Alhamisi, 25 Februari 2016

Jamaa Wakasema Wananitoa Pepo la Ngono!



Nimelazimika kuelezea kisa hiki ili kwamba wengine nao wajifunze kupitia tabia zangu nilizokuwa nazo mwanzoni lakini kwa sasa nimebadilika kabisa na nimekoma, kwa ujumla mimi nilizaliwa katika familia ya watoto nane na wengi wa walionitangulia walikuwa ni wanawake nikimaanisha kuwa wanne wote walikuwa ni dada zetu kisha alifuata kaka ambaye ni watano na mimi ni wa sita na wakamalizia wadogo zangu wawili nao wa kiume, wote tumekuwa watu wazima sasa na kila mmoja ameoa na kuolewa isipokuwa mimi nilikawia kuoa eti ili niyafurahie maisha kwanza, nilikuwa muhuni mpenda sifa na mpenda wamama kwa sana  na kigezo kikuu kilichonipelekea kuwa na tabia hiyo ya ufedhuli ni pamoja na malezi niliyokulia yaliyochangiwa sana na dada zangu.

 
 Kweli Mapepo ya ngono yaliondoka kabisa

Dada zangu walikuwa wakinisifia tangu utoto kuwa mimi ni kijana mzuri sana ‘handsome’ na jambo hili nililisikia likirudiwa na wenzangu shuleni na hata majirani sifa hii ya uzuri niliyokuwa nayo ilinifanya kuwa mpenda wanawake sana na kwa ujumla kila mwanamke niliyekuwa nikimtaka kimapenzi tangu shuleni ilikuwa ni vigumu kunikatalia hii ilinijengea imani kubwa kuwa hakuna mwanamke anaweza kunikatalia. Nilipomaliza shule ya Sekondari pale Lugalo ambayo kwa sasa inaitwa makongo nakumbuka ilikuwa mwaka 1992, niliingia mtaani na kujihusisha na maswala ya biashara lakini wakati wote huo sikuacha kujishughulisha na maswala ya wanawake, Mwanzoni nilikuwa nikiwafuatilia sana wanafunzi wenzangu na wasichana wa kawaida lakini baadaye uovu wangu ulipanda cheo na nikawa napenda sana kutembea na wake za watu tabia hii ilikuwa sugu sana na ikanijengea dhana kuwa kumbe wake za watu ni watamu sana na hivyo niliacha kuwasumbua wasichana wakawaida nikiwaita wanuka chupi tu, nilijifunza sana namna ya kuwapata wake za watu hata wale waliokuwa na uwezo mkubwa sana kwani nilikuwa na muda nao wa kutosha waume zao wanapokuwa makazini, wakati huu biashara yangu ilikuwa ni kusambaza Mboga na matunda kwa kutumia mkokoteni katika maeneo ya Survey Mlalakuwa, mwenge na Sinza, na  nilikuwa nikikusanya bidhaa zangu huko Kariakoo shimoni na kuweka kituo changu pele sinza Magengeni, ambako nilikuwa na bao la kuuzia bidhaa na nilimuacha hapo dada ambaye nilikuwa nimemuajiri, Mimi nilikuwa nikitembeza kwa mkomkoteni maalumu bidhaa hizo majumbani na huko ndiko nilikokuwa nikipata nafasi ya kutembea na wake za watu.

Kitu kikubwa nilichokuwa nimejifunza wakati huu ni kuwa wanaume wengi wanafikiri kuwa wanawake wanahitaji kuwa na masofa, kuishi kwenye mageti makubwa, kuwa na kila kitu lakini walikuwa hawana muda wa kusikiliza hisia za wake zao, na kuwa na muda nao, na pengine kufanya nao mapenzi kichovu kwa sababu ya suluba za kazi hapa Dar, wengi nilizungumza nao kwa kuwaonyesha huruma sana, kwa kuwa bembeleza kustawisha uhusiano nao, na wanapofungua mlango wa kimapenzi nilionyesha uhodari wangu wote kuanzia namna nilivyovinjari maeneo yote nyeti taratibu kwa kujiamini na kufunga magoli kwa ustadi mkubwa na kwa sababu ni hali za wizi hamu ilikuwa haiishi kulikuwa na utamu wa ajabu sana yote hii ilichangiwa na sifa nilizopewa na dada zangu kuwa mimi ni mzuri na imani kuwa hakuna mwanamke awezaye kukataa duniani hii ilikuwa falsafa yangu moyoni na ilinifanikisha sana katika maswala ya dhambii hii ya kuvunja amri ya sita.

Siku moja ambayo ilinipelekea kufikia kuelezea kisa hiki na maisha yangu kubadilika ilikuwa ni kule Kariakoo shimoni ambako nilikuwa nikifika mara kwa mara kwaajili ya kufungasha bidhaa kwa jamaa zangu, huko alikuweko mama mmoja aliyekuwa akijishughulisha na shughuli za kuuza chakula na chai kwa wafanya biashara pale shimoni, nilimtamani sana ingawa pia nilikwisha fahamu kuwa alikuwa mke wa mtu,  ambaye naye ni mfanya biashara ambaye zamani alikuwa kuli yaani wale wanaoshusha mizigo pale shimoni kariakoo, baadaye maisha yalimchanganyia na akawa anafanya biashara ya kuendea bidhaa mikoani na kuzileta pale kariakoo, hivyo wakati huu alikuwa akisafiri mara kwa mara.

Yule mama alikuwa anapendeza sana kwa ujumla alikuwa mzuri kiasi kuwa nilijiuliza kwanini alikuwa akiuza chai na chakula hata ingawa kwa Dar na pale eneo alilokuwako alikuwa akiingiza Fedha sana kuliko wale wanaofanya kazi ofisini,  nilijaribu kumtongoza dada huyu kila nilipokwenda shimoni kuchukua bidhaa, nilianzisha katabia ka kunywa chai au kula chakula kwake, lakini pia nilikuwa nikichukua muda mrefu sana pale kwake na kujaribu kumchombeza chombeza huku nikiuza sura ambayo nilifikiri haiwezi kukataliwa hata siku moja kwa sababu ya uzuri niliokuwa nao, lakini katika namna ya kushangaza dada huyu alinikatalia kabisa,  na kujifanya kuwa ni mtu anayeheshimu sana ndoa yake,  nilijaribu kumkejeli kuwa wake za wakubwa na watu maarufu tu wanaliwa sembuse yeye muuza chai!.. nilipoona kuwa haingii laini niliamua kumfanyia mauzi kwamaana sasa tongoza yangu ilikuwa ya kuuzi na kudhalilisha, dada huyu alionekana kuchukizwa kabisa na mimi na hakutaka hata niwe nafika pale, nikiwa na imani kuwa hakuna mwanamke anayekataa duniani au anayeweza kunikatalia mtu kama mimi sikuamini kuwa dada Yule anaweza kunikataa, kwani ilikuwa mara ya kwanza kabisa kukutana na kisiki cha namna ile, niliendelea kumsumbua kwa mauzi siku hadi siku nikiamini iko siku atanikubalia tu.

Sikuwa nimefahamu kuwa Dada Yule alikwisha kumueleza mumewe usumbufu niliokua nikimfanyia Mumewe ambaye alikuwa mstaarabu hakuonyesha kukasirishwa lakini alikusudia mpango fulani ikiwa nitaendelea kumsumbua lakini hiyo ilikuwa siri yao ambayo nilikuja kuitambua baadaye
Dada Yule siku mmoja nilikwenda kwake kama ilivo desturi yangu niliagiza chai na chapati na kibakuli cha maharagwe kama supu kwani hiyo ndio desturi ya wengi wanaofika hapo, nilivizia watu wamepungua na tumebaki wenyewe na nikaanza tena kumbembeleza vijana wa mtaana wanasema kupiga sound nilimbembeleza sana kwa kulalamika namna anavyoutesa sana moyo wangu kwa siku nyingi siku hiyo dada huyu anayeitwa Mariamu alionekana kuwa amenionea huruma  kwani alinikubalia lakini alinipa masharti kuwa yeye hajawahi kufanya mapenzi katika nyumba za kulala wageni wala wakati wa shughuli kwa hiyo alikuwa akinikatalia kwa kufikiri kuwa sikuwa namaanisha kwani wateja kama mimi waliokuwa wakimsumbua wako wengi kwa hiyo alinichukulia kama moja ya wateja hao lakini kwakuwa aliona kuwa mimi nimemaanisha kwa kumbembeleza mpaka ninalia aliamua kukubali lakini alisema ni lazima nifike nyumbani kwake jioni kwani Mumewe yuko mkoani kwaajili ya kufungasha bidhaa, alinihakikishia kuwa naye alikuwa anavutiwa na mimi lakini alitaka kujua kama nimemaanisha au ilikuwa ni kama ninabeep, alinichorea ramani ya kufika mpaka nyumbani kwake ambako walikuwa wanakaa maeneo ya Msewe nyuma ya chuo kikuu cha Dar es Salaam karibu na nyumba ya chifu mmoja maarufu wa zamani katika serikali ya awamu ya kwanza,  alinibusu na kuniomba kuwa nisimuangushe.

Mwanaume nilioga vizuri sana baada ya shughuli zangu za kazi, nilijipaka mafuta mazuri sana mwili mzima na pafyumu kisha nikauramba yaani kuvaa smati wakati ule tulikuwa tunaita kuuramba mkanda nje, nilipanda Daladala ya mwenge – Ubungo kupitia chuo na kushuka maeneo ya utawala kisha kuteremka kwa miguu upande wa kushoto nyuma ya chuo, nilivuka mfereji ambao kwa hapa Dar ni kama mto Fulani, na pia palikuwa na bustani kadhaa za walima mchicha, niliiona nyumba ya chifu na kaburi lake kama nilivyoelekezwa kisha nikanyooosha njia upande wa kulia kuelekea hapo nilipokuwa nimeelekezwa, na nilifanikiwa kufika kwa Mariamu nyumbani kwake, siku hiyo kulionekana kumetulia sana na kwa kweli walikuwa wamejiendeleza sana, nilikaribishwa kwenye sofa nzuri na Mariamu alinibusu kuonyesha kuwa siku ile ilikuwa ni siku ya kuua tembo kwa ubua kwani Mariamu alikuwa mzuri sana alikuwa ameumbika haswa na nilihisi ilikuwa ni halali anisumbue lakini nilipanga kuwa nitamuonyesha mapenzi ambayo yamepagawisha wengi na kuwa mke huyu wa kuli msataafu atakuwa nyama yangu. Mariamu aliniuliza utatumia kinywaji gani, niliagiza Soda aina ya sprite ambayo huwa naipenda sana, Mariamu aliondoka kuelekea sehemu kama jikoni ambako kulikuwa na Friji na alinitengea soda na glasi akinipoza moyo kuwa siku ile nitalala palepale kwani mzee yuko mkoani. Nilipunguza hofu nakujiweka sawa mwili legeza ili kwamba hata nitakapoingia kwenye shughuli nisiwe na Presha, nilimpania sana mtoto Yule aliyekuwa amenisumbua kwa miezi kadhaa, Mariamu aliaga kwa Muda wakati nakunywa soda alisema samahani kidogo mpenzi laazizi nakuja uwe huru tu, kisha aliinuka kuingia chumbani, kulikuwa na ukimya wa dakika kadhaa na kisha Ghafla walitokea wanaume kama wanne hivi ambao wamejazia kuliko kawaida ni majitu hasa meusi sana walikuja taratibu kama waigiza sinema hivi wakinikabili pale sebuleni, mimi nilikuwa ni kimbaumbau na moyoni kwa haraka netiweki zangu ziliniashiria kuwa leo nimekwisha! nilipigwa ganzi na chini nilihisi kama nguo yangu ya ndani ilikuwa hainitoshi yaani inabana, pia nilihisi kama viungo vya kwenye kiuno vinasinyaa kwa kasi ya ajabu nilipokuwa nikifikira hayo ghafla jamaa waliniinua juu juu na mara walinichojoa suruali yangu kwa dakika chache sana nilijikuta nikiwa uchi wa mnyama nikiwa nimechanganyikiwa sijui la kufanya nilipigwa vibao kadhaa  na kulazimishwa kuinama nikiwa uchi wanaume hao ambao kumbe walikuwa ni makuli wa kule Karaiakoo shimoni walifungua zipu zaona kuni…’ kwa kweli nilidhalilishwa kwa namna ambayo haiwezi kuelezeka, wanaume wale walikuwa na mafuta yaliyokuwa yanateleza sana kwahiyo waliyamimina na kunidhalilisha mno, baada ya kumaliza utaratibu huo wa kwanza walipiga kelele na kunitoa uani ambako wakazi wa msewe walijaa,kushuhudia ugoni nikiwa uchi wa mnyama nilikalishwa kwenye kigoda na mtu mmoja ambae alikuwa kama msanii au mganga wa kienyeji alikuwa na ndoo ya maji yaliyochanganywa na mabonge ya barafu na kata ya kutekea maji alinikalisha kwenye kigoda huko uwani watu wakiwa wamejaa na kuzomea sana jamaa huyu msanii alichota maji ya barafu na kunimwangia huku akiimbisha wimbo wa kunitoa Pepo la ngono, huku watu wakipiga kelele mtoe tumuue  nilihisi mwisho wa dunia kwangu umefika barafu ilipenya mwili mzima ikifuatiwa na kipigo mwili mzima ilikuwa kama nimepigwa ganzi, nashindwa kuelewa ilikuwaje kwani nilikuwa nashindwa kulia au kupiga kelele nilikuwa nagumia tu na kuomba radhi lakini makofi yalizidi na bakora na viboko vilivyotumiwa kunitoa pepo la ngono vilininyeshea kama mvua ndugu usisikie kufumaniwa jambo hili linatisha unakuwa kama popo wakati wa mchana nguvu ya kufanya lolote inakuwa haipo na unahisi ni sawa kwa kila unachofanyiwa kwani unajua wazi kuwa ulikuwa hufanyi vizuri kwa wengine, kisha niliamuriwa kuingia ndani na kurudishiwa nguo zangu na ndipo jamaa mwenye mke alinisomea risala kuwa kuna wanawake wengi wa kuchezea duniani lakini sio wake za watu!. “Aliniambia si kila kichaka kinanyewa” Najua umekodoa mijicho yoye miwili ukitaka kujua ilikuwaje mitanzania kwa umbeya bwana! Kwani utanilipa zawadi gani? au kuna kampuni ya umbeya imekupa tenda ya kufuatilia mambo ya watu? Si nakuuliza! Kwa kufupisha habari kweli pepo la ngono limetoka, Mimi sasa mke wa mtu yeyote Yule namuheshimu kuliko Raisi wa jamuhuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni