Wayahudi wa Madhehebu ya Orthodox huhakikisha kuwa watoto wao wanajua historia yao, dini yao mila zao na desturi zao, na kila mtoto huweza nkuelezea kuhusu familia yake hata vizazi kumi vilivyopita!
Utangulizi!
Katika moja
ya tatizo kubwa ambalo jamii kubwa ya leo tumefeli duniani ni eneo la Malezi ya
watoto, ni wazazi wachache sana ambao leo wamefanikiwa kuwaelekeza watoto wao
na wakawa kama vile Mungu pamoja na wazazi walivyokusudia. Leo hii watu wengi
sana wanalia na wameshindwa kuwadhibiti watoto, Namshukuru Mungu kuwa ameniita
katika huduma ya kuwahudumia watoto, kwa miaka kadhaa sasa nimekuwa mkuu wa
shule ya Sekondari Living Stone Boys’ Seminary, huku vilevile nikiwa Mchungaji
wao, Najua na nimeona jinsi vijana wengi wanavyopoteza muelekeo hasa kwa sababu,
ya kukosa malezi, wazazi wengi leo wako busy na utafutaji wa mali, wako busy na
simu na ufuatiliaji wa Tamthilia na wameshindwa kujihusisha hata kidogo na
maisha ya watoto, na wakati mwingine wamewasukumia shuleni, ili kwamba sisi
walimu tuhangaike na watoto hawa ambao mimi huwaita kizazi cha ma-house girl
Kizazi cha wadada wa kazi. Hili ni tatizo kubwa mno.
Tofauti ya kizazi wakati wa Joshua na kizazi
wakati wa waamuzi.
Kitabu cha
waamuzi ni kitabu cha nyakati za mpito wa historia ya wana wa Israel baada ya
uongozi wa Yoshua, tunakumbushwa katika maandiko na katika kitabu hiki kuwa
watu walimtumikia Mungu wakati wote wa Yoshua, Na kuwa Mungu aliwabariki watu
wake,
Yoshua 24:31 “Nao Israeli wakamtumikia Bwana siku zote za Yoshua, na siku
zote za hao wazee walioishi baada ya kufa kwake Yoshua, hao walioijua kazi yote
ya Bwana, aliyowatendea Israeli.”
Lakini kwenye kitabu hiki watu
waliitumikia miungu na kuabudu sanamu, waliziacha kabisa njiia za Mungu na
walisahahu kabisa matendo ya Mungu wala hawakujua matendo yake wala njia zake,
Ndio maana biblia inasema kikainuka kizazi kingine kisichomjua Mungu!
Waamuzi 2:10 “Tena
watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka
kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi
ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.”
Kwanini tunaona tofauti kati ya kizazi kile
na kizazi hiki? Hawa wote walikuwa wana wa Israel, wote walilellewa na kukulia
katika historia ya matendo ya Mungu, kuna tofauti kadhaa
1. Kizazi kile
kilichomtumikia Mungu walikuwa chini ya uongozi wa Yoshua ambaye alimtumikia Mungu kwa moyo wake wote na waliona matendo
makuu ya Mungu
a.
Waliona
Israel wakivuka mahali pakavu wakati mto wa Yordani ukiwa umefurika
b.
Waliona kuta
za Yeriko zikianguka kwa uwezo mkubwa wa Mungu na melekezo yake
c.
Waliona
Mungu akiwapigania dhidi ya wafalme watano wa waamori na Mungu akiwashushia
matofali ya moto
d.
Waliona Mungu
akiongeza Muda kwa Joshua na majeshi yake kwa kusimamisha jua
e.
Maadui walitiishwa
dhidi yao, kilikuwa ni kizazi kilichojua na kuyaona matendo ya Mungu
f.
Walipitia magumu
mengi na kujitoa sana, kilikuwa ni kizazi cha mashujaa waliojipatia ardhi ya
mkanaani.
2.
Kizazi kilichofuata kilikuwa ni kizazi
kingine ambachoi hawakumjua Mungu wala matendo yake
a.
Walisikia tu
Historias ya matendo ya zamani, waliona tu nguzo za kumbukumbu za baba zao kuwa
walipita pakavu Jordani
b.
Waliona tu
Magofu ya mji wa Yeriko na walisikia tu kuwa ukuita ulianguka
c.
Walijishughulisha
tu kuendeleza nchi ambayo Mungu aliwapa baba zao na wakasahu mambo ya Mungu
mwenyewe
d.
Walikaa katika
miji ambayo wala hawakuihangaikia, walikula matunda ya mizabibu ambayo
hawakuilima
e.
Walikuwa wakifurahia
tu utajiri na mafanikio ambayo baba zao waliyapata kutoka kwa maadui kama nyara
walizoteka
f.
Hawakujua
habari za Mungu kuigawa bahari ya shamu, hawakujua habari za Mungu Kushuka
katika mlima wa Sinai na kuwapa amri kumi na sheria na taratibu nyingine
Sababu kuu ya kizazi hiki kutokumjua Mungu.
Ni muhimu
kufahamu kuwa Mungu hapa sio tatizo, lakini kizazi kile kilichopita ndio
kilikuwa tatizo, waoa hawakufanya yaliyo wajibu wao kwa Bwana, Mungu alikuwa
amekusudia Israel wawafundishe watoto wao njia zake zote na kuwakumbusha
matendo yake yote
Kumbukumbu la Torati
6:1-14 “ Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu,
alizoziamuru Bwana, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile
mnayoivukia kuimiliki; upate kumcha Bwana, Mungu wako, kushika amri zake zote,
na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za
maisha yako; tena siku zako ziongezwe. Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie
kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama Bwana, Mungu wa baba
zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali. Sikiza, Ee Israeli;
Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo
wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya
ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa
bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo,
na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe
katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya
malango yako. Tena itakuwa atakapokwisha Bwana, Mungu wako, kukuleta katika
nchi aliyowaapia babu zako, Ibrahimu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji
mikubwa mizuri usiyoijenga wewe, na
nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vimefukuliwa
usivyofukua wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe
utakula na kushiba; ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya
Misri, nyumba ya utumwa. Mche Bwana, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na
kuapa kwa jina lake. Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa
wawazungukao;”
Musa ni kama
alikuwa ana wa zoom wana wa Israel aliwaonya mapema kwa neno la Mungu kuwa ni
lazima wawaelimishe watoto wao na kuhakikisha kuwa wanampenda Mungu, ilikuwa ni
kwa namna mbalimbali Mungu alitaka maswala haya ya msingi yakumbukwe, kizazi na
kizazi walipaswa kufundishana kwa bidii matendo yote na maneno yote ya Mungu na
kuwa kila kizazi wakumbuke, kile ambacho Mungu alikuwa amekikusudia wampende na
kumtumikia. Mungu alirejea jambo kama
hili kwa Yoshua kwa sababu Moyonimwake Mungu alikuwa anataka kizazi kipya
kiyajue matendo yake ili wamuabudu
Yoshua 4:1-8 “Ikawa,
hapo hilo taifa zima lilipokuwa limekwisha vuka Yordani, ndipo Bwana akanena na
Yoshua, akamwambia, Haya, twaeni watu waume kumi na wawili katika hao watu,
kila kabila mtu mmoja, kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili,
hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara,
mwende nayo mawe hayo, mkayaweke nchi kambini, hapo mtakapolala usiku huu. Basi
Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa amewaweka tayari tangu hapo,
katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja; naye Yoshua akawaambia, Haya,
piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la Bwana, Mungu wenu, mwende pale
katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri
ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli; ili kwamba jambo hili liwe ishara kati
yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni
nini maana yake mawe haya? Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani
yalitindika mbele ya sanduku la agano la Bwana; hapo lilipovuka Yordani, hayo
maji ya Yordani yalitindika; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa
Israeli milele. Basi wana wa Israeli walifanya vile vile kama Yoshua
alivyowaamuru, nao wakatwaa mawe kumi na mawili pale katikati ya Yordani, kama
Bwana alivyomwambia Yoshua, sawasawa na hesabu ya kabila za wana wa Israeli;
wakayachukua wakavuka nayo hata mahali pale walipolala, nao wakayaweka nchi
kuko huko.”
Unaweza
kuona mkakati wa Mungu ni kuwa kila kizazi kiyajue matendo yake, watu wazima
wawafundishe vija nana watoto kumjua Mungu, kuyajua matendo yake ili kwamba
wampende Mungu na kumtumikia na kuacha kuabudu miungu, tatizo kubwa la kuibuka
kwa kizazi kisichomjua Mungu ni kizazi kile kilichokuwa kikifurahia baraka za
Mungu na kusahau kabisa wajibu wa kuwafunza watoto, leo hii dunia imejaa
mafunzo ya ajabu mno, watu wanaohusika na ushoga wameandaa vijitabu vya
kuwafundisha watoto ushoga mapema ili wauone kuwa ni kitu cha kawaida katika
kizazi hiki, kanisa limepuuza maswala mazima ya kuwafundisha vijana na watoto,
dini zimejikita katika maswala ya mafanikio utafutaji wa fedha na
kutokushughulika na watoto ili kumtegenezea Yesu kanisa la baadaye matokeo kama
haya na makosa kama haya ni sawa na yale waliyoyafanya wayahudi wakati wa
waamuzi na matokeo yake wana wa Israel walijifunza tabia mbaya na kuabudu miungu
na kumuacha Mungu aliye hai huku wakifanya maovu angalia
Waamuzi
2:11-13 “Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu
mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali. Wakamwacha Bwana, Mungu wa
baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine,
baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha
mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika. Wakamwacha Bwana, wakamtumikia
Baali na Maashtorethi.”
Leo hii
kanisa linalia na manabii wa uongo, vuingozi wa kiroho wahuni, wasio na
uadilifu, kuuzwa kwa mafuta, maji, sabuni, unga, chumvi, udongo na soda bangili
za upako na kadhalika pamoja na kuweko kwa mafundisho ya ajabu ajabu tatizo
kubwa sio wao tatizo kubwa ni kanisa lenyewe liliweka msingi gani katika
kuwaandaa viongozi wa kiroho walio waadilifu? Unapolia na manabii wa uongo
kumbuka kulina na walimju wa uongo waliowalea, kanisa lilikuwa wapi, wazazi
walikuwa wapi jamii ilikuwa wapi wakati watoto wetu wanaharibika ? nani
anawajibika? Ni sisi wenyewe Hatukujali mafundisho. Leo hii watu wametoa
kipaumbele katika swala zima la kutafuta mafanikio ya kimwili na kusahau
kujenga msingi wa kuifunza jamii juu ya swala zima la kumtafuta Mungu na
kumpenda na kumpa kipaumbele na kumuabudu yeye na kuwa na hofu yake kamwe tusisahahu
kuwa hukumu ya Mungu ipo
2Petro 2:9-10 “basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka
wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu; na hasa wale waufuatao
mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka” Endapo
kanisa na wazazi hawatajali maswala mazima kuhusu ya kukilela kizazi kijacho
katika njia za Mungu na uadilifu wake basi tujue kuwa hatutaweza kuiepuka
hukumu ya Mungu, Zamani tulikuwa tunasema mauti imo sufuriani lakini sasa iko
mdomoni ni lazima tuamke na kuwasaidia jamii yetu kujiandaa kumcha Mungu.
Jinsi
ya kufanya ili kizazi kijacho kimjue Mungu
Wana
wa Israel walikuwa na changamoto ambayo tunaweza kuigawa
·
Kizazi
cha kwanza kioona matendo ya Mungu
·
Kizazi
cha pili kilisikia matendo ya Mungu na
·
Kizazi
chaa tatu hata kusikia hawakusikia
1. Tuwafundishe kujenga na kuimarisha uhusiano na Mungu Mungu alimchagua Ibrahimu kuwa rafiki yake kwa
sababu alijua kuwa Ibrahimu atakuwa mwalimu mwema Mwanzo 18:17-19 “BWANA akanena, Je! Nimfiche
Ibrahimu jambo nilifanyalo, akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika
yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimemjua ya kwamba
atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye
haki na hukumu, ili kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.”
Kanisa,
mzazi na walimu wanaotaka kuwa rafiki wa Mungu ni wale watakaokuwa wanajali
kuwafundisha watoto na kizazi kijacho njia ya Mungu. Lazima kizazi kimoja
kiwaeleze kizazi kijacho na kizazi kijacho kielezee wale wanaokuja
Yoel 1:2-3 “Sikieni
haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi. Je! Mambo haya
yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu? Waarifuni watoto wenu
habari yake, Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie
kizazi kingine.”
2. Hakikisha kuwa unawaelimisha watoto kwa
ghama yoyote Mithali 4:13 “Mkamate
sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako” kkatika kuhakikisha kuwa vijana wanapata
Elimu na uadilifu ni lazima tukumbuke kuwa kuna walimu wakuu wanne, 1 Wazazi
hawa ndio walimu wa kwanza, wao ndio msingi wa maisha ya kila kitu unapoona
mwanao unajiona wewe waoni picha ya nyumbani kwao, 2. Shuleni, unampeleka
katika shule ya aina gani, walimu wake wakoje ja wanamcha Mungu. Hakikisha kuwa
watoto wanaosma kama huna ada fanya kazi na muombe Mungu aliyekupa hao watoto
kwamba afungue mlango wa ada ili waende shule wasome, je ni nani anataka kuzaa
house girl nani anataka kuzaa kuli, nani anataka kuza machinga, nani anataka
kuzaa wazurulazi, wauza mayai tuwasomeshe tuwapatie elimu 3 Ibadani mwanao ataabudu wapi huyu ndio
mwalimu wa ngazi ya juu kabisa hivyo lazima tuchague mahali sahihi kwa vija na
wetu kujifunza mambo ya Mungu pia, 4 Shetani nimwalimu mbaya mno atawanyoosha
wote ambao hawakuweka msingi unaoeleweka kwa vijana, kama kuna kitu
tunapungukiwa Watanzania ni kutokuwaelimisha watoto wetu, Rafiki yangu mmoja
alisema Japan ni inchi Tajiri na iliyoendelea sana kwa sababu waliwekeza katika
elimu lakini hawana rasilimali nyingi kama tulionazo, na Tanzania ni inchi
yenye rasilimali nyingi sana lakini tumepigwa na ukwasi kwa muda kwa sababu
hatukuwa na maarifa ya kutosha, watoto wetu wanazaliwa na vipawa na karama na
majaliwa makubwa sana lakini tunaweza kuyadidimiza kwa sababu tu tumeshindwa
kuyachohcea kwa kutokuwapa maarifa yanayohitajika, tusiwapeleke watoto mbali na
Mungu Yesu anawahitaji waje kwake Mathayo
19:14 “Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje
kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.”
3. Usimnyime mtoto mapigo.
Maandiko matakatifu yanataka kwanza
tuutangulize upendo tuwapende vijana na watoto wetu kwa viwango ambavyo
wataelewa kuwa tunawapenda, lakini tusiwadekeze, lazima watutii na watuheshimu,
Biblia imesema lazima tufanye hayo, Padre mmoja aliyeitwa Don Bosco alisema
atakwenda mtaani atakusanya vija na walioshindikana na atawakusanya na kuwapa
elimu bila kuwachapa kiboko na watamtii, Padre huyu kutokana na mafanikio yake
makubwa shule nyingi sana zimeanzishwa duniani na zinaitwa kwa jina lake Don
Bosco kukumbuka uwezo wake mkubwa sana katika maswala ya nidhamu, lakini hata
hivyo kama watoto hawasikii biblia imesema wapigwe viboko, sheria inayokataza
watoto kuchapwa ni ya kishetani, kila dini inasema watoto waadhibiwe kuna
sheikh hapa? Mtume Muhamad (SAW) alichapwa, alikuwa hajui kusoma na kuandika
malaika jibril alipomtokea katika pango alimlazimisha asome na akariri kwa jila
la mola wake “Iqraa bism rabik laz kalaaq” alilazimishwa mpaka aliugua aliumwa!
Baada ya kulazimishwa kusoma, wewe lunasema viboko ni haramu? Mungu
anasema wacharazwe
Mithali 13:24 “Yeye asiyetumia fimbo yake
humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.” Kila tabia mbaya tutakayoiona kwa watoto
tuiondoe mapema kwa kuwacharaza, kuna matumaini kama tutawachapa kwa upendo
bila kuzidi kiasi na kuwaumiza au tukiwa na hasira
Mithali 19:18 “Mrudi mwanao, kwa maana liko
tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.” Maandiko
yanasema kuna matumaini tukiwadhibu kuna matumaini tukiwarudi, tena biblia
inasema kwa kuwaadhibu tunaodoa ujinga ndani ya akili zao na mioyo yao na
tunawaopa maarifa
Mithali 22:15 “Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya
adhabu itaufukuzia mbali.” Bilia inaonyesha kuwa fimbo itafukuzilia
mbali ujinga kwa hiyo tusiwanyime adhabu tusiwanyime mapigo
Mithali 23:13-14. “Usimnyime
mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, Na
kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.” Biblia inasema hatakufa ukimchapa
bali utaiokoa nafsi yake na kuzimu, ni fimbo ndio itaweka nidhamu, ni fimbo
ndiyo itakayompa hekima na akili
Mithali
29:15-17 “Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa
humwaibisha mamaye. Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki
watayatazama maanguko yao. Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha
nafsi yako”
mtoto wako akiisha kujua nini mzazi anakitaka mapema
sana atayashika mausia yako na utakuwa ni muongozo mkubwa utakaomsaidia kijana
wako, atajua lipi jema na lipi baya, lazima tuwe na muda na watoto wetu na
kuwaelekeza, na kuwafundisha utii, walekeze kuamkia watu wazima, walekeze
kujilinda na maadui, waelekeze dalili za kujua mtu mwema na mtu mbaya,
waelekeze kujisomea wewe mwenyewe ukiwa kielelezo cha hayo, mara nyingi watu
hulaumu viongozi wa dini kuwa hawa jamaa wanahubiri tu lakini hawatendi sawa na
kuhubiri kwao, haya yameanzia majumbani mzazi anamkataza mtoto wake kunywa
pombe yeye mwenyewe anakunywa, unamkataza asivae mavazi ya kikahaba wewe
mwenyewe unavaa, Lazima tujikite katika kuwalea waoto wetu kwa hali na mali,
wasipotusikiliza baada ya hayo tutakuwa na uwezo wa kutoa Hesabu kwa Mungu,
kuwa sisi tulijitahidi kufanya kila tuliloliweza kwaajili yao, lakini sehemu
nyingine nilikuachia wewe Mungu na sitawajibika kama baba au mama aliyeshindwa kumpatia
mtoto kile alichopaswa!
Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
0718990796
Kwenye swala la kanisa.je ni kanisa lenye misingi gani lina roho wa mungu au ni kweli
JibuFutaIpo Vizuri
JibuFuta