Malaki 2:14-16 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa
sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda
mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. Hakuna mtu mmoja
aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja
atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye
yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia
kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa
udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije
mkatenda kwa hiana.”
Utangulizi:
Mojawapo ya changamoto kubwa zinazoukumba ulimwengu
wa leo ni pamoja na changamoto kali katika ndoa, kila kunapokucha na katika
kila mazungumzo, mafundisho na mijadala swala la ndoa na changamoto zake
haliwezi kukosekana swala hili linasumbua wengi katika jamii masikini kwa
matajiri, wenye cheo kwa wasio na cheo, wenye elimu na wasio na elimu wakristo
na wasio wakristo na kadhalika; Kuna tatizo kubwa sana katika swala la ndoa,
hata kwa wataalamu wa saikolojia, walimu na hata watumishi wa Mungu wenye
kuzijua ndoa kwa kina na mapana na marefu bado linapokuja swala la ndoa watu
wote huingia katika malalamiko ya changamoto hii! Walimu wengi wa Ndoa na
mahusiano wamejaribu kutoa ufahamu wa aina mbalimbali katika ndoa ili ndoa
ziweze kuwa na amani na zinaweza kufanya kazi kwa kiwango flani lakini huwa
wanasahau kuzungumzia swala moja la muhimu kuhusu VITA VYA KIROHO DHIDI YA NDOA! Wengi watafundisha kuhusu ndoa,
majukumu ya mwanamke na mwanaume, wajibu wa mke na mume, maswala ya mahaba na
staili na mitindo, vyakula muhimu vya wana ndoa sijui nini sijui nini lakini wanasahau
kuzungumzia kwamba kuna vita vya kiroho dhidi ya ndoa hili ni muhimu kujulikana
kwa kila mwana ndoa vinginevyo hakuna kitakachoweza kufabnya kazi, masomo yote
ni ya muhimu lakini kama changamoto bado ziko hapa linabaki swala la mapambano
ya kiroho kwa ajili ya ndoa yako!
Ndoa ina vita zake hii ni muhimu kufahamu.
2Wakoritho 2:11.”Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana
hatukosi kuzijua fikira zake.” Ni muhimu kufahamu kuwa ziko mbinu za utendaji
wa ibilisi zinazopambana na ndoa sahihi ili isiweze kufanya kazi, na shetani
anaweza kukupa amani ambayo unaweza kudhani kuwa ni amani ya kweli kwa kukubali
kuweko kwenye ndoa bandia baada ya kushindwa vita katika ndoa Halisi, watu
wengi sana wanadhani kuwa wana amani sasa kwa kuweko kwenye ndoa ambazo sio
mpango wa Mungu na huko wanaweza kusema kuwa ndoa ile sio mpango wa Mungu,
labda mwanzoni nilikosea au pale nimeingia cha kike swali kubwa la kujiuliza
kwanini ile ndoa yako ya awali ilikuwa na vita kiasi kile ? na sasa je unadhani
una amani ya kweli kwa kuwa sasa uko katika ndao ya pili? Je hujawahi kujiuliza
kuwa amani hiyo sio ya Kristo? Imetokana na kuwa shetani hawezi kukupiga vita
tena kwa sababu umeshashindwa vita na umekuwa mateka wake ukijifariji katika
ndoa isiyokuwa ya halali hata kama imefungwa na mchungaji flani! Angalia!
Shetani anaitwa mungu wa dunia hii na moja ya kazi yake ni kupofusha fikra uwezo
wa kufikiri au kumgundua na kupata upenyo, anapofusha fikra za watu wa
ulimwengu huu wasiijue kweli ambayo itawaweka huru 2Wakoritho 4:4 “ambao ndani yao mungu wa
dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya
utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.” Yeye ni muongo ni mwenye
hila na kwa kutumia hila zake anauwezo mkubwa sana wa kuudanganya ulimwengu ona
pia Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani,
aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na
malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Unaona maandiko yanamuita
shetani joka Mkubwa, joka la zamani anaujuzi wa kupanga mambo, ana ujuzi wa
kushambulia ana ujuzi wa kutenda kwa hila ili audanganye ulimwengu ana vita
dhidi ya kanisa ana vita dhidi ya taasisi inayoitwa ndoa, kabla ya kupigana na
kanisa zamani sana alianza kupigana na ndoa, ndo ndio taasisi yake ya kwanza
kupambana nayo, fikiria leo alivyofanikiwa kusambaratisha maneno ya Yesu Kristo
mwana wa Mungu aliye hai leo ynaonekana kama maneno yasiyotekelezeka na
yaliyojaa uongo je ni ili shetani aonekane kuwa mkweli? Tujikumbushe maandiko
kuhusu kile alisema Yesu hapa Mathayo
19:3-10 “Basi Mafarisayo
wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa
kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo,
aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye
na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata
wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu,
mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa
hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo
yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha
mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye
amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na
mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.” Kutokana na uongo wa
ibilisi kifungu hiki kimewashinda wengi kukitii na kukifanyia kazi katika
ulimwengu wa leo, kumbuka hata Dunia na mataifa makubwa na makanisa makubwa
yanapofikia ngazi ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja leo hii ni muhimu kwetu
kukumbuka kuwa hii ni mojawapo ya dalili ya kiwango cha juu cha shetani
kupambana na kitu kinaitwa ndoa, wengi wamekivunjilia mbali kifungu hicho cha
maandiko wakijihalalishia ndoa zisizo sahihi chini ya amani ya muda mfupi ya
shetani, Sheatani anachukizwa na ndoa shetani anachukizwa zaidi na ndoa ya
Kikristo, shetani anapiga vita ndoa sahihi, kwa sababu anajua kuwa kwa kufanya
hivyo anaizuia injili isiwafikie walengwa na watu hao wakakokolewa kwa sababu
kwenye ndoa kuna siri kubwa sana inayofananana na siri ya kuwepo kwa kanisa Waefeso 5:32-33 “Kwa sababu hiyo
mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili
watakuwa mwili mmoja.Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na
Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke
asikose kumstahi mumewe.” Ni kwaajili ya jambo hili ni muhimu kwetu kuangalia kwa undani kuhusu
vita vya kiroho katika ndoa ili kujiepusha na kuangalia upande mmoja wa
shilingi ikiwemo swala la mahusiano, mawasiliano, taili, uongozi, wajibu na
majukumu, malezi na kadhalika na tusisahau kuwa pamoja na
umuhimu wa haya yote ndoa inapigwa vita kali sana !
Ndoa katika mpango wa
Mungu!
Mungu alimuumba mwanadamu katika sura na mfano wake
Mwanzo 1;27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa
Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Mwanamke na mwanaume
wanapofunga ndoa wanafunua mpango maalumu wa Mungu neno kuumbwa kwa Mfano wa
Mungu kwa kiyunani linatumika neno “imago
dei” ambalo kwa kiingereza ni
intellectual ability, Moroal decision and the ability to make wilful choice,
purity and ruling, uwezo wa kiakili, maamuzi ya kimaadili, uwezo wa kuchagua
usafi na utawala kwa hiyo mwanadamu aliumbwa awe mwakilishi wa Mungu na Mungu
alimuamuru mwanamke na mwanaume kuitawala Dunia kueneza utukufu wake kumfanya
yeye asifiwe huu ndio ulikuwa msingi wa mwanzo kabisa wa Ndoa Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni,
mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Kuzaa na kuongezeka hapa ni kuendeleza uzao wa Mungu duniani kwa jamii
ya watu wanaomtii na kumuheshimu Mungu na kutangaza utukufu wake Kwa kupitia
ndao hii ya kwanza tunauona wazi kabisa Mpango wa Mungu ni kuzalisha watu
watakaomtukuza yeye Duniani, watu watakaodhihirisha uhodari wa kutembea na
uwepo wa Mungu na Biblia katika fundisho hili inaonyesha wazi kupitia uumbaji
huu Mungu alikusudia kwamba
·
Ndoa iwe ya mke mmoja Mume mmoja
·
Ushirikiano wa tendo la Ndoa uwe ni wa jinsia ya kiume na ya kike
·
Kiongozi katika ndoa aliwajibika kuwa Mwanaume kutokana na kuumbwa
kwanza
·
Ndoa ilikusudiwa iwe ya kudumu na yenye umoja usioweza kutenganishwa
maneno ya Adamu huyu ni Mfupa katika mfupa wangu na nyama katika nyama yangu
yanatumika kuonyesha umoja usioweza kutenganishwa yaani Adamu na Eva walikuwa
kitu kimoja na umoja wao ulikuwa wa kudumu na msikamano wao ulikuwa
ukitenganishwa ni kifo ndio kingetokea kwao wote Neno Mfupa wangu na nyama
yangu katika agano la kale lilitumika kumaanisha Undugu ambao kwa namna yoyote ile
hauwezi kukanushika ona Mwanzo 29:14 “Labani akamwambia, Ndiwe kweli mfupa wangu na nyama
yangu. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja.” Ona pia Waamuzi 9:2 “Haya,
neneni tafadhali masikioni mwa waume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi
lililo jema kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini,
watawale juu yenu, au kwamba mtu mmoja atawale juu yenu? Tena kumbukeni ya
kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.” Linganisha pia 2Samuel 5:1 “Ndipo
kabila zote za Israeli wakamwendea Daudi huko Hebroni, wakasema naye, wakinena,
Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako.” Tungalie pia 2Samuel 19:12 “Ninyi
ni ndugu zangu, ninyi ni mfupa wangu na nyama yangu; mbona basi ninyi mmekuwa
wa mwisho wa kumrudisha tena mfalme. “ 1Nyakati 11:1 “Ndipo Israeli wote
wakamkusanyikia Daudi huko Hebroni, wakisema, Tazama, sisi tu mfupa wako na
nyama yako.” Unaona neno Mfupa wangu na Nyama yangu lilitumika
kumaanisha umoja usioweza kutenganishwa kamwe, muunguno usioweza kukanushwa
sasa ukaribau anaokuwa nao mke na Mume na muungano wao wa kimapenzi na uwezo
wao wa kushirikiana tendo la ndoa na Baraka za Mungu huwafanya wao wawe karibu
zaidi kuliko ndugu wa kawaida kwa lugha nyingine unapoacha mumeo aende au mkeo
aende zake yaani mnapoachana unaacha uchi wako uende zake, mwili wako uende
zake, mifupa yako iende zake, na mwili wako uende zake, na kuanza kutumiwa na
watu wengine, Mungu alikusudia Ndoa ibebe huduma ya kuongezeka duniani na
kuitawala dunia chini ya mamlaka ya uungu kwa kumtii, kwa kulitambua kusudi
hili kila ndoa iliyo sahihi iliyo katika mapenzi na mpango wa Mungu itaanza
kupigwa vita kali na ibilisi kwa sababu Shetani anajua wanando wasichokijua kwa
hiyo anawataka wasumbuke wapigane wagombane wafarakane waachane watendane mambo
ya hiyana wasemane vibaya wanyimane unyumba wasimtii Mungu atawasumbua mpaka
wakimbie na atawapa nafuu wanapokuwa katika ndoa ya pili isiyokuwa mapenzi ya
Mungu
Shetani atafanya hivi kwa sababu yupo na yuko tayari kupingana na Muumba
wake, atawadanganya wanadamu atawavuruga ili wamuasi Mungu wasitii neno lake
akitumia hila na ujanja mwingi sana hatimaye aweze kuharibu na atakupa amani
bandia kwa sababu anajua umeshaasi na kifo kinakuhusu yaani utakwenda katika
ziwa la moto wa milele kwa sababu sasa unazini milele wewe ni mali yake hawezi
kukuvuruga tena amefanikiwa kukupata na ndio maana utaona wale walioachana na
wake zao na waume zao wa awali unaweza kukuta sasa wanaamani ya kutosha huko UZINZINI kwa mtu asiye Mfupa wake wala
nyama yake kwa sababu amekuwa mtumwa wa dhambi na chombo cha ibilisi hata kama
mambo yanakwenda “smoothly” yaani shwari usifikiri wewe ni mjanja kwamba
umeshinda vita hapana umeshindwa vita wewe ni mali ya ibilisi hii ndio mbinu
yake tangu awali ona Mwanzo 3:1 anasifiwa kwa uhodari wake ujanja na
udanganyifu au werevu Mwanzo 3;1 “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu
aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema
Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?” neno mwerevu hapo
katika kiingereza linatumika neno “crafty”
ambalo maana yake ni Clever at achieving
one’s aims by indirect or deceitful methods Yaani mwerevu ni mwenye ujanja wa kufikia
malengo yake kwa kutumia njia isiyo ya wazi moja kwa moja au kwa kutumia njia
za udanganyifu kwa kutumia hila hizo sasa Shetani alifanikiwa kumdanganya Eva
na kisha kummalizia Adam na kuwafanya waasi na kwa njia hii kufanikiwa kuleta
mauti duniani na uharibifu mkubwa na kupitia wao wanadamu wote wamekuwa
wavunjifu wa sheria ya Mungu namaanisha neno lake kama ilivyokuwa kwa Adamu Hosea 6;7 “Lakini
wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana.”
Ona pia Warumi 5:12-21 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni,
na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote
wamefanya dhambi; maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini
dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; walakini mauti ilitawala tangu Adamu
mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la
Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. Lakini karama ile haikuwa kama lile
kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana
neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo
kimezidi kwa ajili ya wale wengi. Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya
dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja
ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta
kuhesabiwa haki. Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa
sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa
cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. Basi tena, kama
kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki
watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.
Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika
hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa
katika hali ya wenye haki. Lakini sheria
iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa
nyingi zaidi; ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo
hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana
wetu.” Unaona sasa hasara kubwa sana imaupata ulimwengu mzima
kutokana na kazi ya ibilisi kwa Adamu na Eva na nikwambie kuwa hasara kubwa
inaupata ulimwengu kupitia wewe na mimi kwa kuasi kwetu na kuvunja amri na
maagano na Mungu wetu, ndoa sasa haiwezi kuwa kamilifu duniani na ikiwa ni ya
watu wa Mungu inakuwa na vita kubwa sana na wapiganaji wakiwa hawaelewi
zitavunjika sana na watapewa ndoa ambazo zina amani ya muda mfupi lakini
zinawapeleka Motoni kimya kimya vita ilitangazwa kati ya shetani na uzao wa
mwanamke kwa mtazamo mpana uzao wa
mwanamke ni Yesu Kristo lakini kwa mtazamo rahisi sisi wanadamu wote ni uza wa
mwanamke kwa hiyo mafarakano katika ndoa ni vita ileile alioianza shtani katika
bustani ya Edeni, kwa hiyo kama vile mtu akiokoka tunamfundisha kuwa imetupasa
kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi yaani vita nyingi ni
muhimu vile vile wana ndoa wakaelewa kuwa pamoja na sarakasi zote
mtakazofanikiwa au mtakazojifunza iwe uwazi katika maswala ya fedha, mahusiano,
ndugu, staili, kujituma, vyakula, majukumu ya mke na mume, malezi na kuchekeana
na kadhalika lazima ujue shetani na mapepo yako kazini kuhakikisha kuwa
yanapambana na ndoa yako mpaka mwisho wa dahari kwa hiyo 1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa
kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta
mtu ammeze.“ shetani anazunguka zunguka popote palipo na kusudi la
Mungu ili awaharibu wana ndoa.
Ndoa katika mpango wa Ibilisi
Unapoyachunguza maandiko utaweza kuona sasa Shetani kama mpinzani wa
Mpango wa Mungu naye ana mipango yake inayolenga kuleta uharibifu katika ndoa,
Ni muhimu kukumbuka sasa wakati dhambi inaingia ulimwenguni kupitia kazi za shetani
taasisi ya kwanza kushambuliwa na vita ya ibilisi ilikuwa ni ndoa kwa haraka
sana tunaona sasa katika kitabu cha Mwanzo wanadamu wakiondoka katika mapenzi
ya Mungu kuhusu ndoa na kujiingiza katika mapenzi ya ibilisi na matakwa yao au
tamaa zao. Hapa ziko aina nyingi za
uharibifu wa ndoa ambao maandiko yanaonyesha kuwa shetani aliufanya kwa
ulimwengu hatua kwa hatua na kuwapeleka wanadamu kwenye uharibifu mkubwa sana
wa ndoa iliyokusudiwa na Mungu, Dalili zifuatazo ni Ishara ya kazi za shetani
kutokomeza mapenzi ya Mungu katika ndoa.
1.
Ndoa ya mke zaidi ya mmoja.
Moja ya dalili kubwa kabisa ya matokeo ya
dhambi ilikuwa ni ndoa ya wake wengi ona katika Mwanzo 4:19 “Lameki akajitwalia wake
wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.” Wakati huu kutoka katika ndoa ya mke mmoja ambaye
ni mfupa katika mfupa na nyama katika nyama kuelekea kwenye wanadamu kutekeleza
tamaa zao kuoa wake wengi ilikuwa ni sihara ya uharibifu wa uadilifu katika
ndoa, ndoa hizi zimeonyesha na kuashiria kutokuwepo kwa haki, kuwepo kwa
mafarakano, visa na mikasa katika biblia tumeona kuwa hata pale ndugu wa
familia moja walipoolewa na mtu mmoja kama Leah na Raheli bado mapungufu
makubwa yaliashiria kuwa ndoa hizi hazikuwa mpango wa Mungu, sio hivyo tu
wanadamu waliondoka katika ndoa ya mke mmoja kuelekea wake wengi, shetani
aliendelea kuwatoa wanadamu kutoka hatua ya kuoa wanawake kwa kujitakia bila
kufuata utaratibu.
2.
Ndoa za watu wasiofuata utaratibu.
Ukiyachunguza maandiko hapo katika Mwanzo 4:19 kuna neno KUJITWALIA neno hili
laonyesha wazi kuwa Lameki alikuwa mtu wa kwanza wa uzao ule wa Kaini ambao
ulijitenga na uso wa Mungu na kwa matakwa yake mwenyewe alijitwalia wake zaidi
ya mmoja tofauti na mpango wa kwanza wa Mungu ambao ulikuwa mke mmoja na mume
mmoja Mwanzo 2:24 “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye
ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.” Tabia hii ya lameki
baadaye ilienea hata miongoni mwa uzao wa watu waliokuwa wanamcha Mungu na
hivyo watu walianza kujiolea bila kufuata utaratibu ona Mwanzo 6:1-2 “Ikawa wanadamu walipoanza
kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona
hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote
waliowachagua.” Unaweza kuna maana yake sasa watu waliingia katika
kujitwalia wake wowote waliowachagua neno kujitwalia maana yake ni bila kufuata
utaratibu, uchafu wa tendo la ndoa na kutokuheshimiwa kwake na watu kujifanyia
vyovyote watakavyo bila kufuata utaratibu ulikuwa ni mpango wa ibilisi kuvuruga
mpango wa Mungu kadiri dunia inavyoharibika leo, hizi vurugu za shetani
zitaonekana ni kitu cha kawaida katika jamii, watu hawatafuata utaratibu, kwa
nini Mungu anataka utaratibu ufuatwe? Tusipofuata mpango wake itafikia hatua
watu watazaa watoto wakiwa hawajui baba wa watoto hao ni nani, wanaume
watakanusha watoto kwa nsababu hawana uhakika kuwa mimba hiyo ni yake au ya
mwanaume mwingine ni jambo la kusikitisha Mungu alihukumu kizazi hiki cha watu
wasiofuata utaratibu
3.
Ndoa ya watu wa jinsia moja.
Baada ya ndoa za watu wasiofuata utaratibu
biblia inatuonyesha uharibifu mwingine huu ni wa ndoa za jinsia moja yaani wanaume kwa wanaume na au wanawake kwa
wanawake mifano ikiwa ni miji ya Sodmoma
na Gomora ona Mwanzo 19: 1-25 “Basi,
wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa
Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. Akasema,
Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale,
mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema,
Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. Akawasihi sana, nao wakaja,
wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa
nao wakala. Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka
nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote. Wakamwita Lutu,
wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate
kuwajua. Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake. Akasema, Basi,
nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. Tazama, ninao binti wawili ambao
hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema
machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari
yangu. Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu
kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe
vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje
mlango. Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao
nyumbani, wakaufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa
upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango. Basi wale watu
wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo
wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; maana tutapaharibu sisi
mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA; naye BWANA
ametupeleka tupaharibu. Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti
zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu
mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze. Hata alfajiri ndipo
malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili
waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. Akakawia-kawia; nao wale watu
wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi
BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. Ikawa walipomtoa nje,
mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo
bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo, bwana
wangu! Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema
zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani
nisipatwe na yale mabaya, nikafa. Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni
mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi. Akamwambia,
Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo
uliounena. Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata
uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari. Jua lilikuwa
limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. Ndipo BWANA akanyesha juu ya
Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa BWANA. Akaangusha
miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea
katika nchi ile.” Ndoa zinapofikia kuwa ni za jinsia moja hapo ndio
huwa ni kilele cha juu kabisa cha uharibifu wa ndoa katika mipango ya shetani,
Shetani alifanikiwa kuharibu Ndoa kwa kiwango hiki Mungu alitaka Ibrahimu
alishuhudie tukio hili ili iwe fundisho kwa wana wa Israel na wale wote
wanaomuamini Mungu wa Ibrahimu kuwa wasifanye mambo kwa mfano wa watu wa
Sodoma.
4.
Ndoa ya Ndugu wa damu au ndugu wa karibu
sana.
Muda mfupi sana mara baada ya tukio hili la
kuangamizwa kwa miji nya Sodoma na Gomora
Biblia inatupa kisa kingine tena namna na jinsi shetani alivyoendelea na jitihada zake za kuhakikisha kuwa kila
aina ya uchafu na mambo yanayovuruga na kuleta uharibifu katika ndoa yanastawi sasa hata tunaona Lutu
na binti zake wakilala na kuzaa hii ni aina nyingine ya mipango ya ibilisi
katika kuchafua na kuharibu ndoa angalia sasa Mwanzo 19:30-38 “Lutu akapanda kutoka Soari
akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa
katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili. Yule mkubwa
akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi
atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. Haya, na tumnyweshe baba yetu
mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. Wakamnywesha baba yao
mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari
alipolala wala alipoondoka. Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo,
Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie
ukalale naye. Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo
akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Basi hao binti
wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Yule mkubwa akazaa mwana,
akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo. Na yule mdogo
naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata
leo.” Hili lilikuwa ni tukio la kushangaza sana namna na jinsi
shetani alivyoweza kuharibu Familia hii ambao walikuwa wameokolewa kutoka
Sodoma sasa wanaingia katika uchafu huu, dhambi ya aina kama hii inaonekana
kufanyika pia katika kanisa la Koritho wakati wa kanisa la Kwanza 1Wakoritho 5:1-2 “Yakini
habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika
Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika,
ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.” Unaweza
kuona kuwa tabia za uchafu wa aina hii unaweza kufanywa hata na watu walioko
kanisani kama hawatasimama na kushindana na ibilisi katika kupingana na
uharibifu anaokusudia kuufanya katika ndoa ni kwaajili ya haya Musa alitangaza
laana kubwa sana kwa watu wanaoweza au kuthubutu kutaka kufanya mapenzi ngono
au tendo la ndoa na jamii ya watu waliokaribu nao na ambao ni ndugu zao ona Mambo ya walawi 18:1-24 “BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie,
Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri
mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka;
wala msiende katika amri zao hao. Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika
amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Kwa ajili
ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi
kwa hizo; mimi ndimi BWANA. Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe
aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. Utupu wa
baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue
utupu wake. Utupu wa mke wa baba
yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. Utupu wa umbu lako, binti ya baba
yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba
alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa
binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe.
Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako,
usifunue utupu wake. Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni
jamaa aliye karibu. Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa
ya mama yako ya karibu.Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe
huyo; yeye ni shangazi lako. Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa
mwanao; usifunue utupu wake huyo. Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni
utupu wa nduguyo. Usifunue utupu wa
mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake,
ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. Wala usitwae
mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili
atakapokuwa yu hai. Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa
kutengwa kwa ajili ya unajisi wake. Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi
naye. Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapitisha kwa Moleki, wala
usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA. Usilale na mwanamume mfano wa
kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia
unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.
Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa
nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;” Mungu
aliweka sheria hizi zote kwa kusudi la kulinda uadilifu na kuweka utaratibu
miongoni mwa watu wake kwa sababu mataifa na dini zile za kanaani zilifanya
haya hawakuishi kwa utaratibu wa kimungu bali wa kishetani na Mungu akliwataka
watu wake kutunza uadilifu, Hata hivyo sheatani aliendelea na vita byake dhidi
ya ndoa hata kufikia utaratibu wa ndoa kuwa utaratibu wa mikataba yaani ndoa
zenye talaka, Mpango wa talaka ni ishara nyingine ya kuharibiwa kiuadilifu kwa
ndoa je inawezekanaje mtu ambaye ni mfupa wako na nyama yako sasa ikafikia
ngazi ya kuachana kwa karatasi na wino?
5.
Ndoa ya mikataba kupeana talaka.
Talaka haina tofauti na ndoa za mikataba tu,
watu wanaingia makubaliano wanaishi kwa muda flani halafu wanaachana huu
haukuwa mpango wa Mungu, Kisheria Musa aliruhusu hati ya talaka katika torati,
hii ni kwaajili ya maswala ya kimahakama au kimaamuzi kwa vile Musa pia alikuwa
mwamuzi wa Israel Judge, Lakini katika uadilifu na mpango wa Mungu, Mfupa wako
na Nyama yako haviwezi kutenganishwa kamwe, watu ambao wamekuwa mwili mmoja
wanatenganishwaje ? lakini kutokana na uharibifu wa kimaadili hati ya talaka ilikubalika
ona maandiko Kumbukumbu 24:1-4 “Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali
machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha,
akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake. Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana
ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na
kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba
yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; yule wa kwanza
aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni
machukizo mbele za Bwana; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo Bwana, Mungu
wako, iwe urithi.” Yesu
Kristo nabii mkuu au mkuu wa manabii au mwenye kutuma manabii ambaye manabii
wote walizungumza habari zake yeye ndio kiongozi mkuu wa wokobvu wetu alipokuja
Duniani katika mafundisho yake hakukubaliana na swala zima la hati ya talaka,
kwani hili halikuwa msingi wa mwanzo wa mpango wa Mungu kupeana talaka ni
kutoka nje ya mapenzi ya Mungu Mungu alonyesha wazi kuchukizwa na tabia ya
kuachana na hata kunyimana unyumba ambako kuliitwa kutendana mambo ya hiyana
ona Malaki
2:14-16 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu
gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako,
uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna
mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu;
mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi
nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake
kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu,
msije mkatenda kwa hiana.” Ni wazi kuwa Mungu anachukia kuachana
Yesu alionyesha wazi kuwa watu waadilifu na wale wanaomfuata yeye wanapaswa
kukubali kuwa kutoa talaka ni ngazi ya juu kabisa ya ugumu wa moyo uliokosa
msamaha mapenzi ya Mungu kamili kwetu ni kuwa ndoa zidumu mpaka kifo
kiitenganishe ona Mathayo 19:3-10 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia,
Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia,
Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata
wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu,
mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa
hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia,
Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu;
lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha
mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye
amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi
wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.” Kutokana na kifungu hiki ndio maana utasikia usemi
kama ule Ndoa ni pingu za maisha, au utasikiwa wamefunga pingu za maisha usemi
huu una maana gani? Wanafunzi wa Yesu (Mitume) walimuelewa
sana Yesu alipozungumzia Maswala ya ndoa hasa pale alipokuwa akijibu
maswali ya mafarisayo kuhusu ndoa, Mafarisayo walimuuuliza Yesu kwa kumjaribu
kama Ni halali mtu kumuacha mkewe kwa kila Sababu,Majibu ya Yesu yalionyesha kuwa
hakuna sababu ya mtu kumuacha mkewe hata
kama mmojawapo wa wanandoa amefanya zinaa! Wanafunzi kwa kulielewa hili
walisema mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivi haifai kuoa.
Najua
utakuwa umeshitushwa sana na Mtazamo huu hapo juu lakini nataka nikupeleke
katika msingi wa mafundisho ya Kristo kuhusu ndoa na Kuachana, Ni muhimu
ikaeleweka wazi kuwa wakati mafarisayo wakimuuliza Yesu maneno hayo walikuwa
tayari wameathiriwa na shule kuu Mbili za marabi maarufu waliofundisha
theolojia za kiyahudi Rabi wa kwanza aliitwa Rabi Shimney huyu alikuwa na msimamo mkali alipinga Kuachana akisimamia
vilivyo mafundisho ya Musa na rabi wa pili aliitwa Rabi Hilel huyu alikuwa na mrengo wa kushoto na msimamo wa wastani yeye
alikazia kuwa waweza kumuacha mkeo kwa sababu zozote na ukaoa mwingine
akisimamia Sheria ya Musa, Kimsingi Mafarisayo wengi walipendezwa na msimamo wa
Hilel katika maswala ya ndoa na
kwakuwa walimuona Yesu kuwa Kama rabi mwenye msimamo wa wastani walitaka kujua kuwa angelielemea katika Eneo
gani kati ya haya Mawili; katika namna
ya kushangaza sana Yesu alionekana kuwa na Msimamo mkali katika Eneo la ndoa
kuliko Hilel, Shimney na Hata Musa Mwenyewe Yeye alionyesha kuwa hakuna sababu
yoyote ambayo inakubalika katika Mungu kuwa Inaruhusu Mtu kumuacha mkewe au
kuachana na ya kuwa hata Musa aliruhusu talaka kama matokeo ya ugumu wa mioyo
waliyokuwa nayo wayahudi kwa vyovyote ugumu huu ni ile hali ya kutokusamehe.
Watu
wengi sana leo wamewaacha wake zao au hata waume zao kwa sababu ya ugumu wa
mioyo yao ugumu wa kutokusamehe wamekuwa wakiwaona kuwa wenye dhambi sana ni
wangapi ambao wamefanyiana mambo ya hiyana lakini leo wako pamoja inashangaza
leo hii kuona hata wapendwa (watu waliookoka) wakiingia katika hali hizi za kuvunja ndoa na kushindwa na
watu wasio mjua Mungu na huku wakiungwa mkono na viongozi wao wa dini kwa nini
watu waachane kama Yesu yupo? Yeye alikuwa na msimamo thabiti wa kutokupenda
watu waachane je leo tunamfuata Yesu au tunaona kuwa alipitwa na wakati maana
wakati wake hakukuwa na Magonjwa na changamoto kama hizi zilizoko leo? Kuachana
ni kumvunjia Mungu Heshima na kudhalilisha mafundisho mazuri ya Kristo na
kuvunja kanuni zake za uumbaji na utaratibu wake tangu mwanzo acha mawazo ya
kuachana katika jina la Yesu, tafuta kutengeneza nyumba yako na sio kuibomoa
Yesu alionyesha wazi kuwa hakuna sababu za kuachana. Hii ina maana gani? Hakuna
sababu ya Kuachana. Kifungu kile tulichosoma katika Mathayo 19;3-10.
Kimsingi katika mistari hii Yesu alifafanua kuwa hakuna sababu ya Kuachana
isipokuwa kifo tu ni muhimu kufahamu msingi wa Mungu kuwa Yeye
anachukizwa na kuachana tangu zamani Kama tulivyoona pia katika kitabu cha
nabii malaki hapo juu Malaki 2;16.
Hata hivyo kuna utata wa kitheolojia kuhusu Mathayo 19;3-10 kwamba Yesu alisema Mtu anaweza kumuacha mkewe kwa
sababu ya Uasherati ni muhimu kuchambua Maana halisi ya Mistari hii ili kupata
maana halisi ya kile anachokisema Bwana Yesu, Kwanza ni muhimu kwetu
kuchanganua Maneno haya Mawili Uzinzi na Uasherati huku ukitilia maanani kuwa
Yesu alitumia neno uasherati.
Tofauti ya Uzinzi na Uasherati;
Katika
tafasiri za kawaida za Kiswahili uasherati ni tendo la kujamiiana linalofanyika
nje ya watu waliooana au tendo la ngono linalofanywa na watu au mtu ambaye
hajaoa au kuolewa mtu wa jinsi hii anapofanya hayo huitwa Muasherati, Uzinzi ni
tendo la ndoa linalofanywa na wanandoa nje ya ndoa.
Kwa
msingi huu Yesu alipotumia neno Uasherati alimaanisha watu ambao hawajaoana
bado isipokuwa wana uhusiano wa kutaka kuoana yaani ni wachumba, hii ni kwa
sababu katika jamii ya Kiyahudi hawakuwa na neno mchumba kama tulilonalo sisi, Hivyo
Binti bikira ambaye anatarajiwa kuolewa au amelipiwa mahari huyu aliitwa mke na
huyu angeweza kuachwa kama angebainika kuwa amefanya uasherati kabla ya ndoa
basi uhusiano huu ungevunjika, Mfano mzuri ni ule wa Yusuphu na Mariam walikuwa
ni Mtu na mchumba wake ambaye alikuwa amemposa, Hivyo kwa tendo la Yusuphu
kumuona Mariam akiwa na Mimba alikusudia kumuacha kwa siri Hata hivyo katika
Kumuasa asimuache Malaika na Biblia
inatumia Neno “Usimuache Mkeo” Unaona! Mathayo 1;18-25 “Kuzaliwa
kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na
Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho
Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake
kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.
Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika
ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana
mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita
jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Hayo
yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii
akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina
lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana
alivyomwagiza; akamchukua mkewe; asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita
jina lake YESU.” kwa Msingi huu basi Yesu alimaanisha kuwa anayeweza
kuachika ni Mchumba na si mke, Yesu anasemaje kwa Wanandoa? Kwa wanandoa endapo
wataachana kwa sababu ya zinaa wote aliyeacha na aliyeachwa watakaa bila kuoa
au kuolewa tena, na endapo watafanya hivyo yaani mume ataoa na mke ataolewa
tena “Remarried” watakuwa wanazini milele yaani wanaishi katika maisha ya
dhambi. Yesu anatoa ushauri gani? Wanaweza kumaliza tofauti zao na kupatana
tena na kurudiana angalia 1Wakoritho 7;
10 “Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala
hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;” kwa nini kwa
sababu watu wanapooana wanakuwa mwili mmoja na kinachoweza kuwatenganisha ni
kifo tu kama vile ambavyo ndugu wanakuwa ndugu siku zote za maisha yao duniani
mpaka ndugu huyo anapofariki Dunia ona Warumi 7;2-3 “
Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati
anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume. Basi
wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe
akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa
na mume mwingine.” Unaona kwa hivyo ni kifo tu ndicho
kinachoruhusiwa kutoa upenyo wa mtu kuoa au kuolewa tena! Na hakuna kosa lolote linalohalalisha ndoa
kuvunjwa na kama ikitokea wanandoa wakaachana wanapaswa kukaa hivyo hivyo
maisha yao yote au kurudiana kinyuime cha hapo wanafanya uzinzi Ni kwa sababu hii wanafunzi wa Yesu walisema
Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivi haifai kuoa, Kimsingi Yesu alionyesha wazi
kuwa wale walioachana wakati wa Musa waliachana au Musa aliruhusu wafanye hivyo
kwa sababu ya ugumu wa mioyo yaani hali ya kutokutaka kusameheana, Hakuna dhambi
isiyosameheka hivyo kimsingi kama tunashindwa kusamehe ni Ngumu nasi kupokea
msamaha kutoka kwa Mungu. Aidha katika agano la kale wazinzi walipigwa kwa mawe
hata kufa na jambo hili lilimfanya mtu mwenye haki awe mume au mke aliyebaki
kuoa au kuolewa tena hivyo kanuni inabaki vilevile kuwa kifo tu ndicho kingetenganisha
wanandoa Adamu angeamua kumuacha Hawa ingekuwa sawa na kujiharibu mwenyewe je
mtu aweaza kujikata sehemu ya mwili wake na kujitupa? Kama watu wakioana
wanakua mwili mmoja unadhani kuna usalama watu wanapoachana rudi kwenye msingi
wa neno, sasa tunapoona watu wanaachana leo na wanaolewa tena tujue kuwa
shetani yuko kazini anafanikisha kazi yake ya kuharibu mpango wa Mungu kwa wanadamu
na wote waliotengana na kuamua kuolewa tena wameshindwa vita na kama wana amani
ni amani ya bandia, na kama wanamtumikia Mungu sijui ni kwa Biblia gani lakini
msimamo wa bwana Yesu uko wazi zaidi ndoa nyingi sana zimepigwa leo, na watu
wameoa tena na wengine ni wachungaji kama msimamo huu umekushinda ni vema
ukauza nyanya, kwa sababu kama ndoa imekushinda unapoteza sifa ya kusimamia
ndoa nyingi zilizoko kanisani, kama ndoa imekushinda huna sifa ya kuhubiri
msamaha, huna sifa ya kuhubiri uvumilivu, huna sifa ya kufungisha ndoa, huna
sifa ya kuwa kiongozi, maana umeshindwa hata kujisimamia mwenyewe!, huna sifa
ya kuwa kiongozi wa maombi na mapambano ya kiroho kwa sababu umeshindwa vita na
mapambano dhidi ya ndioa yako mwenyewe!
6.
Ndoa ya binadamu na mnyama.
Kama maswala ya uharibifu wa ndoa kwa talaka
na mikataba hautoshi shetani ameshambulia sana ndoa na kuifikisha katika hatua
ya wanadamu kutokutamani kuwa na binadamu wenzao sasa watu wanahangaika na
kuzini na wanyama, katika karne hizi maswala haya yamezidi watu wanafikia hatua
hata ya kufanya ngono na farasi, mbwa, nguruwe na kadhalika haya pia ni
machukizo na machafuko ambayo Mungu aliyakemea ona Kutoka 22:19 “Mtu awaye yote alalaye na
mnyama sharti atauawa.” Kwa nini haya yote yanatokea huu ndio mpango
wa ibilisi katika kutaka kuharibu kabisa mpango wa Mungu kuhusu Ndoa, Muda
usingeweza kutosha kuelezea kila kitu kibaya ambacho kinaashiria uharibifu
mkubwa wa ndoa kwa aina binadamu, lakini hili ndio kusudi kubwa la shetani
kuharibu na kushindana na kupambana na kupigana na ndoa kwa wanadamu wote, ndoa
hizi zote za aina hii ni mpango wa ibilisi katika kushambulia na kuharibu
kusudi kubwa la Mungu kutukuzwa kupitia uadilifu wa watu wake na ndoa zao.
7.
Ndoa ya watu wa Imani tofauti.
Mpango mwingine wa ibilisi katika kuharibu
kusudi la Mungu katika ndoa yeye pamoja na majeshi yake ya pepo katika
ulimwengu wa roho watataka watu waoane na watu wa imani tofauti kumbuka hapa
sio kabila bali imani tofauti, Mungu alipowakataza wayahudi kuolewa na au kuoa
mataifa wengine sababu kubwa haikuwa kabila zao bali imani zao, walikuwa
wanaabudu miungu mingine na hivyo mpango na makusudi ya Mungu yangeharibika kwa
shetani kulazimisha watu wa Mungu waolewe au waoe watu wasiokuwa na imani au
wasioamini katika Mungu wa Ibrahim na Isaka na Yakobo mtego mkubwa wa ibilisi kwa
watu wa mungu ni kuwa wao na watoto wao waabudu miungu mingine jambo ambalo ni
machukizo kwa Mungu Kumbukumbu 32:16 “Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa
machukizo”. Imani hizi ni
mbaya na zina ushetani mwingi na uovu mkubwa sana Zaburi 106:37 “Naam, walitoa wana wao na
binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani.” Mungu hataki kwa namna yoyote
watu wake kushirikiana na mashetani 1Wakoritho
10:20-21 “Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka
wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na
mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi
kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.” Mungu
alipowakataza wana wa Israel wasioane na watu wa mataifa yale yanayowazunguka
sababu kubwa ilikuwa ni kuzilinda imani zao, kuwalinda wasiingie kwenye wimbi
kubwa la kuabudu miungu na kushiriki ibada za kishetani, Mungu aliwaonya kuwa
ndoa ni moja ya kwa watu hao wa imani tofauti ni moja ya mtego wa ibilisi
atakaoutumia kuwaingiza katika ibada hizo na tabia mbaya isiyo ya kiadilifu na
itakayoharibu utukufu wa Mungu duniani Kutoka
34:11-16 “Liangalie neno hili ninalokuamuru leo;
tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi,
na Myebusi. Ujihadhari nafsi yako, usije
ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako.
Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata
maashera yao. Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina
lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu. Usije ukafanya agano na wenyeji wa
nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu
yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake. Ukawaoza wana wako binti zao, nao
binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye
uzinzi na miungu yao.” Unaona
hakuna hekima unaweza kuitumia hapa kuwavuta wao kwa Mungu, wewe ndio
utakayevutwa kuelekea upande wao na kujikuta ukiingia katika mtego wa ibilisi
ni kwa kutumia ndoa shetani atajitahidi kuwanasa watu wa Mungu waingie katika
mtego wa ibilisi ndoa na watu wa imani tofauti nay a Mungu wa kweli iko mifano
kadhaa katika biblia ambapo muda usingeweza kutosha kuiona ya watu ambao walioa
wanawake wa aina hiyo na baadaye wakajikuta wanaabudu miungu moja ya mifano hii
ni Mfalme Sulemani aliyegeuzwa moyo na kumuacha Mungu wa baba yake kwa sababu
ya kuoa binti za wanawake wa falme za kipagani 1Wafalme 11:1-6 “Mfalme Sulemani akawapenda
wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa
Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa Bwana
aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika
wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa
kuwapenda. Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao
wakeze wakamgeuza moyo. Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake
wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu
kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. Kwa kuwa Sulemani
akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.
Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa
utimilifu, kama Daudi baba yake.” Wewe huwezi kudai kuwa una hekima
kama Suleimani lakini hata pamoja na kupewa hekima kubwa aligauzwa moyo na
kuabudu miungu kwa sababu ya mtego wa ndoa, wakristo hawana budi kuvumilia na
kusubiri kuolewa na mtu mcha Mungu wa jamii ya Kikristo, usikubali kuingia
katika mtego wa ibilisi na kusukumwa kuoa au kuolewa na mtu wa imani tofauti na
yako, unaweza kudhani kuwa mtazamo huu ni wa gano la kale tu hapana katika
agano jipya pia Paulo mtume alikazia vikali kutokufungiwa nira na watu
wasioamini ona 2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo
sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika
gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?
Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano
gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye
hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea,
nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao,
asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba
kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,” andiko
hili linakataza sio tu kuoana lakini hata kushirikiana katika maagano au vutu
vyenye kutufunga pamoja na wasioamini, kwa kuwa tunazungumzia ndoa hapa nataka
kukazia kuwa Mungu hajaruhusu ujiolee tu mtu wa imani tofauti na ya Mungu wa kweli n ukioana na mtu awaye
yote ambaye yuko nje ya ushirika na Yesu umeingia katika mtego wa ibilisi
katika ndoa yako wewe na watoto wako, unapooa mtu wa imani tofauti na yako
maana yake unaunganisha mwili wako na mtu anayetokea katika chanzo kingine cha
kiroho jambo hili litazuia kuendelea kuenezwa kwa utukufu wa Mungu duniani Kumbukumbu 22:10 . “Usilime kwa ng'ombe na punda wakikokota jembe pamoja”
mwenye masikio ya kusikia na asikie
8.
Ndoa ya watu waovu.
Ni muhimu kufahamu kuwa shetani akitaka kuleta uharibifu katika kanisa
hutumia ndoa mbovu ya watu waovu, kama katika kanisa kutakuwa na ndoa mbovu ni
rahisi kuwa na kanisa bovu au kuwa na viongozi waovu, Tangu kanisa lilipoanza
kwa nguvu siku ya Pentecost tunaona Shetani hajawahi kutajwa tena mpaka katika Matendo 5:1-11 1. “Lakini
mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa
siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja
akaliweka miguuni pa mitume. Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza
moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani
ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa
mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo
wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo
mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu
nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. Vijana wakaondoka, wakamtia
katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe
akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani
hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo.Petro akamwambia, Imekuwaje hata
mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo
mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake akafa;
wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na
mumewe. Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya.”
Hapa shetani anatajwa kwa mara ya kwanza katika kanisa la kwanza akiwa
amewatumia wana ndoa Anania na Safira wao ni wana ndoa walioshindwa kumpinga
shetani ili kusudi wasitumbukie katika mtego wa dhambi, kutokana na tabia yao
na mwenendo wao waliliathiri kanisa kwa kumpa ibilisi nafasi na wakapatana
pamoja ili walidanganye kanisa hii inatufundisha nini kwamba Shetani anaweza
kuzitumia ndoa kupinga mpango wa injili, kuna wanadoa wengi wanaotaka kujitoa
kwaajili ya kanisa lakini shetani anaweza kuwazuia wenzi wao wasitoe, kuna
wahubiri wengi wazuri wameanguka na kushindwa kuwa Baraka kwa kanisa kwa sababu
ya ndoa mbovu, unasikia muhubiri mkubwa sana anayetumiwa na Mungu kwa mamlaka
ya ajabu sana, mkewe anavunja maagizo ya neno la Mungu la kutokunyimana agizi
ambalio liko wazi msinyimane wao wanawabania waume zao na kuharibu huduma zao
katika karne hii haya tumeyaona sana Petro aliona ni afadhali hawa wafe lakini
Kanisa liendelee, watu wengi kwaajili ya ubinafsi, choyo, ujinga na kutokuelewa
hawafikiri kuwa wao ni wa muhimu sana katika huduma za kanisa kupitia ndoa zao,
kupitia uovu wa wana ndoa kazi ya Mungu inakataliwa, mabinti wengi na wamama
wamekwaza katika huduma zao kwaajili ya mama wachungaji wenye wivu mkali wa
kimapenzi, eti mumewe anapofanya huduma yeye anawaza kuwa mumewe ataibiwa,
mabinti wanapotaka kumtumikia Mungu wao wanawaza ujinga, shetani amepata nafasi
sana ya kulishambulia kanisa kupitia ndoa za watu waovu. Watu wengi wameingia
katika mtego wa ibilisi kupitia wake zao akiwemo Adam kwa msingi huo ni muhimu
kwa kila mwanandoa kujua na kutambua kuwa usafi wake wa moyo una umuhimu mkubwa
kwa kanisa na kuwa tabia zao zina umuhimu mkubwa kwa kanisa fikiria kama
Mariamu na yusufu wangekuwa hawana msimamo katika ndoa yao Je wangeweza kuwa
Baraka kwa ulimwengu kwa kumlea Masihi!
9.
Kukataza watu wasioe wala kuolewa.
Paulo alimuonya Mwangalizi askofu Timotheo
kuwa awe makini kwa sababu wengine watamfuata shetani na kufuata roho
zidanganyazo nyakati za mwisho kutakuwako na aina nyingi sana za mafundisho na
ni mafundisho ya mashetani na yatakuwa na nguvu sana katika kanisa na hivyo
watu wa Mungu wanapaswa kuwa makini katika maonyo hayo yote utaweza kuona
shetani hataacha kutumia ndoa angalia katika 1Timotheo 4:1-3 “Basi
Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani,
wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu
wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na
kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani
na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.” Unaona hapa shetani
analishambulia kanisa kwa njia muhimu, halishambulii kanisa kwa kukanusha kuwa
hakuna utatu, au Kuwa Yesu sio Mungu hapa shetani anaingiza kwa werevu
mafundisho yenye kukataza watu kuoa au kuolewa, katika nyakati hizi kulikuwa na
mafundisho kuwa kutokuoa ndio kujitoa kwa viwango vya juu sana katika maswala
ya wokovu na huko Coritho walifundisha wazi kuwa unaweza kuoa lakini tendo la
ndoa ni najisi na hivyo kujiepusha nalo ni kwa muhimu sana katika kujitoa kwako
kwa Mungu kiasi ambacho wakristo walinyimana sikiliza nikuambie ni wazi kabisa haya ni mashambulizi ya nshetani
na ni muhimu ikaeleweka wazi kuwa kukataza Wakristo kuoa au kuolewa ni sawa na
kukataza injili isihubiriwe.
10.
Ndoa ya watu Kunyimana unyumba
Ndoa inaimarika kwa kushirikiana kwenye
tendo la ndoa la mara kwa mara au ikiwezekana kila siku na kila saa nafasi
ipatikanapo na kama afya zinaruhusu,
1Wakoritho 7:2-5 “Lakini kwa sababu ya zinaa kila
mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake
mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki
yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu
ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate
faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na
kiasi kwenu.”
Kushirikiana katika tendo la Ndoa kwa wana
ndoa mara kwa mara ni jambo zuri na linakubalika sana mbele za Mungu, katika
kanisa la Koritho kulikuwa na tatizo la watu kufikiri kuwa huenda tendo hili ni
dhambi, kwa hiyo watu walikosa kiasi na kujitoa kwa Mungu katika kufunga na
kuomba wakishindwa kuwa na kiasi katika kukumbuka ndoa zao, Paulo mtume
aliwakumbusha wajibu wa kila mwana ndoa kuhakikisha kuwa wanashirikiana tendo
la ndoa 1Wathesalonike 4:3 “Maana haya ndiyo
mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;” jambo au
wazo la kufikiri kuwa tendo la ndoa ni dhambi lingeharibu hali ya utakatifu wao
lakini tendo hili linapofanyika ndio linaimarisha utakatifu miongoni mwa
wanandoa, swala la kujinyima tendo la ndoa kwa kufikiri kuwa ndio kujitoa kwa
Mungu yalikuwa ni mafundisho potofu kwa kanisa la Korintho, Paulo mtume
alieleza kwa uwazi kwamba mke na mume wanapaswa kushirikiana tendo la ndoa bila
vikwazo kwa hiyo aliwaamuru wasinyimane (Mst5) Kumpa mwenzi wako tendo la ndoa
ilikuwa ni moja ya wajibu ambao uliamuriwa katika Torati Kutoka 21:10 “Kwamba ajitwalia mke
mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.”
Kumpa mkeo ngono au mumeo ngono ni wajibu kwa kuwa ni haki ya mwenzi wako
iwapo mtu hatatoa haki hiyo kimaandiko Mungu atakuja kumuhukumu kwa kosa la
kutokutoa haki na kutokumuogopa yeye angalia Malaki 3:5 “Nami nitawakaribieni ili
kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na
juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya
mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake,
wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.” Lugha aliyoitumia
Paulo mtume kuhusu kupena haki inafanana na lugha inayotumika kudhulumu au
kutoa haki kwa mtu aliyeajiriwa na kutokumpa au kumpa haki yake au ujira wake au mshahara wake ona
katika Yakobo 5:4 “Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu,
ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni
mwa Bwana wa majeshi.” Kwa msingi huo kitendo cha kumnyima mwezi
wako kinafanana na kuzuia haki ya mtu au mshahara wa mtu au kumdhulumu kwa hiyo
kilio cha mwezi wako kuhusu tendo la ndoa au kunyimwa hali yake kitaingia masikioni
mwa Bwana na Bwana atahukumu! Sasa Paulo mtume sio tu anaonya na kuwataka
wanandoa kupeana haki lakini vilevile anaonya kuwa kunyimana huko kutampa
ibilisi nafasi yaani watu wanaonyimana tendo la ndoa au kukosa kiasi kwa
visingizio vya kujitoa kwa Mungu na kumnyima mwezi wako tendo la ndoa ni
kumkaribisha shetani kuingilia ndoa yenu, shetani akifanikiwa kuwaangusha au
kumuangusha mwanandoa mmoja mnakuwa mmewapa nafasi maadui wa Yesu Kristo
kukufuru 2Samuel 12:14a “Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za Bwana
nafasi kubwa ya kukufuru,” kwa hiyo jina la Bwana litadhaulika watu
wanaofundishwa na kuhubiriwa injili watakuwa na moyo mgumu na unasababisha
kikwazo kwa injili ya Mungu kusambaa ulimwenguni kote, njia sahihi ya kutatua
tatizo hili ni kuhakikisha kuwa wana ndoa wanapeana tendao la ndoa kila wakati,
na wote mnalifurahia tendo hilo, kinyume cha hayo mnakaribisha mashambulizi ya
shetani kwenye maisha yenu na huduma zenu. Baraka kubwa na mafanikio makubwa ya
mwanadamu yamefungwa katika ndoa kama wanadamu wataharibu ndoa wataondoa baraka
zote ambazo Mungu amezikusudia acha kuzuia baraka zako, acha kuharibu mpango na
kusudi la Mungu kwa mwenzi wako kwa kumnyima au kwa kunyimana kumbuka shetani
yuko kazini kukuharibia ndoa yako na ndoa yako ikiharibika umeingia dosari.
Jedwali hapa chini linaonyesha ndoa katika
mpango wa Mungu na ndoa katika mpango wa ibilisi
NDOA KATIKA MPANGO WA
MUNGU
|
NDOA KATIKA MPANGO WA
IBILISI
|
Mwili mmoja
Iwe njema
Mke na mume
Mke mmoja
Enye utaratibu
Bila zinaa
Hakuna kuachana
Ya kudumu
Yenye amani na utulivu
Yenye utakatifu
Yenye kupeana
Imani moja
Binadamu kwa binadamu
Nnia sahihi
|
Mali ya kila mmoja
Watu wanyimane
Jinsia moja
Wake wengi
Isiyo ya utaratibu
Enye zinaa
Yenye talaka
Ya mikataba
Mafarakano na kero
Yenye uchafu
Yenye kunyimana
Imani ya mashetani
Binadamu na wanyama
Njia isiyosahihi
|
Jinsi ya kupambana na kuitetea ndoa yako
Sheatani pia ataishambulia ndoa ya Kikristo kwa mashambulizi ya aina
mbalimbali yakiwemo magonjwa na mateso
mengine yakiwa na uhusiano na uzazi au viungo vya uzazi moja kwa moja ili Ndoa
ya Wakristo iweze kuwa imara na yenye kusimama kama lilivyo kanisa wanandoa
wanapaswa kuvaa silaha zote za Mungu ili waweze kuzipinga hila za shetani
Waefeso 6:10-20 10. “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu
zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa
maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na
mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza
kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni,
hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa
miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya
imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa
Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika
Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu”
kitabu cha waefeso ndio kimezungumzia kwa undani zaidi mapambano ya vita
vilivyopo katika ya shetani na kanisa kuliko kitabu kingine chochote, ni kweli
tunafahamu kuwa shetani ameshindwa pale Msalabani, lakini ni muhimu kukumbuka
sehemu ya hukumu yake haijalkamilika mpaka mwisho wa dahari kwa msingi huo
akiwa bado ni mungu wa dunia hii yeye na majeshi yake anapambana na kanisa
lakini vilevile anapambana na wana ndoa kwa msingi huo basi ni muhimu kwa
wanandoa kusimama imara na kupambana kiume dhidi yake ili waweze kushinda kama
ningekuwa natumia English ningeweza kutumia neno “you
must be very aggressive” ndio maana biblia inasema tuwe Hodari hii ni lugha
ya kivita tuwe hodari katia uweza wa nguvu zake, wanandoa wana nguvu kubwa sana
ya kumsabaratisha shetani kama ndoa yao itasimama imara Kumbukumbu
la torati 32:230 “Mmoja angefukuzaje watu elfu,
Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana
asingaliwatoa? “ unaweza kuona pia katika Muhubiri 4:9-12 “9. “Afadhali kuwa wawili
kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka,
mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala
hana mwingine wa kumwinua! Tena, wawili
wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje
kuona moto? Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili
watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.” Biblia
inaonyesha kuwa wawili hii ni wale walioshikamana walio na umoja wana nguvu
kubwa sana wana uwezo mkubwa sana wa kusambaratisha adui katika ulimwengu wa
roho na ndio maana shetani hupigana na wana ndoa ili kuondoa umoja na
mshikamano na wakati mwingine ugomvi vita na mafarakano, kinyongo na
kutokusameheana ili yamkini hata wana ndoa wasiweze kuomba pamoja na kama wana ndoa wakifarakana kisha mmoja
aakaomba peke yake hawezi kufanikiwa na kupenya 1Petro 3:7 “Kadhalika ninyi waume, kaeni na
wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na
kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.”
Ili wanandoa waweze kuwa na ushindi dhidi ya vita kali dhidi ya Shetani
wanapaswa kuishi kwa amani wanapaswa kuitafuta sana amani ili kusudi maombi yao
yasizuiliwe, kumbuka tunapambana na shetani hivyo tunapaswa kuwa makini sana
tunapaswa kuvaa silaha zote za Mungu ili tuweze kuzipinga hila zake asili ya
vita yetu hii ni ya kiroho lakini matokeo yake ni ya kimwili, shetani atataka
kutushambulia na kutuvuruga akitaka kuhakikisha kuwa mke anakuwa kinyume na
mumewe na mume anakuwa kinyuma na mkewe au watoto kinyume na wazazi, aidha vita
hii itaathiri wote wanaowazunguka likiwemo kanisa.
Mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda!
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Mafundisho mazuri sana,ubarikiwe sana mtu wa Mungu.
JibuFutaNimeelewa sana
JibuFutaMungu akubariki sana.
JibuFuta