Mwanzo 31:24 “Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.”
Utangulizi:
Je umewahi kupitia mambo magumu katika
maisha yako mpaka unaamua kukimbia? Umewahi kupitia mitihani mizito mpaka
unaamua kufanya maamuzi magumu? Maisha
ya Yakobo yaani Israel duniani hayakuwa mepesi kama tunavyoweza kufikiri,
alipitia mambo magumu mno, alipitia maisha ya taabu na dhiki kuliko Ibrahimu na
Isaka baba zake ona
Mwanzo
47:7-9 “Yusufu akamleta Yakobo babaye ndani
akamweka mbele ya Farao Yakobo akambariki Farao. Farao akamwuliza Yakobo, Je! Siku za miaka ya
maisha yako ni ngapi? Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu
ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za
taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za
kusafiri kwao.”
Moja ya maeneo ambayo huenda Israel
aliyakumbuka katika taabu alizozipitia ni pamoja na maisha yake ya ujombani, alikokuwa akimtumikia Laban
Mjomba wake, Hatimaye Yakobo na wake zake na wanae waliamua kuondoka kwa mjomba
kwa kutoroka bila hata kuaga kwa kuhofia kuwa huenda Labani atamuonea tena
Yakobo kama alivyomuonea siku zote za maisha yake, Hata hivyo Labani aligundua
kutoroka kwa Yakobo na kuwa msafara wake ulikuwa ukielekea Gilead akamuwahi na
kumkuta baada ya wiki nzima
Mwanzo
31:21-23 “Basi akakimbia yeye na yote aliyokuwa
nayo; akaondoka akauvuka mto, akaelekeza uso wake kwenda mlima wa Gileadi. Hata
siku ya tatu Labani akaambiwa ya kwamba Yakobo amekimbia, akatwaa ndugu zake
pamoja naye, akamfuata mwendo wa siku saba. Akampata katika mlima wa Gileadi.”
Hatuwezi kujua kuwa Labani alikusudia
kumfanya nini Yakobo? Hatujui nini kilikuwa katika akili zake lakini bila shaka
alikuwa amenogowa na utumishi wa Yakobo, alitamani kuendelea kumfanya yakobo
kuwa mtumwa wake siku zote, hakufikiri wala kutamani kuona kuwa siku moja
Yakobo anakuwa huru, anamuabudu Mungu wa baba zake kwa uhuru, ana kuwa na
kabila zake mwenyewe, anajitawala na kutimiza hivyo kusudi la Mungu, labani
alikuwa ni muabudu miungu, hakuweza kujua kusudi la Mungu ndani ya Yakobo.
Lakini alikuwa na hisia zilizowazi kuwa mtu huyu anaye Mungu aliye hai, anajua
na kufahamu kuwa Yakobo alitajirika kwa jasho lake huku Mungu wa baba zake
akiwa ameweka mkono wake kumbariki mtu huyu aliyeonewa na kupangiwa maisha
tangu siku ya kwanza, Labani asingeweza kukubali hata kidogo kumuachia Yakobo
kama farao alivyokataa kuwaachia wana wa Israel Kule misri baadaye, Yako mambo
ambayo ulimwengu hauwezi kukubali kutuachia wala shetani hakubali kukuachia kwa
sababu uweza wa Mungu uko juu yako na adui zako wanafaidika na uwepo wako,
Africa wazungu hawawezi kukubali kukuachia ujitawale hawawezi kukuacha uchakate
kila ulicho nacho kwa sababu wanafaidika na utumwa wako, wakati mwingine ili
tuweze kuwa huru katika eneo Fulani ni mpaka Mungu aingilie kati, na Mungu
huingilia kati pale anapoona tu mechoshwa na hali hiyo, hata hivyo Labani
hangekubali na hivyo Mungu wa Israel aliingilia kati na kumuonya katika ndoto
kwamba Usimwambie Yakobo neno la heri
wala la Shari!
Kwa Lugha nyingine usiiingilie kati
kusudi la Mungu lililoko ndani yakem usimzuie, Yakobo ni lazima aishi kanaani,
ni lazima aende katika nchi ya ahahdi ndani yake kuna kusudi Yeye anajua na
Mungu anajua kwa hiyo umemtafuta umemuona lakini lazima umuache aende zake
usmwambie la heri wala la shari katika uamuzi wake huu unasikia labani? Labani
alikuwa amefikisha Hatua ambayo angeingia kwenye ugimzi na Mungu, alikuwa
akimuonea Yakobo mara kadhaa na inawezekana kabisa pia alitaka kumdhuru wakati
ulikuwa umefika sasa Yakobo lazima awe huru, na Labani achague kurejea katika
nchi yake ama akutane na mkono wa Mungu! Ona
Mwanzo
31:6-16 “Nanyi mmejua ya kwamba kwa nguvu zangu
zote nimemtumikia baba yenu. Na baba yenu amenidanganya, akabadili mshahara
wangu mara kumi; lakini Mungu hakumwacha kunidhuru. Aliposema, Walio na
madoadoa watakuwa mshahara wako, wanyama wote wakazaa madoadoa. Aliposema,
Walio na milia watakuwa mshahara wako, ndipo wanyama wote wakazaa wenye
milia. Hivi Mungu akamnyang'anya mali
yake baba yenu, na kunipa mimi. Ikawa, wakati wale wanyama walipochukua mimba,
naliinua macho yangu nikaona katika ndoto, na tazama, mabeberu waliowapanda hao
wanyama walikuwa na milia, na madoadoa, na marakaraka. Na malaika wa Mungu
akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Akasema, Inua, basi,
macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa,
na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani. Mimi ni Mungu wa
Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka
katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa. Raheli na Lea wakajibu,
wakamwambia, Je! Imetubakia sehemu au urithi katika nyumba ya baba yetu?
Hakutufanya kama wageni, maana ametuuza, naye amekula fedha zetu kabisa? Maana
mali yote ambayo Mungu amemnyang'anya baba yetu, mali hiyo ndiyo yetu na ya
wana wetu. Basi yo yote Mungu aliyokuambia, uyafanye.”
Unaona unaposoma kifungu
hicho unaweza kuona na kupata picha ya
kuwa maisha ya Yakobo, hayakuwa rahisi, kulikuwa na kila aina ya ukatili na uonevu kutoka ujombani, Labani alijaribu kwa kila namna kumfanya
yakobo awe mtumwa wake wa kudumu, mtumwa wa maisha yake yote, Mungu alikuwa ni shahidi
wa kile Labani alikuwa anamfanyia Yakobo, ni jambo la kushangaza kwamba mjomba
wako mwenyewe kaka wa mama yako anakuwa kikwazo cha kusudi la Mungu maishani
mwako sasa ilikuwa lazima Yakobo aende Nyumbani, aende alikozaliwa arudi
Betheli kwenye nyumba ya Mungu, anede kwenye kusudi la Mungu, aende kwa baba
yake aende akamuabudu Mungu wa baba yake katika nchi ya ahadi, Mungu mwenyewe
alisema aende na kuwa atakuwa pamoja naye
Mwanzo 31:2-3 “Yakobo
akaona uso wa Labani, ya kuwa hakumtazama vema kama jana na juzi. BWANA
akamwambia Yakobo, Urudi mpaka nchi ya baba zako na kwa jamaa zako, nami
nitakuwa pamoja nawe.”
Inaonekana kulikuwa na
hali ngumu katika nyumba ya labani na ni wazi kuwa Israel alikuwa mvumilivu
mno, ziko hali zinaweza kukuta mpaka majirani wakaona jinsi unavyoteseka na
kuvumilia, ziko hali zinaweza kukukuta mpaka Mungu mwenyewe anakuambia sasa
toka na kuwa nitakuwa pamoja nawe
Ni Mungu pia
aliyemshauri Yakobo kurejea na ni Mungu aliyemuahidi atakuwa pamoja naye,
yakobo alitoroka kama mahusiano yalikuwa mema haiwezekani kutoroka kwa mjomba
lakini kutoroka huku kimya kimya kunaashiria kuwa hakli haikuwa nzuri ujombani,
Labani anagundua bila shaka anamfuatilia Yakobo akiwa na hasira kali, akiwa amekusudia
kumdhuru na kumfanyia jambo baya sana Lakini Mungu wa wote wenye mwili
alimkemea Labani alimuonya katika ndoto alimtokea na kumueleza waziwazi Usimwambie Yakobo neno la heri wala la Shari! Ndio kuna watu ni wakorofi, hatuwawezi kwa akili
zetu na unyonge wetu, ndio wenye nguvu, ndio waliotuajiri ndio wajomba zetu
lakini Mungu akiwa upande wako hatakuacha uonewe, atamkemea kila mtu
anayesimama kinyume na kusudi la Mungu ndani yako kumbuka
Zaburi
105:14-15 “Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme
aliwakemea kwa ajili yao. Akisema,
Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.”
Haijalishi audi zako wana uwezo kiasi
gani, wana nguvu kiasi gani, wana uzoefu kiasi gani wana mali kwa kiasi gani
vyovyote iwavyo Bwana atawakemea Mungu alimkemea Labani kwaajili ya Yakobo, Mungu atamkemea kila mmoja
anayesimama kinyume nawe kwa kuwa wewe umtumishi wake, Labani ni lazima
akumbuke kuwa hawezi kushindana na kusudi la Mungu lililo ndani yako Lazima
akumbuke jinsi Mungu alivyomuonya na kusema naye, ana nguvu ana uwezo anaweza
kukudhuru lakini Bwana amesema naye ajihadhari asiseme le heri wala la shari
nini kingemtokea unajua unaelewa hakuna mtu anaweza kushindana na kusudi la
Mungu hata kidogo Labani angeshughulikiwa lakini afadhali alikumbuka maonyo ya
Mungu ona
Mwanzo
31:25-29. “Labani akamfikia Yakobo, na Yakobo
alikuwa amepiga hema zake katika mlima, na Labani na ndugu zake wakapiga hema
zao katika mlima wa Gileadi.Labani akamwambia Yakobo, Umefanya nini?
Umenihadaa, ukawachukua binti zangu kama mateka waliotwaliwa kwa upanga. Mbona
umekimbia kwa siri ukanihadaa, wala hukuniambia, nipate kuagana nawe uende zako
kwa furaha, na nyimbo, na ngoma, na kinubi?Wala hukuniacha niwabusu wanangu, na
binti zangu; basi umetenda upumbavu. Ninao uwezo mkononi mwangu wa kukufanyia
madhara; lakini Mungu wa baba yako usiku huu ameniambia, akisema, Ujihadhari,
usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.”
Nakuombea neema kwa Mungu, wewe
unayeteseka kwa sababu mbali mbali, natamka maneno ya kinabii juu yako dhidi ya
adui zako dhidi ya wanaokuonea dhidi ya wenye kutunga hila juu yako, kwamba
wakuache wajihadhai wasinenen neno la Kheri wala la shari juu yako! Wewe una Mungu aliye hai, wewe hauabudu
vinyago, wewe una kusudi la Mungu ndani yako nasema wakuache nasema wakuache
nasema wasikusimange nasema wasikusengenye nasema kwa lugha ya kinabii
nawakemea wenye kukusudia mdhara juu yako wasinene wasipange la kheri wala la
shari wakumbuke neno hili kwani Mungu yule yule wa Israel Mungu yuleyule wa
Yakobo na baba yetu Isaka na Ibrahimu huyu huyo ndiye mtetezi wetu, huyo huyo
ndiye atakayefanya njia , huyo huyo ndiye
jemedari wetu, huyo huyo hataacha mtu atuoneee hata kama ni wenye uwezo
na mamlaka atawakemea
Baraka za Mungu yule nimuabuduye na
ziwe na kila aneysoma waraka huu, Bwana kubariki na kuwa upande wako, wasinene
la Kheri wala la shari dhidi yako katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth amen
Rev.
Innocent Kamote
Mkuu
wa wajenzi mwenye Hekima!
UBA4IKIWE
JibuFuta