Somo la kumi na nne
Vijana na Nguvu za Mungu
Hakuna jambo linalompendeza
Mungu kama kijana kutembea na nguvu za Mungu,kila Upande ungependa kuwatumia
vijana, Shetani hupenda sana vijana na Mungu hitaji sana vijana,n.k.Biblia
inaonyesha jinsi ambavyo wakati wa
ujana ndio wakati mzuri na unaofaa sana
kwa kujitoa kumtumikia Mungu, Hii haimaanishi kuwa mungu hawapendi wazee au
makundi mengine la hasha ana wapenda
lakini anataka uzee uwe matokeo ya kutembea na Mungu (Muhubiri 12;1-7) Kumkumbuka muumba wetu humaanisha kurudi katika
kusudi la Mungu la kutuumba, shetani hakutuumba; Mungu ndiye aliyetuumba hivyo
ni lazima tuishi kwa kutimiza kusudi lake,Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia
vipengele vitatu vifuatavyo;-
- Kulitumikia shauri la Mungu.
- Vijana na Nguvu za Mungu.
- Vijana na kanisa la Mungu
Kulitumikia shauri la Mungu.
(Matendo 13; 36)Ni muhimu kwetu sisi vijana kuwa makini kuangalia
Mungu anataka nini na kutimiza kile anachokitaka;Roho mtakatifu aliangalia kazi
iliyofanywa na kizazi kilichofuata baada ya Adamu, lakini mambo waliyoyatimiza
yalikuwa ni kuongeza idadi ya watu duniani tu kwa kuzaa, lakini wengi wao
hawakufanya zaidi ya hayo wengi hawakutembea na Mungu (Mwanzo 5;6-21) ni Mtu mmoja tu Henoko yeye alifanya kitu cha ziada
yeye alitembea na Mungu alienda na Mungu (Mwanzo
5;22-24)Mungu anataka watu ambao hawataishi duniani na kuzaa na kuongezeka
tu, bali anataka watu ambao wanaliangalia shauri la Mungu na kulitumikia,
Daudi siku zote alitaka kujua kua Mungu anataka nini na kufanya, Yeye aliitwa
akiwa kijana lakini alitembea na Mungu kwa uhodari, ni lazima tumtumikie Mungu
wetu tukiwa tungali vijana Yeremia,Yoshua,Yesu,nk. walitumika wakiwa vijana tu
Vijana
na nguvu za Mungu
Ni muhimu kufahamu kuwa
hatuwezi kulitumikia kusudi la Mungu Bila nguvu za Mungu, ili tuweze kufanikiwa
kutembea katika utumishi kwa Mungu kila kijana ni lazima azingatie mambo muhimu
yafuatayo ambayo yatachochea nguvu za Mungu maishani mwake kwa nini kwa sababu
tunachangamoto nyingi zinazotuzunguka sisi vijana na Bila nguvu za Roho Mtakatifu
ni vigumu kwetu kukabiliana nazo bila Roho. wake mambo ya muhimu ya
kuyazingatia sisi vijana ni pamoja na;-
- Lazima tusome neno la Mungu.
Biblia inasema neno la Mungu na
likae kwa wingi ndani yenu ni neno linaloweza kutusaidia katika wakati huu wa
changamoto ngumu za kidunia (zaburi
119;9,Yoshua 1;7-8,!Falme 2;1-3).
- .Lazima Tupende kuomba kuabudu na kuishi maisha ya kumtumainia Mungu. Daniel, shedrak, Meshak na Abdnego waliweza kukabiliana na changamoto zilizowakabili kwa sababu walijaa Roho na walipenda kuomba Tumuombe Mungu atujaze kwa Roho wake kila siku.
- Lazima tujifunze kumfanya Mungu kuwa wa kwanza katika kila jambo (Mathayo6;33)
- Usijidharau wala kujiona kuwa u mtoto Mungu yu aweza kukutumia (Yeremia 1;4-7 1Timotheo 4;12-16)
- Jizoeze kufunga na kuomba na kufanya maombi ya alifajiri au meditations Mungu awe nawe.
Mkumbuke Muumba wako siku za Ujana wako Muhubiri 12:1-8
Vijana
na Kanisa la Mungu.
Kanisani ndilo eneo lako la kujikuzia na
kuchochea vipawa,Mtumikie Mungu kwa uaminifu kwenye kanisa lenu na chini ya
Mchungaji wako waheshimu na kujionyesha kuwa wewe huna moyo wa kutaka kumuasi
Mungu isibitishie jamii kuwa Mungu anaokoa vijana na anatembea nao na
anawatumia hii itaondoa ile dhana ya watumishi wengi wa mungu kufikiri kuwa
vijana wengi ni watenda dhambi huku wakisahau kuwa dhambi haina cha mzee wala
cha kijana,kuwa karibu na watumishi wa Mungu jifinze kutoka kwao iige imani yao
washirikishe mambo yako Heshimu wazazi wako, muheshimu kila mtu, simama
barabara wakati wa majaribu. Mungu na akubariki sana nakutakia ujana mwema na
ujazwe nguvu za mungu na uwe kiongozi bora katika taifa letu Niombee na mimi
kwa kazi hii ngumu ya kutoa muelekeo kwa jamii ili niwe msaada kwa watu wengi
Mungu atulinde hata tuonane,
Ahsante sana mtumishi Mungu akubariki sana kwa mafundisho mazuri Na awe pamoja nawewe siku zote
JibuFutaMungu akubariki
JibuFutaMungu akubariki na azidi kukulinda milele,hata tuonane
JibuFuta