Utangulizi:
Leo nataka kuchukua muda wa
kutosha pamoja na wewe msikilizaji na msomaji wangu kuzungumzia moja ya jambo
muhimu la kibiblia litupasalo sisi kujifunza na hili lina uhusiano mkubwa na
SIKU YA BWANA (JUMAPILI), Katika fungu la maandiko ya msingi utaweza kuona
jambo la kushangaza kuwa Mtume Yohana japo alikuwa utumwani uhamishoni katika
kisiwa kiitwacho Patmo kwaajili ya Mateso, Bado aliweza kuwa katika Roho siku
ya Bwana! (JUMAPILI) Hili ni jamnbo la kushangaza sana na ni muhimu tukalipa
kipaumbele kwani kuna kitu cha kujifunza:
Mtume Yohana alikuwa mzee wa siku
nyingi sana na alikuwa amepelekwa uhamishoni mbali na ndugu jamaa na marafiki
mbali na makanisa na mbali na wale wote waliokuwa naye katika imani, alitupwa
katika kisiwa kikame chenye mawe katika inchi ya Ugiriki visiwani, ili asiweze
kuendelea kuihubiri injili na wala kumuelezea Yesu Kristo kwa watu wengine, kwa
ufupi alikuwa mfungwa kwaajili ya injili. Lakini pamoja na kutengwa mbali na
jamaa zake na watu wake anaandika kuwa alikuwa katika “ROHO SIKU YA BWANA!” (Jumapili) hii maana yake nini? Alikuwa katika
roho siku ya JUMAPILI! kama katika mazingira magumu namna hiii mtume Yohana
alikuwa anakumbuka bila kalenda akiwa mbali akiwa porini akiwa kisiwani akiwa
matesoni kuwa leo ni siku ya Bwana yaani ni jumapili, maana yake ni kuwa hatuna
udhuru au sababu za kutosha kuacha kuipa umuhimu siku hii siku ya jumapili
ambayo hujulikana katika maandiko kama siku ya Bwana.
Maana ya siku ya Bwana!
Ni muhimu kufahamu kuwa Neno siku
ya Bwana linapotamkwa katika Kiswahili au linapoandikwa katika Kiswahili,
linatunyima aina fulani ya upana wa kulizungumzia kwa raha inayokusudiwa hii ni
kwa sababu katika kiigereza kuna maneno makuu mawili ambayo yanatumika kuelezea
siku ya Bwana mfano angalia “THE DAY OF THE LORD” na angalia pia neno “THE LORDS’ DAY” Misamiati hii miwili yote kwa lugha ya Kiswahili huitwa “SIKU YA BWANA” kwa misngi
huo sasa Ni muhimu kufahamu kuwa
neno siku ya Bwana kinabii linaweza kuwa na maana pana sana tofauti na ile
ninayotaka kuizungumzia leo, Neno siku ya Bwana kinabii (THE DAY
OF THE LORD) linamaanisha siku za mwisho, ama majira ya neema na majira ya
hukumu kuanzia ujio wa Yesu Kristo mara ya Kwanza kwa wokovu mpaka ujio wake
mara ya pili kwa hukumu, kipindi hiki kinabii kinaitwa vilevile siku ya Bwana.”THE DAY OF THE LORD” Kwa mfano
1. Siku
Mungu alipotangaza hukumu kwa watu wake Wayahudi au Israel kuwaonya au kuruhusu
wavamiwe na maadui zao kinabii hii pia iliitwa siku ya Bwana Isaya 2:12 “Kwa
maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na
majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.” Unaona
hapa siku ya Mungu kuhukumu watu wake kwa sababu kadhaa inaitwa siku ya Bwana
yaani siku ya Hasira siku ya kuadhibu watu wake unaweza pia kuona katika Amos 5:18-20 “Ole
wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza,
wala si nuru. Ni kama mtu aliyemkimbia
simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake
ukutani, nyoka akamwuma. Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam,
yenye giza sana, wala haina mwanga.”
2. Siku
ya Bwana kinabii vilevile ilimaanisha siku za mwisho yaani tangu ujio wa Yesu
Kristo mara ya kwanza, alipozaliwa, umwagiko au ujio wa Roho Mtakatifu, unyakuo
wa kanisa, kuja kwa Yesu mara ya pili,
kuja kuhukumu ulimwengu, na kuja kutawala
na mbingu mpya na nchi mpya au kipindi cha neema hiki pia manabii
walikiita siku ya Bwana Yoel 2:31 “Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja
hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.” Pia nunaweza kuona katika Matendo 2:14-20 “Lakini
Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia,
Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili,
mkasikilize maneno yangu. Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni
saa tatu ya mchana; lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii
Yoeli, Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu,
na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee
wenu wataota ndoto. Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na
wanawake Roho yangu, nao watatabiri. Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na
ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi. Jua litageuka kuwa
giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo
dhahiri.”
3. Siku
ya bwana kinabii pia humaanisha wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa na
kurudi kwa Yesu mara ya pili na
pia wakati wa hukumu ya watakatifu na mengineyo unaweza kuona katika 1Wathesalonike 5:2 “Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja
kama vile mwivi ajavyo usiku.” 2Wakoritho 1:14 “14. vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu
sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya
Bwana wetu Yesu.”
Unaweza kuona kwa hiyo siku ya
Bwana (The Day of The Lord) ni siku
ya Bwana kinabii ina maana kdaa kama zilivyoainishwa hapo juu na siku ya Bwana
(The Lords’ Day) inayotajwa pekee
katika ufunuo 1:10 ni siku tofauti, ni siku ya jumapili ni siku ambayo katika
somo hili ndio tutakayoizungumzia zaidi kwa kusudi la kuonyesha kwanini
tunaabudu jumapili.
Siku ya Bwana tofauti na siku ya sabato!
Wengine hufikiri kuwa siku ya
Bwana inaweza kuwa siku ya Sabato kwa sababu ni siku iliyotengwa na Mungu mwenyewe
ili wanadamu wapate kumkumbuka na kumuabudu na kupumzika, siku hii inadhaniwa
kuwa ni ile sabato ambayo Mungu aliwaamuru wana wa Israel waiadhimishe kwaajili
kukumbuka ukombozi wao kutoka utumwani kule Misri!
Kumbukumbu la Torati 5: 14-15 “ lakini siku ya
saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe,
wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng'ombe
wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya
malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.
Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa
Bwana, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa;
kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.”
Kwa kawaida sabato hii ya
wayahudi huanzia ijumaa jioni na kuishia jumamosi jioni, siku hii ilikuwa ni
siku ambayo Mungu aliamuru Israel wasifanye kazi yoyote, wao wala watoto wao wa
kiume, wala binti zao,wala watumwa wao, wala wanyama wao, siku hii pia ilikuwa
ni siku ya kuadhimisha kazi ya uumbaji wa Mungu na kuikumbuka kama siku ambayo
Bwana mwenyewe anatajwa katika maandiko kuwa alipumzika au alistarehe! Na
aliiitakasa siku hiyo:-
Mwanzo 2:2-3 “Na siku ya saba Mungu alimaliza
kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake
yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika
siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na
kuifanya.” Ona pia
Kutoka 20:8-11 “Ikumbuke siku ya Sabato
uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni
Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana
wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa
kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote
vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato
akaitakasa.” Na pia
Kutoka 23:12 “Siku sita utafanya kazi yako, na
siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng'ombe wako na punda wako wapate
kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika.”
Sabato ilikuwa ni ishara kwa wana
wa Israel yaani wayahudi kwamba Mungu amewafanya kuwa taifa tofauti na mataifa
mengine ili waweze kumcha Bwana Mungu wao. Lakini ni muhimu kufahamu kuwa
hakuna mahali popote katika maandiko Sabato imewahi kutajwa kama siku ya Bwana
hata kidogo, Sabato iliendelea kutajwa kama sabato katika Biblia agano la kale
na agano jipya na sio siku ya Bwana siku
ya Bwana ni siku tofauti
Mathayo 12:5 “Wala hamkusoma katika torati,
kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia?
“ angalia pia;-
Yohana 7:23 “Basi ikiwa mtu hupashwa tohara
siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi
kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?”
Aidha kwa mujibu wa Mafundisho ya
Mitume inaonekana wazi kabisa kuwa sabato ilikuwa ni kivuli, yaani “typology” kuhusu pumziko halisi la
rohoni ambalo ni Yesu Kristo. Sabato ni alama ya kinabii kuhusu Pumziko halisi
ambalo Mungu atalileta kwa watu wake, Neno Sabato kwa ufupi maara yake ni Raha,
katika biblia ya kiingereza hutumika neno “Rest”
au kustarehe raha zimatajwa katika biblia Mara sita mara tano ikiwa ni raha ya
kinabii inayotabiriwa kuwa watapewa wanadamu baada ya taabu zao za hapa duniani
jumla ya raha zote zinazotajwa katika maandiko ni pamoja na raha
1. Raha au starehe ya Mungu mwenyewe Mwanzo
2:1-3 “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake
lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza
kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake
yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika
siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na
kuifanya.”
Sabato hii ya Bwana ni sabato ya kinabii, katika kitabu cha Mwanzo Mungu mwenyewe alikuwa nabii kabla ya kutuma manabii, ana ametabiri maswala kadhaa yajayo, Mungu alitabiri kuhusu starehe ijayo kupitia sabato hii, hii ni sabato yake, juu ya kazi zake haitajwi tena popote au labda Musa aliiweka kwaajili ya mkazo wa sabato ya kiyahudi ili Israel waweze kujifunza kutoka kwa Mungu, lakini ni wazi kuwa Mungu hapumziki Yesu alisema baba yangu anatenda kazi hata sasa Yohana 5:16-17 “Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato. Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.” Wayahudi walikuwa na fikra potofu kuhusu siku ya sabato, walifikiri Mungu anaopumzika Yesu alikuwa na ujuzi tofauti kuhusu pumziko hili la Mungu, Mungu hakustarehe hii ilikuwa ni alama ya kinabii ya kuja kuwaokoa watu wake na kuwapa sterehe ya kweli baada ya maisha na kazi ngumu za duniani
Sabato hii ya Bwana ni sabato ya kinabii, katika kitabu cha Mwanzo Mungu mwenyewe alikuwa nabii kabla ya kutuma manabii, ana ametabiri maswala kadhaa yajayo, Mungu alitabiri kuhusu starehe ijayo kupitia sabato hii, hii ni sabato yake, juu ya kazi zake haitajwi tena popote au labda Musa aliiweka kwaajili ya mkazo wa sabato ya kiyahudi ili Israel waweze kujifunza kutoka kwa Mungu, lakini ni wazi kuwa Mungu hapumziki Yesu alisema baba yangu anatenda kazi hata sasa Yohana 5:16-17 “Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato. Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.” Wayahudi walikuwa na fikra potofu kuhusu siku ya sabato, walifikiri Mungu anaopumzika Yesu alikuwa na ujuzi tofauti kuhusu pumziko hili la Mungu, Mungu hakustarehe hii ilikuwa ni alama ya kinabii ya kuja kuwaokoa watu wake na kuwapa sterehe ya kweli baada ya maisha na kazi ngumu za duniani
2. Raha au Starehe ya Sabato Kutoka 20:8-11”
Ikumbuke siku ya
Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya
saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe,
wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala
mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku
sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe
siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.” Mungu
aliiweka sabato hii katika amri zake kwa kusudi la watu wa Mungu kuwa na nafasi
ya Mungu katika mioyo yao, kwa nini ilikaziwa sana ilikuwa ni kivuli cha
starehe halisi pumziko halisi ambalo ni Yesu Kristo.
3. Raha au starehe ya Ndoa Ruthu 3:1” Kisha Naomi akamwambia mkwewe, Je! Mwanangu, si vizuri
nikutafutie raha, ili upate mema?” hii ni aina ya sterehe, au
Pumziko ambalo kila mwanamke hutamani kuwa nalo katika maisha yake ndoa
4. Raha au starehe ya kanaani iliyotolewa na Yoshua
Waebrania 4:8 “Maana kama Yoshua angaliwapa raha,
asingaliinena siku nyingine baadaye. “ Mungu aliwaahidi Israel
waliokuwa wakipata shida Jangwani, aliwaahidi starehe aliwaahidi pumziko katika
nchi ya kanaani pumziko ambalo Yoshua alikuwa amekabidhiwa kuwapa hii ni sabato
ya kanaani, hata hivyo hawakuweza kustarehe, walipambana na maadui baada ya
kufa kwake Joshua, raha ya kanaani ilikuwa ni ubnabii tu war aha kamili
itakayoletwa na Yesu Kristo.
5. Raha au Starehe ya wokovu ni raha ya nasfi
inayotokana na kumpokea Yesu Mathayo 11:28-29 “Njoni
kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
nJitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa
moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;” Mtu akimuamini Bwana
Yesu anapata starehe sabato, pumziko la nasfi hata sasa pamoja na taabu zote na
changamoto za dunia liko pumizko katika mioyo ya watu waliomuamini Bwan wetu
Yesu
6. Raha au starehe ya watu wa Mungu wakati
Mungu atakaposimamisha utawala wake hii ndiyo iliyokuwa imetabiriwa katika
maandiko Waebrania 4:9 “Basi, imesalia raha ya sabato
kwa watu wa Mungu.” Hii ndio sabato iliyo tabiriwa kwa watu wa Mungu
itawapata watu wote waliomuamini Yesu Kristo huu utakuwa ni wakati ambapo
masikani ya Mungu itakuwa pamoja na wanadamu milele.
Wakolosai 2:16-17 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi
katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au
sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo”.
Paulo anayazungumza haya akiwa na ufahamu kamili kuwa sabato ni KIVULI yaani TYPOLOGY au unabii wa
pumziko la mwanadamu, Raha hii iliyoahidiwa ndiyo ambayo watu wa Mungu
wanapaswa kuhakikisha kuwa wanaingia hii ni raha ya Mbinguni. Ona:-
Waebrania 4:1-11 “Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya
kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.
Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini
neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani
ndani yao waliosikia. Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; kama vile
alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu: Kwa
maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba,
akaziacha kazi zake zote; na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu. Basi, kwa
kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale
waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,
aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii,
Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo,kama mtaisikia sauti yake, Msifanye
migumu mioyo yenu.Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku
nyingine baadaye. Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana
yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama
vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi, na tufanye bidii kuingia
katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa
kuasi”
Ni wazi kuwa sabato haijawahi
kuitwa siku ya Bwana katika maandiko bali iliitwa sabato hivyohivyo na hii
ilikuwa muhimu kwa wayahudi na sio mataifa mengine, Wayahudi waliomuamini Masihi nyakati za
kanisa la kwanza waliendelea kuitambua sabato kama siku takatifu kwa sababu
ilikuwa mila na desturi yao, aidha ilikuwa ni siku ya makusanyiko na
yangeliweza kufaa kwaajili ya kuihubiri injili na hata mataifa walioamini
nyakati zile kwaajili ya ndugu zao wayahudi,kaka na dada zao waliendelea
kuiheshimu Sabato kama njia ya kumuheshimu Mungu, kwa hiyo kumuabudu Mungu siku
ya sabato sio tatizo, Mungu haangalia usahihi wa siku ya kuabudu bali huangalia
usahihi wa msukumo wa Moyo kama mioyo yetu inasukumwa kuiheshimu na kuishika
sabato kama sehemu ya kuishika sheria basi hapo moyo wako hauko sahihi mbele za
Mungu na tayari umetengwa na Kristo! Ona
maandiko yanasema:-
Wagalatia 5:4 “Mmetengwa na Kristo, ninyi
mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.”
Kama dhamiri zetu ziko safi mbele
za Mungu tuko huru kuabudu siku yoyote ile iwe jumamosi au jumapili au hata
nyinginezo Mungu anapendezwa na dhamiri au mikao yetu ya moyo na sio siku, au
kujitia chini ya Sheria, Mungu hapendezwi na watu wanaomuabudu yeye kwa midomo
tu huku mioyo yao ikiwa mbali naye, awaye yote ambaye anakuja katika ibada kwa
sababu tu ni lazima aje siku hiyo au kwa sababu ya sheria za kibinadamu moyo
wake hauna nafasi katika Mungu bali uko mbali naye.
Isaya 29:13 “Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa
hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami,
na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;”
Mathayo 15:7-9 “Enyi wanafiki, ni vema
alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo;
Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho
Yaliyo maagizo ya wanadamu.”
Mungu hafurahishwi na watu
wanaoshika sheria, maagizo na matakwa lakini anataka moyo unaowakwa kwa upendo
kwake kama mtu anampenda Mungu na kwa moyo wake wote akaamua kuabudu siku
yoyote iwe jumamosi, au jumapili, au jumatatu au jumanne au jumatano, au
alhamisi au ijumaa Mungu ataukubali moyo wa Mtu huyo biLa kujaLi anaabudu lini!
Waebrania 12:28-29 “Basi kwa kuwa tunapokea
ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu
ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho; maana Mungu wetu ni moto
ulao”.
Zaburi 51:15-17 “Ee Bwana, uifumbue midomo
yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako. Maana
hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. Dhabihu za Mungu ni roho
iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.”
Unaona Mungu hataudharau moyo wa
mtu mnyenyekevu, mwenye kumcha yeye moyo uliovunjika na uliojawa na shukurani
kama moyo huo utamuendea siku yoyote ile kwa unyenyekevu bila kujali siku hiyo
ni siku ya namna gani moyo wa aina hii Mungu atautazama
Isaya 66:2 “Maana mkono wangu ndio uliofanya
hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu
ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka,
atetemekaye asikiapo neno langu”
Neno siku ya Bwana katika Biblia
ya kiyunani linasomeka kama neno (mia)
limetumika mara nyingi zaidi katika injili kumaanisha siku aliyofufuka Yesu,
siku hiii ndio ambayo wakristo wa nyakati za kanisa la kwanza waliiheshimu na
kuitumia kwa ibada zaidi na ikijulikana kama siku ya Bwana, Msingi mkuu wa somo
hili ni kuangalia sababu za kimaandiko na za kihistoria kwanini wakristo
wameichagua siku ya Bwana yaani jumapili kuwa siku rasmi ya ibada na kwanini
tunaabudu jumapili, huku hoja ya msingi ikibakia kuwa kwa Mungu siku zote ni
sawa na Mungu humkubali awaye yote anayemuabudu kwa dhati bila kuacha
kuzingatia kuwa siku hii Kristo alijifunua na anajifunua katika siku hii muhimu
ambapo mauti ilimezwa kwa ushindi wa Kristo dhidi ya kifo katika siku ya kwanza
ya juma!
Nalikuwa katika roho siku ya Bwana!
Baada ya kufahamu hasa maana ya
siku ya Bwana na mapenzi ya Mungu kuhusu kuabudiwa kwake ni muhimu kufahamu
kuwa siku ya Bwana inayotajwa katika Ufunuo 1:10 ni siku ya Jumapili hili ni
swala lililo wazi kimaandiko, siku hii ni siku ambayo wakristo wa nyakati za
kanisa la kwanza waliadhimisha kila wiki kama siku muhimu aliyofufuka Yesu
Kristo na ilijulikana kama siku ya kwanza ya juma, ni wazi kuwa neno hili siku ya Bwana katika agano jipya
linatajwa hapa tu, Lakini ni ukweli usiopingika kuwa Yohana alikuwa akiwandikia
watu wakristo ambao walikuwa wanajua wazi kuwa akitaja siku ya Bwana namaanisha
jumapili yaani siku ya kwanza ya juma, jambo ambalo wakristo wa nyakati za
kanisa la kwanza walikuwa wakilijua wazi kwamba siku walizokuwa wakikutana
kuabudu ilikuwa siku ya kwanza ya juma ambayo ni jumapili na sababu kubwa ni
kuwa ilikuwa ndio siku ambayo Bwana Yesu alifufuka kutoka kwa wafu, siku hii
iliitwa au kujulikana kama siku ya kwanza ya juma, ilikuwa ni siku ya namna
gani kwa mujibu wa maandiko na historia
ya kanisa:-
1.
Ilikuwa ni siku ambayo Yesu alifufuka kutoka
kwa wafu Mathayo 28:1-7 “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma,
Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. Na
tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana
alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. Na sura
yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. Na kwa kumwogopa,
wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. Malaika akajibu, akawaambia wale
wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa.
Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali
alipolazwa. Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika
wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha
waambia.”
Marko 16:1-6 “Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu
Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda
kumpaka. Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua
lilipoanza kuchomoza; wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia
lile jiwe mlangoni pa kaburi? Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe
limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno. Wakaingia kaburini wakaona
kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu. Naye akawaambia,
Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa;
patazameni mahali walipomweka”
Luka 24:1 “Hata
siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta
manukato waliyoweka tayari. Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na
kaburi, Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu. Ikawa walipokuwa wakifadhaika
kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo
za kumeta-meta; nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao
waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Hayupo hapa, amefufuka.
Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya,”
2.
Baada ya kufufuka kwake iko wazi katika
maandiko kuwa Yesu alikuwa na tabia ya kuwatokea wanafunzi wake katika siku hii
ona:-
Marko 16:9 “Naye
alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu
Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.”
Yohana 20:19 “ Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma,
pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja
Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.”
Yohana 20:26 “Basi,
baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao.
Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu.”
3.
Kuja maalumu na umwagiko wa Roho Mtakatifu
ulifanyika jumapili siku ya kwanza ya juma hii ni wazi kutokana na desturi kuwa Pentecost
iliadhimishwa siku ya 50 baada ya kukamilika kwa sabato saba sawa na
agizo la
Walawi 23:15-16 “Nanyi
mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mliyouleta
mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba; hata siku ya pili ya hiyo
Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea BWANA sadaka ya unga
mpya.”
Neno Pentecost maana yake “50” Hamsa au hamsini siku hii
ilihesabiwa siku 50 tangu baada ya pasaka yaani zikiisha kupita sabato saba
siku ya pili yake waliadhimisha siku ya Pentecoste ni katika siku hii wanafunzi
walipokuwa wamejifungiwa wakiwa wanaomba Roho Mtakatifu alikuja maalumu duniani
na kuwajaza wote na kanisa lilianza rasmi katika siku hii ambayo kismingi nayo
ilikuwa siki baada ya sabato yaani siku ya kwanza ya juma angalia katika
Matendo 2:1-4 “Hata ilipotimia siku
ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja
ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza
nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama
ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu,
wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.”
4.
Nyakati za kanisa la kwanza watu walikutana
kila siku kuabudu nyumba kwa nyumba angalia
Matendo 2:46 -47 “Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu
ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao
kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu
Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale
waliokuwa wakiokolewa.”
Hata hivyo
kutokana na kuongezeka kwa majukumu mbalimbali katika maisha ya kila siku na
kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi walifikia muafaka kuwa ni vema
ikatengwa siku maalumu kama siku ya kuabudu na ikatengwa siku ya bwana kama
siku ya kuadhimisha siku ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, aidha pia ilikuwa
ni maalumu kwa kuonyesha kuwa wakristo wako mbali au huru kutoka katika sheria
za Musa na siku iliyofikiriwa ilikuwa ni siku ya bwana yaani jumapili, Kwa hiyo
mitume akiwepo na Paulo waliiadhimisha siku hii na kuitumia kamasiku ambayo
waamini wa Kikristo wangekutana na kumuabudu Mungu kwa pamoja
Matendo ya mitume 20:7 “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega
mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza
maneno yake hata usiku wa manane.”
1Wakoritho 16:2 “Siku
ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa
kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;”
5.
Kitabu cha Ufunuo wa Yohana kilifunuliwa
kuanzia siku ya Bwana yaani jumapili Ufunuo
1:10-19 “Nalikuwa
katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, Kama sauti ya
baragumu, ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo
makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na
Filadelfia, na Laodikia. Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na
nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu; na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano
wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu
matitini. Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama
theluji; na macho yake kama mwali wa moto; na miguu yake kama shaba
iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama
sauti ya maji mengi. Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na
upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake
kama jua liking'aa kwa nguvu zake. Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake
kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope,
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na
tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za
kuzimu. Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale
yatakayokuwa baada ya hayo.”
Unaweza kuona ni katika siku hii ya Bwana yaani Jumapili Yohana akiwa anamuabudu Mungu akiwa amezama rohoni akikumbuka wazi kuwa ndio siku ya ushindi na ndio siku ambayo wakristo hukutana kuabudu yeye alikuwa katika roho akiungana nao kumuadhimisha Yesu na ndio unaona sasa Yesu akimtokea katika siku hii na kumuagiza aandike kitabu cha ufunuo ni wazi kabisa kuwa kibiblia siku hii sio ya kupuuzwa na uko umuhimu mkubwa wa kuabudu katika siku hii sawa na fundisho la mitume na kama yanenavyo maandiko
Unaweza kuona ni katika siku hii ya Bwana yaani Jumapili Yohana akiwa anamuabudu Mungu akiwa amezama rohoni akikumbuka wazi kuwa ndio siku ya ushindi na ndio siku ambayo wakristo hukutana kuabudu yeye alikuwa katika roho akiungana nao kumuadhimisha Yesu na ndio unaona sasa Yesu akimtokea katika siku hii na kumuagiza aandike kitabu cha ufunuo ni wazi kabisa kuwa kibiblia siku hii sio ya kupuuzwa na uko umuhimu mkubwa wa kuabudu katika siku hii sawa na fundisho la mitume na kama yanenavyo maandiko
6.
Ushahidi
wa Mababa wa kanisa
-
Ignatius
aliandika hivi “hatupaswi kuihika sabato tena. Lakini tunapaswa kuishi sawa na
siku ya Bwana ambayo nuru ya kweli iliangaza”
-
Justin
mfia dini alisema alipokuwa akiutetea Ukristo “Jumapili ni siku ambayo sisi tu
akusanyika kwa sababu ni siku ambayo Mungu alileta mabadiliko makubwa kwa
kuondoa giza ulimwenguni na ndio siku ambayo Yesu Kristo mwokozi wetu alifufuka
kutoka kwa wafu
-
Mafundisho
ya mitume yaliyokusanywa Mwaka 105 AD ynasema hivi, “Mitume kwaajili ya hayo
waliichagua siku ya Bwana siku ya kwanza ya juma kwaajili ya ibada na kwaajili
ya kusoma maandiko na kushiriki Meza ya Bwana kwa sababu ni siku ya kwanza ya
Juma ndipo Yesu alifufuka”
-
Eusebous
mwana historia aliyeheshimika sana nyakati za kanisa hata wakati wa mfalme
Contantine aliandika hivi “Tangu mwanzo
wakristo walikusanyika siku ya kwanza ya juma kwa makusudi ya kuabudu kusoma
maandiko, kuhubiri na kushiriki meza ya Bwana , kwa sababu Yesu alipata ushindi
dhidi ya kifo siku hii na amakuwa wa kwanza katika cheo na hivyo anapaswa
kuheshimiwa kuliko sabato ya kiyahudi”
7.
Yesu
Kristo ndiye Bwana wa Sabato
Ni muhimu
kufahamu maana ya maneno haya Yesu ndiye Bwana wa Sabato, Meneno haya
yamerejewa mara kadhaa katika injili za
Mathayo 12:8 “Kwa
maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato”. na Marko 2:28 “Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.” Na
Luka 6:5 “Akawaambia, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa
sabato.”
Yalikuwa ni
maneno ya Yesu mwenyewe kuwa Yeye ndiye bwana wa Sabato Yesu alikuwa
anamaanisha nini kusema haya? Alikuwa akimaanisha Yeye ndiye mwenye mamlaka
dhidi ya sheria zote na taratibu zote ikiwemo sheria ya Sabato, Yesu alisema
kwa maneno mengine yeye ni mkuu kuliko sabato, yeye ni mkuu kuliko sheria ,
yeye ndiye mfanya sheria , Mafarisayo walikuwa wameikazia sheria na kutunga
shetria zipatazo 39 za kuikazia zaidi siku ya sabato na kuisimamia kana kwamba
wao ndio wafanya sheria Yesu alikuwa akiwaambia wazi kuwa yeye ndio Muumba na ndio kwa asili mwanzilishi wa
sabato hakuna mtu mwenye mamlaka ya kumuamrisha aitumiaje ilihali yeye ndiye
mtawala wa kanuni hiyo
Yohana 1:3 “Vyote
vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.”
Ona pia
Waebrania 1:10 “Na
tena, Wewe,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za
mikono yako;”
Yeye
ni zaidi ya Mafarisayo na ndiye mwenye mamlaka ya kuwakosoa mila na desturi zao
wanazofikiri kuhusu Matumizi ya sabato yeye ndiye mwenye mamlaka kamili ya
kutafasiri matumizi sahihi ya sabato Yeye kama mtawala dhidi ya sheria zote
ikiwemo sabato ana mamlaka ya kuitumia kama apendavyo yuko juu ya sheria hii,
Yeye ndiye sabato yenyewe hakna mwanadamu anaweza kupata pumziko la kweli
pasipo Yesu, yeye alikuja na kufa na kufufuka ili atukomboe nalaana yote ya
torati ikiwemo mateso ya kuishika sabato, Wokovu tulio nao katika Kristo
umeifanya sheria ya agano la kale ikiwemo sabato isiwe na maana tena kimsingi sabato ilifanyika yaani iliwekwa au ilikuwepo
kwaajili ya mwanadamu na sio mwanadamu kwaajili ya sabato
Marko 2:27 “Akawaambia,
Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.”
maana yake
sabato ilikuwa ni unabii kwaajili ya kuwapa wanadamu pumziko baada ya kufanya
kazi kwa mikono yao wenyewe kwa siku sita, tafasiri sahihi ni kuwa hakuna mtu
anaweza kujiokoa kwa kazi zake mwenyewe wokovu wa kweli na pumziko la kweli
ljnatoka kwa Mungu, sasa tunaweza kustarehe katika neema yake badala ya
kuhangaika kutafuta kibali cha Mungu kwa nguvu zetu wenyewe Yesu amkuja
kuifanya kazi hiyo
Mathayo 11:28 “Njoni
kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa
moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;”
Sasa hapa Yuko
mfalme na hapa iko katiba, hapa ziko mali na hapa yuko mtoa mali, hapa uko uhai
na hapa yuko mtoa uhai, hapa iko sabato na yuko bwana wa sabato, wewe utachagua
nini? Aliyeweka sheria au sheria yenyewe, wale wanaoadhimisha ibada siku ya
jumapili wamemchagua Yesu mwenyewe na wale wanaoadhimisha sabato wamechagua
sheria ya Musa
Sabato, muandamo
wa mwezi na kadhalika zilikuwa ni alama kivuli alama za kinabii zinazomuhusu
Yesu Kristo na hivyo wakristo hawapaswi kuhukumiwa na mtu awaye yote kuhusu
maswala hayo ambayo kwa sasa hayana maana, huku tukitilia maanani kuwa
hatupaswi vilevile kuwahukumu wanaozing’ang’ania kama wana dhamiri safi na
hakuna anayepaswa kumshambulia mwenzake muhimu ni Yesu Kristo
Wakolosai 2:16-17 “Basi,
mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au
mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili
ni wa Kristo”.
Ikumbukwe pia
wazi kuwa jumapili siku ya Bwana wala sio mbadala wa sabato, yaani kwa maneno
mengine jumapili sio sabato ya wakristo, ni siku ya kumuabudu Yesu, pamoja na
kuwa tunaweza kujichagulia siku yoyote kwa mapumziko na kumuabudu Yesu
aliyekufa na kufufuka kwaajili yetu na sio kwa misingi ya Torati ya Musa,
Warumi 6:14-15 “Kwa
maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini
ya neema. Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali
chini ya neema? Hasha!”
Watu
waliookolewa wako huru kumuabudu Mungu siku yoyote na hakuna siku yenye maana
kuliko nyingine awaye yote anayekuja na hoja ya kufikiri au kubishana kuhusu
siku ni mpumbavu na hayajui maandiko, hakuna sababu ya kumuhukumu mtu awaye
yote anayeabudu siku fulani kama anaabudu kwa moyo, cha msingi ni nani anayeabudiwa na sio siku gani anaabudiwa, Mtu
aliyekomaa kiroho hawezi kupata shida ya ipi ni siku ya kuabudu Paulo mtume
alishafunga mjadala kuhusu siku ya kuabudu, lakini ni vema ikaeleweka wazi kuwa
sabato ilisisitizwa kama alama kivuli cha starehe au raha ijayo ambayo ina
uhususiano na raha ya wokovu na raha ya milele pumziko la kweli la wanadamu
lililoandaliwa na Mungu.
Warumi 14:4-5 “Wewe
u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama
au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha. Mtu mmoja
afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa.
Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.”
Hitimisho:
Siku ya Bwana ni
muhimu kwa sababu ndio siku ambayo Yesu alifufuka, ndio siku ambayo sabato
halisi alitukomboa na kutuweka huru, ndio siku ambayo Yesu alikuwa akiwayokea
wanafunzi wake, ndio siku ambayo tamaduni za kanisa la kwanza walikuwa
wakikkutana kusoma neno, kuomba, kuumega mkate na kushirikiana na ndio siku
ambayo mtume yohan a alikuwa katika roho, na ni siku ambayo inajitofautisha na
wale waliomkataa Yesu wakiwemo baadhi ya wayahudi, ni siku ya kipekee
inayoonyesha kuwa tuko huru mbali na sheria ya Musa na kongwa zima la sheria za
kiyahudi ambazo haziwezi kuokoa ni siku ya neema ya Mungu! Mwenye masikio ya kusikia na
asikie!
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima!
0718990796
Nimekuelewa mtumishi wa Mungu , nilikuwa natafuta maana ya siku ya bwana. Nimesoma na nimeelewa sana . mungu akubariki sana
JibuFutaMungu akubariki sana mtu wa Mungu kwa kunifungua ufahamu. Asante sana.
JibuFuta