Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Ufahamu Kuhusu Viungo vya Uzazi !



Vijana na Ufahamu kuhusu viungo vya uzazi.
Viungo vyetu tulivyopewa na Mungu ni zawadi ya pekee sana ambavyo vinaweza kutumiwa kwa utukufu wa Mungu na kutupa baraka duniani pia vinaweza kutumika vibaya na vikasababisha madhara ikiwemo kupoteza maisha, si dhambi kuzungumzia viungo vya uzazi na matumizi yake kwani kwa haraka sana vijana wanaweza kudhani kuwa wanaelewa na pia wanajua kuvitumia viungo hivyo vya uzazi, inawezekana dhana hiyo ikawa kweli lakini bado tunahitaji kujifunza biblia insema nini juu ya hilo, mtu akidhani ya kuwa anajua neno hajui bado kama impasavyo kujua. (1Koritho 8;2).tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo;-

  • Ufahamu kuhusu viungo vya uzazi.
  • Dhana potofu kuhusu viungo vya uzazi
  • Jinsi ya kutumia viungo vya uzazi kwa halali.
Ufahamu kuhusu viungo vya uzazi.
   (Mathayo 19;4) Mungu alipoumba mtu mume na mtu mke maana yake  aliumba mtu mmoja akiwa na jinsia ya kike na mwingine akiwa na jinsia ya kiume ili kupitia muunganiko wao waweze kuzaliana na kuongezeka na kufurahiana au kuyafurahia maisha kupitia tendo hilo ambalo ni zawadi (Mwanzo 1;26-28) baraka ile yakuzaa na kuongezeka ni tofauti na ile ya kulima bustani ya eden na kuitunza (Mwanzo 2;15) kazi ya kuitunza bustani iliweza kufanyika kwa mikono lakini ile ya kuzaliana  na kuongezeka hufanywa na viungo hivi maalumu ambavyo Mungu ametupa, Bahati mbaya viungo hivi vinafichwa sana na havionekani hovyo vinaitwa vya siri, na vinapotajwa watu hushituka na kuona ni dhambi kwa mtindo huu  hata kuvizungumzia kunaonekana ni kinyume na maadili na watu wengi huinama vinapotajwa hivyo ujuzi kuhusu viungo hivi ni  unakuwa mdogo na unapovielezea watu wanataka umalize kwa haraka. Viungo hivi tutavichambua kwa picha na baadae kuelezea kazi za kila kiungo.

                             
Pichani ni mfumo wa kiungo cha uzazi cha  mwanaume, mboo inapokuwa imekatwa katikati, mfuko mweupe juu kabisa ni kibofu cha mkojo Bladder, Mrija mweusi ni (tube) njia ya mkojo na shahawa ambayo huitwa Uretha, Mfuko unaobembea chini kwa ndani ni Testicals, mapumbu au makende, na Mfuko unaobeba kwa nje ni kifuko cha mapumbu scrotum, Nyuma ya kibofu na mrija wa shahawa na mkojo ni tezi maalumu zinazotengeneza majimaji yanayobeba mbegu au ghala ya shahawa  hii huitwa Seminal vesicle, Mbele ya mapumbu na mfuko wake ni Mboo yenyewe Penis. (Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya mwandishi Innocent  Mkombozi Kamote)


                               
        Pichani ni mfumo wa kiungo cha uzazi cha mwanamke,kuma inapokuwa imekatwa katikati,Pale kilipo kidole ndio kuma vargina  ni mahali panapotumikazaidi wakati wa kujamiiana,kutoa damu ya hedhi,kuzalia na kukojolea,Juu kwa pembeni ni kibofu cha mkojo bladder,Mfuko uliolala kuegemea kulia ni mji wa uzazi uterus ni eneo linalotumika kukuzia mtoto wakati wa ujauzito,

         Juu ni Mfumo wa kiungo cha uzazi cha mwanamke kikiwa kwa sura ya mbele,kuma ikiwa katikati ya mapaja juu ni mji wa uzazi na matawi tuyaonayo kwa pembeni ni mirija ya kulia na kushoto ya kupitishia mayai pembeni mwake kulia nakushoto ni ni kokwa za kubebea mayai yai la mwanamke ukubwa wake ni kama punje yamtama hivi.

Jinsi ya kutumia viungo vya uzazi kwa halali.
 Viungo hivi ambavyo muumba alitupa kama zawadi pia alitoa vidokezo kadhaa katika Biblia namna ya kutumia viungo hivyo kwa mfano wakati wa agano la kale Mungu alitoa maelekezo haya yenye uhusiano wa moja kwa moja na Viungo vya uzazi ilikuwa ni najisi kumbikiri bint na endapo mtu angefanya hivyo angelazimika kumuoa (Kumbukumbu 22;13-18). Mtu aliyebaka alipaswa kuuawa (Kumbukumbu 22;25),Kutokupiga kelele ni dhambi kama unabakwa (Kumbukumbu 22;23). Mtu kahaba hakupaswa kuwepo (Kumbukumbu 23;17),ilikuwa kuumizana sehemu za siri ni dhambi (kumbukumbu 25;11-12),Viungo hivyo pia viliwekewa sheria kama vile kutokulala na wanyama (Lawi 20;15-16) kuvitumia watu wa jinsia moja kama wanaume kwa wanaume ilikatazwa na imekatazwa katika agano jipya pia (Lawi 18;22,Rumi 1;18-27) aidha wanawake kwa wanawake pia si halali (Rumi 1;18-27). Na pia haikuwa halali kuvitumia kwa wanandugu walio karibu (Lawi 18;6-29).Unaweza kuona kama Mungu ni muumba na alitupa viungo hivi pia alitupa namna ya kuvitumia kwa halali kutumia viungo hivi kinyume na mpango wa Mungu kunaweza kusababisha madhara ya aina mbalimbali ikiwa Mungu anaguswa na viungo hivi basi kuvitumia isivyo halali kunaweza kutupelekea kuhukumiwa na Mungu kwani kunaweza kuharibu mfumo na utendaji uliokusudiwa na Mungu aidha kwa sababu hii pia kisheria kuna hukumu za uhalifu wa kimapenzi katika nchi mbalimbali “Sexual Crimes” hizi zimetungwa ili kulinda utendaji ngono usio sahihi hii yote ni kwa sababu Mungu hapendi tutumie isivyo halali.

Hakikisha unakua msafi kwa viungo vya uzazi.
   Kwakuwa viungo hivi vya uzazi viko sirini vinafunikwa na Nguo hatuna budi kuhakikisha kuwa tunavitendea haki kwa kuvifanyia usafi,oga mara kwa mara safisha viungo vyako vya uzazi ili kuvilinda na bacteria na vipele vya joto au vya uchafu,ili kujikinga na harufu,aidha hakikisha kuwa unajikausha vizuri kwa taulo na kama unaweza kupaka poda ni vema,Fua chupi zako na nguo za ndani mara kwa mara hasa wanaume kwani wanawake wengi hufanya usafi wa nguo zao za ndani mara kwa mara,lakini sivyo ilivyo kwa wanaume,Biblia inaunga mkono swala zima la usafi wa viungo hivi ikikazia swala zima la  kutokwa na vitu najisi kama damu ya hedhi na shahawa (Lawi 15;16-18,19). Hivyo ni muhimu basi kwa vijana kuhakikisha wanakuwa wasafi, kama ni damu ya hedhi  tumia vitambaa safi vilivyokaushwa vizuri na kupigwa pasi,na kama una uwezo tumia vitu kama always n.k vifaa vya dukani vya kuzuia damu ya hedhi, Kwa wanaume kama umetokwa na shahawa hakikisha unaoga na kufua chupi na mashuka,vijana ni muhimu wakajifunza kuwa na tabia ya kunyoa vikwapa vyao na mavuzi katika sehemu za siri na maeneo mengine, hakikisha unakua smart Mungu anapenda tuwe wa safi Biblia na hata Quran zinakazia sana usafi wa mwili pia chumba chako na kitanda chako na maeneo mengine yote yawe safi uwe na tabia ya kupenda usafi kwa gharama yoyote.

Dhana potofu kuhusu Viungo vya uzazi.
    Ni muhimu kufahamu kuwa yako mafundisha potofu duniani yahusuyo viungo vya uzazi ambayo yanaweza kujenga dhana potofu kwa vijana kuhusu matumizi ya viungo vya uzazi ambayo mengine yako kinyume na neno au muongozo wa kimungu.
     Iko dhana kuwa endapo utakaa muda mrefu bila kuvitumia viungo hivi  vitumikavyo kwa kujamiiana kunakuwa na madhara,Madhara yanayotajwa ni kama vile ,kutoka chunusi nyingi usoni,Kuchanganyikiwa,kuwa na ugonjwa wa kisaikolojia wa kukosa mwanaume,kuumwa na tumbo wakati wa kuingia katika hedhi,nk. Dhana hii haina ukweli kwani biblia inatia moyo watu vijana kusubiri hta wakati wa kuolewa(1Koritho 7;1,36),kuishi maisha ya kujitunza ilikuwa ni Desturi ya kawaida kwa waisrael na nyakati za kanisa la kwanza,na ilikuwa ni upumbavu mtu kuharibu ubikira wake (Mwanzo 34;1-9,2Samuel 13;10-15). Kwa msingi huu vijana wa kike na wa kiume wanaweza kuishi maisha ya ubikira hata zaidi ya miaka 30 hivi yusufu aliishi na hata kupewa mke akiwa na Umri wa miaka 30 na alizaa watoto watu wanaotia moyo dhana hii wanataka kuwaongoza vijana nje ya mpango wa kimungu biblia inasema jinsi gani kijana aisafishe njia yake ni kwa kutii neno la Mungu akilifuata daima (Zaburi 119;9).

   Ni muhimu kufahamu kuwa chunusi si sababu inayotokana na kutokushiriki mapenzi,lakini mtu anapo anza kuwa mtu mzima yaani anabalehe  mwili huwa katika mchakato wa mabadiliko ya aina mbalimbali katika wakati huu ngozi huwa inapokea vinururisho vya kuifanya ionekane nzuri hivyo kunakuwa na kusambazwa kwa aina Fulani ya mafuta mwilini ukiwemo uso,hii hupelekea baadhi kuwa na ngozi  yanye mafuta mengi na wengine kuwa na ngozi kavu  kwa wale wenye ngozi yenye mafuta yanayozalishwa kwa wingi ndio hukumbwa na tatizo la kuweko kwa chunusi nyingi hivyo tatizo hili haliwezi kumalizwa kwa kufanya ngono bali kwa aina za mafuta tunazozitumia kama ni lotion basi inashsuriwa wale  wenye tatizo hili kutokupaka mafuta au kupaka lotion yenye griselini nyingi lakini griselini nyingi itawafaa wale wenye ngozi kavu, pia inashauriwa kutumia poda kwa watu wenye nyuso zenye mafuta mengi,kutumia maji ya vuguvugu na njia nyinginezo.

     Dhana nyingine ambazo huongoza katika matumizi mabaya ya viungo vya uzazi ni kupunguza hamu ya mapenzi kwa kubusiana,kushikana shikana,kugusana uume au uke au kwa kujichua yaani kupiga punyeto master bathion, nia hizi hufaa kupunguza ashki za kimapenzi bila kufanya ngono dhana hii ni sahihi kwa vijana wa kawaida kama ifundishwavyo mashuleni hata hivyo si njia sahihi kibiblia mapenzi ni kama moto na huwezi kufanya mahaba haya kisha ukatoka salama (Mithali 6;27-28),Biblia haishauri kutumia njia zenye kuchochea mapenzi kabla ya wakati sahii akisisitiza hilo Sulemani anasema hivi “Nawasihi enyi Binti za Yerusalem kwa paa na kwa ayala wa porini Msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha hata  yatakapoona vema yenyewe”(Wimbo ulio bora 2;7,3;5).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni