Jumapili, 7 Februari 2016

MUHAMAD NA YESU KRISTO MKUBWA NANI?


Hapo juu tulikuwa na swali upi ni muongozo wa Mungu wa kweli Quran au Biblia? Swali lile lilikuwa tamu maana tuliona jinsi qurani inavyokiri yenyewe kuwa Biblia ni Muongozo wa kweli,swali hilo halina tofauti na hili tunalojiuliza sasa isipokuwa tu hili la sasa ni gumu zaidi lakini ni muhimu likajibiwa tena mapema kwani kizazi hiki ni kizazi chenye utafiti mkubwa na kinachotatizwa sana na ukweli uko wapi?Kati ya viongozi hawa wakubwa ambao wameanzisha dini na hatimaye wamefanikiwa sana na wana wafuasi wengi sana duniani je katika hawa mkubwa nani? nani anastahili heshima na kuaminiwa?tutaangalia mambo ya msingi ya maisha yao.

   Ufahamu kuhusu kuzaliwa kwa Muhamad na kuzaliwa kwa Yesu.
Katika somo nyeti kamahili ni vema tukaanza kuchambua maisha ya viongozi hawa polepole na taratibu kiasi cha kumsaidia kila mmoja aweze kuelewa yampasayo kuelewa Muhamad alizaliwa akiwa na Baba na mama kama mtu wakawaida,babae aliitwa Abdallah na mamae aliitwa Amina hivyo Muhamad alikuwa mtu wa kawaida,hatuambiwi kuwa alitabiriwa na manabii,alitangazwa na malaika au neno la Mungu hapana!Tena wazazi wake waliabudu sanamu nayeye mwenyewe wakati wa utoto wake aliabudu sanamu zilizokuwepo pale al-kaaba(soma maisha ya Muhamad uk 5kifungu cha mwisho).
     Yesu hakuzaliwa kwa njia ya kawaida kama watu wengine alizaliwa kwa uwezo wa Roho mtakatifu wa Mungu,alichukuliwa mimba na bikira Mariam tendo hili pekee linamfanya Yesu asiwe wa kawaida yeye ni Roho iliyotoka kwa Mungu hivi ndivyo Quran isemavyo (an – nisaa 4;171) Yesu ni muujiza kwa ulimwengu (al-anbiyaa 21;91)Yesu ni roho inayotokana na Mungu (tahryym 66;12) Malaika alimtangazia Mariam habari njema kutoka kwa mungu kuwa yeye angemzaa Yesu (al-imran 3:45),alizaliwa mtakatifu bila dhambi (Maryam 19;19)Kwa hivyo quran inatupa ushahidi kuwa Yesu hakuwa mwanadamu wa kawaida alipozaliwa alipelekwa hekaluni na wazazi wake walikuwa wacha Mungu.

  Ufahamu kuhusu heshima ya Muhamad na Heshima ya Yesu
Katika quran Tunasoma moja ya heshima aliyopewa Yesu masihi hata kabla hajazaliwa katika (al-Imran 3;45)Tunaona kuwa Yesu ana heshima huko Mbinguni na Duniani na kuwa Yu karibu na Mungu,pia anaitwa Neno (au Tamko)la Mungu(al-Imran3;45 na nisaa4;171)Manabii wote walipewa au kuamriwa kuusema neno la Mungu,Lakini yesu sio kuwa alisikia au kuamriwa bali yeye Mwenyewe alikuwa Neno la Mungu maana yake ndani yake kulikuwa na Mamlaka kamili ya neno la mungu lenye nguvu ya kuumba, kuhuisha, kusamehe kufariji na kutia Nguvu mpya (Yohana 1;1-3,14). Quran haituambii popote kuwa Muhamad alikuwa ni neno la Mungu, lakini alikuwa tu akipokea aya (wahy) kupitia malaika na kuzikariri kwa wasikilizaji wake, mama yake hajapata kujulishwa juu ya kuzaliwa kwake, Wala hakujazwaRoho mtakatifu kama ilivyokuwa kwa Mariam ambae quran inasema alitukuzwa kuliko wanawake woote soma (al-imran 3;42).
    Jina Mariam limetajwa mara 34 katika Quran ambapo jina la mama wa Muhamad halikutajwa hata mara moja, tunaambiwa muhamad alipomuombea mama yake aliyekuwa ameshakufa mungu alimkatalia ombi lake jambo lililomfanya alie kwa uchungu sana

Ufahamu kuhusu maisha ya dhambi kati ya Muhamad na Yesu masihi
Inasimuliwa katika hadithi kwamba siku moja wakati wa utoto wa Muhamad,Malaika wawili walifika wakamchukua kando na wakampasua kifua na kusafisha moyo wake kwa maji ya zamzam,Wanazuoni wa kiislamu kwa kuzingatia kifungu hiki katika Quran (surat alm-Nashrah 94;2-5). Baada ya kuondolewa Dhambi (mizigo mizitomizito) ndipo akaambiwa ajipendekeze kwa Mola wake (aya ya 8).
     Kwa upande wa Yesu masihi  alikuwa mtakatifu tangu kuzaliwa (Maryam 19;19)Maulaamaa na wanazuoni wa kiislamu wanakubali kuwa neno Mtakatifu sana linalotumika katika aya hiyo hapo juu maana yake ni kutokuwa na waa lolote au dosari au dhambi,Yesu alimpendeza Mngu na wanadamu (Luka 2;52),wanazuoni hao wa kiislamu ni pamoja na  al-Tabari,al-Baidan na al-Zamakhshari.Quran imeshuhudia kuwa manabii mbalimbali walitenda dhambi isipokuwa Yesu peke yake,Muhamad alikiri wazi mara tatu katika Quran kwamba alilazimika  kuomba msamaa kwa Mungu allah(al-Muumin 40;55.Muhamad 47;19,al-Fat’h 48;1-2.)
     Hivyo tunahitimisha kifungu hiki tukiwa na uhakika wazi kuwa Muhamad alikuwa wa kawaida kama wanadamu wengine wowote,aliishi maisha ya kawaida kama mwanadamu mwengine wowote,alikuwa mwenye dhambi na alitenda dhambi na ndio maana aliomba asamehewe,Bali Masihi alizaliwa kwa uwezo wa Roho mtakatifu,alikuwa ni Neno la Mungu .alizaliwa pasipo kufanya dhambi,aliishi maisha matakatifu bila kufanya dhambi jiridhishe kwa kusoma (Yohana 8;46,2Korithian 5;21,Ebrania 4;15,1Petro2;22,1Yoh 3;5)

 Ufahamu kuhusu Ishara na miujiza Aliyotenda Muhamad na aliyotenda Yesu Kristo.
     Bado tunaendelea na utafiti wetu kutaka kujua Muhamad na Yesu mkubwa nani, tukimpata huyo tutakuwa tunamsikiliza zaidi kama Tulivyopata kitabu ambacho ni muongozo wa kweli wa Mungu sasa Tunatafuta Nabii ambae tutamuamini na kumsiliza zaidi.
   Wasomi na waalimu wa Kiislamu wanadai kwamba miujiza pekee ambayo Mungu alimpa Muhamad imejidhihirisha kwenye aya zaQuran, Hii ina maana ishara na mijiza ya Muhamad ilikuwa ni maneno tu na sio vitendo!
  Kama hivyo ndivyo mimi sioni ajabu kwani manabii wengi walipewa vitabu na aya hata wanafunzi wa Yesu kama Yohana alipewa kitabu cha ufunuo namna wanavyopokea aya hizo ni vilevile
  Lakini Quran Inamshuhudia Kristo kwamba alikuwa na uwezo wa pekee wa kuponya wagonjwa,hakulaani,wala kuhukumu,alikuwa na huruma na upendo na rehema,Uweza wa kimungu ulidhihirika kwake kwaIshara na miujiza mingi ambayo aliifanya waziwazi, Quran inasema aliwezesha vipofu kuona bila dawa na aliponya kwa kutamka maneno yake yenye uweza na nguvu kuu Maryam 19;31,Mungu alimfanya mbarikiwa popote alipo yeye ni chemchem ya uzima na Baraka kwa watu woote wa vizazi vyoote (al-Imran 3;49 na al-Maida 5;110) aliwaponya wenye ukoma,Alifufua wafu,aliumba ndege na yule ndege akawa hai al Imran 3;49,alilisha watu kwa mikate al-Maida 5;112-115,Yesu alijua siri za Mungu huku Muhamad alikiri kuwa hajui siri za ndani za Mungu isipokuwa yale yale ambayo alidai kwamba amefunuliwa na Mungu al- Imran 6;50,Lakini Kristo yeye ni tofauti Muhamad mwenyewe ameshuhudia kuwa Kristo alijua siri al-Imran 3;49 Aidha quran inatuambia kwamba Kristo alileta sheria iliyojaa neema na hekima,aliwaruhusu watu wake kula vyakula vilivyokatazwa katika sheria ya Musa sawa na Mathayo 15;19 Qurani inathibitisha kuwa Kristo alikuwa na mamlaka ya pekee na kukiri kwamba hakuwa na sababu ya Kuwa chini ya sheria bali alikuwa juu ya sheria na mkamilishaji wa sheria ( Imran 3;50)Muhamad alishauriwa kuwa kama anaona shaka  juu ya hayoaliyoteremshiwa basi awaulize  wakristo na wayahudi yaani waliopewa kitabu  kabla yake soma Yunusi 10;94; Kristo hakuhitaji kutafuta waalimu kuhusu ufafanuzi wa sheria kwani yeye mwenyewe alikuwa ni neno la Mungu Hivyo anapaswa kufuatwa na Watu kumtii Al-Imran 3;50.
Kristo haelekezi wale wanao mfuata Mungu tu Bali anaamuru wamfuate na kuzishika amri zake, qurani inasisitiza na kuwapa majina ya pekee wafuasi wa kristo na kuwaita wasidizi wa Mungu.
 Wale wanaomfuata Yesu quran inasema wamewekewa Upole na Rehema katika mioyo yao Al-Hadyd (Chuma) 57; 27.quran pia imeahidi kuwa Yesu na wale wanaomfuata watawekwa juu ya wale wanaokufuru al-Imran 3;55
     Aidha quran inathibitisha kuwa wanaomfuata Yesu ni wa tofauti na wapekee kati ya wanadamu ni wapole hawaqjivuni wala hawajitakii makuu ona hayo katika Al-maida 5;82,Hii ni sawa kwani Kristo ni mnyenyekevu wa moyo hivyo wamfuatao pia ni wanyenyekevu.  
            
Ufahamu kuhusu Kifo cha Muhamadi na Kristo
 Ibn Hishim ametueleaza kwamba kifo cha Muhamadi kilitokana na homa kali,inasemekana kwamba muhamad alipokaribia kufa alisema kwamba sumu alivyolishwa na Myahudi ndiyo iliyovunja moyo wake,Hii ilitokana na kwamba mjakazi wa kiyahudi (Mtumwa wa kike ambaye Muhamad alitaka kumuoa baada ya kutekwa vitani alikataa) hivyo siku moja alitia sumu kwenye chakula cha Muhamad ambacho alikuwa amemwandalia Mgeni wake ambae alipokula alikufa palepale,Muhamad alipokionja alikitema upesi na baadae inasemekana ndio ilipelekea kifo chake.
     Hata hivyo Kifo cha Yesu Kristo kilitabiriwa wazi kabisa katika quran kwamba  ni kwaajili ya kutimiza mpango wa Mungu wa kuwa baraka  kwa wanadamu wote Surat Al-Imran 3;55 “Nitakufisha Kisha Nitakuinua Kwangu” Ingawa maneno hayo hayaonekani katika Biblia hata hivyo yanathibitisha  kwamba Kristo hakufa  kama wanadamu wa kawaida bali alikufa kwa kusudi na mpango kamili wa Mungu kwa ajili ya amani ya wanadamu (surat Maryam 19;33). Baada ya vifo vyao ni wazi kuwa Muhamad alizikwa Madina na kaburi lake liko pale hadi leo na waislamu wanaamini kuwa roho yake iko mahali pa wafu (yaani Barzakh) ikingoja siku ya hukumu na waislamu woote wanahimizwa kumuombea mtume wao ili kwamba Mungu amrehemu. Bali tunasoma kwamba Mungu alimpaisha Kristo kama alivyomuahidi na anakaa huko mbinguni soma surat al-Imran 3;35 na inathibitishwa ahadi hii katika an-Nisaa 4;158Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake”. Kaburi la Yesu liko wazi kwa sababu hayuko kaburini Amefufuka kama alivyosema kabla hajakamatwa na wayahudi na kuuawa.

Maoni 1 :

  1. Nisawa kwa mtazamo wako pia mtume huja baada ya mtume.hivyo mtume yeyote alie tumwa na Mungu ali stahiki kufuatwa kwa kipindi chote ambacho hajafa na kuletwa mtume mwingine. Anae stahiki kufuatwa mafundisho yake hadi sasa ni Muhammad.kwa maana yeye ndiye mtume wa mwisho.

    JibuFuta