Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Uhusiano



Somo la pili.
Vijana na Uhusiano.
 Katika somo lile la kwanza sehemu ya pili somo lile la vijana na stadi za maisha niligusia  kuhusu uhusiano.Uhusiano ni mojawapo ya swala la muhimu katika maisha ya mwanadamu,Hatukuumbwa tuwe peke yetu,hivyo basi kukosekana kwa mahusiano kwa kweli kunaweza kusababisha fikira potofu,upweke na kukosa kuelewa ukweli kuhusu maisha,si unajua kuwa tunahitajiana ndio na si sisi tu ukweli ni kuwa tunahitaji mpaka viumbe vingine visivyo vya aina yetu kama mimea wanyama,nk.lakini wanadamu tunahitajiana sana na hilo ndilo ninalotaka kulizungumzia hapa.tunahitaji marafiki,ndugu,jamaa na ushirika,tunahitaji marafiki hata wa jinsia tofauti na sisi.


  Hitaji la kuwa na marafiki.
       Kama mtu angeniuliza swali leo kuwa ni wakati gani katika maisha uliweza kuishi kwa furaha ningemjibu vema kwamba ni wakati wa utotoni au wakati nilipokuwa ninasoma shule ya msingi na sekondari na vyuo,baada ya hapo siwezi kueleza tena kama ninayafurahia maisha,na sababu kubwa ni kuwa sasa nina marafiki wachache sana na ambao huwapata kwa muda mfupi tu na wakati mwingi ninaishi maisha ya upweke nitakuelezea vizuri athari za upweke tutakapofikia hatua hiyo lakini  ninachotaka kukazia hapa ni umuhimu wa kuwa na marafiki katika maisha yetu kama wanadamu,Maisha ya kuwa mchungaji kama nilivyo leo yalinipunguzia sana kuwa na marafiki sisemi kuwa kazi hii ni mbaya hapana lakini ni gharama tunazolipa za kuwa watumishi wa Mungu hii ni pamoja na kuwa na vipindi tengefu ambapo tunakuwa kama tumetengwa au tumejitenga. Ninahisi kuwa katika mazingira Fulani vijana nao hupitia hali kama hizi kwa hiyo naona ni muhimu kuwa na marafiki.

     Je kila mtu anafaa kuwa rafiki?
       Hata pamoja na umuhimu wa kuwa na marafiki ni muhimu kufahamu kuwa si kila mtu anaweza kuwa rafiki,ni kweli kuwa tunapaswa kuwa na amani na watu woote lakini si woote wafaao kuwa marafiki hivyo ni lazima tuchague marafiki sawa na mapenzi ya kimungu. Si tunakumbuka kuwa marafiki wana uwezo mkubwa wa kuchangia katika kujenga au kuharibu maisha yako na tabia yako (Ikoritho 15;33). Katika mstari huu Biblia inasema hivi “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” Ki msingi biblia hapa inazungumzia marafiki, na sio mazungumzo tu, watafasiri wa biblia yetu ya Kiswahili walitumia neno mazungumzo mabaya, ambalo katika biblia ya kiingereza hutumika hivi, “ Do not be deceived; evil companionships corrupt good habits.” .  Kwa msingi huo kinachozungumzwa hapo ni zaidi ya mazungumza kama biblia ya Kiswahili isemavyo, hapa panazungumzia marafiki!Unaona!. Hivyo kumbe kama tutakuwa na marafiki waovu wanaweza kuchangia kuharibika kwa tabia zetu njema tulizo nazo ni muhimu kufahamu kuwa tabia mbaya huambukiza kwa haraka kuliko ilivyo kwa tabia njema.

    Ninawezaja kuchagua marafiki walio wema wema?.
     Kabla ya kuzungumzia swala la kuchagua marafiki nataka nikupe hadithi moja ya mnyama aliyeitwa ngamia,Siku moja msafiri mmoja wa jangwani alikuwa na ngamia kadhaa waliokuwa wamembebesha mizigo,Hata walipokuwa wakiendelea na safari jangwani ngamia mmoja aliugua na kushindwa kuendelea na safari hivyo alizimia, msafiri alifungua mizigo na kuibeba kwa ngamia mwingine kisha akamwacha jangwani akijua kuwa ngamia yule amefariki baada ya muda Fulani ngamia yule alipata nguvu na kuamka akijikuta peke yake jangwani,kwa bahati kulikuwa na majani mazuri mahali na hivyo aliweza kuishi vizuri, Siku moja mfalme wa jangwa Simba na rafiki zake watatu kicheche,fisi na chui walikuwa pamoja nae,Simba alishangaa kumuona mnyama huyo wa kufugwa akiwa peke yake jangwani na alimuuliza kulikoni ngamia alimwelezea simba yoote yaliyomkuta,Simba alimhakikishia Ngamia usalama na kumwambia kuwa hakuna atakayemgusa na kuwa wataishi pamoja kwa amani hivyo ngamia alifurahi sana .Siku moja Mfalme simba alijeruhiwa vitani huko nyikani katika vita waliyopigana na tembo hivyo alizidiwa na kuishi pangoni rafiki zake walimletea chakula cha mawindo kila siku hata hivyo wakati huu kulikuwa na hali ngumu ya upatikanaji wa mawindo na hivyo ilikuwa kwamba mfalme alikuwa hashibi na hali yake ya ugonjwa ilizidi kuwa mbaya, Siku moja fisi alitoa wazo kwamba ni vizuri mmoja wao ajitoe kama chakula kwa mfalme ili kunusuru uhai wake fisi alitoa wazo hili huku akijua kuwa kwa kuwa wao ni wanyama wa jamii moja hawawezi kulana wao kwa wao lakini waliamua kuigiza ili kwamba wamle ngamia ambaye alikuwa mkubwa na kingekuwa chakula cha kutosha kwa muda mrefu kiasi  hivyo kicheche alianza kwa kujidai anajitoa kwa mfalme hata hivyo mfalme alikataa kwa kuwa alidai kicheche alikua ni mdogosana na asingeliwatosha wote,kabla mjadala haujaisha fisi alidakia mfalme na anile mimi kwani fisi ni mdogo lakini kabla mfalme hajajibu chochote Chui nae alidakia kuwa yeye alikuwa mkubwa kiasi cha kutosha na angelifaa kuliwa na mfalme hata hivyo mfalme alikataa kujitoa kwa chui kwani woote hawa walikuwa wanyama wa jamii moja na woote wanakula nyama na si majani na kwa kawaida wanyama wa jinsi hii huwa hawalani,Ngamia alipoona kuwa kila mnyama aliyejitoa ofa kwa mfalme mfalme alikataa ofa yake yeye naye alijipeleka na kumwambia mfalme na anile mimi kwani wao ni wa jamii moja na ni wadogo wasingelimtosha mfalme ndipo Mfalme aliposema  nimekubali ofa yako ee ngamia muungwana na mara akamrukia na kumla na rafiki zake hadithi hii inatufundisha umuhimu wa kuchagua marafiki wa kweli.
  Waswahili wana msemo usemao kuwa ndege wa aina moja kwa kawaida huruka pamoja, msemo huu unaweza kuungwa mkono na maneno ya nabii Amosi katika (Amosi 3;3) ambapo Biblia inasema “Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja  wasipokuwa wamepatana?” hii ina maana kuwa mara nyingi tunaweza kuvutwa na watu ambao tabia zao zinapatana na za kwetu,kwa msingi huu lazima marafiki zetu wawe wale ambao kwa namna Fulani wana tabia au mtazamo unaolingana na matakwa yetu, Vijana wengi ambao huvuta sigara au bangi hupendelea kukaa vijiweni kwa wenzao ambao wanaweza kuvuta nao pamoja kuwapatia moto au hata sigara ama bangi na viberiti vya kuwashia,kwa hivyo ni muhimu kujua rafiki zako wana mtazamo gani na wewe unapendelea nini. Hiki ni kipimo kizuri cha uchaguzi wa urafiki.
        Aidha waswahili wana msemo mwingine usemao akupendaye wakati wa dhiki huyo ndiye rafiki, msemo huu unaweza kuungwa mkono kibiblia na ile mithali katika ( Mithali 17;17) ambapo biblia inasema “Rafiki hupenda siku zote Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu Ki msingi rafiki wa kweli ni yule ambaye atakupenda siku zote hata wakati wa matatizo,rafiki wakweli hatakuacha uingie pabaya kisha aseme nilijua tu  utaingia pabaya lakini niliogopa kukuambia,siku zote rafiki wa kweli ni yule ambaye anakueleza ukweli hata pale ambapo hutapendezwa na anayokuambia maadam tu anajua kua alilokuambia lina faida na ni la muhimu kwako.
       Ni muhimu kuwa na rafiki ambaye kwako atachangia uwe na tabia chanya kwa kadiri unavyoshirikiana naye unabadilika kitabia anakupandikizia mambo mazuri na unafaidika kwa kuwa naye katika mtazamo wenu, maana yake kama woote mmeokoka atakuwa kichocheo kikuu katika maswala yote ya kumcha na kumtumikia Mungu, Jihadhari na rafiki yeyote anayeonekana kuwa na tabia za kinafiki kama Yuda aliyeonekana akimbusu Yesu kumbe anatoa ishara ya kukamatwa kwake,rafiki wa kweli atakuwa anakuwazia mema (Mithali 27;6) atahakikisha kuwa anakulinda na madhara (1Samuel 18;1-4,20;1-4) atakuwa anatoa ushauri wenye kujenga na kukulinda,atakuwa ni mtu muaminifu anayeweza kukushirikisha hisia zake au wewe kumshirikisha hisia zako katika wakati woote huu kumbuka kuwa hakuna mwanadamu aliye mkamilifu hivyo kutakuwa na mapungufu ambayo kwayo mtakuwa mkichukuliana.kumbuka kuwa wewe pia sio mkamilifu.wakati woote huu  sheria ya dhahabu itakuwa ikipewa kipaumbele ile sheria husema hivi;-
 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.”Wakati wote huu ni muhimu pia kuwa na ujuzi kuwa biblia inatahadharisha kuwa na urafiki na watu wenye mizaha (zaburi 1;1-6) au watu wenye ushawishi dhidi ya kutenda uovu (Mithali 1;10-19). Na kwa vijana waliokoka wanapaswa kuwa makini kiimani kufungiwa nira na mtu asiyeamini (2koritho 6;14-18) hapa inazungumzia ushirika wa ndani sana  na wale wasioamini sisemi kuwa hatupaswi kushirikiana na watu wa dunia hii lakini ushirikiano wa mkristo na mtu asiyeamini ni wa lazima au muhimu pale tu inapolazimu kwa kusudi la kujenga jamii au uchumi au katika kuwaonyesha wasioamini njia ya wokovu,lakini si kibiashara,ndoa,uchumba n.k.Hii ni kwa sababu kihistoria popote pale watu wa Mungu walipojisahau na kujichanganya na watu wa duinia watu wa Mungu walivutwa duniani na kupoteza maadili yao na wakati woote huu zingatia rafiki ambaye atakupa ushari ulio sawa na imani yako na sio kinyume (2Samuel 13;1-5,16;21-22).

Swala la urafiki na Jinsia tofauti.
 Kimsingi urafiki wa watu wa jinsia tofauti haupigwi vita katika biblia na kinyume chake tunayo mifano  katika maandiko ya watu wanaume ambao wamekuwa na marafiki wanawake (mf.Yesu katika Luka 10;38-39,Yohana 11;5,Paulo mtume katika Warumi 16;1,3,6,12).Urafiki huu ni urafiki wenye dhamiri safi,ni urafiki unaohitaji kuwa na fikira adilifu,watu wengi hushindwa na aina hii ya urafiki na hujikuta wakiishia pabaya ni muhhimu urafiki wa na jinsia tofauti ukajengwa katika misingi ya uadilifu kama tutajifunza kufanya hivyo,urafiki na jinsia tofauti una raha zake na unamuimarisha mwanadamu kisaikolojia,mwanamke hawezi kuwa mkamilifu bila mwanaume halikadhalika mwanaume hawezi kuwa mkamilifu bila Mwanamke “Walakini si mwanamke pasipo mwanamume,wala mwanamume pasipo mwanamke katika Bwana”(1Wakoritho 11;11)Hii ina maana kuwa jinsia zote mbili zinahitajiana kimaumbile na kunahitilafu kubwa za kimaumbile zinazoweza kujitokeza endapo binadamu atakua katika mazingira ya kuikosa jinsia nyingine,Mtaalamu mmoja wa Saikolojia ya wanadamu alikuwa akihojiwa katika television kuhusu kuwepo kwa tabia za ushoga na usagaji mataalamu huyu alisema moja ya sababu kati ya nyingi zinazochangia tabia hii kujitokeza ni pamoja na jinsia moja kukaa pekee katika mazingira Fulani kwa muda mrefu bila muingiliano na jinsia nyingine mtaalamu huyu alitoa mfano wa Magerezani,Shule za bweni n.k,alisema kimaumbile hali hizi hupelekea kuzaliwa kwa tabia hii aidha kwa muda mfupi na wakati mwingine kwa muda mrefu. Hivyo wanawake na wanaume wanahitajiana kimuingiliano katika jamii hata kama si katika mahusiano ya kingono. Yako magonjwa ya kisaikolojia ambayo huwapata wanawake wanapokosa muingiliano na wanaume kwa muda Fulani na wakati mwingine magonjwa hayo ya kiakili huweza kufikiriwa kuwa ni pepo wabaya ,lakini pamoja na kuwepo kwa pepo wabaya ni muhimu tukakubali kuwa tatizo hili lipo kama vile kulivyo na kifafa cha kipepo na kifafa cha kawaida.kumbe basi kuna umuhimu wa kuwa na marafiki wa jinsia tofauti.Lakini ni muhimu pia kukawepo na mambo ya kuyazingatia tunapokuwa na marafiki wa jinsia tofauti ili kutulinda tusijiingize katika mahusiano ya kingono.

Mambo ya kuzingatia katika urafiki na watu wa jinsia tofauti.
   Kama nilivyogusia awali kuwa kuna umuhimu mkubwa kimaumbile kuwa na urafiki na jinsia tofauti kwa jamii nzima na kwa wakristo pia, jambo la muhimu ni kujenga msingi wa kimaadili kwanza hii ina maana ya kuwachukulia rafiki hawa kuwa kama kaka na dada akimshauri mchungaji kijana Paulo mtume alimshauri Timotheo kuwaona wanawake wazee kama mama na wanawake vijana kama ndugu wa kike katika usafi wote. (1Timo 5;2).kwa msingi huu ni muhimu kuwa na mijadala,mahubiri ya pamoja,kusalimiana  na kuwasaidia katika mazingira ya kuhitaji msaada,Paulo mtume alifanya kazi ya injili na wanawake wengi sana wakiwa ni wadau au watenda kazi pamoja naye soma wafilipi 4;3Biblia inasema hivi, “Naam nataka na wewe pia mjoli wa kweli,uwasaidie wanawake hao kwa maana waliishindania Injili pamoja nami,ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima”Unaona!. Ni wazi kuwa Euodia na Sintike walifanya kazi ya injili pamoja na mtume Paulo.Hivyo kuwa na marafiki wakike na wakiume inaewzekana lakini ni lazima tuzingatie mambo ya msingi kwani kuna tatizo.
         Tatizo kubwa la urafiki huu hasa kwa vijana  ni zile tamaa za ujanani na ule ukuta wa fikira adilifu ambao haujajengeka miongoni mwa vijana,hii ni fikira kuwamba kuwa na urafiki huu hupelekea watu kufanya ngono,(2Timoth 2;22). Hivyo ni lazima vijana wachukue tahadhari wanaporuhusu urafiki wa jinsia tofauti kwa sababu ni kweli urafiki huu kiutafiti unaonekana kufanikiwa kwa watu wachache na wengi huushindwa.
   Utafiti wa hivi karibuni uligundua kuwa aina hii ya urafiki hupelekea watu kuwa na upendo uliopumbazika,utafiti huu umebaini kuwa 87% ya wasichana na 97% ya wavulana waliokuwa na urafiki wa jinsia tofauti waliishia kufanyana ngono,hata hivyo 65% ya wasichana na 43% wavulana walikuwa na urafiki na watu wa jinsia tofauti bila ya kufanya ngono.
  • Mmoja ya wasichana aliyekuwa na urafiki na mtu wa jinsia tofauti akaishia kufanya ngono alitoa ushuhuda huu,Dada huyu aliyeitwa Loretta aliyekuwa na umri wa miaka 22 alisema tulivyoanza urafiki na mwanaume  kadiri siku zilivyoendelea tulihisi kupendana na kuhusika kwa karibu kwa hisia za kila moja wetu,lakini hatimaye tulikuwa tuna kumbatiana,baadaye tuliona hakuleti msisimuko tena hivyo tulianza kupeana busu,pia baadaye tuliona ni jambo lisiloleta msisimko na tulianza kutomasanatomasana na ikafikia hata kutomasana sehemu za siri,wakati huu nilijihisi niko tayari kabisa kutoa penzi langu kwa mvulana yule kwani nilijihisi kuhemkwa na kuhitaji kutimiziwa hamu ya kingono na kama ujuavyo wavulana huwa wepesi kusimamisha uume na kuwa tayari kimapenzi tuliishia kupeana mapenzi.
Jaribu kuwaza matokeo yaliyomtokea Loretta unahisi alikuwa na hali ya namna gani?Loretta aliishi maisha ya wasiwasi sana alikuwa akiwaza kuwa walikuwa hawajapima damu zao,kwani hawakuwa wachumba,hakuna aliyebeba kondom kwani hawakuwa wamejipanga kufanya mapenzi walikuwa marafiki na hakujua kuwa amepokea ujauzito au la. Kwa kweli kama vijana hawajaandaliwa vya kutosha kukabiliana na urafikiwa jinsia tofauti wanaweza kujikuta wameishia kuharibu urafiki wao.
     Ni kwa sababu hii Wachungaji wengi hubaki wakifukuzana na vijana na kuwafikiri kuwa ni wazinifu na kuwawekea sheria kali ambazo kwa kawaida hazisaidii kuzuia tamaa za mwili,na kunawajengea vijana nidhamu ya woga, ni muhimu vijana wasibanwe kwa sheria za kifarisayo badala yake wapewe mafundisho yatakayo wajenga katika uadilifu,ni muhimu kufanyika kaka au dada halisi kwa kila msirika katika kanisa,tukiishi kama ndugu si rahisi kufikia katika mawazo ya kingono, ni vizuri kina dada wakivaa kwa kujistahi kama mtu afanyavyo mbele ya kaka yake kwa ni mvao unapeleka ujumbe na unaweza kutongozwa kwa sababu ya muonekano tu (Mithali 11;16),Tafakarini gharama ya kufanya dhambi kwani dhambi ni nzuri lakini inagharama,jifunze kutofautisha kati ya upendo na tama,shirikisha rafiki zako namna unavyojisikia kihisia ili uweze kusaidiwa kwani kwa wakati Fulani kila mwanadamu hushambuliwa na mawazo ya kingono wakiwemo viongozi wa dini kwani wao sio malaika. Jifunze kuulinda moyo na mwelekeo wake(Yeremia 17;9). Jizoeze kuwa mwenye dhamiri njema (Mdo 24;16),na ikiwezekana kuweni katika mfumo wa timu inayozidi idadi ya kawaida ya kugawana,kaeni katika mazingira yasiyo na mashaka msijifiche.
 Vijana ni muhimu tu wakafahamu kuwa Mungu alipofunua neema ya wokovu alikuwa anataka waliookolewa waishi kwa kiasi angalia biblia inasema hivi “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;nayo yatufundisha kukataa ubaya na tama zote za kidunia;tupatekuishi kwa kiasi na haki na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa”( Tito 2;11-12),soma pia (Tito 2;6) “Vivyo hivyo na vijana wanaume uwaonye kuwa na kiasi”  Kwa msingi huu nami nikuonye kama maandiko kuwa hakuna jambo zuri duniani kama kuwa na marafiki wa jinsia tofauti lakini hakikisha haufunui,yaani haushiriki ngono nahii itadumisha heshima na urafiki mwema,ukifunua utaharibu uhusiano hata huo wa urafiki,mimi nami kama mtumishi wa Mungu sipendi vijana wabanwe na sheria lakini nataka vijana kwa hiyari yao na kwa kuutambua wokovu  na kuishi kwa kiasi bila kumvunjia Mungu heshima kwa faida ya maisha yetu mungu akubariki.

Jinsi ya kuchukuliana na watu tofauti tofauti
    Kuna wakati inatulazimu katika maisha kuvunja urafiki na baadhi ya watu kutokana na kushindwa kuchukuliana nao au kushindwa kuwaelewa wewnzetu kuwa ni watu wa namna gani na ni wa kundi gani katika tabia sehemu hii itatusaidia kufahamiana na pia kijifahamu ili iwe rahisi kwako kuchukuliana na watu woote rafiki aliyekomaa hawezi kupoteza marafiki kwani anawajua rafiki zake nguvu zao na udhaifu wao Biblia ina tuambia kuna aina nne za watu ona (Mithali 30;11-14).jamii hizi kisaikolojia huitwa Melancholic (mst 11),Phlegimatic (mst 12),Sanguine (mst 13) na Colerich(mst 14). Jamii hizi zina sifa na madhaifu, mbalimbali ambazo ni taa ya kutuonyesha sifa zao Sifa hizo ni kama ifuatavyo;-

Melancholy Kundi la watu wenye Nafsi inayoumia.
 Kwa kawaida hili ni kundi la watu makini, wenye kuweza kunyambulisha mambo,ni wenye kupendelea ukamilifu,wana mpangilio wa mambo wana mawazo mazuri na wenye kujitoa jamii hii ya watu wengi wamekuwa wanasayansi wasanii wanafalsafa na wagunduzi wa kubwa pia ni wachoraji,Hata hivyo ni kundi la watu wasiojichanganya na jamii wapweke na wanaoumia mioyo,wanatazamia mambo ya kuumiza ni wabinafsi,hana ushirikiano anatunza visasi wanahitaji tunda la roho la furaha na amani.

Phlegmatic. Kundi la watu wenye Nafsi iliyotuliana taratibu.
 Hili ni kundi la watu wanaojiamini,wanaojitegemea na kujitosheleza na ni wapenda amani,kundi hili ni la watu wasioweza kubadilika kwa haraka na hupenda kusanifu mambo,hata hivyo kundi hili hupenda kujilinda ni waoga,wachoyo hawahamasiki na ni wavivu wanapenda usingizi na mambo yao ni polepole na ni wachokozi chinichini hufanya chochote wanachoshauriwa

Sanguine. Kundi la watu wenye Nafsi Changamfu.
 Kundi hili ni kundi la watu wachangamfu sana wanaweza kufanya marafiki kwa haraka sana ni waigizaji wazuri na wasanii,ni wasemaji sana ,wacheshi,ni marafikihawatulii na wasiojitegemea,hata hivyo sanguini ni wadhaifu,wanaonekana kama hawana nidhamu waoga,wana haraka.

Choleric .Kundi la watu wenye Nafsi Katili.
 Kundi hili ni kundi la watu jasiri,wanaojiamoni,ni viongozi hufanya mambo yatokee ni watendaji wanaona mbali wanaweza kufanya maamuzi lakini ni wenye hasira ,hila,kujigamba,hana hisia za huruma,ni katili anajitoa sadaka kwa kufanya kazi kupita kawaida.
  Kuna uwezekano wa kujijua kuwa uko kundi gani kwa kuangalia sifa za makundi hayo nzuri na dhaifu kisha unachukua idadi ya sifa utakazozipata unazidisha kwa mia na kugawa kwa idadi ya sifa zote hapo utajijua.
Mfano tunamjadili Kamote kujua kuwa Yeye ni kundi gani hivi ndivyo tutakavyofanya
Melancholy


Phlegmatic


Sanguine


Choleric


Anauchungu                                                                                 

Anajiamini


Mcheshi


Ni katili


Ana jitoa
ΓΌ   
ΓΌ   
Mtaratibu


Msemaji

Anahasira


Ana kipawa
ΓΌ   

Anajitosheleza


Muigizaji


Jasiri


Ni mkamilifu


Habadiliki

Anakelele

Mzalishaji


Mbunifu


Hahamasiki

Muoga


Mtendaji


Makini


Ana sanifu

Muongo

Kiongozi


Hashirikiani

Mvivu

Muhamsishaji


Anaamua


Hanaharaka

Ana choyo

Hana aibu


Anakisasi


Mgunduzi


Hana haraka


Si mtendaji


Hujisifu


Mchoraji


Hujilinda


Kigeugeu

Ana hila


hunyambulisha
ΓΌ   

Hupendaamani


Ana haraka


hajihurumii



Unaweza kuona kuwa alama za x zinaonyesha sifa ambazo Kamote hana hivyo katika Melancholy Kamote hana alama tatu  na alama nane zilizo tupu ni sifa alizo nazo sifa zitakazopatikana utazigawa kwa 12 sawa na jumla ya sifa zote za kila sifa hivyo katika melancholy Kamote ana sifa nane na anakosa tatu hii ni kusema kuwa katika melancholy na sifa nnyingine Kamote atakuwa na sifa zifuatazo kwa kila moja ile itakayokuwa na asilimia kubwa zaidi ya wengine ndiyo sifa ya mtu huyo mfano mzuri ni huo hapo chini 

Melancholy kwa Kamote ni = 8/12 X 100=66 %
Phlegmatic kwa Kamote ni= 7/12X 100=58%
Sanguine kwa Kamote ni=7/12X100=58%
Choleric kwa Kamote ni = 12/12X100=100%

Hivyo Kamote ni Choleric kwa asilimia 100 lakini anazo sifa nyingine kutoka katika makundi mengine na kwa kawaida zile zinazojitokeza kwa wingi zaidi zile mbili hutabiri wazazi wa Kamote kuwa mmoja ni Melacholy na mwingine ni Choleric na kwa kawaida  Melancholy akioana na choleric melancholic huumizwa hivyo mmoja wa wazazi wa Kamote katika ndoa alikuwa ni nafsi iliyoumizwa na kitaalamu Yule anayeumia hufa haraka na ni kweli mzazi mmoja wa Kamote yaani mama yangu alikufa mwaka wa 1984 hivyo chati hizi husaidia hata kujua sifa za wazazi na taabu zao katika ndoa na kama mmoja yuko hai au l



                                                                      Enye Nguvu
 
                        Ana kisasi                                                                                 Ni katili
            Ni mwenye kujitoa                                                                                    Ana hasira kali
          Ana kipawa                                                                                                  Jasiri
        Ni mkamilifu                                                                                                        Ni mzalishaji
     Ni mbunifu                                                                                                                 Ni mtendaji
  Ni makini                                                                                                                       Ni kiongozi
Hashirikiani                                                                                                                      Anamaamuzi





  Ni mcheshi                                                                                                                       Anajiamini
   Ni muigizaji                                                                                                                    Ni mtaratibu
  Nimsemaji sana                                                                                                            Anajitosheleza
      Ana kelele                                                                                                                Habadiliki
         Ni muongo                                                                                                          Hahamasiki
           Muoga sana                                                                                                  Ni mwenye sanifu
                  Anakigeugeu                                                                                     Mvivu sana
                     Hana nidhamu                                                                         Ni mwenye choyo
                                                                         Dhaifu

    Mchoro huu hapo juuna ule wa box pale juu zaidi  husaidia katika kufanya hesabu za kujifahamu kuwa uko kundi gani kati ya hayo na sifa ulizonazo ,kwa kawaida kila mwanadamu anasehemu zote hizo nne iliyo yake ni ile inayojitokeza kwa kiwango kikubwa zaidi kwa asilimia ingawaje nyingine zinaweza kijitokeza kwa viwango vingine tunapofanya hesabu hizo kusudi sio kwa ajili ya kumcheka mtu bali kujua yuko kundi gani anahitaji matunda ya roho ya kiasi gani na watu watawezaje kuchukuliana naye hivyo Hesabu hizi zisitumike kama kigezo cha kuchekana au kusanifiana naamini utautumia kwa busara michoro hii hapo juu
(Michoro yoote Na hesabu Kwa niaba ya mwandishi wa somo hli Mchungaji Innocent Kamote)

Maoni 1 :