Mstariwa Msingi 1wakoritho 9;27 “Bali nautesa mwili wangu na
kuutumikisha isiwe nikiisha kuwahubiri wengine mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”
Adam na Eva wakifukuzwa katika Bustani ya Eden (Neno Eden maana yake Uwepo wa Mungu)
Tunapokuwa tumeokolewa kwa kutubu
dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha na
kuliitia jina la bwana na damu yake ili
itutakase dhambi zetu tunakuwa
tumealikwa katika harusi ya mwana kondoo Yesu Kristo na furaha ya baba yetu
aliye mbinguni, hata hivyo ni makosa kufikiri kuwa kila mtu aliyeitwa na
kuokolewa kuwa atakwenda mbinguni bila kujali kuwa anafanya nini . Yako
mafundisho potofu yaitwayo “Eternal Security” yanayoeleza kwamba mtu akiisha
kuokolewa ameokolewa (once saved forever saved ) basi hata afanye nini yeye ni mtoto wa Mungu na ataingia mbinguni
na hutumia maandiko yafuatayo kufundisha
uzushi huo Warumi 8;33, Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu?, Mungu ndiye
mwenye kuwahesabia haki”Warumi 8;1”…..Hakuna hukumu ya adhabu juu ya hao walio
katika Kristo Yesu” Yohana 10; 27-29 “….Nami nawapa uzima wa milele wala
hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu” ni makusudi ya somo hili basi kujifunza ili kuifahamu
kweli juu ya jambo kama hilo ili tuwekwe huru mbali na mafundisho yaliyo potofu
Mfano wa safari ya wana wa Israel.
Safari hii ni kama mfano au
kielelezo cha safari ya watu waliookolewa kuelekea mbinguni, kama vile wana wa
Israel walivyookolewa kutoka Misri kuelekea kanaani, jambo la kushangaza ni
kuwa sio wana wa Israel wote waliotoka Misri
kuelekea kanaani walifika. Neno la Mungu linatuonyesha kuwa wengi waliangamizwa
Jangwani ili kuwa mfano kwetu 1Wakoritho 10;1-6.
Mfano wa Paulo Mtume .
Mtume Paulo ingawa alikuwa
Muhubiri mkubwa wa injili na mwalimu wa Neno la Mungu mwenye wingi wa mafunuo
na miujiza ya kupita kawaida iliyoambatana na huduma yake bado alikuwa anajua
kuwa hajafika bado alijua kuwa anaweza kukataliwa ikiwa hata kishika kile
alicho nacho mpaka mwisho 1Wakoritho 9;26-27 mtume Paulo hapa anasema hata mimi
Mstari wa 26 ikiwa Paulo angeweza
kukataliwa baada ya kuitwa ni zaidi sana wewe na mimi.
Ulinganifu wa maandiko unaofundisha uwezekano wa kukataliwa baada ya
kuitwa
Biblia imejaa maandiko mengi
yanayotuthibitishia kuwa kuna uwezekano wa kukataliwa baada ya kuitwa, tunaona
pia kumbe kuna uwezekano wa Mtu kufutwa katika kitabu cha uzima maandiko haya ni pamoja na
Kutoka 32;32-33, Yoshua 24;20,
1Nyakati 28;9,2Nyakati 15;2,Yeremia 18;10,Ezekiel 18;24 Ezekiel
33;12-13,Mathayo 5;13 ,10;22, Yohana 15;6,Warumi 11;22, 1Timotheo 1;19, Waebrania
3;12-14, 8;9 2Yohana 1;8, Ufunuo 22;18-19
Waitwao ni wengi bali wateule ni wachache Mathayo 22;14
Wateule ni wale ambao hata baada
ya wokovu wanaendelea kumtii Mungu katika kila eneo la Neno lake, malaika
walioendelea kumtii Mungu baada ya malaika mkuu Lucifer kuasi na ambaye sasa ni
shetani wanaitwa malaika wateule soma 1Timotheo 5;21 Warumi 8;33 Biblia
inaposema ni nani atakayewashitaki wateule inamaanisha wale ambao baada ya
kuitwa wanaendelea kuongozwa na kulitii
Neno la Mungu hao hakuna atakayewashitaki
mtu anayempendezaa Mungu siku zote ni ngumu kupata jambo la kumshitaki
kama ilivyokuwa kwa Bwana Yesu Yohana 8;29, kila mtu ambaye maisha yake
yanaongozwa na neno la Mungu hawezi kuadhibiwa Warumi 8;1, Kristo Yesu ndiye
neno la Mungu lenyewe Ufunuo 19;13 kila anayemfuata Yesu na kushika kielelezo
chake hataweza kuadhibiwa.
aidha ni muhimu kufahamu kuwa
Biblia inaposema kuwa wala hawatapotea
kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu Yohana 10;28 ina
maanisha nini kumbuka kuwa hakuna mtu aliyekuwa katika mikono ya Yesu kama Yuda
Iskariote aliyekuwa mweka hazina wake
lakini amepotea yuko motoni milele,
pamoja na kutumiwa katika kuhubiri na kutoa pepo Yuda alipotea ili mtu asipotee ni lazima aisikie sauti ya
Yesu na pia kumfuata maana yake ni kuwa
lazima tuishi sawa na neno la Mungu ili
tusipotee Zabiri 119;9
Mambo sita ya msingi ya kuyaangalia ili tusiwe watu wa kukataliwa baada
ya kuitwa
·
Maisha Yetu katika wokovu ni lazima yawe sawa na
injili yuote na sio sawa na dhehebu fulani Warumi 2;16
·
Tusikubali kufarijiwa na kukataa kuonywa ,
kukaripiwa na kukemewa kwa neno la Mungu
Ayubu 16;2, Isaya 30;20-21, Wafilipi
3;12-14
·
Penda mafundisho zaidi baada ya kuokoka kuliko
mahubiri, mahubiri lengo lake ni kutuleta kwa Yesu na mafundisho ni kutupa
maarifa ili kujua yatupasayo kujua kwani kuna aina mbili za dhambi (a). Kutenda
yasiyotupasa 1Yohana 3;10 na (b). kutokutenda yanayotupasa kutenda Yakobo
4;17 bila mafundisho hatuwezi kufahamu
yanayotupasa kutenda mpaka tumedumu
katika mafundisho Mambo ya Walawi 5;17
·
Tusikubali kuandamana na mkutano katika kutenda
uovu, neno mkutano maana yake ni watu
wengi hatupaswi kuridhika kufanya jambo
eti kwa sababu watu fulani wengi wanafanya, wakati wa Nuhu watu wote ulimwengu
mzima waliangamizwa na ni watu nane tu walioachwa hai Luka 13; 22-23, Kutoka 23;2 tumwangalie Yesu
tu na sio wanadamu Zaburi 37;37
·
Inatupasa kulifuata neno la Mungu bila kuchagua
la kufuata Kumbukumbu 1; 35-36.
·
Kila unapogundua kuwa umamfanya Bwana dhambi
inakupasa kutubu 1Yohana 2;1-2, kumbuka kumkana Bwana ni kujitafutia mauti
Hesabu 15;30-31 tunahitaji kuvumilia hata mwisho ili kukamilisha wokovu wetu
Mathayo 24;12-13.
Je dalili ya kwamba umekataliwa na mungu ni ipi
JibuFuta