Jumanne, 21 Aprili 2020

Unapozungukwa na kamba za mauti!


Zaburi 116:1-6Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa.”



Utangulizi:


Ni moja ya zaburi ya kipekee sana, Mwandishi haonyeshi kama iliwahusu watu wote lakini ilimuhusu yeye binafsi na hali iliyomzunguka na anaonyesha njinsi anavyompenda Bwana kwa kuwa anamsikia zaburi hii imegawanyika katika maeneo makuu matatu, anamsifu Bwana na kuonyesha ji kwanini anamsifu na anampenda, lakini pia anaelezea mambo magumu yaliyomkuta na jinsi bwana alibyomuokoa na anaelezea namna anatavyo mshukuru, kwa hiyo ni zaburi ya shukurani binafsi kutokana na kuokolewa na mitego au kama au hali zinazolazimisha afe!


Zaburi hii haijulikani mwandishi ni nani na tukui husika ni lipi lakini inaonekana mwandishi alikuwa akimshukuru Mungu kwa kumuokoa na mauti au hali za kifo zilizokuwa zikimuandama, uchunguzi wa kimaandiko unaonyesha kuwa huenda zaburi hii ni ya Nabii Yona ingawa hatuna ushahidi wa kutosha kama Yona alitunza Zaburi, vyovyote vile iwanvyo inaonekana Yiona akliisema zaburi hii alipookuwa akimuomba Mungu kwenye tumbo la Nyangumi, na kinabii inamuhusu Masihi ambaye alipokufa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu tuona 


Yona 2:1-10Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu. Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.  Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu;  Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu, Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana.Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.” 


Unaona ni Zaburi ambayo tukio lake linafanana kabisa na tukio la Yona Lakini mambo ambayo tunaweza kujifunza kutoka katika zaburi hii ya shukurani ni maswala makubwa matatu



1.       Mwimbaji anaonyesha sababu za kumshukuru Mungu
2.       Mwimbaji anaonyesha nini cha kufanya tunapozungukwa na kamba za Mauti
3.       Mwimbaji anaonyesha mwitikio wa Mungu wetu tunapoliitia jina lake



Sababu za Kumshukuru Mungu.


Ziko sababu nyingi sana za sisi wanadamu kumshukuru Mungu, na kumpenda hata tunapokuwa katika wakati mgumu, sisi kama wenye dhambi Mungu anapotuonyesha kuwa hatustahili na kuwa wakati wowote anaweza kutuangamiza kwa hasira yake kwa kuwa hakuna hata mmoja anayefaa tunaweza kujikuta tunataabika sana na tunajawa na hofu kubwa na huzuni, Hakuna mwanadamu hata mmoja anayestahili kuwa hai wakati Mungu anapoikasirikia Dunia, hakuna anayeweza kudhani ya kuwa yeye anafaa, hakuna kuhani wala nabii, sheihk wala padre askofu wala mpagani, hakuna hata mmoja tunayeweza kusema hastahili kutubu Ni kwa rehema zake tu ndio maana hatuangamii, hakuna asiyejaribiwa au kujaribika hata mmoja ujumbe wa toba unamuhusu kila mmoja kwa sababu neno la Mungu linasema wote wamepotoka wameoza wote pia hakuna mtenda mema kla hata mmoja kwa tendo moja tu la kuwa na uhai na kugundua kuwa yuko Mungu huilo pekee linalazimisha tumpende Mungu na kama tukimuita na akatuitikia hilo nalo linapaswa kuongeza upendo wetu kwake, Yona alipogundua tu kuwa Yuko hai na alipokuwa akimuitia Mungu kama nabii na kujua kuwa Mungu anamuitikia akikumbuka jinsi alivyokataa kutii kwa makusudi akikumbuka jinsi mauti ilivyokuwa ikimuandama hata kura za kifo zilimuangukia yeye akikubalia kwa hiyari yake afe ili wengine wawe salama kwenye melikebu, alimezwa na samaki, alilia katika tumbo la Nyangumi na kuweka nadhiri na Mungu akamisikia tukio hili pekee lilimfanya awe na wingi wa shukurani!


Yona 1:6-17 “Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee. Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona. Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu. Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha. Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata. Lakini wale watu wakavuta makasia kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana. Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda. Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka. Ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri. Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku


Unaona ni kupitia hali hii bahari ilichafuka na kura zilionyesha kuwa yuko mtu ameacha kumtii Mungu na ni kwaajili yake mabaya yanatokea hivyo ingawa alikuwa amelala hana wasiwasi Yona alikuwa anakambiliwa na mauti, kamba za mauti zilikuwa zimemzunguka na kwa kuliitia jina la bwana akaokolewa na hali ile ni kwa sababu hii anaona ziko sababu za kumshukuru Mungu, Yuko Munghu anayeisikiliza sauti yetu hata kama tumemkosea hili ni jambo la kushukuru kwamba tukiliitia jina lake atatusikia na atatujibu, wakati huu sasa dunia inapitia katika majanga ya aina mbali mbali mazito na tishio kubwa sana la kiuchumi hakuna mtu anayeweza kujigamba kwamba yuko salama wote tumeasi, wote tumekosea kuna mahali hatuko sahihi, hatuwezi kuwasingizia watu fulani tu wala hatuwezi kusema kuwa sisi ni bora kuliko wengine Mungu yu atuita katika toba, sio toba ya Kenya pekee, wala sio toba ya Tanzania pekee wala New York Pekee wala Brazil, Ni toba ya ulimwengu mzima nchi chache zimeweza kugundua siri ya kuliitia jina la bwana walifanya vema nchi chache na viongozi wachache sehemu fulani fulani za dunia wameweza kufunnga na kuomba kwaajikli ya janga hili la Corona ambalo ni janga la dunia sasa ni wakati wa umoja wa mataifa kutambua kuwa yuko Mungu wa kweli, sio kenya pekee wala tanzania pekee wala Brazil pekee wao wameshafanya sehemu yao kila mtu anapaswa kufanya toba kwa sehemu yake Lakini wito kwa viongozi wa umoja wa mataifa na mashirika makubwa ya kimataifa ulimwenguni wanapaswa kutambua kuwa Yuko Mungu aliyehai, ambaye tukimuita kwa pamoja bila jujali itikadi zetu atatuitikia katikamelikebu wale watu waliomba na Yona waliomba bila kujali itikadi zao na melikebu ikatulia Yona naye aliomba kwa namna yake na Mungu akamsikia Yona hapa anawakilisha Israel na watu katima melikebu wanawakilisha ulimwengu na Nahodha wa melikebu anawakilisha umoja wa mataifa kupata suluhu hapa ni kuliitia jina la Mungu aliye hai kwa dunia nzima, tukifanya hivi dunia itatulia na wote tutampenda Mungu, Lazima sasa dunia ionyeshe upendo kwa Mungu kwa sababu yeye alitupenda kwanza 

1Yohana 4;19 “Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.” Mwandishi anampenda Mungu aamtukuza kwa kuwa ni Mungu anayesikia maombi na kuyajibu.


Tunapozungukwa na Kamba za mauti   

 
Kifo ni moja ya adui yetu mkubwa duniani chenyewe huanza kututafuta dakika moja kuanzia unapozaliwa kitakuandama tu kuhakikisha kuwa kinakuondoa duniani, hivyo hatupaswi kujisahahu hata kidogo, tunazungukwa na kamba za mauti zinatuvuta tufe Mungu ametufundisha mambo ya ajabu kupitia gonjwa hili la corona linatunyoosha linatishia kifo cha kiuchumi, linatishia matajiri linatishia masikini Mungu ameruhusu, ni kamba za mauti zinatuzunguka kila mahali bila kujali wewe ni nani, narudia tena bila kujali wewe ni nani? Kama mtoto wa malikia wa uingereza anaugua Corona, kama waziri Mkuu wa uingereza anaingia ICU kwaajili ya Corona, ni Fundisho kuwa wewe na mimi kama si Bwana hatuwezi kupenya, bila neema ya Mungu hatuwezi kutoboa ni kamba za mauti zinazunguka kila mahali, je ni nabii gani sasa anaitisha maombezi dhidi ya korona mbona imebadili mifumo yatu ya maisha mpaka mifumo ya kuabudu, Je ni shetani? Je ni Pepo? Vyovyote iwanvyo yesu ndiye mwenye funguo za mauti na kuzimu bila ruhusa yake corona haiwezi kuitikisa dunia ukiona hili Mungu maeruhusu, ili tuwe wanyenyekevu, ili tukumbuke kumuheshimu, ili tukumbuke kuwa yeye yupo ili tukumbuke kuwa dunia sio ya taifa fulani, Hatari za kifo zilimzunguka mwandishi wa zaburi hii na sio hatari tu mwenyewe anaziita kamba za mauti, shida za kuzimu na taabu na huzuni vilimuandama hii ndio hakli ya dunia kwa sasa, Dunia inazungukwa na kamba za mauti kila mahali watu wamejaa hofu ya kifo, idadi ya wagonjwa inaongezeka na idadi ya vifo inaongezeka, hakuna usalama watu hawaaminiani wala hawajiamini hata wao wenyewe, wale wanaougua ndio zaidi na hata wale waliopona wanaweza kukusimulia maumivu makali waliyokutana nayo, ndoto nza kaburi walizoziona je unapopokea taarifa kuwa una Corona unakuwa katika hali gani, familia ambazo ndugu zao au jamaa zao wamebainika kuwa wana Corona na hata wataalamu wa Afya wanaowauguza wagonjwa hao wako katika hali gani? Unaposafiri nani anakuamini, mbuga za wanyama zina hali gani, sekta za usafiri zina hali gani, secta ya utalii ina hali gani, wafanyakazi wa serikali na secta binafsi zina hali gani wakati huu? Hata makanisa na mkisikiti na vionghozi wa dini tuna hali gani? Kamba za mauti zinaizunguka dunia, Mwandishi anasema


  Zaburi 116:3-4Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; Nikaliitia jina la Bwana nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu  


Hii ni halia inayomzunguka mtu aliye hai lakini anayezingirwa na halia ya mauti anakiona kifo kikiwa kinamuwania kwa kila namna hatuwezi nkukikwepa kiko hewani tu, hata kiliowakuta walitoka wakijiamini kama wewe na mimi, Mwandishi anasema alipoona anazungukwa ma kamba za mauti na shida za kuzimu zilimpata na aliona taabu na huzuni yeye aliliitia jina la Bwana, dunia inaangalia suluhu kwamba itapatikana wapi pamoja na tahadhari zote tunazozichukua suluhu ni kuliitia jina la Bwana 

WARUMI 10:13 “KWA KUWA KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA

 hakuna nafasi kwa mwanadamu kujiokoa yeye mwenyewe Mungu alimleta mwokozi kwaajili ya ulimwengu wakati huu ni lazima tumuite Yesu kwaajili ya usalama wetu tumeweza kufanya kitaifa lakini kanisa linaweza kuendelea, Biblia inatuagiza kuomba bila kukoma, kwa nini tumuombe yeye Mungu mwandishi anasema Mungu ni mwenye rehema ona 

Zaburi 116:5-6 “Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika akaniokoa”, 

unaona Mungu ataziokoa nafsi zetu, Mungu ataiokoa nafsi yako kwa sababu ni wa neema na haki, kwa sababu ni mwenye trehema kwa sababu huwalinda wasio na hila na tunapodhikika hutusikia ni maombi tu ndio njia pakee ya kututoa katika janga hili Yesu Kristo mwenyewe alitufundisha kivitendo umuhimu wa kumuomba Mungu 

Luka 6;12  Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.” 

Mungu atashughulika na kila aina ya kamba za mauti zinazokuzunguka. Ukiacha corona ziko kamba nyingine za mauti zinazokuzunguka zote kumbuka kuzisogeza mbele za Munhu wetu naye atakusaidia hatoakuacha


Mwitikio wa Mungu wetu tunapoliitia jina lake


Mwandishi alipokuwa katika hali hizo ngumu zlizomzunguka katika maisha yake na taabu zilizomzunguka katika maisha yake na magumu yaliyokuwa yakimzunguka katika maisha yake Mungu aklimuitikia kwa msingi huo aliweza kugundua kuwa kwekli Mungu ni mwema mno Mungu ni mwingi wa rehema , mwenye huruma na neema naye huwahurumia watu wake wanaoteseka na huwaokoa ndivyo neon lake lisemavyo angalia 

Zaburi 86:5 “Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.” 

Hatustahili kuishi, tulistahili kufa kwa sababu wote ni wenye dhambi hakuna aliye mwema lakini trehema za mungu na neema yake zinamfanya atuitikie na zinamfanya atuokoe na mauti na kutuweka huru kutoka katika kamaba za Mauti, jambo pekee litakalotuletea neema ya mungu ni kumlilia yeye na kumwambia Eeebwana utuhurumie, eee mwana wa Daudi utuhurumie Roho Mtakatifu utuhurumie, roho zetu na za familia zetu na za watu wa taifa letu na taifa lako Israel na jamii ya dunia na irehemiwe mbele zako na Mungu atasikia dua zetu, tuache ushabiki, wakati huu, tusijitukuze sana wakati huu na kujifikiri kuwa sisi ni bora sana wakati huu hapa ni toba tu bila kujali wewe ni nani na kuziitia rehema za Mungu


Mungu atafanya nini?  Zaburi 116: 6 “Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa Mungu alimuokoa na Mungu alimlinda mtumishi wake mwandishi wa zaburi hii kwa sababu wakati huu aliacha hila aliacha nia mbaya aliacha kiburi na alijinyenyekeza, Neno hilo Nalidhilika maana yake nilijishusha nilijinyenyekesha sikujifanya mtu maalumu, nilijishusha nilishuka chini, nilijinyenyekeza kwenye nafasi ya mtu anayehitaji msaada, wakati huu tuache kiburi cha kidhehebu, tuache kiburi cha kidini, tuache kujifanya sisi ndio manabii na mitume na wachungaji wakubwa na kadhalika tujinyenyekeshe na Mungu wetu ataturehemu, wakati mambo yanapokuwa mabaya acha kujitokeza na kujifanya kuwa wewe ndio msemaji wa Mungu, pekee duniani, Ndio maana wako waliosema corona itafutika na corona ikaendelea huu sio wakati wa kujifanya wewe ni mtu maalumu ni wakati wa kujidhili na wakati wa magoti, ni wakati wa kutulia na kumuacha Mungu atusaidie Mungu asipokuwa msaada wakati huu nafsi zetu zitanyamazishwa ona 

Zaburi 94:17 “Kama Bwana asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya. Wale wenye hekima ya dunia hii na wenye kiburi wanaweza kudhani kuwa Mungu sio msaada wao wakati huu, Lakini huu sio wakati wa kujitukuza na kutafuta kiki, lazima sasa tumuachie Mungu apangue, asafishe afanye yaliyo mapenzi yake na kwa unyenyekevu Mkubwa Mungu atatuponya tu, kwa sababu tuko mbali na hila na kiburi na tumeamua kujinyenyekeza, kumbuka kuwa  Bwana huwapinga wenye kiburi bali huwapa wanyenyekevu neema, sote tuko katika umbo la Nyangumi na tunapaswa kuomba rehema za Mungu naye atatusaidia katika njia anayoijua yeye, sio wakati wa kunyooshea kidole mtu Fulani dhilika yaani nyenyekea, usijifany mwenye hekima wakati huu zaidi ya toba hekima kubwa wakati huu ni toba wala tusidhani imetosha nni toba wala tusiombee kingine chochote ni toba na rehema tu na Mungu atatuitikia alimuitikia yona kwenye tumbo la Nyangumi atatuitikia na sisi katika nchi ya walio hai haleluya!

  1Wakoritho 1:27” bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;asomaye na afahamu.


Na Mchungaji. Innocent Kamote


Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni