Jumatano, 11 Oktoba 2017

Mnamwamini Mungu,Niaminini na mimi


Andiko:Yohana 14:1Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.”


Utangulizi.

Injili ya Yohana ni injili inayokazia kuhusu kumuamini kumuamini Yesu, kusudi kubwa la mkuandikwa kwa injili hii ni ili watu wapate kumuamini Yesu kuwa ni mwana wa Mungu  Yohana 20:30 -31 Biblia inasema “Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake

Katika andiko la msingi tunaona Yesu akiwatia moyo wanafunzi wake kwamba wasifadhaike mioyoni mwaoa na kuwa wanapaswa kumuamini yeye kama wanavyomuamini Mungu, kwa nini Yesu anasema swala hili kwa sababu alikwisha kuwaambia wazi kuwa Yuda atamsaliti Yohana 13:21, Petro atamkana mara tatu, Yohana 13:38, na pia kuwa na pia Yeye anakaribia kuondoka tena kupitia mauti, kwa ujumla hii ilikuwa hali ngumu kwa wanafunzi wa Bwana ambao walikuwa wameacha vyote ili kumfuata Yesu, Jambo hili liliwakatisha tamaa.

Mara kwa mara katika maisha yetu tunaweza tukawa na nyakati ngumu na za kukatisha tamaa katika maisha, tunaweza kukutana na hali zilizo ngumu na hata tukayaona maisha yetu kuwa giza mbele, tunaweza kujawa na hofu, kwamba mambo yatakuwaje Biblia inatoa jibu kuwa tumamini Yesu, Yesu anasema mnamwamini Mungu, niaminini na mimi, hii maana yake ni kuwa kumuamini Mungu ni sawa kabisa na kumuamini Yesu, Yesu ni Mungu na hivyo tunapaswa kumwamini na kumtegemea yeye, naye atatutokea na kutupa uzima

Mfano.

Kulikuwa na mkwea milima mmoja maarufu sana ambaye alikuwa na tabia ya kupanda milima mirefu duniani, siku moja mpanda milima huyu alichelewa kushuka mlimani, hivyo giza kuu lilimkuta akiwa juu, hakukuwa na mbara mwezi wala nyota na ilikuwa ngumu sana kuweza kuona anakokwenda kwa vile kulikuwa na wingu zito na giza nene

Mpanda milima huyu alijaribu kushuka kutokakatika mlima lakini kwa bahati mbaya aliteleza na akaanza kuanguka akiwa hewani kwa kasi ya ajabu, alikuwa akiona vitu vyeusi tu alipokuwa anakwenda chini kwa kasi, ilikuwa hali ya kutisha sana akajua kuwa ni kaburi tu ndilo linalomsubiri
Aliendelea kuanguka kuelekea chini akiwa na hofu kubwa sana akawaza kuwa sasa anakaribia kufa ghafla alisikia kamba ikiwa imekamata kiuno chake kwa nguvu sana na mara mwili wake ulianza kuning’inia alihisi kuwa kama imekamata bara bara kiuno chake na ikimshika kwa nguvu lakini alikuwa bado yuko hewani ananinginia, naye aliishikilia kwa nguvu zake zote, lakini alikumbuka kuliitia jina la Yesu na kuomba ee bwana Yesu nakuomba uniokoe na mauti hii

Mara moja alisikia sauti ikimwambia kutoka mbinguni Je unataka nikufanyie nini? Alisema uniokoe ee Mungu wangu, Yesu alimwambia unaamini kuwa naweza kukuokoa? Akasema ndio bwana nakuamini Yesu akamwambie kata kamba yako iliyokushika kiunoni uende zako

Baada ya sauti hiyo kulikuwa kimya kwa muda, na muda ukazidi kwenda mpanda milima yule aliendelea kushikilia kamba yake huku akinin’ginia na hakukubali kuiachia kamba aliishikilia kwa nguvu zake zote

Asubuhi waokoaji walimkuta mpanda milima akiwa amekufa huku akiwa ameshikilia kamba yake kwa nguvu kubwa sana watu walisikitika sana na kulia kwani ilikuwa ni futi moja tu kutoka ardhini
Wengi tumefungwa na vitu vidogo tu vinavyotuzuia kumuamini Mungu, ni lazima tuachie kama hiyo na kumtegemea Mungu mwokozi wetu, kamwe tusimuachie Mungu

Sijui unapitia hali gani katika maisha yako lakini najua jambo moja tu kuwa Mungu ataweka kila kitu sawa katika maisha yako kwa wakati mkamilifu, wakati mwingine unaweza kuchanganyikiwa na wakati mwingine unaweza kukosa faraja, lakini Mungu anabaki kuwa mwaminifu katika kututendea mema, kumbuka maneno ya bwana Yesu Usifadhaike, Unamwamini mungu muamini nay eye, usiogope, wakati wote nenola Mungu linatutaka tumwamini Mungu 

2Nyakati 20:20Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.”

Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Kamote

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni