Jumapili, 10 Desemba 2017

Siri kuu Muhimu kuhusu toba!


Mstari wa Msingi: Matendo 2:38Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Utangulizi:

“Tubuni” alisema Petro, Hii ilikuwa sehemu muhimu ya ujumbe wa Petro iliyotolewa chini ya uwepo wa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste siku ambayo ilikuwa sikukuu kwa Wayahudi lakini Mungu katika mpango wake alikusudia Kanisa lizaliwe, Toba ilikuwa ni sehemu muhimu kwa watu kupokea Roho Mtakatifu, Toba ilikuwa ni sehemu muhimu mara kanisa lilipoanza, toba lilikuwa ni jibu Muhimu kwa swali muhimu lililoulizwa katika Matendo 2:37Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?”

Toba ni sehemu muhimu sana katika msingi wa imani ya Kikristo, Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anaiweka toba kama moya ya mafundisho ya awali ya Kristo Waebrani 6:1-2Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.” Waebrania 5:12 pia, kwa msingi huo kama toba ni moja wapo ya msingi muhimu katika imani yetu haipaswi kupuuziwa hata kidogo.

Kimsingi mafundisho na ukweli kuhusu toba katika agano jipya hauwezi kupuuziwa Hasa ukizingatia kuwa toba ilikuwa ni kiini kikuu au kilele cha mahubiri ya watu wote maarufu katika agano jipya

·         Yohana mbatizaji alihubiri toba Mathayo 3:1-2Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”

·         Yesu Kristo alihubiri toba Mathayo 4:17Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”

·         Paulo Mtume alihubiri toba Matendo 20:21nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo

Kwa msingi huo basi si jambo la kushangaza kuona Yesu akiwaagiza wanafunzi wake kuhubiri na kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi huku kiini cha ujumbe kikiwa tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia Mathayo 28:19-20Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari

Luka 24:47na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.”

Kwa hiyo unaweza kuona kuwa toba ndio msingi wa mafundisho ya ukristo, awaye yote anayebatizwa katika ukristo kwanza ni lazima awe na uelewa kamili wa maana ya toba, anapaswa aelewe wazi, huzuni ya kimungu, Neema ya Mungu na imani iokoayo.

Kwani toba ni agizo kuu kwa watu wote wa aina zote wa mahali popote Matendo 17:30Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.”

Kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa Toba ni mojawapo ya somo linalotakiwa kufuatiliwa kwa makini na kwa undani zaidi, toba ni sehemu muhimu sana katika kujiunga na ufalme wa Mungu Dr, David A DeSilva alisema “toba ni neema ya Mungu yenye kurejesha uhusiano wa Mungu na mwanadamu”

Zifuataza sasa ni siri kuu muhimu kuhusu toba.

1.       Toba ni badiliko la nia na tabia.

Tunzapozungumzia toba kwa ufupi tunasema toba ni badiliko la nia na tabia, ni kuachana na njia ya kwanza ya kawaida uliyokuwa ukiifuata kuelekea katika njia nyingine unayopaswa kuifuata, kuacha kufuata nia ya mwili wako na kufuata nia ya Mungu, mwanadamu anapoamua kubadilisha nia yake na mtazamo wake mara moja na tabia yake hubadilika

Warumi 12:2Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Mathayo 21:28-32Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende. Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. . Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.”

Toba huambatana na kutii na kutenda mapenzi ya Mungu,toba inamtoa mtu kutoka katika mtazamo hasi aliokuwa nao kuelekea katika mtazamo chanya toba inaleta badiliko kuu sana katika maisha ya mtu, kwa mfano wote tunatambua jinsi Paulo mtume alivyokuwa katika njia zake alikuwa tishio kubwa sana la Ukristo na alidhamiria kuhakikisha kuwa anawashughulikia wakristo kama watu wahalifu 

Matendo 9:1-2, “Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.” Mtu huyuhuyu ambaye alikuwa na nia mbaya kuhusu Wakristo na aliyetumia nguvu zake nyingi kuwasumbua wakristo sasa alipotubu alibadilika na kuwa mtu mwingine akithibitisha kuwa Yesu kristo ni Bwana  

Matendo 9: 20-2220. Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaharibu walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani? Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.”

Tunapozungumzia toba maana yake ni ufunguo mkubwa wa mabadiliko ya akili yaani nia na tabia mtu anapodai kuwa ametubu hatarajiwi kuonekana na tabia zile za kwanza tena lakini anapaswa kuwa na matendo mapya yanayoendana na toba yake Matendo 26:20bali kwanza niliwahubiri wale wa Dameski na Yerusalemu, na katika nchi yote ya Uyahudi, na watu wa Mataifa, kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.”

2.       Toba humfanya Mungu arudishe uhusiano na sisi.

Dhambi zinaharibu uhusiano mwema na Mungu, Mungu hasikilizi wenye dhambi Yohana 9:31Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.” Yesu Kristo alihakikisha kuwa anadumisha uhusiano wake na Mungu wakati wote alimtii Mungu na hivyo alisikilizwa sana na Mungu na hatimaye kuwa sababu ya wokou kwa watu wote 

Waebrania 5:7-9Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;” Toba ni kurejesha uhusiano na Mungu na ambao ulivunjika au unavunjika kutokana na kutokutii au dhambi, ni mbaya sana kupoteza uhusiano na Mungu. Hakuna jambo zuri sana duniani kama kuwa na uhusiano na Mungu, mwanadamu kukosa uhusiano na Mungu ni sawa na kufariki dunia kabla ya wakati, hatuwezi kuwa na amani ya kweli kama hatuna amani na Mungu, kwa hiyo ni muhimu sana kurejesha uhusiano wetu na Mungu, watu wengi wanatamani lakini uhusiano wao na Mungu umevunjika Dhambi zinazuia uhusiano mwema na Mungu na ndio maana Mungu anatoa wito wa sisi kumrudia yeye 

Isaya 59:1-2. Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” Sababu kubwa ya watu wengi kupoteza uhusiano na Mungu ni makosa na dhambi Lakini Mungu anasema ameweka njia ameweka mwaliko ambao tunaweza kuutumia kurudisha uhusiano wetu na Mungu, njia hii ni toba pekee, kupitia njia hii anaweza kutusamehe, kuturejesha na kutusafisha. 

1Yohana 1: 8-10Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu”. Mungu anatuthibitishia kuwa yuko tayari kusamehe na kutufikia na kuturudia endapo sisi tutakubali kufanya sehemu yetu yaani kutubu kwa kumaanisha kuacha.

Zekaria 1:3 “Basi, uwaambie, Bwana wa majeshi asema hivi, Nirudieni mimi, asema Bwana wa majeshi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi.”

2Nyakati 7:12-14 “Bwana akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.” 

Wakati wote Mungu ametamani sana kuwa na uhusiano thabiti na sisi, au na mimi na wewe lakini kikwazo kikubwa ni dhambi na maovu ni wito wa rehema na neema ya Mungu na ahadi zake kubwa kwetu kwamba tukimuita atatuitikia, Kama tunahitaji uponyaji kwa taifa letu na maisha yetu na mafanikio na baraka na mvua nzuri ni toba pekee inayoweza kufungua milango ya Baraka kwa Mungu wetu.

3.       Toba ni ishara ya unyenyekevu.  
             
Swala la kutubu ni zawadi kutoka kwa Mungu ni karama sio swala rahisi kama tunavyofikiri, wanadamu wengi hupenda kujihesabia haki, tunatabia ya kufikiri kuwa sisi ni bora kuliko wengine na tunatabia ya kufikiri kuwa jambo hililinamuhusu mtu fulani na halinihusu mimi tunayo tabia ya kukwepa kuwajibika tuna tabia ya kufikiri kwamba tna ubora fulani kuliko wengine na kwa sababu hiyo tukakataa kutubu bila kuelewa, toba sio kitu rahisi kwa mtu anayejihesabia haki, na kujihesabia haki nintabia ya kiburi na kukosa unyenyekevu 

Luka 18: 9-14Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.  Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.”                  

Unaona sio rahisi kwa mtu anayejifikiria kuwa na haki kukubali toba , sio rahisi, sio rahisi kwa mtu mwenye kiburi kutubu, toba inakaa na wanyenyekevu, watu wanaovunjika moyo ka haraka ukiwa mtu wa toba unaweza kuomba msamaha kwa wanadamu na hata kwa Mungu lakini vilevile unaweza kuomba radhi kwaajili ya watu wengin.

Mungu anafananisha toba na unyenyekevu, Mungu anaiona toba kama vunjiko la moyo, Mungu anaiangalia toba kama unyenyekevu na kuwa nje ya kiburi jambo hili sio jepesi bila neema ya Mungu.

Katika Biblia hususani agano la kale maombolezo makubwa sana yenye kuonyesha kupoteza tumaini yalifanyika kwa watu kuvaa Magunia na kujipaka majivu, au kurarua mavazi ya na kurusha michanga juu, hii ilikuwa ni ishara ya nje ya maumivu makali na kuonyehsa unyenyekevu, Yakobo alivaa magunia na kuomboleza kwa siku nyingi sana alipofikiri kuhusu kifo cha mwanaye Yusufu, Daudi alimamuru watu kuvaa magunia akiomboleza kwaajili ya Abneri alipouawa, wakati mwingine pia toba ilifanyika kwa kiwango sawa na maombolezo kama ya kufiwa.

Moja ya stori ya kusisimua katika agano la kale ilikuwa ni habari ya mfalme Ahabu 1Wafalme 21: 19-26Angalia, nitaleta mabaya juu yako; nami nitakuangamiza kabisa, nitamkatia Ahabu kila mume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli. Kisha nitaifanya nyumba yako iwe kama nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya, kwa ajili ya chukizo ulilonichukiza, hata kunighadhibisha, ukawakosesha Israeli. Tena Bwana alinena habari za Yezebeli, akisema, Mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli. Mtu wa nyumba ya Ahabu afaye mjini, mbwa watamla, na yeye afaye mashambani ndege wa angani watamla.  (Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana ambaye Yezebeli mkewe alimchocheaAkachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.).” 

Ni wazi kabisa katika stori hii kuwa hakuna mtu aliyewahi kuwa muovu katika wafalme wa Israel nyakati za agano la kale kama Ahabu, na kutokana na maovu kadhaa wa kadhaa, Mungu alimtuma nabii kutangaza hukumu mbaya dhidi ya Ahabu na familia yake lakini Ahabu aliposikia hukumu hii mbaya badala ya kumshambulia nabii na au kuamuru kumuua aliamua kuwa mnyenyekevu na kujinynyekeza kwa Mungu kwa njia ya toba  

1Wafalme 21:27-29Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole. Neno la Bwana likaja kwa Eliya Mtishbi, kusema, Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu? Basi kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake.”   

Mungu aliheshimu toba ya ahabu na kuamini kuwa amenynyekea mbele zake, toba ni sihara ya unyenyekevu, toba na unyenyekevu huenda pamoja Mithali 3:34Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.” Mungu huwapinga wajikwezao bali huwapa neema wanyenyekevu. Yakobo 4:6

4.       Toba humfukuzia shetani mbali nasi.

Mara tunapokuwa tumemkosea Mungu, tunaweza kujikuta tunapungukiwa na imani, tunaacha kumuamini Mungu na neno lake, tunasikia sauti za mashaka, hukumu katika mioyo yetu na dhamira zetu, unahisi kama Mungu hatakupa nafasi nyingine tena au Mungu amekuchoka, na kisha unakosa amani.

Lakini mara mkristo anapotubu na kurejea kwa Mungu sauti hizo za kishetani hukimbia mbali sana na wewe Biblia inasema mtiini Mungu mpingeni shetani naye atawakimbia Yakobo 4:7Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” Katika mstari huo maana na kumtii Mungu na kumpinga shetani ni nini? Maana yake ni kutubu, kujinyenyekesha, kutubu, ni kuacha dhambi, ni kuacha kuwa vuguvugu angalia Yakobo 4:8-10Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.  Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.

Dhambi inampa nguvu shetani ruhusa kuwa karibu nasi, Shetani huwa karibu na wale wanaotenda mapenzi yake kama Mungu anavyokuwa karibu nwatendao mapenzi yake 1Yohana 3:8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” Shetani huwa karibu na wale wanaotenda mapenzi yake Yohana 8;44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.”

Unaweza kuona kwa msingi huo tunapotubu Shetani anakosa nafasi ya kushitaki na kutudai kama mali yake na hivyo tunaweza kumpinga na kupambana naye na kuondoa nguvu yake yote ya ushawishi katika maisha yetu.

5.       Toba inatuweka huru kutoka katika mateso ya dhambi.

Yohana 8:34 -36 “Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.”

Dhambi inampa shetani kibali cha kututesa na kutuonea, inatoa kibali kwa kila kitu kuwa adui yetu, inatoa kibali kwa magonjwa, jambo hili lina ukweli katika maisha yetu, tunapoendelea na maisha yetu ya dhambi, utagundua kuwa anayeteseaka zaidi ni wewe na mimi, ingawa dhambi huonekana kuwa njema na tamu tunapoitenda lakini kilele chake kina maumivu makubwa sana kuliko ahadi ambayo dhambi imetuahidi, Na ndio maana kwa kiasi kikubwa Yesu alipowasaidia watu waliokuwa na matatizo mbalimbali kwa sababu ya dhambi aliwaonya kwamba wasifanye dhambi tena

Yohana 8:10-11Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?  Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]”

Yohana 5:14 “Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.”

Magonjwa, uvamizi wa kipepo, mashambulizi ya ibilisi na hatari za mauti vinaruhusiwa kutuandama tukiwa katika maisha ya dhambi, na ndio maana Yesu anatoa tahadhari kutokuirudia dhambi tena ili kuepuka mateso yake,  Ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba tunapotubu dhambi zetu tunapokea Rehema, na kwakuwa Yesu Kristo ndiye kuhani wetu mkuu hutuombea kwa kuingilia kati kwaajili yetu
 Waebrania 4:14-16 “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.”

Waebrania 7:24-25bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.”

Ni kwa sababu hiyo basi neno la Mungu linatuahidi kwamba toba inatuleta kwa Mungu na kumfanya Mungu afutilie mbali dhambi zako na tusipotubu hatuwezi kuwa huru kutoka katika mateso na vifungo vya dhambi. Matendo 3: 19Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;”

6.       Toba huongoza katika maisha na Yesu Kristo.
Kwa kawaida dhambi huongoza katika mauti na mauti ya milele Biblia iko wazi kabisa kuwa Mshahara wa dhambi ni mauti

Warumi 6:23Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Na Yesu alitoa maonyo kuwa tusipotubu bila shaka nasi tutaangamia

Luka 13: 1-3 “Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao. Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo”.
Lakini inapokuwepo toba maangamizi huahirishwa na wokovu hupatikana

Matendo 11:18Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima.”

2 Wakoritho 7:10 “Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
Toba ina tabia ya kumkaribisha Yesu Kristo, na kumfanya Mungu awe na ushirika na sisi katika maisha yetu, Yesu alikazania sana swala la toba kwa makanisa yale saba ya asia katika ufunuo lakini hatimaye alisema

Ufunuo 3:19-20Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” Ni furaha kubwa sana kuwa na ushirika na Yesu Kristo na Mungu, Yeye alishinda kifo na mauti ili aweze kutupa uzima huu na uzima wa milele, Uzima wa milele haunza tutakapokuwa tumeenda mbinguni bali unaanza sasa hivyo ni furaha kubwa sana kama tutatubu na kuacha dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha ili tuwe na ushirika wa kudumu na Bwana wetu Yesu Kristo.

7.       Toba ni Agizo la Mungu ni ushauri wa Mungu.

Paulo mtume alisumbuliwa sana na jamii ya watu waliokuwa wanafalsafa wa Areopago waliokuwa wakiabudu sanamu pale Athenes Ugiriki na kuwaambia wazi mapenzi ya Mungu ni kila mtu wa kila taifa popote pale anapaswa kutubu, Mungu alijifanya kuwa haoni uovu wao zamani za ujinga lakini saasa anaagiza toba kwa kila mtu na kila taifa Matendo 17:30 “Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.Mafundisho kuhusu toba yanamuhusu nkila mmoja iwe ni mataifa au wayahudi iwe ni kanisa au wasio kanisa ili kurejesha uhusiano wetu na Mungu tunapaswa kutubu, kumbuka hatupaswi kumlazimisha mtu kutubu lakini tunapaswa kuhubiri toba na kuwapa watu uwezo na maamuzi ya kuchagua, toba ni sehemu ya njia ya uzima na kutokutubu ni kuchagua mauti Kumbukumbu la Torati 30:19Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;” Unaona ili uwe hai uwe na uzima Mungu anakushauri kuchagua toba hii ndio namna pekee utakayoweza kuepuka Mauti, Yesu alipokuwa akiyaonya makanisa yaliyoko Asia ndogo aliwashauri mara kwa mara faida za toba na kuwaonya madhara ya kutokutubia kile alichowashauri:-

Ufunuo 2:5 EFESO “Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.”

Ufunuo 2:14-16. Smirna “Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.

Ufunuo 3:2-3  SARDI “Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako

Ufunuo 3:19, Laodekia “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.”Wakati wote maandiko yanakazia na kutoa wito wa kutubu, ushauri wa kutubu, maoni ya kutubu,hivyo toba inabaki kuwa agizo na ushauri wa Mungu kwa faida ya mwanadamu katika ufalme wa Mungu.

8.       Toba inaleta furaha kubwa sana Mbinguni.

Yesu kristo katika mafundisho yake alikazia sana furaha na shangwe inayotokea Mbuinguni pale mtu mmoja anapotubu, Luka 15: 1-7 biblia inasema “Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize.Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao. Akawaambia mfano huu, akisema, Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone? Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi. Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.”  Biblia au Bwana Yesu amerudia tenana tena kwamba kuna furaha mbinguni, kwa malaika wa Mungu kwaajili ya mwenye dhambi mmoja tu anapotubu, ni wazi kuwa toba ni mapenzi ya Mungu yanayopendeza na kusubiriwa sana mbinguni ili kwamba mtu aweze kuyatimiza. Mtu anapokuwa dhambini kibiblia anaitwa mfu au anafananishwa na mtu aliyekufa kwa sababu ya dhambi aidha toba inaleta neema ya Mungu inayotuokoa kama tutakavyoona baadaye lakini neno la Mungu lasema dhambi hutufanya kuwa wafu na tunapotubu neema ya Mungu hutusaidia kuokoka Waefeso 2:1-9 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” Watu walioko dhambini Mungu, anawatazamia kuwa watatubu kwani biblia inawaita wafu na waliopotea na wanapotubu inawaita walifufuka na walioonekana  Luka 15, 32 “Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.” Mungu angeweza kuuhukumu ulimwengu kwa haraka na Yesu angeweza kurudi mara ya pili kwa haraka lakini kukawia kwake ni uvumilivu kwa wanadamu ili kwamba watu wote wafikie toba, 2Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.”

9.       Yesu alikuja kwaajili ya wenye dhambi ili watubu.

Tumeona maana halisi ya toba kwamba kutubu ni kugeuka Metanoia kwa kiyunani, kwamba mtu anageuka na kuiacha njia mbaya na kuyatoa maisha yake kwa Mungu, Toba ni kama wito na kwaasili unaanza na Mungu, anatufungua akili kwa neema yake na kisha tunaitikia kwa kuomba naye analeta msaada kwetu,na kutubadilisha kupitia neno lake, tunapolisoma neno lake tunaanza kurekebisha imani zetu, tamaduni zetu, tabia zetu na namna na mwenendo wa kuishi kwetu neno la Mungu likiwa ndio kipimo kikuu cha maisha yetu!

Kwa msingi huo toba ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu ya imani Yesu mwenyewe anaeleza wazi kuwa kusudi kubwa la ujio wake duniani ni ili watu watubu Luka 5:32Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”

Yesu licha ya kusisitiza kuwa alikuja kuwaita wenye dhambi wapate kutubu pia alilihubiri kusudi hili kila mara alipoihubiri injili Marko 1;14-15Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili”.  na Mathayo 4:17Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Yesu alifundisha kuwa moja ya mambo muhimu sana ni kuurithi ufalme wa Mungu Mathayo 6:33Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Yesu alisisitiza kuwa ufalme wa Mungu ndio wa Muhimu zaidi lakini njia pekee ya kuupata alisisitiza kuwa ni toba, Maandiko yanasisitiza kuwa ufalme wa Mungu unapatikana kwa wale wanaotubu.

10.   Toba inaleta wokovu

Njia kuu ya kupokea zawadi ya wokovu na kuingia katika ufalme wa Mungu nji kwa njia ya toba, hakuna namna yoyote mtu anaweza kuokoka bila kutubu, toba ndio msingi mkuu wamafundisho ya wokovu na ufalme wa Mungu, Waebrania 6:1-2. “Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele”. Kuzitubia kazi zisizo na uhai maana yake ni kuacha dhambi, Yesu alikwisha kutoa maonyo kuwa kama hatutatubu uko uwezekano mkubwa wa kuangamia Luka 13:1-5 “Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao. Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo?Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.” Onyo la Kristo halimaanishi kuwa anataka watu waangamia hapana anataka watu watubu ili wasiangamie ni ushauri uliojaa upendo kama watu hawatatubu kweli hawataokolewa Mungu ni mvumilivu kwa sababu anataka watu wote tufikie toba 2Petro3:9Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Maandiko yanatoa wito wa toba kwani Mungu atamuhukumu kila mtu kwa kadiri ya matendo yake na ndio maana manabii walioonya wakati wote walitoa wito kwa watu kutubu Ezekiel 18:30-32 Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu.   Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli? Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi”. Unaona dhambi huleta maangamizi huleta kifo lakini Mungu hafurahii kufa kwetu na ndio maana anatoa wito tutubu toba ina faida gani toba inaleta wokovu, tunapomuamini Bwana Yesu maana yake tutatubu kwa imani kupitia kazi za rehema zilizofanya na Yesu pale msalabani ili tuweze kuokolewa Matendo 16:30-31kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?  Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.

Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni