadamu Fulani na ikawa Bwana hakumchagua huyo Baada ya Mathiya kupigiwa kura na kushindwa kwa kura katika Matendo 1;23-26 hatuoni  jina lake likitajwa tena katika Biblia najua kuwa Vitabu vya kihistoria vinaeleza kazi alizozifanya  Lakini hatuoni tendo la upigaji kura likirudiwa tena katika agano jipya Mungu ndiye anayechagua Viongozi katika 1Samuel 16;6-7 Samuel alimchagua Eliabu Lakini Bwana hakuwa amemchagua huyo, Ni marufuku kuchagua kiongozi wa kanisa kwa kumpigia kura swala hili limeleta migogoro mingi katika makanisa Kiongozi wa juu wa kiroho ndiye anayechagua  Viongozi walio chini yake  kwa kuongozwa na Roho wa Mungu Luka 6;12-16 Matendo 15;40-41;14;23;Toto 1;4-5 au Mungu kusema Kupitia Roho Mtakatifu Matendo 13;1-3.


  1. Kuchaguliwa na Mungu Mwenyewe.
Mungu anaweza kuchagua mwenyewe Viongozi mbalimbali wa kanisa Yeremia 1;15 Hata hivyo Mungu anapochagua mwenyewe huduma ya mtu huyo itakuwa dhahiri katika kanisa na kutakuwa na udhihirisho wa wazi wazi  unaothibitisha kuwa huduma ya mtu huyo imetoka kwa Mungu
  1. Kuchaguliwa na Mungu Kupitia watumishi wake.
Yoshua alichaguliwa na Mungu Kupitia mtumishi wake Musa Hesabu 27;16-18.elisha alichaguliwa na Mungu Kupitia Eliya 1Falme 19;15-16 Paulo mtume alimchagua Silla  kwa uongozi wa Mungu Matendo 15;40 halikadhalika Viongozi wengi wa Nyakati za kanisa la kwanza walichaguliwa na watumishi wa Mungu kwa uongozi wa Mungu Matendo 14;23,Tito 1;4-5 kwa msingi huu basi Mchungaji akimchagua mtu kuwa kiongozi wa kanisa la nyumbani sehemu au zone au kuongoza idara nyingine yoyote hufanya hivyo kwa uongozi wa Mungu na hivyo mtu huyo aliyechaguliwa hakujitwalia mwenyewe heshima hiyo Waebrania 5;4 na anakuwa ameitwa na Mungu.
Aina ya watu wanaoitwa na Mungu
     Mungu katika Hekima yake huwaita watu wengi wasio na Hekima ya mwilini au wasio na nguvu wasio na cheo au wanaoonekana kuwa wapumbavu na dhaifu wanyonge na wanaodharauliwa ili adhama na sifa kuu ya uwezo wa iwe ya Mungu mwenyewe na sio ya mtu yule dhaifu 1Koritho 1;26-29, 2Koritho 4;7 hivyo hatupaswi kujiona kuwa hatufai Kuchaguliwa . Musa alikuwa na kigugumizi, Yeremia alikuwa mtoto n.k sisi nasi tunaweza kujiona kuwa tuna mapungufu Fulani wakati Mungu anapotuita kwenye utumishi hayo yasikukatishe tamaa kwani yeye ndiye atakaye tuwezesha si kwa nguvu wala kwa uwezo bali kwa Roho wangu asema Bwana wa majeshi Zekaria 4;6 Warumi 9;16.
Neema ya kuwekewa mikono katika Mpango wa Mungu.
     Tunapochaguliwa kuwa Viongozi wa kanisa na kuwekewa mikono na yule aliyetuchagua kuwa Viongozi kwa uongozi wa Mungu Sehemu ya heshima yake na uwezo wake aliopewa hutushukia Hesabu 27;18-23. Yoshua baada ya kuwekewa mikono na Musa  alibadilishwa kabisa na watu wakamuheshimu Kumbukumbu 34;9.Kuwekewa mikono namna hiyo huchochea karama zilizofichika ndani yetu na kizifanya zijitokeze 2timotheo 1;6 Kwa msingi huo Mchungaji anapotuwekea mikono ili tuwe Viongozi wa Makanisa na idara na sehemu nyinginezo sehemu ya uwezo aliopewa huja kwetu na kutusaidia kikamilifu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni