Jumatano, 24 Januari 2018

Huifanya miguu yangu kuwa kama ya Kulungu!



Habakuki 3:19YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya MIGUU YANGU KUWA KAMA YA KULUNGU, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.”



Utangulizi:

Leo hii tutachukua muda kutafakari kwa kina na upana ma urefu kuhusu mnyama mwingine anayesifiwa sana katika maandiko anayejulikana kama “KULUNGU” tunapojifunza kuhusu mnyama huyu utaweza kugundua kweli nyingine za kibiblia ambazo zinaanika upendo wa Mungu kwetu.
Katika tamaduni za mashariki ya kati Kulungu au kwa kiarabu Ayyalah (maana yake Mbuzi pori) ni mnayama anayetumika kuelezea symbol ya Mamlaka ya kiroho, pia ni myama ambaye pembe zake zinauwezo wa kukua na kuvunjika au kuanguka kisha kuota nyingine ni alama ya “kuanza upya”au “kuzaliwa upya” regenereation na ni alama ya Huruma na kujitoa au kujali kwa Mungu dhidi ya watoto wake yaani wana wa Mungu.

Tutajifunza somo hili kwa kuangalia vipengele vitatu vya muhimu vifuatavyo:-

·         Ufahamu kuhusu “KULUNGU”
·         Sifa kuu za Kulungu
·         Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya Kulungu!


Huifanya miguu yangu kuwa kama ya Kulungu!

Ufahamu kuhusu Kulungu.

Kulungu ni mnyama aina ya jamii ya swala ambae kwa kiingereza anaitwa “Deer” kwa jina la kisayansi huitwa “Cervidae” nimnyama mwenye uwezo wa kuishi kati ya miaka 15-25 mnyama huyu amesifiwa kuwa na mbio na miguu mwepesi,  katika maandiko kwa vile anauwezo wa kukimbia kati ya speed 60-80 km/h yaani mbio kati ya kilomita sitini mpaka themanini kwa saa, pia ni mnyama hodari katika uwezo wa kuruka na kukwepa vihunzi vya aina mbalimbali, anauwezo wa kukimbia katika nyika na kuruka kwa madaha kutokana na wepesi wa miguu yake, na kwa vile Mungu amemuumba Kulungu kuwa mwepesi na mwenye uwezo wa kutokomea kwa haraka Adui zake hukata tamaa katika kumfuatilia, kwani ni vigumu kumpata na anaweza kupita katika eneo lolote ambalo kwa wanyama wengine linaweza kuwa ni lenye kuleta changamoto.

Kulungu au ayyala wanapenda sana kuishi milimani na kwenye majabali wawapo nyikani au mwituni hii humsaidia kuweza kuona maadui kwa mbali, lakini pia katika majabali huwa anakuwa mwepesi zaidi kuliko katika matope, Daudi alikuwa na ujuzi kuhusu Kulungu kwa vile aliishi nao katika milima yao wakati akimkimbia Sauli, ISamuel 24:2, "Ndipo Sauli akatwaa watu elfu waliochaguliwa katika Israeli wote, akaenda kumtafuta Daudi na watu wake juu ya majabali ya mbuzi-mwitu."    

Aidha kulungu aliwekwa katika orodha ya wanyama safi wasio najisi Kumbukumbu 14:4-5. “Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima;”   
           
Adui zake wakubwa ni Simba, Dubu na Chui, ambao humwinda na kumfanya kuwa kitoweo, kwa ujumla ni mnyama mzuri sana na pia kama ukipata nafasi ya kula nyama yake ni tamu sana ayala hufananishwa na mke mzuri wa halali.

Sifa kuu za Kulungu.

Kulungu ni mnyama wa nane Duniani kwa mbio
1.       Baada ya mnyama aina ya chui au cheter ambaye ana uwezo wa kukimbia kwa kasi zaidi ya 110-120 km/h mnyama anayefuata kwa nafasi ya nane katika mbio  ni Kulungu 60-80 km/h sawa sekunde 0.016 kwa kilomita moja. Kwa msingi huo sifa kubwa ya mnyama huyu ni wepesi  Inyakati 12:8Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa WEPESI kama kulungu juu ya milima;

Habakuki 3:19YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya MIGUU YANGU KUWA KAMA YA KULUNGU, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.”
2Samuel 2:18Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa MWEPESI WA MIGUU KAMA KULUNGU.”

2.       Kulungu ni mnyama mzuri sana na hivyo sifa zake hufananishwa na mwanamke mrembo  wa wakati wa ujana, Mithali 5:18-19Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.”

3.       Kulungu hupenda kukaa juu, ni mnyama mwangalifu sana kwaajili ya kujikinga na maadui na kujilinda wakati wote huhakikisha usalama wake na maisha yake ni ya muhimu sana  Zaburi 18:33MIGUU YANGU ANAIFANYA KUWA YA KULUNGU, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.”

4.       Kulungu wanajua kufurahi wakati wanapokuwa na amani, wana ujuzi wa kuruka ruka kwa furaha Isaya 35:6Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani.”

5.       Kulungu wanapenda sana maji, alisema mtaalamu mmoja njia pekee ya kuwavutia Kulungu, au ayala ni kuwapatia maji ya kunywa, Zaburi 42:1-5Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako. Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu. Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu

Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu!

Ni muhimu kufahamu kuwa Nabii Habakuki alinukuu maneno ya mfalme Daudi Habakuki 3: 19 ““YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya MIGUU YANGU KUWA KAMA YA KULUNGU, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.”

Inafanana na Zaburi 18:31-40 “Maana ni nani aliye Mungu ila Bwana? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu? Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.  Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza. Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza. Nitawafuatia adui zangu na kuwapata, Wala sitarudi nyuma hata wakomeshwe. Nitawapiga-piga wasiweze kusimama, Wataanguka chini ya miguu yangu. Nawe hunifunga mshipi wa nguvu kwa vita, Hunitiishia chini yangu walioniondokea. Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo, Nao walionichukia nimewakatilia mbali.”

Mwandishi wa Zaburi Pamoja na Nabii Habakuki wanarudia umuhimu wa mtu anayemtegemea Mungu
1.       Kwamba ukimtegemea Mungu yeye anageuka kuwa chanzo cha nguvu zako, anakufanya kuwa mwepesi dhidi ya adui zako, anakuweka juu Mahali palipoinuka ili uweze kuwaona na kuwasanifu
2.       Anaifanya njia yako kuwa kamilifu, anakusaidia usijikwae anakuwekea wepesi, ananyoosha mapito yako miguu yako inakuwa mwepesi kukwepa vohuzi vya kila aina ya adui,
3.       Anakuweka mahali pa juu, palipoinuka anazungumzia ushindi, heshima katika jamii, anakupa uwezo wa kuona vikwazo na kuvikwepa anakupa uwezo wa kuzijua hila za adui na kuzizima au kuzikimbia anakupa namna ya kwenda bila kupata madhara, utakuwa unapita juu ya hatari na unaziangalia kwa chini na adui zako ni ngumu kukupata.
4.       Bwana na akupe neema ya kuifanya Miguu yako kuwa kama ya Kulungu katika jina la Yesu Kristo. Bwana na akufanyie wepesi katika kila unalolifanya mwaka huu mpya, Bwana na akupe wepesi dhidi ya adui zako, bwana ana akupe njia na kukuweka mahali pa juu

Kulungu ni alama ya:-
·         Usafi/utakatifu – utaishi kwa mafanikio bila kulaumiwa na mtu utajikinga na maadui zako
·         Ibada/kiu na njaa ya haki/uhitaji wa Mungu - Mungu ndiye tegemeo lako tamani kudumisha uhusiano na Mungu
·         Ulinzi wa Mungu, miguu yao haitelezi, Mungu atakulinda usijikwae usianguke katika mitego ya adui
·         Mapenzi – Onyesha kumjali na kumuheshimu kila mmoja
·         Furaha – shetani hupenda sana uwe na huzuni Furaha ya bwana ndio nguvu zetu usihuzunike furahi katika bwana siku zote
·         Wepesi katika kazi, katika kukwepa mitego ya adui – Mungu akufanyie wepesi katika kila ulifanyalo
·         Kukaa katika amani na salama./mahali palipoinuka. – Mungu akupe akili ya kujihadhari na maadui zako
·         Mungu akupe pembe mpya, njia mpya na mbinu mpya unapokuwa umechoshwa na maswala ya zamani, usiangalia nyuma songa mbele.

Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.
Rev. Innocent Kamote.

Maoni 24 :

  1. Nimependa kuusu kulungu..nimesoma Leo Ila kwa nimesoma na hii nimeelewa zaidi nashkulu Mungu awazidishe

    JibuFuta
    Majibu
    1. Hakika,ninamtukuza Mungu kwaajili yenu,nilihitaji ufahamu huu kwa majira haya,Mungu mwema awape hatua zaidi

      Futa
  2. Ooh thank you made me aware

    JibuFuta
  3. Barikiwa sana Mtumishi.Nime elewa hii maana ya Kulungu ktk biblia

    JibuFuta
  4. Ubarikiwe mtumishi Kwa udadavuzi huu wa mnyama huyu kibiblia ndiyo maana biblia ni msitu mnene nimeongeza maarifa Leo.

    JibuFuta
  5. Barikiwa sana mtumishi wa Mungu, hakika nimejifunza jambo kubwa sana

    JibuFuta
  6. Barikiwa Sana mtumishi kwa kunifumbua kuhusu mnyama huyo nilikuwa cjui anything kuhusu kulungu

    JibuFuta
  7. Ubarikiwe sana na Bwana Yesu Kristo kwa ufafanuzi mzuri kuhusu kululunga, nimebarikiwa na nimejifunza.

    JibuFuta
  8. Asante kwa maarifa haya nimepata vingi 🙏

    JibuFuta
  9. New knowledge in my head🤌 nimependa Kaka a FOOD OF THOUGHT

    JibuFuta
  10. Nilitamani kujua nimejua

    JibuFuta
  11. Nilitamani kujua nimejua

    JibuFuta
  12. Nimejifunza kitu kikubwa sana. U barikiwe

    JibuFuta
  13. Kwa kweli nimependa ufafanuzi huu

    JibuFuta
  14. Nimejifunza mengi Sanaa mungu anifanyie wepesi Nitshill kama kulungu

    JibuFuta
  15. Somo zuri sana

    JibuFuta
  16. Nimeelewa kwa undani maana ya Kulungu, umeongezea na picha, basi umefanya vema sana; Neema ya Mungu ikufunike kwa huu ufunuo, Mungu wa Mbinguni ashukuliwe kwaajili yako, Amina

    JibuFuta
  17. Nimeelew ubarikiwe sana

    JibuFuta
  18. Nimeelewa sasa ubarikiweee

    JibuFuta
  19. Ameni barikiwa mno

    JibuFuta
  20. Asante sana Kwa somo zuri Namuomba Mungu anifanye niwe na sifa njema kama kulungu

    JibuFuta
  21. Hasante kwa kwa tafsiri ya jina kulungu

    JibuFuta
  22. Asante sana Kwa mafundisho yaliyosheheni maandiko matakatifu
    Barikiwa Sana mtumishi

    JibuFuta
  23. MUNGU akubariki sana mtumishi kwa somo zuri ambayo limeongeza kitu kingine leo katika uelewa wangu wa maandiko na somo la biblia asante sana kwa kazi nzuri barikiwa

    JibuFuta