Kiwango cha chini cha maombi ni lisaa
limoja!.
“Kiwango
cha chini cha maombi ni lisaa limoja!”ni moja ya mikazo ya wahubiri inayowatia
watu katika kongwa kiasi ambacho wanashindwa au wanajikuta kuwa hawaombi kabisa
hata dakika tano kwa nini kwa sbabu ya mkazo mkubwa kuhusu maombi baada ya
kuokoka andiko linalotumika ambalo limetumika vibaya kuleta fundisho hili ni
Mathayo 26;40-45. Tofauti na mikazo ya wahubiri Kristo hapa hakumaanisha kuwa
kiwango cha chini cha kuomba ni saa moja Yesu alisema hivi “Hamkuweza kukesha name
hata saa moja?” kwa tafasiri sahii za andiko hilo ni
muhimu kufahamu kuwa wakati wa Yesu kihistoria saa zilikuwa bado
hazijagunduliwa na kwa mujibu wa Waebrania waligawa muda kwa kutumia neno zamu
hasa kwa wakati wa usiku zamu ya kwanza ilikuwa ikianzia saa moja mpaka saa
tatu usiku zamu ya pili saa nne mpaka saa sita hivi kasha zamu ya tatu saa saba
mpaka saa tisa hivi na zamu ya nne ni saa kumi mpaka saa kumi na mbili hivyo
ndivyo wayahudi walivyogawa muda kihistoria lakini neno saa katika Biblia yetu
ya Kiswahili liliingizwa na wazee wetu waliotafasiri Biblia mwaka 1952 wakati
huu saa zilikuwa zimekwisha gunduliwa na katika kawaida ya Kiswahili saa moja
pia humaanisha jambo dogo
Biblia iliposema Ombeni Bila kukoma ilimaanisha Maombi hayana kiwango cha Muda
Kwa
tafasiri ya Kiyunani neno hilo saa moja hutumika Neno “HORA” ambalo kwa kiingereza ni “a little while” ambalo kwa
Kiswahili chepesi ilimaanisha hata kidogo au Mara kwa kiibrania neno linalotumika ni “SODI” ambalo maana yake ni ileile hata kidogo au hata mara moja kwa
msingi huu tafasiri ya kweli ya kimaandiko ni kuwa wanafunzi wa Yesu siku ile
hawakuomba hata kidogo yaani hawakuomba kabisa na matokeo ya kutokuomba kwao
yanaonekana wazi baadaye kidogo kwa wao kushindwa kustahimili majaribu wakati
wa kukamatwa kwa Yesu na ndio maana Yesu aliwaambia maneno haya “Ombeni ili msiinge
majaribuni” Yesu mwenyewe aliomba hivo alitiwa nguvu kukabili
majaribu ya kukamatwa na kusulubiwa aliweza kukabili mateso ya msalaba kwa
ujasiri hiii maana yake ni kuwa kama mitume wangeomba japo kidogo tu wangetiwa
nguvu kukabili majaribu aliyokuwa mbeleni lakini kwa kutokuomba kabisa
walimkana Yesu, wakamwacha wakakimbia na kusambaratika Mkazo mkuu hapa ni kuwa
wakristo hawapaswi kupuuzia maombi kabisa na kona kuwa dakika chache za kuomba
si za muhimu ni za muhimu sana kwanini wakristo wengi leo waliookoka hawaombi
kabisa je unafahamu hilo mimi najua nawafahamu wakristo weng ambao walipokuwa
katika makanisa yao ya zamani kabla ya kuja katika makanisa ya kipentekoste
walifundishwa maombi mafupi mafupi “Simple prayers” kulikuwa na sala ya Bwana,
na sala nyinginezo zilikuwa nyepesi sana walipokuja katika jamii ya makanisa ya
kipentekoste hawakufundishwa maombi mepesi badala yake walikutana na mkazo mkuu
kiwango cha chini cha kuomba ni lisaa limoja! Kwa hiyo mwanzon walijitahidi
lakini sasa wanapojaribu kuomba lisaa limoja wanajikuta kwa sababu ya shughuli
nyingi hawawezi kufikisha lisaa limoja na kwa sababu hawakujifunza maombi
mepesi sasa hata zile sala walizotoka nazo katika makanisa yao ya zamani
hawazitumii tena na hivyo wengi hujikuta wamelala na kuamka bila kuomba kabisa
sasa kwanini mkazo ulipuuzia maombi mafupi sasa matokeo ni nini? Kongwa
limekuwa zito hawawezi lisaa sasa inakuwaje wanakuwa wapagani kuliko kabla
hawajaokoka wana wa jehanamu mara mbili hawaombi kabisa!
Hili ndio tatizo la
kongwa unapowabebesha watu kongwa kwa kutumia maandiko isivyo halali unawafanya
wengi kuwa wana wa jehanam mara mbili
zaidi kabala ya kuamini kwao ni muhimun kufahamu uwa tunaweza kumuomba
Mungu katika nyakati fulan maombi rahisi kwa ufupi na yakafanya kitu Kipofu
Batholomeo alipiga tu kelele Yesu mwana wa Daudi unirehemu na maombi yake yalisikilizwa, Mathayo 8;1-3
wakoma wale kumi waliomba maombi ukitaka waweza kunitakasa je walichukua masaa
mangapi kujibiwa maombi yao je walifunga? Jibu ni la Mathayo 14;29-31 au je
wanafunzi walpokuwa wanazama katika dhuruba walichkua msaa mangapi kumuamsha
Bwana kuwa wanaangamia kumbuka kuwa maomi mafupi mafupi yakiombwa kwa
kumaanisha yanafanya kitu kuliko kutokuomba kabisa Kristo alipokuwa msalabani
pia alikuwa na muda wa kuomba maombi mafupi mafupi kama Mungu wangu Mungu wangu
mbona umeniacha? Au Baba mikononi mwako naiweka roho yangu, kumbuka kuwa maombi
hayana kiwango kila muhubiri anapenda wau wawe waombaji lakini ni muhimu
kufahamu kuwa Munu anaheshimu kiwango chochote cha maombi chimi ya neema yake
mtu atakachoomba kwa moyo wa kweli bila kujali anatumia masaa mangapi mbele za
Mungu dakika ina faida na masaa pia yanafaida tukifahamu hili hakutakuwa na
kiburi wala huwezi kujigamba kuwa wewe ni muombaji kumbuka kuwa ungu hafanyi
kwa sababu unaomba saa anafanya kwa sababu ya neema yake na upendo wake na mkao
wako wa moyo, wengi wa wale wanaotangaza kuwa wanaomba sana kimsingi
hawatofautian na mafarisayo na wanataka kujilinganisha au kutuwekea kongwa kuwa
ni kiwango fulani cha maombi ndicho Mungu hukisikia na kuwa kiwango kidogo
Mungu hasikii ? hii sio dhana ya kweli kwa Mungu ambaye ni baba Yeye ni Mungu
aliye Karibu. Maombi ni swala la siri kla mtu na aombe kwa kadiri ya neema
aliyopewa kle kiwango chako utakachokuwa umefikia ni chako wewe sio cha
mwengine usimpandikizie wala usidharau chakwake ninachokisema kuwa maombi
yaliyo bora ni yale ambayo Mungu anayasikia na kuyajibu bila kujali kiwango ni
vizuri kukaa sana miguni pa Mungu kama ukiweza lakini Mungu hajibu mtu kwa
sababu anakaa sana anajibu kwa sababu yeye ni baba aliye mwema kuwapandikizia
watu kubeba masaa na masiku kibao ya kufunga ni kuwabebesha kongwa hivyo pamoja
na uzuri wa maombi ni muhimu kufahamu kuwa maombi hayana kiwango na ubora wa
maombi ya mtu si wingi wake bali ni vile anavyojibiwa mwenye masikio ya kusikia
na asikie. Asomaye na afahamu
Imenisaidia
JibuFutaNimeisoma yote, na imenisaidia sana. Mungu akubariki sana mjenzi
JibuFuta