Ijumaa, 18 Novemba 2022

Fikirini Maua ya Mashamba!


Mathayo 6:28-32 “Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?  Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.


Utangulizi:

Katika moja ya hutuba yake nzuri na ya muhimu maarufu iama hutuba ya Mlimani, Yesu Kristo anatumia mfano wa Ndege wa angani na Maua ya kondeni, kutengeneza hoja za kifikra akilini (logic of comparison) kuonyesha namna Mungu anavyowathamini wanadamu kuliko ndege wa angani na maua ya kondeni na kama Mungu anaweza kujali sana vitu hivyo vidogo mno katika uumbaji wake basi kwa hakika anawajali sana wanadamu ambao ni kilele cha uumbaji wake, na ambao ameutawaza juu ya kazi zake zote

Zaburi 8:4-8 “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.

Katika nyakati za leo wasomaji wengi wa neno wanaweza wasielewe au isiingie akilini kwanini Yesu alitumia mfano huu na je watu wa nyakati zake waliweza kumuelewa?

Kwanini maua ya mashamba?

Kal Vahomer ni kanuni ya siri ambayo Yesu aliitumia, Neno la kiibrania KAL VAHOMER ni neno linalohusiana na kanuni ya kiualimu iitwayo kutoka wazo dogo kwenda wazo kubwa au kutoka wazo rahisi kwenda wazo gumu From minor to the Major au from simple to Complex hii ilikuwa ni moja ya kanuni iliyotumiwa na walimu wengi wa nyakati ya karne ya kwanza, kulikuwa na kanuni kama saba walizotumia marabi wa kiyahudi kutafasiri maandiko au mafundisho na KAL VAHOMER ilikuwa ni mojawapo kutoka jambo dogo kulinganisha na jambo Kubwa, kama Mungu anajali maua je si zaidi au je hatazidi, mtondo huu pia Yesu aliutumia katika sehemu nyingine za mafundisho yake au maneno yake mfano

Luka 23:31  Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

unaona kwa msingi huo ujengaji wa hoja alioutumia Yesu hapo unafanana na ule ujengaji wa hoja alioufanya katika mfano wa maua ya kondeni, ikiwa wanautendea mti mbichi hivi, itakuwaje kwa mti mkavu?, yaani kama mwenye haki anatendewa mambo kama haya itakuwaje kwa mtu asiye haki? kwa hiyo hapa yesu tena alitumia kanuni ya ufundishaji iliyoitwa KAL VAHOMER ambayo ilikuwa imeenea wakati huo na ilikuwa ya Muhimu sana Kwa hiyo ilikuwa ni rahisi kwa jamii ya nyakati za karne ya kwanza kuweza kuelewa jambo hili.

Fikirini Maua ya Mashamba!

Kimsingi Yesu Kristo alikuwa anazungumza na kundi la watu wa chini sana waliokuwa masikini na hata kufikia ngazi ya kukosa mahitaji yao ya kila siku kama chakula na mavazi ambayo kimsingi ni mahitaji ya msingi sana ya mwanadamu, Kristo anataka kuwaondoa watu hawa katika mawazo ya kufikiri kuhusu chakula na mavazi na kutaka kuwatia moyo waache kuhofu kuhusu hayo na badakla yake wamtegemee Mungu, kuhofu au kuogopa ni ibada, kama mtu atakuwa anawaza ale nini au avae nini mawazo yake yataelekea katika kuitumikia fedha ili apate mahitaji yake, Yesu anataka tuwe na imani tuisjisumbue, anataka kutujengea uwezo wa kuamini  kwamba Mungu anatujali sana kama maua hayafanyo kazi yoyote na Mungu huyavika na kuyafanya yapendeze sana hata kuliko fahari ya Sulemani, ikiwa Mungu huyavika maua kwa fahari kubwa ingawa kimsingi hayana maisha marefu ukilinganisha na mwanadamu lakini maua hayaogopi na kama Mungu anaweza kuyafanyia hivyo maua hashindi kutufanyia sisi wanadamu mahitaji yetu Maandiko yanatufundisha ya kuwa Mungu anajishughulisha sana na mambo yetu

1Petro 5:6-7 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. 

Kimsingi umasikini hauko katika chakula mavazi tu Yesu alizungumzia hayo kutokana na hadhiranya watu wa wakati ule ambao wengi walikuwa masikini, inawezekana katika jamii ya leo tukawa chakula na nguo kwetu sio jambo la kuhofia lakini watu wanahofia kodi za nyumba, wanahofia ada za shule za watoto, wanahofia mikopo ya chuo, wanahofia marejesho ya vikoba, weanahofia magonjwa na changamoto mbalimbali, wanahofia kupanda kwa bei za bidhaa kama mafuta na vyakula, wanahofia mmomonyoko mkubwa wa maadili, ziko fedhea na mizigo ya aina nyingi sana ambayo inaumiza watu katika maisha haya haya yote tunapoyaleta kwa Mungu wetu ambaye anatujali sisi kuliko anavyojali maua na ndege wa angani uwezekano wa Mungu kukutana na mahitaji yetu na kutuondolea hofu ni mkubwa kuliko hofu yenyewe

Mathayo 11:28-30 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Yesu anataka tuiweke mbali hofu ya aina yoyote katika maisha anataka kutupa Pumziko yeye mwenyewe ameonyesha ya kuwa kuhofia hakuwezi kutuongezea kitu hakuwezi hata kuongeza lisaa limoja la uhai wetu Luka 12:25 “Na yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? unaiona kwa msingi huo maandiko yanatuonyesha ya kuwa tunapoogopa tunapokutana na hofu watakatifu waliotutangulia hata katika hali ngumu na duni na stresses za maisha wao bado  waliweka tumaini lao kwa Mungu

Zaburi 118:5-7 “Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi. Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.”

Kwa msingi huo hatupaswi kuhofia jambo lingione lolote na badala yake tuaxchie kila kitu katika mahitaji yetu kijulikana na Mungu, Mungu anawalisha ndege wa anagali na kuyavisha maua mavazi ya rangi mbalimbali za kupendeza na hayafanyi kazi yoyote wala hayana maisha marefu lakini kama Mungu anaweza kuyajali kiasi kile ni wazi na upana ya kuwa Mungu anatujali sisi kuliko tunavyoweza kufikiri, kwa msingi huo kila amwaminiye Mungu hapaswi kuishi kwa hofu na wasiwasi tumwamini Mungu kwa mahitaji yetu yote ya kiwmili na kiroho naye atashughulika maua hayafanyi kazi lakini afadhali sisis tunafanya kazi na Mungu katika mapenzi yake tukimtegemea na kumuomba atatujibu sawasawa na kuhitaji kwetu kwa mapenzi yake

Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!     

Jumatano, 16 Novemba 2022

Jinsi ya kuwa Adui wa Roho Mtakatifu!


Isaya 63:9-10Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.”


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu wetu ni mwingi wa rehema huruma na neema, Sifa za Mungu wetu kamwe haziwezi kulinganishwa na mwingine awaye yote, Musa alipotaka kumjua Mungu Mungu alijifunua kwake kwa sifa nzuri zenye kuwavutia sana wanadamu zinazoashiria kuwa Mungu ni mwema mno ona

Kutoka 34:6-7 “BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.”  

Unaona tunamwabudu na kumtumikia Mungu mwenye huruma nyingi, mwenye fadhili, na si mwepesi wa Hasira mwingi wa rehema na kweli nani mwenye kuonea watu huruma hii ni sifa kubwa sana ya Mungu aliye baba na muumba kwetu sifa hii na tabia hii ya uungu iko kwa Mungu etu ambaye amejifunua kwetu kama Baba, mwana na Roho Mtakatifu, yeye ni mwingi wa huruma kama maandiko yanenavyo 

Zaburi 145:7-9 “Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu. Wataiimba haki yako. Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, Bwana ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.”

Hata hivyo pamoja na wingi huu wa rehema na neema na huruma za Mungu wetu, ni ukweli ulio wazi kwamba maandiko yanatuonya sana sana sana kutokumkosea ROHO MTAKATIFU Onyo hili limerudiwa tena na tena kama tahadhari kubwa sana katika maandiko ya kwamba katika maisha yetu kama mtunataka kufurahia neema ya Mungu na uwepo wake basi katika ufunuo wa Mungu wetu hasa kuhusiana na ROHO MTAKATIFU tunaonywa sana kutokumfanyia dhambi au kasirani ROHO MTAKATIFU hii maana yake ni nini maana yake mtu anaweza kutengeneza uadui na Roho Mtakatifu na akajikuta yuko matatani.  Katika nafsi hizi tatu kwa mujibu wa mafundisho ya Yesu mwenyewe tunaweza kumkosea Mungu baba na Mwana pia na mlango wa neema ukapatikana lakini tahadhari kubwa inatolewa kuhusu kumkosea ROHO MTAKATIFU.

Mathayo 12:31-32 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.”

Unaona maneno hayo ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye anatuonya sana namna ya kujihadhari ili tusiweze kuwa na uadui na Roho Mtakatifu kwani tunaweza kujikuta katika wakati Mgumu  hii maana yake ni nini maana yake tunaweza kujikuta tunamtenda dhambi Mungu Roho Mtakatifu na akageuka na kuwa adui yetu na kupigana nasi!          

Namna ya kutengeneza uadui na Roho Mtakatifu.

Taasisi nyingi leo zinazomtaja Mungu, na zilizokuwa na nguvu sana duniani zilianza kupoteza umaarufu wake mara baada ya kuanza kupingana na kazi za Roho Mtakatifu na kufanikiwa kutengeneza uadui naye, ni jambo la kusikitisha kwamba katika nchi nyingi za ulaya na ikiwemo Uingereza makanisa mengi sana yaliyokuwa taasisi kubwa yamebakiwa na majengo ambayo mengine yamenunuliwa na kuwa misikiti au kuwa maduka au majumba ya makumbusho na pia kuwa makasino lakini ukichunguza kwa kina chanzo kikubwa cha kufikia hatua hiyo ni kupoteza uamsho na kufikia ngazi ya kufanikiwa kuwa na uadui na Roho Mtakatifu! Uwepo wa Roho Mtakatifu una nafasi kubwa sana katika maisha yetu na mafanikio yetu ya kimwili na kiroho hata hivyo hatuna budi kuzingatia tahadhari zilizotolewa na Mungu kwa neno lake kuhusu Mungu Roho Mtakatifu ni namna gani tunaweza kutengeneza uadui na Roho Mtakatifu

1.       Angalieni msimtie Kasirani -  kumtia kasirani maana yake ni kumuudhi kwa sababu ya manunguniko na malalamiko na kutokuamini, wakati tunapokuwa tumeokolewa hatuna budi kufahamu kuwa ni kazi ya roho Mtakatifu kutuongoza na kutusaidia yeye ni msaada ulio karibu sana anafanya kazi katika kiwango kile kile ambacho angekifanya Kristo akiwa katikati yetu yeye huitwa msaidizi Yohana 14:16 – 18 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.”

 

Unaona Mpango wake Mungu ni kuwa pamoja nasi, Pamoja na kuwa Yesu alipaa Mbinguni lakini hakutuacha yatima ametuletea Msaidizi yaani Roho Wake mtakatifu ili akae nasi ni rafiki wa karibu na ni kiongozi wetu hivyo hatupaswi kumtia kasirani ona

 

Kutoka 23:20-22Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.”

 

Ni muhimu kufahamu kuwa malaika anayetajwa hapa na Bwana kwamba atawaongoza wana wa Israel na kuwa wajihadhari wasimtie Kasirani ni ROHO MTAKATIFU Yeye katika agano la kale anaitwa malaika wa uso wake kama unavyoweza kuona katika andiko la Msingi

 

Isaya 63:9-10Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.”

 

Unaweza kuona maonyo ya kibiblia kwamba tunaweza kumkosea ROHO MTAKATIFU kwa kumtia kasirani na hatimaye akageuka na kuwa adui na kupigana nasi, haya yalifanywa na wana wa Israel walipookolewa kutoka Misri lakini njiani mara kwa mara walimkosea Mungu Roho Mtakatifu kwa kufanya maovu ambayo yaliwafanya waangamizwe jangwani  ona

  
1Wakoritho 10:1-11Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani

 

Unaona? Wana wa Israel kwa rehema na huruma za Mungu waliokolewa kutoka utumwani Misri kwa nia nzuri ya upendo wa Mungu ili kusudi awapeleke katika nchi ya mkanaani akawape raha na maziwa na asali na kila walichokitamani, hata hivyo katika namna ya kushangaza sana utaweza kuona walimuhuzunisha Mungu na kumtia kasirani Roho wa Mungu na hatimaye wakaangamizwa jangwani.

 

Ni kwa sababu ya somo hili Paulo mtume anasema mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano ili kutuonya sisi tuliofikiwa na miisho ya zamani hizi yaani zamani hizi ni zama hizi ambapo ROHO MTAKATIFU Yuko kazini hapa duniani akifanya kazi pamoja nasi, kwa msingi huo basi kanisa au taasisi yoyote inayomtaja Mungu kama haitajali kutunza uwepo wa ROHO MTAKATIFU kwa heshima kubwa ni ukweli ulio wazi kuwa tutakuwa na uadui naye!

 

2.       Wala Msimuhuzunishe - Namna nyingine ambayo tunaweza kujenga uadui na Roho Mtakatifu ni Pamoja na kumuhuzunisha ona Waefeso 4:30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.”  Kumuhuzunisha ROHO MTAKATIFU huambatana na kumkasirisha  neno la kiyunani linalotumika kuhusiana na kumuhuzunisha ROHO MTAKATIFU Katika kiyunani ni LYPEITE Kwa kiingereza ni Cause Grief Ambalo maana yake ni kumsababishia MAJONZI hili ni wimbi zito la masikitiko na kukasirishwa kunakotokana na kupingwa kunakosababishwa na ugumu wa mioyo ya watu kwa makusudi jambo la namna hii lilimtokea Masihi pale watu walipiokuwa wanataka asiponye mtu kwa sababu ni siku ya sabato Marko 3:4-5 “Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza. Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.”        Katika taasisi mbalimbali na madhehebu mbalimbali ya Kikristo wakati mwingine wamekuweko watu ambao kwa makusudi kabisa wanapinga na kazi za Roho Mtakatifu katika taasisi au maisha ya mtu, wako watu wanaweza kupinga maombi, wanaweza kupinga uponyaji au hata ustawi wa tabia njema iliyoko ndani ya Mtu ambayo imetokana na kazi za ROHO MTAKATIFU shughuli kama hizo zinamuhuzunisha sana Mungu Pale katika Marko 5:6 ukisoma utaona viongozi wa dini sio tu walichukizwa na Yesu kuponya siku ya sabato lakini vilevile walikuwa na makusudi ya kumuangamiza! Wako watu pia wanaopinga na mahubiri, au muhubiri au kazi zinazofanywa na wahubiri wa Injili,  nimefanya kazi ya kichungaji miaka 12, na kufundisha vyo vya Biblia miaka 12 na pia kuongoza taasisi ya kielimu kwa shule ya seminari miaka 10 na mara kadhaa nimeona watu wakishindana na ROHO MTAKATIFU wazi wazi na wakati mwingine nilidhani wananichukia mimi jambo ambalo nimeshalizoea lakini kumbe niligundua baadaye kuwa kazi ile ambayo Roho wa Mungu ameiweka ndani yangu ilikuwa inapingwa vikali, sio hivyo tu mahali popote ambako watu wanaishi kwa MANENO MAOVU, UCHUNGU, GHADHABU, HASIRA KELELE NA MATUKANO NA UBAYA WA KILA NAMNA  Hayo nayo hayo nayo ni sababu kubwa ya kusababisha MAJONZI kwa ROHO MTAKATIFU hili ndio tukio lililopelekea Paulo Mtume kuwataka Kanisa la Efeso wawe mbali na maswala ya aina hiyo kwani ndiyo yanayopelekea kuhuzunika kwa Majonzi kwa ROHO MTAKATIFU jambo ambalo litapelekea aliache kanisa, aondoke au asifanye kazi tena na hapo uadui nay eye huwa unaweza kufikia kikomo. Waefeso 4:29-31 “Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia. Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;”

 

3.       Msimzimishe Roho1Wathesalonike 5:19 “Msimzimishe Roho;” Ni muhimu kukumbuka kuwa  katika kumueleze ROHO MTAKATIFU  moja ya alama zinazotumika keelezea utendaji wa Roho Mtakatifu ni pamoja na MOTO, wote tunaweza kuwa na ufahamu juu ya umuhimu wa Moto katika maisha ya Mwanadamu, tunajua kuwa maendeleo makubwa ya mwanadamu yalichangiwa pia na ugunduzi wa Moto, Roho wa Krito vilevile hufanya kazi kama Moto katika maisha ya waaminio

 

Isaya 4:3-4 “Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza.”

 

Unaona maandiko yanatufundisha wazi kuwa utendaji wa Roho Mtakatifu ni kama mfano wa Moto hufanya kazi ya kuichoma mioyo yetu na kuteketeza yasiyofaa ndani yetu ili tuweze kuwa watakatifu, upendo wa Mungu huwaka ndani yetu, upendo wa kuhubiri, kuabudukumtumikia Mungu kwa uaminifu, kufanya maombi, kuwasaidia wengine moto huo wa kihuduma ndani yetu huwashwa na ROHO MTAKATIFU tangu anapokuja ndani yetu ona Matendo 2:3-4 “Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.” 

 

Unaona hii ni Ishara ya Roho wa Mungu kuwasha moto wa uamsho ndani yetu ili tumpende Mungu na wenzetu, kwa msingi huo hatupasw kamwe kuuzima moto huo, Neno linalotumika katika maneno ya kiyunani kuhusu KUZIMA  ni neno SBENNUMI – “sben-noo-mee” kwa kiingereza to extinguish  ambalo maana yake ni tendo endelevu la kuzima moto, msimzimishe ROHO kanisa ua taasisi au mtu binafsi anaweza kuendelea kuuzimisha moto wa Roho Mtakatifu kwa kukosa furaha, kuacha kuomba, kuacha kushukuru, kupinga unabii, kupinga mapenzi ya Mungu, kupinga mambo mema na kutokujitenga na uovu au ubaya wa kila namna haya ndio mojawapo ya maswala yanayochangia kumzimisha ROHO WA BWANA ona 1Wathesalonike 5:14-22 “Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote. Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote. Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. Msimzimishe Roho; msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; jitengeni na ubaya wa kila namna.”        Unaona kwa mujibu wa maelezo na maonyo ya Mtume Paulo matukio yote hayo yakifanyika kwa waamini na taasisi za kidini tunamfanya Roho wa Mungu auzunike na kwa sababu hiyo tunatengeneza uadui na Mungu nay eye atatutapika na matokeo yake taasisi au watu binafsi wanapoa ona

 

Ufunuo 3:13-22 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa

 

Unaona kwa msingi huo kama watu watauzima moto wa Roho kwaajili ya sababu mbalimbali tulizojifunza hapo juu ni ahadi ya ROHO MTAKATIFU mwenyewe ya kuwa watatutapika, yeye hapenzi watu vuguvugu, yeye anatutaka tutubu na kama hatutafanya hivyo hakuna kingine tunachoweza kuzawadiwa bali tutapoteza Rehema na neema yake na kujikuta tumeunda uadui na Roho Mtakatifu. Nisikilize Mungu habadiliki, tabia ya Mungu ni ileile sisi wanadamu hubadilika Kabla ya gharika ya wakati wa Nuhu iliyofutilia mbali wanadamu wengi na kumuacha Nuhu na familia yake wanadamu walitenda maovu, walijaa uovu waliacha kumsikiliza ROHO MTAKATIFU kwa kufanya uovu na kuwaza kufanya mabaya kila wakati hivyo walimuhuzunisha na walimzimisha pia na walishindana  naye nadhani ni pale alipokuwa akiwashauri kuwa wema na wao wakapuuzia  Mwanzo 6:3-6BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu, wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo” unaona madhara watu waliposhinda ana Roho ya Mungu, miaka ya kuishi mwanadamu ilipunguzwa, Mungu aklijuta kumuumba mwanadamu, rehema zake na huruma zake zikafikia mpaka akahuzunika akawafuta wanadamu, watu wanaopinga ana mapenzi ya Mungu, taasisi zinazopigana na kusudi la Mungu, na watu wenye tabia endelevu ya kushinda ana kazi ya Mungu kupitia roho Mtakatifu watapunguziwa maisha, watafutwa kwa sababu wameamua kuwa adui wa Mungu

 

4.       Msimpinge Roho Mtakatifu – Matendo 7:51-52 “Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo. Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua;”            Namna nyingine ya kuwa adui wa Roho Mtakatifu ni kumpinga ni neno gumu na lenye kusikitisha sana kadiri nilipokuwa naendelea kujifunza somo hili nilikuwa nawaza maoyoni hivi somo hili ni sehemu ya INJILI kweli au kuwatisha watu? Lakini Roho Mtakatifu akanikumbusha maeno ya BWANA YESU na haya ya STEFANO kwa habari ya ROHO MTAKATIFU maonyo ya kucheza naye hayana utani wala mchezo kabisa, hakuna mzaha linapokuja swala la kucheza na Roho Mtakatifu lugha ya kimaandiko ni kali na ngumu na haina mzaha! Kumpinga Roho Mtakatifu ni dhambi nyingine ambayo wanadamu wanaweza kumtendea Mungu aidha walioamini au hata wasioamini maadamu tu utaingia kwenye anga zake na kumpinga madhara yake yatakuhusu, Kumpinga Roho Mtakatifu katika lugha ya kiyunani linatumika neno ANTIPIPTO ambalo kiingereza chake ni resist au oppose kwa kuwa Roho Mtakatifu hawezi kuonekana kwa macho ya kibinadamu

 

Yohana 14:16-17 “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”          

 

Sasa unawezaje kumpinga yeye usiyemuona kwa macho, ukweli ni wazi kuwa kumpinga ROHO MTAKATIFU Huambatana na kuwapinga watumishi wake, wale wanaobeba ujumbe wake NI YUPI KATIKA MANABII AMBAYE BABA ZENU HAWAKUMWUUDHI Wayahudi walipinga ana Musa, walipinga ana manabii, walimpinga yesu Kristo waliwapimga mitume na hata kuwaua walipinga maneno yale na ujumbe ule ambao waliubeba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu leo anaweza kugeuka adui na akapigana nasi kama tu tunazuia kazi mzake na kupinga ujumbe wake huku tukiwadharau na kuwapiga na kuwapinga watumishi wake na kushindana na kazi yake hiki ndicho ambacho mafarisayo na Masadukayo walikifanya na wayahudi wengi wenye wivu walishindana sana na wajumbe wa injili hata wakitaka wasihubiri wala kumtaja Yesu ona

 

Matendo 4:1-10 “Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu.Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni. Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu, na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu.Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya? Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa, jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.”     

 

Matendo 5:14-39 “walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake; hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao. Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa. Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu, wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza; lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu. Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete. Hata watumishi walipofika hawakuwaona gerezani, wakarudi wakatoa habari, wakisema, Gereza tumeikuta imefungwa salama, nao walinzi wamesimama mbele ya mlango; lakini tulipoufungua hatukukuta mtu ndani.  Basi jemadari wa hekalu na wakuu wa makuhani waliposikia haya, wakaingiwa na shaka kwa ajili yao, litakuwaje jambo hilo. Mtu mmoja akaja akawapasha habari ya kwamba, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu. Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe. Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza, akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu. Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi. Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio.Wao waliposikia wakachomwa mioyo yao; wakafanya shauri kuwaua. Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo kidogo, akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda watu hawa. Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu. Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika. Basi sasa nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.”

 

Wakati wote unaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume ambacho kimsingi ndio tunasoma kwa kina na mapana na marefu utendaji wa Roho wa Mungu ndio utaweza kuona jinsi watu kadha wa kadhaa walivyoweza kupinga ana kazi ya Mungu na wajumbe wa ile kazi na hiki ndicho anachokikemea STEFANO na kuwaonya wayahudi kwamba waache kumpinga ROHO MTAKATIFU   ikiwa ni pamoja na kushupaza shingo zao. Kumpinga Roho Mtakatifu na kazi zake au watumishi wake leo limekuwa moja wapo ya Dhambi inayopelekea Mungu kuwaacha watu wake Roho Mtakatifu leo anapingwa sana na waliokoka na wasiookoka yako mashirika leo na wako watu leo wamefilisika kiroho na wanafanya kila jitihana waweze kuinuka tena lakini inashindikana sababu kubwa ni kupinga ana Roho wa Mungu, watu wanapinga uamsho, wanapinga ujazo wa Roho, wanapinga miujiza, wanapinga wajumbe wa Mungu, wanahakikisha kuwa mnakuwa na usumbufu na mnakosa utulivu ili mradi tu kuharibu hali ya kiroho na injili. Ukitaka kuwa adui wa ROHO MTAKATIFU hakikisha kuwa unapinga anaye, yeye aliye na sikio na alisikie neno hili.

 

5.       Usimwambie uongo Roho Mtakatifu - Matendo 5:3-5 “Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.”  Kumwambia uongo ROHO MTAKATIFU  ni mojawapo ya dhambi mbaya ambayo nyakati za kanisa la kwanza ilisababisha watu kufa mara moja, lakini hata leo watu wanaweza kutengeneza uadui na ROHO WA MUNGU kwa mtindo unaofanana na Anania na Safira kimsingi watu hawa walifanya unafiki, walikuwa wakiigiza jambo ambalo sio sahihi mbele za Mungu kwanza tuichambue asili ya dhambi yao

 

Kulikuwa na mpango wa watu kuishi kwa umoja na kwa pamoja na kwaajili ya kanisa watu wengi walikuwa wakiuza mali zao na kukabidhi kwa mitume kwa kusudi la kuwasaidia wengine moja ya watu waliofanya hayo na kupata umaarufu na sifa kubwa katika kanisa ni Barnabas ona

 

Matendo 4:34-37 “Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji. Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.”

 

Nadhani ni kutokana na watu kadhaa kusifiwa na mitume kwa moyo wao wa utoaji tayari Anania na Safira nao walipata msukumo wa kufanya hivyo lakini nadhani wakiwa na nia ya kujipatia sifa tu, kutoa mali zako na kuziuza kwaajili ya utoaji wa kanisa halikuwa tatizo, na hata kuzuia sehemu ya fedha kwaajili ya familia haikuwa tatizo, kama Petro Mtume alivyohoji

 

Matendo 5:4 “Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.”               

 

Swala kubwa lilikuwa kumdanganya ROHO MTAKATIFU na kumjaribu, Shetani alikuwa ameshamjaza Anania na mkewe nia ovu nia yao ilikuwa ni kutaka sifa, kutoka katika jamii ya kanisa, wao waliwaambia mitume kuwa wametoa vyote kumbe kuna ambacho walijifichia, walikuwa wakijaribu kuwadanganya watu hasa wa jamii ya kanisa kumbe kiuhalisia walikuwa wakimdanganya ROHO MTAKATIFU ona

 

Matendo 5:3-5 “Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.”

 

Mungu alikusudia kanisa lake liwe kama mfano wake yeye aliyetuumba ni agizo la kibiblia kwamba tuuvue kabisa utu wa kale na kuacha kabisa kuambiana uongo angalia Wakolosai 3:9-10 “Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.”

 

Leo hii sio ajabu watu kuambiana uongo, kumekuwa na watu waogo na wadanganyaji kuliko nyakati za kanisa la Kwanza, kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanafiki na wanaotaka sifa na kujijengea jina katika jamii kupitia umaarufu feki, vyovyote iwavyo kusema uongo ni ishara iliyo wazi kuwa Ibulisi ambaye ni baba wa uongo anatawala ona

 

Yohana 8:44 “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.”

 

Kwa misingi hii unaweza kuona ya kuwa kama unadanganya watu na kutaka sifa na kudanganya watumishi wa Mungu ni wazi kuwa unatengeneza uadui na ROHO MTAKATIFU jambo ambalo litakugharimu.

 

6.       Kumfanyia Jeuri Roho wa Neema – Waebrania 10:26-29 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?Nyakati za agano la kale mtu aliyeivunja sharia ya Musa aliuawa pasipo huruma

 

Hesabu 15:30-35 “Lakini mtu afanyaye neno lo lote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake. Kwa sababu amelidharau neno la Bwana, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake. Kisha wakati huo wana wa Israeli walipokuwako jangwani, wakamwona mtu mmoja akikusanya kuni siku ya Sabato. Hao waliomwona akikusanya kuni wakamleta kwa Musa na Haruni, na kwa mkutano wote. Nao wakamweka kifungoni, maana, lilikuwa halijasemwa atakalotendwa. Bwana akamwambia Musa, Mtu huyo lazima atauawa; mkutano wote watampiga kwa mawe huko nje ya marago.”

 

Agano jipya ni agano lililobora zaidi ya lile la agano la kale kama mtu angeliweza kuuawa kwaajili ya kuvunja sharia katika agano la kale ni zaidi sana mtu anapoivunja sharia ya kifalme katika agano jipya kama asemavyo mwandishi wa kitabu cha Waebrania, Mwandishi anatoa maonyo makali sana kuhusiana na ukengeufu, kurudi nyuma na kumkana Yesu Kristo jambo ambalo ni kinyume na utendaji mzima wa Roho Mtakatifu ambaye hufanya kazi ya kuwapa watu neema ili watubu na kumuamini Yesu kwa msingi huo mtu anapoifanya shingo yake kuwa ngumu na kutukana maswala kadhaa ya wokovu na kuukana anajiweka kwenye uadui na Roho wa Kristo nani sawa kabisa na kumfanyia Jeuri ROHO WA NEEMA kwa msingi huo kufanya dhambi kusudi, kunaleta hukumu yenye kutisha kwa sababu kufanya hivyo ni kumfanyia jeuri yeye.

 

7.       Kumkufuru Roho Mtakatifu. – Kilele cha juu zaidi katika dhambi zinazoweza kumfanya mtu kuwa na uadui na Roho Mtakatifu ni kumkufuru, neno Kukufuru katika lugha ya Kiyunani linatumika neno Blasphemia – sawa na neno Blasyphemy katika kiingereza ambalo maana yake ni kusema maneno mabaya au kuzungumza vibaya kuhusu Mungu, jambo hili limezungumzwa na Bwana wetu Yesu Kristo Mwenyewe

 

Mathayo 12:31-32 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.”

 

Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ndio dhambi pekee ambayo haina msamaha kwa mujibu wa maelekezo ya Yesu kristo, na ndio maana utaweza kuona kumekuweko na maonyo ya kutosha kuhusu kuacha kutenda dhambi kinyume na mapenzi ya ROHO MTAKATIFU,  ukimkufuru Roho umefanya dhambi ya milele, kukufuru ni hali ya kuzungumza mabaya, au kutukana na kuudhi maswala yote Matakatifu yanayohusiana na Mungu Yesu alitoa maonyio ya namna hii katika mazingira ambayo mafarisayo walikuwa wanapinga kazi zote za Mungu alizokuwa akizifanya hata kufikia ngazi ya kutukana na kusema ya kuwa kazi hizo za kiungu zinafanywa na shetani kupoitia Yesu ona

Mathayo 12:22-32 “Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.  Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo. Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu. Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake. Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya. Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

 

Matendo na maneno yote anayosemewa na kutendewa Roho Mtakatifu kilele chake kinakamilika katika kumkufuru na hivyo kila wakati inapotokea anahuzunishwa, anazimishwa, anaongopewa, anapingwa, anafanyiwa jeuri, anafanyiwa kasirani kielele chake ni kuondoka, kuacha, kutokujishughulisha na ninyi tena na kutokusababisha moyo wa toba utokee na hatimaye kusababisha kuhesabika kana kwamba umekufuruau umemkufuru, Ndio maana leo tunaweza kuiona watu wengi, makanisa mengi na taasisi nyingi zimechwa na ROHO WA BWANA  kwa sababu hawakuzingatia maswala kadhaa yanayimuhuzunisha Mungu ROHO MTAKATIFU  na kumfikisha katika hatua ya kuondoka na kwenda mbali nasi.

Hitimisho:

Kuondoka kwa Roho Mtakatifu katika maisha yetu sio tu kunatutengenezea uadui naye lakini inshara ya kuondoka kwa utukufu wa Mungu, mar azote maandiko yameeleza kuwa wanadamu wamepungukiwa na utukufu wa Mungu mara baada ya kutenda dhambi Warumi 3:23  kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;” Utukufu wa Mungu unakuwepo kwetu kwa ukamilifu wakati ambapo Roho wa Mungu akiwa hai ndani yetu, akiwa anatenda kazi akiwa anatuongoza, ikiwa tunamsikiliza, lakini tunaelezwa kuwa tunapomuasi anageuka anakuwa adui anapigigana nasi, kwa kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu ieleweke wazi kuwa nafsi hii katika utatu wa Mungu inapokasirishwa na kufikia hatua ya kupigana nasi ujue hakuna mwamuzi tena

 

1Samuel 2:22-25. “Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania. Akawaambia, Mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote. Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa Bwana. Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu Bwana amekusudia kuwaua.”  

 

Inapofikia ngazi Mungu mwenye rehema na neema nyingi mwingi wa huruma na asiye mwepesi wa Hasira anafikia ngazi ya kumuua mtu ujue jambo hilo limekuwa machukizo makubwa kwa Mungu wetu, unapokuwa na uadui na Mungu kinachofuata ni kifo na wakati huo huo Mungu anaweza kuamua kukuacha na kuondoa utukufu wake hakuna jambo baya duniani kama kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Israel walipokuwa wamemtenda dhambi ukweli ni kuwa utukufu wa Mungu ulikuwa ukiondoa hatua kwa hatua na hatimaye ukaenda katika inchi ya mbali ona katika kitabu cha Ezekiel uwepo wa Mungu ulikuwa ukiondoka taratibu kutoka katika patakatifu hata kwenye kizingiti, kutoka kizingitini hata ukutani, kutoka ukutani hata mlimani na kutoka mlimani hata ukaldayo katika nchi ya utumwa

Ezekiel 10: 4. “Utukufu wa BWANA ukapaa kutoka kwa kerubi yule, ukasimama juu ya kizingiti cha nyumba; nayo nyumba ikajazwa na lile wingu, na ua ulikuwa umejaa mwangaza wa utukufu wa BWANA.,”

Ezekiel 10:18-19. “Kisha huo utukufu wa BWANA ukatoka pale juu ya kizingiti cha nyumba, ukasimama juu ya makerubi.Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu, hapo walipotoka nje, nayo magurudumu yakawa kando yao; wakasimama mahali pa kuingilia pa mlango wa upande wa mashariki wa nyumba ya BWANA; na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.”                

Ezekiel 11:23-25. “Utukufu wa BWANA ukapaa juu toka katikati ya mji, ukasimama juu ya mlima wa upande wa mashariki wa mji. Na roho hiyo ikaniinua, ikanichukua katika maono, kwa nguvu za roho ya Mungu, hata Ukaldayo, kwa watu wale wa uhamisho. Basi maono niliyoyaona yakaniacha. Ndipo nikawaambia watu wa uhamisho habari ya mambo yote aliyonionyesha BWANA.” 

Kadiri watu wa Mungu wanapofanya machukizo ya aina mbalimbali, Mungu huupunguza utukufu wake na kuondoka kidogo kidogo utukufu wa Mungu ni sihara ya uwepo wa Mungu ni uwepo wa Roho wake Mtakatifu, Israel walipotenda ya kuchukiza uwepo huo uliondoka na kwenda utumwani Babeli na ndipo sa unapoweza kuona watu waliokuwa utumwani walikuwa na nguvu na uwezo mkubwa sana wa Kiroho na Mungu alitukuzwa lakini Israel panyewe pakabaki ukiwa, Mtu wa Mungu wewe ndio hekalu la Mungu je utukufu wa Mungu umeondoka na kufikia ngazi gani kama utukufu umekuacha na kwenda Babeli huna budi kulia na kutubu, Leo hii mtakapoisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa Migumu. Chunga sana hakuna jambo baya duniani kama kutengwa mbali na uso wa Mungu hakuna jambo linatisha duniani kama kumuasi Roho Mtakatifu na kumuacha akawa adui yetu na kupoigana nasi Bwana ampe neema kila mmoja wetu asiwe adui wa ROHO MTAKATIFU KATIKA JINA LA YESU AMEN.

Na. Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima.      



Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu!


Luka 16: 9 - 12Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele. Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe? Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.


Utangulizi:

Mojawapo ya kifungu kigumu katika tafasiri za mafundisho ya Yesu ni pamoja na maneno haya ambayo Yesu aliyasema kama sehemu ya Hitimisho ya mfano tajiri na wakili wake, katika Luka 16:1-8 ambako kimsingi Yesu Kristo alikuwa anatufundisha wazi namna ya kutumia fedha na mali tulizopewa na Mungu na ujuzi ya kuwa hatuna tunachomiliki duniani, na kuwa tunwajibika namna tunavyotumia mali na fedha na kwamba tutatoa hesabu ya kila alichotupa Mungu. Baada ya fundisho hilo Muhimu ndipo sa Yesu alianza kuweka mikazo ya maneno haya tunayojifunza leo JIFANYIENI RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU! Kimsingi Yesu alikuwa anafundisha namna ya kujipatia utajiri wa kweli. Yesu qanawataka wanafunzi wake kutumia fedha na mali za ulimwengu huu walizonazo kujipatia thawabu za kudumu katika ufalme wa Mungu. Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

Ø  Tafasiri ya Mali, fedha, Utajiri na udhalimu wakati wa Yesu Mst9-11

Ø  Jifanyieni rafiki kwa mali ya Udhalimu Msta 9-12

Ø  Jinsi ya kumtumikia Mungu na Mali Mst 13

Tafasiri ya Mali, fedha, Utajiri na udhalimu wakati wa Yesu (Mst9)

Luka 16:9-11 “Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.  Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.  Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli?”

Ni muhimu kufahamu kuwa wakati wa Yesu Kristo katika mwili Duniani falsafa kuhusu Mali utajiri na fedha ilikuwa na mitazamo mikubwa mwiwili, hasa katika jamii ya mafarisayo na watu wa ulimwengu wa wakati ule Katika mtazamo wa kwanza wa Mafarisayo hasa katika lugha ya KIARAMU, kuwa na Mali, fedha na utajiri kulihusishwa moja kwa moja na dhuluma (UDHALIMU). Kwa kiyunani ni “ADIKOS”- Wicked, treacherous, unjust au unrighteousness,  Matajiri walikuwa wanafikiriwa kuwa ni watu dhalimu na kuwa walivyonavyo wamevipata kwa kudhulumu au kwa njia zisizofaa kwa hiyo walivipata kwa kufanya dhambi, kwa njia za uovu, kudhulumu watu  kwa hila, au isivyo sawasawa na pia walivitumia kwa anasa na ubinafsi mkubwa ona 

Yakobo 5:1-6 “Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.”

Kwa hiyo fedha na mali na utajiri ulifikiriwa na kuhusishwa na choyo na dhambi katika mtazamo wa kwanza, lakini vilevile katika mtazamo mwingine au falsafa ya pili fedha ilifikiriwa kuwa ni Baraka kutoka kwa Mungu kama mmiliki alikuwa amezipata kwa haki huku akiwa anamcha Mungu,

Marko 10:17-23 “Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako. Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu. Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!

Hata hivyo Matajiri wote wale waliofikiriwa ni wadhuluma na wale wa haki wote walikuwa na matatizo wote walikuwa wanakabiliwa na choyo na ubinafsi, na hivyo Yesu yeye alizuiona fedha mali na utajiri wa dunia hii kama havitatumika kwa usahihi madamu ni mali za duniani zote aliziita mali za udhalimu, kwa nini kwa sababu haziwezi kuwapa wanadamu manufaa ya kudumu katika ulimwengu wa ufalme wa Mungu.

Jifanyieni rafiki kwa mali ya Udhalimu Msta 9-12

Kama tulivyojifunza hapo awali ya kuwa Yesu aliona matumizi yote ya fedha kwa watu wa dunia hii bila kujali mali zao wamezipataje mali zao zingeliweza kuwapa manufaa ya kudumu kama watakosa akili na ufahamu wa kutosa katika kuzitumia, akiendelea kukazia mfano wa wakili dhalimu alioutoa katika Luka 16:1-8 Kwamba pamoja na kuwa wakili yule alikuwa afukuzwe kazi, alikumbuka kuwa kuna maisha baaya ya kufukuzwa kazi na hivyo alikumbuka kujiandalia marafiki kwa mali yake ya udhalimu ilia je kunufaika baadaye, aidha matajiri wa dunia hii vilevile  wakati ule waliweza kutumia fedha kujipatia marafiki na hata kujiongezea umaarufu duniani na ilikuwa rahisi kukubalika kwa sababu ya uwezo mkubwa wa kifedha waliokua nao

Mfano hata leo kama utahitaji kugombea ubunge na vyeo vinginevyo vya kikampeni, utaweza kuona kwamba ni lazima uwe na fedha za kutosha kuweza kuongeza ushawishi kujipatia nafasi uitakayo wazo hili hili alilokuwa nalowakili dhalimu kuhusu kesho yake lingeweza vilevile kutumiwa na wanafunzi wa Yesu kuwa na ujuzi na hekima na akili ya kujitengenezea maisha ya baadaye kwa kuwekeza katika Mungu, tunaweza kutumia fedha mali na utajiri  kwa makusudi mema, tunaweza kuzitumia mali fedha  na utajiri wao (Kwa Mtazamo wa Kiaramu Mali ya Udhalimu) kwa lengo zuri la kuujenga ufalme wa Mungu, badala ya kutumia fedha na mali na utajiri wetu kujifurahisha, kwa choyo na ubinafsi, tunaweza kuitumia kujijengea jina kwa kuwekeza kwa Mungu na kuwatendea mema wengine jambo litakalotufanya tuwe matajiri katika kazi njema kwa msingi huo   Agizo hili la Kristo linaweza kutafasiriwa sambamba na,

1Timotheo 6:17-18 “Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;”  

kwa hiyo kama hatutakuwa waaminifu kuitumia mali, fedha na utajiri huu wa duniani (Wa Kidhalimu) kwa Mungu wetu, Mungu naye hatatatutumia au kutuamini katika mambo Halisi ya kweli ya ufalme wa Mbinguni, huko tutakuwa na hazina isiyoharibika,  Kimsingi Yesu hakuwa anamaanisha kuwa na fedha ni jambo baya wala hakuwa anatia moyo kuwa watu wajitafutie fedha kwa nia mbaya au kwa njia zisizofaa, lakini kama waili yule muovu alikuwa na uwezo wa kufikiri kuhusu maswala yajayo kwanini matajiri wa kawaida wawe wachoyo  na kushindwa kuutumia utajiri wao ambao kimsingi utawanufaisha tu hapa duniani kisha wasahau kujiwekeza katika ufalme wa Mbinguni. Aidha tunaweza kuzitumia fedha zetu sio kwaajili ya kutafuta umaarufu lakini kuwasaidia wengine wenye uhitaji jambo ambalo pia linatupa thawabu Mbinguni, Mungu anapotumilikisha fedha mali na utajiri maana yake ametuamini kuwa tunaweza kutunza kwaajili ya wote na sio kwaajili yetu, hivuo kila Mkristo anapaswa kuwa mwaminifu katika kutumia rasilimali ambazo Mungu ametupa kwa faida ya ufalme wake!

“Luka 6:11 Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu (mali fedha na utajiri wa Duniani), ni nani atakayewapa amana mali ya kweli (ya ufalme wa Mungu, na umilele)”?

Jinsi ya kumtumikia Mungu na Mali Mst 13

Kimsingi Bwana wetu Yesu Kristo anauona mlango ni mdogo sana kwa wenye utajiri kuingia katika ufalme wa Mungu kwa sababu ya ubinafsi na choyo, Wakristo ni lazima waende mbele zaidi na kujifunza kumpa Mungu kipaumbele kikubwa zaidi na jamii,  Mungu anapokuwa ametubarikia wingi wa mali, fedha na utajiri vilevile anataka tuvutumie kwa utkufu wake na kumuabudu yeye 

Kutoka 10:8-11 “Musa na Haruni wakaletwa tena kwa Farao; naye akawaambia, Nendeni, mkamtumikie BWANA, Mungu wenu; lakini ni kina nani watakaokwenda? Musa akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda na kondoo zetu na ng'ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia BWANA sikukuu. Lakini akawaambia, Ehe, BWANA na awe pamoja nanyi, kama nitakavyowapa ruhusa kwenda zenu pamoja na watoto wenu; angalieni, kwa kuwa pana uovu huko mbele yenu. Sivyo; endeni ninyi mlio watu wazima, mkamtumikie BWANA; kwa kuwa ndilo jambo mtakalo. Nao walifukuzwa usoni pa Farao.”

Mungu anapotuita Kumuabudu yeye na kumfanyia ibada hatuiti nusu  nusu anakuwa ametuita sisi  na kila tulichonacho, kama sisis ni watumishi wake basi kila tunachomiliki ni kwaajili ya utumishi ulioko mbele yetu, sisis ni mawakili tu ambao tumeaminiwa na Mungu,  na tunawezaje kuonyesha imani yetu kwa Mungu ni pamoja na kumuabudu Mungu na kila tunachokitaka! Tunaweza kuonyesha imani yetu kwa Kristo kwa kumtumikia pamoja na mali zetu, katika kila jambo lazima tumpe Mungu kipaumbele na kuonyesha ya kuwa ni yeye anayetawala na wala sio mali zinazotutawala, kutawaliwa na fedha kuliko kutawaliwa na Mungu ni kosa la kiufundi katika maswala ya kiroho, lazima Bwana awe juu ya kila kitu na kila kitu kitiishwe chini yake

Luka 16:13 “Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali

1Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”

Unaona kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza kuwa je ni

1.       Mungu anayemiliki kila kitu katika maisha yake?

2.       Je una moyo wa ukarimu au kuna hali ya choyo katika maisha yako?

3.       Je unatenga fungu la kumtolea Mungu katika maisha yako?

4.       Je unahofu ya kuwa utapungukiwa?

Mafarisayo ambao kwa kweli walikuwa wamekwisha zama katika mtego wa kupenda fedha walijikwaa kwa mafundisho ya Kirsto na kumpuuzia kwa sababu choyo kilikuwa ikmetawala nia zao na mioyo yao ili hali wakati huo huo wakijikinai kuwa ni watumishi wa Haki. ona

Luka 16:14 -15 “Basi Mafarisayo, ambao wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia hayo yote, wakamdhihaki. Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu.”

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!



Akikulazimisha maili moja nenda naye mbili !


Mathayo 5:39-41Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.”


Utangulizi:

Mathayo 5:38-42 ni  mojawapo ya sehemu muhimu sana katika hotuba ya Yesu Kristo ya Mlimani ambapo Yesu anafundisha namna ya kuonyesha muitikio wakati mtu anapokudhalilisha au kukutesa, wakati kanuni za msingi wa agano la kale zilikuwa zinakazia usawa na malipo ya jino kwa jino au jicho kwa jicho zikimaanisha kwamba mtu akikufanyia kosa Fulani alipaswa kulipizwa sawasawa na ukubwa wa kosa hilo, yaani kimahakama mtu apewe adhabu inayolingana na makosa yake, Lakini Kristo anakuja na mtazamo tofauti mno wakati mtu anapotendewa mambo yasiyo ya haki, Yesu anawataka wakristo kuonyesha uvumilivu mkubwa sana bila kulipiza kisasi, badala yake kuwapenda maadui na  hata kuwatendea mema yaliyopitiliza!

Akikulazimisha maili moja nenda naye mbili !

Nyakati za Biblia wakati wa Yesu Kristo, Israel pamoja na mataifa mengine yalikuwa chini ya utawala wa kikoloni wa warumi, Wakoloni wa kirumi hata hivyo kuna wakati hawakuweza kuwatendea haki raia wa kawaida na hasa raia wa kiyahudi, waliwaburuza barabarani na pia kuwalazimisha kubeba mizigo mizito kama watumwa  hali hii ilipelekea wakati mwingine kuamsha gahadhabu na kuchochea watu kutaka kujilipizia kisasi, kitamaduni ilikuwa inawasukuma sana wayahudi kutaka kujilipizia kisasi na kujitangazia uhuru na utawala

Baadhi ya wale waliokuwa wakimfuata Yesu, kwa kuwa walitambua kuwa ndiye Masihi walikuwa na fikra kuwa ataushimamisha ufalme wa Mungu kwa kuuondoa utawala wa Warumi hata hivyo amri ya Yesu Kristo na fundisho lake lilikuwa kinyume na matarajio yao na liliwashangaza sana  yeye aliwafundisha kuwa wakubaliane na mateso yale hata ikiwezekana zaidi ya kile walichokuwa wakifanyiwa, Yesu alisisitiza kuwa wakilazimishwa maili moja na waende nao mbili.

Kimsingi Yesu hakuwa anafundisha wanafunzi wake kuwa dhaifu kama wengi wanavyoweza kudhani, badala yake Yesu alikuwa anamaanisha kuwa hakuna mtu dhaifu duniani, Yesu alikuwa anatufundisha kuwa watu Hodari na wavumilivu kiasi cha kuweza kuvumilia watu waovu na kuwapa maadui zaidi ya kile wanachokitarajia, Kristo hakutaka wakristo washindwe na ubaya badala yake alikuwa akitutaka tuushinde uovu kwa wema

Warumi 12:19-21 “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.”  

Yesu anawataka wafuasi wake watoe zaidi ya kile ambacho ulimwengu unaweza kutoa, Yesu hataki tuwe dhaifu lakini anataka tuwe wavumilivu kwa wanadamu ambao ni wadhaifu sana, wakristo wanapaswa kuwa hodari na wenye nguvu kiasi cha kuzalisha mambo bora wakati wengine wakizalisha uovu, hatuwezi kuwa sawa na wana wa ibilisi, sisi ji lazima mtuwe wakamilifu kama baba yetu wa Mbinguni alivyo mkamilifu,  Ubaya wa watu waovu kamwe haupaswi kuwa sababu ya kuvunjika moyo kwa wakristo na badala yake lazima sisi tuzalishe jamno lililobora ili kuonyesha kuwa wao ni wapuuzi.

Maandiko yanamsifia mtu anayejitawala kuwa bora kuliko shujaa, mtu anayeweza kujizuia nafi yake asikasirike ni mwema sana kuliko hata mtu mwenye uwezo wa kuteka mji, Wakristo waliokomaa kiroho hawasukumwi kamwe na misukumo ya kihisia bali wanakuwa wenye nguvu ndani kwa kuonyesha kuwa wanaweza kujizuia hata pale mtu anapotaka wakasirike

Mithali 16:32 “Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.”

Mtu mwenye ukomavu wa hali ya juu ni yule ambaye anaweza kuwasamehe adui zake na kuwapenda, Daudi ni moja ya Mfano wa watu waliokuwa wanaweza kuushinda ubaya kwa wema hakuwahi kufurahia hata kufa kwa adui zake kabisa   

2Wafalme 19:4-6 “Mfalme akajifunika uso; na mfalme akalia kwa sauti kuu, Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwanangu! Basi Yoabu akaingia nyumbani kwa mfalme, akasema, Wewe leo umefedhehesha nyuso za watumishi wako wote, waliokuokoa leo roho yako, na roho za wanao, na za binti zako, na roho za wakezo, na roho za masuria wako; kwa kuwa unawapenda wakuchukiao, na unawachukia wakupendao. Maana umetangaza leo ya kuwa wakuu na watumishi wako si kitu kwako; maana leo nimetambua hivi; kama Absalomu angaliishi, na sisi sote tungalikufa leo, ingalikuwa vyema machoni pako.”

Luka 6:27-30 “Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.”

Mitume wa Bwana adiha walisisitiza pia fundisho hili la bwana na kuwataka wakristo kutokuwa watu wa kulipa baya kwa baya, wala laumu kwa laumu na wanatakiwa kubariki hata watu wanaowafanyia  maovu kwa kufanya hivi inaashirikia ukomavu mkubwa na unaonyesha kuwa sisi kweli tumekuwa wanafunzi wa Yesu kweli kweli jambo hili linapaleka habari njema kwa maadui wa Ukristo na kuwafanya wamkubali Kristo!

1Petro 3:9 “Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.”

Hitimisho:

Aina hii ya muiikio ndio utakaosababisha watu wauone uzuri wa Mungu hata katika maisha ya wale wanaowashutumu, kuwaonea na kuwatesa, aidha hii itamfanya mtu muovu akome kuutumia uovu wake kukomoa wakristo, kwa hiyo mateso na nia ovu za watu wabaya hazitakuja zishinde nguvu ya Mungu na uwepo wa utendaji nwa Kristo katika maisha yetu siku zote za maisha yetu. Nabii Elisha aliwahi kuitumia njia hii na washamu wakaacha kuwafuatia Israel kwa muda mrefu ona

2 Wafalme 6:19-23 “Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria. Hata walipokwisha kuingia Samaria, Elisha akasema, Bwana wafumbue macho watu hawa, wapate kuona. Bwana akawafumbua macho wakaona; kumbe! Walikuwa katikati ya Samaria. Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige? Akamjibu, Usiwapige; je! Ungetaka kuwapiga watu ambao umewatwaa mateka kwa upanga wako na uta wako? Weka chakula na maji mbele yao, wapate kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao. Basi akawaandalia chakula tele; nao walipokwisha kula na kunywa, akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikosi vya Shamu havikuja tena katika nchi ya Israeli.

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia

 

Mathayo 23:23-28. “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.”



Utangulizi:

Katika Mathayo 23:13-36, kuna mahubiri makali ya maonyo kutoka kwa Yesu Kristo kuelekea kwa mafarisayo na viongozi wa dini waliokuweko katia nyakati hizo, Neno ole ni sawa na onyo la kulaani au kuonya juu ya hukumu kubwa ya Mungu kwa watu ambao maonyo hayo yanaelekezwa kwao,Krito alikemea vikali kwa maneno mazito hata wakati mwingine akitumia neno vipofu na wanafaiki, Sababu kubwa ni kuwa watu hawa walikuwa wakiwashawishi watu wafuate imani zao na matiokeo yake ilikuwa ni kama kuwapeleka Jehanamu, wakikazia katika mafundisho yao maswala yasiyo ya msingi wa Neno la Mungu na kuwaelekeza katika mapokeo ya kibinadamu zaidi, huku wakipuuzia msingi wa sharia ya Mungu ambayo ni ADILI, REHEMA na IMANI

Kwa maana nyingine Kristo alikasirishwa na Jinsi ambavyo viongozi wa kidini walishindwa kuwatafasiria watu kile ambacho sheria ya Mungu inakipa kipaumbele na badala yake wakaanza kukazia sharia za kidini zinazotokana na mapokeo, mikazo hiyo haikuwa dhambi hata hivyo lakini ilikuwa si Muhimu, tabia mbaya waliyokuwa nayo Mafarisayo ilikuwa ni mkazo wa utoaji wa zaka hususani kutoka katika mazao ambao kimsingi ulikuwa ni urithi wa watumishi wa Mungu yaani walawi kwa wakati ule

Hesabu 18:20-24 “ Kisha Bwana akamwambia Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lo lote kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli. Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.  Mwanzo wa sasa wana wa Israeli wasikaribie hema ya kukutania, wasije wakachukua dhambi, nao wakafa. Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi. Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.”

Kumbukumbu la torati 14:24-29 “Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako; ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe. Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.”                       

Unaweza kuona Mafarisayo na viongozi wa dini walikazia sana kuhusiana na vifungu vinavyokazia kuhusu utoaji wa zaka na kwa kweli kutokana na uroho walikazia utoaji wa zaka mpaka ya mnanaa, Bizari na jira kwa faida zao, Mnanaa ni mmea wenye majani madogo madogo ya kijani kwa kiingereza unaitwa Mint mmea huu unatumika kutibu magonjwa mbalimbali kama Aleji, kuvimbiwa, maumivu ya tumbo na kutibu magonjwa mengine kama kisonono, bawasiri na maumivu katika njia ya mkojo, mmea huu ulitumika kama tiba kwa miaka elfu nyingi sana duniani,

Bizari kwa kiingereza Dill ni kiungo cha manjano BINZARI ambacho tutumika kuweka rangi ya mchuzi na kuifanya iwe wa manjano au mwekundu na shughuli nyinmginezo za kimapishi na ladha au harufu nzuri kwenye chakula pia hutumika kama tiba ya magonjwa

Jira kwa kiingereza cummin ni vijijani vyenye vitunda vidogo vidogo sana vya kijana ambavyo vikianikwa huwa na rangi ya kijivu hivi ni viungo ambavyo huchanganywa na viungo vingine na kuleta ladha maalumu katika kama pilau na mchuzi na kadhalika, jira ina uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwepo, kusaidia kupunguza uzito, kuondoa msongo wa mawazo, kuyeyusha mafuta hatarishi mwilini, kisukari, na magonjwa mengineyo. Kwa ujumla vitu hivi vilikuwa vinahusiana na UPONYAJI, UZURI NA UNONO. Mafarisayo walisisitiza sana utoaji wa zaka hata wa vimimea hivi vidogo vidogo kwa mkazo mkubwa sana kwa makusudi tu wakuu wa dini wanufaike na utamu wa vyakula vyao na afya nzuri, Yesu hakuhukumu utoaji wala utoaji wa zaka lakini kuna kitu nyuma ya mkazo wa viongozi wa dini ambacho Kristo alikuwa anakikemea huku akiwakemea kwa kuacha kusisitiza maswala ya msingi na ya muhimu

Mafarisayo waliacha kuweka mkazo katika maswala makubwa ya msingi ya kiroho ambayo yangekuwa na faida kubwa kwa watu kuliko yale ambayo yangekuwa na faida kubwa kwao  waliacha maswala ya ADILI – Maswala ya kuhukumu kwa haki linapokuja swala la Mtu Fulani amekosea, REHEMA – Kushindwa kuwahurumia watu waliokosea na wale wanaohitaji msaada wa kibinadamu au walio kwenye mateso, IMANI -  Biblia ya kiingereza inatumia neno FAITHFULNESS ambalo linahusiana na UAMINIFU

Kuchuja mbu na kumeza ngamia

Wakati mwingine unaweza kudhani kuwa shida hii ilikuwa ya mafarisayo pekee wakati wa Yesu Kristo la hasha hata sasa ziko tabia Fulani zinazoweza kukemewa katika mtindo kama huu wa Masihi, Leo hii pia wako watu wameacha mambo ya msingi na kukazia mambio ya siyio ya msingi, kwa mfano sio vipaya kuhubiri uponyaji na mafanikio kwa vile ni wazi kuwa watu wanahitaji mafanikio na uponyaji na hakuna jambo baya kama umasikini, lakini ni ukweli ulio wazi kuwa injili inahitaji balansi, lazima wahubiri wasisahau kuwa tunapaswa kuhubiri injili kamili, mara kadhaa unaweza kukuta wahubiri wansisitiza juu ya utoaji lakini sababu kubwa ni kwaajili ya mahitaji makubwa waliyo nayo,  na wakati mwingine kwaajili ya ubinafsi na kujinufaisha, tunaweza kuhubiri kuhusu uponyaji lakini tusisahahu kuwa watu wanapaswa pia kuishi maisha matakatifu na kukumbushwa kuhusu toba na kusamehewa dhambi na sio uponyaji pake yake

Zaburi 103:3 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,” unaona wakati tunasisitiza kuhusu Uponyaji ni lazima vile vile tukumbuke kusisitiza toba na msamaha wa dhambi, itajkuwa ni hasara kubwa sana kama mtu ataponywa magonjwa yake yote lakini hajawahi kuambia atubu dhambi au aishi maisha matakatifu, na sio sahihi vilevile kuhubiri mafanikio na afya njema bila kusahau kuwa afya halisi inapaswa kuanzia rohoni

3Yohana 1:3 “Mpenzi naomba ufanikiåe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo

lakini vilevile inaweza kuwa makosa sana kuwahukumu watu kutokana na muonekano wao, au hali yao ya kifedha au cheo chao na kuacha kuweka uthamani wa mtu katika mizani ya kiroho, aidha kumekuweko na upendeleo katika utoaji wa haki, wako watu kwa sababu ya utajiri wao wanaweza kupewa heshima Fulani na hata wakifanya dhambi wanaweza kuhifadhiwa lakini wewe ambaye huna kitu ukadhalilishwa

Yakobo 2:1-5 “Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?

 Unaona watu hawajali umuhimu thamani ya nasfi na roho ambayo ni moja bali wanaangalia muonekano, wako watu ambao wanaweza kuhukumu mambo pia kwa sababu tu wamesikia umbeya na uongo bila hata kujithibitishia uhalisia wa mambo,  Pamoja na mahitaji ya watu wenye njaa, wenye uhitaji lazima tuonyeshe rahema kwa watu kwa kuwasaidia kukutana na mahitaji yao. Mtu anaweza akaonekana anahudhuria ibada na kutii kila kinachoamuriwa kanisani lakini maisha yake binafsi yakawa na uchafu wa kila aina, je tunaishi vipi na waume, zetu, wake zetu, watoto wetu, na je akilini tunawaza nini?  Wako watu wanahukumu wengine lakini akilini mwao ni waongo,  wana hasira, wachonganishi wamejaa fitina majungu na uzushi, kutaka sifa na kujitwalia utukufu, Yesu anachokitaka ni tuwe wakamilifu pande zote hatupaswi kuchagua kipi cha kutii na kipi sio cha kutii

Mathayo 23:23-24 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.”

Yesu anacho kitaka wetu ni kuwa pamoja na mambo mengine tusiache kukazia maswala ya muhimu na kuyapa kipaumbele, kama tunahubiri injili na kuichukia dhambi basi tuhakikishe kuwa tunapambana na kile kitu, ukikataza ulevi kataza na tamaa, ukikataza uzinzi kataza na hasira, haki haki, rehema rehema na adili ni adili, hatuwezi kuhubiri uaminifu katika eneo Fulani na wakati huo huo eneo lingine tukawa tumelilegezea, huko ni kuchuja mbu na kumeza ngamia, nusu utii ni sawa na kutokutii haya ni machukizo sawa na namna Mungu alivyochukizwa na Sauli alipomwambia aangamize kila kitu cha amaleki yeye akabakiza  nab ado akawa anasisitiza kuwa ametii

1Samuel 15:1-23Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya Bwana. Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari waliopanda farasi mia mbili elfu, na watu wa Yuda kumi elfu. Sauli akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Enendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri, unaokabili Misri. Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa. Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, kusema, Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha. Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia ukumbusho, akageuka, akapita, akatelemkia Gilgali. Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na Bwana, nimeitimiza amri ya Bwana. Samweli akasema, Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa. Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia Bwana usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha kabila za Israeli? Naye Bwana akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. Kisha Bwana akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia. Mbona, basi, hukuitii sauti ya Bwana, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana? Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali. Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.”

Ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda!

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!