Jumamosi, 5 Machi 2016

Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo



 Maana nawaambia Haki yenu isipozidi Hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo Hamtaingia kamwe katika Ufalme wa Mbinguni.

Moja ya maandiko ambayo hutumiwa vibaya na wahubiri wengi wa injili ni Mathayo 5;20 kimsingi kutokana na maandiko haya wakristo waliookoka wametengenezewa makongwa mengi sana  kwa kawaida mstari huo inasomeka hivi “Maana nawaambia haki yenu isipozidi Hiyo haki ya waandishi na mafarisayo hamtaingia kamwe katika ufalme wa Mbinguni” ndugu msomaji wakristo wengi wamefanywa kuwa watumwa na kubeba mizigo isiyowahusu kupiia andiko hili jinsi andiko hili lilivyo na kile kinachotafasiriwa au kukaziwa na wahuiri ni tofauti sana na hata na jinsi Kristo alivyokusudia  andiko hili kutumika kwa ujmla kile ambacho wahubiri wengi wanakimaanisha katika maandiko haya ni kama maandiko haya yanasomeka hivi “Maana nawaambia Matendo yenu  yasipozidi Hayo Matendo ya waandishi na mafarisayo hamtaingia kamwe katika ufalme wa Mbinguni” nimewahi kuwasikia wahubiri wakikazia wakristo kuwa na matendo yanayowazidi mafarisayo na waandishi yaani waalimu wa sheria tunapounganisha na swala zima la wokovu mafundisho ya aina hiyo sio injili tuliyoipokea oka kwa Bwana, wakati Fulani kwa sababu ya mafundisho ya aina hiyo nilikuwa nimejipangia kuwa ni lazima niamke kuomba Alfajiri kama vile waislam wafanyavyo na kwakuwa niliamini kuwa wao hawana Mungu wa kweli kama niliye naye kwa msisitizo wa mahubiri ya wachungaji wengi nilijifunza kuwa ninalazimika kuamka kabla ya Waislamu na kumuomba Mungu ili matendo yangu yazidi hayo matendo ya mafarisayao na kwakuwa maisha yangu ya mwanzo kabla ya kumjua Mungu nilikuwa nikilala na kuamka kwa saa nilizotaka uamkaji wa Alfajiri lilikuwa jambo jipya katika maisha yangu niliambiwa kuwa huko Korea Ya kusini wakristo huamka alifajiri na kumuomba Mungu na wamepata mafaniko makubwa sana lakini sisi Afrika Mashariki wamishionari wetu hawakuwa wametufunza hivyo kwa hiyo nilichapa usingizi lakini nilipomjua Mungu na kujifunza kuhusu kuamka alifajiri nligunduia kuwa ninapaswa kuwawahi waislamu na siku kama ikitokea nimechelewa kuamka na wakanitangulia nilijihisi vibaya na kuona kuwa siku hiyo ni chungu na sio siku nzuri io niliiishi kwa maumivu ambayo sikuwa nayo kabla ya kuokoka kwa nini nilijifunza kuwa matendo yangu lazima yazidi yale ya Mafarisayo. Kumbe nilikuja kugundua siri kutoka kwa roho wa Mung kuwa Mungu hakumaanisha kile nilichokianya kimsingi Yesu alikuwa akizungumzia “HAKI” na sio “MATENDO” nililazimika kujifunza kuhusu haki kamamstari halisi unavyosema na niligundua kuwa kwanza hakuna mwanadamu mwenye haki hata mmoja Warumi 3;10-12,Biblia inasema hivi “Kama ilivoandikwa ya kwamba hakuna mwenye haki hata mmoja hakuna afahamuye, Hakuna amtafutaye Mungu Wote wamepotoka wameoza wote pia hakuna mtenda mema la! Hata mmoja” nilijiuliza kama hakuna mwenye haki hata mmoja inakuwaje Yesu aseme haki yet isipozidi haki ya mafarisayo hatutauona ufalme wa Mbinguni? Nikagundua kuwa kumbe Mafarisayo hawakuwa na haki hawakuwa na haki ya kweli haki waliyokuwa nayo ilikuwa haki ya nje tu Mathayo 23;25-28 Yesu anawaonya mafarisayo “Ole wenu waandishi na Mafarisao wanafiki ….. kumbe mafarisayo walikuwa wanafiki hawakuwa na haki ya kweli haki yao ilikuwa haki ya nje walifanya mambo ili waonekane na watu Mathayo 23;5a “Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu;” kumbe mafarisayo haki yao ilikuwa ni haki ya nje haki ya kujionyesha tu walionekana na watu kuwa ni wenye haki lakini kwa kweli hawakuwa na haki ya kweli na ndio maana Yesu alisisitiza kuwa ni lazima iwepo haki mbadala ,haki ambayo ni tofauti na haki na ile ya mafarisayo haki ya nje  sasa ili mtu aweze kuingia katika ufalme wa mbinguni hawezi kuingia kwa haki kama ile ya mafarisayo ambayo ilikuwa ya nje ni kweli walionekana wanshika sheria walionekana wanaomba, walisifu na kufunga walisoma neno la Mungu  na hata kuhudhuria ibada  hata hivyo walifanya hayo ili waonekane na watu wasifiwe waonekane kuwa wao ni wa kiroho na washika dini wakubwa huu haukuwa mtazamo sahii haki mbadala ni haki ambayo haitokani na matendo ya sheria  ni haki kutoka moyoni ni haki itokanayo na imani  ni neema ya kukubali kazi aliyoifanya kristo kwaajili yetu Msalabani ni haki itokanayo na Kristo Warumi 3;21-26 Waefeso 2;1-9 hii ndio haki mbadala aliyoizungumzia Bwana Yesu kwa hiyo Kristo hajatuita katika mashindano ya kuwazidi wale tunaowaita mafarisayo kwa matendo kama ukifanya hivyo wakikushinda unakuwa chni ya kongwa ambalo hata kabla ya kuokoka hukuwa nalo na unaweza kujikuta ukichomwa moyo kama mimi nilipokuwa nikikosa maombo ya alfajiri kumbe lilikuwa kongwa!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni