Jumapili, 13 Februari 2022

Twaishi ikiwa ninyi Mwasimama katika kwa Bwana.


1Wathesalonike 3:6-10Lakini Timotheo alipotujia hivi sasa kutoka kwenu, alituletea habari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote; mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi kuwaona ninyi. Kwa sababu hiyo, ndugu, tulifarijiwa kwa habari zenu, katika msiba na dhiki yetu yote, kwa imani yenu. Kwa kuwa sasa twaishi, ikiwa ninyi mnasimama imara katika Bwana. Maana ni shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu; usiku na mchana tunapoomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu, na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu?

Utangulizi:

Katika maandiko hayo hapo juu, Paulo mtume anamshukuru Mungu kwa habari alizopokea kutoka kwa Timotheo kuhusu wanafunzi kule Thesalonike kwamba wanaendelea vizuri katika imani, na upendo huku wakimkumbuka Paulo mtume na watenda kazi wengine ambao kwa kiwango Fulani walilazimika kuondoka Thesalonike kwa sababu ya dhiki na mateso makubwa yaliyokuwa yakiwakabili kwaajili ya injili yaliyolazimisha Paulo na Sillas na watenda kazi wengine kwenda katika mji wa Beroya mbele ya Thesalonike kwaajili ya usalama wao


Matendo ya Mitume 17: 1-10Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi. Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo. Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache. Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako, na Yasoni amewakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na kwamba yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu. Wakafadhaisha ule mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo. Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yasoni na wenziwe wakawaacha waende zao. Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi” 


Kutokana na fujo zilizojitokeza waliamua kumuacha Timotheo ili aweze kuimarisha kanisa lililokuweko Thesalonike, Hata Timotheo alipowajia Paulo mtume na kuwataarifu habari ya kanisa lililokuwako Thesalonike, na jinsi wanavyokua katika imani na upendo na ya kuwa wanawakumbuka sana mitume na kuwa wanatamani kumuona tena, habari hii ilikuwa njema sana kwa Paulo mtume na alifurahi sana ya kuwa pamoja na mapito yote waliyoyapitia  na majaribu na dhiki ilifurahisha kuwa wathesalonike walisimama katika imani, Paulo alifurahi na aliwajulisha katika waraka wake kuwa anaendelea kuwaombea na kwamba iko siku atawatembelea ili aweze kuwaimarisha katika imani, Kanisa la leo tunapaswa kufurahia kuona watu hususani watoto wachanga kiroho wakidumu na kusimama katika imani, ni jambo lanye kutia moyo kuiona kazi uliyoianzisha ikiendelea vizuri, watoto wetu wa kiroho wakikua na kuhubiri kama sisi, na kuomba kama sisi na wakiitetea imani kuandaa na kuhubiri vilevile kama wanavyojifunza kutoka kwetu jambo hili linaleta furaha kubwa tunajifunza somo hili twaishi ikiwa ninyi mnasimama imara kwa Bwana kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-


1.       Maana ya kusimama Imara

2.       Umuhimu wa kusimama Imara 


Maana ya Kusimama imara!

Moja ya furaha kubwa sana aliykuwa nayo Paulo mtume ni kuona watu wa Mungu waliozaliwa kiroho katika hali ya dhiki nyingi sana wakisimama imara katika imani maneno yanayotumika kuelezea kusimama imara katika kiyunani ni “STEKETE” neno hili katika kiyunani ni neno la kijeshi lenye maana ya kuwa tayari kwa mapambano, ni kusimama kama anavyosimama askari aliyepewa amri ya tahadhari kuwa tayari kukabiliana na adui, hii maana yake wathesalonike walikuwa tayari wako imara tayari ka mapambano dhidi ya shetani aliyekuwa akilishambulia kanisa kwa dhiki na kwa mafundisho ya kiyahudi ya walimu wa uongo waliokuwa wakifundisha kinyume na injili ya mtume Paulo, Wathesalonike walikuwa tayari wameshajifunza ile kweli na walikuwa wameipokea imani katika dhiki na walikuwa wako tayari kikakamavu kukabiliana na upinzani wa aina yoyote STEKETE ni anchor au attention, wao walikuwa kama askari ambao wako tayari sasa kumkabili adui wako tayari hata kufa na kupoteza maisha yao wakiitetea kweli na hawakuwa tayari kurudi nyuma na kuiacha imani,  Paulo mtume alifurahi na luha hii anayoitumia aliwahi kuwaambia wakoritho vilevile kwamba waimarike, wasitikisike, na wamtumikie Bwana siku zote ona


1Wakoritho 15:58 “Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.”


Maneno ya kiingereza yanayotumika ni kama “steadfast, immovable” hii ni hali ya kusimama imara bila kuyumbishwa mara kwa mara Mungu anatamani tuwe katika hali kama hiyo hatupaswi kubabaika kwa namna yoyote ile.


Wafilipi 1:27-30 “Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili; wala hamwaogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara mathubuti ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu. Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa

unaona Yesu Kristo na mitume wanafurahi kuwa na wanafunzi imara, hata mimi nataka watu imara watu wanaosimama imara na kuitetea imani, wakiishindania injili, watu ambao wako tayari hata kwaajili ya mateso, wakitwaa mfano wa mitume na manabii ambao walivumilia magumu, leo hii ukisikia mtu ameiacha imani unaweza kushangaa, mtu anaiacha imani kwaajili ya mwanamke tu mwenye mapaja makubwa, mtu anaisha imani kwaajili ya chipsi na soda, mtu anaiacha imani kwa kukosa mume wa kumuoa, mtu anaiacha imani kwa sababu uchumba umevunjika, mtu anaiacha imani kwa sababu za kipuuzi sana ambazo ni ngumu hata kumueleza Mungu na kujaza katika faili lake Nyakati za kanisa la kwanza watu walipambana na kusimama kidete wakiitetea imani, lugha ya ujenzi ya kanisa sio lele mama ni lugha ya kivita nitalijenga kanisa langu juu ya mwamba na wala malango ya kuzimu hayataliweza leo hii ni tofauti, watu hawamjui shetani wala hajawajui namna ya kzuipinga nhila zake watu wamekuwa laini kama mlenda waklichukuliwa na upepo wa kila aina wa imani, hawana hata uwezo wa kupambanua jema wala baya, Yesu alikuwa hana mpango na watu dhaifu hata siku moja Yesu alikuwa ana mpango na watu watakaojenga nyumba zao juu ya mwamba ambao hakuna upepo utaziangusha nyumba hizo,


Mathayo 7:24-27 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.”


Umuhimu wa kusimama imara


Lilikuwa ni jambo la kufurahisha sana kwamba Kanisa la Thesalonike watu wanasimama imara licha ya kuwa walizaliwa katika hali ya dhiki na majaribu makali, Lakini baada ya kumuacha Timotheo na kuliimarisha kanisa anakuja na habari njema sio tu imnaonekana kumfurahisa Paulo mtume bali inamfurahisha sana Mungu Mungu hafurahishi na watu vuguvugu katika imani anataka watu wawe motoooo watu wanaositasita Mungu hapendezwi nao ona


Waebrania 10:38-39 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.”


Wakristo wa kweli hawapaswimkuwa watu wenye kusitasita Mungu hapandezwi na watu wasitao mwandishi wa kitabu cha waebrania anaeleza kuwa sisi hatuko miongoni mwao wasitao, Mungu ambariki kila mtu asiyesitasita katika imani na kuishi maisha ya uvuguvugu ambayo yatapalekea kutapikwa na Yesu Kristo


Ufunuo 3:15-16 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.”


Mungu anataka mtu aliye moto, anayesimama imara, sio anayetetemeka vitani kama hatutazingatia swala la kusimama imara tutatapikwa na mfumo utatukataa, Wakristo bado tunakabiliwa na imani potofu, bado shetani analishambulia kanisa kwa namna nyingi sana na leo tumekuwa na wakristo wepesi sana wepesi mno, Mungu atupe neema ya kusimama imara katika bwana katika jina la Yesu Mwana wa Mungu akliye hai amen!

Na Rev. Innocent Kamote.

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima! # 0718990796 #

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni