Alhamisi, 7 Septemba 2017

Jinsi ya kujitakia kisasi kwa Bwana!



Andiko la Msingi: 2Wathesalonike 1:6Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi

 Musa akimuomba Mungu kwaajili ya kuwaangamiza Amaleki walioinuka kinyume na Israel

Ni muhimu kufahamu wazi kuwa kuonewa kwa mtu wa Mungu, sio mpango wa Mungu, wala sio mapenzi yake, watu wengu hususani wakristo kwa kutokuwa na ujuzi wa maandiko wamefikiri kuwa kuonewa ni sehemu ya maisha ya ukristo dhana hii sio mpango kamili wa Mungu, Biblia inatufundisha wazi kuwa Wakristo wanayo namna yao ya kulipiza kisasi, na hata kudai au kujitakia kisasi kwa Bwana Mungu wetu pale tunapoonewa, Maandiko yanayotumika vibaya na kupelekea wakristo wengi kuonewa na shetani kwa sababu ya kutokuelewa ni kama “Mathayo 5: 38-39  Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.     Ni kutokana na kuweko kwa andiko hili wengi wamefikiri kuwa wakristo hawana namna yao ya kulipiza kisasi  na kuwa wakionewa basi kila kitu kimeishia hapo, hayo sio mapenzi ya Mungu kamwe.tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele kadhaa vifuatovyo;-

·         Bwana Ndiye Mlipiza Kisasi
·         Jinsi ya kujitakia kisasi kwa Bwana!
·         Pale unapolazimika kujitakia kisasi!
·         Jinsi ya kuharibu Ngome za adui

Bwana Ndiye Mlipiza Kisasi. 

Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu wetu habadiliki Yeye ni Yeye Yule Jana Leo na hata milele, watu wengi sana hususani Wakristo wameonewa na shetani pamoja na watumishi wake kwa sababu ya kufikiri kuwa wakipigwa shavu la kuume wanapaswa kugeuza lile la pili, na kwa sababu hii shetani amepata nafasi ya kutuibia haki yetu ya kujilipizia kisasi dhidi ya wanaotuonea, wengne wameweza kupoteza haki zao na kutokuzidai kwa namna yoyote ile kwa sababu ya dhana hii,  Biblia inaonyesha jinsi ambavyo wakristo wanavyoweza kulipa kisasi, au kujitakia kisasi kwa Bwana, haya ni mapenzi ya Mungu kabisa, Biblia inaonyesha wazi ya kuwa tunaweza kumsihi Mungu ainuke na kushughulika na adui zetu Zaburi 68:1-3 Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika, Nao wamchukiao huukimbia uso wake.  Kama moshi upeperushwavyo, Ndivyo uwapeperushavyo wao; Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto, Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu. Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa furaha.”

Ni muhimu kufahamu Biblia ya Kiswahili hapo ilitafasiriwa kwa lugha yenye kupoteza maana kidogo andiko hilo katika biblia ya kiingereza NIV linasomeka “May God arise, may his enemies be scattered” ni kama ingesemwa “Mungu uinuke na watawanyike maadui zako” KJV insomeaka hivi “Let God arise, let His enemies be scattered” ni kama ingekuwa hivi “Acha Mungu ainuke adui zake watawanyike” andiko laonyesha wazi kuwa Mungu yuko pamoja na wenye haki yaani watu wake na kuwa kila aliye adui wa mtu wa Mungu pia ni adui wa Mungu, kuinuka kwa Mungu ni hatua ya Mungu kuwachukulia hatua walio kinyume naye na walio kinyume na watu wake.

Yesu mwenyewe ametufundisha ni namna gani tunaweza kujiombea au kujitakia, akimaanisha kuwa tunaweza kumlilia Mungu atupatie haki yetu dhidi ya adui zetu haki hii ndio kujitakia kisasi kwa Bwana angalia Luka 18:1-8a, Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.  Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima. Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?  Nawaambia, atawapatia haki upesi;” Hebu angalia kwa makini maandiko hayo Mungu anatufundisha nini ? Yeye ndiye hakimu wetu yeye ndiye amabaye tunaweza kumlilia na kuugua kwake mpaka haki ipatikane, kumbe basi Mkristo haitakiwi ukidhulumiwa tu unakubali, ukionewa tu unakubali, ukitukanwa tu unakubali, ukifukuzwa tu unakubali hapana haiwezekani wakupige tu haiwezekani usikae kimya yuko hakimu mkuu yuko Jaji anza kumlilia yeye atakulipia kisasi, Mungu akufungue uweze kuelewa maandiko haya inaweza kuwa vigumu kwako kwa sababu ndivyo ulivyozoezwa kwa miaka mingi makanisani leo mBwana na akufunulie hili ili uweze kupatiwa haki yako katika jina la Yesu. 

Hakuna shaka kuwa Mathayo 5:38-39 imetafasiriwa vibaya  na watu wengi wakati wote na umetumika vibaya , kwa mfano watu wametumia kifungu hiki kufikiri kuwa wakristo wanapaswa kuwa wapumbavu na wajinga na kuwa mtu yeyote akitaka kuwadhulumu wakristo atawadhulumu atakavyo, maandiko haya yametumika pia kama aya za kupinga vita na kila aina ya uasi n.k, tafasiri za aina hiyo sio za kimantikikatika eneo hili, Yesu aliweka wazi kuwa hakuja kuivunja torati bali kuitimiza na kuwa hakuna hata nukta moja ya torati itakayoondolewa Mathayo 5:17-19,Hii ni sheria inayohusu heshima, utii na kulinda haki za binadamu, sheria hii iliwekwa ili kuwalinda watu wasijichukulie sheria mkononi na pia kulipana kisasi kwa kuvizia dhidi ya maadui, lakini pia inazitaka mahakama kuhakikisha kuwa zinawatendea watu haki, Hivyo kimsingi Yesu hakuondoa kisasi na badala yake alikuwa akitufundisha wakristo kuwa iko namna yetu ya kujilipia kisasi, ambayo ni tofauti nay a watu wa dunia hii waliopotea, Mungu ametupa njia ya kujitakia Kisasi ili kukomesha uonevu kwa kumuachia yeye ashughulike na adui zetu, lakini hii haina maana kuwa kisasi hakipo!

Angalia kwa makini Biblia yako Warumi 12:19-20 “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.” Angalia kwa makini sana Biblia inaposema Msijilipizie kisasi maana yake nini Msijichukulie sheria mkononi, msjitafutie haki ninyi wenyewe, Biblia inasema ipisheni ghadhabu yaani achieni Hasira ya Mungu iamue, kwa nini kwa sababu ameahidi katika neno lake kuwa kisasi ni kazi yake na ni lazima atalipa, sisi tumeamuriwa kuwatendea mema adui zetu na maana yake unap[omtendea mema nini kitatokea? UNAMPALIA MAKAA YA MOTO KICHWANI PAKE, yaani ndio unaharibu na kuifanya hukumu ya Mungu dhidi ya adui yako au zako izidi kuwa tamu, kama nitakavyokuelekeza baadaye.

Mungu ni Mungu wa Kisasi, mafuta na upako wa Roho Mtakatifu hakuo kwaajili ya mema tu wala hakuo kwaajili ya kutangaza habari njema tu, lakini upako wa Roho Mtakatifu uko pia kwaajili Bwana kujilipizia kisasi angalia vizuri Isaya 61:1-2Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;” Umeona habari njema sio kwa wajeuri na wenye kiburi habari njema ni kwa wanyenyekevu, wanaogangwa ni wale waliovunjika moyo, wanaotangaziwa uhuru ni wale waliotekwa, wanaofunguliwa ni wale waliofungwa na unapotangazwa mwaka wa Bwana wa jubilee pia Kisasi cha Mungu wetu kwa wale wanaolia au walioonewa.

Unaona Mungu wetu ni Mungu wa kisasi, Kisasi maana yake Ni kurejesha maumivu ya kujeruhiwa kwako kwa nguvu kwa mtu aliyekudhulumu katika wakati ambao hangependa iwe hivyo, ni kurejeshewa maumivu kutokana na kosa lililofanyika mwanzoni, ni kurejeshewa kwa mtu kwa kutendea mabaya, Mungu emomba mwenyewe katika maandiko kwamba kazi hii iwe yake yeye atalipa Warumi 12:19b Mizani na kipimo cha adhabu ya wema au ubaya anayo yeye, yeye ndiye anayejua atapimaje kwa kupitia Hasira yake takatifu, Mungu analipa kisasi na kuwaadhibu waovu kwa vipimo vya haki yake.

Mungu hatamuacha mdhalimu aende zake kwa amani tu bila kumshughulikia Nahumu 1:3Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.” Kumbe Mungu ana namna yake na ni lazima atashughulika na mtu muovu, yeye hataki sisi tulipe katika hasira zetu, kumbuka kuwa yeye si mwepesi wa hasira ana uwezo mwingi yaani ana nguvu zote atashughulika tu.

Na ndio maana anasema Kisasi ni juu yake ameahidi kuwa atatupigania nasi tutanyamaza kimya Kutoka 14:14 wakati mwingine hatuwezi kuwa naamani mpaka tumekuwa na vita , na ni muhimu kufahamu kuwa kazi ya adui ni kuhakikisha kuwa wakati wote kunakuwa na machafuko tu, na muhimu zaidi kufahamu kuwa hatuwezi kuwa na mpenyo ama amani ya kweli kama adui zetu hawatatokomezwa kabisa “Hawa wamisri mnaowaona leo hamtawaona tena milele” ni lazima adui aondolewe, na ili uwe na uhakika  wa uhuru wako ni ni lazima aondolewe milele.

Kutoka 22:18 Biblia inasema “Usimwache mwanamke mchawi kuishi.” Unajua biblia inamaanisha nini usiruhusu shughuli za kichawi zikakuharibu,  maana yake hakikisha hakuna shughuli za kichawi wala mchawi mwenyewe, hii ina maana gani Ulinzi wa uhakika wakati mwingine ni kumsambulia adui yako na kuimmaliza, iko kanuni isiyobadilika inayosema hivi “Usipowamimamisha watakusimamisha wewe” Unaona shughulika na adui zako katika ulimwengu war oho kabla hawajainua hata silaha zao, Mungu tunayemtumikia ni Mungu mwenye wivu, atatangaza siku ya kisasi kwa adui zako, shuhuda nyingi namatukio mengi ya ushindi yanatokea Mungu anapokuwa ameingilia kati dhidi ya adui zako.

Jinsi ya kujitakia kisasi kwa Bwana!

Tumekwisha kuona sasa kuwa kisasi ni mapenzi ya Mungu lakini ni kuwa Mungu amejitwika yeye jukumu hilo na kuwa atawalipia kisasi adui zetu, lakini sasa ni namna gani tunaweza kujitakia kisasi kupitia Bwana Mungu wetu? Zifuatazo ni namna mbalimbali ambazo tunaweza kujilipizia kisasi.

1.       Fungua kesi ya uliyotendewa Mbinguni.

Mara moja unapoumizwa au kuonewa sio vema kukaa kimya na kusema tu namwachia Mungu, ni Muhimu kesi hiyo ikaripotiwa mbinguni haraka, Nyakati za kanisa la kwanza hawakuwa wajinga walichukua hatua za haraka wakamwambia Bwana yaangalie matisho ya watu hawa, walinukuu na vifungu jinsi masihi Yesu anavyofanyiwa ghasia kisha iachie Mbingu itashughulikia kesi yako Matendo 4:23-31.23. Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee. Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?  Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake. Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.” Unaona nyakati za kanisa la kwanza walijua nini walichotakiwa kukifanya walishitaki kwa Mungu yale waliyotendewa, Sisi hapa Afrika na hapa Tanzania na hapa Tanga na sehemu nyingine mbalimbali tunafahamu jinsi watu wachawi na wauaji wengine wa kishirikina wanavyojua kushitaki kwa miungu yao na kujitakia kisasi, Wakristo wamekuwa wajinga tu wananewa tu na kamwe awapeleki taarifa za uonevu wao huko mbinguni,

Mwanaume mmoja huko Muheza katika kijiji kimojawapo aliibiwa Nazi shambani kwake na alipokuta kuwa ameibiwa nazi alisikitika sana, waliokuwa wamemuibia nazi walizifua na kuacha maganda ya nazi shambani kwake, mwanaume huyo alipiga mbiu kuwa kila mtu aliyehusika kuchukua nazi shambani kwake azirejeshe na alitahadharisha kuwa mtu asinunue nazi hizo wala kuzitumia alitangaza kuwa siku saba tu itakuwa “grace period” yaani siku za kujisalimisha na baada ya hapo mwanaume huyo alichukua maganda ya nazi na kuyaweka juu ya kichuguu cha mchwa kisha akalia na kusema maneno juu ya adui zake waliokuwa wameiba nazi zake,  baada ya siku chache sana ndugu wengi sana wa watu waliomuibia nazi walianza kupatwa na misiba mfululizo hali iliyopelekea nyuma ile yote kuwa ukiwa kwa kufa.

Kwa nini nimeweka stori hii hapa wana wa dunia hii wako siriasi sana wanapoonewa, wana wa ufalme wanazubaa ni lazima ulie ni lazima uipeleke kesi kwa hakimu wetu mbinguni ni lazima umtaarifu na kumueleza jinsi ulivyoumizwa na kile anachokutendea au walichokutendea wadhalimu.


2.       Peleka vitisho vyote mbele za Bwana

Ni muhimu kumweleza Mungu kile ambacho adui amekutamkia, mweleze Mungu wamekuita jinga, wamekudharau. Wamekutishiawamekuonyesha shuhuda zao kuwa wametesa wengi na kuwa wewe sio lolote, sio chochote, wanaonyesha nguvu zao na uwezo wao katika shuhuda zao ili kukuonyesha kuwa huwezi kufanya lolote inawezekana ikawa kweli madai yao lakini Mungu ni mwenye nguvu peleka vitisho vcya adui zako kama vilivyo, usipunguze wala usiongeze , angalia kwa mfano tishio la Senekarebu 2Wafalme 19: 10-13Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema, Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru. Tazama, umesikia ni mambo gani wafalme wa Ashuru waliyozitenda nchi zote, kwa kuziangamiza kabisa; je! Utaokoka wewe? Je! Miungu ya mataifa wale, ambao baba zangu waliwaangamiza, imewaokoa? Yaani, Gozani, na Harani, na Resefu, na wana wa Adini waliokuwa katika Telasari? Yuko wapi mfalme wa Hamathi, na mfalme wa Arpadi, na mfalme wa mji wa Sefarvaimu, na wa Hena, na wa Iva? ” Unaona hapa Mfalme Senekarebu alikuwa amepeleka habari za kutisha na kutaka kudhuru huku akiwa na kiburi kwamba mfalme Hezekia asijidanyanye katika habari za Mungu wake kwa kuwa yeye ana uzoefu wa ushindi na amepiga nchi ambazo pia zilikuwa na miungu, alimpa na shuhuda waulize wenzio yuko wapi mungu wa Gozani na harani na Resefu n.k unafanyaje unapopokea vitisho kutoka kwa mtu mwenye nguvu kukuzidi, ana pesa kukuzidi, wewe sio tajiri kama yeye na anakunyanyasa na kukuambia kuwa nenda kokote huwezi kunifanya lolote unamfanyaje?lazima umripoti kwa Mungu mwenye nguvu hiki ndicho alichokifanya Hezekia 2Wafalme 19:14-20, “Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya Bwana, akaukunjua mbele za Bwana. Naye Hezekia akaomba mbele za Bwana, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.  Tega sikio lako, Ee Bwana, usikie; fumbua macho yako, Ee Bwana, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, ambayo amemtuma mtu aje nayo ili kumtukana Mungu aliye hai. Ni kweli, Bwana, wafalme wa Ashuru wamewaharibu mataifa na nchi zao, na kuitupa miungu yao motoni; kwa maana haikuwa miungu, bali ni kazi ya mikono ya wanadamu; ilikuwa miti na mawe tu, ndiyo sababu wakaiharibu. Basi sasa, Ee Bwana, Mungu wetu, utuokoe na mkono wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe Bwana Mungu, wewe peke yako. Ndipo Isaya, mwana wa Amozi, akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akisema, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa kuwa umeniomba juu ya Senakeribu, mfalme wa Ashuru, mimi nimekusikia.” Ikawaje wakati huu Bwana alituma malaika na jeshi lake lote lilipigwa nay eye mwenyewe mwenye jeuri aliuawa na watumishi wake soma Mstari 35-37 35. Ikawa usiku uo huo malaika wa Bwana alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia. Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akaondoka, akaenda zake, akarudi akakaa Ninawi. Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake. “ Unaona mtaarifu Mungu usiache adui yako akakutukana na kukufuru hata kama ana nguvu kiasi gani ni lazima watambue kuwa tunaye Mungu mwenye nguvu zaidi.

3.       Tangaza vita dhidi ya adui zako.

Biblia inatufundisha kwamba kunapotokea vita dhidi ya adui zetu wanaotuonea tupige kelele ya kugutusha kwa tarumbeta na Bwana atatukumbuka Hesabu 10:9Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za Bwana, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu.” Biblia inamaanisha nini hapa Tangaza vita kwa kuabudu unakumbuka jinsi ukuta wa Yeriko ulivyoanguka tarumbeta zilihusika yaani pembe za kondoo mume endapo unayo pembe halisi kutoka Israel hapo ndipo mahali pake ipulize abudu lia mbele za bwana mwambie ninatangaza vita na adui yangu na Mungu ayashikaye maagano atakukumbuka.

4.       Omba kwamba Mungu aingilie kati.

Nimuhimu kufahamu kuwa hatupaswi kukawia kumsihi Mungu aingilie kati mara moja adui zetu wanapotushambulia Nehemia alikuwa kiongozi Hodari na alifanikiwa kuujenga ukuta wa Yerusalem chini ya upinzani mkali, akielewa wazi kuwa ni mapenzi ya Mungu ukuta na mji huo kujengwa tena hakuweza kupoteza muda pale adui walipomsumbua aliomba dua awarudishie mashutumu adui zao Nehemia 4:1-5Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi. Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe. Sikia, Ee Mungu wetu; maana tunadharauliwa; ukawarudishie mashutumu yao juu ya vichwa vyao, ukawatoe watekwe katika nchi ya uhamisho;  wala usiusitiri uovu wao, wala isifutwe dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao wanaojenga.” Unaona mara moja Nehemia aliwasilisha shutuma na dharau kwa Mungu hakutaka kujibu mashambulizi kimwili, alitaka kujibu kiroho, alitaka Mungu aingilie kati mara moja, Usikawie kuingia katika uwanja wa mapambano mara moja Daniel 6: 8-10Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika. Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku. Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo”.     Unaona Biblia inataka hatua za haraka zichukuliwe mara moja ni kama vile linapotupwa Kombora kutoka katika jeshi la maadui, kutokuchukua hatua kwa haraka kunaweza kumpa nafasi zaidi ya kuleta shambulio lingine jibu mashambulizi mara moja kwa kumsihi Mungu aingilie kati haraka.

5.       Maombi yako lazima yatoke Moyoni kwa uchungu

Unapoomba maombi ya kujitakia kisasi kamwe haupaswi kuomba kwa kinywa chako tu, tunajua yako maombi unaomba kwa kusema, yako maombi unatumia ulimi, yako maombi unatumia akili kwa kutafakari, lakini maombi ya kujitakia kisasi ni lazima yatoke kwenye kiini cha uchungu wa moyo wako omba kwa kulalama, kwa kulia kwa kuugua kwa manung’uniko hii ndio inaitwa Dua, Kisasi kinaombwa kwa kilio na sauti kubwa Ufunuo 6:10Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?” Unaona! Mlilie Mungu wakati wa shida zako atakusikia.

6.       Mwambie Mungu yatosha sasa!

Ili Maombi ya kisasi yawe na nguvu lazima uonyeshe kuwa umechoshwa na hali hiyo na kuwa hapo ilipofikia adui amepitiliza mpaka, wakati mwingine uko uonevu ambao unaweza kuvumilika katika hali ya kawaida ya kibinadamu na kuwa ukichanganya na imani yetu kwa Mungu inakuwa ni rahisi kusamehe na hata kuchukuliana nalo, hata hivyo uko uonevu mwingine ni udhalilishaji na haukubaliki ni lazima tukate rufaa kwa Mungu na kumwambia Mungu hili limezidi angalia mfano huu 1Wafalme 20:1-6 Biblia inasema hivi “Basi, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya jeshi lake lote; nao walikuwapo wafalme thelathini na wawili pamoja naye, na farasi, na magari: akakwea akauhusuru Samaria, akaupiga vita. Akatuma wajumbe kwa Ahabu mfalme wa Israeli, mjini, akamwambia, Ndivyo asemavyo Ben-hadadi. Fedha yako na dhahabu yako ni zangu mimi; na wakezo na wanao, walio wema, ni wangu. Mfalme wa Israeli akajibu, akasema, Ni kama ulivyosema, bwana wangu, mfalme; mimi ni wako, na vyote nilivyo navyo. Wajumbe wakarudi tena, wakasema, Ndivyo asemavyo Ben-hadadi, Hakika nimetuma kwako kusema, Fedha yako, na dhahabu yako, na wake zako, na wanao, utanitolea mimi; lakini kesho kama wakati huu nitatuma kwako watumwa wangu, ili watazame-tazame nyumba yako na nyumba za watumwa wako; na itakuwa kila kipendezacho machoni pako watakitia mikononi mwao,na kukichukua”. Hapa unaweza kuona Dhuluma inayofanywa na mfalme Ben-Hadadi alikuwa ni mfalme mwenye nguvu na alipiga zaidi ya wafalme 30 hivyo alikuwa na uhakika wa kuwa ataivuruga Israel ya kaskazini na mji wake mkuu wa Samaria, Ingawa Ahabu hakuwa mfalme mwema lakini aliuliza ushauri kwa wazee nao walimwambia usikubali, ziko aina za uonevu ambazo hupaswi kukubali na kwamba lazima upigane kulinda Heshima yako, Lazima umwambie adui hapa imetosha sasa na umwambie Mungu aingilie Kati na kujilipizia kisasi dhidi ya udhalimu wote.

7.       Omba hukumu ya Mungu dhidi ya adui zako.

Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu anapohukumu na kukulipia kisasi hali inakuwa si ya kawaida kwa vile ni hukumu ya Mungu, Hapa muomba kisasi anapaswa kutamka namna ngumu ambayo anataka adui yake afanyiwe na Mungu ni lazima utangaze hukumu yake Biblia imejaa mifano mingi ya matamshi ya aina hii, ona Hesabu 16:1-4Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni; nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa;         nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, Bwana naye yu kati yao; n'nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa Bwana? Musa aliposikia maneno haya, akapomoka kifudifudi;” Kifungu hicho kinaonyesha wazi kuwa kundi kubwa la watu wenye sifa walikuwa wamemuasi Musa huu ulikuwa umati mkubwa sana wa uasi kupata kutokea, walimkataa Musa na Haruni, na sasa walikuwa hawako tayari kusikiliza Musa aliwaonea huruma kwa uasi wao aliwaombea na alisema nao vizuri lakini hawakusikiliza Ndipo Musa alikasirika na kuomba Dua ya kisasi hata hivyo hawakujali kwa Jeuri  Hesabu 16:15-19 Musa akakasirika sana, akamwambia Bwana. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao. Kisha Musa akamwambia Kora, Wewe na mkutano wako wote iweni hapa mbele ya Bwana kesho, wewe, na wao, na Haruni; mkatwae kila mtu chetezo chake, na kutia uvumba juu yake, mkavilete mbele za Bwana, vyetezo mia mbili na hamsini; wewe pia, na Haruni, kila mtu na awe na chetezo chake. Basi wakavitwaa kila mtu chetezo chake, wakatia na moto ndani yake, wakatia na uvumba juu ya moto, na kusimama pale mlangoni pa hema ya kukutania, pamoja na Musa na Haruni. Kisha Kora akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa Bwana ukatokea mbele ya mkutano wote”. Kutokana na Ujeuri wa Kora pamoja na Musa kuomba reheza za Mungu dhidi yao lakini waliendeleza uasi Ndipo Musa akatangaza hukumu ya kupita kawaida Hesabu 16:28-3228. Musa akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa wakifa kifo cha sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi. Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana, Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.” Unaona ! Musa aliomba na kutangaza hukumu ya Mungu dhidi ya adui zake ilikuwa lazima kiwe kitu cha tofauti ili watu wajue kuwa Musa ameitwa na Mungu, Unapoomba dhidi ya adui zako Mungu akulipizie kisasi omba hukumu ya kupita kawaida, Hanna aliyekuwa amenyanyaswa vya kutosha na Penina kwa sababu ya kukosa Mtoto,alimlilia Mungu sana aweze kuzaa mtoto na kuweka nadhiri, hata hivyo Mungu alipomjibu na kumsikiliza aliomba kwa uchungu Mungu afanye kitu, angalia 1Samuel 2:1-10Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia Bwana, Pembe yangu imetukuka katika Bwana, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako; Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani. Pinde zao mashujaa zimevunjika, Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu. Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.  Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.     Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.” Unaona Musa aliomba aridhi ifunue kinywa na kummeza wahusika, hana anaomba Bwana awapige radi, ili ijulikane kuwa Mungu ameingilia kati haiwezekani adui ashughulikiwe katika namna ya kawaida, adui atashughulikiwa kwa namna ambayo kila mtu natajua kuwa Mungu ameshughulika naye tunaweza pia kuangalia mfano wa Eliya kwa wale askari waliotumwa kumkamata ilikuwaje 2Wafalme 1: 9-15Ndipo mfalme akatuma akida wa askari hamsini pamoja na hamsini wake, wamwendee Eliya. Akamwendea, na tazama, ameketi juu ya kilima. Akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka. Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake. Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi. Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza, yeye na hamsini wake. Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako. Tazama, moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza wale akida wa hamsini wawili wa kwanza pamoja na hamsini wao; laiti sasa roho yangu na iwe na thamani machoni pako. Malaika wa Bwana akamwambia Eliya, Shuka pamoja naye; usimwogope. Akaondoka, akashuka pamoja naye hata kwa mfalme.” Hapa watu 102 wanakufa kwa neno la Eliya anashusha moto kutoka mbinguni na kuwaunguza walikuwa wametumwa kumkamata, wakati wote tunapoomba hukumu ya Mungu baadaya ya kuchoshwa na kuonewa na adui zetu hatuna budi kujitakia jambo la kupita kawaida, Lazima tuombe Mungu afanye kitun ambacho adui hata kisahau maishani mwake, unaposoma katika eneo hili unaweza kudhani kuwa sasa mkuu wa wajenzi anafundisha nini ? jambo hili sio jema labda huenda ni kinyume na injili jibu ni hapana Yesu mwenyewe alikuwa akijitakia kisasi kwa vitu vyenye maudhi dhidi yake mfano Marko 11:12-14,20-21 biblia inasema hivi, “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa. Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini. Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia., Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka.” Hebu tujiulize Yesu alikuwa anatufundisha nini kumbuka kuwa mtini huu haukuwa umemkosea Yesu neno, Ni Yesu ndiye aliyekuwa na njaa na mwandishi anatuambia wala haukuwa wakati wa tini unaona kunmbe hata wakati haukuwa wa tini Lakini kitendo cha Yesu kukosa huduma kutoka katika mti huo aliusemea maneno na mtini ulinyauka, Sio hivyo tu, Luka 23:27-31Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata, na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua na kumwombolezea.Yesu akawageukia, akasema, Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.  Kwa maana tazama, siku zitakuja watakaposema, Heri walio tasa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha. Ndipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tufunikeni. Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?” Unaona Yesu anatamka maneno kwaajili ya kizazi kile na mji wa Yerusalem wanahistoria wote wanajua kuwa maneno haya ya Yesu yalitimizwa mwaka wa 70 baada yake kitendo cha Warumi kumsulubisha Yesu kilikuwa na maana ya wazi kabisa kuwa kuwa hukumu kubwa ingekuja kutoka kwa warumi kuja kwa wayahudi walioshuhudia kuwa Yesu asulubiwe ukweli maneno hayo yaliwadhuru hata leo, Je hili sio agano jipya? Je Yesu hana uwezo wa Kusamehe? Anao lakini angalia alimuonya hata Yuda kwa kitendo cha kumsaliti alisema ole wake mtu yule atakayenisaliti ingekuwa heri kwake kama asingalizaliwa Mathayo 26:21-25Nao walipokuwa wakila, alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti. Wakahuzunika sana, wakaanza kumwuliza mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana? Akajibu akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika kombe, ndiye atakayenisaliti. Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa. Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabi? Akamwambia, Wewe umesema.” Angalia kwamba Yesu alitoa onyo kali kwa Yuda kutokana na Tendo la Kumsaliti Yesu hakukuwa na msamaha kwake, najua unaweza kusema kuwa si ulikuwa mpango wa Mungu? Tungewezaje kukombolewa ilikuwa ni muhimu Yuda atumike kumsaliti! Lakini mtu ambaye angemsaliti Yesu alikuwa na laana kali sana ambayo ilikuwa imekwisha andikwa katika zaburi hivyo kila mwanafunzi wa Yesu alikuwa na wajibu wa kukwepa kutimiza andiko hilo baya dhidi yake, lakini kwa sababu ya tamaa Yuda alipatwa na mabaya je Zaburi ilikuwa imetabiri nini dhidi ya mtu atakayemsaliti Yesu ? Angalia Zaburi ya 69 : 1-20Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamazeKwa maana wamenifumbulia kinywa; Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure.  Badala ya upendo wangu wao hunishitaki, Ijapokuwa naliwaombea. Wamenichukuza mabaya badala ya mema, Na chuki badala ya upendo wangu. Uweke mtu mkorofi juu yake, Mshitaki asimame mkono wake wa kuume. Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki, Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi. Siku zake na ziwe chache, Usimamizi wake na atwae mtu mwingine. Wanawe na wawe yatima, Na mkewe na awe mjane. Kutanga na watange wanawe na kuomba, Watafute chakula mbali na mahame yao. Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo, Wageni na wateke mapato ya kazi yake. Asiwe na mtu wa kumfanyia fadhili, Wala mtu wa kuwahurumia yatima wake. Wazao wake waangamizwe, Jina lao likafutwe katika kizazi cha pili. Uovu wa baba zake ukumbukwe mbele za Bwana, Na dhambi ya mamaye isifutwe. Ziwe mbele za Bwana daima, Aliondoe kumbukumbu lao duniani. Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamfisha mtu aliyevunjika moyo, Naye alipenda kulaani, nako kukampata. Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye, Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake.  Na iwe kwake kama vazi ajivikalo, Na kama mshipi ajifungao daima. Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa Bwana, Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.Unaweza kuona hii ilikuwa ni zaburi yenye laana yenye maombi ya kisasi dhidi ya mtu atakaye msaliti Yesu Mtume Petro alinukuu katika Matendo ya Mitume 1:20 akionyesha kuwa imeandikwa nafasi yake aitwae mtu mwingine, ilikuwa ni lazima kuepuka tendo la kumsaliti Yesu kwani lilikuwa limetamkiwa mambi mabaya sana lakini kutokana na kiburi na ukaidi ndanin ya Yuda laana hii ilimpata Yesu alitakiwa au huenda aliiomba hii na ndio maana alionya mtu yuleatakayemsaliti, Ndugu Biblia imejaa fundisho hili la kujitakia Kisasi kwa Bwana.

8.        Tangaza hukumu na kisasi dhidi ya adui zako.

Biblia imejaa mafundisho ya kutosha namna ya kujitakia kisasi kwa Bwana sio tu  kwamba utaomba kisasi dhidi ya adui zako lakini pia unaweza kutangaza au kutabiri namna adui yako atakavyoshughulikiwa matamshi haya yanafanyika kwa imani na uchungu na katika uwepo wa Roho Mtakatifu angalia mfano wa uasi wa Abimeleki na jinsi Yonathan nduguye alivyomtangazia hukumu yake Waamuzi 9:1-6Abimeleki, mwana wa Yerubaali, akaenda Shekemu kwa ndugu za mama yake, akanena nao, na wote waliokuwa wa nyumba ya baba ya mama yake, akasema, Haya, neneni tafadhali masikioni mwa waume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo jema kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini, watawale juu yenu, au kwamba mtu mmoja atawale juu yenu? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu. Hao ndugu za mama yake wakanena habari zake masikioni mwa hao watu wote wa Shekemu maneno hayo yote; na mioyo yao ikaelekea kumwandama Abimeleki; kwa kuwa walisema, Huyu ni ndugu yetu. Wakampa vipande vya fedha sabini vilivyotoka katika nyumba ya Baal-berithi, na kwa fedha hizo Abimeleki akaajiri watu wapuuzi mabaradhuli, wafuatane naye. Kisha akaenda nyumbani kwa babaye huko Ofra, akawaua nduguze, hao wana wa Yerubaali, watu sabini, akawaua juu ya jiwe moja; lakini Yothamu, mwana mdogo wa Yerubaali, alisalia; kwa maana alijificha. Kisha hao watu wote wa Shekemu wakakusanyika pamoja, na jamaa yote ya Milo, wakaenda na kumtawaza Abimeleki awe mfalme, karibu na huo mgandi ulio karibu na ngome iliyo katika Shekemu.” 

Unaweza kuona kitendo kiovu kilichofanywa na Abimeleki aliwaua ndugu zake ili apate kutawala yeye nduguze walikuwa wapata sabini aliwaua katika jiwe moja, Lakini nduguye mmoja Yothamu aliokoka kwa kukimbia Yothamu alishuhudia nduguze wakiuawa na alielezwa hatuoni kuwa Yothamu alikuwa nabii hapana lakini kwa vile kilichotendeka sio haki alitabiri alitangaza kisasi cha Bwana dhidi ya Abimeleki na watu wa shekemu angalia Waamuzi 9:7-21Kisha walipomwambia huyo Yothamu, yeye akaenda, akasimama juu ya kilele cha kilima cha Gerizimu, akapaza sauti yake, akapiga kelele, na kuwaambia, Nisikieni mimi, enyi watu wa Shekemu, ili kwamba Mungu naye apate kuwasikia ninyi. Siku moja miti ilitoka ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti mzeituni, Tawala wewe juu yetu. Lakini huo mzeituni ukaiambia, Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu wamheshimu Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti?  Kisha miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu. Lakini huo mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende nikayonge-yonge juu ya miti? Kisha miti ikauambia mzabibu, Njoo wewe, utawale juu yetu. Huo mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti? Ndipo hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu. Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu kwelikweli, basi njoni mtumaini kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni. Basi sasa ikiwa mmetenda kwa uaminifu na uelekevu, katika kumtawaza Abimeleki awe mfalme, na ikiwa mmemtendea mema Yerubaali na nyumba yake, na kumtendea kama ilivyostahili mikono yake; (kwa maana baba yangu aliwatetea ninyi, na kuhatirisha uhai wake, na kuwaokoa na mikono ya Midiani; nanyi mmeinuka juu ya nyumba ya baba yangu hivi leo nanyi mmewaua wanawe, watu sabini, juu ya jiwe moja, nanyi mmemtawaza Abimeleki, mwana wa kijakazi chake, awe mfalme juu ya watu wa Shekemu kwa sababu yeye ni ndugu yenu;)   basi ikiwa mmemtendea kwa uaminifu na uelekevu Yerubaali na nyumba yake hivi leo, basi furahini ninyi katika huyo Abimeleki, yeye naye na afurahi kwenu ninyi;  lakini kwamba sivyo hivyo, basi, moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo; kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na kumteketeza Abimeleki. Kisha Yothamu akaenda zake na kukimbia, akaenda Beeri, na kukaa kuko, kwa kumwogopa Abimeleki nduguye”. Unaweza kuona Yothamu alitangaza hukumu hii, hii ilikuwa ni namna ya kutangaza kisasi au hukumu kwa tendo lisilo la haki na je tangazo hili lilitimizwa? Angalia  Biblia inasema hivi Waamuzi 9:50-57Ndipo Abimeleki alipokwenda Thebesi, akapanga kinyume cha Thebesi na kuutwaa. Lakini ndani ya huo mji palikuwa na buruji yenye nguvu, na watu wote waume na wake wakakimbilia huko, na watu wote wa mji, nao wakajifungia ndani, wakapanda paa la buruji. Abimeleki akaiendea hiyo buruji na kupigana nayo; naye akaukaribia mlango wa buruji ili auteketeze kwa moto. Na mwanamke mmoja akabwaga jiwe la kusagia la juu, nalo likampiga Abimeleki kichwani, na kulivunja fuvu la kichwa chake. Ndipo akamwita kwa haraka huyo kijana aliyekuwa anamchukulia silaha zake, na kumwambia, Futa upanga wako, uniue, ili watu wasiseme juu yangu Aliuawa na mwanamke. Basi huyo kijana wake akamchoma upanga, naye akafa.      Basi hapo watu wa Israeli walipoona ya kuwa Abimeleki amekufa, wakaondoka wakaenda kila mtu mahali pake. Basi hivyo Mungu akalipiza kisasi juu ya uovu wa Abimeleki aliomtenda baba yake, katika kuwaua hao nduguze watu sabini; uovu wote wa watu wa Shekemu Mungu alilipiza juu ya vichwa vyao; na hiyo laana ya Yothamu mwana wa Yerubaali ikawajilia juu yao.”

Ni wazi  kuwa Mungu ameweka nguvu ya ziada katika kinywa chako unapotendewa jambo lisilo haki unaweza kutangaza namna Bwana anavyoweza kukulipia kisasi au kushughulika na adui yako, ni vigumu kunukuu kila andiko ili upate kusadiki lakini nitanukuu mfano wa Daudi kwa Goliath ambao wote walitamka laana na kutangaziana hukumu kwa vinywa vyao na kila mtu kwa jina la Mungu wake ni wazi kuwa Mungu wa Israel aliye hai alijilipizia kisasi kwa vile mfilisti alikuwa amawatukana Israel nah ii ilikuwa ni sawa na kumtukana Bwana, awaye yote anayekudharau na kukutukana na kukuonea na kukulaani huku wewe unamtegemea Mungu aliye hai anajitafutia gharama za kulipa 1Samuel 17:43-47Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake. Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni. Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.” Unaona ni mapenzi ya Mungu kumtangazia adui yako namna atakavyomalizika ajijue wazi afahamu mwisho wake utakavyokuwa mtamkie kwa uchungu na maumivu mengi na katika upako na wivu wa Mungu wetu naye Bwana atalitimiza neno lako.

9.       Mpe ishara ya kumtia Nidhamu!

Wakati mwingine ni vigumu watu wakorofi na jeuri kukumbuka kwamba yanayowapata yametokana na adhabu maalumu kutoka kwa Bwana kupitia wewe na hivyo kumtangazia hukumu ambayo yeye haijui, hajaisikia na hana dalili kunaweza kuwa kwenye mafanikio madogo ya kujua kuwa anatengenezwa kwa sababu ya ujeuri wake hivyo ni muhimu wakati mwingine kutangaza wazi kuwa ishara hizi zitampata ili atambue kuwa wapi alikosea na kwaajili ya nini anapatwa na yanayompata hata kama ni kutoka moyoni angalia kwamfano  Matendo ya Mitume 13: 6-12 Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana”. Ni wazi kuwa mchawi huyu alipata adhabu ya kuwa kipofu kwa muda Paulo mtume alitumia mamlaka yake ya kitume ana kitumishi kumshikisha adabu mtu ambaye alikuwa akizuia kwa uchawi mkuu wa mkoa asiokoke kwa kuisikia injili, kumtia nidhamu huku kulifanya Liwali yaani mkuu wa mkoa aokoke na wale waliolionatukio waliamini na kumpa Bwana utukufu.

10.   Hakikisha unalia kwa Uchungu.

Maombi ya kujitakia kisasi ni maombi yanayojumuisha uchungu na kulia au kulia kwa uchungu kisasi hakiombwi kavukavu kinaombwa kwa kilio, Mungu huwajibika anaposikia kilio angalia kilio cha Habili kwa nduguye aliyedhulumu uhai wake Kaini kilisababisha adhabu na laana kubwa kwa Habili Mwanzo 4:8-12 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.” Unaona kilio cha uchungu kina maana kubwa sana Daudi alikuwa anaifahamu siri hii waziwazi hivyo mara kadhaa katika Zaburi zake alikuwa akilia kwa uchungu mfano katika Zaburi 5:1-2 “Ee Bwana uayasikie maneno yangu, Ukuangalie Kutafakari kwangu. Uisikie Sauti yangu ya kilio change, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana wewe Ndiwe nikuombaye.” Mungu huyaangalia machozi na uchungu kwani ni muhimu kuomba na kuonyesha hisia za kuumizwa kwetu na ndipohaki yetu itapatikana, Kumbuka Yesu alisema hivi katika Luka 18:7Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake WANAOMLILIA mchana na usiku,naye ni mvumilivu kwao?”  Unaona ni wazi Yesu anakubaliana nasi kuwa sio maombi ya kawaida yanatumika pale unapotaka haki bali ni maombi ya kulia, ni kulia ndiko kunakoweza kuleta  mageuzi makubwa dhidi ya mipango mibaya ya adui dhidi yetu.

11.   Tumia silaha ya sifa!

Ni muhimu kufahamu kuwa kuna siri ya ziada katika kumsifu Mungu, sifa zina tabia ya kuwasambaratisha maadui zetu, ushahidi wa kibiblia, mara moja adui wanapokushambulia hakikisha kuwa unamwimbia Mungu na kumtukuza na kumsifu hii ndio ilikuwa silaha kubwa ya Daudi, katika agano jipya maandiko yanaonyesha Jinsi Paulo na Sila walivyoweza kufanikiwa kuwasambaratisha maadui kwa kutumia sifa Matendo 16:22-26 “Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora. Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.”
Aidha wote tuna kumbuka jinsi Mji wa Yeriko ulivyoangushwa kupitia kumsifu Mungu, Yoshua 6:1-5, Israel walipiga kelele baada ya matarumbeta na kupitia agizo hili kuta za mji wa Yeriko zilianguka na  wakaweza kuteka mateka na kuwashambulia adui, Njia hii ni ya kujipatia ushindi pia.

12.   Tangaza laana kwa wanaokulaani

Tunayo ahadi ya kudumu kutoka kwa baba yetu wa imani Abrahamu, Mungu Baba yetu alipomuita Ibrahimu baba aliahidi kuwa ngao kwake na alimpa ahadi ya ulinzi na usalama na kwamba yeye anauwezo wa kuwa chanzo cha Baraka lakini vilevile kusababisha laana kwa watakao mlaani Mwanzo 12:1-3BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”. Unaona ahadi hii inatuhusu moja kwa moja inukuu na kumkumbusha Mungu na mara unapoanza kutamka laana dhidi ya adui yako kupitia ahadi hii Mungu anaanza kulifanyia kazi kwa kulipa kisasi.

13.   Omba kwa kunena kwa Lugha kwa Muda mrefu.

Tuko vitani katika hali ya kawaida vita za duniani majemadari huwa wanawasiliana kwa kutumia lugha za mficho ili adui asije akagundua, ni muhimu kunena kwa lugha kwa muda mrefu sana aidha pia unaweza kuitumia Damu ya Yesu na ushuhuda yaanineno lake na kumkumbusha Mungu yalke ambayo amewahi kukutendea na jinsi alivyoweza kukupa ushindi katika vita mbalimbali,Ufunuo 12:11Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.” Pia unaweza kutumia nadhiri na utoaji wa sadaka maalumu kwaajili ya kuwashughulikia adui zako.

14.   Fuata nyayo za Daudi

Daudi alikuwa ndio kiongozi Bora zaidi aliyekuwa na mafanikio makubwa sana dhidi ya adui zake alifanikiwa katika kila vita na hakuwahi kushindwa vita Yesu alitumia mamlaka ya daudi katika uanadamu wake Ufunuo 3:7Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.” Daudi alikuwa mtu aliyeupendeza Moyo wa Mungu, alikuwa na upako wa kinabii,upako wa kifalme na upako wa kishujaa, alijaa sifa na ibada aliabudu kwa upako na uwepo, alikuwa muombaji, alikuwa na upako wa kikuhani, alikuwa na upako wa kuokoa watu, alikuwa na ujuzi wa vita, alimpiga Goliath, aliwapiga wafilisti mara kadhaa,Hajawahi kushindwa vita, hivyo ni muhimu sana kujifunza utendaji wake na maisha yake katika swala zima lamaombi ya kujilipia au kujitakia kisasi kutoka kwa Bwana.

Pale unapolazimika kujitakia kisasi!
Ni nyakati gani tunalazimika kujitakia kisasi? Ni pale tunapokutana na changamoto mbalimbalia kama ilivyokuwa kwa muombaji maarufu wa kisasi yaani Daudi, utahitaji kujiombea kisasi kwa Bwana katika sababu kadhaa zifuatazo.
Ø  Ni pale unapokuwa na adui mwenye kutisha kama goliath, au unapokuwa na mtu mwenye nguvu anayekutafuta kama ilivyokuwa kwa Sauli aliyekuwa akimtafuta Daudi apate kumuangamiza, Kama Daudi utaomba maombi kama yake kwa vile u mfalme lakini bado unaishi kama mtumwa.
Ø  Utahitaji maombi ya kujitakia kisasi unapokuwa wewe ndiye lengo la Adui au unapokuwa umezingirwa na mtandao wa wachawi au unapokuwa umezingirwa na wimbi la majaribuna umezama katika dimbwi la taabu na shida.
Ø  Unapotaka kurekebisha maisha yako ya baadaye, unapozingirwa na hatari za kifo, unaposumbuliwa na magonjwa na kufanya kazi kwa bidii bila kupata maendeleo, taabu mbalimbali zinapojitokeza na ukaanza aina hizi za maombi taabu huanza kujitokeza katika kambi ya maadui zako, Maadui wanaweza kuinuka na kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe, wakati wote kumbuka kuwa kila unapotaka kujitakia kisasi kwa Bwana basi maombi ya Daudi katika zaburi ni ya muhimu sana kuyatumia, unapoanza kuomba aina hii ya maombi adui wanaanza kukosa amani.
Ø  Pale unapoomba njia yao iwe giza ukweli ni kuwa wanaanza kuchanganyikiwa na kukosa namna ya kufanya na hatimaye wataangamia, Mungu unapomuomba awapige kofi awavunje taya maana yake wataanza kukosa maneno ya kusema na maneno yao wanayotamka juu yako yatashindikana kutimia, kuvunja meno yao pia ina maana ya kuharibu kila aina ya silaha wanazozitumia, kwa hiyo kila mara unapotaka kujitakia kisasi kwa Bwana omba kama mwandishi wa zaburi.
Jinsi ya Kuomba Maombi ya kujitakia kisasi kwa Bwana !
1.       Lazima wewe mwenyewe utubu
2.       Acha kuwa adui wa Mungu
3.       Fanya urafiki na Mungu mwenyezi
4.       Jitenge na ulimwengu wa dhambi, usifanye dhambi
5.       Jiandae kwa vita dhidi ya maadui zako wote
Mambo ya kuombea.
1.       Ee Bwana kilio changu kikufikie na unipe msaada wa malaika zako leo katika jina la Yesu
2.       Ee Bwana nipe jina litakalokuwa Baraka kwangu leo katika jina la Yesu
3.       Ee Bwana kila vizuizi vya yule mwovu,na mipango yake yote kinyume name na malaika wangu viunguzwekwa moto katika jina la Yesu
4.       Ee Bwana unilinde mimi mtumwa wako na mawe yote ya kishetani ninayotupiwa na wanaonichukia katika jina la Yesu
5.       Kila aina ya uasi dhidi yangu ukaaibishwe katika jina la Yesu
6.       Uniokoe mimi na keleleza Shetani katika jina la Yesu
7.       Uniokoe na watu nwabaya na wenye nia mbaya katika jina la Yesu
8.       Kila mwenye kunikusudia mabaya atawanywe na kutupwa katika nchi ya upweke katika jina la Yesu
9.       Nakushukuru kwa kunisikia maombi na dua yangu
Jinsi ya kuharibu Ngome za adui.

Ni muhimu kufahamu kwamba Biblia ni kitabu cha vita! ni kitabu cha kijeshi, unapoifungua Biblia na kuanza kupitia ukurasa mmoja hadi ukurasa mwingine hata mwisho utagundua kuwa imejaa misamiati ya kijeshi na vita
Katika 2Wakoritho 2:11 Biblia inasema “Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Neno Fikra katika biblia ya kiingereza linatumika neno “Schemes” ambalo maana yake ni Mipango au miakakati inayopangwa na adui kwa kusudi lakukushinda katika vita  kwa msingi huo basi ni muhimu kwa kila mmoja anayataka kujilipizia kisasi kutoka kwa mBwana kukumbuka kuwa tuko vitani na adui ana hila kwa msingi huo ni lazima tufahamu kwanza lugha za kivita ili tunapoingia katika ulimwengu wa roho kutangaza hukumu au kutamka kisasi dhidi ya adui na kujilipizia kisasi ni kwa sababu hii biblia imetupalugha nyingi za kivita

Biblia inatumia neno Kushindana mieleka (wrestle) hii ni kama inaashiria kuwa ziko vita za ana kwa ana ni mapambano yenye kutumia nguvu na akili na ni lazima umshinde adui yako, pia kuna neno kushambulia au kuvamia Smiting, kuna neno kama kukatilia mbali Slaughter na kutokubali kupinga strife na kadhalika haya yote yanazungumzia mapambano ya kivita, Biblia pia inazungumzia kuwashinda maadui, kuvukuza, kuchukua mateka, kuzuia, kufukuza majeshi ya aduim kuzima,kuepuka,kushambulia kumtupa chini adui n.k. hizi nilugha za kivita Waefeso 6:12-18Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.     
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.      Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;”

Historia ya mwanadamu imefunikwa na vita tu, Biblia inafunua kuwa hata malaika mbinguni wamewahi kupigana vita, Katika ufunuo tunaambiwa kuwa Mikael na malaika zake wakapigana na lile Joka  na kumshinda, kwa msingi huo unapozungumza kuhusu vita ni lazima waweko majemadari wa vita na ndio wapiganaji, Vita sio kitu cha kimyakimya, unapoingia vitani kupambana unashambulia ngome za maadui, unajishughulisha na ngome na ndio maana biblia inatumia lugha za kivita katika kututia moyo kusonga mbele kwa gharama yoyote

Kama shetani atamshambulia mwanadamu na kuweka vikwazo kiasi kwamba kikwazo hicho kikamfana mwanadamu kushindwa kuendelea mbele hilo ni shambulizi na ni ngome imewekwa dhidi yako, Shetani anapopanga mipango na ikawa inafanikiwa dhidi yetu huo ni uvamizi,ni kikwazo tayari ni jambo ambalo litakuwa limewekwa na shetani ili kutuzuia, Zaburi 124:6-8 inasema “Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.” Mtego unaotajwa hapo ni hila na mipango ya shetani  na maajenti wake kutuhusu sisi na hutokea hasa tunapokuwa vitani, ni mpaka uwe na ujuzi wa kujitoa katika mipango hiyo ndipo unapoweza kuwa huru

Ngoja nikuambie Ndugu kuna mikakati mingi ya shetani mibaya kukuhusu katikamaisha yako lengo kuu likiwa ni kuharibu kabisa maisha yako

Kijana mmoja ambaye anatokea katika familia masikini sana, na ni yeye tu aliyekuwa wa kwanza kufanikiwa kwenda Chuo kikuu katika Familia yao, alikuwa na mtihani wa muhimu wa kumalizia mtihani huu ulikuwa ndio uamue hatima yake na kuleta faida katika familia yao na mpenyo katika maisha yake,kijana alijisomea kwa bidii sana wiki ile na wakati mwingine hakulala, siku moja  ambayo kesho yake ilikuwa ndio ya mtihani alijitahidi usiku kucha kwaajili ya kujiandaa na kisha asubuhi pia alijiandaa dakika chache sana kabla ya mtihani alisoma kupitiliza mpaka akawa amechoka, siku ile ya mtihani ikiwa imebaki saa moja tu kabla ya kuingia katika chumba cha mtihani ambako angetembea kwa dakika tano tu kutoka chumbani kwake alijisemea njoja apumzike kidogo kama dakika kumi na tano hivi, akiwaamepumzika jambo laajabu alikuja kushituka usingizini mtihani aliokuwa amejiandaa ulikuwa umeisha na hivyo alilazimika kurudia mwaka mzima kwaajili ya mitihani hiyo na alipokuja kurudia mwakani alifeli na ndoto ya mafanikio yake na familia yake ilikuwa imeishia hapo, Mambo kama haya ndugu ni mashambulizi ya kishetani.

Miaka kadhaa nyuma binti mwenye miaka 37 alipata Mchumba wa kumuoa na uchumba ukaendelea ikiwa imebaki wiki moja tu waoane kijana akasema hajisikii tena kumuoa mwanamke huyo kwa sababu ni mfupi na amesikia kuwa watu wafupi ni wajeuri na wakorofi, alipofikisha miaka 39 alipata mtu mwingine aliyekuwa anataka kumuoa maandalizi yaliendelea ikiwa imebaki wiki moja tu kabla ya harusi yao kijana aligongwa na basi lililokuwa limeacha njia na kufa papo hapo, alipofikisha miaka 41 alipata mchumba mwingine maandalizi yaliendelea na siku ya harusi ilifanikiwa ikafika saa ya ibada wakati Mtumishi wa Mungu anuliza nani mwenye kizuizi kwa watu hao wasioane alijitokeza mwanamke na kujitambulisha kuwa anayeoa ni mume wake wa halali! Hiki ninini ?

Ni mashambulizi mkaubwa ya shetani kwa mwanamke huyu, Ndugu kuna mapambano kwaajili ya maisha yako na mafanikio yako, kuna mikakati maalumu ya kishetani inawekwa kwakko kukuumiza, kukufanya ukate tamaa, kukufanya uwe na nuksi, kukufanya ukataliwe, kukufanya usizae, kukuharibia kazini, kukufanya udhoofike, kuna mashambulizi ya kishetani, kuna mashambulizi ya kichawi hizi zote ni ajenda za shetani kuharibu kabisa maisha yetu, kuna mambo ambayo sio ya kawaida yanaendelea katika maisha yetu ambayo sio ya kawaida lazima tupambane na kujitafutia kisasi kwa Bwana !

1.      Kuna wala nyama na wanywa damu za watu wanaweza kuweka mikosi katika maisha ya watu
2.      Kuna nguvu za giza na kichawi
3.      Kuna mizimu katika koo za watu mbalimbali zenye kuwadhuru
4.      Kuna dini za kichawi
5.      Kuna roho chafu majini na mapepo
6.      Kuna roho chafu za umasikini na ukandamizaji wa kila aina
7.      Kuna maswala ya kurithi yananayoweza kuathiri familia
8.      Kuna majina uliyopewa ambayo yanaweza kubeba mkosi katika maisha yakom Mfano mtu anayeitwa ayubu maana yake Achukiwe, Isabela maana yake chungu cha uchawi cha porini, Rebecca maana yake ngombe mdogo,Yoel maana mbuzi wa mlimani lazima ulipitie jina lako na kuliangalia kama linamchango gani katika maisha yako, Kumbuka kama shetani atakupaka na nuksi hizo rafiki zako watakukimbia na wale wote wanaotakiwa kutoa msaada wakati unashambuliwa na shetani wanakimbia mbali au wanageuka kuwa maadui, Unaweza kuota ndoto mbaya, utasumbuka na unashangaa hufanikiwi, utawaota hata waliokufa, unaweza kusikia sauti za ajabu ajabu, ni kwa sababu hii ni lazima kufanya kila linalowezekana kuondoa uvamizi huo wa ibilisi katika maisha yetu, Nuksi na mikosi ya kivamizi kutoka kwa shetani inaposhughulikiwa vilivyo unaanza kuwa na shuhuda katima maisha yako, utaanza kuona miujiza ya ajabu ikijitokeza katika maisha yako na mambo mazito yataanza kuwapata waliokuwa wakikusakama katika maisha yako!

Jinsi ya kuharibu Ngome za kivamizi za shetani

·         Yakabidhi maisha yako kwa Yesu
·         Tubu kila aina ya dhambi unayoikumbuka na usiyoikumbuka katika maisha yako, dhambi ina tabia ya kumpa adui nguvu za kukushambulia
·         Tambua kila aina ya uvamizi wa kishetani katika maisha yako
·         Tangaza vita na kulia kwaajili ya uvamizi dhidi yako.

Jinsi ya kuomba.

·         Mikosi kutoka kwa ukoo wa Baba yangu na mama yangu dhidi yangu na dhidi ya maisha yangu nakuharibu katika jina la Yesu
·         Malaika wa giza ambao mnazuia maombi yangu, nawatawanya na kuwasambaratisha katika jina la Yesu
·         Nguvu za shetani zilizotumwa kinyuime na nyota yangu, kuififisha, nakuua katika jina la Yesu
·         Kila aina ya mwizi, katika maisha yangu, huna mamlaka dhidi ya maisha yangu nakuua katika jina la Yesu
·         Mapanya ya kishetani, wanaokopera na kuniibia lisikie neno la Bwana muda wako umekwisha nakuua kabisa katika jina la Yesu
·         Kila nguvu ambayo imetumwa kwangu, kunipotezea muda na kunipotezea mavuno yangu nakumaliza katika jina la Yesu
·         Ndege wachafu wanaoruka kinyume name katika jina la Yesu kristo nakusambaratisha
·         Kisha chukua muda wa kumshukuru Mungu kwa imani katika maombi

Jinsi ya kungoa Pando asilolipanda Baba wa Mbinguni.

Mapando ya shetani yako kila mahali duniani, shetani amekusudia kuharibu kila Nyanja ya maisha ya watu wa Mungu na kwa sababu hiyo unapaswa kuwa na ujuzi huu ili utamke kisasi kwaajili ya kila eneo ambalo limepadwa mbegu mbaya na kungoa mbegu hiyo mbaya katika jina la Yesu. Mathayo 13:24-30Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo.  Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.” Unaona shetani anaweza kupanda taabu katika kila eneo la maisha yako ni muhimu kutambua mambo ya kawaida ya yasiyo ya kawaida tusimkubalie kabisa shetani kufanya anayotaka kuyafanya katika maisha yetu katika Jina la Yesu.

Uwe na hasira takatifu!

Ni muhimu kufahamu kuwa ulimwengu unazidi kuwa na uovu siku hadi siku,na ufalme wa giza unajipanga kuharibu maisha ya watu siku hadi siku, ni lazima sasa kuwakabili manabii wa baali na majeshi yake yote bila huruma, lazima kuitumia mamlaka yetu kwa viwango vya juu mpaka watuogope, Ni wakati wa kukabilia na na kila aina ya vitisho vya ibilisi na kuwatamkia maneno magumu yeye na watumishi wake au awaye yote ambaye wakati huo anatumika kama chombo cha shetani ni wakati wa watu wa Mungu kujitokeza na kuutisha ufalme wa giza na kuwanyamazisha na kuondoa maneno na matendo yao ya vitisho! 
Ili tufikie ngazi ya kuyafanya hayo ni lazima kuwa na hasira takatifu, uwe mgumu na ikiwezekana kuwa na vurugu za kiroho ili pale wanaposema kuwa hakuna njia sisi ndio tunapita, pale wanapodhani kuwa hakuna ushindi sisi tunakuwa nao, na nilazima tuwe washindi kwani Yesu mwenyewe ni mharibifu wa Uovu Biblia inasema kwa maana “alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi” 1Yohana 3:8Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi

Nguvu za Mungu hazina mipaka, Ni Mungu habadiliki ana nguvu zote omnipotent hajawahi kushindwa na hatawahji kushindwa ni mkuu na matendo yake ni makuu ni zaidi ya utoshelevu, nimkuu sana atafanya mambi makbwa ya kutisha na kushangaza katika maisha yetu, Mungu alipomtuma Saul kuwauwa waamaleki maelekezo yake yalikuwa wazi tu kuwa asibakize hata mmoja auwe hadi wanyama Biblia inasema sasa shoka limewkisha kuwekwa tayari kila mti usiozaa matunda utakatwa na kutupwa motoni.

Angamiza kabisa.!
Baada ya mti kukatwa kumbuka kuwa unaweza kutumika kwa kutengenezea vifaa na fanicha za majumbani na kadhalika, pia inaweza kutumika kama kuni na kupikia chakula agizo linataka kuteketeza kabisa kwa sababu hiyo chochote kile ambacho kinaweza kuchangia haribiko lako kinafaa kuharibiwa kabisa, chochote ambacho hakitaki wewe uwe na furaha maishani mwako na nguvu yoyote inayotaka kukuletea mauti haistahili kuishi adhabu yake ni kuharibiwa kabisa.

Kumbukumbu la torati 13: 6-11 Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako; katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia; usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche; mwue kweli; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote. Nawe mtupie mawe hata afe; kwa kuwa alitaka kukupotoa na Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.   Na Israeli wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako.

Mungu anataka ufutilie mbali kila kinachosimama kinyume nawe, ukiue kabisa kila kinachopingana nawe na kukifutilia mbali milele, yeyote anayetaka kukuua hastahili kuishi pia Mungu anapokomesha adui humkomesha milele

Maandiko yanarekodi habari za uadui wa kudumu kati ya Isarael na waamaleki, Mungu aliamuru na kuelekeza Israel kuhakikisha kuwa wanawafutilia mbali waamaleki na kuwaondoa kabisa juu ya uso wa dunia angalia Kutoka 17:8-13 Biblia inasema “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.   Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.” Unaweza kuona kuwa Bwana aliapa kuwa atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi kwa nini nitakueleza baadaye tuongeze maandiko mengine zaidi kuhusu Amaleki
1Samuel 15:2 Biblia inasema “Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.” Unaweza kuona kwa nini amri  ya Mungu inakuwakali sana kwa waamaleki na kwa nini Mungu anataka waangamizwe kabisa wao na kila kitu walichokuwa nacho na mpaka mifugo yao? Kwa sababu waliwapinga wana wa Israel njiani walipokuwa wakitoka Misri, tuone maandiko zaidi Kumbukumbu la Torati 25:17-19 Biblia inasema haya Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri; jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahauUnaona Musa naye anakazia kwamba Israel asisahau kuhusu Amaleki na matendo yasiyo ya Huruma aliyoyafanya Israel wakati Israel wakiwa wamechoka wanatoka Misri, wakiwa na kiu wakiwa wanyonge Amaleki walifanya jambo la kuhuzunisha hawakumuogopa Mungu waliwapinga Israel Jangwani? Ni kwa sababu ya jambo hili Mungu aliweka kinyongo na Ameleki aliweka Kisasi cha milele alisema ni lazima waharibiwe kila walichonacho wasiachiwe uhai watokomezwe kabisa

Unyama wa amaleki dhidi ya Israel ndio uliomfanya Mungu awakumbushe Israel kila wakati kuhakikisha kuwa wanakifuta kizazi hiki duniani unaona ni mapenzi ya Mungu kuwaangamiza adui zako kabisa bila kusaza, wakati mwingine wewe uko katika dhiki,na safari ya Jangwani badala ya mtu kugeuka kuwa msaada mkubwa kwako anakuwa adui kwako anakudhalilisha akipingana na Mungu. Na mapenzi ya Mungu katika maisha yako Mungu anaamuru usibakize jina  la amaleki juu ya uso wa dunia wafutwe kabisa na hapo ndipo utakapokuwa huru kwelikweli usisahau! Mungu alionyesha msisitizo.

Maombi ya kusambaratisha

Vifungu hapo juu vimetufundisha jinsi ya kushughulika na adui na uovu wake kama ilivyo mbele za Mungu, kila mwenye kusikia na asikie kuna maombi ya kujenga lakini vilevile kuna maombi ya kuharibu, kuna ya kupanda na kuna ya kung’oa, Mungu alimwambia Yeremiah nimekuita Yeremia 1:8-10 “angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda  Unaona! Mwandishi wa Zaburi anasema Mara watakapoisikia sauti yangu watanitii, wageni watainama wenyewe mbele zanguunaweza kuona vilevile unapoisoma biblia vema hususani kuhusu habari za Yesu utaweza kuona  na kushangaa Yesu akizungumza na magonjwa kama uziwi, ukoma, upofu, dhuruba, mti, magonjwa na maiti, maneno anayoyatumia ni kama Funguka, Tulia, toka, inuka uende, na kadhalika kumbe basi Mungu anataka kila kitu kitamkiwe kulingana na uharibifu kiliosababisha kila nguvu ya uharibifu inahitaji maombi ya kuharibu na kusambaratisha, “Kwa maana mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisiNi lazima tubadilishe mtazamo wa maombi yetu na kuzungumza uharibifu kwa kila kinachotaka kutuharibu, umefika wakati sasa watu wa Mungu kuachana na unyonge  na kusimama na kukabiliana na kila hali ya uovu, na unajua kuwa kuna maeneo mengi sana shetani amefanikiwa kupanda kila mbegu ya uovu na hatuna budi kuyango’a mapando hayo kwa mamlaka tuliyopewa na Mungu.

Sifa za maombi ya kusambaratisha kila pando lililo ovu!
1.      Lazima kufanya maombi yenye usumbufu na magumu yasiyo ya huruma huruma
2.      Maombi yenye kuamuru na kudai haki
3.      Maombi yasiyo na mashaka
4.      Maombi ya kutamka laana za kiungu
5.      Maombi ya kinabii yenye matamsi ya kumshughulikia adui katika ulimwengu wa kiroho kama daudi alivyomtamkia Goliath
6.      Maombi yenye kuhoji nani ewe mlima mkubwa na kuusambaratisha
7.      Maombi yenye kuzungumza na tatizo moja kwa moja na kulikemea
8.      Maombi yanye kutimiza makusudi ya Mungu
Kumbuka unapokuwa umeanza aina hii ya maombi ya kusema na vitu au watu watu wanaweza kufikiri kuna tatizo ndani yako, kuna shida unapotabiria vitu watu wanaweza kudhani kuwa wewe ni kichaa, lakini usiwajali endelea unaweza kuwekea mikono hata mashine na kuondoa roho mbaya ndani yake!

Maombi ya kungoa Pando asilolipanda baba

Ni lazima uwe na maombi ya kungoa kila pando asilolipanda Baba katika maisha yako kila siku, lakini ni lazima uwe umempokea Yesu, ni lazima uyachunguze maishga yako na kuangalia kimwili na kiroho na usiruhusu lolote lisilo la kawaida liwe la kawaida katika maisha yako, angalia kama ni kutokana na uasi na dhambi, kisha yango’oe Biblia inasema kila pando asilolipanda baba yangu wa Mbinguni litamgo’lewa. Utaanza kuona utamu wa kuwa na Mungu tangu sasa.

Mambo ya kuombea wakati wa kungo’a
1.      Pando lolote la giza katika maisha yako life katika jina la Yesu
2.      Pando lolote la mauti katika maisha na ukoo wangu life katika jina la Yesu
3.      Pando lolote na shambulizi lolote dhidi yangu life katika jina la Yesu
4.      Narudisha kule yalikotoka kila aina ya mashambulizi ya ibilisi
5.      Mungu wa kisasi kama Mungu wa Eliya jitokeze na ujidhihirishe katika jina la Yesu
6.      Zika dhambi zangu na maanguko yangu yote katika jina la Yesu
7.      Kila pando na nguvu zinazozuia nisiendelee life katika jina la Yesu
8.      Mikono yangu na iwe shoka la  vita vya Bwana katika jina la Yesu
9.      Damu ya Yesu ingoe’ kila muhuri niliogongwa nisiendelee katika maisha yangu katika jina la Yesu
10.  Mungu usimame na kuwa aibisha adui zangu katika Jina la Yesu.
11.  Asante Bwana kwa kunijibu maombi yangu katika jina la Yesu.

Silaha za mapambano.

Mapambano katika maisha ni jambo lisiloepukika uwe unataka au hutaki, Adui yetu shetani amejipanga kwa vita ana majeshi ya vita na silaha za vita, kwa msingi huo tunahitaji silaha za nguvu kuweza kupambana naye silaha utakazojifunza hapa zitakupa somo ambalo hutalisahau maishani mwako, Shetani anatumia silaha nzito na mbaya za kutisha lakini tutazichambua na kuzibainisha na mara utakapokuwa umezibaini utasimama kwa ushindi na kutangaza kuwa Hakuna kazi ya kufanya

1.      Risasi za rohoni: swala la mtu linapochukuliwa katika ulimwengu wa giza haraka nsana wanatafutwa watu wa familia ya mtu yule wenye nguvu za giza, Kadiri kunavyokuwa na watu wengi wenye nguvu za giza katika familia ya mtu ndivyo na shambulizi la mtu huyo linakuwa baya zaidi, habari zote ambazo adui anazitaka zitakuwa zinatolewa na wanafamilia, na hapo ndipo roho ya mtu huyo inapoweza kushambuliwa na hata kumfanya mtu huyo asiamke tena, unaweza hata kuota umepigwa risasi katika ndoto na ikaingia katika mwili wako, na hapo ndipo magonjwa kama kansa huanza na safari ya kifo huanza taratibu, na kama risasi itakuwa imeingia mguuni au mkononi au tumboni basi maeneo hayo ya mwili yanaanza kutofautiana na sehemu nyingine za mwili
·         Kujitoa hapo unahitaji kufanyiwa upasuaji wa kiroho na kuiondoa risasi uliyopigwa
·         Kisha irudishie kwa aliyeituma
2.      Mshale wa rohoni: iko mishale ya kiroho watu hushambuliana kwa njia mbalimbali inaweza kutokea katika familia kwa mfano zenye wake wenza, kijana ambaye anaweza kuja kuwa ndie kiongozi wa familia au mwenye akili za kupita kawaida au mzuri lakini akatupiwa mishale tangu akiwa tumboni mwa mama yake na kama hilo linafanyika mara nyingi ubongo ndio unakuwa sehemu ya kwanza kushambuliwa na hivyo anaweza kupungukiwa na akili au akawa taahira
·         Kujitoa ni lazima kuuchomoa mshale wa kichawi na kuurejesha kwa aliyeutuma
·         Jiombee uwe na ukuta wa ulinzi wa moto ili mishale ya aina hii isikuweze
3.      Kubadilishiwa mwili: Kuna nguvu za kipepo za kubadilishiwa mwili, kama umebadilishiwa mwili unaonekana kuwa mzee kuliko umri wako, unajisikia vibaya, hauna amani, uzito, unakuwa mbaya, unajikunjakunja, hauelezeki na unachukiwa na ndoa yako inaweza kusambaratika na matatizo mengine mengi, katika ndoa kama mwili wako umebadilishwa unaweza kushangaa mumeo au mkeo anakuchukia kwa namna ambayo sio ya kawaida kiasi ambacho inawezekana hata asitake kukuona hapo lazima utambue kuwa kuna kitu kigeni kimetendeka katika ulimwengu war oho.
·         Hakikisha unaomba ili kwamba mwili wako wa asili uweze kurejea, utakapokwisha kuomba utaweza kuona mabadiliko na utagundua kuwa kweli kuna kitu kilikuwa kinaendelea
4.      Kulishwa vitu vichafu: ukiota ndoto unakula au umehudhuria pati ya kipepo na ukala vitu humaanisha vitu vibaya na mara utaona mikosi inaanza kukuandama, hutakua kiroho na magonjwa yatakuandama.
·         Hapo ni lazima maombi ya kufunguliwa na ikiwezekana mpaka vitu ulivyolisha vitoke
5.      Ndoa za kipepo:  Mtu anapooa au kuolewa katika ulimwengu wa kipepo kwa kukusudia au kwa ndoto atakuwa na vita kali sana, ndoa ya kiroho ni agano kamili kama lilivyo agano la ndoa, hivyo aliyeolewa au kuoa pepo ni lazima atambue kuwa atapambana mpaka tone la mwisho la damu kuhakikisha kuwa anatetea ndoa yake kama umeoa mwanadamu mwezako wa kawaida yule pepo atahakikisha kuwa mnaachana, kutakuwa na chuki ya ajabu, ugomvi usiokuwa wa kawaida, umasikini, kuporomoka kwa biashara,hali ya hatari nyumbani inakuwa ngumu na kubwa mno,muingiliano wa kifamilia nao unakua wenye migogoro mikubwa, na mpezni wa kiroho atahakikisha kuwa anamshambulia wa mwilini mpaka ashindwe.
·         Maombi ya kujikomboa
·         Maombi ya kuhakikisha kuwa mpenzi wako wa kiroho anakufa na unabaki na yule ambaye Mungu amekupa uishi naye, shambulia kila roho mbaya iliyopandikizwa dhidi yako, njia nzuri ya kujilinda sio kujikinga katika damu ya Yesu bali ni kushambulia kubomoa kuharibu na kurudisha mishale yote ya moto wa kichawi kwa adui ili asikushambulie milele.
·         2Thesalonike 1:6Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi;” ni kwa sababu hii ndio maana ukiwarudishia mishale yao wale waliokuonea inafanya kazi kwa sababu ni mapenzi ya Mungu Zaburi 109:17Naye alipenda kulaani, nako kukampata. Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,”
·         Wakati watu waovu wanapofanya mashambulizi yasiyo ya kimungu na kurushia mishale ya kichawi kwa watu wa Mungu ni lazima wanyamazishwe na kurejeshewa wao wenyewe uovu wao na mishale yao, siri moja wapo kubwa unayopaswa kuijua ni kuwa shetani na maajenti wake kama kuna jambo wanaliogopa ni kurejeshewa mashambulizi waliyoyatuma wao wenyewe, na usipowafanyia hivyo wakati mwingine hawatakoma, ndio maana biblia inasema waovu ni lazima wainame kwa wenye haki
Mambo ya kuombea
1.      Jiwwekee mikono na sema kuwa najilinda kwa damu ya Yesu
2.      Taja baadhiya uovu wa ibilisi na maajenti wake na yatume kwao mara saba kwa jina la Yesu mfano
·         Ndoto mbaya
·         Ndoto za kukojoa kitandani
·         Nuksi
·         Hofu
·         Umasikini
·         Mishale ya adui
·         Matatizo katika damu
·         Maumivu ya kichwa
·         Maumivu ya tumbo
·         Mikosi toka katika mito
·         Mikosi kutoka baharini
·         Mikosi ya ndoa za mitala
·         Mikosi kutokana na tohara
·         Mikosi ya utasa na ugumba
·         Mikosi ya kipepo
·         Mapepo ya uadui
·         Mapepo ya kichawi
3.      Silaha za jadi za kishetani, ziniachilie na zirudi kwa aliyevituma katika jina la Yesu.
4.      Weka mkono wako kishwani na mwingine katika tumbo kemea mishale yote ya adui na iamuru kurudi kwa wachawi na wanga na shetani katika jina la Yesu.
5.      Mweleze Bwana kila kitu kigeni na kila hali ngeni unayoipitia na ndoto ulizoziota kisha ziamuru kurudi kwa waliozituma katika jina la Yesu.
6.      Sema kila silaha ya shetani ikoseshwe amani na kusambaratishwa katika jina la Yesu.

Songa mbele:
Ili uendelee kujitakia kisasi cha bwana na kuendelea kuusumbua ulimwengu wa adui ni lazima usonge mbele katika kutembea na bwana na Jeshi lake Biblia inasema katika Yuda 1:3Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.”   Ni muhimu kufahamu kuwa wakati wa uamsho na wakati ambapo neno la  Mungu linashehimika kweli ye neno watu wanaitii na kiwango cha injili kinahubiriwa katika viwango vyake na kiwango cha maadui na uchawi na upinzani vinapanda

Kutokutii kunafananishwa na dhambi ya uchawi, 1Samuel 15:23 hivyo ili kusonga mbele katika mapambano haya, hatuna budi kuhakikisha kuwa tunamtii Mungu kwa gharama yoyote unapoasi madhara makubwa yanaweza nkukupata
1.      Utapungukiwa na uwepo wa Mungu
2.      Inawapa nguvu mapepo na shetani kukushambulia
3.      Kutokutii ni roho
4.      Itakusababishia taabu
5.      Itakaribisha dhoruba kwenye maisha yako
6.      Itakuletea kutokupendelewa na Mungu
7.      Itakueletea usingizi
8.      Itakufanya uwe katika kundi la wana mbuzi na sio Kondoo
9.      Itakufanya uwe unachukuliana na maswala ya dunia. Hakuna uovu mbaya kama kuchukuliana na dunia ukinionyesha mtu aliyerudi nyuma nitakuonyesha mtu aliyechukuliana na dunia kwa siku nyingi, hakuna anguko la ghafla lazima atakuwa amechukuliana na dunia kidogokidogo  na mwishoe anaangulka kabisa, anaweza kuwa amehudhuria chuo cha Biblia na kumaliza masomo yake na kusimikwa kuwa mtumishi na huku ni kutoa cheo cha kiroho bila kuthibitishwa na Mungu.
Achana na Unafiki.
 Ni roho ya kinafiki kukaa kimya mahali unapotakiwa kuzungumza eti kwa sababu unaogopa kuwaumiza marafiki au kwa lengo la kuwafurahisha marafiki ni roho ya kuvumilia uovu kwa sababu hutaki watu wakufanye wewe kuwa adui yao, ni muhimu kujiuliza swali je uko unafiki wowote ndani yangu?
Ni muhimu kuomba kama mwandishi wa zaburi alivyoomba unichunguze uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu Zaburi 139:23-24 inasikitisha kuwa wengi tunapenda kuabudu miungu iliyoko katika ubongo wetu.

Injili ya Mchepuko

Inasikitisha kuwa watu wengi leo wanaweza kuwa wanahubiri injili na isiyokazia kuhusu utakatifu, na kutoonyesha kuwa wanachukia dhambi lakini sababu kuu ikiwa ni kwa sababu wanataka kuwa na umati mkubwa wa watu au wanataka kufungua tawi, wanaifanya injili kuwa laini badala ya kukemea dhambi, wanasengenya, wanatoa mimba, wanatoka nje ya ndoa, mashoga wanawaita kaka poa, watu wengi leo wanachukizwa na mafundish yanayohusu kujitoa, kufunga, utakatifu, na ntofauti iliyoko kati ya watu hao na wa dunia ni kuwa wao wanabeba Biblia tu.

Achana na ukisasa

Ni muhimu kutokusahau kuwa Mungu huyu aliyemtuma Yesu duniani kwa wokovu ndiye yuleyule aliyewachoma moto watu wa sodoma na gomorah, wanasahau kuwa aliyemuita Paulo kunwa mtume ndiye aliyemzamisha Farao kwenye maji, wanawaambia watu wachague ni eneo gani la biblia wanataka kulisoma inasikitisha kwamba maovu mengi ambayo yamefanywa na wazungu kwa jina la Ukristo kwa sasa yamechukuliwa kama njia ya kuwatia moyo watu kurudi nyuma wazungu sasa wamefikia uovu hata wa kuona kwa mapenzi ya jinsia moja na kuyaleta makanisani lazima tuukatae uovu.

Kuifuta namna ya Dunia hii

Biblia inasema wala msiifuatisha nemna ya dunia hii,  namna ya dunia hii inataka Mungu aonekane kuwa mdogo kuliko mawazo yao, inamfanya Mungu aonekane kuwa mwongo, wanafikiri kuwa Mungu anayepaswa kufuatwa ni Mungu atakayewafanya wakati wote wajisikie vizuri, wanataka Mungu ambaye hata ukifanya dhambi anakulipa mshahara, wanataka kuwapa watu wazo kuwa Mungu ni Mungu wa Rehema na hahukumu kwa urahisi, wanataka Mungu akubaliane na kila tunachikifanya na staili yetu ya maisha, wanafikiri kuwa Mungu ni kama anahitaji mtazamo mdogo tu ambao tunaweza kumpa siku ya jumapili tu na kumtolea sadaka, lugha zinabadilisha kuifanya dhambi ionekane kuwa kitu kidogo sana kisicho na madhara, wanacheza aina za muziki unaocheza katika kumbi za disco, muziki unaopigwa hauna tofauti sana na ule wa duniani, inahubiriwa injili inayotoa msahama wa dhambi bila mtu kubadilika au kutubu,inayotia moyo kwenda mbinguni bila kuonyesha kuwa kuna moto, Biblia inaonye katika 1Wakoritho 10:12Yeye ajidhaniaye kuwa amesimama na aangalie asianguke

Maombi.
1.      Naamuru kuchanganyikiwa na fadhaa zilizoratibiwa na shetani Dhidi yangu katika jina la Yesu
2.      Kila mpango mbaya wa ibilisi kinyume na maisha yangu katika jina la Yesu
3.      Kila ina ya laana na mapepo ambayo shetani ameyakusudia dhidi yangu nayadhoofisha katika jina la Yesu
4.      Kila aina ya vita iliyokusudiwa kinyume na amani niliyo nayo naiharibu katika jina la Yesu
5.      Naamuru kuchanganyikiwa kwa ibilisi katika kila mpango wake katika jina la Yesu
6.      Kila aina ya vita inayokusudiwa na kupangwa kinyume nami naiharibu katika jina la Yesu
7.      Kila vita kinyume na amani niliyo nayo naiamuru kwa jina la Yesu
8.      Kisha anza kumshukuru Mungu kwa imani kwani ataanza kujibu maombi yako.
Na Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima 
Rev. Innocent Kamote
)718990796

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni