Jumatatu, 1 Agosti 2016

Ujumbe. Nanena maneno ya kweli na ya akili kamili !


Matendo 26: 24-25 Biblia inasema:-
 
Alipokuwa akijitetea hivi, Festo akasema kwa sauti kuu, Paulo, una wazimu, kusoma kwako kwingi kumekugeuza akili.  Lakini Paulo akasema, Sina wazimu, Ee Festo mtukufu, bali nanena maneno ya kweli na ya akili kamili.”


 Wala sikuyakana yale Maono Matendo 26:19,- "Paulo Mtume"

Utangulizi:
Kifungu hiki ni maneno ya Mtume Paulo, alipopewa nafasi ya kujitetea mbele ya Mfalme Agrippa na Gavana wa Kirumi aliyeitwa Festo, Paulo alikuwa amepewa nafasi ya kujitetea kutokana na mashitaka ya wayahudi waliokuwa wakiipinga Injili, Katika namna ya kushangaza Paulo aliitumia nafasi hiyo kutoa ushuhuda wa Yesu Kristo na wokovu.

Watawala hao wa kipagani walikuwa wanafahamu vema matukio yaliyotokea katika uyahudi na walikuwa wanamfahamu vema Paulo mtume kama mtu msomi, hata hivyo Paulo alikuwa akimuelezea Bwana Mungu aliyemtokea katika maono na jinsi alivyoweza kumuokoa na kumuita katika utumishi huu Festo alipiga kelele kwamba  mtu huyu huenda kusoma kwake kwingi kumempeleka pabaya na kuwa sasa amekuwa na wazimu

Kuwa na wazimu maana yake ni kurukwa na akili ni kuwa nje ya akili zako za kawaida, nje ya usomi wako na utaalamu wako wa kawaida, ni kuwa chizi ni kuwa kichaa

Viongozi hao walimuelewa Paulo alivyokuwa na walimuelewa alivyokuwa akizungumza kabla hajaokoka, baada yakuokoka na kinachoendelea tangu alipokutana na Yesu nay ale ambayo Yesu anaendelea kuyatenda maishani mwake walihitimisha kuwa sasa amekuwa kichaa Lakini Paulo alikazia kuwa Yuko kamili na anazungumza maneno ya kweli na akili kamili

Hivi ndivyo ulimwengu unavyowaona watu waliomuamini Yesu, wanaonekana kama vichaa  na ni vigumu kueleweka kwa akili za kawaida zawadi hii kubwa ya wokovu, ni vigumu hata kuuelwa Ukristo ulivyo makubwa yaliyomchanganya Festo na Agrippa yalikuwa ni maswala haya katika hutuba ya kujitetea ya Paulo 

Matendo 26:12-13 Nuru ipitayo Mwangaza wa jua wakati wa Mchana adhuhuri

Matendo 26: 14- 18 Kutokewa na Yesu na kuagizwa kuhubiri injili

Ni vigumu kuelewa kile anachokisema Paulo kama bado hujaokoka na ni rahisi kudhani kuwa wokovu ni ukichaa lakini kilichomtokea Paulo ni wazi kuwa kinampata kila Mkristo aliyemwamini Yesu 

1.      Kila aliyemwamini Yesu ameona Nuru kuu 2Wakoritho 4:6 1Petro 2:9 Yesu ni Nuru kila aliyeokoka ametolewa gizani kuna nguvu katika nuru hii uwe umekutana nayo usiku iwe imekutana nayo mchana ni nuru ya ajabu ina nguvu ya kuweka Giza lote pembeni na wala havichangamani Yohana 1:1:1-5, tulipokutana na Yesu maisha yalibadilishwa na nguvu mpya ya nuru imeingia ndani yetu

2.      Kukutana na Yesu njiani hili lilikuwa jambo la kuwashangaza viongozi hao wa kipagani walifahamu kuwa Yesu alisulubiwa na alikuwa amekufa, alikuwa mtu dhaifu tu liwali wa kirumi Pilato alikuwa amemuhukumu kifo na kesi yake iko kwenye majalada, ni vigumu sana kuona Yesu anavyowatokea watu na kukutana nao kama uko nje ya wokovu lakini kila aliyeokoka anaelewa uhai wa Yesu Kristo anajua kuwa Kaburi halikumuweza anaelewawazi uwezo wake kwamba yuko hai Ufunuo 1:17-18

3.      Anabadilisha watu bila kujali historia yao
Walimfahamu Paulo kuwa alikuwa
·         Msomi mzuri sana
·         Mtu wa Dini ya kiyahudi aliyebobea
·         Mtu tajiri, mweye uwezo na cheo na ushawishi katika jamii
Sasa amebadilika kabisa tangu alipokutana na Yesu amekuwa kitu kingine kumbe mtu awaye yote wa hadhi yoyote ile akikutana na yesu anakubadilisha 2 Cor. 5:17.Kama watu hawataeewa kuwa Bwana Yesu yuko hai, basi watatambua kuwa yuko hai kwa uwezo wake wa kubadilisha, hakuna kiongozi yeyote Duniani ambaye amewahi kuweko duniani na kuwa na uwezo wa kubadilisha maisha ya watu wake kama Yesu Kristo

Mazungumzo ya Paulo yalikuwa hayaeleweki tena, alikuwa anaonekana kama amevuta bangi
§  Tunaposema Yesu amezaliwa na Bikira, alisulubiwa akafa akazikwa na akafufuka
§  Tunaposema tunaenda kubatizwa na kuzamishwa katika maji mengi kama sehemu ya agizo la kumtii Yesu Kristo watu wanaweza kufikiri kuwa tunawazimu
§  Tunapozungumza kuwa Damu yake inauwezo wa kuosha dhambi zetu
§  Tunaposema nyumbani kwetu ni mbinguni
§  Tunaposema Yesu atakuja tena
§  Tunaposema kanisa litanyakuliwa

§  Wafu watafufuliwa, kutakuwa na hukumu ya mwisho  na mengine yanayofanana na hayo
Watu wanaokuelewa 

Sasa amekamatwa na kushitakiwa kwa sababu hakuyakana yale maono Matendo 26:19 Paulo alikuwa katika vifungo kwaajili ya injili.

Wanaweza kudhani kuwa tumechanganyikiwa kwa sababu ya kumuamini Yesu lakini kuna badiliko kubwa na la ajabu hutokea ndani ya kila aliyemwamini Bwana Yesu, zaidi ya yote tunalo agizo la kuihubiri injili na kutokana na kuihubiri injili tunaweza kupitia majaribu ya aina mbalimbali hata kuwekwa Gerezani kama ilivyokuwa kwa Paulo, Festo alifikiri kuwa kusoma kwake kwingi kumemgeuza akili amekuwa na wazimu lakini Injili Ni maneno ya kweli nay a akili timamu.

Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni