Ijumaa, 10 Machi 2017

Kwa nini Naipenda Israel kwanini Naipenda Yerusalem!



Zaburi 137:5,6Eee Yerusalem nikikusahau wewe Mkono wangu wa kuume na usahau, Ulimi wangu na uganadamane na Kaakaa la kinywa changu nisipokukumbuka, Nisipoikuza Yerusalemu zaidi ya furaha yangu iliyo kuu

 Pichani Jiji la yerusalem Maarfuru kama old Jerusalem ikionekana katika utukufu wake
 
UMUHIMU WA KUIPENDA ISRAEL. (JERUSALEM)

Mji wa Yerusalem ambao ni mji mkuu wa Israel ni mji muhimu sana katika maswala ya kisiasa kiimani na kiusalama mjii huu ni picha ya mji halisi ulioko peponi au mbinguni ambao ni makao makuu ya serikali ya Mungu Mbinguni, 

Mungu ana mji ulioko Juu mbinguni na mji huu unaitwa Yerusalem Wagalatia 4:25- 26Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalem wa sasa kwa kuwa anatumika pamoja na watoto, Bali Yerusalem wa juu ni mwungwana naye ndiye mama yetu sisi” 

Katika maandiko hayo Paulo mtume anaonyesha kuwa kuna Yerusalem ya Duniani naya mbinguni miji yote hii ni makao makuu ya serikali ya Mungu aliye hai, Yerusalem iliyoko Israel ni makao makuu ya Mungu Duniani na Yerusalem ulioko mbinguni ni makao makuu ya serikali ya Mungu.

Mji huu ni wa muhimu sana wengi waliotambua siri ya umuhimu wa mji huu wanaupenda na watakatifu waliotutangulia waliomba wasiisahau Yerusalem Zaburi 137:5,6Eee Yerusalem nikikusahau wewe Mkono wangu wa kuume na usahau, Ulimi wangu na uganadamane na Kaakaa la kinywa changu nisipokukumbuka, Nisipoikuza Yerusalemu zaidi ya furaha yangu iliyo kuu

 unaweza kuona Yerusalemu ni zaidi ya furaha ya watakatifu

Kama ilivyo kwa almasi katika kiti cha sofa ndivyo ulivyo mji wa Yerusalem mji huu ukokatikati ya vilele vya Safu ya milima ya Yudea (Uyahudi) na kwa ujumla ni katikati ya Dunia kijiografia, maisha na hatima ya wanadamu wote duniani iko au imefungamanishwa na mji huu wa kipekee, Tangu wakati wa Ibrahim nabii Israel imekuwa ni makao makuu ya ukombozi wa Mwanadamu, wakati huu dunia inapoelekea ukingoni Israel inaanza kuwa ngome tena ya kufunua makusudi ya Utawala wa Mungu duniani na ngoma ya kuchezwa mbele ya wanadamu na malaika.

Wakristo na hata wasio wakristo wanapaswa kuwa na uelewa wa kutosha Kuhusu Israel na Jerusalem na uhusiano wetu kiimani Biblia inaonyesha upekee wa hali ya juu kuhusu Israel na Yerusalem na kukosa ufahamu huu kunaweza kutunyima Baraka za kipekee zilizofichwa kuhusu inchi hii na mji huu

Nchi yangu na Mji wangu!

Zaburi ya 21:1 “Biblia inasema Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. “ unaweza kuona Biblia inatufundisha kuwa nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana na Dunia yote na watu wote, hivyo kuna uweli kuwa kila inchi ni ya Mungu na kila taifa ni la Mungu na watu wote ni wa Mungu katika ujumla wake, lakini katika upekee wake Israel na mji wake mkuu Yerusalem ni Mji mtakatifu wa Mungu na ushahidi wa kimaandiko upo kuthibitisha kuwa kuna utofauti kwa nchi hii na mji huu

1.    Unaitwa mji Mtakatifu “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, MJI MTAKATIFU; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.” Biblia inasema katika Isaya 52:1
 
2.    Yesu mwenyewe aliupenda mji huu licha ya kuutolea Machozi katika mafundisho yake aliuita mji wa Mfalme mkuu angalia Mathayo 5:35Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;    34. lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;35. wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa YERUSALEMU, KWA MAANA NDIO MJI WA MFALME MKUU” Yesu anatambua kuwa mji huu ndio makao yake makuu, mfalme mkuu ni yeye, mji huu ni wake unawezaje kusema kuwa unampenda Yesu kisha unachukia mji wake na serikali yake na makao yake makuu?

3.    Kiti cha enzi cha Mungu Yeremia 3:17 Wakati ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi cha Bwana; na mataifa yote watakusanyika huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la Bwana; wala hawatakwenda tena kwa ukaidi wa moyo wao mbaya.”

4.    Mungu aliahidi kuliweka Jina lake pale Yerusalem milele soma 2Nyakati 33:4 Biblia inasema ”Akajenga madhabahu katika nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu litakuwako jina langu milele

5.    Maandiko yako wazi kuwa Mungu anajivunia Yerusalem angalia Zaburi 87:1-3 Biblia inasema “Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu. Bwana ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo. Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu.”

6.    Yerusalem ni sababu ya Furaha Isaya 65:19 Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.”

7.    Isaya alisema kwaajili ya Yerusalem yaani sayuni sitanyamaza Isaya 62:31. Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. 2. Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. 3. Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.” Unaweza kuona jinsi mji huu uliyounganishwa na shughuli za kinabii na kiimani wote waliokuwa wakimpenda Mungu kwa dhati waliipenda Yerusalem kwa dhati vilevile

8.    Unabii unaonyesha kuwa siku za mwisho watu wengi sana wataitembelea Israel yaani wataitembelea Yerusalem makundi kwa makundi Isaya 2:3 “1. Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi katika habari za Yuda na Yerusalemu. 2. Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.  3. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. 4. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. 5. Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana”.Unaona unabii wa Isaya watu wote wataiendea Yerusalem huko ndiko itokako amani ya watu wote huko ndio asili nya Neno la Mungu, huku ndio asili ya mafundissho yote Yerusalem Yerusalem!

Mungu hajamaliza na Yerusalem ya Asili

Ni muhimu kwa kila mkristo kuwa na uelewa huu kuwa Mungu hajamaliza kazi yake na mji huu Yerusalem wa Duniani, nasema hivi kwa sababu mtu anaweza kujenga Hoja za kimaandiko kuwa isis kama Ibrahimu tunautazamia mji wenye misingi ambao mwenye kuujenga na kuubuni ni Mungu, akiwa na maana ya Yerusalem ya Mbinguni  sawa na Waebrania 11:10 ambapo Biblia inasema “Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. 9. Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.” 

Maandiko yanaonyesha kuwa Ibrahim kwa Imani alikuwa akiutazamia Mji wa Mbinguni kwa vyovyote vile Yerusalem wa Mbinguni, Pia tunaweza kuona msisitizo wa Paulo Mtume kwa Wafilipi 3:20Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;” na tunaambiwa kuwa Yerusalem wa Mbinguni ndio mama wa yote Waebrania 12:22 na kuwa kila aliyeamini ameungamanishwa na Sayuni ya Mbinguni au Yerusalem ya Mbinguni  Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,”

Na Kama haitoshi Yesu mwenyewe alionyesha kuwa ndani ya agano jipya watu wangefurahia uwepo wa Mungu katika roho na kweli ikiwa na maana ya ibada halisi haitategemea Hekalu Yerusalem wala mlima Fulani kwa vile Mungu anataka kuabudiwa katika roho na kweli angalia Yohana 4:21-24 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.  Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli”. 

Kama utaviangalia kwa makini vifungu vyote vya maandiko hapo juu unaweza kudhani kuwa Mungu hana kazi tena na mji wa Yerusalem wa sasa na Taifa la Israel, unaweza kufikiri kuwa makusudi yake yamekwisha 

Lakini turudi tena katika Mathayo 5: 35 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; 34. lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;35. wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa YERUSALEMU, KWA MAANA NDIO MJI WA MFALME MKUU” Yesu anaonyesha kuwa tusiape kwa Yerusalem kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu hii ina maana gani kwa nini asiseme kwa vile ulikuwa mji wa mfalme mkuu? Kwanini Mungu Hajamaliza kazi yeke na mji huu wa Yerusalem wa asili

Yesu alisema Yerusalem utakanyagwa na mataifa kwa kitambo Luka 21:24 “…..Na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia” 

“Kama Maandiko yametoa nafasi ya kukanyaga Israel na Yerusalem naamini ni vema wakristo tukaitumia nafasi hiyo ya kwenda Israel na kutembelea nchi hiyo ya kipekee kwani utakuja wakati itakuwa ngumu sana kuitembelea Israel hata kama utakuwa na uwezo huo” huu ni mtazamo wa kinabii wa mkuu wa wajenzi hapa.

Maneno hayo ya kinabii yanamaanisha kuwa mataifa wataukanyaga kwa muda na hatimeye mjii huu utarejeshwa katika utukufu wake , Yesu Kristo atakaporudi katika utukufu wake atasimamisha serikali yake kutoka mji huu na kutawala akiwa MFALMA WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA Kutoka Israel Yerusalem angalia

 Zekaria 14:4, 9Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini. , Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja” 

Kwa hiyo iko wazi kuwa mjii huu bado uko na uhusiano mkubwa na maswala ya kiimani ni wazi kuwa kuna Baraka za kimungu kama tunautakia mafanikio, na hata ingawa kunaweza kusiwe na Uhusiano wa kiibada na Israel au Yerusalem lakini huwezi kukataa kuwa kuna ahadi za mafanikio kwa wanaoiombea Israel na wamnaoutakia mema Yerusalem

Utakieni Yerusalem Amani!

Zaburi ya 122 :6-9 inasema hivi:- “Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao;. Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako. Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe.  Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu, Nikutafutie mema

Biblia inaamuru “Utakieni Yerusalem Amani” na inaunganisha Baraka kubwa na wale waipendao Yerusalem wafanikiwe wakupendao, Mema yataambatana na kila Mkristo na mtu aiye mkristo anayeitakia Mema Israel na Yerusalem

Mungu anataka tufurahi pamoja na Israel Isaya 65:18 , 19 a na 66:10-13 Biblia inasema haya

“18. Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha. 19. Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza. 10. Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake; 11. mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake. 12. Maana Bwana asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa. 13. Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu.”

Yesu aliipenda Yerusalem kiasi cha kuulilia mji huu, Nehemia aliugua na kufunga na kuomba kwaajili ya Yerusale, Yesu anaitamani Yerusalem mpango wake ni kuukumbatia ni kuukusanya kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake! Mathayo 23:37Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka! “ Yerusalem walikataa mapenzi ya Mungu kwa kumkataa masihi na kumsulubisha nje ya mji huu, lakini Mungu anawatamani sana Israel na ni mapenzi ya Mungu waokolewe na mjii huu kwa vyovyote vila ndio utakuja kuwa makao makuu ya Masihi Yesu.

Siri ya tai ya rangi ya blue katika shati Jeupe!
 

Kwa nini Viongozi katika Israel na Marekani huvaa tai ya rangi ya Blue? Ngoja nikuambie siri ya tai ya rangi ya blue na Nyekundu kwa Marekani, Bendera ya marekani ina rangi nyeupe, Nyekundu na blue, Chama cha republican huwakilihwa na rangi nyekundu na chama cha democratic huwakilishwa na rangi ya blue hii ni alama kubwa sana kwa taifa lao, wanapovaa tai viongozi wao huvaa kuonyesha uzalendo wa taifa lao katika maswala ya kitaifa

Pia kwa vile wamarekani wana uhusiano mkubwa sana na Israel pia kuvaa tai ya blue kwao humaanisha wazi kuipenda na kuiunga mkono Taifa la kiyahudi, Wayahudi bendera yao ni yeupe na ina mistari ya blue na nyota ya Mfalme Daud iliwa na rangi ya blue hivyo viongozi wa kitaifa kwao huvaa tai ya blue
Uganda bendera yao ina rangi nyekundu,mkenya pia na nyeusi na njano, Rais Museven hupenda kuvaa tai ya Manjano kwa vile ni rangi ya taifa lao katika bendera yao
Ukiona kiongozi wa kitaifa katika taifa ambalo halijamwaga Damu amevaa tai nyekundu maana yake huvaa tu bila kuzingatia amevaa kwa maana gani

Tai ya blue ikivaliwa na mtu anayejua maandiko humaanisha wazi kuwa anaipenda Israel, scafu na kadhalika kwa msingi huo kama unaipenda Israel katika kuonyesha mapenzi yako kwa taifa hilo vaa tai ya blue kuna siri kubwa katika jambo hilo kwaajili ya kuonyesha unaiunga mkono Israel
Kwa bahati njema kwa watanzania tai ya blue pia itakuwa ni sehemu ya Bedera yetu katika zile rangi nne mamarufu kwa hiyo tai ya blue itamaanisha uzalendo kwa taifa lako lakini kiroho Israel, hii ni siahara nyingine ya kuipenda sayuni.

Ujumbe na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni