Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Tatizo la Upweke !



Somo la Nne
Vijana na Tatizo la Upweke!
     Upweke ni mojawapo ya tatizo kubwa sana la mwanadamu Upweke kwa lugha ya kiingereza “ Isolation” ni kutengwa mbali na wengine,ni uhalisi wa kuwa mwenyewe ni kutengwa na wengine, It is a state of being isolated or sepatation from others,The fact of being alone and separated from others. Tatizo hili kwa mujibu wa biblia lilijitokeza mara tu baada ya kuumbwa Adamu hata kabla ya anguko la mwanadamu, Hivyo swala la mwanadamu kutokupenda kuwa pekee ni la kimaumbile (Mwanzo 2;18).Upweke hushusha moyo,hukatisha tamaa huleta huzuni na kufanya mtu asione umuhimu wa maisha,Ni kwa sababu hii Mungu alisema si vema huyo mtu awe peke yake, na kwa kuwa vijana ni moja ya kundi linalotatizwa na swala hili hapa mwandishi wetu atakuwa akidadavua namna ya kukabibliana na tatizo hili, katika somo hili nitazungumzia maeneo makubwa matatu yafuatayo;-

  • Tatizo la Upweke.
  • Fundisho katika Upweke.
  • Namna ya kukabiliana na tatizo la upweke.
Tatizo la Upweke!.
    Kama nilivyokwisha kugusia awali kuwa upweke ni moja ya matatizo yanayowakabili watu wengi sana duniani wakiwemo zaidi vijana, Kadiri ulimwengu unavyoendelea ndivyo na jinsi tatizo la upweke linavyozidi kukua duniani, Huko ulaya anaeleza Binti mmoja wa kitanzania anayeishi nchini Ujerumani alipoulizwa kuwa angependa kuishi ulaya baada ya kumaliza masomo yake? Binti huyu alisema kwa haraka nitarudi nyumbani,na nisingependa kuishi ulaya,Sababu kuu aliyoitoa binti huyu  aliyekuwa akihojiwa na shirika la habari la kiingereza BBC, alisema ni upweke! Alisema yeye hukutana na marafiki zake akiwa shuleni tu na inapofika mwishoni mwa wiki “Weekend” anachokisikia ni milio ya ndege tu,watu wengi huelekea kwenye majumba makubwa ya starehe na mitaa huwa kimya,na unakuwa na wakati mgumu na unapopata japo barua pepe yani E-mail kutoka kwa rafiki zangu wachache niliowaacha Tanzania ninakuwa kama nimepata Dhahabu. Hii inatufundisha kuwa kumbe unaweza kuishi katika nchi nzuri, jumba zuri au katika mazingira mazuri sana au hata katika Bustani kama ilivyokuwa kwa Adamu pale Eden  lakini kama ukiwa mpweke maisha hayo yanakuwa hayana maana, kwa ajili ya upweke watu wengine hufikia hatua hata ya kutaka kujiua kwa kukosa matumaini. 

 Wengi wanapoulizwa sababu ya upweke hutoa sababu nyingi kati ya hizo kubwa zaidi ni hizi, Kukosa kazi, Maumbile ya upole sana au aibu sana, kuchokozwa, Kukatishwa tamaa, Kutofikia malengo, Unyanyapaa, Kujichukia, Hali ya kujiona duni, Kukataliwa na jamii, mazingira mume au mchumba au jamaa na ndugu wa karibu, kutengwa, Kuugua, Kufungwa gerezani, kufiwa na jamaa, ndugu mzazi au mtu uliyempenda sana, Talaka, kukosa hamu ya moyo na kutokujisamehe baada ya kufanya dhambi.

   Kwa ujumla kunaweza kukawepo sababu nyingi zaidi ya hizi zinazopelekea watu kujihisi Upweke,upweke usipodhibitiwa unaweza kusababisha misukumo mingiyenye madhara kwa vijana upweke unaweza kupelekea mtu kujiingiza katika kufanya dhambi kwani upweke na dhambi ni jamaa walio karibu sana ni mapacha  yaani alipo upweke dhambi naye hayuko mbali mtu anaweza hata kujiingiza katika ukahaba wa kupindukia na sababu ikiwa ni upweke na watu wasijue ni kwanini,upweke unaweza kukufanya utumie dawa za kulevya,upweke unaweza kukufanya uone kuwa kila mtu anakuchukia,upweke unaweza kukufanya ujiuwe, na unaweza kukufanya uwe mlevi na sababu kadhaa wa kadhaa nilipowahoji watu kadhaa waloopitia katika tatizo la upweke kuwa walijisikiaje,hisia walizokabiliana nazo zilikuwa nini, haya ndiyo majibu ya baadhi yao, Ahaa unakuwa hauna raha hata! unahisi hufai na unavunjika moyo,Unahisi mambo ni mabaya tu,unakuwa hupendi watu unahisi watu hawakupendi wala hawakujali, Unalala hovyo tu, au unakosa usingizi unahisi hovyo maumivu si maumivu uchovu si uchovu, kazi huwa haziendi, unaweza usione umuhimu hata wa kula, Uwezo wa kufikiri unapungua, unarudia mawazo yaleyale, unatamani ukazurule,Unahisi heri ufe,Unaweza kuua,Unahisi hata Mungu hana msaada unamlaumu Mungu, n.k.
    Unaona Kama watu tena wengi wao ni wale waliookoka wanaweza kuhisi matatizo kama hayo hapo juu basi ni lazima tukubali kuwa upweke si tatizo la kupuuzia lazima tukubali kuwa tatizo hili ni baya si wengine wanataka kujiuwa au kuuwa au kumlaani Mungu je ni jambo jepesi hili? Kwa nini kuna upweke? Kwa nini huwa tunausikia upweke ni fundisho gani tunalipata katika Upweke hilo sasa linatupa kutafakari kipengele kinachofuata fundisho katika Upweke.

Fundisho katika Upweke.
      Ni muhimu kufahamu kuwa ingawa upweke ni tatizo kubwa kiasi hiki bado ndani yake tunajifunza mambo mengi ya maana katika maisha na ambayo ni muhimu kuyazingatia, Mtu mpweke ni kama kaa la moto lililotengwa peke yake toka katika makaa mengine ya moto hivyo ni rahisi kuzimika, hivyo mtu mpweke yumo hatarini zaidi, lakini upweke una kitu gani

     Upweke unatufundisha mambo mengi na ya muhimu yafuatayo miongoni mwa hayo ni;-
  • Tunahitaji kuwa na ushirika na watu wengine wa Mungu (Mithali 18;1) Biblia inasema hivi “Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake Mweyewe,Hushindana na kila shauri jema”Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hakutuumba  kama kisiwa ili tuishi wenyewe tu tunahitajiana sanasana hivyo hatuwezi kukabili matatizo yetu wenyewe kila mmoja anahitaji ushirika wa mwingine, linapojitokeza tatizo hili ni wakati muhimu wa kurejea zile stadi za maisha na kujihoji kuwa tunahusiana vipi na wengine? Kwa nini kwa sababu wakati mwingine sisi wenyewe tunaweza kuwa ndio sababu ya hali tunayoipitia na kama hivyo ndivyo basi tujifunze kuwatafuta wengine wako wapi na tufanye ushirika nao (Filipi 2;1-4,Waebrania 10;24-25).
  • Upweke unatufundisha kuwa tunahitaji ushirika na Mungu.
Ni muhimu kufahamu kuwa upweke unaweza kukabiliwa vizuri kama una uhusiano mzuri na Mungu, lazima tuuchunguze uhusiano wetu na Mungu kwani maisha ya dhambi huweza kutufanya tuhisi upweke kwa sababu tumetengwa na Baba yetu wa kimbinguni, Hivyo kama tumefanya dhambi uhusiano wetu na Mungu huingia dosari na ni Budi kuungama na Kuutafuta Uso wake yeye  amesema hivi “Tazama mkono wa Bwana haukupunguka hata ashindwe kuokoa wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu Na dhambi zenu zimeuficha uso wake Hata hataki kusikia” (Isaya 59;1-2).Mungu ametoa mwaliko wa kukaribia kwake kwa toba (Isaya 1;18-19) Adhabu kubwa na ya juu kabisa dunuani ni kutengwa na uso wa Mungu (Mwanzo 4;13-16).Kama unapitia hali za namna hii fanya kama mwanampotevu zingatia moyoni mwako rudi kwa baba yako na kwakuwa yeye ni mwema atakupokea (Ebrania 12;14,Mwanzo 3;8-10)

  • Upweke unatufundisha kuacha Kiburi na ubinafsi ili tunyenyekeane.
     Upweke unatufundisha kuwa hatuwezi sisi wenyewe na hivyo tuwanyenyekee wenzetu na kuwatumikia, Biblia inasema atakaye kuwa mkubwa kati yenu ni lazima awe kama yule atumikaye, tunapowatumikia wengine watatunena vizuri na hivyo tutakuwa na furaha, tuwasalimu wengine na kuwafanyia mema kila mwanadamu ni dhaifu hivyo tuchukuliane na kukubali kuwaheshimu wengine yale ambayo tunataka kufanyiwa na wengine ni muhimu sisi tukiwa wa kwanza katika kuyatimiza (Marko 10;43-45,Efeso 5;19-21)


Namna ya kukabiliana na tatizo la Upweke!.
       Sasa tumeona jinsi upweke ulivyo na mambo Fulani ya msingi unaotufundisha unafundisha mambo mazuri sana  ya muhimu lakini kama hatuyajui hayo bado upweke unabaki kuwa tatizo kubwa sana na bado litatupasa kujua jinsi ya kuukabili kama nilivyogusia kuwa upweke ni ndugu pacha na dhambi lazima tujifunze namna ya kuutawala katika mtazamo chanya.

  1. Tumia Upweke Kama nafasi ya kukaa Na Mungu.
     Kumbuka kuwa watu wengi ambao wametumiwa na Mungu na hata kufanya ugunduzi mkubwa sana duniani na kuacha falsafa mbalimbali duniani walikuwa wapweke sana, lakini moja ya njia iliyowafanya kufanikiwa waliamua kuutumia upweke walionao kumtafakari Mungu.
Musa alikuwa mpweke ,alikataliwa na watu wake ,alifukuzwa na farao akitafutwa kuuawa alikwenda mbali na nduguzake na kuchunga kondoo za mkwewe Ruthu jangwani aliutumia upweke kuomba na kutafakari na haimaye kuona maono ya Mungu akimtaka akawatoe ndugu zake katika utumwa mzito  ni jambo la kusha ngaza watu wanaweza kumkataa mtu lakini akawa mwenye kipawa kikubwa chenye kuwafaa wengine! Kukataliwa si mwisho wa maisha yako angalia Biblia inasema hivi Musa huyo waliyemkataa,wakisema ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi?Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti(Matendo 7;35-36). Muda haungeweza kutosha kukupa shuhuda za watu walioishi maisha ya upweke na wakautumia upweke wao na Mungu na wakakamilisha mambo makubwa duniani Daudi alikuwa maporini mara nyingi, Yusufu,Samsoni, Yohana mbatizaji,Eliya n.k. lakini si hivyo tu bali hata viongozi wa dini nyingine kama Islamu watakubali kuwa Muhamad alikuwa na tabia ya kukaa peke yake jangwani akifunga na kuomba hata alipopata maono,Budha mwanzilishi wake Gautama aliishi pekee porini akitafakari kweli kadhaa kuhusu maisha ikiwa ni pamoja na kujiuliza kwa nini wanadamu wateseke na akaangaziwa kumbe kuutumia upweke kutafakari mambo ya kiroho ni afya muhimu ya kiakili na kimwili, basi wakati mwingine tunapokutana na magumu upweke ni dawa ya kutatua tatizo hili (Mwanzo 28;10-15,32;24)Yesu Kristo aliuutumia muda wa upweke kutafakari na kuomba akiongozwa na Roho kumbe upweke unaweza kuwa sababu ya nguvu nyingi za kiroho na udhihirisho wa karama na utendaji wa R oho mtakatifu na kujifunza kuisikia sauti ya Mungu. 

2.       Usikawie kuoa,
upweke mwingine  unaweza kudhibitiwa kwa kuamua kuoa au kuolewa Ingawa ni wazi kuwa si wakati woote kuoa au kuolewa kunaondoa upweke lakini Mungu alitibu tatizo la Adamu la upweke kwa kumpa Hawa (Mwanzo 24;62-67,26;8) Isaka alipata utulivu baada ya kuoa.

Kwa wale waliomwamini Mungu kamwe hatupaswi kuishi kama watu wasio na matumaini (1Thesalonike 4;13-18) Kama watu wametukosea tumwachie bwana yeye Ndiye alipaye kisasi dhidi ya waonevu wetu samehe usiwe na uadui na mtu,Tumia upweke kuabudu kuomba,kutafakari kwenda kuwatembelea watu na kujadili maswala nyeti kuhusu dini,siasa na taifa lako au kuuliza maswali ya muhimu kuhusu maisha au mambo usiyoyajua,tumuombe Mungu aondoe kiburi na ubinafsi au tabia zozote zinazotunyima marafiki , Tuache kujiona, Mabinti wa Lutu walifikia hatua ya kuzaa na baba yao kwa sababu hawakuwa na majirani waliishi peke yao hawakuwa na jamaa ya karibu ni naamini kuwa Mungu atakubadilisha ili utumie nafasi za upweke Kwa faida na Si kwa hasara kama unapenda michezo shiriki michezo fanya mazoezi jichanganye cheza hata bao au karata n.k hususani unapokuwa na muda wa kufanya hivyo Endapo una Computer kuna michezo Games ambayo inaweza kukuchangamsha akili Neema na amani na Upenda wa Bwana ukae nawe amen!.


Mwanafalsafa Plato ni moja ya Wanafalsafa wakubwa sana Duniani (428-347 k.k.) alikuwa mbunifu na mwenye mvuto sana katika Falsafa alikuwa mtaalamu wa fizikia,Siasa na hisabati,alizaliwa huko Athene Ugiriki,Babaye aliitwa Arston toka katika familia za kifalme alikufa mapema na hivyo mamaye aliolewa na baba wa kambo,Plato aliishi maisha ya upweke alitamani kuwa mwana siasa lakini alikataliwa na viongozi wa kisiasa wakimuona kuwa ni mzushi na kuwa hana mawazo sahihi bali muongo na aliyekosea,alifuata falsafa za Socrates na alipofariki Socrates alikimbia akiogopa kuuawa lakini baadaye alirudi Athene na kuanzisha chuo kikuu katika taaluma za Sayansi, Fizikia, Hisabati na siasa ,Ni mtu anayeheshimika ulimwenguni leo.Unaonaje angeamua kujiua? Hakukata tamaa wewe pia usikate tamaa kwani Mungu amekupa kitu cha ziada!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni