Jumapili, 8 Januari 2017

Bwana Mungu wako Atakutangulia.


Mstari wa msingi: Kumbukumbu la Torati 31: 8


" Naye Bwana yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia, wala kukuacha usiogope wala usifadhaike"

Huu ni Mwaka mpya 2017 kwa kawaida wako watu wanaopenda mabadiliko lakini wako pia wanaoogopa Mabadiliko

Miaka inabadilika
Siku zinabadilika
Watu wababadilika

Kadiri miaka inavyokwenda mambo pia hubadilika
Musa alitembea na wana wa Israel kwa miaka 40 katika Jangwa, watu walikuwa wamemzoea lakini Mungu alimwambia Musa kuwa hutavuka MTO huu wa Jordan na alimuandaa Joshua kuwaongoza Israel

Wakati huu Israel na makuhani pia walikuwa na Hofu kuwa itakuwaje sasa
Kila wakati tunapokabiliana na Mazingira mapya, majira mapya, msimu mpya wa masomo, kazi mpya, miradi mipya, uongozi mpya, nk na hata Mwaka mpya huwa tubajiuliza itakuwaje?
Musa aliyajua Mashaka ya Israel, Mungu anayajua Mashaka yako katika Mwaka huu mpya anakutia Moyo

Atakutangulia, jangwa hili ni pana ni zito wakanaani wako mbele yetu ni lazima tuwakabili lakini kibinadamu hatuwezi wenyewe kabisa
Musa anatia Moyo

1. BWANA MUNGU WAKO ATAKUTANGULIA

2.ATAKUWAPAMOJA NAWE

3.HATAKUPUNGUKIA

4.HATAKUACHA

HIVYO HATUPASWI KUOGOPA WALA KUFADHAIKA MAANA MUNGU ATATUFANIKISHA

Mungu anapokutangulia hufanya miujiza mikubwa atakufungulia hazina zilizofichwa na utajiri na kusawazisha mapito yako, lakini vilevile atakupigania

Isaya 45:2-3.

 "2. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma;    3. nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli."

Mungu na akutangulie Mwaka huu
Na. Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni