Jumatano, 2 Machi 2016

Hapa yupo Aliyemkuu Kuliko Sulemani


Mathayo 12: 38-42 Biblia inasema “38. Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. 39. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.  40. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.  41. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42. Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.” 



Kifungu hicho hapo juu cha maandiko ni cha muhimu sana na tunapokifanyia uchambuzi yakinifu itatupa mwanga wa kumfahamu Yesu Kristo kwa kina na upana na urefu zaidi, kifungu hiki ni matokeo ya mjadala uliokuweko kuhusu Yesu Kristo, Baada ya Wayahudi hasa jamii ya  mafarisayo kumnenea Yesu maneno mabaya zaidi, Baada ya kuwa Yesu amemponya mtu aliyekuwa ana pepo, kipofu na ni Bubu, Mathayo 12:22-23, Muujiza huu uliwashangaza watu na kumfanya Yesu aanze kukubalika miongoni mwa jamii kuwa “MWANA WA DAUDI” hii ilikuwa ni wazi kuwa walikubali kuwa Yesu ndiye MASIHI, ni wazi kuwa kwa kazi hii na nyinginezo alizozifanya Yesu zilipelekea watu kumuamini na kuondoa shaka kuwa ndiye mfalme ajaye kwa JIna la Bwana, Hata hivyo kwa sababu ya wivu wa Mafarisayo ambao waliona Yesu anaheshimika zaidi na kuwa gumzo kuliko wao waliamua kwa makusudi kuharibu kibali cha Yesu kwa kusema kuwa anatoa pepo kwa nguvu za mkuu wa Mapepo Belzebuli (Mathayo 12:24)

Yesu Kristo akitambua hilo alitoa hutuba kali sana ya maonyo dhidi ya watu wanaopinga kazi ya Mungu Roho mtakatifu, na zaidi ya yote aliwaonya watu kuhusu kuzungumza maneno yasiyo na maana kwa vile watatoa hesabu kwa kila neno lisilo na maana wanalolitoa katika vinywa vyao, Mathayo 12:33-37.

Baada ya hutuba hii ya Yesu ambayo ilikuwa kali na yenye maonyo baadhi ya Mafarisayo waliogopa sana Lugha “Hapo” inatumika kuonyesha kuwa iliwalazimu sasa waombe ishara ya kumfahamu Yesu vema kuwa yeye ni nani, Tupe ishara itakayotusaidia kukutambua wewe ni nani? Ndipo Yesu aliwajibu kwamba watamtabua kupitia Ishara kuu mbili.

1.       Ishara ya Nabii Yona.
Yesu aliwaeleza kwa uwazi kuwa Ishara ya kumtambua Masihi iko wazi, ishara hii ndiyo iliyowavutia watu wa Ninawi wakatubu na kumgeukia Mungu kupitia mahubiri ya Yona, Mathayo 12:38-41, Kimsingi Yesu alitaka kukazia kuwa kile kilichomtokea Yona kilikuwa ni ishara halisi, na kilikuwa ni kivuli cha kumtambua Masihi, ambaye Yesu alikazia kuwa ni mkuu kuliko Yona, Yesu alikazia kuwa namna njema ya kumtambua yeye nip ala atakapokufa na kufufuka siku ya Tatu, hii ndio kazia kubwa ya ukombozi itakayowavuta wengi katika ufalme wa Mungu.

2.       Ishara ya Malkia wa Sheba.
Yesu aliwapa Mafarisayo Ishara nyingine ya muhimu. Ambapo sasa anaeleza kuhusu Malkia wa kusini yaani Sheba kwamba alitoka mbali sana pande zamwisho wa Nchi kuja kusikiliza Hekima ya Sulemani, Yesu ni kama alikuwa anakazia kuwa njia nyingina ya kumtambua ni kumsikiliza, usikivu ungeliwasaidia kujua kuwa hakuna mwingine anayeweza kunena au kutenda katika kiwango kama cha Yesu, Mathayo 12:42 hata hivyo  mahali hapa ndipo paliponisukuma zaidi kufanya Uchambuzi hususani Yesu alipohitimisha kuwa malikia huyu alisafiri kutoka mbali kusikiliza Hekima ya Sulemani, hata hivyo Yesu alitamka wazi kuwa Yeye ni mkuu kuliko Sulemani.

Suleimani ni mfalme aliyeishi kwa anasa na ufahari wa hali ya juu, mfalme huyo alikuwa na Hekima na ufahamu na maarifa ya hali ya juu sana kuliko wafalme wote ambao wamepata kuweko, Biblia inasema kabla yake hajakuweko na badala yake hatokuweko 1Wafalme 3:9-13, 4;29-34 unaweza kuona!, wengi waliosikia Hekima ya Suleimani katika enzi zake walisafiri kutoka mbali ili kwenda kumsikiliza, Lakini ziara ya kifahari na maarufu sana na iliyoelezewa kwa kina ni safari ya Malkia wa Sheba au Ethiopia ambaye alikwenda kwa mikogo mingi na mikubwa  1Wafalme 10:1, 2Nyakati 9:1-6 Biblia inasema malkia huyu alikwenda akiwa na maswalai magumu sana “She came to Jerusalem to test him with Hard Questions” pamoja na ziara yake ya kifahari na zawadi kibao alizozibeba alipofika Yerusalem kwa Suleimani alijibiwa maswali yake yote  na mambo yake yote hata aliyokuwa ameyaficha sirini, hakuna kilichofichika kwa Suleimani, alitosheleza mahitaji yake yote na hisia zake zote zilijibiwa na kuzidi.

Dunia ya leo ina maswali magumu mengi yasiyo na majibu, pamoja na kuendelea na kukua kwamaarifa na uvumbuzi wa kisayansi na Teknolojia, Watu wanazidi kuharibikiwa dunia imejaa hekina ya uharibifu, wizi,ufisadi,uchochezi,uchoinganishi, majungu na fitina, kuliza wengine, kutoa mimba udanganyifu, na hakuna majibu ya maswala muhimu katika matatizo ya watu, Sulemani alikuwa na ujuzi zaidi ya wa kibailojia, Chemistry, Physics, aliishi kwa anasa kuliko mtu yeyote, mwisho aliona hekina na maarifa bila ya Mungu ni upuuzi au ubatili,alishauri watu kumkubuka Muumba wao siku za ujana wao, Muumba huyu ndiye mkuu kuliko Sulemani, Yesu Kristo anatajwa kama Hekima yetu 1Wakoritho 1:18 kwa kiyunani Epignosis sofia, Full of wisdom Knowledge and Understanding, yesu aliposema Hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani alimaanisha Yeye ndiye aliyemuumba huyo Sulemani, Yeye ndiye mwenye majibu yote hata ya mambo magumu, Yeye ndiye Masihi, ni zaidi ya mfalme Sulemani, watu watatoka kila pande za dunia kumjia yeye, na atawahukumu wote waliomkataa yey.

Hapa yupo aliye mkuu Kuliko Sulemani.

Maoni 1 :

  1. Mungu azidi kukutumia pastor Umonifaa sana kama baba kwangu...

    JibuFuta