Jumatatu, 27 Novemba 2017

Kuwa wajinga Katika mambo mabaya !



Mstari wa Msingi: Warumi 16:19Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.”

Ni lazima watoto walelelwe katika njia iwapasayo kabla mioyo yao haijawa zege iliyokauka na Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Utangulizi.

Ni muhimu kufahamu kuwa tunaishi katika nyakati za mwisho zaidi na katika nyakati hizi nza mwisho Shetani amekusudia kuharibu kanisa na kuiharibu jamii kupitia mmomonyoko wa maadili, na ili aweze kufanikiwa kuharibu jamii anaweza kupata mafanikio makubwa kama atakusudia kuwaharibu watoto ambao ndio kanisa na taifa la kizazi kijacho.

Kwa muda mrefu katika jamii ya wasomi wa Kikristo kumekuwako na mijadala mikubwa miwili, mmoja ni msimamo mkali unaolenga kuwa watoto ni lazima wafundishwe njia za Mungu mapema kabisa katika maisha yao ili neno la Mungu likae ndani yao kwa iwngi kabla ya kuwa watu wazima, lakini wazazi wengine na baadhi ya wanatheolojia wa kikristo wanapinga kwa madai kuwa watoto hawawezi kuzaliwa na Ukristo wetu hivyo ni muhimu wakaachwa na kujifunza mema na mabaya na kuijua Dunia kisha wakutane na Mungu wao binafsi ndipo watakuwa na imani ya kweli, hata hivyo wazo hili la pili ingawa linaweza kuonekana kama lenye hekima ni wazo baya zaidi kupata kutokea duniani kwani liko kinyume na maandiko.

Biblia imeagiza kuwa ni lazima watoto waelekezwe na kukua katika njia ya Mungu,  

Kumbukumbu la torati 6:1-9Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru Bwana, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; upate kumcha Bwana, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe. Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali. Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;  nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.  Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.” 

Biblia inaonyesha kuwa watoto wakifundishwa vema njia ya Mungu hawataiacha hata watakapokuwa watu wazima  

Mithali 22:6Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” 

Kutokuwalea watoto katika njia iliyonyooka na kosa kubwa sana katika mapenzi ya Mungu Nyakati za Biblia hususani wakati wa waamuzi kulitokea kizazi ambacho hakimjua Mungu wala njia zake na hivyo waliishi kwa kutenda kila aina ya uovu  

Waamuzi 2:10-11Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli. Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.” 

Kwa sababu hiyo ni jukumu la Wachungaji walimu na wazazi kuhakikisha kuwa watoto wanaikulia njia ya Mungu, na hawajifunzi uovu kutoka kwetu, na kuhakikisha kuwa tunawasaidia kwa namna yoyote ile kukua kiakili, kimwili, kitaaluma na kiroho, huiku wakiwa wenye nidhamu thabiti, Yesu alitangaza hukumu kubwa sana kwa watu watakaowakwaza watoto na kuwafanya wakengeuke alisema yafaa wafungiwe jiwe kubwa la kusagia na kutoswa katika kilindi cha bahari  

Mathayo 18:6bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.

Mungu alimchagua Ibrahimu na kumfanya kuwa Baraka kubwa sana Duniani lakini sababu kuu ya kumchagua Ibrahimu Mungu anaieleza katika  

Mwanzo 18:17-19BWANA akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye haki na hukumu, ili kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.  
             
Kumbe ni kwa kusudi hili katika andiko la Msingi Paulo mtume anatoa wito kwa kanisa la rumi kuwa na hekima Yaani ujuzi wa kutosha katika mambo mema na kuwa wajinga katika mambo mabaya neno kuwa wajinga katika biblia ya kiyunani linasomeka kama “AKERAIOS” Ambalo maana yake kuwa incorruptible au kuwa Innocent,  kwa Kiswahili ni kuwa safi kabisa, wasiochanganywa, kutokuujua kabisa uovu wala mwenendo wa Dunia, Biblia inatumia neno hilo pia katika

 1Wakoritho 14:20Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima.”

Unaweza kuona kwa msingi huo basi Msingi wa kibiblia haufudnishi kuwaachia huru watoto, Bibloia inataka watoto wabanwe katika sheria, waelekezwe nini cha kufanya na nini sio cha kufanya , haiwezekani watoto waachiwe kufanya lolote wanalojisikia kilifanya, tusiwaruhusu kukaa katika njia ya shetani eti ili nao wakutane na neema ya Mungu binafsi, ni lazima sisi tutumike kama chombo cha kuwanyoosha wakae katika njia iliyonyooka, kujua maovu kuna mateso mengi sana ni waarabu na wayahudi tu Duniani ndio wanaojua kuwalea watoto wao na kuwafanya wafuate imani zao kwa uthabiti na kuwarithisha kama Ibrahimu, sehemu nyingi duniani na wakristo wameshindwa kabisa kufanya wajibu huu

Hatupaswi kuwaacha watoto wakajikulia tu kana kwamba kuna bahati nasibu ya kukua kwao, lazima tuhusike katika kuwajenga na kuwalea watu wengi sana wanatumia mamilioni ya fedha duniani kusomesha wachungaji, walimu madaktari na wataalamu mbalimbali na hata makanisani lakini hakuna watu wanaofanya utafiti wa kutosha kuhusu watoto zaidi tu tunasoma kina “Maria Montessori” mwana falsafa wa zamani tu wakizungumza kuhusu watoto na namna yao ya kujifunza, Zamani kulikuwa na kozi katika chuo cha biblia Inaitwa “Children Ministry” mimi niliisoma katika ngazi ya Diploma zamani sijui kama mkozi hii siku hizi ipo lakini kanisa limepuuza kabisa huduma ya watoto na ukiwauliza Wachungaji wengi watakuambia kuwa tatizo watoto hawana mafungu ya kumi, 

Ni lazima tufanye kila jitihada ya kuwalinda watoto wetu katika udanganyifu wa dhambi na maasi ili kuwalinda watoto wetu na uovu duniani Roho mtakatifu anataka wawe wajinga katika mambo ya uovu

Tukiwaachia watoto wetu waijue dunia watabikiriwa kama Dinah binti Lea wa Yakobo Mwanzo 34:1-2, 7 Wana wa Yakobo waliposikia walikasirika sana na walisikitika waliona kuwa dada yao amefanyiwa mambo ya kipumbavu kwa nini hii ni kwa sababu Yakobo alikaa na watu wabaya karibu nao ni lazima tuwalinde watoto wetu, Naamini ya kuwa hukuchagua mahali hapa kwa bahati mbaya, wazazi waliochagua mahali hapa wanajua kuwa watoto wao wako katika mikono salama na hatutaruhusu mambo ya kipumbavu yatokee Katika jina la Yesu amen

“Songs “Bless the Lord” Rebbeca Malope”
Rev. Innocent Kamote.

Mkuu wa Wajenzi mwenye hekima

Maoni 3 :