Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Hatari ya Kushiriki Ngono !



Somo la sita.
Vijana na Hatari ya mapenzi (Ngono)
 Somo hili linatahadharisha tu hatari itokanayo na ngono au mapenzi, Hakuna jambo zuri kama mapenzi hapa duniani lakini pia hakuna jambo la hatari duniani kama mapenzi hivyo ni muhimu kuwa tahadharisha vijana kuhusiana na mapenzi.tutajifunza somo hili kwa kuzingatia maeneo matatu hivi yafuatayo;

  • Tahadhari ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa.
  • Madhara ya kujichua Punyeto.
  • Athari za kuangalia Picha za Ngono.
Tahadhari ya Kufanya mapenzi kabla ya ndoa.
   Kama tulivyoona katika masomo yaliyopita Biblia ikitahadharisha kutokuyachochea mapenzi kabla ya wakati wake (Wimbo uliobora 3;5). Biblia inakataza na kukemea vikali maswala ya ukahaba ikiwa na maana  ya mapenzi holela nje ya ndoa, huku inatia moyo kufanya mapenzi ndani ya ndoa (Mithali 7;6-23,5;15-23) kwa msingi huo ni vema vijana wakijitunza na kusubiri wakati, ujana ni kipindi cha mpito kutoka katika utoto kuelekea katika utu uzima  katika kipindi hiki vijana hupata mabadiliko ya kimwili na kiakili na kimtazamo,wakati huu mwili na akili hupevuka na ni kipindi kizuri cha kuweka msingi kwa maisha ya baadae,kujihusisha na mapenzi wakati huu ni kujiwekea msingi mbaya  wa maisha  na kuvuruga shughuli zako za kimaendeleo na mpango wa Mungu alioukusudia kwako kwa vipi unaweza kujiharibia mtiririko wako wa kimasomo,kazi zako,Mimba kabla ya wakati au maandalizi,majukumu kabla hujajitegemea,watoto wa mitaani,magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi na ugumba au kifo,hivyo ukijitambua kuwa wewe una umuhimu gani au una thamani gani katika maisha haya utajilinda kujihusisha na ngono kabla ya wakati husika.


       Hata hivyo kuna maono mbalimbali kuhusiana na kushiriki katika ngono kabla ya ndoa na kushiriki ngono ukiwa ndani ya ndoa kwa wanaounga mkono swala la kuoa au kuolewa ukiwa bikira wana hoja kuwa bikira anakuwa hajui kile kinachoendelea huko na huko duniani hivyo ni rahisi kutulia na kuridhika akiwa ndani ya ndoa maana hana ujuzi na wanaume au wanawake  wa nje ambao wanauwezo na ujuzi tofautitofauti katika utendaji mapenzi.

      Kundi jingine ni lile linalounga mkono kuwa ni vizuri vijana wakiingia katika ndoa huku wakiwa na ujuzi kamili wa tendo la ndoa kivitendo inadaiwa kuwa wenye ujuzi huu wanakuwa hawana usumbufu ukilinganisha na wale wasiojua kitu, dhana hizi zote mbili zinaweza kuwa na ukweli Fulani. Chukulia kuwa una mke uliyemuoa akiwa bikira au mume ambaye ni bikira na hawana ujuzi wowote kuhusu kinachoendelea kule nje kwa kweli kabisa jaribu lao kuu litakuwa ni udadisi wa kutaka kujua kinachoendelea upande wa pili hasa watakapokuwa wakisikia habari mbalimbali za kimapenzi kutoka katika vyanzo mbalimbali vya huko wasikojua hawa watasumbuka,Rafiki yangu mmoja aliniuliza swali hili akitetea hoja ya kundi hili la Pili “Kamote hebu fikiria kama umeoa mke bikira kasha akawa anatoka nje ya ndoa,au umeoa mke aliyekuwa hana bikira kisha akatulia ndani ya nyumba bila kutoka nje ungechagua yupi?”Dhana hii inatufundisha situ ubikira ni kitu kingine na uaminifu ni kitu kingine bali pia inatuonyesha kuwa mwanamke aliyeonja kasha akapata mahali anapoweza kutulizwa kiu yake barabara hawezi tena kuyatafuta huko nje lakini yule asiye na ujuzi akijaribiwa na udadisi wake akagundua kuwa kuna jamaa wanaweza mchezo kuliko jamaa yake kule ndani kuna uwezekano akaamua kuchonga mzinga, Tunaporudi katika msimamo wa kibiblia tunaona ikiunga mkono sex after marriage yaani ngono ndani ya ndoa na si vinginevyo.

Madhara ya kujichua Punyeto.
   Vijana wengi wa kike na wa kiume hupitia tabia ya kupiga punyeto,Punyeto imethibitishwa kuwa haina madhara ya kiafya,lakini ina madhara ya kisaikolojia na kidhamiri hasa unapokuwa unalihusisha swala hili na mambo ya kiroho au kiimani basi dhamiri yako inaweza kukushitaki na ukajihisi kuwa u mwenye dhambi na mwenye kushuka moyo,Tabia ya kufanya punyeto ina miaka mingi sana duniani lakini Biblia iko kimya kuhusiana na swala la kufanya punyeto,hata hivyo kama kiongozi wa kiroho nashauri kuwa tabia hii si nzuri bila kuwahukumu wale wanaolifanya zoezi hili,Mimi mwenewe nilifanya sana wakati wa umri Fulani wa ujana,(Efeso 4;17-19).Hii ni tabia tuliyojifunza darasani katika somo la kawaida kama baiolojia tukitiwa moyo kuwa ni njia salama ya kimapenzi na kupunguza msisimmko na tama za kimapenzi huenda nawe umewahi kusikia au kujifunza tabia hizi,Katika utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa karibu asilimia 97% ya wanaume wamefanya punyeto na asilimia 87% wanawake wamefanya punyeto,Muhubiri maarufu duniani amabye kwa sasa ni Marehemu Keneth Heghine alikuwa akitetea swala zima la ufanyaji Punyeto hata hivyo tendo hili linaweza kuwa si tatizo endapo anayefanya hatakuwa na picha ya mwanaume au mwanamke katika mawazo yake afanyapo punyeto jambo ambalo linawezekana kufaulu kwa asilimia 60% tu za vijana wenye nguvu ya kujidhibiti wasitamani lakini zaidi ya hayo wengi hufanya tendo hili wakiwa na picha kichwani ya mwanmke au mwanaume aliyempenda au kumtamani,na wengine hufanya hayao kama matokeo ya tama endapo jambo hili litafanyika kama matokeo ya tama basi ni wazi kuwa swala hili kibiblia ni dhambi Biblia inataka tuvitiishe viungo vyetu katika mwili ikiwemo mawazo mabaya kumbuka kuwa kutamani ni dhambi kamili kama kutenda (Kolosai 3;5,warumi 1;26-27,Mathayo 5;27-28),utafiti pia unaonyesha kuwa wengi wa waliofanya punyeto waliweza kufanya tendo kamili la ngono pia.

    Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa  punyeto huwa na madhara ya kisaikolojia,vifaa vingi vinavyotumiwa na wafanya punyeto hasa wanawake vinawatengenezea mazingira ya kutokutoshelezwa na wanaume zao wa kawaida,kwani vifaa hivi huwa katika hali ya kusimama kwa Muda mrefu tofauti na uume ambao huwa unasinyaa,kwa sasa dunia ilivyoendelea kuna vifaa vya kingono vya umeme au mkanda wenye uume bandia unaoweza kuvaliwa na mwanamke na akafanya ngono na mwanamke mwenzake,au vifaa vya plastiki wanavyoweza kuvitumia kujiridhisha kimapenzi wenyewe ukiachia njia za kizamani za kutumia mimea kama karoti tunda kama ndizi,vigongo vya kuchongesha n.k. Nchi ya Ufaransa ndiyo inayoongoza duniani kwa utengenezaji wa vifaa bandia vya kujiridhisha kimapenzi na vina soko kubwa sana na inasemekana hata wajane wengi sana huvitumia. Kwa kweli mwanamke kijana ambaye atakuwa amejizoeza kujiridhisha kwa vifaa hivi bandia anapoolewa kunakuwa na uwezekano akaathiriwa na vifaa hivyo na hivyo kuona kuwa haridhishwi na mwanaume wake. Kwa upande wa pili yaani kwa wanaume pia kunaweza kuwepo na tabia endelevu ya kujichua kwa kutumia utelezi utokanao na sabuni n.k kwakuwa wanatumia vidole vya mkono basi msuguano wa mkono unakuwa mkali kuliko ule wa uchi wa kawaida wa mwanamke kwa msingi huu basi anapooa uchi wa mkewe hautaweza kutosheleza hamu yake ya kingono na hivyo kuna uwezekano wa kuendelea kwa tabia hiyo hata baada ya kuoa kwa kuzingatia athari hizi za kimaumbile zinazoweza kujitokeza tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa tabia hii si nzuri na ni muhimu kujifunza kuiacha kwani inapingana na maumbile ya utendaji uliokusudiwa na Muumba, Ili vijana wajiepushe na tabia hii unaweza kujifunza kutokwenda kitandani mapema kwani kutakupelekea kufikiri zaidi katika tama ya kufanya punyeto hivyo unapokwenda kitandani ukiwa umechelewa utalala mapema bila kufikiri hayo,Unapokwewnda bafuni hakikisha unaoga kwa haraka kama mtu mwenye haraka hivi,shiriki michezo,Ibada na shughuli nyinginezo,maombi na kufunga n.k ili kujizoeza kutoka katika hali hizi au anza kupunguza kidogokidogo idadi ya upigaji punyeto kwa kila wiki au mwezi taratibu hadi sifuri Muombe mungu akuwezeshe kwani yasiyowezekana kwa wanadamu kwake Yanawezekana.

Athari za kuangalia picha za ngono
    “Mimi ni mtaalamu niliyefanikiwa sana na ni meneja katika kampuni kubwa isiyo ya kiserekali au iliyobinafsishwa,Nimekuwa muathirika wa kuangalia picha za ngono kwa zaidi ya miaka 40,sikuzaliwa nikiwa na tabia hii lakini nilijikitakatika mkumbo tu wa kuziangalia nikiwa na miaka tisa” ni moja ya shuhuda za mtazamaji wa picha za ngono akishuhudia.Hili ni tatizo kubwa sana duniani vijana wakubwa kwa wadogo mpaka wabunge na mawaziri na watu ambao tunaweza kuwapa heshima kubwa sana wakiwemo viongozi wa dini na hata maaskofu wsamenaswa na picha,mikanda ya video,cd,vcd,dvd,vijarida na story zilizoandikwa zenye kusisimua sana swala zima lihusulo ngono,Picha hizi za ngono zina nguvu,zina mvuto zinagusa hisia na akili na zinapenya katika ubongo wa mwanadamu kuliko hata tabia uliyozaliwa nayo,Nyingine hatuwezi kuziepuka kwani waandaaji wa matangazo ya bidhaa mbalimbali  hutumia wanawake wazuri wenye mvuto wa kingono wanapotangaza bidhaa zao,wanamuziki wengi huimba nao mivao yao n.k vinaweza kabisa kufanya usalama wetu kuwa mdogo.
     Biashara ya picha za kingono inapesa sana duniani kuliko biashara yoyote ile hivyo wengi huzitengeneza makusudi kwani wanataka pesa huko marekani picha za kingono hutengeneaza mapato ya Dollar billion nane kwa mwaka na hiyo ni takwimu ya mwaka 1985, Picha za kingono zimeathiri watu wengi sana na kuharibu mitazamo yao angalia ushuhuda huu,;-
  “Nilipofikia umri wa miaka 22 hivi nilianza kuhisi matatizo ya tabia yangu mbaya niliyokuwa nayo,kuna wakati nilishindwa kufikiri kitu kingine chochote bali mawazo yangu yalijaa picha za kujisisimua kingono kwa miaka mitatu tu nilikuwa na mikanda,magazeti na vitabu zaidi ya 200”
    “Kujiingiza katika utazamaji picha za ngono ni utumwa wenye kutisha sana ambao mwanadamu hapaswi kuishi nao kwa mtu wa kiwango chochote kile awe dereva au waziri nahisi kuna mamia ya watu kama mimi ambao wako kwenye kifungo nilichonacho tena ni wanawake kwa wanaume na idadi yao inaongezeka”
      “Sikuamini kama wanaume kwa wanawake wanaoangalia picha za ngono  kwa muda mrefu na kutegemea kuwa wanaweza kuwa na uhusiano na wapenzi wengine……Leo nikiwa na miaka ya arobaini na nane hivi nikiwa na watoto wane….Ninasumbuliwa kila siku na mawazo na picha na tamaa ya picha za kingono nilizoangalia miaka hiyo…mawazo haya yanaharibu kabisa uhusiano wangu na mke wangu,na kila mwanamke ninae mwona hata wale wa kanisani na hata binti zangu nawatamani nafikiri hili linachangia sana katika uharibifu wa ndoa nyingi na kupelekea kuweko kwa talaka katika siku za leo”
      “Niliangalia picha za ngono kwa zaidi ya miaka 30 zimeharibu ndoa yangu….Kwakweli zimeniibia penzi langu la kweli na kuharibu uhusiano na vimeathiri hata watoto wetu ingawa hakujua kuwa tumeathiriwa na picha za ngono na walishituka tulipotangaza kuwa tunapeana talaka tulipendana sana lakini sasa najua kuwa picha za ngono zimeharibu ndoa yangu alisema mama mmoja aliyeachika”
   Hizo ni baadhi ya shuhuda ya watu wanaotibiwa ili kupona katika tatizo la uangaliaji wa picha za ngono na athari zake kwa kweli zina madhara makubwa na sasa madhara haya yanalikabili bara la Afrika na inchi yetu ya Tanzania utafiti unaonyesha kuwa hata viongozi wakubwa wa kidini wamejihusisha kwa namna moja au nyingine katika uangaliaji wa picha za kingono na kwa sababu hii kumekuwa na maoni yanayotolewa katika kuzitetea au kuzipinga maoni ya wanaoziona kuwa zinafaa ni kama ifuatavyo;-
     Zinachochea nyege na kuongeza hamu ya kufanya tendo la Ndoa, Zinaongeza nguvu, Zinafurahisha na kukufanya ulipende tendo la ndoa,Zina sisimua sana,Zinaongeza ujuzi,zinasaidia katika maandalizi ya kukutana kimwili haya ni baaadhi tu ya maoni ya wenye kutetea picha za kingono Hebu sasa tuangalie maoni ya wale wenye kuziona kuwa zina Athari
     Kwa upande wa wale wenye kuona kuwa zina athari wao huwa na maoni yafuatayo;-
 Zinaharibu mahusiano ya kinyumba,zinaharibu dhamiri hasa ya Mtu aliyeokoka,zinakufanya uone ni halali kuendelea kuziangalia,zinachochea kutafuta kutoshelezwa zaidi nje ya ndoa,Hazionyeshi athari za upande wa pili wa ngono kama magonjwa ya zinaa ukimwi,mamba, ubakaji,zinachochea mazungumzo ya wazi zaidi kuhusu ngono,zinatoa majaribu ya kuzifanyia kazi au kuigiza,Hazitoi uhalisi wa mambo zinaingiza imani potofu kuhusu utendaji wa tendo hilo,zinajenga hali ya kutokuaminiana,zinaleta athari katika mawasiliano nyumbani,zinaharibu uhusiano wetu na Mungu.
  Ni muhimu kufahamu kuwa Kama picha hizi zinafaa kusingekuwa Na madhara makubwa Kama Yale tuliyoyaona katika shuhuda hizi Ni wazi kuwa hili Ni tatizo Na Ni lazima kanisa Na serikali ikubali isikubali linaiharibu jamii, Ni muhimu pia kuangalia Biblia inasemaje kuhusu kuangalia picha za ngono? Biblia inasema hivi “Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu.Kazi ya waliopotoka naichikia,haitaambatana nami”(Zaburi 101;3).Katika uadilifu wake Ayubu anasema alifanya agano na macho yake kumwangalia msichana (Ayubu 31;1) hii ilimaanisha kuwa Ayubu aliyapiga macho yake marufuku kutamani msichana ni wazi kuwa hili linatukumbusha jinsi ambavyo Daudi aliyekuwa masihi wa Bwana alijikuta akifanya mambo ya aibu ambayo chanzo chake kilitokana na kuangalia mwanamke aliyekuwa uchi anaoga na hili liliamsha hisia zilizopelekea kufanya mipango ya kumpata mwanamke yule ingawa hatujui mipango hiyo ilichukua muda gani lakini tunaweza kuwa na hakika moja tu kuwa kule kuona na kuangalia kulimjegea picha isiyofutika ya mwanamke yule Bathsheba na kwa hivyo moyo wa kutamani ulimzidi nguvu na kuacha kuzitii amri za Mungu, Yesu alionya kule kumwangalia mwanamke kwa kumtamani kuwa ni sawa na zinaa kamili unaonaje leo Yesu angesemaje kuhusu Kanda za kingono na picha zilizoenea kila mahali za kingono? Moja ya viungo ambavyo ni vyenye kiwango cha juu kabisa katika kuhisi kibinadamu macho hupewa nafasi ya Kwanza, kisha viungo vingine kama sikio,pua, kuonja na kuhisi kwa ngozi hufuata,Hivyo unaweza kuona umuhimu wa kweka agano na macho Yetu kuwa ni kwa muhimu kiasi gani kwani kwa mtindo huu watu wanaweza kuwa wazinzi mioyoni mwao (Mathayo 5;27-28) Kama umenaswa katika mtego huu kuna njia kuu tatu tu za kukusaidia kutoka katika jaribu hili nazo ni moja maombi,Kutokuruhusu kuangalia tena na  kujilinda kimwili kabisa kuepuka na kutokujihusisha na jaribu hili la kuangalia picha za ngono lazima ujue kuuweza mwili wako (1Thesa 4;3-5).Endelea na zoezi la kukataa kuangalia picha hizi na utaweza kuona wema na fadhili za mungu zikikufuata siku zote za maisha yako ili kukuleta nyumbani mwa Bwana(zaburi 23;6) hata kama umezama katika kuangalia picha hizi kiasi gani hii haimaanishi kuwa Mungu hawezi kukutoa huko mungu yu aweza kukutoa na sisi woote alitutoa katika hali ngumu kama hizi hata kama hatukuzama katika kuangalia picha za ngono lakini kuna eneo ambalo kila aliyeokolewa alikuwa amezama na bwana akaweza kukutoa huko Endelea kustahimili jaribi hilo na utaipokea taji ya uzima (Yakobo 1;12) Toa kipaumbele kulisikia neno la mungu (Mithali 4;20-23) na Ulinde sana Moyo wako kuliko chochote ukilindacho.

Maoni 1 :