Jumatatu, 11 Novemba 2019

Hata Malaika wapo!


Zaburi 34:7Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.

Hatuko peke yetu! Watu wengi sana huwa wanasahau hili, wanapopita katika changamoto za iana mbalimbali huwa wanadhani kuwa Mungu amewaacha, nasio tu kudhani kuwa Mungu amewaacha lakini hawana ufahamu kuwa watu wa Mungu wanalindwa na Majeshi ya malaika tunasahau kuwa Hata malaika wapo! Ndio Malaika wapo

Biblia inasema Hawa malaika ni roho wanaotumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu Waebrania 1: 13-14; “Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”
Unaona Biblia inasema kuwa malaika ni viumbe wa kiroho wanaotumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu, Malaika wapo, wakati unalia na kushangaa wana wanakushangaa kwanini unalia, kwanini huwatumii je unajua waoa hutuhudumia je unajua wao hututazama kwa macho mengine  wao hututia moyo pale tunapojihisi kuwa sisi ni Duni wao hutuona kuwa sisi mashujaa, Ndugu wewe ni zaidi ya Rais unalindwa na malaika pande zote usimtie Mungu aibu, wala usimfanye Mungu kuwa Bodigadi wako, How comes ulindwe na Mfalme wa wafalme ili hali majeshi yake yapo. Wapo wapo kukupa msaada unaoutaka kumbuka wanakuita wewe shujaa ona Waamuzi 6:12 “Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa.Hakukuwa na mtu muoga duniani kama Gideon Lakini malaika alimuita Ee Shujaa, Ndio ni shujaa kwa sababu haendi peke yake Malaika kibao wapo wanaenda pamoja naye iweje asiwe shujaa, angalia mtu anayelindwa na mabaunsa pande zote anawezaje kutembea kama mtu mnyonge? Ni Shujaa ndio ni shujaa kwa nini kwa sababu anazungukwa na ulinzi wa kutosha na kupewa msaada wa kila ainna autakao.

Malaika hawana Nguvu zote kama Mungu, lakini wana nguvu kuliko binadamu, katika rekodi za juu za kibiblia, Maandiko yanasema Malaika mmoja anauwezo wa kupiga watu 185,000, ndio nasema ndio malaika mmoja tu anauwezo huo soma Isaya 37:36Basi malaika wa Bwana alitoka, akaua watu mia na themanini na tano elfu katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.         

Sasa wewe unaogopa nini? Unaogopa wachawi? Unaogopa changamoto gani Biblia inasema malaika wa Bwana hufanya kituo (Hufanya Patrol) akiwalinda wale wanaomcha Mungu, na hawa unaona mmoja tu anauwezo wa kupiga watu 185,000, Ndio maana Daudi aliimba Bwana ni ngome yangu, Jeshi lijapojipanga kupigana nani moyo wangu hautaogopa!, Malaika wapo dada, malaika wapo, kaka, malaika wapo baba, malaika wapo ndugu yangu, waache wao watumie Majini, waache watumie uchawi waache watumie kila silaha wanayoweza sisi, tunatumia Malaika tunawaamuru Malaika waingilie kati katika kila hali inayotuzunguka na watatupigania

Malaika wanauwezo wa kukutoa katika kifungo cha aina yoyote, Matendo 12:5-11Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono. Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha. Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.  

  
Petro alipokuwa Gerezani katikati  ya ulinzi mkali, kila mtu akitarajia kuwa atauawa Malaika alikuja na kumtoa gerezani, jamani malaika wapo, wakristo mailka wapo Hakuna sababu ya kuogopa chochote ni lazima na muhimu kumuamini Mungu, kuamini uweza wake kujua uuumbaji wake aliumba viumbe vinavyoonekana na visivyoonekana, Malaika hawaonekani lakini maandiko yanasema wapo, Mimi naamini wapo najua wanawajibika katika kile alichowaagiza Mungu najua wanafanya kituo, sihitaji ulinzi wa mabausa, wala Bodigadi wao wapo kwaajili yangu, wapo pia kwaajili yako huna sababu ya kuogopa mchana wala usiku kwa sababu wao wapo! Mungu amenituma nikujulishe tu kuwa viumbe hawa wapo, wapo wametumwa na Mungu kwa Makusudi ya kutuhudumia kwanini uteseke watumie usiogope hatuko peke yetu Malaika nao wapo
Hata malaika wapo!

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Rev. Innocent Kamote
0718990796.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni