Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Hatari ya Madawa ya Kulevya



Somo la tatu
Vijana na Hatari ya madawa ya kulevya
Nyakati hizi tulizonazo ni tofauti sana na nyakati zilizopita dunia inakabiliwa na matatizo mengi yakiwemo mmomonyoko mkubwa wa maadili,rushwa,utoaji wa mimba, kuongezeka kwa vitendo vya ushoga na usagaji,ubakaji, uhalifu, watoto wa mitaani,ulevi wa kupindukia,  na wimbi kubwa la umasikini ,likiwemo wimbi hili la matumizi ya dawa za kulevya,kama kanisa litakaa kimya,jamii hii ya watu wanaokumbwa na mikasa ya aina hii ndio wataathiri hali ya taifa na kanisa la leo,na kama ilivyo kwa ukimwi,kushindwa kuzungumzia msimamo wa kibiblia dhidi ya hali ya madawa ya kulevya ni sawa na kuwa tayari na jamii au kanisa la watu dhaifu wasioweza kutumainiwa kwa namna yoyote ile kuliendeleza kanisa na taifa, kwani madawa ya kulevya  yana athari kubwa kwa msingi huo nitazungumzia hali hii katika maeneo makuu matatu.

  • Ufahamu kuhusu madawa ya kulevya.
  • Madhara yatokanayo na madawa ya kulevya.
  • Jinsi ya kuepuka madawa ya Kulevya.
Ufahamu kuhusu madawa ya kulevya.

   Madawa ya kulevya ni kemikali yoyote asilia au ya kutengenezwa kiwandani, ambayo huleta badiliko la kihisia au ufahamu pindi inapotumiwa. Dawa hizi huumba hali tegemezi (Drug dependens) ambayo ni athari za kisaikolojia na madhara  yatokanayo na madawa haya hali hii tegemezi ni hali ya kutoweza kufanya lolote bila kuyatumia au kushindwa kufanya jambo baada ya kuamua kuacha na kuwa kadiri unavyotumia uajikuta unahitaji kutumia kwa kawaida madawa haya yana shughuli maalumu kwani mengine hutengenezwa kwa kusudi latiba za kibinadamu isipokuwa yanapotumika vibaya athari zake ni kama hizi,dawa nyingine zozote pia zinapotumika nje ya maelekezo ya daktari au vipimo husia huweza kuleta athari Fulani ikiwa ni pamoja na kuharibu ini,moyo,ubongo n.k. tabia hii huitwa matumizi mabaya ya dawa (Drug abuse).katika somo hili sizungumzii zaidi matumizi mabaya ya dawa bali nazungumzia madawa ya kulevya  ambayo yamo katika makundi kama matano;

  • Zinazopunguza maumivu makali na kasi ya ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu,hizi ni heroine,morphine,codein n.k.
  • Zinazo punguza kasi ya utendajikazi wa ubongo (depressant) hizi ni kama vile valium, pombe, viyeyushia gundi, petrol, rangi n.k.
  • Zinazoongeza kasi ya utendaji kazi wa mfumo wa fahamu (Stimulants) hizi ni kama Caffene,mandrax, nicotine,zikiwemo sigara,bangi,mirungi na pariki.
  • Zinazoleta maono yasiyo na uhusiano halisi day dreeming hizi ni pamoja na bangi,aina Fulani za uyoga na mescaline n.k.
    Dawa hizo nyingine ni za asili na nyingine za viwandani, haya ndiyo madawa yanayotumiwa na watu wengi hususani vijana.

Madhara yatokanayo na madawa ya kulevya.
 Madawa ya kulevya yana madhara makubwa sana kijamii, kiuchumi, kiafya na kiroho kwa msingi huu hatushauri kabisa vijana kujiingiza katika swala zima la utumiaji wa madawa ya kulevya.

 Pichani mtu yuleyule aliyetumia Dawa za kulevya kwa miaka mitatu tu

Athari za kijamii.
   Matatizo ya madawa ya kulevya  yanaweza kusababisha  matatizo makubwa  katika jamii ,ikiwemo migogoro ya aina mbalimbali,kwa mara ya kwanza kabisa katika biblia ,tunaonyeshwa jinsi familia ya Nuhu ilivyokumbwa na matatizo yaliyotokana na ulevi ambapo ilibidi Nuhu kumlaani mjukuu wake kupitia mwanae Hamu, Hii ni kwa sababu ya kutokujiheshimu kwa Nuhu baada ya kuwa mlevi wa kupindukia na kupalekea mtumishi huyu wa bwana kuwa uchi na mwanae na mjukuu wake wakaona uchi wa baba yao,(Mwanzo 9;20-23)Ulevi unapelekea kuvunjika kwa heshima hata kama mtu huyo ni mwenye kuheshimika,ulevi unaweza kupelekea kuwepo kwa ngono hata zile zisizotegemewa walevi wengi hujikuta wanafanya ngono bila tahadhari za kutosha na hivyo kujikuta wakiwa na maambukizi, Biblia inaonyesha pia jinsi Lutu alivyolala na binti zake na kuzaa nao watoto baada ya kufanikiwa kumlevya baba yao na kufanikiwa kufanya naye ngono (Mwanzo 19;30-38) kwa ujumla muda usingeweza kutosha kusimulia visa na mikasa itokanayo na ulevi katika jamii hata hivyo familia ambazo  zimekulia katika ulevi huathirika sana na baadhi ya maeneo ambayo watu huathirika ni pamoja na ,Ugomvi wa kupindukia mateso na hata familia kukosa matunzo (Mithali 20;1),aidha tabia za kutumia vilevi yakiwemo madawa hupelekea watu kuwa wezi,majambazi,vibaka na kuwepo kwa tabia ya kuibiwa vitu vidogo kwa vikubwa,watu wa jinsi hii hawashindwi kabisa kufanya ubakaji,kutokujali,umalaya uliokithiri, kukosa elimu, maendeleo duni, kufukuzwa kazi kufanya uhalifu, kuharibu mamba au kuathiri afya ya mtoto kufungwa,ajali za barabarani na uhalifu wa kutumia silaha, Aidha jamii inakosa mtu au watu wa kuwatumainia kwa jambo lolote, na wakati mwingine kuwa na jamii ya watu tegemezi.
Athari za kiuchumi.
   (Isaya 55;2).Watumiaji wa madawa ya kulevya pia huathiriwa na maswala ya kiuchumi (Mithali 23;19-21).Kwa sababu madawa haya ni ghali na hivyo mtumiaji anahitaji fedha ili kujikidhi na maawa hayo,Watumiaji hao wakati mwingine  kwa sababu ya ulevi huvunja vyombo majumbani au kusababisha ajali za magari barabarani,Kunakuwa na gharama za kimatibabu za kuwatibu punde wapatapo ajali au wanapotibiwa kuwarejesha katika hali ya kawaida, watu hao huthamini ulevi kuliko chakula.

Athari za Kiafya.
    Miili tuliyonayo ni mali ya Mungu,tunapookolewa tunakuwa Hekalu la roho mtakatifu (1koritho 3;17,6;19-20), miili hii ni zawadi kutoka kwake na hivyo tunapoitumia visivyo halali  ni lazima tutawajibika kuitolea hesabu,Bahati mbaya sana watimiaji wa madawa ya kulevya wanakuwa addicted  yaani wana kuwa na tabia endelevu ya kutaka kuyatumia madawa hayo,na inakuwa vigumu kuyafurahia maisha bila kutumia,Watumiaji wa madawa ya kulevya hukabiliwa na tatizo la maambukizi  ya vvu Virusi vya ukimwi kwa sababu ya tabia zao za kuyatumia madawa hayo ambayo wakati mwingine huhitaji kujichoma kwa kutumia sindano moja,Wengine hupoteza uwezo au hamu ya kujamiiana au kushiriki tendo la ndoa,Wanawake wanaotumia madawa hayo huwa na uwezekano wa kuzaa mtoto punguani yaani wenye akili taahira au ulemavu,kuna magonjwa kama maradhi ya mapafu,Moyo,kansa, matatizo ya fahamu,usingizi kuuokosa au kulala sana,kupoteza kumbukumbu,maamuzi ya hovyo homa ya ini na kupungua uzito kwani watumiaji wengi hususani wa barani Afrika lishe zao ni duni hivyo wanakondeana kupita kawaida.

Athari za Kiroho.
  Hebu jaribu kuwaza kuwa watu hawa walioathiriwa na madawa ya kulevya  wanaokolewa na kuja kanisani na kuwa mshirika ama kiongozi au hata kuwa na wito wa kumtumikia mungu je unadhani  wanaweza kutumika ipasavyo(Efeso 5;18) “Tena msilewe kwa mvinyo ambamo mna ufisadi bali afadhali mjazwe Rohokimsingi Biblia inakataza ulevi na inaeleza  kuwa walevi hawana nafasi katika ufalme wa Mungu (1Koritho 5;11,Galatia 5;19-21,1Koritho 6;9) Mtu mlevi au muathirika wa madawa ya kulevya ni vigumu kwake kuabudu katika roho na kweli kwa ni madawa haya huharibu nguvu ambazo zingehitajika kwa utumishi (Mithali 20;29).Mungu hangependa kabisa kuwatumia vijana walioharibika akili kwa dawa za kulevya kwani wakati mwingine wanakuwa wagumu kuelewa,busara imeharibika,Hii haimaanishi kuwa walevi hawapokelewi na Mungu hapana wanapokelewa isipokuwa watakua na athari za madawa yale na hivyo ni ngumu kuwatumia kwa utumishi,Biblia inasema mpende Bwana Mungu wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote,tunawezaje kuzitumia nguvuzetu na akilizetu zilizo haribiwa na madawa ya kulevya katika kumpenda Mungu? Muhubiri 12;1 Biblia inasema “Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako,kabla  hazijaja siku zilizo mbaya  wala haijakaribia miaka utakaposema Mimi sina furaha katika hiyo” Ningependa kuwaasa vijana kuwa wautumie ujana wao vizuri kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya taifa letu zuri alilotupa Mungu nchi ya baba zetu, tukiutumia ujana wetu kwa faida ya mungu na jamii inayotutegemea na kama umejiingiza katika janga hili bado ziko namna ya kutoka huko sehemu ifuatayo  inatuelekeza namna  ya kujikwamua na janga hili ubarikiwe unapoendelea kujifunza.

Jinsi ya Kuepuka madawa ya kulevya.
     Kwa kawaida wengi wanao tumia mdawa ya kulevya huwa na visingizio mbalimbali vingi sana, ambavyo huvitumia ili kuhalalisha matumizi yao ya madawa ya kulevya, ulevi na uvutaji vifuatavyo ni baadhi ya sababu wazitoazo watumiaji wa madawa ya kulevya wanasema wao hutumia ili kusahau matatizo, au baada ya kushawishiwa na marafiki zao,kwa ajili ya upweke,kupunguza mawazo,umasikini,udadisi au kuijifunza kutoka katika familia zao,kukataliwan.k.

    Sababu hizi zote zinazotolewa na watumiaji wa dawa za kulevya hazina msingi kama watakuwa wamezingatia zile staid za kimaisha tulizojifunza katika somo hili.kama ni ushawishi kwa vyovyote ukizingatia uchaguzi sahihi wa aina za marafiki huwezi kushawishika,Nimesema sababu hizi si za msungi kwani Yesu Kristo alipitia aina yoote hiyo ya matatizo,ambayo vijana wengi hupitia ,alifiwa na baba yake mlezi Yusufu alikuwa mpweke duniani kuliko mtu awaye yote alikuwa na huzuni, na masikitiko,alikuwa masikini roho yake ilikuwa na huzuni nyingi kiasi cha kufa alisalitiwa na watu wake  na hata rafiki yake wa karibu aliyemgharamikia,aliteseka msalabani na kuaibishwa akiwa uchi kabisa mbele ya watu waliomheshimu lakini pamoja na hayo yoote hakutafuta faraja kwa kilevi kwani hata alipokuwa msalabani mtu alimletea kileo ambacho kingemfanya aiwena fahamu,apunguze migandamizo na upweke lakini alikataa (Marko 15;23) lakini alipopelekewa kinyaji ambacho sio mvinyo alikipokea (Yohana 19;18-30)Pamoja na yote ambayo Yesu aliyapitia yakiwemo mashitaka ya uongo,kukataliwa,kusalitiwa bado hakukatataamaa na kuamua kuwa mlevi.

     Dawa ya kuvunjika moyo na kukatishwa tama na upweke ni kujitoa kwa Mungu,katika sala na maombi,biblia inasema na tumtwike yeye fadhaa zetu zote maana yeye hujishughulisha sana na mambo yetu,furaha ya kweli haipatikani kwa kunywa gongo au madawa ya kulevya furaha ya kweli hupatikana kwa Yesu kwa kumkubali na kumwamini moyono Yeye alisema njooni kwangu ninyi nyote wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha ,Mjaribu Yesu,vunja urafiki na walevi,jifunze kujitia nidhamu jiwekee mipaka,muombe Mungu na tembea na wenye hekima, Kuwa mtu waibada na utakuwa huru toka katika madawa ya kulevya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni