Jumatano, 24 Februari 2016

Shule ya Watendakazi!



UTANGULIZI.

Shule ya watenda kazi ni shule maalumu inayoandaa na kuweka tayari watu waliookoka  kuwa tayari kumtumikia Mungu au kufanya kazi Pamoja na Mungu Huwezi kutenganisha wokovu na kumtumikia Mungu Tumeokolewa ili Tumtumikie Mungu, Mungu alipo waokoa wana wa Israel Kutoka katika Nchi ya utumwa alirudia mara kwa mara kusudi la kuwaokoa kuwa ni ili wamtumikie fuatilia mistari hii (Kutoka 7;15-16. 8;1,20.9;1,13,10;3) Kumtumikia Mungu ni jukumu letu kuu  kwa sababu sisi tu wafanyakazi  pamoja na Mungu (1Koritho 3;9a) Hivyo mungu anatutegemea kama sisi nasi tunavyomtegemea.

         Mapenzi ya mungu ni kuwaona watu wanaokolewa kwa wingi na kuacha maovu jukumu hili ametupa (Ezekiel 33;11,18;23,32.Timotheo 2;4,2Petro 3;9) Bwanawetu Yesu alikuja kufanya mapenzi ya Mungu (Yohana 5;20,4,34).Pia alihubiri na kufundisha kila mmoja wetu kufanya mapenzi ya Mungu (Mathayo 7;21,12;50,2;28-31,Luka 12;47-48).

        Ni wajibu wa kila mtu aliyeokolewa kubeba mzigo wa kuona watu wanaokolewa na wanadumu katika imani,hili ni jukumu la kujivunia sana ,Mungu katika hekima yake hakuwapa malaika kazi hii alitupa sisi wanadamu kwani sisi tunao ushuhuda,Malaika wanaitamani sana lakini Mungu kwa heshima kubwa ametupa sisi jukumu hili (Mathayo 28;19-20).Yeye Mungu hufanya kazi siku zoote na hufanya kazi kuliko sisi,yeye kama baba yetu ni muhimu sisi tukifanya kazi pamoja nae (Marko16;20,Matendo 8;1,4;29-35,11;19-21) Wenzetu nyakati za kanisa la kwanza  walikuwa hodari katika kulitimiza kusudi hili loa kumtumikia Mungu

     Hivyo basi kila mtu aliyeokoka ana jukumu la kufanya kazi ya kuwaleta watu kwa Yesu huduma ya kiinjilisti kwa gharama yoyote bila kukwepa (Mithali 24;11-12,Yakobo 5;19-20),Hili si jukumu la wachungaji peke yao ni jukumu la kila mmoja wetu,Tunapoendelea kujifunza shule hii ya uinjilisti au shule ya watenda kazi tutajifunza masomo maalumu yatakayotupa hekima katika kuzivuta roho za watu shule hii itakufanya utoke katika hatua moja ya ukristo na kuingia katika heshima ya kufanya kazi na mungu hivyo kila anayehitimu shule hii tunamtegemea atakuwa mtu mwenye uewzo wa kuwaleta watu kwa yesu na kusimamia kuendelea kwa watu waliookoka kukulia wokovu hivyo unakua ni mtenda kazi pamoja na mungu na pia ni mtenda kazi pamoja na watumishi wa mungu shambani mwake ,Hivyo unapohitimu shule hii wewe si mkristo wa kawaida bali ni Mtenda kazi katika Shamba la Bwana (2koritho 8;2324) watu hawa wanapaswa kuonyeshwa upendo na heshima kwani watakuwa wkitaabika kwa ajili ya watu wa Mungu  kwa ajili ya kutenda kazi kwao katika kanisa watu hawa ni washirika wa karibu na Mtumishi wa Mungu kwani kuchapa kazi kwao kunaweka nafasi kubwa katika kutoa nafasi kwa mtumishi kuutafuta uso wa mungu na kulihudumia lile neno na kufanya maombezi kwa ajili ya Kondoo woote kwa ujumla na kushauri wale wanaokuja kwa ajili ya ushauri na maombezi kazi hii ni pana na inahitaji watenda kazi wengi,Mungu akubariki kwa kupata neema ya kuingia katika shule hii au kupata muhktasari wa masomo haya na kujisomea na kuyafanyia kazi yoote yaliyomo katika masomo haya wako katika Utumishi Mchungaji Innocent Kamote.


 Mungu ataipima Kazi ya kila mmoja wetu Duniani
 

Somo maalum shule ya watenda kazi

                  Somo;   KUPIMWA KWA KAZI YA KILA MTU
       Ni muhimu kufahamu kuwa watu tuliuookolewa tumeokolewa ili tumtumikie mungu,na kuna thawabu kubwa tutakazizipata mbele za Mungu kwa kumtumikia,Thawabu hizi zitatolewa kulingana na utendaji kazi wa mtu,kwa hivyo kazi kazi ya kila mkristo itapimwa tutajifunza spmo hili kwa kuzingatia vipengele vitano vifuatavyo;-
·         Kusudi la kuokolewa
·         Utumishi aliopewa kila Mtu aliyeokoka
·         Kupimwa kwa kazi ya kila mtu
·         Baraka ya kufanya kazi ya mungu kwa hiyari
·         Faida za kuitenda kazi ya Mungu.

Kusudi la kuokolewa.
     Hatuna budi kufahamu tene na tena kuwa mara baada ya kuokolewa kwa kumkiri Yesu Kristo kama bwana na mwokozi wetu,sio mwisho wa kila jambo bali tumekubali kuwa wayumwa wake naye ni mtawala wetu,kwa sababu ametununua kwa damu ya thamani hivyo tunao wajibu wa kumtumikia,Kusudi letu la kumtumikia Mungu halitofautiani na lile Bwana alilokazia alipokuwa akiwaokoa Waisrael kule Misri (Kutoka 7;16) Kwa msingi huo katika maisha yetu ya wokovu ni muhimu sana kutumika Kutumika sit u kuna thawabu bali kunatusaidia kukua kiroho na kukomaa katika utumishi na pia kunaendelea kututakasa,Mungu ameweka mkazo katioka swala zima la kumtumikia (Kutoka 8;1,20;9;1,13) jambo hili kwa jinsi mungu alivyolikazia lilipelekea  hata farao kutambua kusudi la Waisrael kuitwa na Mungu wao (Kutoka 10;11,10;26), Na mataifa pia yalitambua kuwa Mungu wa Israel ni Mungu wa pekee aliye wapenda ) makanisa mengi sana leo yako nyuma na hayaongezeki kiidadi kwa sababu wameacha kutilia mkazo  swala la kumtumikia Mungu na kuwaachia wachungaji peke yao  (Matendo 2;18,8;1,4,2Timotheo 2;2)

Utumishi aliopewa kila Mtu aliyeokoka.
     Kila mtu aliyeokoka ni mtumishi na amepewa utumishi na analazimika kuhubiri na kufundsisha ,hata kama ana umri mdogo (Yeremia 1;4-8) Mungu huweza kutuita hata tuikiwa katika umri mdogo kama apendavyo kwa ajili ya kazi yake (marko 16;15),Licha ya kuwa tumeagizwa kuihubiri injili ,kila mtu aliyeokoka ni tawi la mzabibu ambaye ni Yesu hivyo Bwana anatutarajia tuzae matunda (Yohana 15,2,6) Hivyo kuna hatari ya kutupwa nje kama hatumzalii Bwana matunda, Kadiri tunavyomtumikia Mungu ndivyo na kuzaa sana ndivyo Anavyotukuzwa (Yohana 15;8,Luka 15;10,7) Yesu alihakikisha alipokuwa duniani baba yake anatukuzwa,ni namna gani tunaweza kumtukuza Mungu ni kwa kuhubiri injili na kuwafuatilia waliookoka kuwafundisha ili waukulie wokovu na kudumu kazi hii ndiyo inadhihirisha kuwa  Tunampenda sana Bwana  (Yohana 21;15-17) neno lisha humaanisha kufundisha na chunga ni kutoa huduma za kichungaji kwa kondoo wa Mungu wenye mahitaji mbalimbali, Bwana atupe neema ya kumtumikia.

Kupimwa kwa kazi ya kila mtu.
     Pamoja na kuwa tumeokolewa ni muhimu kufahamu kuwa watu waliookoka watahukumiwa kulingana na matendo yao,kazi ya kila mtu itapimwa,na kila mmoja atakuwa na utukufu wa tofauti mbinguni  kwa sababu ya utumishi wale waongozao wengi katika kutenda haki watang’aa kama Mwangaza wa anga (Daniel 12;3,Mithali 11;30). Woote tunaweza kuingia mbinguni lakini kutakuwa na madaraja tofauti kulingana na kazi mungu ni mwenye haki (1Timotheo 3;13) kwa msingi huu basi kazi ya kila mmoja itapimwa ili kuamua kwa haki nani anastahili nini (1Samuel 2;3.1Koritho 3;11-15 Warumi 14;12) kwa msingi huo basi itakuwa aibu kuifanya kazi ya mungu kilegevu(Warumi 12;11,) na ni lazima kukamilisha kazi(Yohana 4;34),Makanisa mengi hufanya kazi kubwa nay a gharama yakuwaleta watu kwa Yesu kasha hubakia kufurahia idadi ya watu waliookoka na kufurahia bila kukamilisha kazi kwa kuwalea watu wa Mungu waliookoka kwa kuwafuatilia na kuwafundisha ili wadumu katika Imani tusipofanya hivyo kazi yoote tuliyoifanya inakuwa ni Bure au kazi isiyokamilika (1Lonike 3;5)

Baraka ya kufanya kazi ya Mungu kwa hiyari.
 Mungu atatupa ujira au ijara kwa ajili ya kazi hii tuifanyayo (2Nyakati 15;7),hata hivyo hatuna budi kuifanya kazi hii kwa hiyari,Mungu huwabariki watu wanaoifanya kazi yake kwa hiyari na si kwa kusukumwasukumwa(1Nyakati 29;14-18,6),Ni muhimu tukitumika huku tunajua yakuwa kazi hii tunayoifanya ni ya Mungu na sio ya mwanadamu (1Koritho 9;16-17),kuna tofauti kuifanya kazi hii kwa hiari au kwa sharti kwa hiyari inathwabu kubwa sana sisi tumeitwa kuifanya kazi hii kwa hiyari 

Faida za kuitenda kazi ya Mungu.
     Wanafunzi wa Yesu walimuuliza kuwa baada ya kuwa wameifanya kazi hii watapata nini basi? Kuna malipo makubwa kabisa Heshima ya kumtumikia Baba itatuweka pale Kristo atakapokuwa (Yohana 12;26,Kutoka 23;25-27) Tutapata mema mengi hapa duniani na mbinguni ziko ahadi nyingi sana kwa watu woote wanaomtumikiaMungu,ataondoa magonjwa ,hapatakuwa na aliye tasa na mbinguni tutalipwa mara mia (Mathayo 19;27-29)

Somo maalum shule ya watenda kazi.

Somo: UMUHIMU WA KUFANYA UFUATILIAJI.
   Upo umuhimu mkubwa sana wa kufanya ufuatiliaji kwa ajili ya kuwafuatilia watoto wachanga wa Kiroho ,Kazi hii ni ya muhimu kuliko tunavyofikiri (Matendo 15;36), Makanisa mengi na watumishi wengi wa Mungu hufanya kazi nzuri ya kuhubiria watu injili ya wokovu na watu wanaokolewa kwa wingi,Hata hivyo kazi hii haiwezi kuwa kamili kama utaondoa ufuatiliaji Ni makusudi basi ya Roho wa mungu kutufundisha somo hili ili kazi tunazozifanya za kuhubiri injili ziweze kuwa kamili.Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia  vipengele vitano vifuatavyo;-

  • Urahisi wa kuua kiumbe katika wakati wa uchanga
  • Jinsi ya kuwaficha watoto wachanga wa kiroho
  • Sababu zinazopelekea watoto wachanga wa kiroho kuuawa.
  • Jinsi inavyochukiza Mbele za Mungu mmoja apotee.
  • Umuhimu wa kufanya ufuatiliaji.
Urahisi wa kuua kiumbe katika wakati wa uchanga.
    Ni muhimu kufahamu kuwa ni rahisi kuua kitu katika uchanga kuliko kikiwa kimekomaa,Mmea mchanga unaweza kuuawa kirahisi unapokuwa mchanga  hata kwa kukanyagwa na kuku tu , Takwimu nyingi zinaonyesha kuwa Barani Afrika vifo vingi vya watoto vinavyotokea ni vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitani mapaka sifuri,Mtoto mdogo aweza kufa hata kwa kumlalia vibaya tu (1Falme 13;16-19),katika malezi watoto wanahitaji uangalifu mkubwa sana,kinga zao zinakuwa bado hazijaweza kustahimili magonjwa ya dunia,watu waovu wenye tabia ya kupenda kutoa mamba hupendelea kutoa mamba ikiwa changa kuliko ile iliyokomaa Kwa ufahamu huu kuwa ni rahisi kuua kitu katika uchanga wake shetani hupendelea kuwaua watoto wachanga wa kiroho kabla hawajakomaa,mpango wa Shetani kumuangamiza Yesu au Musa  ulifanywa na shetani mapema katika uchanga wao (Kutoka 1;15-18,22,2;1-6,Math 2;13-16) Mtu nanapookoka hata kam ni mzee katika hatua zake za mwanzoni za wokovu ni mtoto mchanga kiroho (1Petro 2;2).

Jinsi ya kuwaficha watoto wachanga wa kiroho
     Ni muhimu basi kanisa likawa na mkakati kabla hata ya mikutano ya injili kuwaandaa watenda kazi ambao watakuwa tayari kuwafuatilia watoto wachanga kiroho,aidha kanisa ni muhimu likafahamun kuwa baada ya mkutano kwisha sio ndio muda wa mapumziko umewadia hapana ndio kwanza kumekucha na kazi inaanza,katika wakati huu watu wengine maalumu watakuwa wakiwaomea watoto hao wachanga kiroho,na watenda kazi wakifanya ufuatiliaji haraka sana  mara baada ya kuokolewa kwa watoto hao kabla ya saa ishirini na nne (IThesalonoke 3;5,2Koritho11;3) ni Vema basi tukaanza kuwanyonyesha mara moja wanapokuwa wamezaliwa hakuna mama anayezaa kasha akaanza kunyonyesha  siku ya tatu au ya nne,Tuwaombee na kuanza ufuatiliaji mara moja.

Sababu zinazopelekea watoto wachanga wa kiroho kuuawa.
     Kwa nini Watoto wengi wa kiroho hawaendelei na wokovu mara wanapokuwa wameokoka,moja ya sababu ni kuwa Shetani hakati tama wala hapumziki Yeye hufanya ufuatiliaji haraka kabla mtendakazi hajafanya ufuatiliaji woote tunakumbuka siku wana wa Israel walipotoka Misri kuwa farao alifanya uamuzi wa kuwafuatilia kabla hata hawajafika kokote ili awarejeze tena utumwani ndani ya masaa 24 (Kutoka 14;9-10,Ebrania 5;13-14,2Koritho 11;3) Mtoto mchanga kiroho ni rahisi kuuawa kwa sababu hawajui sana neno la haki nirahisi kudanganywa hata kwa maneno ya kawaida na kukata tama bado hawana silaha zote za mungu za kuwasaidia kupambana (Efeso 10-18) kwa hiyo katika uchanga wake hajui vita vya kiroho wala namna ya kutumia silaha,Mungu alipowaokoa wana wa Israel alitaka wajue vita (Kutoka 13;17-18).
1.       Wavae kweli yaani neno la Mungu (Yohana 8;12)
2.       Wavae dirii ya haki ,matendo ya haki (Matendo 22;25-29)
3.       Wawe na ngao ya Imani (warumi 1;17)
4.       Wavae chepeo ya wokovu yaani wawe na hakika ya wokovu ( Zaburi 103;12)
5.       Awe na upanga war oho kujua namna ya kulitumia neno (mathayo 4;4-11)
6.       Ajue kuomba na kujaa roho kunena kwa lugha
Watoto wachanga wa kiroho wakifikia hatua ya kuyajua hayo wanakuwa na nafasi nzuri ya kuendelea mbele,Mambo hayo hayawezi kufanyika kwa wiki moja tu yanahitaji muda

Jinsi inavyochukiza Mbele za Mungu mmoja apotee.
   Mungu hapendi mtu yeyote apotee bali anataka watu woote wafikie toba (2Petro 3;9.Marth 18;14,1Falme 20;39-40,Ebrania 2;13) Ikiwa Mungu anachukizwa kwa mmoja kupotea kama watenda kazi tunapokuwa tumekabidhiwa watoto wachanga wa kiroho na kuwafuatilia Mungu anakuwa ametukabidhi ili tuwalee kwa niaba yake (Math 25;33-40) na tunapowaacha hata wakafa kiroho bila kuonyesha jitihada zozote Damu yao itatakwa mikononi mwetu (Ezekiel 3;17-19)

Umuhimu wa kufanya ufuatiliaji.
    Katika hali ya kawaida mama aliyezaa atahakikisha anamtunza mtotop aliyemzaa kwa gharama yoyote (Wagalatia 4;1-2,4;19-20,1Thesalonike 3;5),Hakuna jambo muhimu wakati wa mavuno kama ufuatiliaji,Lazima tuhakikishe tunawafuatilia kwa ukaribu na kujua mahitaji yao na kuanza kuwafundisha neno la Mungu ,tusikubali kuridhika na semina za kanisani pekee mwalimu wa ufuatiliaji anapaswa kuwa makini kuwa mtoto wake wakiroho anapitia mazingira gani kasha kumfundisha masomo ya mwanzo ya wokovu ambayo ni maziwa yasiyoghoshiwa,huku tukikwepa kuwafundisha vitu vigumu kama kupunguza wake zake iwapo ana wake zaidi ya mmoja n.k.Wakati wa ufuatiliaji ni wakati wa kujikana nafsi kwani iakulazimu kupanga ratiba na mwanafunzi wako na hivyo itakulazimuni wakati mwingine kukutana saa ambazo umetoka kazini,wanafunzi hao wa kiroho wanahitaji uvumilivu mkubwa kwani wengine watakuwa bado wanakwenda  katika makanisa yao ya zamani,na wengine ukuaji wao ni wa taratibu sana na wengine haraka,wengine itakulazimu kuwasaidia kazi ndogondogo n.k. somo lifuatalo

Somo maalum shule ya watenda kazi

Somo: GHARAMA ZA KUFANYA UFUATILIAJI.

     Katika hali ya kawaida mtu anapojifungua mtoto pamoja na furaha ya kuzaliwa kwa mtoto huyo kutakuweko Gharama za malezi ya mtoto huyo mapaka pale atakapoweza kujitegemea,Mambo hayo yanafanana na mabo ya rohoni ,Watu wanapookolewa  kunakuwa na Gharama za kuwalea mpaka waweze kujitegemea kiroho ni kwa msingi huu Roho wa mungu anataka tujifunze somo hili sasa gharama za ufuatiliaji tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-
·         Gharama kubwa huambatana na chochote chenye faida
·         Ulinganifu wa malezi ya watoto wa changa kiroho na  kimwili

Gharama kubwa huambatana na chochote chenye faida
     Kama tulivyogusia katika utangulizi kuwa katika hali ya kawaida wazazi watakuwa na furaha ya kuzaliwa kwa mtoto, lakini swala la kugharimika kwa malezi liko palepale,Kadhalika katika hali ya kiroho, baada ya watu kuokolewa hatupaswi tu kushangilia mavuno pekee bali tunapaswa kufahamu kuwa tunawajibu wa kuwalea au kuwafuatilia katika wakati  huu tutagharimika kwa mambo mengi kama kuwafuatilia ,kujikana nafsi kuwa na muda nao,ili kuwafundisha ,kujitoa kwa nauli au kuwatolea nauli ili waje kanisani,kuwatolea kopi za masomo ya mwanzo ya wokovu,kuwaombea,nk.kwa ujumla ufuatiliaji unagharama,Lakini kugharimika wketu si bure ,Kuna heshima kubwa sana ,Wakati wa kunyakuliwa tutakuwa kama kuku anayeambatana na Vifaranga vyake,wale woote ambao tuliwasaidia kusimama katika wokovu watatuzunguka (2Timotheo 2;6).Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa kitu chochote chenye  Thamani  kina gharama kubwa sana (2Samuel 24;21-25) Tunapopata taabu kwa ajili ya kazi ya bwana  tutakuwa wa kwnza kupata matunda(2Timotheo 2;6,Zaburi 126;1-3,5-6;Yohana 16;21-22,2Thesalonike 2;19-20).

Ulinganifu wa malezi ya watoto wa changa kiroho na  kimwili
    Watoto wachanga wa kimwili wanahitaji maangalizi ya karibu na watoto wa kiroho, pia tunapaswa kuwaangalia sana, Chakula cha watoto wa kimwili ni maziwa na chakula cha watoto wachanga wa kiroho pia ni maziwa  ni lazima tuwe waangalifu tusizungumzie mambo magumu kwao kama ubatizo,utatu,malipizi ya ndoa,n.k. Kama ilivyo kwa vyakula vya watoto wachanga nivya gharama na watoto wa kiroho tutagharimika kuwafundisha na kuwahudumia mara kwa mara hata masomo ya ziada yanayotatua matatizo yaliyonayo,Watoto wadogo ni rahisi kudanganywa kadhalika watoto wa kiroho pia wahitaji kufundishwa masomo ya kinga kuwalinda na imani potofu,Watoto hawajui thamani ya vitu (2Koritho 12;14-15,17-18) matoto mchanga ni rahisi kutoa ahadi lakini ikawa ni vigumu kuitekeleza,Tusijali wala tusi wahukumu,wanahitaji uvumilivu (Luka 8;15)Itatupasa kuwavumilia katika maeneo mengi hata kiama unamkuta anacheza dansi usimhukumu kwa haraka,Tunapaswa kujua wanalielewa vipi neno la Mungu n.k.Watoto huwa hawaridhiki na chakula cha nyumbani kadhalika watoto wa kiroho wanaweza kurudi katika mapokeo yao tuendelee kusoma nao neno na kuwafuatilia bila kukata tama wakati mwingine inaweza kukugharimu miezi hata sita kumfuatilia mtu mmoja kabla hajaonyesha muelekeo,Bwana atupe kuzaa matunda kwa uvumilivu mwingi.

                                       
Somo maalum shule ya watenda kazi

SOMO: NJAA NA KIU YA KULIONA KANISA LIKIONGEZEKA.

      Mtu awaye yote anapokuwa ameokolewa na kuifahamu kweli ana paswa sasa kutulia na kuanza kumtumikia Mungu bila kutangatanga isipokuwa kwa sababu maalumu tu sizizoweza kuzuilika,Pamoja na kuwa Yesu Kristo ametuweka huru bado hakuna uhuru usio na mipaka ,Lazima tutulie katika sehemu moja na kuanza kuujenga ufalme wa mungu tuikiwa na njaa na kiu ya kuliona  kanisa tunaloabudu linaongezeka  kwa msingi huo tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vinne vifuatavyo;-
·         Njaa na kiu ya haki.
·         Kuumbika kwa Kristo ndani yetu.
·         Njaa na kiu ya kuliona kanisa linaongezeka.
·         Jinsi ya kufanya ili kanisa liongezeke.

Njaa na kiu ya haki.
     (Mathayo 5;6),kuwa na haki ni kuwa na sifa  ambazo Mungu anataka uwe nazo,kiu au njaa ni uhitaji wa nuhimu anaokuwa nao mtu,Mungu kwa kawaida hampi mtu kitu asichokuwa na haja nacho,chochote tunachokihitaji kutoka kwa mungu lazima kitanguliwe na kiu na njaa,Watoto wanapotaka kitu kutoka kwa wazazi wao kwa kawaida huomba na wakati mwingine hulia na kugaragara ,Tunapokuwa na uhitaji wowote kutoka kwa mungu ni muhimu kwetu kuomba na kumlilia chochote iwe ni mtoto,Nyumba,Gari, mchumba na karama za rohoni vinapatikana kwa maombi, hii ni hali halisi katika ulimwengu war oho kuwa lazima tuombe yale tunayotaka yafanyike katika kanisa letu.Wako watu wengine ambao ni vigumu kuwapata katika ufalme wa mungu bila miujiza na uponyaji wa aina mbalimbali ni lazima tumuombe Mungu awatumie watumishi wake kwa vipawa na karama mbalimbali ili wale wasioamini wapate kuamini kwa neno au kwa tendo(1Koritho 2;4),Hivyo hatuna budi kumuomba Mungu kwa bidii kwa ajili ya yale yoote ambayo tunataka kuyaona au kuyafanya katika kanisa letu (1Koritho 12;31;4;1).Ni muhimu kumuomba Mungu na kuugua na kulia kwa ajili ya kukua na kuongezeka kwa kanisa letu.

Kuumbika kwa Kristo ndani yetu.
      Kristo kuumbika ndani yetu ni jambo la msingi sana ,tunaweza kuwa tumeokolewa Muda mrefu  lakini Kristo akawa hajaumbika ndani yetu (Galatia 4;19) Kristo anapoumbika ndani yetu tunakomaa kiasi cha kufikia kuwaza,kusema na kutenda katika tabia na mwenendo kama Kristo mwenyewe alivyo,Mtu anaweza kufikia hata ngazi ya utumishi lakini kristo akawa hajaumbika kwa wingi ndani yake Kristo akiumbika ndani yetu tutakuwa na shauku hamu kiu na njaa kama ile iliyokuwamo ndani yake.

Njaa na kiu ya kuliona kanisa linaongezeka.
      Mtenda kazi ambaye Kristo ameumbika ndani yake kwa wingi atakuwa na njaa na kiu ya kuyaleta mavuno katika ufalme wa Mungu (Yohana 44;6-8,9-15,31-35).Kila siku njaa ya Yesu Kristo ilikuwa ni kumuona mmoja akiokolewa,kama Kristo ameumbika ndani yetu tutakuwa na hamu ya  kumuona mwenye dhambi mmoja akitubu na kumwamini Yesu (Yohana 1;37-45,Isaya 60;22a,Luka 15,10,7,2Petro 3;9) Kama Kristo ameumbika ndani yetu hatutapenda Mtu yeyeote apotee,Nyakati za kanisa la kwanza wenzetu walikuwa na njaa na kiu ya kuona kanisa likiongezeka (Matendo 2;41,4;4,5;14,9;31;12,24,17;4.13;1), Kanisa la Antiokia kwa mujibu wa waandishi wa karne ya kwanza lilikuwa na watu laki tano (500,000),walioabudu sehemu moja nab ado hawakuridhika kuwa na hao tu,ni lazima tusikubali kuwapoteza watoto wachanga wa kiroho (Yohana 17;12) wala tusiridhike kuwa na watu wacheche,Hili litawezekana kama tu tutakuwa na watendakazi ambao Kristo ameumbika ndani yao; 

Jinsi ya kufanya ili kanisa liongezeke.
Ø  Ni lazima tufahamu kuwa wajibu wa kushuhudia na kuwaleta watu kwa Yesu sio wa wachungaji pekee
Ø  Lazima tumuombe Mungu kila saa na kila siku kwamba Kristo aumbike ndani yetu
Ø  Tumuombe Mungu awaokoe Ndug,jamaa,marafiki,majirani na wengineo
Ø  Wakati mwingine tuwaalike kuja kanisani na watakutana na neno hukohuko.
Ø  Tuwashuhudie katika uinjilisti wetu Binafsi na kuwakaribisha katika makanisa ya Nyumbani au cells
Ø  Tusikubali kuridhika kuona watu wachache kanisani wakati wa ibada,tuwapitie kuja nao ibadani huku tukiwasaidia kazi zinazowazuia kuja kwa haraka au kuwafanya kutolea udhuru.
Ø  Tuwatumie wale ambao ni wachanga na hawajadumu sana katika neno wawaalike wengine na kuwaleta kwa Yesu au kanisani (Yohana 1;40-42;4;28-39).
Ø  Tukubali kuwa katika hali zoote ili tuwapate isipokuwa dhambi
Ø  Tumuombe Mungu kuumbiwa mzigo wa kuhudhuria Ibada zoote huku tukiwapitia wageni wakiwa peke yao wanajisikia kukata tama
Ø  Funga na kuomba kwa uzito mkubwa kwa ajili yao na wengine ili Mungu awalete wale waliookoka kwa kumaanisha
Ø  Kama tumewqaalika watu tumuombe Mungu awaokoe wale woote tuliowaalika.
Ø  Tujitahidi kuwa nuru ili kuwavuta wale wasiookolewa kama taa ivutiavyo wadudu
Ø  Tutumie mbinu zozote tutakazofunuliwa na Roho wa Mungu ili kuwaleta kwake kwa gaharama yoyote.


Somo maalum shule ya watenda kazi.

SOMO: MTENDA KAZI KAMA TAI.
     Tai ni  miongoni mwa ndege hadari sana ambao sifa zao zimejaa kwa wingi sana katika Neno la Mungu,Roho mtakatifu huwafananisha watendakazi hodari na ndege huyu tai,tutajifunza somo hili mtendakazi kama tai kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo;-

·     Mtenda kazi kama tai.
·     Mambo yatupasayo kufanya

Mtenda kazi kama tai.
      Watu wanaotenda kazi kwa moyo ndio wanaoitwa wanao mngoja Bwana (Isaya 40;30-31),Waatendakazi  ambao wanafanya kazi ya Mungu kwa uhodari wanafananishwa na tai,Mungu anatarajia kuwaona watenda kazi wakiwa kama tai wakifanya kazi yake kwa uhodari na si kwa ulegevu (Yeremia 48;10,Warumi 12;11),Juhudi nyingi sana zinahitajika katika kati ya Mungu kuliko hata ya kaisari,Watuwe ngi hufanya kazi za kaisari kwa bidii kwa sababu wanaogopa kufukuzwa kazi,lakini kazi ya Mungu huifanya kwa kusukumwasukumwa, bila juhudi zozote katika roho zao,Nyakati za biblia mtu au kitu hadari kilifananishwa na tai (Yeremia 4;13) tai hupenda kuishi juu kwa kuyaangalia yaliyo juu,watendakazi nao wanapaswa kuyaangalia yaliyo juu (2Koritho 4;16-18) Paulo mtume alikuwa mtume hodari yeye alifanya kazi kuliko mitume woote kwa Muda alioitwa na Roho mtakatifu kufanya hivyo,utu wake wa nje ulichakaa lakini alifanya kazi sana . Ni muhimu kufahamu kuwa sisi nasi hatuna budi kufahamu kuwa dhiki zitaambatana nasi katika kazi ya Mungu kwa namna isiyo ya kawaida, Hata hivyo dhiki hii ni nyepesi ukilinganisha na malipo atakayotupa Mungu na mambo ya milele.
       Waalimu wa ufuatiliaji na watendakazi kwa ujumla wanatakiwa kuwa wepesi kama tai (Maombolezo 4;19) Tai huwa wepesi sana katika kujua na kufuatilia mizoga hata bila kupewa taarifa (Luka 17;37),Mizoga ni watu ambao bado hawajaokolewa ambao kwa mujibu wa biblia wamekufa kwa ajili ya dhambi zao (Efeso 2;1-2).Kuja kwa Bwana kunakaribia hivyo sisi kama tai tutakusanyika naye siku ile (Luka 17;37,Yuda 1;14,Zekaria 14;4,Ufunuo 19;17-18) hii maana yake ni muhimu kuwakaribu kihuduma wakati wowote wanapokuwepo wenye dhambi ili waokolewe iwe ni katika mikutani ya injili au huduma za maombezi na za kiinjili za ndani (Mathayo 9;35-38,Matendo 13;2).
      Roho mtakatifu ndiye Bwana wa mavuno na ndiye anayehusika katika kuwapeleka watenda kazi katika katika shamba lake ambao ni sawa na watunzaji wa shamba la mizabibu (Luka 13;6-9,19;13).Kufanya uinjilisti ni sawa na kufanya Biashara (Wimbo uliobora 1;6 1Koritho 3;9;Rumi 10;13-15).Mungu hutenda kazi Pamoja na wanadamu (Efeso 4;30) Lakini tunaweza kumhuzunisha  na kumkatisha tama.tunakuwa marafiki na Roho mtakatifu pale ambapo hatutaaacha  kukusanyika siku za uinjilisti wetu,Kule kuwa tayari kwetu humfanya Roho mtakatifu afanye kazi pamoja nasi kama kuokoa na kuponya na pale ambapo hatutaacha mtu apotee (Mathayo 18;14) .Uamsho katika kanisa unaletwa na upepo yaani Roho mtakatifu (kutoka 14;21;Yohana 3;6-8,Hesabu 11;31).Upepo ni Roho mtakatifu. (IThesalonike 5;19).Tunaweza kumhuzunisha  na pia kumzimisha (Zaburi 2;8)Hivyo ni muhimu kumuomba Roho Mtakatifu ili asituache na huku tukizidi kuwa hodari kama tai.

Mambo yatupasayo kufanya.
       Ni muhimu kufahamu kuwa kuokoka au kuokolewa ndio muujiza mkubwa sana tena ndio wa kwanza kuliko yote, hivyo sisi kama tai hatuna budi kufurahia mizoga yaani kufurahi na kushangilia pale watu wanapoamua kuokoka ni lazima tuwafuatilie na kuwatia moyo na kuwaeleza kuwa uamuzi waliofanya ni wa muhimu na bora na wa busara.Tuwatie moyo kuendelea mbele na kuhudhuria ibada katika kanisa kuu na makanisa ya nyumbani bila kukosa kwa gharama yoyote.mungu na atubariki tukiyatenda.

Somo maalum shule ya watenda kazi.
      
SOMO: MISINGI YA UFUATILIAJI
Katika ufuatiliaji iko misingi ya muhimu ambayo tunapaswa kuizingatia kama watendakazi na waalimu wa ufuatiliaji, Bwana atupe neema ya kuizingatia Misingi hiyo na kuzidi katika jina la Yesu.Tutajifunza somo hili misingi ya ufuatiliaji kwa kuzingatia vipengele vitano vifuatavyo;-
  • Madhara ya mwalimu wa kwanza
  • Yatupasayo kufanya kabla ya kufanya ufuatiliaji.
  • Umuhimu wa ufuatiliaji katika saa ishirini na nne (24).
  • Umuhimu wa kufanya utafiti wa mwanzo.
  • Kuzaa matunda kwa uvumilivu.
Madhara ya mwalimu wa kwanza
  Wengi wetu tuko hivi tulivyo kutokana na mwalimu wetu wa kwanza,Kama wazazi wetu wanazungumza lugha Fulani  lugha hiyo itapandikizwa katika hatua za mwanzoni.katika hatua za mwanzoni ni rahisi kupandikiza chochote  iwe ni kitu kibaya au kizuri ,mwalimu wa kwanza anauwezo wa kupandikiza tabia yoyote na kuipandikiza ndani yetu (Ezekiel 16;44-45) Mwalimu wa kwanza ana nafasi ya tabia yake kuigwa na wale anaowafundisha ,Mfano kama mwalimu wa darasa la kwanza atakuwa na mwandiko mbaya  upo uwezekano wa wanafunzi wake kuwa na mwandiko mbaya na ndio maana ni vizuri kuumba mwandiko,Inchi nyingi za Afrika zimeiga  tabia ya inchi zile  ambazo zili tutawala.Mambo hayo ndivyo yalivyo katika ulimwengu wa kiroho mwalimu wa kwanza wa kiroho anaweza kuwaambukiza  hata sauti yake  au lolote katika tabia usemi na mwenendo n.k. Mwalimu wa kwnza ana nafasi ya  kubwa ya kuleta madhara makubwa  kwani kama vile alivyo ndivyo na mtoto  wake wa kiroho atakuwa vilevile (2Timoth 1;5),Hata imani ya mtu hutokana na wazazi au waalimu wa kwanza ndio maaana maandiko ya natuonya kuwa kielelezo kwa waaminio kwani mwalimu wa kwanza wa ufuatiliaji ana uwezo wa kusaidia kujenga kanisa zuri au kuliua (Rumi 11;16),Tunapokuwa waalimu wa ufuatiliaji  tunakuwa tumetumwa na Roho mtakatifu,Hivyo  ni muhimu kuepuka kuwa  kikwazo  kwa tunaowafuatilia,ikiwa hatutakuwa kielelezo na kuwa mbali na dunia  tunaweza kuwa kwazo,Haki yetu inapaswa izidi ile haki ya mafarisayo (Math 5;20,1Tomoth 4;12) ni muhimu kuwa kielelezo  katika usemi,mwenendo imani na usafi,ikiwa tutawakwaza mojawapo ya wadogo hawa  Damu yao itatakwa mikononi mwetu.Bwana ampe neema kila mtendakazi  kuwa na hekima na kuifanya kazi hii tuliyouitiwa na kuzidi katika jina la Yesu.

Yatupasayo kufanya kabla ya kufanya ufuatiliaji.
      (1Thesalonike 3;10) Hatuna budi kuomba usiku na mchana ili wale tunao wafuatilia wasimame katika imani,kuomba ni sawa na kumwagilia maji (1Koritho 3;6,Luka 22;31-32) Bila maombi ya kutosha watoto wetu wachanga kiroho hawataweza kubadilishwa (Converted) na hatimaye wataiacha imani.Hivyo maombi ni muhimu sana .

Umuhimu wa ufuatiliaji katika saa ishirini na nne (24).
      Kama tulivyogusia katika masomo mengine ya awali shetani adui wa Mungu na watu wake hatafurahia kuona mtu aliyeokolewa akiendelea na kudumu katika wokovu,hivyo yeye huanza ufuatiliaji katika masaa 24 tu mara baada ya mtu kuokoka hii ni kama vile farao alivyowafuatilia wana wa Israel walipotoka Misri kwa wokovu ndani ya saa 24 tu (Kutoka 14;5-7,9-10) siku ileile shetani atataka kumrudisha nyuma mtu aliyeokoka Kwa msingi huo tusipo mfuatilia  mtoto mchanga kiroho katika kipindi cha saa 24baada ya kuokolewa tunakuwa tumempa nafasi shetani kufanya kazi kubwa ndani ya saa hizo na kuwarejesha nyuma au kuifanya kazi ya ufuatiliaji kuwa ngumu.Kwa msingi huu ni muhimu kulifuatilia hili na kuwatia moyo na kuwafundisha masomo ya mwanzo ya wokovu yale yaliyo muhimu.

Umuhimu wa kufanya utafiti wa mwanzo.
       Ni muhimu kuwa na hekima katika hatua za mwanzoni kabisa za ufuatiliaji ili tupate matokeo mazuri.Kwa msingi huo utafiti wa mwanzo kwa mtu tunayemfuatilia ni wa Muhimu,ni lazima tujue  kuwa mtu huyu tunaemfuatilia Je amezaliwa mara ya pili? Na tunaweza kumfahamu mtu aliyezaliwa mara ya pili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo
Ø  Mtu aliyezaliwa mara ya pili huonyesha furaha, kulipenda neno la Mungu na kutokuonea haya wokovu,atawekewa ndani yake kuchukia dhambi (1Koritho 2;14). kwa kawaida mtoto wa Ibilisi hapendi neno la Mungu.(1Yohana 4;8)
Ø  Roho wa Mungu atashuhudia ndani yake kuwa ameokoka na amekuwa mwana wa Mungu (Rumi 8;1,16,Luka 1;77,1Yohana 2;6-27).Ni muhimu pia kufanya utafiti wa kimwili mkuwa mtu tunayemfuatilia yukoje Anacheo,Msomi,Tajiri,Umri mkubwa kuliko wako,n.k.Endapo utagundua hayo ni vizuri kutafuta mtu wa aina kama yak wake ili waweze kuendana kifikira kihali na kijinsi na umri ili wasionyeshe dharau kwetu,kama ni wasomi ni muhimu akifuatiliwa na msomi mwenzie (Amosi 3;3).

Kuzaa matunda kwa uvumilivu.
     (Luka 8;15) Wakati mwingine itatulazimu kuvumilia tunapofanya ufuatiliaji,watoto wengine wa kiroho huchukua muda mrefu sana kukua Mchungaji mmoja Jimmy Sakuye wa FGBF Arusha wakati akiwa mshirika  alimfuatilia  mtu mmoja kwa miezi sita  kwa shida sana kwani wakati mwingine mtu huyu alikuwa akienda kwenye dini yake ya mapokeo Sakuye alivumilia na kuendelea kumfuatilia  mtu huyo sasa ni Askofu wa jimbo Mwanza FGBF David Chamoto hii inatufundisha kuwa Nyakati nyingine itatugharimu  kwani watoto wengine hukua kwa shida sana inatupasa kuwa wavumilivu,Kuna kuwaombea kuwavumilia wanapoonyesha mambo ya kidunia au kusakata dansi kupiga wake zao n.k hayo yoote yanahitaji uvumilivu mkubwa na upeo mkubwa wa Kiroho. Bwana ampe kila mmoja wetu neema ya kuzaa matunda kwa uvumilivu katika jina la Yesu Kristo amen.

Somo maalum shule ya watenda kazi.

Somo: HEKIMA NA MAARIFA YA UFUATILIAJI.
Katika kuwafuatilia watoto wachanga kiroho kunahitajika hekima na maarifa namna ya kuingia na kutoka mbele zao ili kusudi tusiweze kuharibu kazi na mpango mzima wa Roho Mtakatifu wakati wa ufuatiliaji tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vinne vifuatavyo;-
  • Hekima ya kuwafuatilia waliotaka maombezi tu.
  • Hekima ya kuwalea watoto wachanga wa kiroho.
  • Mpangilio wa masomo ya mwanzo ya wokovu
  • Jinsi na namna ya kuwafundisha.
Hekima ya kuwafuatilia waliotaka maombezi tu.
       Ni muhimu kufahamu kuwa  wako watu wengine amabao wanakuja kwenye mahubiri kwa lengo la kuombewa tu,hata watu wanapoalikwa kuokoka  anaweza kuwa miongoni mwao lakini nia yake ni maombezi tu ,watu hawa hawako mbali na ufalme wa Mungu (Marko 12;34,Zaburi 119;67,71) Wakati mwingine Mungu huruhusu mateso yawapate ili watu wapate kumjua yeye na wengine ni vigumu kuokoka mpaka wabanwe kwenye kona kidogo (Yohana 4;52-53,11;45).Watu wengine humwamini mungu baada ya kufanyiwa muujiza (Yohana 12;9-11) aidha Mungu huwaponya wengine ili wamwamini(Luka 8;1-4)Mfano Mariam Magdalene aliyekuwa kahaba na kutolewa pepo aliponywa na akawa anamtumikia Mungu.Kwa msingi huu tunapofanya utafiti mwanzoni na kugundua kuwa mtu huyu alifuata maombezi akaponywa tunamfuatilia kwa kumjenga jinsi ya kuutunza muujiza wake ambako kwa usalama ni kuokoka,Pili kama alifuatilia maombezi na hakuponywa  tunapaswa kumfundisha jinsi ya kung’ang’ania na kuupata muujiza wake ambapo ni kuendelea kuja ibadani,aidha kwa kuwa watenda kazi pia huenda kwa niaba ya Yesu Kristo unaweza kuomba nao kuwaombea kuwawekea mikono na hatimaye Bwana atawaponya na wataokolewa Hivyo tusiwapuuzie watu wanaofuata maombezi(Luka 10;1,17) wakati mwingine majaribu hutupata ili tuwasaidie wale watakaojaribiwa (Waebrania 2;18).
Hekima ya kuwalea watoto wachanga wa kiroho.
       Biblia inasema wenye hekima huvuta roho za watu (Mithali 11;30) Watoto wachanga kiroho ni wale  waliookoka hivi karibuni,Hata hivyo Mtu anaweza kuwa kuwa ameokoka siku nyingi lakini akawa ni mchanga bado (Waebrania 5;11-14)Hwa wa muda mrefu ni wale waliodumaa kiroho wanahitaji tiba lakini wale wachanga kabisa wanahitaji maziwa (1Petro 2;2) kwa msingi huo yako maarifa  ya muhimu ya ufuatiliaji na hekima katika ufuatiliaji,mambo kadhaa yafuatayo ni muhimu kuyazingatia.
Ø  Hatupaswi kuwaharakisha (Mwanzo 33; 12-14).Si vizuri kuwafundisha masomo magumu kama malipizi ya ndoa ,utatu wa Mungu,n.k wakati wa uchanga wao kama amepokea muujiza mfundishe namna ya kuutunza muujiza wake.
Ø  Tusiwahukumu katika makosa wayafanyayo katika hatua za mwanzoni (Warumi 14;13) katika hatua hii ya mwanzoni hata kama una shida na unayemfuatilia ana uwezo jihadhari usimkope,Tumetumwa kufundisha tu (2Koritho 12;14-18,Isaya 65;13-14)
Ø  Tuwalinde kwa kuwaombea kwani hawajui kuomba ili wakue kiroho (Maombolezo 2;1-4,18-19).
Mpangilio wa masomo ya mwanzo ya wokovu.
Yako masomo maalumu ya ufuatiliaji ambayo ni muhimu sana kwa watoto wa kiroho kufundishwa wakati wa kuwafuatilia masomo mawili ni maalumu kwa watu waliofuata maombezi na kuponywa au kuto kuponywa wakiwa hawajaokoka kama alikuja kwa maombezi na hajapona tunamfundisha somo (Muujiza mkubwa kwa watu wanaong’ang’ania) Kami ni mtu aliyepata muujiza wake lakini hajaokoka tunamfundisha somo (Jinsi ya kuutunza muujiza wako). Hali hizi zoote tunazigundua wakati tumefanya ule utafiti wa mwanzo.katika utafiti ule wa mwanzo kama tumegundua kuwa Tuliyemfuatilia ameokoka kabisa hawa sasa inatupasa kuanza kuwafundisha masomo ya mwanzo ya wokovu ambayo yako kumi na tatu na tutayafundisha kwa kuzingatia mpangilio ufuatao.
Namba ya somo
Jina la somo husika
Aina ya somo hilo
Siku ya kulifundisha
Somo No  1
Furaha baada ya kuokolewa
Somo la utangulizi
Siku ya 1 ya ufuatiliaji
Somo No  2
Hakika ya Wokovu
Somo la kinga
Siku ya pili ya ufuatiliaji
Somo No  9
Mfahamu adui shetani
Somo la kinga
Siku ya tatu
Somo No  8
Yeye Ashindaye
Somo la kinga
Siku ya nne
Somo No 10
Kujaribiwa kwa imani ya Mtu alliyeokoka
Somo la kinga
Siku ya tano na sita
Somo No  4
Tumaini letu kuu
Mwongozo
Siku ya saba
Somo No  7
Kuteswa kwa ajili ya Kristo
Kuimarisha
Siku ya nane
Somo No  3
Furaha katika wokovu
Maarifa
Siku ya tisa
Somo No  5
Jinsi ya kuukulia wokovu
Maarifa
Siku ya kumi
Somo No 11
Jinsi ya kuomba
Maarifa
Siku ya kumi na moja
Somo No 12
Uwezekano wa kukataliwa
Maarifa
Siku ya kumi na mbili
Somo No  6
Kugeuka Nyuma na kuacha wokovu
Maarifa
Siku ya kumi na tatu
Somo No 13
Umuhimu wa kuhudhuria Ibada zoote
Maarifa
Siku ya kumi na nne

Baada ya kuwa tumewafundisha masomo hayo pia tunaweza kuwaimarisha kupitia masomo mengineyo mbalimbali tunayojifunza katika kanisa letu kama misingi ya imani n.k
Jinsi na namna ya kuwafundisha.
    Ni muhimu kukumbuka kuwa kuwafundisha ndio kunyonyesha kwenyewe kwa hiyo kila tunapowatembelea tufundishe na tuache kupiga story nyingine tusitoke katika lengo (Maombolezo 4;3-4),Sisi wenyewe ni muhimu kujifunza kujaa neno na ufahamu wakati waufuatiliaji tutakutana na maswali mengi ni muhimu kujiandaa basi kabala ya kwenda kufundihs hili litatuimarisha nasisi wenyewe” When you teaches you learn twice” tumuombe Mungu atupake kabali aya kwenda kufundisha  ili Mungu awabadilishe kwani maneno yetu tu hayawezi kuleta mabadiliko (2Timoth 4;13,Matendo 6;4) Tukiwa na wanafunzi wengi wa ufuatiliaji tunaweza kuwa na madarasa ya tirano (Matendo 19;8-10) Tuwahoji maswali ili kuelewa ufahamu wao,tuwakumbushe kuhudhuria ibada,kuwahi ibada,kusikiliza kaseti za neno la Mungu,Na kuwa mtu akisha okolewa mikutano ya injili kwake si ya muhimu kama kujifunza neno katika mafundisho (Mathayo 28;19-20) Mtu aliyeokoka haitaji kuhubiriwa bali kujifunza neno.

Somo maalum shule ya watenda kazi.

SOMO: KUSHUHUDIA KWA MANENO MACHACHE
Mithali 11;30 Mwenye hekima huvuta roho za watu, tunaweza tukawa ni watu tunaopenda sana kushuhudia lakini tukawa hatupati matokeo yanayokusudiwa endapo hatutakuwa na hekima.Nyakati za kanisa la kwanza  waliposhuhudia walipata matokeo mazuri zaidi na kuweza hata kuupindua ulimwengu (Matendo 17;5-6) Na nyakati zao ilikuwa ngumu sana kuifanya kazi ya kuhubiri injili,ilikuwa usipo mkiri kaisari kuwa ni Bwana unauawa kwa kutupwa kwenye matundu ya simba katika viwanja vya michezo ya Olympic sasa tutajifunza somo hili kushuhudia kwa maneno machache kwa kuzingatia vipengele vinne vifuatavyo;-
  • Madhara ya kutokuwa washuhudiaji.
  • Kushuhudia kwa maneno machache.
  • Umuhimu wa kukwepa kutumia maandiko mengi wakati wa kushuhudia.
  • Misingi minne ya kushuhudia kwa maneno machache.
Madahara ya kutokuwa washuhudiaji.
     (2Falme 6;24-33,7;1-9,Tito 1;15-16) Nyakati za Biblia wakoma wanne najisi waliamua kupeleka habari njema kwa watu wa mji. Hawakuweza kuwasahau wengine pale Mungu alipowafanyia wao muujiza kwa sababu ya njaa iliyokuwepo. Ikiwa watu hawa najisi waliona si shani kufurahia wokovu wa Bwana peke yao kwani walijua kuna madhara yatawapata sisi nasi tulikuwa najisi kabla ya kuokolewa na kwakuwa Mungu ametuokoa hatuna budi kuwashirikisha habari njema hizi na wengine ili waokolewe vinginevyo nasi madhara yatatupata tuwaalike wengine waje kula neno la Mungu (Ezekiel 3;7-9).
Kushuhudia kwa maneno machache.
      Kushuhudia kwetu mara nyingi kunapaswa kuzingatia uhusiano wa mwanamke na mwanaume katika wokovu, kama ilivyokuwa kwa Paulo (Matendo 12;3-4), kushuhudia mtu wa jinsia tofauti wakati mwingine kunaleta matokeo bandia.Kushuhudia  kwetu lazima kuzingatie kutumia maneno machache, Paulo mtume alikuwa mtu hatari sana  katika ushuhudiaji wa maneno machache ilikuwa ukimpa nafasi tu  anakugeuza kuwa mkristo (Matendo 26;27-28).Tusitumie maneno mengi wakati wa kushuhudia  maneno yetu hayaokoi anayeokoa ni Roho wa Mungu yeye atawashuhudia kwa habari ya haki, dhambi na hukumu.(Yohana 15;26-27,16;8,1Koritho 2;10),Tufahamu kuwa watu tunaowashuhudia wana shughuli zao hivyo maneno mengi yanaweza kuonekana kama unawapotezea wakati,Hivyo niu muhimu kutumia maneno machache sana wakati huo.
 Umuhimu wa kukwepa kutumia maandiko mengi wakati wa kushuhudia.
       Mtenda kazi anapaswa kuwa na ufahamu wa kutosha kutofautisha kati ya kuhubiri na kufundisha (Mathayo 28;19) Tunaposhuhudia tunahubiri tu kwa lengo la kumleta mtu kwa Yesu au kutubu dhambi zake na kuokolewa hapa tunahubiri watu kumuamini Yesu baada ya kuwa watu wameamini ndipo mafundisho hufuata  kwa msingi huo basi wakati wa kushuhudia hatuna budi kukwepa kutumia ufundi mwingi wa maandiko Yesu alikuwa akihubiri kwa kuyataja tu maandiko ingawa ulikuweko wakati alipopaswa kufunua na kutafuta maandiko (Mathayo 5;21-27,38,Luka 4;16-17)
Misingi minne ya kushuhudia kwa maneno machache.
     Yako mambo machache ambayo ni ya msingi kuyalenga wakati wa kushuhudia haya ndio kiini cha injili yetu wakati wa kushuhudia misingi hii ya ushuhudiaji iko minne;-
Ø  Wote tumefanya dhambi (Warumi 3 10-12,23, 5;12)
Ø  Hatuwezi kuzishinda dhambi kwa nguvu zetu (Yohana 15;5)
Ø  Uwezo wa kushinda dhambi unapatikana kwa Yesu tu (Waebrania 4;15)
Ø  Afichaye dhambi zake hatafanikiwa Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata Rehema (Mithali 28;13;Luka 1;77,1Yohana 1;9-10)
    Baada ya kuzingatia misingi hii minne katika ushuhudiaji muongoze sala ya toba. Aidha ni Muhimu wakati wa ushuhudiaji kutumia nneno TU badala ya U mfano woote TU mefanya dhambi badala ya Umefanya hii inapunguza ukali wa maneno na kupunguza hali ya kujihesabia haki mitume waliitumia wakijijumuisha na wao Mfano ktk Yakobo 3;2 1Yohana 1;8-9 twajikwaa,twatia n.k haya ni ya muhimu kwa ushuhudiaji Ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda.

Somo maalum shule ya watendakazi.

Somo: MSAADA KWA MTU ANAYESHUHUDIA
     Msaada kwa mtu anayeshuhudia ni somo maalumu lenye kutoa mwanga wa majibu husika kwa maswali au vikwazo wanavyokutana navyo watu wanao kwenda kushuhudia Hapa tunatoa baadhi ya mistari inayo faa kuwajibu wale wanaojificha katika kona za mambo kadhaa ili kukwepa kumpokea Yesu ingawa kumpokea Kristo ni hiyari lakini mshuhudiaji anapokuwa na uhodari wakujibu hoja hizo kwa kutumia maandiko inamweka mahali salama na kumfanya kuwa na majibu ya kibiblia kwa kila kikwazo anachokutana nacho maswala hayo ni kama ifuatavyo;-
  • Nimekusikia vizuri lakini uamuzi wangu wa kuokoka nitautoa siku nyingine
JIBU; Walakini hamjui yatakayokuwako kesho uzima wenu ni nini?…Mithali 27;1,Yakobo 4;14,2Koritho 6;2,Muhubiri 9;12.
  • Nitaokoka ngoja nitengeneze pesa na nizidi kuhifahamu dunia
JIBU; Kujitayarisha kwa Mungu ni jambo muhimu Luka 12; 15-21, Marko 8; 36
  • Nitaokoka nikiwa mzee basi
JIBU; Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako Muhubiri 12; 1, 10; 14, Mathayo 24; 42-44.
  • Siwezi kuiacha dini ya Baba yangu.
JIBU; Baba hatabeba mzigo wa mwana wala mwana hatabeba mzigo wa baba yake Eekieli 20;18, Marko 7;8-9 usiliache neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo
  • Kwani kunywa Pombe ni dhambi?
JIBU;Mithali23;20
  • Kwani kuvuta sigara,bangi,madawa ya kulevya,mirungi na ugolo  vimeandikwa wapi katika Biblia?
JIBU; Isaya 55;2
  • Mimi ni mtoto wa kikristo na nilibatizwa tangu utoto
JIBU; Tito 1;16,Luka 6;46,Warumi 10;13-14
  • Mungu ni mmoja tu ni njia tu ndo zinatofautiana lakini woote tunaelekea huko
JIBU; Yakobo 2;19 1Timotheo 2;5 Yohana 15;23,1Yohana 2;23 Yohana 14;6, 10;7,9
  • Haiwezekani kuokoka au kuwa mtakatifu ukiwa hapa duniani
JIBU; Yesu alikuja duniani ili kuokoa,kama wokovu ni mbinguni hapa alikuja kufuata nini,Watakatifu walioko duniani ndio waliobora …Luka 19;9-10,Yohana 5;34,Zaburi 16;3,Tito 2;11-12,Wafilipi 4;13,Tito 3;4-4
  • Mimi naenda kanisani kila siku sikosi,naimba hata kwaya nimzee wa kanisa pia natoa sadaka sana
JIBU; Marko 7; 6, Amosi 5;21-22,Ezekiel 33;31-32
  • Nikiokoka naona nitakuwa maskini
JIBU; Mathayo 27;57,.3Yohana 1;2 Hagai 2;8
  • Muziki wa dansi umekatazwa wapi katika Biblia?
JIBU: Isaya 5;12-14
  • Niliwahi kuokoka kisha nikaacha itakuwaje?
JIBU; 2Petro 2;20-22,Ufunuo 2;4-5 Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka ukatubu....
  • Bado nafikiria
JIBU Mithali 29;1.
  • Mi mpaka nimuelezee mume wangu anielewe anikubalie
JIBU; Wagalatia 6;5 Luka 20;34-36 Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe!
  • Naogopa kuwa mnafiki wengi walijifanya wameokoka na tunawaona wakifanya dhambi
JIBU, Warumi 14;12 Zaburi 37;37 Kila mtu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu
  • Endelea kuniombea siku nikiamua ndo iatakuwa moja kwa moja bila unafiki
JIBU Warumi 9;16 Zekaria 4;6
  • Maisha ya siku hizi unayajua sasa nitaisije na mshahara wa halali tu ikiwa nitaokoka
JIBU Mathayo 6;25-33,1Petro 5;6-7
  • Mi sipendi kutanga tanga
JIBU Mathayo 13; 45, Matendo 26;4-5,9-18 Mitume waliacha madhehebu yao
  • Mimi nauza pombe na nnaishi kwa hiyo na ninasomesha watoto sasa nikiokoka nitaishije?
JIBU Marko 9;43-48. mkono wako ukikukosesha ukate
  • Mi baba yangu ni mchungaji na ni muhubiri mkubwa
JIBU: Ezekiel 14;14,16,20.
  • Ninyi ndio wale manabii wa uongo waliosemwa watatokea
JIBU;  “Manabii wa kweli wa Mungu ,husema yaliyo ya Mungu  yaani sawa na neno la Mungu 2Nyakati 18;13,Yohana 3;34,Hesabu 22;18,Ezekieli 2;7 Nabii wa uongo huwaambia watu amani tu wakati ni maangamizi na hupoteza watu Ezekieli 13;9-10, Hakuna amani kwa wabaya Isaya 48;22
  • Kuokoka ni kwa watu maskini na mimi sina shida au nna shida gani?
JIBU; Mathayo 27; 57, Matendo 17;12. Wanawake wengi kwa wanaume wenye vyeo waliamini
  • Kanisa let undo la kwanza na lina watu wengi sana duniani kote;
JIBU; Yohana 14;6 10;7,9,Mathayo 7;13-14,Luka 13;24-25.
  • Hali ya uchumi ni ngumu inawezekanaje kuokoka katika hali hii
JIBU; Mathayo 19;25-26. Kwa wanadamu haiwezekani bali kwa Mungu yote yawezekana


Somo maalum shule ya watenda kazi.

Somo: WAJIBU WA KUTOA RIPOTI.
Mtu awaye yoote ambaye ni mtenda kazi katika shamba la Mungu anawajibika kutoa ripoti,Kwa msingi huu ni muhimu kwa kila mtenda kazi kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na somo hili  Wajibu wa kutoa ripoti amablo tutajifunza kwa kuzingatia vipengele sita vifuatavyo;-
  • Wajibu wa kila mtenda kazi kutoa ripoti.
  • Mfano wa Yesu Kristo katika kutoa Ripoti
  • Utoaji ripoti nyakati za kanisa la kwanza.
  • Mfumo wa kutoa ripoti na utekelezaji wake
  • Faida za kutoa ripoti.
 Wajibu wa kila mtenda kazi kutoa ripoti.
      Kila mtenda kazi ana wajibu wa kutoa ripoti ;katika kazi ya Mungu ni muhimu kufahamu kuwa tumetumwa na hatujajituma wenyewe,kwa kawaida mtu yeyeote aliyetumwa anaporudu huridi kwa aliyemtuma na kutoa Ripoti.Kutoa ripoti kunaonyesha tabia ya uaminifu (Hesabu 13;1-3,17-20) watu hawa walitumwa na waliporudi walitoa ripoti (Hesabu 13;25-27,Yoshua 2;1) Wengine walitumwa wakati wa Yoshua pia walitoa ripoti (Yoshua 2;23-24,7;2-3,1471,) Yoshua alitoa ripoti kwa Musa,sisi nasi kama watenda kazi tumetumwa(Isaya 6;8,Luka 9;2,Mathayo 28;19-20) Hao walitumwa (Yohana 17;18). Kama Yesu alivyotumwa na Babaye yeye naye ametutuma sisi, ikiwa tu watumwa kwa Mungu inatupasa kujizoeza tabia ya kurudi na kutoa ripoti (Luka 17;10).
Mfano wa Yesu Kristo katika kutoa Ripoti
Yohana 8;42.Yesu alikuja duniani kama Mtumwa aliyetumwa na Baba (Warumi 8;3). Yesu alitumwa aje kutukomboa  (Galatia 4;4-5 1Yohana 4;9-10,14) Na alifanya kazi kama alivyotumwa (Yohana 4;34) alipoikamilisha kazi ile aliyotumwa alitoa ripoti (Yohana 17;1-4;6-8,12-14) Ikiwa Mungu Yesu Kristo alitoa ripoti sisi ni nani basi tusitoe ripoti ni muhimu kujifunza kutoa ripoti ya kile tunachikifanya mara baada ya kazi
Utoaji ripoti nyakati za kanisa la kwanza.
      (Mwanzo 8; 6-12). Mtu asiyetoa ripoti anafananishwa na kunguru aliyetumwa wakati wa Nuhu na asirudi, Yeye aliyetoa ripoti anafananishwa na njiwa aliyerudi kutoa ripoti.
Ø  Kutokutoa ripoti ni udhalimu (Luka 16;10-12) wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu (1Koritho 6;9a)
Ø  Kutokutoa ripoti ni kumdarau aliyekutuma (Isaya 2;30) Tunaheshimika mbele za Mungu kwa kumtumikia (Hesabu 14;23,Isaya 1;4)
Ø  Mtu asiyetoa ripoti ni kama amerudi nyuma amefarakana na Mungu.
Ø  Kutokutoa ripoti ni dalili ya kiburi na kujiona kuwa tu zaidi ya Bwana Yesu na mitume (Mithali 11;2) inatupasa kuwa wanyenyekevu kutoa ripoti ni ishara ya utii na unyenyekevu (Mithali n16;18.29,23.Yeremia 30;29,31-32,Malaki 3;18,4;1)
 Mfumo wa kutoa ripoti na utekelezaji wake
 Kila mtenda kazi anapaswa kujitolea ripoti ya kile anachokifanya kila siku kuhusu kazi ya Mungu na kutoa ripoti ya wiki au mwezi au mwaka kulingana na mapatano ya kanisa husika maeneo ya muhimu yanayopaswa kzingatiwa wakati wa utoaji ripoti ni pamoja na
Ø  Ushuhudiaji,Umeshuhudia wapi,kina nani na matokeo yake
Ø  Ufuatiliaji,Umefuatilia wapi,kina nani,wamehudhuria ibada au la na matokeo
Ø  Kusoma neno,Umesoma wapi,umeelewaje kitabu gani sura gani mistari ipi
Ø  Kusikiliza neno, Umehudhuria ibada?,Umejifunza nini,semina,mkutano n.k
Ø  Maombi umeombea nini muda uliotumika matokeo n.k
Kila mtenda kazi atajitolea ripoti katika maeneo hayo makuu matano Mungu atuwezeshe.
Faida za kutoa ripoti.
      Ziko faida nyingi sana zinazoambatana na wajibu wa kutoa ripoti baadhi ni kama zifuatazo;-
Ø  Zinatupa changamoto ya kuishi maisha ya kukesha na kuomba (Mathayo 24;42-44)
Ø  Hufanya mchungaji wako ajue vipawa ulivyo navyo karama  na ni namna ya kukusaidia ili kukupa msaada zaidi au kwa ajili ya Utumishi wa juu (2Tomoth 1;6)
Ø  Inatusaidia kujitiisha kwa kiongozi wa kanisa Yesu Kristo na kutufanya tuwajibike tuonywe na kukemewa (Ebrania 12;5-13)
Ø  Inamsaidia mchungaji katika kulichunga kanisa.
Ø  Inatuzoeza kuwa wanyenyekevu na watii
Bwana na ampe neema kila mmoja wetu kuyazingatia haya tuliyojifunza na kuyafanyia kazi na kuzidi katika jina la Yesu.

Somo maalum shule ya watenda kazi.

SOMO: NGUVU KWA AJILI YA UTUMISHI
     Ni muhimu kufahamu kuwa pamoja na mafundisho mazuritunayoyapata katika shule hii ya watenda kazi mafanikio yetu katika mambo yoote tuliyojifunza hayawezi kufanikiwa endapo tutamweka Pembeni Roho mtakatifu,Roho mtakatifu hutoa nguvu itakayotufanya kuwa mashahidi wazuri na ndio maana pamoja na mafundisho mazuri aliyoyatoa Yesu Kristo kwa wanafunzi wake kwa karibu zaidi miaka mitatu na nusu  Bado aliwasisitiza wanafunzi wake wasitoke mpaka wamevikwa uwezo utokao juu, (Luka 24;49,Matendo 1;8) .Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo;-
  • Umuhimu wa Nguvu za Roho Mtakatifu.
  • Jinsi ya Kupokea nguvu za Roho Mtakatifu.
Umuhimu wa Nguvu za Roho Mtakatifu.
         Roho mtakatifu ni wa muhimu sana katika maisha na utumishi wa mkristo yeyote, Lakini ni wa muhimu zaidi sana kwa watu wanaotaka kumtumikia,Kwa ufupi yeye hutoa nguvu kwa ajili ya utumishi.Nyakati za kanisa la kwanza swala la mtu kujazwa  Roho mtakatifu lilikuwa ni swali muhimu kwa wakristo kama ilivyo wokovu au kuongoza mtu nsala ya toba (Mdo 8;14-17,19;1-7) kwa nini ni wa muhimu hivi ;-
Ø  Ni suluhisho la maongozi (Mwanzo 41;38-40,Daniel5;5-12,Hesabu 11;10-17)
Ø  Ni suluhisho la uonevu dhidi ya maadui (Waamuzi 14;5-6,15;3,14-16)
Ø  Ni suluhisho la upinzani wa kidini (Matendo 6;8-10,7;55).
Ø  Ni suluhisho dhidi ya Nguvu za giza (Kutoka 7;10-13,Daniel 5;7,Hesabu 23;7-8,22-23,Matendo 8;4-21,13;6-12)
Ø  Tatizo la uonevu dhidi ya Ibilisi (Luka 4;18-19,Mdo 10;38)
Ø  Ni suluhisho la kutupa hekima (1Falme 3;16-27,Mdo 15)
     Kwa msingi huo basi iwapo Mungu anatutuma kati ya watu wanaoonewa na wenye shida za aina mbalimbali Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana ukilinganisha na uhitaji ulioko wa matatizo ya watu tunaokwenda kuwahudumia ,Kila mtenda kazi ni lazima ahakikishe amejazwa na Nguvu za Roho mtakatifu na anadumu katika nguvu hizi na ndipo tutakapoweza kufanya huduma hii kwa ufanisi Mkubwa.
Jinsi ya Kupokea nguvu za Roho Mtakatifu.
     Roho mtakatifu ni Mtakatifu kwa msingi huo kuwa mbalu na dhambi ni jambo la muhimu ili yeye akae ndani yetu.(Yohana 3;3-6).
Roho mtakatifu ni ahadi ya Mungu kwetu hivyo ni lazima tuipokee kwa imani (Matendo 2;38-39). Wakati wa maombezi ya roho mtakatifu tusiogope kupokea roho nyingine Mungu si dhalimu kile tuombacho ndicho atupacho (Luka 11;9-18)..Wakati wa maombi kuhusu ujazo wa Roho mtakatifu inashauriwa watu waombe kwa sauti kubwa hii itasaidia wewe kupokea lugha ya kimbinguni na kusikika ukinena kwa Lugha mpya usiyoijua, (Luka 3;21-22) Tunaweza pia kupokea Roho mtakatifu na nguvu zake kwa kuwekewa Mikono (Matendo 8;17).

Maoni 1 :