Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Dhambi ya Utoaji wa Mimba !



Somo la Saba.
Vijana na dhambi ya utoaji wa Mimba.
 Utoaji wa Mimba ni moja ya matatizo makubwa yanayokua kwa kasi duniani ni tatizo linalowakumba hasa vijana na ziko sababu nyingi ambazo huonekana kuwa ni halali au ni haki kwa watu kujihusisha na utoaji wa Mimba kama ilivyo kwa tatizo kwa utazamaji wa picha za kingono kama hakutakuwa na njia yoyote ya udhibiti wa picha za kingono tatizo la utoaji wa mimba litaongezeka kwani ni moja ya matatizo pacha Hii ni dhambi kubwa kama ilivyo kwa dhambi nyingine Gazeti moja maarufu nchini Marekani The Washington post  la januari 23, 1983  liliripoti kuwa kati ya mimba nne zinazotungwa nchini humo moja huishia kutolewa iwapo jambo hili lilikuwa hivyo 1983 unafikiri hali ikoje sasa hapa nchini ni muhimu basi sisi nasi tuka liangalia somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo;

  • Jinsi Mungu anavyouangalia uhai ulioko Tumboni.
  • Hukumu ya mungu dhidi ya wale wanaojihusisha na utoaji wa mimba
  • Wajibu wa wakristo juu ya utoaji wa mimba.
Jinsi Mungu anavyouangalia uhai ulioko tumboni.
   Ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu wakati ambapo dunia inaona utoaji mamba ni jambo halali kwa sababu zao mbalimbali sisi tunapaswa kuliangalia jambo hili kama Mungu anavyoliangalia, Mungu hujali sana uhai ulioko tumboni, Mungu huwa na taarifa za kila kiumbe na hatua za kila kiumbe vikiwemo vile vilivyoko Tumboni na maandiko yanatufundisha hivyo Isaya 44;24 hapo Biblia inasema “Bwana,mkombozi wako yeye aliyekuumba  tumboni asema hivi mimi ni Bwana nifanyaye vitu vyote…”  Mwandishi wa zaburi anaonyesha jinsi Mungu alivyokua akijishughulisha na uumbaji wa mwanadamu mfupa kwa mfupa na kiungo kwa kiungo huku akiamuru miaka ya kuishi kwa mwanadamu huyo hata kabla ya kuishi hii humaanisha maisha ya tumboni ni maisha kamili na halali kabisa mbele za Mungu, (Zaburi 139;13-16) wako watu wanaofikiri kuwa uhai kamili wa mtu huanza mara anapozaliwa lakini kisayansi na kisaikolojia na kibiblia inakubalika kabisa kuwa Maisha ya Mwanadamu huanzia tumboni tena siku ya mimba kutungwa,kisayansi inakubalika kabisa kuwa virithia vya kibinadamu kitaalamu genetic codes za mtu huanza kuamuliwa na kuwa tayari kuwa mwanadamu huyu atakuaje tangu siku ya kutunga mamba hizo genetics virithia huamua kuwa mtu huyo atakuaje kimwili,kiakili,kihisia,na kwa kweli vitaendelea katika maisha ya mwanadamu huyo vikiboreshwa tu na maswala ya kimazingira,Kibiblia  tunazo shuhuda nyingi za Mungu kujihusisha na viumbe vilivyoko tumboni kama viumbe kamili Malaika Gabriel alitabiri kujazwa Roho Mtakatifu kwa nabii Yohana tangu akiwa tumboni (Luka 1;15) hii inamaanisha kuwa  kuwa Mungu anahusika na maisha ya viumbe vilivyoko tumboni yakiwemo maisha ya kiroho,Daudi alipokua akitubia uovu wake alisema kwa asili alikuwa muovu tangu tumboni mwa mamaye (Zaburi 51;5) Si hivyo tu lakini tunaona jinsi Mungu alivyomchagua nabii Yeremia alisema maneno haya  “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua,na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa,nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” (Yeremia 1;5),Unaona tunawezaje basi kuhalalisha utoaji wa mimba kwa madai kuwa kiumbe hicho hakijaanza kuishi mbona wako watoto wanaozaliwa wakiwa na miezi 6 au7 au 8 na wameishi wakiwa wanadamu kamili  hebu tujiulize ni nani ana haki ya kuishi kati ya mtu mwenye umri wa miaka 70 na mimba ya miezi mitatu au mtoto wa miaka miwili? Uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu uwe ni wa miezi miwili au miaka 30 woote wana haki sawa ya kuishi Mungu atawahukumu wale woote wanaocheza na uhai, Mimba inaweza kutolewa tu endapo kitaalamu inahatarisha maisha ya mama au mtoto aliye tumboni yanapotokea matatizo ya moja aishi moja afe ili kuokoa mojawapo.

 Vitoto vingi vinauawa vikiwa tumboni na jamii ya kisasa na kisomi imenyamazia ugaidi huu

Hukumu ya Mungu dhidi ya wale wanaojihusisha na utoaji wa mimba
   Kama uhai wa viumbe walioko tumboni unathamani kwa Mungu je unafikiri Mungu anawaza nini kwa watu wanaotoa mimba au wanaojihusisha na kusaidia utoaji wa mimba? Biblia inasema nini?(Mwanzo 9;5-6) “Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka;na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka na kwa mkono wa mwanadamu nitaitaka,kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu,Atakayemwaga damu ya mwanadamu,damu yake mtu huyo itamwagwa na mwanadamu,maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.” Muda usingelitosha kunukuu kila andiko lakini  Mungu alikataza kumwaga damu isiyo na hatia (kutoka 23;7) aidha biblia inatamka laana kwa kila mtu anayemwaga damu isiyo na hatia (Kumbukumbu 27;25 Yerenia 22;17,2;34-35) mtu yeyote anayejihusisha na uuaji wa viumbe walio tumboni ni muuaji kama wauaji wengine,mimi kama mtumishi wa Mungu na nabii nitoe wito wa toba kwa woote waliowahi kujihusisha na utoaji wa mimba wawe madaktari ambao kwa kutumia taaluma zao ambazo hulenga kuokoa maisha ya mwanadamu wao wametumia kuangamiza uhai watubie dhambi hii aidha wasichana au wanawake waliojihusisha na utoaji wa mimba watubie aidha nichukue nafasi hii kutoa changamoto kwa serikali na bunge  kutokupitisha sheria zinazohalalisha vitendo hivi haraamu na pia kuchukua hatua kali kwa wale wenye kujihusisha na vitendo hivi katili vya mauaji ya Binadamu wadogo wachanga wasioweza kujitetea ambao vilio vyao huishia kwa Mungu na hivyo kuleta hukumu ya mungu kwa taifa letu.

Wajibu wa wakristo juu ya utoaji wa mimba
Kila mkristo anawajibika kupinga vikali vitendo vya utoaji wa mimba ziko baraka zinazo ambatana na kulinda viumbe vichanga visivyo na uwezo wa kujitetea juu ya maisha yao wakati Fulani farao alikuwa ametoa amri kuuawa kwa watoto wote wa kiebrania wakati walipokuwa wakizalishwa lakini wazalishaji walikataa agizo la farao kwa sababu walimuhofu Mungu kwakweli Mungu aliwabariki wazalishaji wale na kuwasimamishia nyumba zao ( Kutoka 1;15-21),Leo hii wako madaktari wasio mcha Mungu ambao kwa tamaa ya fedha husaidia metendo hayo ya utoaji mimba hii ni dhambi ni vizuri kutokutoa mimba kwa sababu zozote zile hata kama umebakwa ukaachiwa ujauzito kaa nao na Mungu atakubariki ni swala la kimasomo zaa kwanza kisha nenda kaendelee na masomo najua ziko sababu nyingi ambazo zinaweza kutolewa ili kuhalalisha utoaji huo lakini kwa bahati mbaya hapa mimi siko katika mdahalo wa kuonyesha inafaa au haifai ila natumia mamlaka ya juu kabisa neno la Mungu kupiga marufuku swala zima la utoaji wa mimba nikichukua nafasi hii kulaani aina yoyote ile ya utoaji wa mimba na mjadala umefungwa.                                            

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni