Jumapili, 22 Januari 2017

Siri ya Kufanya mambo ya Kushangaza!



Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu amemkusudia kila mwanadamu kuwa na uwezo wa kufanya mambo ya kushangaza, Mwanadamu hakuumbwa kama kiumbe kingine cha kawaida, wanadamu sio viumbe wa mchezo mchezo, wanadamu sio tu viumbe vya kijamii lakini inaonekana kuwa mwanadamu ni kiumbe kilichobarikiwa uwezo mkubwa sana wa kubuni mambo na kutengeneza vitu na vingine vikadumu kwa muda mrefu sana, Mwanadamu ni kiumbe wa kushangaza, Nyani wanaweza kushangaza namna wanavyoruka toka tawi moja hata lingine lakini hakuna jipya wanaloweza kulifanya, sivyo ilivyo kwa wanadamu ni kiumbe wa ajabu Mungu amaemuumba kwa ajabu mno mno.

Matendo 6:8 Biblia inasema “Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.”

Biblia inatuambia kuwa Stefano alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu, maana yake Mungu anaweza kumtumika kila mtu kwa karama yake kufanya mambo makubwa ya kutisha na kushangaza

·         Maana ya neno Kushangaza
·         Mifano ya watu waliofanya mambo makubwa ya kushangaza
·         Siri ya kufanya mambo ya kushangaza

Maana ya neno Kushangaza.

Neno Maajabu tunalolizoma katika Matendo 6:8 limatokana na neno la Kiyunani “TERAS” Kiebrania “PALA” ambalo kiingereza husomeka kama “WONDERS”, “MARVELLOUS”, au “ TREMENDUS” Kwa hiyo kufanya maajabu maana yake ni kufanya mambo ya kushangaza, kila mmoja anaweza kuushangaza ulimwengu kwa kadiri ya neema na uwezo aliopewa na Mungu.

Mifano ya watu waliofanya mambo makubwa ya kushangaza
Dunia imakuwa na historia ya watu wengi waliofanya mabo makubwa ya kushangaza na wengine wanakumbukwa hata leo, kutokana na mambo makubwa waliyoyafanya
Muda hauwezi kutosha kuelezea Jinsi wamisri walivyojenga Pyramid  zaidi ya miaka 2500 kabla ya Kristo ni majengo ya ajabu sana hawakuwa na cranes wala winch lakini katika ujuzi mkubwa wa kihesabati waliweza

1.       Huko ufaransa katika jiji la Paris uko mnara mkubwa sana unaojulikana kama Iron Lady wenyewe wanauita “La Dame de Fer” yaani mwanamke wa chuma mnara huu unavutia maelfu ya watu kila mwaka kwenda kuuangalia mnara huo wa chuma mzuri na wa kuvutia lakini jambo la kushangaza mnara huu pia ujulikanao kama “Eiffel Tower” umejengwa mwaka 1889 na ulibuniwa na Enjinia “Gustave Eiffel  inaweza kukushangaza mnara wa siku nyingi hivyo unamvuto mkubwa mpaka leo duniani



2.       Empire states Mimi niliwahi kufika mahali hapa katika jiji la New York Jengo hili lilikuwa ndio jingo refu zaidi katika jiji la New York na lilikuja kupitwa baadaye na Trade towers zilizojengwa mnamo miaka ya 1931-1975, kwa miaka zaidi ya 40 kabla ya 1931 Jengo hili limekuwa ni la aina yake.



3.       Stature of Liberty ni Sanamu iliyoshikilia Mwenge iko katika lango la bandari ya jiji la New York ni moja ya sanamu yenye mvuto mkubwa sana hata leo lakini ilizinduliwa tarehe 28 October 1886 na mbunifu wake aliitwa Fredrick Berthold  




4.       Ikulu ya marekani WHITE HOUSE ni ikulu yenye mvuto mkubwa sana ilianza kukaliwa na maraisi wote walioko Marekani tangu rais Adam ni nzuri naya kifahari watu wengi hutembelea hapo mimi pia nilipata nafasi ya kupiga picha hapo, pamoja na mvuto mkubwa wa nyumba hiii ya kifahari na yenye kupendeza huwezi kuamini kuwa ilijengwa kati ya mwaka 1792 – 1800.


    Tukiwa White House  kutoka kushoto Athur Chikoka, Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye hekima, William Boniventure Kifutumo Nyadili, Yohana Martin Komba, Imani Peter Mngazija, Onstard Mashauri, Hubert Gumbo na baraka kolombo tulipotembelea Marekani mwezi Juni 2014 

5.       Kwa nini mifano hii yote? Ni kuonyesha kuwa wanadamu wanauwezo mkubwa sana wa kufanya maajabu wa kufanya mabo ya kutisha na kushangaza, tunaweza kufanya katika, masomo yetu, katika kuimba, katika kucheza soka katika kufundisha katika kupika na kila eneo Mungu analotupa tunaweza kulifanyia kazi kwa bidii na juhudi na kwa maarifa makubwa na tukaonekana watu wa tofauti

Mungu ndi ye mfanya maajabu makubwa zaidi duniani na Mbinguni kwa uwezo wake neema yake na roho wake anaweza kabisa kutusaidia kufanya mamnbo makubwa ya kupita kawaida ya kutisha na kushangaza
Siri ya kufanya mabo ya kushangaza
1.       Jiunganisha na Mungu kwa wokovu
2.       Jaa Roho Mtakatifu
3.       Omba neema na uweza Matendo 5:12, 6:8, 19:11
4.       Muombe Mungu Ishara na maajabu vifanyike Matendo 4:43
5.       Mwambie Mungu akujalie Matendo 14 :3
6.       Uwe na Bidii katika kila unalolifanya 

Ukiyajua hayo Heri wewe ukiyatenda.
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni