Zaburi 119:9 “Jinsi gani kijana
aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.”
Ni muhimu kufahamu kuwa mojamya
maswali muhimu sana ya kujiuliza au yaliyopatwa kuulizwa katika maandiko ni
pamoja na swali hili Jinsi gani kijana aisafishe njia yeke! Swala hili ni nyeti
na muhimu mno ni swali la kifalasafa, Katika zaburi hii ya Hekima mwandishi
anataka kutuonyesha wazi kuwa mwanadamu anapaswa kuishi maisha yanayompendeza
Mungu katika maisha yake yote,lakini katika wakati wote wa maisha ya mwanadamu
hakuna kipindi hatari kama kipindi cha ujana kwa hiyo mwandishi ni kama
anaziona changamoto za vijana na kisha anahoji akiangalia wakati tulio nao na
changamoto walizo nazo vijana Mwandishi wa zaburi hii ni kama anauliza, Je
kijana anawezaje kuishi maisha matakatifu kivitendo katika wakati huu wa sasa?
Ni kijana moyo wa wakati wa ujana unawaka sana , Shauku ya vijana iko juu
lakini wakati huohuo maarifa yao bado ni machanga na pia hawana ujuzi au uzoefu
sasa anawezaje kwenda sawasawa ni wakati gani wa kujiuliza swali hili la
muhimu? Je ni wakati ambapo tumezeeka au wakati ambapo tumeshakosea sana?
Wakati wa ujana ndio wakati muhimu sana wa kujiuliza swali hili ndio wakati wa
kuchagua njia itakayokufaana kuiendea , ili kijana asifanye makosa kama makosa
yaliyofanywa na wengi waliotutangulia, njia ya kijana ndio inayowindwa zaidi
ili iharibike, ni vijana ndio ambao wana muda mrefu zaidi wa kukabiliana na
magumu, vikwazo na changamoto, watakuaje na furaha je ni kwa kusubiri waharibu
katika ujana wao kisha waje wajute katika uzee wao, wanawezaje kutembea katika
njia ya haki? Je mwanzoni mwa maisha yao, au siku zote za maisha yao au mpaka
wakati wakiwa wazee? Wanakabiliwa na
magumu sasa ili njia yao iweze kuwa njema tangu awali wanapaswa kutii na
kulifuata neno la Bwana!
Neno la Mungu lina ushauri mwingi
na wa kutosha namna na jinsi vijana wanavyopaswa kuenenda, Biblia inamtarajia
mtu mzee kuwa mwenye hekima kubwa kutokana nay ale aliyojifunza wakati wote wa
maisha ya ujana wake, Mzee anapaswa kuwa mwalimu wa vijana Mithali 20:29 “Fahari ya vijana ni nguvu zao,
Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.” Biblia inapotaja mvi
inamaanisha ukomavu katika ujuzi na uzoefu unaoweza kuwafaa wengine na nguvu ni wakati wa kutenda vijana
wanapaswa kuyatendea kazi maneno ya Mungu na ushauri wake katika neno la Mungu
ambao utawapa mwelekeo utakawaosaidia katika maisha yao yote.
Mstari wa msingi una mambo makuu mawili hapa;-
·
Jnsi gani
kijana aishafishe njia yake ni swali linaloulizwa toka kwa vijana
·
Kwa
kutii, akilifuata neno lako anajibu mtu mwenye hekima
Msingi wa kwanza na ambao ni wa muhimu kwanza ni lifuata neno la Mungu:
a. Neno
la Mungu lina utoshelevu wa ajabu sana wa kuifanya njia ya kijana na mtu yeyote
yule kuwa njema, Neno la Mungu lina nguvu ya kutosha katika kuyaongoza maisha
yetu na kutuondolea vikwazo, lina uwezo wa kututia nguvu na kutufariji na
kutupa msaada wa namna na jinsi inavyotupasa kuenenda hata tukahitimisha maisha
haya tukiwa wenye furaha ya ajabu na kuwa walimu wenye busara wakati wa uzee
wetu.
1. Kumcha Bwana ndio chanzo cha maarifa
Mithali 1:7, “Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau
hekima na adabu.” Mithali 9:10-11, ”Mwelimishe
mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi
kuwa na elimu; Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.”
Mithali 15:33 ” Kumcha Bwana ni maonyo ya hekima; Na kabla ya heshima
hutangulia unyenyekevu.” Kumbe basi mtu awaye yote anayetaka
kufanikiwa katika njia yake ni lazima kwanza awe anamcha Mungu, awe mtu wa
ibada anayemuabudu Mungu, awe mtu anayeishi kwa hofu ya Mungu, Mungu hapaswi
kuwa kichaka cha kujichimbia na kuishi kama tunavyotaka Mungu ni lazima apewe
kipaumbele cha kwanza katika maisha ya mtu awaye yote na katika ujana wetu hii
ndio msingi wa maarifa mema yatakayotusaidia katika maisha yetu ili baadaye
tusijute tusiyadharau maonyo na hekima
na adamu tukawa wapumbavu.
2. Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako
Muhubiri 12:1-7
“Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla
hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina
furaha katika hiyo. Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza;
Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;
Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetema; Hapo wenye nguvu
watakapojiinamisha; Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba; Na hao wachunguliao
madirishani kutiwa giza; Na milango
kufungwa katika njia kuu; Sauti ya kinu itakapokuwa ni ndogo; Na mtu kusituka
kwa sauti ya ndege; Nao binti za kuimba watapunguzwa; Naam, wataogopa
kilichoinuka Na vitisho vitakuwapo njiani; Na mlozi utachanua maua; Na panzi
atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka; Maana mtu aiendea nyumba
yake ya milele, Nao waombolezao wazunguka njiani. Kabla haijakatika kamba ya
fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; Au mtungi kuvunjika kisimani; Au gurudumu
kuvunjika birikani; Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho
kumrudia Mungu aliyeitoa.”
Neno la Mungu linatuasa kwamba wakati wa
kumchua Mungi ni sasa, hatuwezi kusubiria mawazo ya kijinga sana kufikiri kuwa
tuna muda wa kutosha duniani, ni mawazo ya kijinga kusubiri umche Mungu
utakapokuwa mzee, ni uzembe kusubiri wakati ambapo hata biblia itakuwa taabu
kuisoma, ni ujinga kusubiri wakati ambapo hata kuhudhuria mikesha itakuwa tabu
kwako, ni ujinga kusubiri meno memomonyoka ndio umkumbuke Mungu, lakini neno la
Mungu pia linatuonya kuwa mtungi unaweza kuvunjikia kisimani, yaani ule wakati
wa muhimu tunaoufikiri lolote laweza kutokea na ukashindwa kutii kiu ya kumcha
Mungu ambayo uneiamua leo lakini ikaishia njiani Neno la Mungu linazidi
kutuonye kuwa tunaweza kufikiri kuwa wakati wa ujana ndio wakati wa kujipa raha
na kujifanyia lolote tunalopenda kulifanya ni wakati wa kuupa moyo wako lolote
unalopenda kuupa ni kweli lakini lazima ukumbuke yuko Mungu atakayekuhukumu kwa
kila utakalolifanya na ndipo utakapokumbuka kuwa ujana nao ni ubatili na utu
uzima pia heri usingepoteza muda wako
Muhubiri
11:9-10 “Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo
wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika
maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu
atakuleta hukumuni. Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya
mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.”
3. Fuata njia ya Mungu
Maandiko bado yanawaasa vijana kufuata njia ya Mungu
kwamba nnia ya Mungu itakupa kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu na
italeta mafanikio makubwa sio hivyo tu itakupa maisha marefu na yenye furaha
Mithali 3:1-4 “Mwanangu, usiisahau sheria yangu,
Bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka
ya uzima, na amani. Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako;
Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,
Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu” Vijana wanaonywa na wenye
hekima kwamba wafuate njia za Mungu katika wakati huu wa sasa inaweza kuonekana
kuwa ni jambo la kipuuzi na la kijinga na ushamba kuishi katika njia ya Mungu
lakini neno lake linatuasa tumfuate nah ii itatupa kupendwa na Mungu na
wanadamu na kufanikiwa ni lazima tuliweke neno la Mungu ndani yetu na
kuhakikisha kuwa limekaa kwa wingi na kuwa ndilo linalotuongoza akijibu swali
alilojiuliza mwandishi wa mashairi yanzaburi ya 119 ana jijibu kuwa ili kija a
afanikiwe ni muhimu na lazima afanye yafuatayo Zaburi 119:10-12 “Kwa moyo wangu wote
nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka
neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Ee Bwana, umehimidiwa, Unifundishe amri
zako” Ni vijana wangapi leo wanaweza kuweka nadhiri kama hii?
Wanaweza kuamua kwa moyo wao wote kumfuata Mungu? Wanaweza kukubali kunyenyekea
chini ya mkono wa Mungu na kukubali kujifunza maagizo yake na kulitunza neno ma
Mungu moyoni mwao na kuiogopa dhambi? Nani anaweza kukubali leo kufundishwa
amri za Mungu, watu wanaweza kuwa na bidii kujifunza mambo mengine mpaka
wanayaweza lakini ni wachache wanaweza kuwa na bidii ya kujifunza neno la Mungu
na mari zake.
4. Mtumaini Mungu katika njia zako zote.
Moja ya tatizo kubwa sana kwa jamii ya vijana ni
pamoja na kumuamini Mungu kumtegemea yeye katika njia zetu zote hii nayo ni
habari nyingine usifikiri ni rahisi kumtegemea Mungu katika njia zetu zote
usidhani ni rahisi Lakini ili tuweze kufanikiwa ni lazima tumtegemee Mungu Mithali 3:5-6 “Mtumaini
Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye
atayanyosha mapito yako.” Mtumaini Bwana lugha njyingine ya kibiblia
ni mtegemee Bwana trust him, ushindi wa mwanadamu yeyote yule ahata ka ahayuko
sahihi uko katika kumtegemea Mungum bilia inaonyesha kuwa kuna baraka kubwa
sana kwa mtu anayemtegemea Mungu na kuna laana kwa mtu anayemteemea mwanadamu,
kumtegemea mwanadamu ni pamoja na kujitegemea wewe mwenyewe badala ya Mungu
Kumtegemea Mungu kuna baraka kubwa sana
Yeremia 17:5-7 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule
amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake
amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema;
Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana
atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto;
Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala
hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.” Kumtumaini
Bwana kunalipa hususani wakati wa ujana Biblia imejaa mifano kibaoya vijana
waliomtumaini bwana na Mungu hakuwaacha labda walikuwa wamejifunza Zaburi 125:1 “Wamtumainio
Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.” Shadrak,
na Meshack na Aberdnego walikuwa ni mifano ya vijana waliomtegemea Mungu na
kamwe hawakuwahi kuytikisika katika imani yao kwa Mungu je ni wakati gani siisi
nasi tunaweza kuiga mfano wao je tutasubiri tukiwa wazee? Tutasubiri tukiwa
tumechoka? Lazima tuithibitishie Dunia kuwa sisi ni watu wa tofauti na kuwa
tumemtegemea yeye tangu utoto wetu. Kila
jambo gumu lilipotokea wao pamoja na Daniel waliutafuta uso wa Mungu
walifunga na kuomba waliyatafuta mapenzi ya Mungu walkionyesha wazi kuwa wao
hawakuwa na tegemeo lingine lolote isipokuwa Yehova tu Nguvu yao ya ujana waliyoiwekeza katika
kumtegemea Mungu ilifanya watu wote wamuamini Mungu wao Daniel 3:1-30 “Nebukadreza, mfalme, alifanya
sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake
dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.
Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na
makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote,
ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza
aliyoisimamisha. Ndipo maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza
hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili
kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya
ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele
akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, wakati
mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na
zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu,
mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa
saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao. Basi wakati huo, watu wa kabila zote
walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na
zomari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu
ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Basi baadhi ya Wakaldayo
wakakaribia, wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi. Wakajibu, wakamwambia mfalme
Nebukadreza, Ee mfalme, uishi milele. Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba
kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na
santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile
sanamu ya dhahabu; na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuru ya
moto uwakao. Wako Wayahudi kadha wa
kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki,
na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako,
wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. Basi Nebukadreza akatoa
amri kwa hasira na ghadhabu, waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego.
Basi wakawaleta watu hao mbele ya mfalme. Nebukadreza akajibu, akawaambia, Enyi
Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu
wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi sasa, kama mkiwa
tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na
santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu
niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika
tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono
yangu?
Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu,
wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili.Kama
ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto;
naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme,
ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya
dhahabu uliyoisimamisha. Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake
ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie
moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto. Kisha akawaamuru
baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego,
na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. Basi watu hao wakafungwa,
hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine,
wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. Basi kwa sababu amri
ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule
moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Na watu
hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa,
katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Ndipo Nebukadreza akastaajabu,
akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu
watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli,
Ee mfalme. Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa,
wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni
mfano wa mwana wa miungu. Kisha Nebukadreza akaukaribia mdomo wa ile tanuru
iliyokuwa inawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na
Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na
Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto. Na maamiri, na manaibu, na
maliwali, na mawaziri, waliokuwa wamekusanyika pamoja, wakawaona watu hao, ya
kuwa ule moto ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao
hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata
hata kidogo. Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na
Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake
waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili
wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe. Basi mimi
naweka amri ya kuwa kila kabila ya watu, na kila taifa, na kila lugha,
watakaonena neno lo lote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki,
na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa
hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.Kisha mfalme akawakuza Shadraka,
na Meshaki, na Abednego, katika wilaya ya Babeli.”
5. Kubali maonyo.
Ndugu hekima ujuzi na maarifa haviji hivi hivi wakati
mwingine ni lazima ukubali kuonywa lazima ujue kuwa katika maisha kuna maonyo,
hatupaswi kupuuzia maonyo, tukipuuzia maonyo tutakuwa wapumbavu, neno la Mungu
linatutaka tuwe watu wenye kupenda maonyo na tusiyadharau yanapokuja kwetu Mithali 1:7 “Kumcha
Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.” Biblia
inaonyesha kuwa wapumbavu hudharau maonyo kuonywa ni sehemu ya maisha
yanayotufanya tukae katika njia iliyonyooka, tuwapo duniani tutapokeamaonyo
kutoka katika maeneo na mazingira mbalimbali tutaonywa na wazazi wetu
Mitahli 1:8-9 “Mwanangu, yasikilize mafundisho
ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,Kwa maana hayo yatakuwa kilemba
cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako” unaweza kuona pia
katika Mithali 4:1-5 “Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio
mpate kujua ufahamu. Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu.
Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu. Naye
akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu
ukaishi. Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya
kinywa changu” unaweza nkuona npia katika Waebrania 12:5-11 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na
wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa
naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana
amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana;
maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa,
ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa
halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi;
basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni
hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye
kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu wakati wake
haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao
waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.” Jamii yoyote au mtu
nawaye yote aliyedekezwa au kukulia katika familia yenye kudekeza watoto
anaweza kujikuta anaharibikiwa na awaye yote ambaye amekulia katika jamii ya
watu wenye kupokea maonyo unatewe kuona kuwa maisha nyanaweza yasimsumbue ,
ndio maana neno la Mungu linatutaka tusiyaouuzie maonyo ni lazima tukubali
kuonywa ndani ya maonyo kuna uzima, maonyo ni muongozo, maonyo ni ulinzi maonyo
ni unabii, maonyo ni nuru wakati wa giza, yatakuepusha na majanga mengi ya
kutisha Kama mtu anakupenda kweli upendo wa kweli utadhihirika vilevile kupitia
maonyo Mithali 13:24 “Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye
ampendaye humrudi mapema.”
6. Usifungiwe nira na wasioamini
2 Wakoritho
6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa
jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena
pana shirika gani kati ya nuru na giza?Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo
na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena
pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu
la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na
kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa
hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho
kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu
wanangu wa kiume na wa kike”, Namna nyingine ya kuishafisha njia
yako kama kijana ni kuhakikisha kuwa haufungiwi nira na asiyeamini, yaani
lazima uangalie wale wanaokuzunguka na unaowafanya kuwa washirika wako wa
karibu kuwa ni watu wa namna gani, biblia inaonyesha kuwa wawili hawawezi
kuambatana pamoja wasipopatana Amosi 3:3
“Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa
wamepatana?” ni lazima uhakikishe kuwa unavunja mapatano na watu
wasiofaa, kama mtu sio wa imani yako ni muhimu kuhakikisha kuwa unavunja naye
urafiki biblia inakataza hata kuoa mtu asiye wa imani yako Kumbukumbu la Torati 7:1-4 “Bwana, Mungu wako,
atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke
mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi,
na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; wakati Bwana, Mungu
wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe
kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao; binti yako
usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. Kwa kuwa
atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo
itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.” Mungu
aliweka wazi wazi kabisa sababu ya kutokuwaona au kuwaoza vijana kwa watu wasio
wa imani yako kwa sababu watakuongoza katika kuiabudu miungu mingine, sio hivyo
tu watu waliokaidi amri hii Mungu alihakikisha kuwa wanapata taabu maisha yao
yote kwa wanawake hao au wanaume hao kuwa miiba mbavuni mwao Yoshua 23:12-13 “Lakini
mkirudi nyuma kwa njia yo yote na kushikamana na mabaki ya mataifa, yaani,
mataifa haya yaliyobaki kati yenu, na kuoana nao, na kuingia kwao, nao kuingia
kwenu; jueni hakika ya kuwa Bwana, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa haya
mbele ya macho yenu, bali watakuwa mtego kwenu na tanzi, na mjeledi mbavuni
mwenu, na miiba machoni mwenu, hata mtakapoangamia na kutoka katika nchi hii
njema, ambayo Bwana, Mungu wenu, amewapa ninyi.” unaweza kuona pia
katika Waamuzi 2:1-3 “Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda
Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami
nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele
sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi; nanyi msifanye agano lo lote na
hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia
sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani? Basi kwa ajili ya hayo mimi
nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba
mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu.” Biblia sio tu
imetukataza kufungiwa nira na wasioamini lakini pia inahoji kuna urafiki gani
kati ya Haki na nuasi? Tena Pana shirika gani kato ya nuru na giza, tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na
beliari na tena aaminiye ana ehemu gani
na yeye asiyeamini na tena pana patano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu?
Watu wengi sana wameingia katika migogoro na matatizo yasiyokwisha hata kwa
maombi kwa sababu ya kufungiwa nira na wasioamini, kimsingi biblia imeonya
vikali kuwa asiyeamini hana nafasi kwa aaminiye, jambo hili limepuuziwa na
kanuni hii imekiukwa kimsingi wanapochanganyika watu wasiomcha Mungu na
wanaomcha Mungu wasiomcha Mungu ndio watakaonyonywa kiroho na kuisha kabisa,
hata uwe na hekima kiasi gani utageuzwa moyo, watu watakupima na jinsi
ulivyokuwa mwanzo na ulivyo sasa baada bya kufungiwa nira na mtu asiyeamini na
itabainika wazi kuwa umekwisha kwa sababu ya kufungiwa nira na wasioamini 1Wafalme 11:1-6 “Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi
wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa
Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa
Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu
kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. Akawa na wake mia
saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. Maana
ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu
mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa
Daudi baba yake. weweKwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa
Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni
pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.”
Vijana wengi leo ukiwaambia usiolewe na huyo au usioe huyo sio wa imani yako
hawataki hata kusikia, huyu n hajaokka wewe umeokoka achana naye hawataki
kusikia wanafikiri kuwa watawaweza Sulemani na hekimayake yote aligeuzwa maoyo
na dhambi yake ikawa tatizo la Israel kwa muda mrefu sana, Wako wengine wana
madai ya kimaandiko kwamba Mbona Rahabu alikuwa kahaba lakini aliolewa na
Muislaeli au mbona Ruth alikuwa mmoabu lakini aliolewa na Boazi? Ilivyo ni kuwa
wanawake hao waliingia katika mkutano wa watu wa Mungu kwa sababu walimuamini
Mungu wa Israel angalia Yoshua 6:25
“Lakini Yoshua
akamhifadhi Rahabu, yule kahaba, na watu wa nyumba ya baba yake, na vitu vyote
alivyokuwa navyo; naye akakaa kati ya Israeli hata leo; kwa sababu aliwaficha
wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko.“ Kwa
nini Yoshua alimuhifadhi hai kahaba Rahabu ambaye baadaye anatajwa kuolewa na
watu wa Yuda na kuja kuwa Bibi za Yesu Kristo sababu kubwa ni kuwa alimuamini
Mungu wa Israel alifanya maamuzi magumu kwa imani Yoshua 2:9-13 “akawaambia wale wanaume, Mimi najua ya kuwa Bwana amewapa
ninyi nchi hii, na ya kuwa hofu imetuangukia mbele yenu, na ya kuwa wenyeji
wote wa nchi wanayeyuka mbele yenu. Maana tumesikia jinsi Bwana alivyoyakausha
maji ya bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo
mliyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa huko ng'ambo ya Yordani,
yaani, Sihoni na Ogu, mliowaangamiza kabisa. Na mara tuliposikia hayo mioyo
yetu iliyeyuka, wala haukusalia ujasiri wo wote katika mtu awaye yote, kwa
sababu yenu; kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, katika mbingu juu na
katika nchi chini. Basi sasa, nawasihi, niapieni kwa Bwana, kwa kuwa
nimewatendea ihisani, ya kwamba ninyi nanyi mtaitendea ihisani nyumba ya baba
yangu; tena nipeni alama ya uaminifu; ya
kwamba mtawaponya hai baba yangu na mama yangu, na ndugu zangu wanaume na
wanawake, na vitu vyote walivyo navyo, na kutuokoa roho zetu na kufa.’’
Ni katika hali kama hii ambapo Rahabu
alionyesha imani na badiliko gumu la kiimani aliweza kukubalika katika jamii ya
Israel na ndivyo ilivyokuwa kwa Ruthu, angalia maneno ya Ruthu utaweza kuna
kuwa aliamini na kuongoka na kuwa miongoni mwa hao waaminio kutokana na imani
yake kwa Mungu wa Israel aifanya maamuzi magumu
Ruthu 1:16-18 “Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane
nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa
watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; Pale utakapokufa nitakufa nami,
Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga
wewe nami. Basi alipomwona kuwa amekaza nia yake kufuatana naye, aliacha kusema
naye.” Unaona kwa msingi huo basi haiwezekani kuwa na ushirika wa
ndani na mtu asiyeamini, tunapozungumzia ushirika wa ndani maana yake ni kama
kuungwa kwa agano mfano wake halisi ni ndoa, au maagano au mikataba na hususani
ile inayowafungamanisha kwa nafsi na imani
, ili kijana aishafishe njia yake isijekuwa ya majuto hana budi
kulizingatia hilo.
Hivyo basi :-
a.
Mithali
1:10 Mwanangu,
wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali.
b.
Mithali
1:15 Usiambatane
nao Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito
yao.
c.
Mithali
4:14-15 usiifuate njia yao “Usiingie katika njia ya waovu, Wala usitembee katika njia ya
wabaya. Jiepushe nayo, usipite karibu nayo, Igeukie mbali, ukaende zako”
d.
Kwa nini
Mungu hakutaka mchangamano na mataifa? Wasioamini
i.
Kwa nini tusifungiwe nira na wasioamini? Hii
maana yake ni nini? Neno la Mungu halimaanishi kuwa tujitenge na watu wa dunia
hii kwani hapo ingetulazimu kuhama duniani, Lakini Mungu anamaanisha kuwa watu waliamini ni jamii tofauti kabisa na
wasioamini na kwa jinsi hiyo hatupaswi kufanya au kuishi kwa mfano wao Zaburi 1:1 “Heri
mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia
ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.”
ii. Hatupaswi kutenda sawa sawa na watu
wasioamini Kumbukumbu 22:10 “Usilime kwa ng'ombe na punda wakikokota jembe pamoja.”
iii. waamini
ni taifa takatifu, ukuhani mteule na watu wa miliki ya Mungu 1Petro 2:9-12 “Bali
ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya
Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie
katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa
la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. Wapenzi,
nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na
roho. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa
watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya
kujiliwa”
kwa msingi huo
huwezi kuwa sawasawa na mtu asiyeamini,lazima uwe tofauti
a. Wewe ni mwenye haki wao ni waasi
b. Wewe ni nuru wao ni giza
c. Wewe ni wa Kristo wao ni wa Beliari
(Shetani) wa yule muovu
d. Wewe ni muamini yeye ni asiyeamini
e. Wewe ni Hekalu wao ni sanamu
Kwa hiyo hatuwezi kufungamana katika agano (Covenant)
na moja ya maagano yaliyo wazi ni kuoana nao.
Waefeso 5:11 “Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali
myakemee”
Usikubaliane na
uovu au waovu Warumi 1:32 “ambao wakijua sana hukumu ya
haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo,
wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”
Wala
usiifuatishe namna ya dunia hii Warumi 12:2 “Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate
kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”
7. Jaa neno la Mungu!
Zaburi 119:11
“Moyoni mwangu
nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.” Mwandishi wa Zaburi hii anaonyesha kuwa
namna nyingine ya kijana kuisafisha njia yake ni kuliweka neno la Mungu Moyoni,
kuyakumbuka maagizo ya bwana Neno la Mungu likijaa moyoni mwetu ni vigumu
kukengeuka na kumtenda Mungu dhambi, Neno la Mungu litatupa ufahamu wa jambo
lipi ni jema na jambo lipi ni baya na kama ni baya ni baya kwa kiwango gani,
Ushindi mkuwa katika maisha yetu ya ujana utategemea kujaa kwetu neno, Maisha
yetu na mafanikio yetu yamefungwa katika maagizo ya Mungu wetu Yoshua 1:5-8 “Hapatakuwa
mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama
nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia
wala sitakuacha. Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha
watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na
ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa
mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate
kufanikiwa sana kila uendako. Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,
bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa
na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako,
kisha ndipo utakapositawi sana.” Unaweza kuona pia 1Wafalme 2:1-3 “Basi siku ya kufa
kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema, Mimi naenda njia
ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume; uyashike mausia
ya Bwana, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri
zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati
ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;”
Lazima vijana tuhakikishe kuwa tunajaa neno la Mungu, maisha yetu yafurike neno
la Mungu, mwenendo wetu uwe unaongozwa na neno la Mungu, kula neno jaaa neno
mpa aucheue neno la Mungu, ushindi wetu na mafanikio yetu ujae katika neno la
Mungu katika agano jipya tunaelezwa kuwa neno la Kristo na likae kwa wingi
ndani yenu Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima
yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku
mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.” Usisubiri uwe mzee ndipo
ujae neno la Mungu utalihubiria wapi lazima ukubali kujaa neno la Mungu sasa
ili uisafidhe njia yako.
8. Waheshimu baba yako na mama yako!
Zaburi 119:11-19 “Ee
Bwana, umehimidiwa, Unifundishe amri zako. Kwa midomo yangu nimezisimulia
Hukumu zote za kinywa chako. Nimeifurahia njia ya shuhuda zako Kana kwamba ni
mali mengi. Nitayatafakari mausia yako, Nami nitaziangalia njia zako. Nitajifurahisha
sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako. Umtendee mtumishi wako ukarimu,
Nipate kuishi, nami nitalitii neno lako. Unifumbue macho yangu niyatazame
Maajabu yatokayo katika sheria yako. Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche
maagizo yako” Mwandishi
anaonyesha kuwa yuko tayari kujifunza neno la Mungu, yuko tayari kutangaza
lakini vilevile anatamani mafanikio na kuishi maishga marefu, hii haiwezekani
hivi hivi Biblia inaonyesha kuwa ili mtu afanikiwe kuwa na maisha marefu na
kuwa na heri duniani moja ya maagizo muhimu ya Mungu yenye ahadhi hii ni
kuwatii wazazi Kutoka 20:12 “. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa
nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.” Na katika agano
jipya bado neno hili limerudiwa na kukaziwa tena Waefeso 6:1-3 “Enyi watoto, watiini wazazi
wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri
hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika
dunia.” Ni jambo la kushangaza katika nyakati za leo vijana wengi
hawawaheshimu wazazi, wanawadanganya, hawataki maonyo hawataki kuongozwa
wanawaongoza wazazi wao, wanasema uongo wanawaibia na wengine wamelala na mama
zao au baba zao, hii maana yake ni nini huwezi kufanikiwa, huwezi kuifanya njia
yako kuwa safi kama huwatii wazazi nah ii inaweza kuwa pana zaidi ya wazazi
waliotuzaa mtu awaye yote aliyekuzidi umri ni mzazi, awaye yote ambaye anakulea
ni mzazi awaye, walimu ni wazazi ili tubarikiwe ili tuwe na uheri duniani
huitaji kutambika huitaji kwenda kutambikia Mizimu iliyokwisha kufa baba yako
na mama yako wazazi wako ni mzimu tosha wahehimu Kumbu kumbu la Torati 5:16 “Waheshimu baba yako
na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi,
nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.”kumbe
ukitaka kuzidisha siku zako hapa duniani basi wahehimu wazazi, watii tena
biblia inasema watii katika kila jambo na kuwa jambo hili linampendeza Mungu Wakolosai 3:20 “Ninyi
watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza
katika Bwana.” Biblia inatuambia kuwa Yesu ingawa alikuwa na uweza
mkubwa wa uungu ndani yake aliwatii wazazi wake Luka 2:51-52 “Akashuka pamoja nao mpaka
Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.
Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na
wanadamu.” Wewe bado hujawa maarufu kama Yesu, huna lolote lakini
hutaki kuwaheshimu wazazi wako, Mungu ampe neema kila mmoja wetu kuwa na
heshima kwa wazazi wetu ili tupate miaka mingi na heri duniani, tusiwaache
wazazi wetu wakaaibika, tuwatunze, tuwafunike aibu zao tusiufunue utupu wao.
9. Jilinde na kiburi
Zaburi
119:20-22 “Roho yangu imepondeka kwa kutamani Hukumu
zako kila wakati. Umewakemea wenye kiburi, Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo
yako. Uniondolee laumu na dharau, Kwa maana nimezishika shuhuda zako.” Mwandishi
anataka kutuonyesha kuwa ili kijana aishafishe njia yake hana budi kuwa mtu
aliyepondeka, mtu aliyepondeka ni mtu mnyenyekevu, na huku akisema uwakemee
wenye kiburi, na uniondolee dharau, kwa nini ?, moja ya tatizo kubwa sana
linaloweza kuondoa kibali kwa Mungu na kutuharibia nji yetu ni tatizo la kiburi,
Mungu anapoona kuwa tuna kiburi ni rahisi sana kutushughulikia kwa haraka,
kiburi kinaondoa kabisa neema ya Mungu juu yetu. Na kinaondoa kabisa uwepo wa
Mungu kati yetu na kinaweza kutuletea aibu Mithali
11:2 “Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa
na wanyenyekevu” Kwa nini ujitie aibu duniani Biblia imeonyesha njia
iliyo njema na njia hii ni unyenyekevu, na una faida nyingi. Kiburi ni nini?
Kiburi ni hali ya kujiona kuwa uko daraja la juu katika ubora kuliko watu
wengine, ni hali ya kufikiri kuwa unajitosheleza wewe mwenyewe kutokana na
mafanikio fulani, au ngazi ya daraja fulani unalotokea ni kujiamini na kujiweka
katika viwango flani vya kutokuhisi kuwa una mapungufu. Sio rahisi sana
kukielezea kiburi, unaweza kuwa tjiri na mwenye mali nyingi sana na ukawa
mnyenyekevu na unaweza kuwa masikini sana na ukawa na kiburi, lakini hata hivyo
kiburi kinaweza kuletwa na aina fulani ya mafanikio tuliyonayo, kiujuzi,
kielimu, kibiashara na hata katika maisha ya utauwa tunaweza kujihesabia haki.
Mwandishi anajua madhara ya kiburi hivyo anakubali kupondeka na kujinyenyekeza
kwa Mungu Isaya 66:2 “Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote
vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu
aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.”
Habari njema ya ufalme wa Mungu ni rahisi kupokelewa kwa wanyenyekevu,
kwaasili mtu mwenye kiburi hawezi kuipokea injili, habari ya maneno ya Mungu
kwa mtu mwenye kiburi ni upuuzi tu ni
watu wanyenyekevu pekee wanaoweza kupokea habari hii na ninaweza kusema katika
njia iliyo wazi kabisa kuwa Maswala ya Mungu yamedizainiwa maalumu kwa watu
wanyenyekevu Isaya 61:1-2 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia
mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga
waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za
kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha
Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;” so mwandishi anakiona kiburi
kuwa ni chenye madhara na kwa bahati mbaya vijana wengi ndio wanaokubwa na hali
ya kuwa na kiburi na hivyo hatuna budi kujifunza unyenyekevu, Unyenyekevu ni
swala la maamuzi ni swala la kujivika sisi wenyewe Wakolosai 3:12-14 “Basi, kwa kuwa mmekuwa
wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu,
upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya
kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya
hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.” Katika
maswala ambayo watu wanapaswa kujivika ni pamoja na unyenyekevu, si vema
kumuomba Mungu akupe unyenyekevu shule yake itakuwa ngumu mno lakini ni vema
kuamua kujivika unyenyekevu, tusipofanya hivyo tutapoteza neema na Mungu
atatupinga na njia yetu haitakuwa njia iliyonyooka 1Petro 5:5-6 “Vivyo hivyo ninyi vijana,
watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa
sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio
hodari, ili awakweze kwa wakati wake;” Kwa msingi huo basi iwapo
kjana anataka kufanikiwa basi hana budi kumsihi Mungu ampe neena ili asijivune
na akubali kuwahesabu wengine kuwa bora kuliko nafsi yake na kuweza kufanikiwa
katika njia zake, kutii neno la Mungu kunategemeana na namna na jinsi
anavyopaswa kuwa na moyo wa unyenyekevu bwana atupe neena kuwa mbali na kiburi
katika jina la Yesu. Njia ya Mungu ya
kupelekwa juu zaidi ni unyenyekevu, na njia ya kupelekwa chini zaidi ni kiburi Wafilipi 2:3-11”Msitende
neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu
na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo
yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo
ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa
sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana
utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena,
alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti,
naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia
Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu
vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI
BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”
Maandiko yanaonyesha wazi kuwa mtu akijinyenyekeza
Mungu humuinua na mtu akijiinua mUngu humdhili Luka 18:10-14 “Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo,
wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee
Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu,
wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa
zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala
hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema,
Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda
nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye
atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.” Biblia inatuonya kuwa
hatupaswi kujivunia chochote hapa duniani majivuno ni sehemu ya kiburi, wala
hatupaswi kujivunia akili bali tukubali kushughulishwa na mambo manyonge
kukubali kufanya mambo ya nchini Warumi 12:16 “Mpatane nia zenu
ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo
manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.”
10.
Muombe
Mungu “Omba”
Zaburi
119:25-29 “Nafsi yangu imeambatana na mavumbi,
Unihuishe sawasawa na neno lako. Nalizisimulia njia zangu ukanijibu,
Unifundishe amri zako. Unifahamishe njia ya mausia yako, Nami nitayatafakari
maajabu yako. Nafsi yangu imeyeyuka kwa uzito, Unitie nguvu sawasawa na neno
lako. Uniondolee njia ya uongo, Unineemeshe kwa sheria yako.” Wote
tunafahamu umuhimu wa Maombi na wote tunajua namna na jinsi Biblia
inavyotuaguza kuomba bila kukoma na kwama haja zetu zote na zijulikane na Mungu
Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbue
kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na
kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili
zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”
Unaweza kuona sasa mwenye Hekima katika Zaburi hii
anaomba, anajua umuhimu wa kuomba anamjulisha Mungu haja zake
a. Nafsi
yake imeambatana na mavumbi maana yake anaelemewa na huzuni kiasi cha kufa,
nafsi imeinama hana furaha na amani ni kama yuko kwenye maombolezo, kwa hiyo
anamuomba Mungu na Mungu alimjibu, alimpa amani alimuinua alifurahia.
b. Anaomba
Mungu amfundishe amri zake anataka kujua wazo lote la Mungu anatamani kujuujua
moyo wa Mungu yaani kujua mapenzi yake ili aendelee kumtafakari Mungu.
Amfahamishe njia zake na mausia yake ni muhimu kufahamu kuwa neno amri za
Mungu, neno njia na neno sheria na neno hukumu na neno shuhuda limetajwa katika
nzaburi hii mara kadhaa kwa mitindo tofauti
·
Law
(Sheria) The Torah limetajwa mara 25 Katika zaburi hii mwandishi alikuwa
anataka awe na ufahamu wa kutosha kuhusu Torati ya Mungu anaomba apate neema na
ufunuo wa kujua sheria za Mungu kwa sababu zingemfanikisha
·
Word
(Neno) Dabar limetajwa mara 24 Mwansihi akiwa anaomba Mungu amjulishe kila
analolisema akijua kuwa akiyashika maneno ya Mungu atafanikiwa
·
Judgement
(hukumu) Mispatim limetajwa mata 23 akimaanisha kuwa anataka awe na uwezo wa
kuzijua sheria na Mungu na kuzitafakari ili awe na uwezo wa kupambanua mema na
mabaya anakjua kuwa akiwa na uwezo huo atafanikiwa
·
Testimonies
(Shuhuda) Edut/Edot limetajwa mara 23
Matendo makuu ambayo Mungu aliyafanya kati yake na Israel mwenye hekima anajua
kuwa akizitunza shuhuda za Mungu na kuyakumbuka matendo yake makuu atafanikiwa
·
Commandement
(Amri) Miswah/Miswot limetumika mara 22 hiiinawakilisha kufuata utaratibu
wote wa kiadilifu ambao Mungu ameamuru Mwandihi anajua kuwa kuwa akizishika
amri za Mungu atafanikiwa
·
Stutus (Maandiko)
Huqqim limetumika mara 21 likimaanisha imeandikwa au maandiko Mwandishi alikuwa
anataka ayajue maandiko na hivyo akiyajua atafanikiwa
·
Tunapomuomba Mungu kuonyesha kuwa tuna moyo wa
dhati ni muhimu kumuomba Mungu pia kuhusukujizua njia zake sio tu kwaajili ya
kuvunjika kwetu moyo.
c. Pia
anaomba Mungu amtie nguvu, amuondolee njia ya uongo na amneemeshe kwa sheria
yake
Wakati wowote
tunapokuwa na uhitaji wa aina yoyote hatuna budi kuhakikisha kuwa tunamuomba
Mungu, Nafsi zetu zinapolemewa na huzuni kiasi cha kufa ni muhimu kumuomba Mungu, Nafsi zetu
zinapozimia hatuna budi kumuomba Mungu, mwandishi anataka Mungu amrejeshee hali
yake ya kuwa na furaha, Mwandishi anaonyesha kuwa anatubu kwa kumuomba Mungu
amuondolee njia ya uongo. Ni ajabu kuwa mwenye hekima hapa anaonekana kuomba
zaidi mahitaji ya kiroho kuliko ya kimwili, swala hili linaweza kuwa sawa
kabisa na Jinsi Bwana alivyotufundisha kuwa tutafute kwanza ufalme wa Munguna
haki yake yote na mengine yote tutazidishiwa Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme
wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Mwenye hekima
anaonyesha hali ya juu sana ya ukomavu wa kiroho, ni rahisi sana kumuomba
Mungumahitaji yetu ya mwilini kuliko mahitaji yetu ya Rohoni, lakini yeye
anatamani sana kuzijua njia za Mungu, Sheria, shuhuda, amri, maagizo, mausia,
na hukumu zake.
11. Chagua njia ya kweli
(choosing the way of truth) Zaburi 119:29-30 “Uniondolee njia ya uongo,
Unineemeshe kwa sheria yako. Nimeichagua njia ya uaminifu, Na kuziweka hukumu
zako mbele yangu.” Moja ya swala gumu sana Duniani kulikwepa ni
kusema uongo, au kutokufuata njia ya uongo, Mashujaa wengi wa Imani katika
Biblia waliweza kusema uongo mara kadhaa sio rahisi kucha au kuushinda uongo
kwa nguvu zetu, mwandishi anamuomba Mungu amuondolee njia ya uongo, amneemeshe
kwa sheria yake na pia amfanye kuwa mwaminifu ili aweze kujua mema na mabaya,
Vijana wengi sana wanakabiliwa na tatizo hili la kufuata njia ya uongo, uongo
unaweza kutugharimu katika maisha yetu unaweza kuzuia mema katika maisha yetu 1Petro 3:10 “Kwa
maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene
mabaya, Na midomo yake isiseme hila.” Neno hila hapo linamaanisha uongo
kwa mujibu wa asili ya maandiko ambayo
Petro alinukuu kutoka katika Zaburi 34:13 “
Mara kadhaa Biblia
inaonyesha Mashujaa wa imani walisema uongo kwa sababu fulani fulani
a.
Ibrahimu alimnena Sara kuwa ni
Dada yake Mwanzo 20:1-5 “Ibrahimu akaondoka huko kwenda
nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari
Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa
Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto
ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa,
maana ni mkewe mtu. Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee Bwana, Je!
Utaua hata taifa lenye haki? Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na
mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo
wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi”
b.
Isaka
alimnena Rebbecca kuwa ni Dada yake Mwanzo
26: 6-9 “Isaka
akakaa katika Gerari. Watu wa mahali
hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu maana aliogopa
kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa
maana alikuwa mzuri wa uso. Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki,
mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akamwona Isaka anacheza-cheza na
Rebeka mkewe. Abimeleki akamwita Isaka,
akasema, Yakini huyu ni mkeo, mbona ulisema, Ni ndugu yangu huyu? Isaka
akamwambia, Kwa sababu nalisema, Nisife kwa ajili yake.”
Isamuel 21:2, 8 na 1Samuel 27;8-10 “Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia
Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu
Telemu, hapo uendapo Shuri, hata mpaka nchi ya Misri., Tena Daudi akaipiga nchi
hiyo, asimhifadhi hai mume wala mke, akateka nyara kondoo, na ng'ombe, na
punda, na ngamia na mavazi; kisha akarejea na kufika kwa Akishi. Naye Akishi humwuliza, Je!
Mmeshambulia upande gani leo? Na Daudi husema, Juu ya Negebu ya Yuda, au, juu
ya Negebu ya Wayerameeli, au, juu ya Negebu ya Wakeni.” Maandiko yanatutaka tuuvue uongo tuwe
waaminifu tunaweza kabisa kuuondoa uongo kama vile tunavyoweza kubadilisha nguo
Wakolosai 3:5-10” “Basi vifisheni viungo vyenu
vilivyo katika nchi, uasherati,uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani,
ndiyo ibada ya sanamu: kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu. Katika
hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo. Lakini sasa yawekeni
mbali nanyi hayo yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano na matusi
vinywani mwenu. Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na
matendo yake; mkivaa utu upya, unaofanywa upya upate ufahamu sawa sawa na mfano
wake yeye aliyeuumba” Kwa hiyo Kuna umuhimu wa kumuomba Mungu atuondolee
njia ya uongo kwa vile ni vigumu sana kukwepa kusema uongo au kufuata njia za
uongo.
12. Chagua njia ya haki
Zaburi
119:33-40 “Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako,
Nami nitaishika hata mwisho. Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, Naam,
nitaitii kwa moyo wangu wote. Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako, Kwa
maana nimependezwa nayo. Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako, Wala usiielekee
tamaa. Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako.
Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako, Inayohusu kicho chako. Uniondolee laumu
niiogopayo, Maana hukumu zako ni njema. Tazama, nimeyatamani mausia yako,
Unihuishe kwa haki yako.” Aina kama hii ya maombi haiwezi kufanywa
na mtu wa kawaida asiyempenda Mungu tunaona mwandishi hapa anakazia kuwa
anataka au ana kiu ya kujua au kufundishwa njia za Mungu na kuwa yaya
atazishika hata mwisho yeye anajua kuwa ni Mungu pakee anayeweza kubadili mioyo
yetu ikamuelekea yeye kwa uwezo wetu sisi hatuwezi kuzijua sheria za Mungu
lakini kama mioyo yetu ikitaka na tukamuomba Mungu basi Mungu atafanya kazi ile
tuitakayo ndani yetu kutaka kwetu na kutenda kwetu Wafilipi 2:13 “Kwa maana ndiye Mungu atendaye
kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake
jema.”
13. Mungu atuepushe na tamaa
Zaburi
119:36-37 “Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako, Wala
usiielekee tamaa. Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika
njia yako” Ni kama mwenye hekina anajua wazi kuwa Tamaa inaweza kuharibu
njia zake na maisha yake na hivyo anajiombea kwa Mungu kwamba amsaidie moyo
wake usiielekee tamaa neno linalotumika
hapa kwa tamaa katika kiibrania ni “BOICE”
maana yake kwa kiingereza “Selfish gain”
Ubinafsi Biblia imejaa mifano mingi ya watu walioahribiwa na tamaa
a. Balaamu aliwakosesha watu wa Mungu na nasfi
yake kwajili ya tamaa Hesabu 22:2, 2Petro 2:14-16 “wenye
macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo
imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana; wakiiacha njia
iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa
ujira wa udhalimu; lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda,
asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii
yule.”
b. Ahabu 1Wafalme 21:1-13 “Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la
mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa
Samaria. Ahabu akasema na Nabothi, akamwambia, Nipe shamba lako la mizabibu
nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa
badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha
sawasawa na thamani yake. Nabothi akamwambia Ahabu, Bwana apishe mbali nikupe
wewe urithi wa baba zangu. Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito,
tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli,
akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso
wake, akakataa kula. Lakini Yezebeli mkewe akamwendea, akamwambia, Kwa nini
roho yako ina huzuni hata usile chakula? Akamwambia, Kwa sababu nimesema na
Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au,
ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa
shamba langu la mizabibu. Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki
ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba
la mizabibu la Nabothi Myezreeli. Basi,
akaandika nyaraka kwa jina la Ahabu, akazitia muhuri yake, akazipeleka zile
nyaraka kwa wazee, na kwa watu wenye nguvu waliokuwa katika mji wake, waliokaa
pamoja na Nabothi. Akaandika katika zile nyaraka, akasema, Pigeni mbiu ya watu
kufunga, mkamweke Nabothi juu mbele ya watu, mkainue watu wawili, watu
wasiofaa, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme.
Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe. Wale wazee wa mji wake, na
walio wenye nguvu waliokaa mjini mwake, wakafanya kama Yezebeli alivyowaagiza,
kama ilivyoandikwa katika nyaraka alizowapelekea. Wakapiga mbiu ya watu
kufunga, wakamweka Nabothi juu mbele ya watu. Na hao watu wawili, watu
wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia
Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua
nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa.”
c. Achan Yoshua 7:21 “Nilipoona
katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya
dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama,
vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake.”
d. Yuda Yohana 12:6 na Mathayo 26:14-16 Yohana
12:6 “Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini;
bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa
humo.”
e. Gehaz 2Wafalme 5:20-26 “Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema,
Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake
vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu
kwake. Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio
anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani? Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema,
Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana
na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili. Naamani
akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta
mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi
wake wawili; nao wakayachukua mbele yake. Naye alipofika kilimani, alivitwaa
mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda
zao. Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia,
Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali. Akamwambia, Je! Moyo
wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je!
Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni,
na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi?” Anania
na Safira Matendo 5:1-8
Watu wote hapo
juu waliharibikiwa kwa sababu ya tamaa, Mwenye hekina anaiona tamaa kama tatizo
kubwa na kuwa bila msaada wa Mungu kwa vile yeye naye ni binadamu anaweza
kujikuta akiingia katika kuyatendea kazi hayo, Tamaa ni kama mbegu ya dhambi na
kwa sababu hiyo tusikubali ikakomaa, hatuna budi kuishughulikia mapema katika
maisha yetu ili isiweze kuzaa Yakobo
1:13-15 “Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na
Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu
mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na
kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile
dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.” Tamaa inaweza kuifanya njia
yako kutokuwa safi na kuharibumaisha hivyo ni vema kuomba iwe mbali nasi kama
mwenye hekima alivyojiombea.
14. Penda neno la Mungu
Zaburi
119:41-48 “Ee Bwana, fadhili zako zinifikie na mimi,
Naam, wokovu wako sawasawa na ahadi yako. Nami nitamjibu neno anilaumuye, Kwa
maana nalitumainia neno lako. Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe,
Maana nimezingojea hukumu zako. Nami
nitaitii sheria yako daima, Naam, milele na milele. Nami nitakwenda panapo
nafasi, Kwa kuwa nimejifunza mausia yako. Nitazinena shuhuda zako mbele ya
wafalme, Wala sitaona aibu. Nami
nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda. Na mikono yangu
nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari amri zako.
Likumbuke neno ulilomwambia mtumishi wako, Kwa sababu umenitumainisha.”
Mwenye hekima anaonyesha kuwa analitumainia neno na
kuwa hataki neno la Mungu liondolewe kinywani mwake anaonyesha kuwa neno la
Mungu ni kila kitu katika maisha yake atalitii kwa vile litampa uhuru kamili
autakao, anadai hatalionea haya neno, atajifurahisha kwa hilo, huku ni kujitoa
kuliko kukubwa sana katika neno la Mungu, kwa nini mwenye hekima anaonyesha
kulitumainia neno la Mungu?
a. anasema linauhisha (Preserve, nourish) Zaburi
119:25,37, 107
b. Linaleta tumaini (gives hope) Zaburi 119:49,
147
c. Ukilijua hutakwazika ( you will never
Stumble) Zaburi 119:165
d. Ni tamu Zaburi 1119:103
e. Linahekimisha kuliko hata umri wako Zaburi
119:100
f.
Linafikuza
waovu Zaburi 119:29, 115
g. Neno la Mungu ni faraja wakati wa taabu
119:50
h. Neno la Mungu ni fimbo ya Mchungaji Zaburi
119:176
15. Mkumbushe Mungu ahadi zake “Remind God on his
Promises”
Zaburi
119:49-50 “Likumbuke neno ulilomwambia mtumishi wako,
Kwa sababu umenitumainisha. Hii ndiyo faraja yangu katika taabu yangu, Ya
kwamba ahadi yako imenihuisha.” Mwenye hekima hapa anamkumbusha Mungu neno
lake au ahadi zake, ambayo anaeleza kuwa imempa matumaini Makubwa, mateso yake
yote anayoyapata anafarijika kwa sababu ya ahadi ya Mungu, Kuna mambo
yanafunuliwa hapa katika mstari huu, kwanza kabisa katika zaburi hii ilikuwa
ngumu sana kufahamu kuwa imeandikwa na nani, lakini kupitia mstari huu wengi
wanafikiri kuwa sasa moyo wa Mwandishi kujificha imeshindikana kwani ni wazi
huyu ni Daudi na ni wazi kuwa alikuwa akitamani ahadi hii itimie 2Samuel 2:16-19 “Na
nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti
chako kitafanywa imara milele. Kwa maneno hayo yote, na kwa maono hayo yote,
ndivyo Nathani alivyonena na Daudi.Ndipo Daudi, mfalme, akaingia, akaketi mbele
za Bwana, akasema, Mimi ni nani, Bwana MUNGU, na nyumba yangu ni nini, hata
umenileta hata hapa? Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Bwana
MUNGU; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumwa wako, kwa miaka mingi
inayokuja baadaye; na hayo kwa namna ya kibinadamu, Ee Bwana MUNGU.” Hii ilikuwa ni ahadi ya kuja kwa Masihi
kupitia uzao wa Daudi, kwa hiyo licha ya kuwa Mungu aliahidi lakini Daudi
aliendelea kumkumbusha Mungu ahadi yake, alikuwa anatamani kuiona kwa macho
yake ikitimia, Mwenye hekima anatukumbusha umuhimu wa kumkumbusha Mungu ahadi
zake kwa njia ya maombi, hii haimaanishi kuwa Mungu hakumbuki hapana au hajui
hapana lakini Mungu katika hekima yake anataka tulisome neno lake na kuzijua
haki zetu na kuzidai kwa jinsi ya maombi angalia Isaya 43:26 “Unikumbushe, na tuhojiane; eleza
mambo yako, upate kupewa haki yako.”
Mungu aliitimiza ahadi hii kimwili kupitia Solomon “
in a narrow cense” na kiroho ni Kwa Yesu Kristo “in a broad cense” 2Nyakati 7:17-18 “Nawe,
ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote
niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu; ndipo
nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba
yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli” Lakini
pia agano au ahadi hii ilikuwa inamuhusu Yesu Kristo angalia Luka 1:68-69 “Atukuzwe
Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa. Ametusimamishia
pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.” Ni vema sana
kuendelea kumuomba Mungu ili aweze kukumbuka na kulitimiza agano lake na kuliangalia
neno lake ambalo alisema nasi, ikiwemo ahadi ya Yesu Kristo kuja tena.
16. Simama imara Zaburi 119:51-54
Mungu huwatumia watu wenye msimamo watu imara watu
wasiotikisika, baada ya kuwa umemjua Mungu na njia zake hupaswi kuyumbishwa
hupawi kuwa mtu wa nia mbili hupaswi kuwa unyasi unaotikiswa na upepo ni lazima
uwe imara 1Wakoritho 15:58 “Basi, ndugu zangu
wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote,
kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.” Ndugu
zangu wapendwa muimarike napenda sana mstari huu unavyosomeka katika biblia ya
kiingereza Stand firm, do not be moved! Mungu anataka tuwe imara katika
kumuamini yeye unaweza kuona Waefeso
6;10-11 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na
katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga
hila za Shetani.” Kusimama imara ni pamoja na kuisimamia imani kwa
gharama yoyote, kuhakikisha kuwa tunasimama katika haki na maelekezo ya Mungu,
hatupaswi kuwa wenye kuyumba linapokuja swala la imani, Shadrack Meshak na
Abednego waliweza kuisimamia imani kwa gharama ya maisha yao hata walipojua
wazi kuwa wanaweza kutupwa katika tanuru ya moto wao walisimama upande wa Mungu
Daniel 3:16-18 “ Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee
Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu
tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na
mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi
hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu
uliyoisimamisha”. Mungu anatarajia kuwa na vijana wenye msimamo
mkali katika imani, vijana ambao watafanya kazi yake katika nyakati za mwisho
wakiisimamia imani bila woga, Nyakati za leo vijana wengi hawana msimamo
wanayumbishwa, kijana wa kiume anafanywa kuwa KIBENTENI anawekwa ndani anafugwa
na sugar momy, wasichana wanauza miili yao, wasichana wa leo hawakatai, kila
unayemtongoza anaingia laini, leo hakuna umri maalumu wa kutembea na mtu kijana
mdogo akikaza anachukua mtu wa umri kama mama yake tu na mtu mzima akikaza
anachukua bnti kama mjukuu wake tu, hakuna heshima, hakuna adabu nani
ataifundisha dunia kuwa wako watu wamefunzwa na wanaitwa wakristo, watu wenye
uadilifu watu wasioyumbishwa, watu walio majasiri, watu waio wepesi watu wasio
unyasi unaotikiswa na upepo, watu wenye msimamo, watu waliojenga nyumba zao juu
ya Mwamba ambao hawayumbishi na mvua, wala pepo wala mafuriko Mungu anataka
watu wa aina hii wenye msimamo.,tafadhali simama imara.
17. Kumbuka jina la Bwana Mungu wako!
Zaburi
119:55-60 “Wakati wa usiku nimelikumbuka jina lako, Ee
Bwana, nikaitii sheria yako. Hayo ndiyo niliyokuwa nayo, Kwa sababu nimeyashika
mausia yako. Bwana ndiye aliye fungu langu, Nimesema kwamba nitayatii maneno
yake. Nimekuomba radhi kwa moyo wangu wote, Unifadhili sawasawa na ahadi yako.
Nalizitafakari njia zangu, Na miguu yangu nalizielekezea shuhuda zako. Nalifanya haraka wala sikukawia, Kuyatii
maagizo yako.”
Mwandishi anaeleza kuwa wakati wa usiku amelikumbuka
jina la Mungu, wakati wa usiku hapa sio lazima uwe ni wakati wa usiku kweli,
hii inawezekana ni wakati ambapo giza la maisha limetanda, ni wakati wa vita
vyake katika maisha ni jinsi gani anaweza kuishafisha njia yake ni pamoja na kulikumbuka jina la Mungu wake
wakati wa changamoto Za aina mbalimbali
Ni muhimu sana kufahamu kuwa nyakati za biblia mara kadhaa
Jina limekuwa na maana kubwa na pana sana kuliko tunavyo fikiri katika wakati
wa leo, Majina hayakutolewa tu bila sababu kwa sababu majina yalibeba maana
kubwa sana kaytika maisha hivyo kuna wakati hata Mungu mwenyewe aliweza
kuwabadili watu majina ili kuakisi kusudi la Mungu dhidi ya mtu huyo, mfano Abramu maana yake “Baba aliyetukuzwa” au “mwana
wa kifalme” Mungu alimbadilisha jina lake kuwa Abrahamu maana yake baba wa wengi au “Mfalme wa wafalme wengi” Yakobo
ambaye jina lake lilikuwa mwenye hila alibadilishwa na kutoka jina mfalme mwenye hila kuwa Mfalme pamoja na Mungu Israel, Sarai kutoka kuwa Malikia kuwa Mama wa wafalme wengi, Tabia
hii ya Mungu iliweza pia kuonekana katika agano jipya ambapo Yesu alibadili
jila la Simeon kuwa Petro au Kefa Yohana
1:42 “Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama,
akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro,
au Jiwe).”
Katika maandiko jina linafunua sifa, uweza na mamlaka,
Yesu alipokuja Duniani yeye alikuwa ni jina kamili la Mungu vile alivyojifunua
alikuwa akiifunua siri ya Mungu Yohana
17;26 “Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha
hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.”
Jina la Mungu ni msaada kamili wa kuwatosheleza
wanadamu wakati wa mahitaji yao, Mwandishi anasema wakati wa usiku alilikumbuka
jina la Mungu, ni wazi kuwa jila la Mungu lina utoshelevu wote katika maisha
yetu ni jina la thamani kubwa sana Israel hawakupenda kulitaja hovyo lakini
walijua kuwa jina la Mungu Ni jina lenye
utoshelevu wa mahitaji yao yote hivyo walimuita Munhgu majina mbalimbali
kutokana na namna na jinsi alivyoukua akijifunua na kujidhihirisha katika
mazingira mbalimbali.
·
Mfano Elohimu
alipojifunua kama Mungu mwenyezi muumba wa mbingu na ardhi na vyote vijuzavyo
ulimwengu
·
Yehova
Nisi alipojifunua kutoa ushindi dhidi ya adui zao
·
Yehova
Rapha alipojidhihirisha kama Mponyaji
·
Yehova
Yire alipojidhihirisha kuwa ni
mtoaji
Mungu ana jina
kwa kila hali ya mahitaji yetu katika maisha ana jina kwaajili ya kila
changamoto tunayokutana nayo, jina lake linadhihirisha uwezo wake na sifa zake
na tabia yakena mamlaka yake na nguvu zake ni jina linaloweza kukimbiliwa na
likatupa amani ''Mithali 18:10- Jina
la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia akawa salama.'' Ni jina ambalo mtu awaye yote akiliitia katika shida aliyo
nayo ataokolewa Matendo 2:21 “Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.
“ Warumi 10:13 “kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la
Bwana ataokoka.“ Jina hili lilikuwa jina adimu sana katika agano la
kale, wayahudi walikatazwa wasilitaje bure jina la Bwana Mungu, jina hili
waliliogopa sana hata kulitaja au kuliandika lakini sisi nyakati za agano jipya
jina hili tumepewa na jina hili liko wazi tunawezxa kuliitia na kulitegemea na
kulitumainia Wafilipi 2:9-11 “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile
lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu
kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”
So Yesu aliagiza tuombe kwa jina
hili nay a kuwa tukiomba lolote kwa jina lake baba wa mbinguni atalifanya
Yohana 14:13-14 “Nanyi mkiomba lo lote kwa jina
langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu,
nitalifanya.” Na ndio maana sasa mwandishi wa zaburi anasema
amelikumbuka jina la Mungu wakati wa usiku yaani analitegemea analiitia anaomba
kupitia hilo wakati aonapo giza katika njia zake so jnsi gani kijana aishafishe
njia yke ni pamoja na kulikumbuka jina la Bwana mungu wetu na kulitegemea na
kulikimbilia
18.
Kumbuka Kumshukuru Mungu!
Zaburin 119: 61-68 “Kamba za wasio haki zimenifunga, Sikuisahau sheria yako. Katikati
ya usiku nitaamka nikushukuru, Kwa sababu ya hukumu zako za haki. Mimi ni
mwenzao watu wote wakuchao, Na wale wayatiio mausia yako. Bwana, dunia imejaa
fadhili zako, Unifundishe amri zako. Umemtendea mema mtumishi wako, Ee Bwana,
sawasawa na neno lako. Unifundishe akili na maarifa, Maana nimeyaamini maagizo
yako. Kabla sijateswa mimi nalipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako. Wewe U
mwema na mtenda mema, Unifundishe amri zako.”
Hakuna jambo muhimu Duniani kama kumshukuru Mungu na kuwashukuru
wanadamu, au wote wanaotuzunguka kwa kuwa kila mmoja anachangia mafanikio yetu
kwa namna moja ama nyingine, Kama hatutakuwa na shukurani kinyume chake
tutakuwa na manung’uniko na lawama jambo ambalo halimpendezi Mungu na linaondoa
baraka za Mungu, Hesabu 11:1 “Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu
masikioni mwa Bwana; Bwana aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa
Bwana ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago.” Wote
tunakumbuka namna na jinsi wana wa Israel walivyoteseka huko Misri na Mungu
alivyowapigania na kuwaokoa na kuwasaidia hata hivyo walipopata taabu
hawakukumbuka mema ya Mungu bali walinung’unika na kunena maovu hawakuwawatu wa
shukurani, licha ya kulishwa mana na kunyweshwa maji lakini hawakupokea mambo
kwa shukurani, tunapokuwa vijana hata tutakapokuja kuwa watu wazima katika
safari yetu ya maisha wako watu watatumiwa na Mungu kututoa katika hatua moja
mpaka kutupeleka katika hatua nyingine hatuna budi kuwa watu wa shukurani,
kuwashukuru lakini vilevile kumshukuru Mungu, Mwandishi wa zaburi hii anasema
katikati ya usiku ataamka amshukuru Mungu, maana yake anataka kumuinyesha Mungu
jinsi anavyokumbuka matedno yake mitego ya wasio haki ilimfunga lakini Bwana
alimuokoa kwanini asishukuru? Je unakumbuka kuwa na Muda wa shukurani? Je
umemshukuru Mungu leo asubuhi? 1Wathesalonike
5:18 Biblia inasema “shukuruni kwa kila jambo; maana
hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.”
Kumshukuru Mungu ni amri, hatuna budi kujifunza kushukuru kila siku
katika maisha yetu, tuache kulalamika, tujifunze kumshukuru Mungu siku zote za
maisha yetu, Kumpa Mungu shukurani huiweka mioyo yetu katika uhusiano sahihi na
Mungu, naye atatuokoa hata katika hali yetu ya nhisia mbaya jambo ambalo
litatuletea amani Waebrania 13:15 “Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa
daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. “ Dabihu ya
sifa humaanisha kushukuru wakati wa mambo magumu Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbue kwa neno lo lote;
bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na
zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo
yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”
19.
Kubali Kujaribiwa
Zaburi 119:69-75 “Wenye kiburi wamenizulia uongo, Kwa moyo wangu wote
nitayashika mausia yako. Mioyo yao imenenepa kama shahamu, Mimi nimeifurahia
sheria yako. Ilikuwa vema kwangu kuwa
naliteswa, Nipate kujifunza amri zako.
Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu, Kuliko maelfu ya dhahabu na
fedha. Mikono yako ilinifanya ikanitengeneza, Unifahamishe nikajifunze maagizo
yako. Wakuchao na wanione na kufurahi,
Kwa sababu nimelingojea neno lako. Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee Bwana,
na kwa uaminifu umenitesa.”
“Ilikuwa vema kwamba
naliteswa Nipate kujifunza Amri zako” vinaja wanapaswa kujua kuwa wakati
mwingine Mungu ataruhusu njia ya mateso kusudi aweze kutufundisha njia zake au
amri zake Wafilipi 1;29 “ Maana
mmepewa kwa ajili ya Kristo si kumwamini tu ila na kuteswa kwaajili yake “
Mungu anazo njia zake ambazo ni njema katika maisha yetu, wakati mwingine
itatuchukua muda mrefu sana kuona ndoto zetu zikitimia kutokana na mpango wake na hekima yake yeye
aliamua na kukusudia kabisa Israel wapiti Jangwani kusudi =awafundishe amri
zake Umbali kutoka Misri kwenda Israel ni kilomita 623 tu. Lakini Musa na kundi
lake (wana wa Israel) walitumia miaka 40 kutembea hadi kufika nchi ya ahadi.
Huu ni wastani wa kilomita 15 kwa mwaka, sawa na kilomita 1.25 kwa mwezi. Hii
ni sawa na mita 42 tu kwa siku, yani umbali nusu ya uwanja wa mpira. Kwa nini
Mungu aliliruhusu ili ni kwa kusdi la kuwafundisha njia zake Kutoka 13:17-18 “Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu
hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa
ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo
watakapokutana na vita, na kurudi Misri; lakini Mungu akawazungusha hao watu
kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi
ya Misri hali wamevaa silaha.”
Kwa nini Mungu aliwapitisha njia ile ngumu ya mateso kwa muda mrefu kuliko
walivyofikiri ni ili aone je watashika amri zake? Kumbukumbu la Torati 8:1-18 “Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi
na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu;
nanyi mtaimiliki. Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako
aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu
kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. Akakutweza,
akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako
hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali
huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana. Mavazi yako hayakuchakaa,
wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini. Nawe fikiri moyoni mwako, ya
kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo.
Nawe uzishike amri za Bwana, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na
kumcha. Kwa kuwa Bwana, Mungu wako,
yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi, na
visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima; nchi ya ngano na shayiri, na
mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali;
nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake;
nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake yafukuka shaba. Nawe utakula
ushibe, utamshukuru Bwana, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa. Jihadhari,
usije ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake,
na sheria zake, ninazokuamuru leo.
Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na
kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na
fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho
kitakapoongezeka; basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako,
aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; aliyekuongoza katika
jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu
isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, aliyekulisha jangwani
kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili
kukutendea mema mwisho wako. Hapo
usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia
utajiri huo. Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za
kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi
leo.” Mungu ana mafunzo mengi sana kwetu anapoamua kutupitisha
katikia njia ndefu, anapoamua kutuacha tuingie katika majaribu, anapotuacha
tuteseka anataka tujifunze amri zake jambo hili lilikuwa wazi kwa mwandishi wa
zaburi hii mwenye hekima alizielewa nia za Mungu so ni jinsi gani kijana
ataishafisha njia yake ni kwa kukubalimnjia za Mungu kwa kukubali kujaribiwa.
20. Wape watu wazuri Nafasi ya pili.
Zaburi
119:76-79 “Nakuomba,
fadhili zako ziwe faraja kwangu, Sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.
Rehema zako zinijie nipate kuishi, Maana sheria yako ni furaha yangu. Wenye
kiburi waaibike, maana wamenidhulumu kwa uongo, Mimi nitayatafakari mausia
yako. Wakuchao na wanirudie, Nao watazijua shuhuda zako.” Ni muhimu
kufahamu kuwa wakati wa majaribu ya aina mbalimbali wako watu wengine
watakukimbia na hawatasimama na wewe ,
wanaweza kufikiri kuwa Mungu hayuko na wewe japo nao wanampenda Mungu, hili ni
jambo la kawaida katika maisha kwa sababu wakati unapitia majaribu sio kila mtu
anaweza kuelewa kwa nini unapitia majaribu Mwenye Hekima anasema yeye ni mwenzao kabisa
watu wanaomcha Mungu Zaburi 119:63 “Mimi ni mwenzao watu wote wakuchao, Na wale wayatiio mausia
yako” Hata hivyo wakati wa mambo magumu walimkimbia wakidhani kuwa
labda Mungu amemuacha, wakati mwingine sio rahisi kuelewa namna na jinsi Mungu
anavyoshughulika na mtu, na hata
tunapokosea watu hawajui ni saa ngapo tumetubu kwa hiyo hata watu wema wanaweza
kudhani kuwa hauko sawa na Mungu na wakajitenga nawe, Hiki kilimtokea mwenye
hekima alipokuwa katika mapito yake kuna wakati hata watu walio karibu wanaweza
wasisimame nawe wakati huu unaweza kusikia maumivu kuachwa na watu wa karibu Zaburi 27:10 “Baba
yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake.” Wakati watu wa karibu wanatukimbia na
kutuacha ni muhimu kuendelea kuweka tumaini letu kwa Bwana Mungu wetu yeye
hatatuacha, lakini ni lazima tukumbuke kuwa kuna wakati wa kuwa wenyewe kuna
wakati wa nkuwa peke yetu huu ni wakati wa kumuita Bwana na kumkimbilia yeye Zaburi 142:5-6 “Utazame
mkono wa kuume ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea,
Hakuna wa kunitunza roho. Bwana, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu,
Fungu langu katika nchi ya walio hai.” Jambo hili sio tu kuwa
lilimtokea Daudi lakini hata Paulo mtume wakati wa kufungwa kwakwe kwa sababu
ya injli, lakini hatuna budi kusamehe
wale wote wanaotuacha kwa sababu hawajua ni nini mapenzi ya Mungu 2Timotheo 4:16 “Katika
jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote
waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.” Ni muhimu
kuwapa nafasi ya pili watu wanaomcha Mungu, watu wema ambao wanatuacha kwaajili
ya kutokuelewa mapenzi ya Mungu wakati nwa mapito yetu, Ayubu 42:10-11 “Kisha Bwana akaugeuza uteka wa
Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko
hayo aliyokuwa nayo kwanza. Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao
wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba
yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana
aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila
mmoja.”
21. Uwe hodari kuliko walimu wako
Zaburi
119:80-100 “Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri
zako, Nisije mimi nikaaibika. Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako,
Nimelingojea neno lako. Macho yangu yamefifia kwa kuitazamia ahadi yako,
Nisemapo, Lini utakaponifariji? Maana nimekuwa kama kiriba katika moshi,
Sikuzisahau amri zako. Siku za mtumishi wako ni ngapi, Lini utakapowahukumu
wale wanaonifuatia? Wenye kiburi wamenichimbia mashimo, Ambao hawaifuati sheria
yako. Maagizo yako yote ni amini, Wananifuatia bure, unisaidie. Walikuwa karibu
na kunikomesha katika nchi, Lakini sikuyaacha mausia yako. Unihuishe kwa
fadhili zako, Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako. Ee Bwana, neno lako
lasimama Imara mbinguni hata milele. Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi,
Umeiweka nchi, nayo inakaa. Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana
vitu vyote ni watumishi wako. Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu, Hapo
ningalipotea katika taabu zangu. Hata milele sitayasahau maagizo yako, Maana
kwa hayo umenihuisha. Mimi ni wako, uniokoe, Kwa maana nimejifunza mausia yako.
Wasio haki wameniotea ili kunipoteza, Nitazitafakari shuhuda zako. Nimeona
ukamilifu wote kuwa na mwisho, Bali agizo lako ni pana mno. Sheria yako
naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa. Maagizo yako hunitia
hekima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo sikuzote. Ninazo akili kuliko
wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu
kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.”
Mwandishi amezungumzia kwa kirefu sana namna na jinsi
anavyoipenda sheria ya Mungu na kuishika amri zake na maagizo yake na mausia
yake, na kuwa atayatafakari mausia ya Mungu, na vile vile alionyesha namna
alivyoayashika mausia ya Mungu na kujionyesha namna na jinsi alivyojitoa kwa
Mungu na neno lake na jinsi ambavyo neneo la Mungu limekuwa faraja yake kubwa
sana hata hivyo, mwenye hekima hapa pia anajisifu kuwa amekuwa na ujuzi hata
kuliko walimu wake, Jambo hili ni la msingi na la muhimu sana kila mtu anapaswa
kuwa Hodari, na biblia inatutaka tuwe hodari, ikiwezekana tuwe na ujuzi kuliko
walimu wetu, Katika mafunzo ya kijeshi cheo cha juu na cha mwisho kijeshi
Duniani ni Gereral – Lakini Mwanajeshi huyo anapokuwa na uwezo mkubwa zaidi ya
ule aliojifuza huwa anaitwa “Field
-marshal” hiki ndio cheo cha juu zaidi cha kijeshi zaidi ya general Marshal
kwa kiibraniamaana yake ni mtu aliye hodari hili neno linatumika katika Waebrania 11:32-34 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni
na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa
imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga
vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga.
Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza
majeshi ya wageni” neno kuwa Hodari maana yake ni kufanya zaidi ya
jinsi ya ulivyofundishwa, kuwazidi walimu wako, uko usemi unaosema au uliosemwa
na Yesu kuwa mwanafunzi hawezi kumpita mwalimu wake Matthew 10:24 “Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana
wake.” Lakini ni ukweli usiopingika kuwa kuna wakati wasomi huwazidi
walimu wao kwa uhodari kwa ujuzi na maarifa Apollo alikuwa mwanafunzi hodari wa
neno la Mungu aliyewazidi hata walimu wake Prisilla na Akila Matendo 18:24-28 “Basi
Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika
Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia
ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha
kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena
kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua
kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi. Na alipotaka kuvuka bahari
aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi
wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa
neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu
wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.” ,
na Paulo mtume alimzidi anania aliyemuwekea mikono kupokea Roho Mtakatifu na
Mchungaji wake barnaba aliyempelekea Antiokia, Daudi naye anaonyesha kuwa
unaweza kujifunza neno la Mungu na kulipenda na ukawa hodaroi kuliko walimu
wako Zaburi 1119:98, Hiki ndicho
Daudi alichokuwa akijisifia katika kifungu hiki cha maandiko kuwa amekuwa na
ujuzi na hekima kuliko walimu wake jitengenezee mazingira ya kuwa na Ujuzi na
elimu pana zaidi kuliko wengine, Daudi nsio tu alikuwa na hekina kuliko walimu
wake bali pia wale watu wa zamani waliokuwa na hekima kabla yake Ayubu
8:8-10 “Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani,
Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; (Kwani sisi tu wa jana tu,
wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;) Je! Hawatakufunza
wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?”
Mwandishi anaonyesha kuwa alikuwa Hodari kuliko mtu
awaye yote katika kizazi chake alikuwa na hekina kuliko adui zake na ufahamu
kuliko wazee, kimsingi Daudi anazungumzia ishu za kijeshi
1v – Lansi koplo
2v – koplo
3v- Sajent
Sir Maojr
Luteni usu
Luteni
Captain
Major
Luteni kanali
Kanali
Brigediaer
Brigedirer General
Luteni General
Genearal
Field Marshal
Katika vyeo vya Kijeshi general ndio cheo cha mwisho
Duniani, lakini unapokuwa field Marshal maana yake wewe ni zaidi ya kawaida,
Daudi alikuwa ni zaidi ya wakuu wa majeshi, aliweza kuwashinda, kina Sauli
nakaka zake na kuwa na ujasiri wa kumpiga Giliath bila kupitia mafunzo ya
kieshi, uhodari wake hapa ndio anaoutaka kuwa ni hekima na ufahamu na ujuzi
mkubwa kuliko waliku wake.
22. Lifanye neno la Mungu kuwa Taa ya Miguu
yako!
Zaburi 119:101-105
“Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya, Ili
nilitii neno lako. Sikujiepusha na hukumu zako, Maana Wewe mwenyewe
umenifundisha. Mausia yako ni matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu.
Kwa mausia yako najipatia ufahamu, Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.”
Mwandishi anatukumbusha na kukazia umuhimu wa neno la
Mungu, na mwenyewe akijua kuwa duniani sisi ni wapitaji na wasafiri, na kuwa
hatuwezi kuwa na ugfahamu na ujuzi wa kilakitu duniani kwa vile sisis ni wageni
basi ni neno la Mungu tu ndilo linaloweza kutuongoza na kutupelekea kule aliko
kusudia Mungu 1Petro 2:11a “. Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa
za mwili zipiganazo na roho.” Paulo mtume anasema kwa maana sisi
wenyeji wetu uko mbinguni Wafilipi 3:20
“Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko
tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;” Dunia inatawaliwa na
matendo ya giza, kuishi duniani kama wageni na wapitaji kunahitaji tuwe na dira
na ramani taa na mwanga ili migu yetu iweze kupita kwa salama na amani na ni neno la Mungu pekee linaloweza
kufanya hivyo katika kile eneo la maisha yetu
Neno la Mungu ni taa Zaburi 119: 105, Nimeapa nami nitaifikiliza, Kuzishika hukumu za
haki yako Litatusaidia wakati wa kufanya maamuzi Zaburi 119:106 Nimeteswa mno; Ee Bwana, unihuishe sawasawa na neno
lako. litatuongoza wakati wa Mateso Zaburi
119:107, Litatulinda na mitego ya adui, litatuongoza kujitoa kwa Mungu Litatuelimisha Zaburi 119:108-109, Ee Bwana, uziridhie sadaka za kinywa changu,
Na kunifundisha hukumu zako. Nafsi yangu imo mkononi mwangu daima, Lakini
sheria yako sikuisahau.Litatulinda na mitegi ya adui Zaburi 1119:109-110, “Watendao uovu
wamenitegea mtego, Lakini sikuikosa njia ya mausia yako” litatupa furaha
na amani Heri kuuelekeza moyo wetu kwenye neno la Mungu daima Zaburi
119:111-112 “Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele,
Maana ndizo changamko la moyo wangu. Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri
zako, Daima, naam, hata milele”
Kwa hiyo jumla ya
majibu yote jinsi gani kijana aishafishe njia yake ni kwa kutii akilifuata neno
la Bwana
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!
Mungu akusaidie kwa Kila Jambo mtumishi wa Mungu kwa kazi yako nzuri unayoifanya kumbuka sio bure ila ipo thawabu mbeleni .naomba mafundisho zaidi ya vijana 0113979985 unitumie kwa Watts app kusudi nikawaweze kuelimika zaidi
JibuFutaBarikiwa Pastor
JibuFutaAmen amen asntee
JibuFutaNaitwa Remi Simon manyara Tanzania +255682225601 Kwa whatsaap pastor barikiwa sana mafundisho haya kama kijana ntayafanyia kazi
JibuFuta