Jumatano, 30 Oktoba 2019

Sisi je! Tutapataje kupona, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII?


Andiko la Msingi: Waebrania 2:1-3Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.  Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,  sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;”




Utangulizi:

Yesu Kristo alikuja Duniani kwa makusudi makubwa mengi, lakini kusudi kubwa ni ili apate kutuokoka! Luka 10:19Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” 

Na ndio maana Yesu pia anaitwa mwokozi, ametukomboa katika mambo mengi lakini kubwa zaidi ametuokoa na adabu ya dhambi  

Mathayo 1:21Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.” Kwa hiyo unaweza kuona kuwa kusudi kubwa la Yesu ni kutuokoa na ametuokoa na mambo mengi lakini zaidi sana ametuokoa na Dhambi zetu, kwa nini kuokolewa nadhambi ni kwa muhimu sana kwa sababu kila aina moja ya dhambi tuifanyayo msahara wake ni mauti ona 

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” kwa hiyo kutokana na kuweko kwa dhambi katika nasfi zetu adhabu yake ilikuwa ni kifo, kifo cha mwili huu na kifo cha kiroho ambacho ni kutengwa na Mungu milele lakini Yesu akaja Duniani akatuelekeza njia kwa mafundisho yake akaandaa watu watakaotufundisha neno lake kisha Yeye mwenyewe alikufa kwaajili yetu yaani kwa niaba yetu, ili damu yake itakayomwagika iwe malipo kwa niaba ya damu zetu na hivyo tukimuamini hukumu hii haina nguvu na tunasamehewa na huu ndio wokovu mkuu, kwa hiyo sasa kazi yetu ni kumuamini yeye na kukubali kazi yake aliyoifanya pale msalabani ili tuweze kuwa na uzima wa milele  

Yohana 3:16Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Kwa hiyo wajibu wako mkubwa ni kumuamini yetu, yaani kutambua na kukubali kuwa alikufa msalabani kwaajili yako na yangu na ukifanya hivyo wewe una uzima wa milele.


Kwa nini wokovu ni mkuu?

Hakuna tukio baya duniani au laana mbaya kama kutengwa na uso wa Mungu! Mwanzo 4:13-14. Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.”

 Mara moja mtu anapokuwa dhambini anatengwa na uso wa Mungu anakuwa mtoro duniani na kila kitu kinakuwa adui yake na hata mbu au bacteria wanaweza kukuua ni jambo bay asana kupungukiwa na utukufu wa Mungu ni hasara ya hali ya juu hata kama una heshima kiasi gani kwaajili ya hayo basi Neno la Mungu linatuonya kutokuuchezea wokovu, wokovu ni neema tu sio wote wanaojaliwa kuukubali, sio watu wote watajaliwa kuupata wokovu au hata kuufahamu, ikiwa wewe umepata neema ya kuufahamu basi usiuchezee wokovu ni mkuu mno, msamaha wa dhambi ni baraka kubwa mno kuliko kutolewa gerezani, ndio maana mwandishi wa kitabu cha waebrania ametuonya kwamba tunapaswa kuuangalia sana kuutunza sana wokovu na tusiuchezee 

 Waebrania 2:1-3Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,  sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;Kwa nini mwandishi anauona 

wokovu kuwa ni mkuu kwa sababu muhimu zifuatazo;-

Ulinenwa na Bwana mwenyewe, yaani ni zawadi ni mpango  wa Mungu mwenyewe tusingeweza kujisamehesha mbele zake ni yeye mwenyewe kwa hiyari yake aliamua kutusamehe
Umethibitishwa ndani yetu, yaani unapoukubali kwa imani unapewa furaha ya dhati moyoni inayokushuhudia kuwa wewe ni wa Mungu tofauti na jinsi watu wanavyokujua na kukufahamu au kukuangalia

Umethibitishwa kwa ishara na miujiza na Roho Myakatifu, yaani Mungu roho Mtakatifu amewaponya wengi na kufanya miujiza mingi kwa kusudi la kututhiboitishia kuwa kama anaweza kutufanyia ukarimu huumkubwa wa kuiponya miili yetu anashindwaje kutusamehe dhambi zetu miujiza iko ili tupate kuamini kuwa Yesu ni mwokozi, kama watu watafurahia miujiza kuliko kuufurahia wokovu na msamaha wa dhambi watakuwa hawajui thamani ya wokovu Zaburi 103:3Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,” Ni msamaha wa dhambi unaoweza kutuletea pia uponyaji wa mwili na nafsi zetu.

Umegharimu maisha ya mwana wa Mungu, ni kwaajili ya kutuokoa ilimpasa Yesu kufa msalabani kwa kifo cha aibu ili mimi na wewe tuweze kuokolewa kuupuuzia wokovu ni kuidharai kazi ya Yesu aliyoifanya pale msalabani, kurudi nyuma na kuacha wokovu ni kudharau msalaba  Waebrania 6:4-6 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.” Tabia ya kuendelea kuukataa na kuupinga wokovu na kuidharau kazi iliyofanywa na Yesu msalabani inaweza kutufikisha mahali pabaya sana na huu ndio unaitwa ukengeufu, hii ni dhambi ya mauti, huku ni kushindana na Roho Mtakatifu, hatujui ni lini na wapi mtu anaweza kufikia dhambi hii ngumu lakini jnaanza na kudharau wema wa Mungu hivyo kama hujui wokovu uligharimu nini usiutukane!


Unatupa Uzima wa milele unatuokoa na dhambi mauti na kuzimu , kama tukiukubali wokovu na kuupokea licha ya kusamehewa dhambi zetu kila wakati pia tunakuwa na uzima wa milele lakini Mungu anatulinda na dhambi ya mauti yaani ya kukataa kazi za Roho Mtakatifu na kuipinga zawadi ya wokovu

Tumeokolewa kwa neema !

Kule kuwa mbali na Mungu ni kifo, lakini kupitia wokovu kama tumeuamini ni zawadi kubwa sana kutoka kwa Mungu hivyo hatupaswi kuichezea neema ya Mungu Waefeso 2:1-5Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;  ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.  Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.”


Nimalizie ujumbe huu kwa stori hii 

Mfanya biashara mmoja alikuwa akifanya biashara ya kuuza chumvi, alisambaza chumvi yeke sehemu mbalimbali akitumia punda, kila alipoelekea sokoni ilimlazimu kuvuka  mto ili aweze kuelekea sehemu mbalimbali kwaajili ya kuuza chumvi yake, siku moja punda wake kwa bahati aliangusha mzigo wa gunia la chumvi kwenye mto, na hivyo chumvi iliyeyuka na kwenda na maji kutokana na hali hiyo gunia la chumvi likawa Jepesi, hali hii ilimpa punda yule furaha kubwa mno.

Kwa hiyo punda yule alianza kuwa na mchezo mbaya ilikuwa kila siku akibeba chumvi akifika eneo lenye mto aliliangusha gunia kwa makududi yaleyale, Muza chumvi alijiuliza ni kwanini hali ile inatokea mwisho aliweza kugundua tabia ya punda wake na akakusudia kumfundisha somo, safari moja alimbebesha gunia la Pamba na punda bila kujalia amebeba nini alipofika pale aliliangusha tena gunia la Pamba, akijua kuwa litakuwa jepesi vilevile kama ilivyokua kwa chumvi, lakini mambo yalikuwa tofauti safari hii, gunia la pamba lilikuwa zito mno kuliko maelezo na hivyo punda alipata taabu sana na akaacha tabia yake ya mchezomchezo na mfanya biashara yule akawa na furaha.

Usichezee neema ya wokovu kwa sababu bahati haiji mara mbili, iko siku unaweza kupoteza kila ulichojaaliwa na Mungu na ukajikuta unapata tabu , shika sana ulicho nacho.
Bwana ampe neema kila mmoja wetu asiuchezee wokovu katika jina la Yesu Kristo amen!

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa Wajenzi mwenye hekima.

0718990796

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni