Jumanne, 16 Februari 2016

Mungu ndiye aliyekua anafukuza Mwizi !



Hii ilitokea mwaka 1998 hapa dar.
 
Alikuwa ni binti mrembo sana kutoka kijiji kimoja huko mkoani Shinyanga wilaya ya Kahama. Alilelewa kwa heshima zote za kisukuma. Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi haikuchukua muda akapata mchumba. Huyu mchumba alikuwa nimuajiriwa katika moja ya idara za serikali hapa dar. Hakuwa akimjua huyu binti zaidi ya kupewa taarifa na wazazi baada ya kuwa wameridhika na tabia za binti, Haikuchukua muda taratibu zikafanywa na kijana akatoka kwenda kuchukua jiko na kuja nae Dar. 

            Matukio mengine hayatokeo hivihivi Mungu hutuma malaika zake wasababishe Haki itendeke

Huyu bwana alikuwa akiishi ubungo-msewe na kufanyia kazi posta. Maisha ya mume na mke yakawa yameanza rasmi. Baada ya huyu Dada yangu(ni marehemu kwa sasa) kuishi kwa takribani miezi 8, alizoeana na mama mmoja jirani yao ambae alikuwa na umri mkubwa lakini hakuwa na mume. Alimuheshimu kama Dada yake na wakawa karibu sana kama ndugu. Huyu Dada ingawa hakuwa na mume lakini alikuwa na mtu wake wa kumkuna ambae alikuwa ni tax-driver.

Siku huyu mama akamwambia yule dada kesho yake amsindikize kwenda mtongani kumuona shangazi yake ambae alikuwa mgonjwa. Kwa vile hakuwa na mazoea ya kutoka bila mumewe, akasita kukubali moja kwa moja na kuahidi atakuwa tayari kama mumewe ataridhia. Jioni baada ya kurudi mumewe alimueleza juu ya ombi la yule mama, kwa vile jamaa huyu alimuamini sana mkewe na hata yule mama, aliwaruhusu.

Kesho yake baada ya staftahi, alikuja yule bwana wa yule mama na gari yake na kuwachukua kuwapeleka mtongani. Kuna sehemu walipita kumpitia rafiki wa huyu taxi-driver maeneo ya ubungo maji. Baada ya kuingia huyu bwana safari ikaendelea. Huyu jamaa aliyepitiwa njiani, alikaa siti ya nyuma sambamba na huyu Dada yangu mke wa mtu.

Jamaa alikuwa mchangamfu sana alijitambulisha kwa jina la Erasto na dada nae akajitambulisha kuwa anaitwa Catherine. Yule mama alikuwa anaitwa Husna na tax-driver Mussa. Huyu erasto alikuwa muongeaji sana haikuchukua muda wakawa wamezoeana kama watu wanaofahamiana siku nyingi. Safari ikawa nzuri sana. Walifika salama, jamaa wakawashusha wakawaacha na hadi jioni walipowarudia. Huo ukawa mwanzo wa kufahamiana erasto na cathy! Km nilivyoeleza awali,Husna na Cathy waliheshimiana sana, lakini siku moja wakiwa wameketi barazani wakipiga story Cathy aliambiwa jambo ambalo hakutarajia kuambiwa na mtu anayemuheshimu kiasi kile! Husna alimwambia Erasto anampenda na anamtaka ki-mapenzi. Cathy alihisi baridi ghafla na Husna aliigundua hali ile na kuamua kuwa mnyenyekevu kwa kumuomba radhi. Zilipita km wiki 2 hivi wakiwa hawaelewani,lkn baadae mambo yakaisha na maisha yakaendelea. Baada ya miezi 2 kupita,Cathy alianza kuhisi kitu kisicho cha kawaida,alianza kuhisi anampenda erasto!


Mwezi mmoja baadae alijikuta akiisaliti ndoa yake kwa mara ya kwanza! Penzi likakolea ingawa walijitahidi sana kuficha ili wasigundulike mapema. Awali walikuwa wakikutana buguruni ktk lodge moja iliyopo pale.

Baadae waliamua kubadilisha na kuanza kukutana kariakoo ktk duka la erasto. Erasto alikuwa na duka la nguo kariakoo,chumba cha duka kilikuwa kimekatwa katikati nyuma kulibaki chumba ambacho kilitumika kuhifadhia mizigo. Baadae erasto aliongeza matumizi kwa kununua kitanda na godoro kwa ajili ya penzi lake Catherine. Penzi liliendelea kukolea siku hadi siku. Walikuwa wanakutana mchana,wakati ambao jamaa(mume wa Cathy)anakuwa kazini.

Ilikuwa siku ya ijumaa ya mwezi august mwaka 1998,mchana. Wapenzi hawa walikuwa wanaendelea kuivunja amri ya sita ya Mungu. Km ilivyo kawaida ya kariakoo,kibaka mmoja alikuwa anajaribu kupora wallet ya mtu mmoja,baada ya kumshtukia alianza kufukuzana nae pamoja na raia wengine.

Kelele za mwizi ziliendelea kusikika na hata Cathy na erasto nao walizisikia lkn hawakuzitilia maanani. Yule kibaka alilijua lile duka na kwa vile alikaribia kukamatwa alikimbia kwa kasi na kuingia hadi ktk kile chumba kwa kuwa hakukuwa na ukuta wa kuzuia zaidi ya zile nguo. Yule mtu aliyekuwa anamfukuza yule kibaka,nae aliingia hadi ktk chumba kile kwa lengo la kumkamata mwizi wake.

Hamadi!!! Waliwakuta cathy na erasto wakiwa uchi wa mnyama wakivunja amri ya 6 Mungu. Unajua aliyekuwa anamfukuza mwizi alikuwa nani!!? Siku hiyo mume wa Cathy alitoka kazini mapema na kupitia kariakoo ambako alikuwa na shida binafsi. Akiwa kariakoo ndipo kibaka mmoja akajaribu kumpora wallet yake kwa bahati akamshtukia na kuanza kumfukuza ili amwadabishe. Baada ya kibaka kuingia chumba kile cha duka na yeye aliingia na ndipo alipokutana kitu asichokitarajia mkewe akiwa na mwanaume mwingine akifanyiwa kilekile anachokifanya yeye.
 

Kibaka alisalimika na tukio la Cathy na erasto ndo likachukua nafasi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni