Somo la kumi na moja
Vijana na maswala ya uchaguzi wa Mchumba
Uchumba
ni kipindi cha mpito kwa vijana kuelekea Ndoa ,katika somo hili tunazungumzia
kipindi hicho ambacho mara nyingi huanza kama Urafgiki,ingawa tulikwisha gusia
swala la kuwa na marafiki katika somo la mahusiano lakini hata hivyo kama kuna
mahali pana hitaji hekima ya kimungu ni wakati wa kuchagua na wakati wa
uchumba,swala hili si jepesi kama ilivyo kwa hakimu anayepaswa kutoa hukumu ya
kunyonga mtu,,hakimu aliye na kesi inayohitaji mtu kunyongwa ni lazima atakuwa
makini sana kupitia madai yoote na ushahidi ili kupata uhakiki na uthibitisho
ili aije akasababisha hatia katika dhamiri yake atakapo hukumu mtu
kunyongwa,hivi ndivyo ilivyo kwa mtu anayedhamiria luwa na mchumba wa kutaka
kuoana naye, Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia maeneo manne yafuatayo;-
·
Umuhimu
wa kuoa mtu wa imani sawa na yako.
·
Dhambi
ya kumchagulia mtu Mchumba.
·
Umuhimu
wa kuwa makini wakati wa kufanya uamuzi
·
Mambo
ya msingi ya kuzingatia unapochagua mchumba.
Umuhimu wa kuoa mtu wa imani
sawa na yako.
Huu ni moja ya msingi muhimu sana mtu
anapotaka kuoa/kuolewa,jambo la kwanza ambalo ni muhimu likapewa kipaumbele ni
hali ya kiroho,Ndoa ni muungano wa watu wawili katika hali zao za
kiroho,mwanamke na mwanaume wanapooana sio miiliyao tu inayokuwa mwili mmoja ni
roho zao,Waebrania walipozungumzia mwili mmoja kwenye akili zao ilikuwa na
maana ya Mwili,nafsi na roho.Hawakumgawanya mwanadamu (Mwanzo 2;21-24,Mathayo 19;6) kwa hiyo alichokiunganisha Mungu
mwanadamu asikitenganishe, Miili yetu ni hekalu la Roho mtakatifu (1Koritho 6;12-20) hii ina maana ya
kwamba mkristo ni roho moja na Mungu,Hivyo unapoungwa na kahaba kwa hiyo
mkristo kuungwa na kahaba ni kuvitwaa viungo vya Kristo na kuvifanya vya kahaba
(Mst 15-16 1Koritho 6).
Kwanini ni Muhimu kuoa mtu wa imani sawana
yako Mungu katika hekima yake aliagiza jambo hilo na alitoa tahadhari kuwa watu
hao wangekua mwiba na kuwa wangeigeiza mioyo ya waisrael isimuelekee Mungu Kumbe basi kuoa/kuolewa na mtu wa imani
nyingine kunaweza kukuletea madhara ya kiroho na kimwili na kinafsi unaona!
soma (Yoshua 23;6-15),unapojifanya
una hekima kuliko Mungu na kulidharau neno lake madhara yanaweza kukupata hii
ilimtokea mfalme Sulemani Soma (1Wafalime
11;1-8), Biblia inasema hivi katika (2Wakoritho
6;14-18) nitanukuu kutoka katika toleo union version la kawaida ambalo
kiswahili chake Hupendwa sana “ Msifungiwe nira pamoja na wasioamini ,kwa
jinsi isivyo sawasawa kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya
nuru na giza tena pana ulinagifu gani kati ya
Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye anasehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu
hekalu la Mungu aliye hai kama Mungu alivyosema ya kwamba Nitakaa ndani yao ,na
kati yao nitatembea mimi nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu kwa hiyo
Tokeni kati yao mkatengwe nao ,asema Bwana Msiguse kitu kilicho kichafu
Nami nitawakaribisha Nitakuwa Baba kwenu nanyi mtakuwa kwangu
wanangu wa kiume na wa kike asema Bwana
mwenyezi”
Unaweza kuona maandiko hayo yanenavyo,
Tunapozungumzia Ng’ombe waliofundishwa kulima sote tunajua taabu iliyopo
unapovalisha jembe kwenye mabega ya ngombe hao ili walime mmoja amefundishwa na
wa pili hajafundishwa nini kinatokea huyu aliyefundishwa anajua kuwa sasa ni
saa ya kuyalima majani asiyefundishwa anajua majani ni chakula hivyo mwenendo
huwa mgumu ndivyo itakavyokuwa ndoa ya watu walio tofauti kiimani hivyo Imani
na kiroho ni msingi wa kwanza katika uchaguzi wa mke au mume.
Dhambi
ya kumchagulia mtu Mchumba.
Tabia ya kuwaunganishia watu ni tabia ya
wachungaji wengi sana huu umekuwa ni mtindo mbaya sana ambao unakomaa siku hadi
siku, Sikatai kuwa Mungu ana njia nyingi katika kuwapa watu wenzi wao ikiwa ni
pamoja na kuwatumia wanadamu lakini ninachotaka kutahadharisha hapa kuwa
kiwango hiki kimezidi! Na kwa mtazamo wangu chimbuko la ndoa ni la Mungu
mwenyewe Kumbuka yeye ndiye aliyeona si vema mtu awe peke yake kisha Biblia inasema hivi “Na ule ubavu alioatwaa katika Adamu
Bwana Mungu akaufanya mwanamke akamleta kwa Adamu” Biblia ya kiingereza
inasema hivi “…God brought her to man.”
Kwa msingi huu Mungu ndiye anayejua nani anamfaa nani? Kumtafutia mtu mke kwa
kuchombezachombeza ni tabia mbaya naya kiburi ya kuchukua nafasi ya Mungu, Ni
vizuri mtu akaamua yeye mwenyewe ili asije akakujutia wewe atakapokutana na
magumu,kibiblia Mungu ndiye anayejua nani anakufaa wewe kijana na sio
mwanadamu,Hata hivyo Mungu hutumia mazingira katika hali Fulani Mungu huweza
kuwatumia hata wazazi,hata ambao hawajaokoka hana mipaka wala upendeleo,lakini
natahadharisha wachungaji kwani ndoa nyingi ambazo zimeungwaungwa na wachungaji
zina matatizo na nyingine zimevunjika na ushahidi wa utafiti wa kutosha ninao
ndio maana nataka kutahadharisha watumishi katika eneo hili ni vema kushauri, ni
vema kupata maongozi ya kiroho lakini linapowadia eneo la uamuzi waache watu
wafanye wenyewe usiwaamulie wala uisiamuliwe.wengi leo wanalia kuwa
isingelikuwa Fulani! Kwa nini wewe mtumishi watu wakulilie kwa kukulaumu
jihadhari na tabia mbaya ya kuchombezea vijana kuwa huyu anakufaa huku unajua
wazi kuwa hafai hii imeliza vijana wengi wache wafanye maamuzi yao wenyewe
wakikutana na magumu watajifunza kuvumilia na sio kukujutia wewe
Umuhimu
wa kuwa makini wakati wa kufanya uamuzi.
Hakuna jambo la kuzingatia
katika maisha kama kufanya uamuzi au uchaguzi katika maishayetu rejea staid za
maisha kipengele cha kufaya maamuzi,Uamuzi tunaoamua leo ndio utakaotufanya
trufurahie au tujute katika swala zima la uamuzi wetu uamuzi ambao huambatana
na kutafuta mapenzi ya Mungu hauna majuto hata kama una magumu ambayo ni
kawaida ya wanadamu (Ruthu 1;8-18),uamuzi
unaozingatia tamaa ya kibinadamu huongoza katika majuto na matokeo yasiyo
mazuri (Mwanzo 13;8-13,29;16-18,31;19,30-32,35;16-19).
Kila mtu aliyeokolewa anapaswa kuzingatia sana maamuzi anayoyafanya ili
yaendane na mapenzi ya Mungu,Mume au mke mwema hutoka kwa mungu na ili
kufanikiwa kumpata fuata kanuni zilizo sahihi fuata mapenzi ya mungu (Mithali 19;14). Kufanya mapenzi na
maamuzi yasiyo ya kimungu kunaweza kukuletea hasara kama yule binti aliyechagua
kichwa cha Yohana mbatizaji(Mithali
14;1-12) kuuliza kutoka kwa bwana ni jambo la muhimu haijalishi uko kiroho
kiasi gani Yoshua alifanya kosa la kuwaapia wagibeoni amani bila kuuliza kutoka
kwa bwana na mungu alikuwa anaona lakini aliacha waingie mkenge amani ya kristo
iamue mioyoni mwenu (Yoshua9;3-20 ) zingatia
mstari wa 14 “…wasitake shauri kinywani mwa Bwana”Kuna wakati tunaweza
kujifanyia mambo wenyewe tu bila kuuliza ushauri kutoka kwa Bwana,Mungu
hataingilia kati ujinga wetu Tumuombe Mungu basi atupe kuwa makini wakati woote
tunapokuwa au tunapokaribia kufanya maamuzi ili kwamba atusaidie katika jina la
Yesu.
wanandoa ambao wanaonekana kufanikiwa sana katika Ndoa Uchaguzi makini Maisha makini na Mafanikio!
Mambo
ya msingi ya kuzingatia unapochagua mchumba.
Yako
mambo ya msingi makuu muhimu mawili ya kuzingatia wakati tunapohitaji kuchagua
mchumba
1. Zingatia kwanza maisha yako
Binafsi.
2. Zingatia ufahamu wakokatika
mambo muhimu matatu
·
Mungu
na mapenzi yake
·
Ufahamu
kuhusu ndoa
·
Ukomavu
katika Pendo la Mungu.
Zingatia kwanza maisha yako
Binafsi (Mathayo 7;12).
Biblia inasema basi yoyote
mtakayo mtendewe na watu watendeeni ninyi vivyohivyo kwanza,Ni muhimu
kuzingatia kanuni hii Mara nyingi tunapenda vitu vizuri au watu wazuri huku
sisi wenyewe hatufanyi bidii ya kuwa wazuri! Kama uanatafuta mtu aliye sawa
anza wewe kuwa sawasawa,kupata mume au mke mzuri hakutegemei neno “NATAKA AWE
HIVI” bali kunategemeana na “ WEWE KUWA SAWA” Huwezi kudai unataka mtu mcha
Mungu haku wewe mwenyewe humchi Mungu,au unataka mwanamke bikira huku wewe
hujitunzi nani unataka akuchague wewe? Hivyo kabla ya kutaka kilicho chema
mungu anakutarajia wewe kufanya mema Kaini aliona wivu nduguye Habili
alipobarikiwa kwa kutoa sadaka njema na alikasirika alipoona kuwa Mungu
hakumtakabali yeye Mungu alimshauri kuwa haitaji kukasirika na kuwa kibali
chake kipo endapo tu nayeye angekubali kutenda vema “Kama ukitenda vyema
hutapata kibali? Usipotenda vyema… (Mwanzo4;3-7)”
Mungu yuko tayari kumbariki kila mtu wala hajaishiwa na baraka lakini wewe
unafanya nini?Mungu alimletea Adamu wa kufanana naye je unafanana na yule
unayemtaka? (Mwanzo 2;18).Hivyo ni
muhimu kwa kila kijana kuamua kuwa karibu na Mungu hali hii itaichonga tabia yako kuwa njema na
kutakufanya uwe makini pale Mungu anapotoa muongozo;-
Mungu
Mwanaume ukaribu Mwanamke
Ukaribu
Ukaribu
Kadiri kila mmoja mwanamke au mwanaume anavyojitahidi
kuwa na uhusiano mzuri na Mungu ndivyo wanavyoweza kuwa karibu, Kiroho, kinafsi
na kimwili na kwa ubara
Ufahamu
wako kuhusu Mungu na mapenzi yake
Mtu
anapotaka Mungu ampatie mume au mke maana yake anatafuta mapenzi ya Mungu,Wakristo
ni lazima watafute mapenzi ya Mungu katika maeneo yote ya maisha Likiwamo hili
la kutafuta mwenza,lazima tuyatende mapenzi ya mungu yote (Matendo 20;27)Mtu anayetafuta mapenzi ya mungu ni lazima atambue
kuwa,Wakati mwingine mtazamo wako hautakuwa sawa na mtazamo wa mungu,Lakini
katika yoote mtazamo wa Mungu ndio halali na unatufaa.Kuyafanya mapenzi ya
Mungu ni lazima kuambatane na kufanya
mambo kadhaa katika maisha yetu yatakayosaidia kuyajua mapenzi ya mungu wakati
Mungu anapotaka kujifunua kwetu
I.
Maombi ni moja ya msaada mkubwa sana katika kuyajua
mapenzi ya mungu (zaburi 40;8;Mithali
3;5-7b),Daudi alikuwa mtu mwenye
kutafuta mapenzi ya mungu,Kristo Bwana
wetu alipenda kile ambacho baba yake anataka kitendeke hivyo aliomba (Marko 1;35)
II.
Kusoma neno la Mungu (Zaburi 119;9-11,105).Kupitia Neno la Mungu tunaweza kujua nini
mapenzi ya Mungu,mungu amatupa maelekezo ya nani wa kuoa na nani wa kutokuoa (Yoshua 23;12-13,2Koritho 6;14-18).Uchumba
au ndoa na mtu asiyeamini umewekwa wazi
katika maandiko Hivyo hayo nayo ni mapenzi ya Mungu,Hata hivyo kama mtu
atakazania tu aolewe na mume au mke asiyeamini Mungu hataweza kumzuia lakini
yatakuwa si mapenzi kamili ya mungu bali mapenzi ruksa (1Samuel 8;1-9 Rumi 1;28-32) Wakati mwingine tunaweza kuwashauri
watu na wakakataa neno la Mungu, tuwaache lakini mungu atawalipa sawa na Neno
lake,watoto wanaweza kukataa hata ushauri wa wazazi bado tuheshimu maamuzi yao
lakini tuwaonyeshe ni madhara gani yataambatana na maamuzi yao lakini Mungu
katika mapenzi yake wakati mwingine anaweza kuwa na sababu fulani Mungu
alimruhusu samsoni kumpenda mfilisti sio ili apate mke bali kutafuta kisasi (Waamuzi 14;1-4)
III.
Kuongozwa na Roho (Wagalatia
5;16-17,Warumi 8;14) Mtu anayeongoza na Roho wa Mungu anaweza kuyafanya
mapenzi ya Mungu kwa usahihi sana Ni rahisi kuyajua mambo ya rohoni, kujua
wakati na kadiri mtu anavyojifunza kutembea na Roho wa Mungu ndivyo
unavyojiweka katika nafasi ya kusema
naye na kukuongoza kupitia, Maandiko, mazingira, ushauri, Amani ya moyo, ndoto
na maono, sauti ya ndani na msukumo, tamaa msisimko na hisia vina sehemu ndogo
sana katika kutusaidia kupata mtu sahii Upendo ni zaidi ya hisia.
Ufahamu kuhusu ndoa.(Mwanzo 18-25).
Ndoa ni wazo la
Mungu “si vema....” ilianzishwa na mungu hivyo tunaoa ili kutimiza mpango wa
mungu ndoa haipaswi kuwa sehemu ya kutimiza tamaa,Mtu anayeoa au kuolewa ili
kutimiza tamaa tu ataendelea kuwa na tamaa hiyo hata baada ya kuwa na ndoa.
Ndoa ni muungano
wa watu wawili (Agano) ambao wanaunganishwa na Mungu hivyo ni Mungu ndiye
anayewaunganisha na ndiye anayejua yupi anakufaa v.18
Muda wa mtu kuoa au kuolewa unaamuliwa na mungu yeye
ndiye anajua muda muafaka “kisha akamleta kwa adamu” v.19-20. Mtu haoi au
kuolewa kwa sababu anajisikia tu elewa kuwa wakati msukumo huo unaanza unaweza
ukawa wakati sahihi au ukawa si wakati sahii
Kukubalika ni mojawapo ya funguo ya mungu kwa
maswala ya ndoa v.23
“Huyu ni nyama katika nyama yangu...”
Mungu amekwisha panga tayari jinsi hao wawili
watakavyoishi, Kuacha, kuambatana na kuwa mwili mmoja v.24 lazima uwe tayari
kuacha wazazi, jamaa na marafiki, uwe tayari kuambatana, kupenda na kutii, na
uwe tayari kushiriki Tendo la ndoa.
Ukomavu
katika Pendo la Mungu
Kila mtu anaweaza kuwa na maelezo yake
kuhusu kukomaa na kila mtazamo ukawaunathamani ya aina yake kwa sababu kukomaa
kunaweza kugusa mtazamo wa kisaikolojia, kijamii, kisayansi kitheolojia, kihistoria
n.k lakini tunaweza kusema kukomaa ni nguvu endelevu ya ufahamu wa maana kuhusu
maisha unaoendana na kiasi kati ya
maswala yoote ya kimwili,kisaikolojia,kijamii,kiroho na mitazamo mingine katika
maisha ambayo inamwezesha mtu kujitosheleza katika maisha akiwa na amani na
mungu ,wanadamu na yeye mwenyewe na kusababisha maana katika ufalme wa mungu na
maisha haya hivyo tunaona kuwa ukomavu
ni nguvu endelevu,ni kutoa maana katika maisha,kuwa na kiasi.kuridhika,amani
katika mahusiano na maana katika ufalme wa Mungu (Mathayo5;43-44) Upendo kama ule upendo wa mungu unaweza
kudhihirisha ukomavu wetu pale tunapowapenda hata adui zetu Mtu anayeingia
katika ndoa akiwa na ukomavu huu hataona shida ya aina yoyote ile katika ndoa
Ni lazima tuwe na upendo wa kweli huu ni tofauti na upendo wa hisia au upendo wa tamaa ambao nauita upendo wenye
shauku ya kipumbavu huu ni upendo uliojaa ubinafsi upendo huu huwa na shuhuda kama hizi
Nikimuona ule weupe wake tu ninachanganyikiwa,ana hadhi ya kipekee anastahili
kunioa,najihisi wa maana ninapokua naye,anaimba vizuri,anahubiri,ni maarufu
sana anauwezo,ni mtoaji,ananipa zawadi, nk.utu wa mtu hauko katika vitu wala
sura au umaarufu (Mithali 31;30) Mwanaume
na mwanamke asiyemcha mungu hta kama ana uzuri kiasi gani anaitwa hana akili na uzuri wake
unafananishwa na lulu katika pua ya
nguruwe (mithali 11;22) “ Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe kadhalika
mwanamke mzuri asiye na akili”au asiye mcha Mungu Hivyo ni muhimu kuwa na
mwenzi atakayekupenda vile ulivyo Kumbuka ule mkanda maarufu wa Filamu Coming to America ,mtoto wa kifalme
alivyojifanya masikini ili apate mtu atakayempenda vile alivyo na si kwa sababu
yeye ni mtoto wa mfalme.
Uchumba
wenyewe
Baada ya kuwa tumeangalia mambo mengi ya
msingi hebu sasa tuuangalie uchumba wenyewe sasa,Uchumba unaweza kufananishwa
na Mimba na kuzaliwa kwa mtoto kunafananishwa na mwanzo wa maisha ya ndoa,Mimba
hupatikana kwa yai la mwanamke kurutubishwa na mbegu ya mwanaume ndipo kiini
huanza kukua na baadae watu huanza kuona tumbo likiongezeka na baada ya muda mtoto huzaliwa hatua hizi
zinafanana na hatua za uchumba kuelekea ndoa kwa msingi huo basi
1. Mwanzilishi
wa uchumba kwa mila na desturi zetu wa Afrika ni mwanaume na hivyo mwanaume
hapaswi kulazimisha kukubaliwa,bali ni lazima aanzishe kwa upendo na wema na mwanamke anapaswa kujibu kwa upendo
na wema hta kama hataki sio lo! Kwani umenionaje mwanaume hata kikombe hujai mi
si saizi yako uchumba huanzishwa na mwanaume Mbugu huziendea yai, hata hivyo
hii haina maana kuwa mwanamke hawezi kumjua mumewe Mungu aweza kusema na mwanamke
pia kama atakuwa makini kwa Roho mtakatifu.
2. Uanzilishi unapokubaliwa ni kama mamba
imetunga, hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa siku mamba inaposhika hakuna mtu
ajuae na huwezi kupiga kelele luwa nina mtoto (hii ni muhimu kwani kabla
uchumba haujajulikana wakati mwingine hata kabla ya mchungaji kujua nendeni
mkaangalie afya zenu kabla watu hawajajua ili endapo mtajibaini kuwa mmoja
ameathirika watu wasijue ibaki kuwa siri yako)
Lakini kama mambo ni mazuri wote tunajua
kuwa mamba inapotunga yai hujifunga na haliruhusu mbegu za watu wengine kupita
hivyo unapokuwa umechumbia huna haja ya kuanza kukubalia wengine ili ufanye
ulinganishi hili sio sahii
3. Uchumba unakua kama mimba inavyokua ndipo
baadae watu hugundua kuwa kuna mimba ni vizuri kukawepo kipindi cha siri cha
kufahamiana baadae ndipo muweke mambo hadharani wako watu wengine akichumbiwa
leo tu kesho asubuhi kila mtaa umeshajua
4. Mtoto
anazaliwa hii ni kilele cha kufikia Harusi na kukabidhiwa mwali na kuapiana kwa
habari ya agano la ndoa,Jambo la msingi wakati woote wa uchumba ili ueweze
kudumu ni kuendelea kufanya mawasiliano,
Jinsi
ya kuutunza uchumba
Endelea kutunza uhusiano wako
na mungu na mahusiano yenu,jitunze katika usafi (Mwanzo 39;10-12 ,2Timotheo 2;22,!thesa 4;3-5),jilindeni mioyo yenu
na tama ya kufanya dhambi (Mithali 4;23)usiangalie
picha za ngono na mchumba wako,tunzeni ushuhuda ili watu wasipate nafasi ya
kulaumu(Yohana 4;21)Yesu alikaa
maeneo ambayo si ya maficho,jihadharini kukaa maeneo yenye maficho yasije
yakachochea mawazo yasiyofaa na msipendelee kukutana usiku ,Lindeni uchumba
usivunjike,endeleeni kuomba zaidi,anzeni kujifunza na kuuliza masali kuhusu
ndoa na kusoma vitabu mbalimbali na maandiko.
na kama nimechagua mchumba kimakosa na sijafanya hayo japo tumejitunza kwa usafi na sina amani moyoni na yeye anadai anaamani nifanyejeJe maana sitaki kuzikosa baraka za BWANA juu yangu
JibuFutaDaniel Aron hakuna bahati mbaya katika mpango wa Mungu endelea kumuomba na amani ya mungu ikutawale kama kiko kitu kinachofikiriwa kuwa ni makosa Mungu anaweza kurekebisha pamoja nawe kabla hamjaingia katika ndoa kumbuka kuvunja uchumba nako sio jambo jema linaweza kuleta uadui, Mungu atakupa hekima namna ya kumaliza au kurekebisha maswala yako kwa amani na haya ndio maombi yangu kwako
JibuFutaUbarikiwe mtumishi maana ninawakati Mgumu mpaka nimefikiria mengi sana, naomba Mungu anipejinsi ya kufanya maana wakati mwingine najikuta namjibu vibaya pasipo sababu maana sisikii Amani moyoni japo wakati mwingine tunaongea vyema na kuelewana, but najua wakati mwingine ni mapambano ya kawaida, Endelea kutuombea tufikie ukamilifu wa MUNGU kuliko kutangatanga na Dunia leo huyu kesho huyu mwishowe tufikie pabaya na kumwacha MUNGU, Nashukuru kwa kuupata ujumbe huu na naua ni kwa wakat sahihi umenifikia
JibuFutaMUNGU akutie Nguvu, umeokoa taifa kubwa
JibuFutaMaoni haya yameondolewa na mwandishi.
JibuFutaBwana Yesu Kristo apewe sifa?
JibuFutaNaomba ushauri wako ndugu,
"ikitokea ukawa na mchumba mlie ahidiana kuoana na mkatambulishana hata kwa wazee, lakini wakati huo wa uchumba mtu mke akatokea aka zini nje bila ww kujua tena zaidi ya mtu mmoja ie wa3, lakini ulimpata hajawahi jua mme, ikafika wakati ukamwoa ndo unakuta alikusaliti wakati wa uchumba, unamuuliza anakiri kufanya, inauma kweli, je mtu huyu afanye nn ili asidhoofu kwenye maisha yake? Ana hali mbaya ju ya hili mtumishi nisaidie ahsante
Habar, Mimi kazi yangu naendesha magar zaidi nimejiari na boda kubwa zaidi lililo nileta hapa nimemuomba Mungu sana na mala kadhaa naona Binti atakae nifaa nikiwashilikisha wananiuliza kuhusu kazi yangu badae wanakuja wakisema moyo wao haujalidhia niangalie sehemu nyingine. Ndugu mwandishi naomba ushauli wako
JibuFuta