Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Ufahamu wa Uwezekano wa Kutokuolewa !



Somo la kumi na mbili
Vijana na ufahamu wa uwezekano wa kutokuolewa
  Kuna ongezeko kubwa la wanawake wasioolewa hasa hapa kwetu Afrika na makanisani,Tatizo hili la kukaa bila kuolewa linaweza kuwa kubwa na linaweza kuleta athari kwa kina dada kujihisi kuwa hawawezi wao wenyewe na kujifikiri kuwa labda hawavutii wanaweza kujichukia na kujiona kuwa wamekosa jambo la msingi na la muhimu katika maisha wengi tunajua wazi kuwa future ya mwanamke Barani Afrika ni kuolewa kwamaana ya kuwa maisha kwa mwanamke ni kuolewa Hivyo anap[olikosa jambo hilin humfanya ajione kuwa amepungukiwa sana ,Hili linaweza kumfanya ajione amekataliwa na jamii na kuwa labda yeye ana tofauti wengine hujiingiza katika ukahaba hivyo ni muhimu nkufikiri kwa upana kuhusu mabinti wasioolewa na kuwahudumia lazima tulione hili kuwa ni tatizo la kulishughulikia na tutalijadili hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo

  • Wajibu wa kanisa kwa maandalizi ya mabinti.
  • Biblia inasema nini kuhusu kutokuolewa
  • Faida za kutokuolewa
Wajibu wa kanisa kwa maandalizi ya mabinti.
  Kanisa lina wajibu mkubwa katika kuliandaa kanisa na mabinti pia ili wajitambue kuwa wako katika nafasi gani ya maisha na jamii si vema kuwapandikizia watu hasa mabinti mawazo ya kuwa wataolewa tu na kufikiri kuwa kuolewa ndio kilele cha ubara wa maisha lazima Tufikiri kwa upana kama kuolewa ni kilele cha ubora katika maisha Kwa nini Kristo hakuoa au baadhi ya Mitume ni wazi kuwa kam Yesu hakuoa basi maisha yana maana pana zaidi ya kuoa au kuolewa Ni lazima basi kweli hii izaamishwe ndani katika maisha ya vijana wa kike waanze kufikiri kwa upana zaidi kuolewa ni kuzuri lakini kama hakujatokea je Tufanyeje?Kanisa linawajibu wa kufundisha kwa ukamilifu Imani na pande zake kuu mbili ili zieleweke vema kwa waamini wetu ni mara nyingi tumefundisha juu ya Imani ya kutoka katika shida na matatizo lakini hatujawahi kufundisha kuwa hata kufia katika tatizo ni imani mwandishi wa kitabu cha waebrania alifundisha hilo (Webrania 11;32-37) ni lazima kanisa lielewe kuwa mungu wetu ni mwokozi na ni mwenyekutia nguvu (He is a Serviour and Sustainer) huwa anaokoa katika majaribu ,lakini huwa anatia nguvu katika majaribu. Kanisa linawajibika pia kuwaajiri wanawake wasioolewa ili wasikae bila shughuli, waamini watoe kazi kwa mabint waioolewa badala ya kuwatelekeza na kuwaona wamepungukiwa eti kwa sababu hawana waume.

Biblia inasema nini kuhusu kutokuolewa
 Watu wengi wanafikiri kutokuolewa au kutokuoa ni balaa, lakini ni muhimu kuangalia nbiblia inasema nini? Yesu mwenyewe hakuoa! Lakini alifundisha kuwa kutokuoa au kuoa ni karama, karama ya kutokuoa au kuolewa ni wito wa hali ya juu sana na umewekewa watu maalumu sana Yesu akasema hivi “Awezae kulipokea neno hili na alipokee…” hii inamaanisha kuwa Mungu ameita au amendaa baadhi ya watu ambao hawataolewa au kuoa kwa huduma maalumu, Paulo mtume alikuwa na neema hii maalumu (1Korith 7;7). Wengi wa wamisionary wa zamani sana hawakuoa wala kuolewa akiwemo Mary Slessor mwanamke wa scotiland aliyeanzisha kanisa Nigeria na wengieo.Mungu bado anahitaji waume kwa wake waliuo single kwa matumizi yake katika ufalme wa Mungu bwana atupe fahamu hii Amen

 si kila mtu ataoa aku kuolewa!
Faida za kutokuolewa
Kihalisi na kwa uzoefu wa miaka katika huduma kuna faida ya kuwa single, wasioolewa wanapaswa kuitumia nafasi hii ya kuwa wenyewe kwa kumtumikia Mungu kwa uhuru zaidi,hizi ni miongoni mwa faida zenyewe;-
1.        Kuwa huru Muda woote,hii ni jambo gumu sana kwa wanandoa huwezi kuwa huru muda woote Mtu aliyeoa au kuolewa atagundua kuna mabadiliko mengi na changamoto nyingi zitakazofanya  Muda usiwe mali yako pekee bali unawajibika kujifunga kwa wengine
2.        Kuwa huru kujiendeleza kielimu,Kusoma huku unafamilia ni swala gumu sana lakini kama uko single ni jambo jepesi sana kujiendeleza kwa elimu ya juu vyovyote utakavyo
3.        Kuwa huru kusafiri kokote utakako,Mtu huru anaweza kuunganisha mikutano ya injili au semina kwa siku nyingi bila kubugudhiwa hii ni ngumu kwa mwenye familia
4.        Kuwa huru kutoka katika udhia na mateso ya ndoa,Ndoa zina mateso yanayogusa hisia na maumivu ya ndani sana si wakati woote katika ndoa kuna furaha na maraha tu waulize wana ndoa  unapojifunga na kuwa na mume na watoto kuna udhia tofauti nah ii inatengeneza nafasi ya kujiudhi zaidi Prophet T.B Joshua alisema “When you add any thing to your family you should also add Prayer” unapoongeza chochote katika familia yako ongeza pia maombi kwa nini kwa sababu umeongeza milango ya mashambulizi ya shetani kukushambulia, hii ni Lugha ya kivita Biblia inasema mmoja atafukuza elfu,wawili watafukuza kumielfu, kwa nini isiwe elfu mbili? Hii inamaana muwapo wawili nguvu inakuwa kubwa kwasababu vita inakuwa kubwa unaweza kuona!
5.        Uhuru wa kufanya huduma ambayo si rahisi kufanya ukiwa na ndoa mwenye hekima na alisikie neno hili ambalo Roho analiambia kanisa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni