Alhamisi, 3 Februari 2022

Jinsi ya kuzidi kuwa Hodari.

Matendo 9:22 “Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo


Utangulizi:

Tunasoma Katika maandiko ya kwamba watu wengi wanaotajwa kama mashujaa wa Imani katika biblia, kwamba walikuwa hodari ona katika

Waebrania 11:32-34 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.”

Kwa msingi huo ni kama kusema watu wote wenye mafanikio na wanaondelea kufanikiwa katika ulimwengu walikuwa na uhodari ndani mwao na huu uhodari pia unaweza kuzidi zaidi na zaidi, maandiko yanatueleza kuwa Sauli akazidi kuwa hodari hii maana yake ni kuwa alikuwa hodari na akaendelea kuwa hodari, kuwa hodari na hata kujilinda na kuendelea katika uhodari huo sio jambo jepesi, kuna mambo ambayo ukiyafanya utazidi kuwa hodari katika maisha yako, kabla ya kuzungumiza jinsi ya kuzidi kuwa hodari, ni muhimu kwetu tukajifunza somo hili jinsi ya kuzidi kuwa Hodari kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-

·         Maana ya neno Hodari

·         Jinsi ya kuzidi kuwa Hodari

Maana ya Neno Uhodari:-

Neno hodari limetajwa mara kadhaa katika maandiko, Kila mtu anayetajwa katika maandiko anatajwa vilevile kuwa alikuwa na uhodari hususani wale wote ambao walikuwa maarufu na ambao Mungu aliwatumia kwa viwango vya juu katika maandiko kwa mfano tunasoma katika

Matendo 7:22 “Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo.”

Unaona tunasoma kuwa Musa alifundishwa Hekima yote ya Wamisri, akawa Hodari wa maneno na matendo, kwa msingi huo basi ili tuweze kufanikiwa katika maisha yetu na tusiweze kuharibikiwa hatuna budi kuhakikisha ya kwamba katika kila  Nyanja ya maisha yetu tunapaswa kuwa na uhodari, na kuzidi.

Matendo 18:24-26 Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu.  Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.”

Kwa hiyo utaona hivyo tena na tena katika maandiko kila wakati neno uhodari likijirudia tena na tena kwa watu waliokuwa na kitu cha ziada kwa msingi huo ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu wa kutosha ili tuweze kujua ni nini maana ya neno hodari au na kwanini agizo la Mungu katika maandiko linatutaka kuwa hodari ona

 Joshua 1:6-7 “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.”:-

Sasa basi ni nini maana ya kuwa Hodari? Manoneo yanayotumika katika maandiko kuelezea maana ya kuwa hodari katika lugha ya kiingereza ni pamoja na:-

Be strong and Courageous Be powerful ambalo maneno mengine yanayorumika sambaba na neno hili ni Capable, Forceful, Mighty, Potent, powerful, Fit na kadhalika, Hata hivyo neno hilo katika lugha ya kivita waebrania wanatumia neno “MARSHAL” ambalo mara nyingi au chache hutumika kwa maofisa wa jeshi wa ngazi ya juu kabisa wenye weledi wa kufanya mambo ya kupita kawaida, au kufanya mambo zaidi ya jinsi ulivyofundishwa katika Nyanja ya kijeshi ni Fidel Marshal – is the most senior military rank, or ordinary senior to the General officer ranks, usually it is the highest rank ina an army, and such few persons are appointed to it  Kwa hiyo tunapozungumzia mtu Hodari ni yule anayefanya mambo kwa weledi, au kwa ubora zaidi ya jinsi alivyoelekezwa na kufundishwa !  kwa hiyo maandiko yanapozungumzia wale mashujaa wa imani kuwa walikuwa hodari maana yake walikuwa na rank za juu zaidi za kijeshi, walifanya mambo kwa weledi kwa viwango vya juu zaidi ya jinsi ya walivyofundishwa

Waebrania 11:32-34 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.”

 Kwa msingi huo sasa Mungu anatutaka na sisi tuwe hodari, lakini kama ni mahodari sasa tuzidi kuwa hodari unaona sasa basi ni kwa jinsi gani tunaweza kuzidi kuwa Hodari?

1.      Uwe mtu wa Haki 

A man of integrity he is or she is a person who is value what is honest, true, noble, trustworthy, kind and right ahead of Personal gain yaani ni mtu mwenye kupenda kweli, mwenye kustahi, mwenye kutenda haki, msafi asiye na lawama, mwema na mwenye sifa njema

 Waefeso 4:8 “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.”

Mtu wa haki anatembea na uwepo wa Mungu, au Mungu hufanya masikani yake au atadumu katika vizazi vyake atadumu katika uwepo wa Mungu atakaa katika masikani za Mungu atafanikiwa

Zaburi 15:1-3 “Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu? Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake.”

Unapochunguza maisha ya watu Hodari utaweza kuona moja ya sifa wanayotajwa kuwa nayo ni kutenda haki, hawakuwa na hila ndani yao andiko lile katika Waebrania linasisitiza kuwa mashujaa wa imani walitenda haki sasa basi ikiwa tutaishi maisha ya haki tutazidi kuwa hodari kwa sababu Mungu atatubariki ona

Zaburi 119:1 -3Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana. Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote. Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake.”

2.      Uwe na dhamiri Njema 

Ni muhimu kufahamu kuwa watu Hodari vilevile ni watu wanaokuwa na dhamiri njema, kila unalilifanya unalifanya bila unafiki, Maandiko yanawataka wakristo kuwa na dhamiri njema ni muhimu kukumbuka kuwa Mungu hatahukumu matendo ya nje Mungu anaangalia ndani ya moyo na kupima dhamiri yetu, Neno dhamiri katila lugha ya kiyunani ni SUNOIDA Neno hili limetajwa mara 34 katika agano jipya mara nne katika injli na kitabu cha matendo ya mitume lakini mara 30 katika nyaraka ka Mtume Paulo wakati wote akisisitiza watu kuwa na dhamiri njema, kutokufanya jambo kwaajili ya unafiki,  ona

1Timotheo 1:5-6 “Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki. Wengine wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili

1Timotheo 1:18-20 “Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo uvipige vile vita vizuri; uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.  Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.”

Matendo 23:1 ”Paulo akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa dhamiri safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hata leo hivi.”

Matendo 24:16 “Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote

1Timotheo 3:8-10 “Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu.wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.”

Muda usingeweza kutosha kuona namna maandiko yanavyokazia tena na tena swala la kuwa na Dhamiri njema SUNOIDA kumfikiri Mungu na wanadamu 2Wakoritho 8:20-21 “Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia; tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.”

3.      Endelea kujisomea siku zote 

Ni muhimu kufahamu kuwa watu waliokuwa hodari vilevile na wanaozidi kuwa Hodari huwa wanasoma na wanajiendeleza katika maarifa, maandiko yanaonyesha kuwa kadiri mtu anavyosoma ndivyo anavyoongeza ufahamu wake zaidi ona

Mathayo 24:15 “Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),

Kusoma kunaleta ugunduzi wa siri nyingi sana za kimaandiko Nabii Daniel aligundua kuwa siku za kukaa kwao utumwani zilitabiriwa kuwa ni miaka 70 na hivyo kwa kusoma vitabu alighundua kuwa wakati huo umefika na akaanza kumuomba Mungu ona

 Daniel 9:1-3 “Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo; katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.”

Unaona kumbe Nabii Daniel aligundua baadhi ya mambo kwa kusoma na akaingiza kumuomba Mungu, ziko siri nyingi zimefichwa katika vitabu, hivyo watu wanaozigundua ni wale wanaosoma asomaye na afahamu, watu wengi huwa wanashangazwa sana na hekima kubwa aliyokuwa nayo Paulo Mtume lakini ukichunguza kwa undani utagundua kuwa mpaka anakuwa mzee alikuwa ni mtu mwenye tabia ya kupenda kujisomea, hakufikiri kuwa amekwisha kufika lakini mara kwa mara alitaka kujiendeleza na alikuwa na tabia ya kujisomea ona,

2Timotheo 4:13 “Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi.”           

Je wewe unajisomea? Unaongeza maarifa kwa kupenda kujisomea? Kusoma kunaongeza maarifa na maarifa yanaongeza ujuzi na ujuzi unaleta weledi na kukufanya wewe kuwa Hodari.

4.      Fanya maamuzi sahihi 

Moja ya mambo ambayo yanawaletea watu wengi sana majuto katika maisha yao ni pamoja na swala zima la kufanya uamuzi, wako watu wengi sana ambao wanajutia maamuzi waliyoyafanya na wanahitaji second chance, lakini imeshindikana kwa sababu ya maamuzi yao! Mashujaa wa imani kila walipotaka kufanya jambo hawakutumia akili zao, waliuliza kutoka kwa Bwana

1Samuel 23:1-3 “Kisha wakamwambia Daudi, kusema, Angalia, Wafilisti wanapigana vita juu ya Keila na kuiba nafaka sakafuni mwa kupuria. Basi Daudi akamwuliza Bwana, kusema, Je! Niende nikawapige hao Wafilisti? Naye Bwana akamwambia Daudi, Nenda ukawapige Wafilisti, na kuuokoa Keila. Ila watu wake Daudi wakamwambia, Tazama, sisi tunaogopa hapa katika Yuda; je! Si zaidi tukienda Keila juu ya majeshi ya Wafilisti? Basi Daudi akamwuliza Bwana tena, Naye Bwana akamjibu, akasema, Ondoka, ukashukie Keila; kwa kuwa nitawatia hao Wafilisti mikononi mwako.”

1Samuel 23:9-13 “Naye Daudi alifahamu ya kuwa Sauli amemkusudia mabaya; akamwambia Abiathari, kuhani, Lete hapa hiyo naivera. Ndipo Daudi akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, mimi mtumwa wako nimesikia hakika ya kuwa Sauli anataka kuja huku Keila, ili kuuharibu mji kwa ajili yangu. Je! Watu wa Keila watanitoa, nitiwe mkononi mwake? Je! Sauli atashuka, kama mtumwa wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumwa wako. Naye Bwana akamjibu, Atashuka. Ndipo Daudi akasema, Je! Watu wa Keila watanitia mimi na watu wangu mkononi mwake Sauli? Bwana akasema, Watakutia. Basi Daudi na watu wake, ambao wapata kama mia sita, wakaondoka na kutoka Keila, wakaenda po pote walipoweza kwenda. Kisha Sauli akaambiwa ya kwamba Daudi amekimbia toka Keila; akaacha kutoka nje"

1Samuel 30:8-9 “Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote. Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikilia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa.”

Unaona Daudi kila alipokuwa anataka kufanya jambo aliuliza kutoka kwa Bwana, kwanini alikuwa anafanya hivi ni ili aweze kufanya maamuzi sahihi bila kutumia au kutegemea akili zake yeye mwenyewe maandiko yanasema hivi katika Mithali3:5-6 “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu.”

5.      Hakikisha unakuwa mnyenyekevu.

Wengi wetu tunatabia ya kupuuzia hali ya kuwa kujinyenyekeza, Mungu anapotuinua tunainuka na kiburi, na kwa sababu hiyo inakuwa ngumu kwetu kufundishika na hata kuonyeka, hasa pale tunapofikiri kuwa labda tuna akili kuliko wengine, au tunaweza kujidhani kuwa sisi ni kitu  maandiko yanaonya sana tabia ya kujiinua na kujikweza na yanatufundisha kuwa wanyenyekevu, unyenyekevu huwa unalipa, Yesu Kristo Bwana wetu aklifanikiwa sana kwa sababu alikuwa mnyenyekevu na Mungu akamuadhimisha mno

Wafilipi 2:3-11 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.  Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”

Kanuni ya Mungu ya kumpeleka mtu juu ni mtu huyo kujishusha, kujinyenyekeza, Yesu mwenyewe alisema hivi katika Luka 14:8-11 “Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe, akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma. Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.”

Watu wengi sana duniani wanabadilika mno wanapopata madaraka au kibali, au pale Mungu anapokuwa amekusudia kuwapeleka kwenye ngazi nyingine, wanapokuwa wamefanikiwa hujisahau na kuwa na kiburi kiasi cha kutokytaka kuwasikiliza wengine, hata watu wa Mungu huonekana kuwa wajinga na hawawezi kusikilizwa katika nafasi yao

2Mambo ya Nyakati 26:16-20 “Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi Bwana, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa Bwana, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia. Azaria kuhani akaingia nyuma yake, na pamoja naye makuhani themanini wa Bwana, mashujaa; wakamzuia Uzia mfalme, wakamwambia, Si haki yako, Uzia, kumfukizia Bwana uvumba, ila ni haki ya makuhani wana wa Haruni, waliofanywa wakfu, ili wafukize uvumba; toka katika patakatifu; kwa kuwa umekosa; wala haitakuwa kwa heshima yako kutoka kwa Bwana, Mungu. Akaghadhibika Uzia; naye alikuwa na chetezo mkononi cha kufukizia uvumba; naye hapo alipowaghadhibikia makuhani, ukamtokea ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa Bwana karibu na madhabahu ya kufukizia. Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamtazama, na angalia, alikuwa na ukoma pajini mwa uso, wakamtoa humo upesi; hata na yeye mwenyewe akafanya haraka kutoka, kwa sababu Bwana amempiga.” 

Unaona hii ni kanuni kubwa sana ya mafanikio kwa mashujaa wa imani, wengi walifanikiwa kwa sababu walifahamu umuhimu wa kuwa wanyenyekevu, na wengine tunawasoma kuwa kwa sababu ya kiburi waliasi na kupatwa na mabaya kanuni za Mungu hazidanganyi kuwa kijapo kiburi ndipo ijapo aibu Mithali 11:2 “Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.” Ni kwaajili ya haya sasa Ndipo Mungu anatutaka katika neno lake tuwe wanyenyekevu, ukijinyenyekeza neema ya Mungu inakuwa kubwa sana, lakini kama hatutajua kanuni ya kujinyenyekeza Mungu atapinga anasi yeye mwenyewe kwani ukiwa na kiburi unashughulikiwa na Mungu 1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”

6.      Uwe mwaminifu.

Hakuna jambo Muhimu katika maisha ya mwanadamu kama uaminifu, kila mtu duniani anapenda mtu mwaminifu, hata mume mzinzi au mke mzinzi bado anataka apatiwe uaminifu kutoka kwa mwenziwe, Maandiko yanatutaka tuwe waaminifu, tena tuwe waaminifu hta kufa

Ufunuo 2:10 “Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

Kuwa mwaminifu ni kujidhabihu, ni kujitoa, commitment- kiyunani DESMEFSI ambalo kwa tafasiri ya kiingereza ni imprisonment - kujifunga au kufanya maamuzi magumu mfano hutafanya jambo Fulani mapaka jambo Fulani limefanikiwa:-

1Samuel 6:9-11 “Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala Bwana hakumchagua huyu. Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku.”

Matendo 23:12 “Kulipopambauka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hata wamwue Paulo.”

Esta 4:15-16 “Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai, Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.”

Kwa msingi huo kuwa mwaminifu kuna maana ya kujifunga, lakini pia kusimamia kitu mpaka kifanikiwe kwamba iwe ni jambo kubwa au kwamba ni jambo dogo, kwa mujibu wa mafundisho ya Yesu Kristo yeye alisisitiza kuwa uaminifu pia unapimwa katika kuanzia na mambo madogo madogo sana Yesu anaamini kuwa mtu akiwa muaminifu katika jambo lililo dogo anaweza kuwa mwaminifu katika jambo lililo kubwa zaidi

Luka 16:10-12 “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?

 Watu wengi sana wameshindwa kuwa hodari katia nafasi walizo nazo na vipawa walivyo navyo kwa sababu tu wameshindwa kuwa waaminifu, Mungu anahitaji watu ambao ni waaminifu Uaminifu ni tabia ya Mungu ili sisi nasi tuwe kama baba wa Mbinguni hatuna budi kuwa na tabia hii ya uungu kwa kuwa waaminifu na Mungu atatufanikisha

Zaburi 145:17 “Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.”

Kwa msingi huo Mungu anatutaka sisi nasi tuwe waaminifu kwa kuingia katika ushirika wa mwanawe ona

1Wakoritho 1:9 “Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.”

7.      Lazima uwe na uvumilivu

Watu hodari vilevile ni wavumilivu, au wenye subira ni vigumu sana kuwa na mafanikio kwa njia rahisi rahisi, mafanikio yanawakuta watu wenye uwezo mkubwa katika uvumilivu, tunaambiwa kuwa manqabii wote walikuwa wavumilivu sana lakini vilevile tunaambiwa kuwa Ayubu alikuwa mvumilivu, Mungu anapoona uvumilivu wetu hatimaye anatukumbuka na kutufadhili ona

Yakobo 5: 10-11 “Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”

Hakuna mafanikio ya kufumba na kufumbua, wala mafanikio hayaji kwa usiku mmoja, watu wote waliofanikiwa duniani walikuwa na tabia ya uvumilivu, kujifunza kuwa wavumilivu kutatuletea hali ya kuzaa matunda, ukitaka kuwa na afya imara lazima ufanye mazoezi, mazoezi sio kitu kitamu, utakimbia, utabeba vitu vizito, utatembea na kufanya hili ama lile mambo ambayo yanahitaji nidhambu ya hali ya juu, kwa ufupi uvumilivu ni nidhamu ya hali ya juu, kila jambo litahitaji uvumilivu Yesu katika mfano wake ule wa mbegu alionyesha wazi kuwa hata zile zinazozaa matunda huwa hazizai bila uvumilivu ona

Luka 8:11-15 “Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu. Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka. Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga. Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote. Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.”

Yakobo anatoa mfano wa Mkulima anavyovumilia mpaka kupata mazao, hakuna kazi ngumu sana duniani kama kulima hasa kama ni kilimo kile cha kutumia mikono lakini ukifuatilia maisha ya wakulima utaweza kuona na kujifunza kuwa ni watu wenye imani na subira wanasubiri mpaka wakati wa Mavuno ufike, sisi nasi hatuna budi kuwa wavumilivu na waaminifu na kufanya majukumu yetu ambayo Mungu ametupa na kwa uvumilivu mkubwa tutafikia malengo na mafanikio na kuzidi kuwa hodari.

Yakobo 5:7 “Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.”

Unaona kwa msingi huo kila kitu kinahitaji uvumilivu, malezi yanahitaji uvumilivu, uanafunzi unahitaji uvumilivu, ualimu unahitaji uvumilivu, uongozi unahitaji uvumilivu, na kila tukifanyacho kinahitaji uvumilivu, kwa msingi huo ili tuwezer kufanikiwa katika kila eneo la maisha yetu hatuna budi kuwa na uvumilivu, na tunapovumilia tutaendelea kuwa hodari zaidi na zaidi.

8.      Jenga mazingira ya kuhitajika.

Maandiko yanasema hivi katika kitabu cha Mithali 14:4 “Zizi ni safi ambapo hapana ng'ombe; Bali nguvu za ng'ombe zaleta faida nyingi.”

Maandiko yanatufundisha kuwa Ngombe wana faida kuwa sana japo wakiwepo zizizni inaweza kuonekana kuwa wanachafua, na wakiwa hawapo yaweza kuonekana kuwa zizi ni safi, lakini ni afadhali kuwa nao kwa sababu wana faida kubwa sana , wao hulima na kusababisha mazao, tutupa nyama, hutupa maziwa, hutupa ngozi na kadhalika, kimsingi tunajifunza umuhimu wa watu wenye bidii, Mungu anataka ufanye kazi kwa bidii na kuwa mwenye faida ili ikiwezekana watu wakuhitaji, watu maarufu katika Biblia waliitwa watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao

Waebrania 11:32-38 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;        ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.”      

Popote ulipo jitume kwa bidii ili watu waone umuhimu wako, uwe na ubunifu, na uwezo wa kujenga mpango utakaofanya wewe uhitajike na uonekane umuhimu wako katika jamiii ona

 Mwanzo 41:33-38 “Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba. Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa. Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote.  Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?”

9.      Usiogope 

Hofu ni mojawapo ya kifungo kikubwa sana, Mungu hafurahii watu wanaoogopa, mtu anayeogopa  na siyejaribu ni kizuizi kikubwa sana na ndio maana mara kwa mara utaweza kuona Mungu akiwataka watu wake wasiogope Yoshua 1:5-9 “Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha. Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.”  

Kwa nini Mungu alimsisitiza Yoshua asiogope kwa sababu woga uliwkosesha Israel Inchi ya kanaani kwa miaka mingi sana walikosa urithi wao, watu wengin wanaotaka mtu asijaribu au mtu asifanikiwe hujaribu kutumia hofu kama njia ya kukuwekea utisho ili uogope na usifanya majaribio, katika wapelelezi wale walioipepeleza ichi ya kanaani kumi kati yao walileta habari ya hofu na kuwatisha watu kiasi cha watu kuogopa na kujikosesha nchi ya maziwa na asali

Hesabu 14:1-9 “Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. Mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri? Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, tukarudi Misri. Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya mkutano wa kusanyiko la wana wa Israeli. Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope.”

Unaona Wana wa Israel walishaogopa mno wakati wao wanaogopa kumbe wakanaani nao walikuwa wamewaogopa muda mrefu sana na hakuna ujasiri uliokuwa umesalia ndani yao, wakati mwingine tunajikosesha Baraka za Mungu kwetu kwa sababu ya hofu ona

Joshua 2:1-11 “Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko. Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi. Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi. Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka; ikawa kama wakati wa kufungwa lango la mji, kulipokuwa giza, watu wale wakatoka, wala sijui walikokwenda; wafuateni upesi, maana mtawapata. Lakini yeye alikuwa amewapandisha darini, akawaficha kwa mabua ya kitani, aliyokuwa ameyatandika juu ya dari. Basi hao watu wakawafuata kwa njia iendayo Yordani mpaka vivukoni; na mara wale watu waliowafuatia walipokwisha kutoka, wakalifunga lango.Tena kabla hawajalala akawaendea juu darini, akawaambia wale wanaume, Mimi najua ya kuwa Bwana amewapa ninyi nchi hii, na ya kuwa hofu imetuangukia mbele yenu, na ya kuwa wenyeji wote wa nchi wanayeyuka mbele yenu. Maana tumesikia jinsi Bwana alivyoyakausha maji ya bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa huko ng'ambo ya Yordani, yaani, Sihoni na Ogu, mliowaangamiza kabisa. Na mara tuliposikia hayo mioyo yetu iliyeyuka, wala haukusalia ujasiri wo wote katika mtu awaye yote, kwa sababu yenu; kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, katika mbingu juu na katika nchi chini.”

Hebu jaribu kuwaza wakati Israel wakiwaogopa wanaowaogopa! Wakanaani walishashikwa na hofu tangu waliposikia matendo makuu ya Mungu lakini warithi wa ile Inchi nyaani waisrael wenyewe walikuwa wanaogopa na iliwachukua miaka 40 kuingia katika inchi ya kaanaani lakini tatioz kubwa likichangiwa na kutokuamini kwao! Kila mtu anayetaka kuwa hodari zaidi inampasa kujifunza kutokuogopa!

10.  Futa msamiati haiwezekani.

Watu wote waliofanikiwa katika maandiko ni wale waliokuwa hawana msamiati wa haiwezekani, msamiati huu sio msamiati wa kiungu hata siku moja Mungu hajawahi kuzungumza kokote kuwa kuna kitu kisichowezekana hususani kama utamshirikisha na yeye

Mathayo 19:26 “Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.”

Mwanzo 18:9-14 “Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani. Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake. Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? BWANA akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.”

Yeremia 32:27 “Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?

Kwa msingi huo tunachopaswa sisi ni kujiungamanisha na Mungu ili tuweze kutenda mambo makubwa sana Zaburi 60:12 “Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.”

Zaburi 108:13 “Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.”

11.   Kumbuka kuukomboa wakati.

Kulitumikia kusudi lolote la Mungu hapa Duniani kumbuka limewekwa katika muda, kwa msingi huo Maandiko yanatutaka vilevile kuwa na hekima ya jinsi na namna ya kuukomboa wakati, kumbuka kuwa kila mwanadamu anayeishi ulimwenguni ana masaa 24 kwa siku, ana siku saba kwa wiki siku 30 kwa mwezi na Miezi 12 kwa mwaka sawa na siku 365, lakini moja ya tatizo kubwa tulilonalo wanadamu ni kutokuujua wakati na kutokujua namna ya kuzitumia nyakati

Luka 19:41-44 “
Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.”         

Yesu aliulilia mji wa Yerusalem ambao ulibomolewa vibaya mwaka wa 70 baada ya Kristo yaani kama miaka 27 baadaye na sababu kubwa ya kubomolewa kwao ni ka sababu hawakujua majira yaani Muda wa kutembelewa na Mungu walipuuza waklimkataa Yesu walimsulubisha na wakati ulifika walijuta lakini wakati huo muda ulikuwa umekwisha kwenda, kila mtu anayetaka kuwa mhodari katika maisha yake lazima ajue kuukomboa wakati, mtu anayeukomboa wakati katika maandiko anaitwa mtu mwenye hekima ona Waefeso 5:15-17 “
Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.” Biblia ya kingereza na NIV inafananisha Muda na nafasi ya bahati OPPORTUNITY –  Kwa KIYUNANI Efkairia maana yake – a time or set of circumstances that makes it possible to do something, yaani ni muda au wakati ambapo unapata mazingira ya kuweza kufanya jambo, kwahiyo matumizi ya muda na matumizi ya nafasi za kipekee ambazo ulipaswa kuzitumia vema, kwa hiyo tiofauti yatu na watu wengine ni sio kwa sababu wao wana muda mwingi zaidi bali kwa sababu wao wana ujuzi wa kutumia nafasi

Muhubiri 3:1-8 “
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.”

Kwa msingi huo kujua nyakati kunaweza kutusaidia kujua nini litupasalo kufanya wana wa Israel walifanikiwa sana hasa nyakati za utawala la Daudi kwa vile lilikuweko kabila la wana wa isakari ambao walikuwa na ujuzi wa nyakati na nini kiwapasacho watu kufanya kwa wakati huo ona

1Nyakati 12:32 “
Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.”

Kwa msingi huo kila mtu anayetaka mafanikio ni lazima aelewe na ajue namna na jinsi ya kuutmia wakati ni hekima kuutumia wakati vizuri! Na ujinga kupoteza muda na kutokujua namna na jinsi ya kuutumia wakati, Bwana na ampe neema kila mmoja wetu ajue jinsi anavyopaswa kuutumia wakati ili tusijute baadaye katika jina la Yesu amen.

12.  Fanya kazi kwa bidii.

Unapofuatilia maisha ya watu waliofanikiwa katika maandiko, utagundua pia kuwa watu hao walikuwa wachapa kazi, hawakuwa wavivu, wote tunafahamu kuwa kazi ya kwanza aliyopewa Adamu haikuwa kuabudu, Mungu alimuweka Mwanadamu katika bustani ya edeni ili afanye kazi ona Mwanzo 2:15 “BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.”, kulima na kutunza sio kazi nyepesi, kwa msingi huo utaweza kugundua kuwa Mungu alimtaka mwanadamu afanye kazi, hata maumbile ya kiulimwengu yanaonyesha mkazo wa kufanya kazi katika siku saba ambazo Mungu ametupa utaweza kuona ametoa siku sita za kufanya kazi na siku moja utamkumbuka bwana Mungu wako ona

Kutoka 35:1-2 “Musa akakutanisha mkutano wote wa wana wa Israeli, na kuwaambia, Maneno aliyoyausia BWANA ni haya, kwamba myafanye. Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa BWANA; mtu awaye yote atakayefanya kazi yo yote katika siku hiyo atauawa

kwa hiyo utaweza kuona ni kama kwa kiwango Fulani hivi neno la Mungu linatutaka tufanye kazi kanuni hii ya kufanya kazi imewafanya watu wa mataifa ya Asia kubarikiwa na kufanikiwa kwa haraka sana, nilipotembelea Marekani nilikuta jamii kubwa ya wakazi wa marekani katika jimbo la Viginia ni wakorea na wanapendwa sana na wamarekani kwa sababu ni wachapa kazi, hata nchi yao imeendelea sana kwa sababu wako aggressive ni wenye juhudi katika kufanya kazi Maandiko yako kinyume na uvivu na yanamtaka kila mmoja afanye kazi kwa bidii na mkazo huu umedhihirika hata kwa mkazo ulio wazi kuwa asiyefanya kazi kula na asile ona

2Wathesalonike 3:10-12 “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine. Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.

Unaona kwa msingi huo kutokufanya kazi ni dhambi, Mungu anataka watu wafanye kazi zao, kila mmoja awe na shughuli yake mwenyewe ya kufanya, na kuhakikisha kuwa anajituma, maandiko yanaionyesha kuwa kuna mafanikio makubwa kama watu watafanya kazi kwa bidii, iko wazi kuwa kila mtu anayefanya kazi kwa bidii na kwa kujitoa anafanikiwa, tunafahamu yako mapito na pia kuwa wakati mwingine haiku wazi kwa sababu wako watu wanafanya kazi kwa bidii nab ado hayaonekani mafanikio, nii ni sehemu ndogo ya matokeo ya kimaisha lakini Biblia inatuongoza kwamba bado ni agizo la Mungu kufanya kazi kwa bidii, tunapofanya kazi kwa bidii bila kujali imani zetu na kabila zetu na rangi zetu ni wazi kuwa Mungu anasimama karibu nasi, kwa hiyo fanya kazi hata kama hujui Mungu yuko kwenye hatua gani kukutokea

Mithali 12:24 “Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.” Neno la Mungu linatutaka tufanye kazi na kutunza familia zetu na jama zetu kama mtu anashindwa hata kuitunza familia yake maandiko yanasema ni mbaya kuliko asiye na imani ona

1Timotheo 5:8 “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini Paulo mtume pamoja na kuwa Muhubiri wa injili alihakikisha kuwa wakati mwingine anafanya kazi kwa bidii ili kujipatia mahitaji yake yeye alijua wazi kuwa ni heri kutoa kuliko kupokea

Matendo 20:33-35 “Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea Lakini maandiko pia yanataka tujifunze kutoka kwa chungu au mchwa kwamba wanafanya kazi ka bidii na wanajiwekea akiba hata kwa wakati wa kiangazi au nukame ona

Mithali 6:6-11 “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silahahatuna budi kuhakikisha kuwa kila tulifanyalo tunalifanya kwa bidii na tunashuhudia mafanikio makubwa sana katika utendaji wetu wa kazi na maisha yetu.

13.  Usiache kumtegemea Mungu

Maandiko yanaonyesha kudumu kwetu na kuendelea kusimama kwetu ni kwa kumtegemea Mungu na kumtumaini mtu anayemtegemea Mungu anafananishwa na mlima sayuni hatatikisika milele

Zaburi 152: 1-5 “Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu. Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo. Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, Bwana atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.”

Mashujaa wote wa imani walioendelea kuwa hodari zaidi walimtegemea Mungu na kamwe hawakuwategemea wanadamu, mara unapo mfanya mwanadamu kuwa kinga yako na kumdaharau Bwana ukweli ni kuwa unajiweka katika laana na hautafanikiwa

Yeremia 17:5-7 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo

Kwa msingi huo pamoja na mambo mengine yote hatuna budi kuhakikisha kuwa tunamtegemea Mungu katika njia zetu zote na maandiko yanatuasa kwamba wala tusizitegemee akili zetu wenyewe

Mithali 3:5-6 “
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.”

Mambo yanapokuwa magumu neno la Mungu linatuagiza kuomba na kumtwika yeye fadhaa zetu zote ona

1Petro 5:6-7 “
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenuhakuna sababu ya kufadhaika

Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu

Ni imani yangu kuwa kanuni hizi zitamsaidia kila mtu anayetaka kuwa hodari zaidi katika Nyanja mbalimbali ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda

Yohana 13:17 “
Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni