Jumatatu, 29 Februari 2016

Mwitaliano Orijino Akaletwa Kwangu!


Nakumbuka mwaka lakini tarehe na mwezi umenitoka kidogo, lakini ilikuwa ni mwaka 2002 Nilikuwa nauza duka la jamaa yangu kule temeke wakati ule, nilikuwa ndiyo nimemeliza kidato cha sita , nasubiri kwenda zangu vyuoni  Nilifika hapo temeke nikitokea nyumbani Handeni, nilipofika hapo niliona nijifanye mimi kuwa mtoto wa mjini  ili nipokelewe vizuri na vijana wenzangu. Ni kweli nilijifanya najua vitu vingi sana, nilikuwa naawaambia rafiki zangu kuwa nimesoma sekondari nchini Namibia ambapo baba alikuwa akifanya kazi kwenye ofisi za FAO. 


Mwitaliano Orijino alitaka kujichanganya jamaa wakaniletea


Nilikuwanawaambia kwamba nilikuwa natembea kwenye inchi kadhaa  za ulaya kwani baba yangu alikuwa akipata tiketi za bure kila mwaka  kusafiri na familia yeke kwa kweli sio siri nilibaini kuwa vijana wa Dar ni washamba  kuliko wale wa vijijini, kwa nini niliamini hivyo? ni kwa sababu waliamini kila nilichokuwa nikiwaambia na kuonyesha kuvutiwa sana kiasi kwamba pale dukani pakawa ni kijiwe kilichositawi, mara nyingi nilikuwa napenda kusisitiza sana kuwa nchini Italia tulikaa kwa miaka mitatu  wakati baba anasoma ambapo aliruhusiwa kwenda na familia yake niliwaambia kuwa hata masomo nilikuwa nasoma kwa kiitaliano na kuwa ninakikumbuka sana.

Nilizidi kuwaambia kwamba huwa ninakwenda ubalozi wa Italia hapa nchini  kupiga stori na baadhi ya watumishi wa pale kwa kiitaliano, niliwaambia huwa nafanya hivyo ili nisikisahau, Walikubaliana name na  kunitazama kwa heshimna kubwa , siku hiyo ya tukio  nikiwa dukani  walikuja jamaa zangu wawili  na Mwitaliano mmoja ambaye gari lake lilikuwa limaharibika  na alikuwa anatafuta msaada na pia ilionekana kuwa kuna jambo linguine anataka kulijua , niliposikia hivyo mashuzi na jasho vilianza kunitoka niliona wazi wazi kuwa kuadhirika kumewasili, Niliwaambia kuwa wakati ule niko bize  siwezi kwenda kumwona muitaliano huyo, wale jamaa zangu walinishawishi wakisema ni jambo zuri kwangu kwenda kani litanipandishia ujiko zaidi,, niliwaambia ni sawa lakini nisingeweza kuacha duka peke yake wala kulifunga. 

Wale jamaa zangu waliridhika na kuondoka, lakini kiasi cha dakika kumi baadaye  niliwaona wakija na mzungu alipofika na wale jamaa zangu waliniambia kuwa Yule ni muitaliano,  nizungumze naye , sikuwa najua hata neno moja la kiitaliano  ilibidi nizuge kwa kusema kwamba Yule jamaa huenda anatoka Italia ya kusini ambapo kiitaliano chao hata wenzao hawakielewi, nilijifanya namsemesha Yule mzungu kiitaliano kwa kusema Fkorsia deminati maneno ambayo hata mimi nilikuwa siyajui maana yake mwitaliano alibaki ameshangaa  na kuonyesha ishara ya kuwa hanielewi, wakati huo huo alipiata mzee mmoja ambaye aliuliza kinachoendelea  na kuamua kuingilia kati  kwa kuzungumza na Yule mzungu , walielewana sana na Yule mzee akampa Yule muitaliano maelekezo, alipoondoka Yule mzee aliniuliza nilipokuwa ninaishi kule Italia Nilimwambia Rome aliniuliza mtaa nikakwama  aluniuliza mambo mengine ambayo wala sikuwa nayajua nikakwama kabisa jamaa zangu walianza kucheka hadi machozi yakawatoka , kwa kweli nilibaki nimeduwaa, Yule mzee alisema hujafika Italia hata kwa kusoma kitabuni, Halafu aliondoka Jamaa zangu hawakuwa na mbavu, ilinibidi nifunge duka siku ile  kwa muda , kilitokea kitu gani baada ya hapo? Unataka nikujibu subiri naomba unionyeshe cheti chenye kuthibitisha kuwa niliwahi kuishi Mirembe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni