Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa
na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi
nimeushinda ulimwengu.”
Utangulizi:
Maisha yetu Duniani yamejaa
yamejaa milima na mabonde, kila mwanadamu anapozaliwa duniani ni kama ameletwa
ili aweze kupambana na changamoto mbalimbali, kuna nyakati za giza na kuna
nyakati za nuru, Katika nyakati hizo za changamoto mbalimbali, wengi wetu
tunaachwa na maumivu makubwa na mateso ya aina mbalimbali na wakati mwingine
tunaweza kupoteza tumaini, wakati mwingine tunaweza kujiuliza hivi kweli Mungu
yupo? Na kama yupo anaona haya tunayoyapitia? Tunaweza kujikuta tunakata tamaa
na kuvunjiika moyo na kupoteza imani kwa
Mungu!, Kristo Yesu katika Yohana 14-16 alipokuwa anahitimisha safari yake ya
kazi duniani alianza kuzungumza maswala kadhaa ynayoashiria dhiki itakayowapata
wanafunzi wake neno analolitumia Yesu hapo ni TRIBULATION ambalo maana yake ni mateso, taabu, changamoto au
vikwazo vya namna mbalimbali anaonyesha kuwa haya yapo kwa sababu tuko duniani
kwa hiyo katika maisha ni lazima tukutane nayo na kuyakabli, kwa msingi huo
kama watu wa Mungu hatupaswi kuvunjika moyo kutokana na vikwazo mbalimbali na
badala yake hatuna budi kukabiliana navyo kwa imani na kuhakikisha tunatoboa
anga jingine katika maisha haya hii ni kwa sababu Yesu ametuhakikishia ushindi
siku zote za maisha yetu! Na adui yetu mkuu amekiwsha kushughulikiwa, Yesu sio
tu ameushinda ulimwengu lakini pia ametuachia njia ambazo kwa hizo tunaweza
kushinda vikwazo vyote! 1Petro 4:12 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu,
unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.”
1.
Kumbuka
Hakuna jambo lililo gumu la Kumshinda Mungu
a. Mwanzo 18:13-14 “BWANA
akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana,
nami ni mzee? Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake
nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.” Abraham na Sara walikuwa wakitazamia
kupata mtoto na muda mrefu sana ulipita hata wote wakawa wazee Sara akakoma
katika siku zake za kawaida ya wanawake Hata Mungu alipowatokea na kuwaahidi
kuwa watapata mtoto Sara alicheka sana bila shaka alifikiri inawezekanaje
katika uzee kama ule yeye kupata mtoto Mungu alimjibu Abrahamu kuwa Hakuna neno
lililo gumu la kumshinda Bwana !
b. Hesabu 11:21-23 “Musa
akasema, Watu hawa ambao mimi ni kati yao, ni watu sita mia elfu waendao kwa
miguu; nawe umesema, Nitawapa nyama, ili wale muda wa mwezi mzima. Je! Makundi ya kondoo na ng'ombe yatachinjwa
kwa ajili yao, ili kuwatosha? Au samaki wote wa baharini watakusanywa pamoja
kwa ajili yao, ili kuwatosha? Bwana akamwambia Musa, Je! Mkono wa Bwana
umepungua urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako, au sivyo.”
Mungu alipokuwa amewaokoa wana wa Israel kutoka utumwani kule Misri alianza
kuwalisha jangwani kwa chakula maalumu kutoka Mbinguni kiitwacho mana kwa
muujiza hata hivyo wana wa Israel walianza kulalamika kuchoshwa na chakula
hicho na wakaanza kumdai Musa awape nyama jambo hili lilionekana kama
haliwezekani kwa Musa lakini Mungu aliahidi kuwa atauliza mkutano ule kwa nyama
tena sio katika siku moja bali mwezi mzima mpaka wazikinai musa aliona kama
jambo hili ni jambo lisilowezekana lakini Mungu alimjibu kuwa Hakuna
lisilowezekana kwa Mungu!
c. Yeremia 32:17 “Aa!
Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa
mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza;” Hakuna
jambo lolote lililo gumu asiloliweza Bwana Mungu wetu hivyo tunapokutana na
changamoto za aina mbalimbali hatuna budi kuliitia jina la Bwana kwa imani
tukijua ya kuwa Mungu wetu anaweza na atatusaidia na kutukomboa na kutupa
ushindi katika hali yoyote tunayoipitia wengi tuliomtumaini alitusaidia na
kutukomboa na kututoa katika kutazamia kwa adui yetu .
2.
Kumbuka
shuhuda zake
Zaburi 124:1-8 “Kama
si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa, Kama si Bwana aliyekuwa
pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia. Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira
yao ilipowaka juu yetu Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu
ya roho zetu; Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo. Na
ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. Nafsi yetu imeokoka kama
ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. Msaada wetu
u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.” Mwandishi wa
zaburi hii amejaa shuhuda za Bwana anakumbuka matendo makuu ya Mungu na uwezo
wake mkuwa wa kuwaokoa Israel anakumbuka hatari zote ambazo wana wa Israel
walipitia na anakumbuka mashambulizi yote wana wa Israel waliyapitia jinsi
walivyokusudiwa mabaya au kumezwa hai, anakumbuka hasira za adui zilivyokuwa
mbaya sana juu yao lakini Mungu aliiokoa nafsi yake na watu wake anakumbuka kuwa
Mungu ni msaada, siku zote tunapokabiliana na changamoto yoyote na jambo lolote
lilolo gumu kumbuka shuhuda zake shuhuda za ushidi ndio zitakukumbusha kuwa
Mungu ni nani na zitakufanya uione changamoto iliyoko mbele yako kuwa ndogo na
kuwa itapita pia ona 1Samuel 17:32-37 “Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa
ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu. Sauli
akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe
u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake.Daudi akamwambia Sauli,
Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba,
au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi, mimi hutoka nikamfuata,
nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake,
nikampiga, nikamwua. Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti
asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu
aliye hai. Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya
dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na
Bwana atakuwa pamoja nawe.” Shuhuda za matendo makuu ya Mungu ni
muhimu kwetu, mkumbuke Mungu alivyokushidnia katika mambo mengi makubwa na
magumu na jua kuwa Mungu yuleyule aliyekusaidia katika 1 na 2 na 3 atakusaidia
na hili unalokabiliana nalo!
3.
Kumbuka
Neno la Mungu.
Waebrania 4:12 “Maana
Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote
ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta
yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.”
Neno la Mungu ni sauti ya Mungu lina mamlaka lina nguvu na ufunguo wa
suluhu kubwa na nyingi ya maisha yetu, Hatuna budi kulisoma na kulitumia katika
kila hali tunayokabiliana nalo, Neno la Mungu lina ahadi na ujumbe kwa kila
hali unayokutana nayo duniani na kwa kila changamoto na vikwazo, tafuta ahadi
za Mungu na kujifunza kuwa ni jinsi gani Mungu anaweza kutusaidia kupitia hali inayotunzunguka
ndani ya neno kumejaa mifano ya jinsi Mungu alivyowasaidia wengine na wakaweza
kupenya atakusaidia na wewe katika kila hali inayokukabili!
4.
Kumbuka
Roho Mtakatifu.
Bwana Yesu
alipokuwa akiwaaga wanafunzi wake na kuwajulisha kuwa watapitia vikwazo vingi,
wengi wao walijawa na huzini na kiwewe, Yesu alikuwa anafahamu kuwa watapitia
changamoto mbalimbali na kuwa wanahitaji msaada wake aliwaahidi kuwa Roho
Mtakatifu atakuwa msaada ulio karibu na hivyo mara kwa mara aliwakumbusha kuwa
atawaombea ili Baba aweze kuruhusu ujio wa Roho Mtakatifu ambaya atakuwa msaada
ulio karibu kama Yesu mwenyewe ona :- Yohana
14:16-17, “Nami
nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala
haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”
Ni kwa msingi huu nyakati za kanisa
la kwanza waliweza kuwa washindi katika majaribu na shida za namna mbalimbali
kwa sababu Roho Mtakatifu aliwatia nguvu kukabuiliana na changamoto hizo ona Matendo 4:1-10 “Hata
walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo
wakawatokea, wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri
katika Yesu ufufuo wa wafu. Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa
kuwa imekwisha kuwa jioni. Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno
waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.Hata asubuhi wakubwa na
wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu,
na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale
waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu.Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu
gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya? Ndipo Petro, akijaa Roho
Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, kama
tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi
alivyoponywa, jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la
Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika
wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.” Petro na Yohana waliweza kushinda vikwazo
vilivyokuwa vinawakabili kwa sababu waklijaa Roho Mtakatifu, Roho wa bwana
aliwasaidia kuwa na ujasiri na kulishuhudia neno la Mungu hata kwa viongozi wa
dini waliokuwa wakaidi na waliokuwa kinyume cha Yesu na ndio maana wakati wote
Katika nyakati za kanisa la kwanza Mitume na washirika walipotaka kuchagua
viongozi moja ya sifa ilikuwa ni kujaa Roho Mtakatifu, kikwazo cha kulihubiri
neno kilipowekwa wao waliomba na Mungu Roho Mtakatifu alikuwa juu yao na
akawajaza tena na wakalihubiri neno lake kwa ujasiri ona Matendo
ya Mitume 4:23-31 “Hata walipofunguliwa, wakaenda
kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa
makuhani na wazee. Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja,
wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na
vitu vyote vilivyomo; nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu
Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari
ubatili? Wafalme wa dunia wamejipanga, Na
wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake. Maana ni
kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli,
walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia
mafuta,ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu
zamani yatokee. Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa
wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na
maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha
kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho
Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.” Kumbe basi
tunamuhitaji sana Roho Mtakatifu Msaada ulio karibu kutusaidia wakati wa
majaribu, vikwazo mtaabu na mateso pamoja na changamoto mbalimbali tunazokutana
nazo katika maisha ulimwengu hautatuweza na magumu yake yote tukimtegemea Roho
Mtakatifu na kumjaa yeye katika maisha yetu, kumbuka kuwa dhana hii ya msaada
kutoka kwa Roho wa Bwana si ya kiagano jipya tu lakini katika agano la kale
tunaona hususani katika kitabu cha waamuzi, pale Israel walipopata vipingamizi
na kutumikiswa katika nchi ya kanaani na makabila yenye nguvu Mungu aliwainua
waamuzi watu ambao aliwajaza Roho wake mtakatify na watu hao wakawa suluhu ya
matatizo ya watu wao Munda hauwezi kutosha kumpitia kila mmoja wetu lakini
angalia kwa mfanio maisha ya Samson moja ya waamuzi wakubwa sana na wa kipekee
waliofaidika na uwepo wa Roho Mtakatifu nyakati za agano la kale ona Waamuzi
13:24-25 “Basi yule mwanamke akamzaa mtoto
mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, Bwana akambarikia.
Roho ya Bwana ikaanza kumtaharakisha katika Mahane-dani, katikati ya Sora na
Eshtaoli.” kumbe Roho
Mtakatifu ndani ya maisha ya mwamini ni msaada mkubwa sana wakati wa vikwazo na
vipingamizi vya namna mbalimbali, kama unataka kufurahia maisha ya ushindi
katika ulimwengu tulio nao tumuombe sana Mungu na kuishi maisha matakatifu ili
tuwe na uhusiano ulio karibu na Mungu wetu Roho Mtakatifu, mara kadhaa tumeona
katika maisha ya waamuzi na hasa Samsoni kwamba kila alipokutana na vikwzo Roho
wa Mungu alikuja kwa nguvu juu yake na kumsaidia kushinda kikwazo Fulani mbele
yake ona kwa mfano katika
Waamuzi 14:1-5 “Samsoni
akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti.
Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke
huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe.Ndipo baba
yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu
zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti
wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana
ananipendeza sana. Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili
ni la Bwana; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti
walikuwa wakiwatawala Israeli. Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake
wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama,
mwana-simba akamngurumia. Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua
kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake;
lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya.“
Samsoni alipenda
Mwanamke wa kifilisti na akazungumza na wazazi wake lakini walijaribu kumpinga
mwisho wakakubaliana naye, Biblia inaonyesha kulikuwa na kusudi la Mungu nyuma
yake hivyo Samsoni alimtaka mwanamke huyo na walikwenda yeye na baba yake na
mama yake lakini njiani mwana simba akamuungurumia Samsoni, simba alisimama
kama kikwako kwa Samsoni lakini kwa uweza wa Roho wa Bwana Samsoni alimpasua
kama aposuavyo mwana Mbuzi, Roho wa
Bwana atatutia nguvu na kutusaidia kila tunapokutana na vikwazo dhidi yetu.
Waamuzi 15:14-16 “Alipofika
Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia
kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani
iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. Naye
akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akapiga watu elfu kwa mfupa
huo; Samsoni akasema, Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda
nimepiga watu elfu” unataka maisha ya ushindi fanya ushirika wa
kudumu na Roho Mtakatifu jaa Roho Mtakatifu!,
5.
Kumbuka
Neema
Ni muhimu
kufahamu kuwa ujumbe wa biblia nzima hususani agano jipya la bwana wetu Yesu
Kristo unahusiana na neema, ujumbe wa injili ni neema Mungu anaonyesha neema
yake kwa kumleta Yesu Kristo katika maisha yetu, ameteseka msalabani kw niaba
yetu kwa sababu sisi tusingeliweza, Mungu ametusaidia ametusaidia madhaifu
yetu, Neema ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu kwa sababu hiyo basi hakuna
tunaloweza kulifanikisha sisi wenyewe bila neema ya Mungu, 2Wakoritho 12:9 “Naye akaniambia, Neema
yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia
udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.” Unaona
neema ni nini neema ni msaada wa upendo na rehema unaotolewa na Mungu kwa
wanadamu bila wao kuwa na jambo lolote la kumshawishi, ni uependeleo pasipo
kustahili ni kuhesabika kuwa unastahili kupitia kazi ya Yesu Kristo msalabani,
Neema ndio iinayotupa kibali hata cha kusogelea uwepo wa Mungu wakati wa maombi
ona Waebrania 4:16 “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili
tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Tunapokabiliana
na changamoto zozote za maisha namna pekee ya kushinda changamoto hizo ni
kuitumainia neema ya Mungu, kumbuka kuwa kuja kwa Yesu duniani ni pamoja na
kutuletea neema ona Yohana 1:17 “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli
zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.” Tunaweza kuwa na maisha ya ajabu na upekee
mkubwa sana duniani kama tutajaa neema Luka
1:26-30 “Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa
na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira
aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake
bikira huyo ni Mariamu. Akaingia
nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Naye
akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya
namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa
Mungu.” Neema ya Mungu itaweka hofu zote mbali na wewe, neema ya
Mungu itakupa fadhili ambazo kila mmoja anazitamani, ukiwa umejaa neema
ahupaswi kuogopa, watu waliofahamu umuhimu wa neema mara kadhaa walimuomba
Mungu wakimsifu na kujumuisha katika maombi yao kwamba Mungu wetu pamioja na
mambo mengie amejaa neema Zaburi
103:8-10 “Bwana amejaa huruma na neema, Haoni
hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Yeye hatateta sikuzote, Wala hatashika
hasira yake milele. Hakututenda sawasawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa
kadiri ya maovu yetu.” Kwa msingi huo wakati tunapopitia majaribu na
changamoto za aina mbalimbali na jambo lolote lile ambalo kwalo twaliona kuwa
ni kikwazo katika maisha yetu ni vema tukakumbuka neema ya Mungu, tukikaribie
kiti chake cha rehema kwa ujarisi ili atupatie neema ya kutusaidia wakati wa
mahitaji. Yesu alifanikiwa sana katika siku zako zote za maisha yake Duniani
kwa sababu alikuwa amejaa neema ona Luka
2:40 “Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa
hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.” Unaona ili maisha yetu
yaweze kuwa na mafanikio ya kila namna tunahitaji neema neno neema katika
kiibrania ni CHEN yaani maana yake
fadhili, wema kupendelewa na kupewa thamani kubwa na Mungu, na kwa kiyunani
neno neema ni CHARIS yaani Msukumo
wa Mungu ndani yako unaona, kutokana na hali hii watu walioelewa umuhimu wa
neema katika nyakati za agano jipya neema ilikuwa ni moja ya salamu yenye
kutakiana Baraka za Mungu hebu jiombee neema kila unapokutana na changamoto na
neema hiyo itakubeba!
6.
Kumbuka
Imani
Mara kwa mara
Yesu aliwakemea sana wanafunzi wake kwa kutokuwa na imani, aliwaona kuwa
hawataweza kukabuiliana na changamoto mbalimbali kama watakosa imani na kwa
msingi huo linapokuja swala la kumuamini Mungu Yesu aliwataka wanafunzi wake
wawe na imani Mungu hana furaha na mtu anayesita sita ona Waebrania 10:38-39 “Lakini mwenye haki
wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao
walio na imani ya kutuokoa roho zetu.” Watu wote walioshinda
changamoto za aina mbalimbali duniani walikuwa watu wa imani ona Waebrania 11:32-38 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta
habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za
manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata
ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali
ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita,
walikimbiza majeshi ya wageni. Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa.
Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate
ufufuo ulio bora; wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa
mafungo, na kwa kutiwa gerezani; walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno,
walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo
na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; (watu ambao
ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na
katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.” Imani ni silaha, imani ina nguvu kubwa
sana na inatuwezesha kufanya mambo mengi na makubwa sana katika ulimwengu wa
roho ona Mathayo 21:21-22 “Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani,
msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima
huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yo yote mtakayoyaomba katika
sala mkiamini, mtapokea.” Kwa msingi huo kila mwanafunzi wa Biblia
anapaswa kuwa mtu wa imani, tukikosa imani kwa Mungu tutajikuta tunashindwa na
kusababisha aibu kubwa katika maisha yetu, kamwe tusikubali kuwa watu wasio na
imani amini Mungu ya kuwa
atakufikisha katika jambo alilolikusudia katika maisha yako, kutokuamini ni
machukizo mbele za Mungu na kunaweza kusababisha ukajikuta unaangamizwa au unakataliwa,
Imani katika Mungu na ushindi itatupatia thawabu kubwa sana na tutafanikiwa!
7.
Kumbuka
maombi.
Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbue
kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na
kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili
zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” Wote
tunafahamu kuwa Neno la Mungu limetufunza kivitendo kwamba maombi yana nguvu na
uwezo mkubwa sana wa kubadilisha mambo, kila wakati Yesu na hata mitume
walitutaka tukumbuke kuomba Petro alisema na tumtwike yeye fadhaa zetu zote
maana anajishughulisha sana na mambo yetu angalia katika 1Petro 5:6-7. “Basi nyenyekeeni chini ya
mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye
fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.” Unaona
hii maana yake ni kuwa hatupaswi kusumbuka wala kufadhaika kazi yetu ni moja
kila tunapokutana na changamoto za aina mbalimbali tukumbuke kuomba na tuingie
kwenye maombi na kuliitia jina la Mungu wetu naye atatusikia tusijali kuwa nini
kinanenwa juu yetu au tunatishiwa kwa kiwango gani sisi tukumbuke kuwa kuna
majibu katika maombi, Nabii Daniel alikuwa moja wapo ya watu waliokutana na
changamoto za aina mbalimbali katika maisha yake lakini alifahamu wazi kuwa
dawa ya kuzishinda changamoto hizo ilikuwa ni kumuomba Mungu aliye hai ona katika
Daniel
6:10-11 “Hata
Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia
nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa
kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru
mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao
wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu
wake.” Tunajifunza pia katika maisha ya mfalme Hezekia alikuwa ni
mfalme aliyemcha Mungu na kujaribu kwa kiwango Fulani kufuata njia za Daudi
katika utawakla wake alipokutana na changamoto hata za kiafya aliuelekeza uso
wake kwa Mungu bila kujali mazingira aliamini kuwa mazingira ya kuomba
yatabadili kabisa hali inayomkabili bila kujali kuwa hatari ya kufa imetangazwa
na nani ona 2Wafalme 20:1-6 “Siku hizo Hezekia akaugua,
akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia,
Bwana asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.
Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema,
Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na
kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana
sana. Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia,
kusema, Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi
baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama,
nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana. Tena, nitazizidisha siku
zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na
mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa
ajili ya Daudi, mtumishi wangu.” Maombi yana uwezo mkubwa sana
katika maisha yetu, kila aina ya dhiki, kikwazo au changamoto yoyote inaweza
kusawazishwa kwa kupitia maombi. Ni kuomba ndiko kutakakotupa ufunguo wa tatizo
letu lolote tunalolipitia, Hezekia alikuwa na uzoefu kuwa Mungu anaweza
kumponya na janga lililokuwa likimkabili, kwa sababu hata alipopata vitisho
kutoka kwa mfalme wa Ashuru aliliitia jina la Bwana kwenye maombi na Mungu
alimsikia na kuingilia kati ona 2Nyakati 32:9-22 “Na
baada ya hayo Senakeribu mfalme wa Ashuru, akatuma watumishi wake waende
Yerusalemu, (naye alikuwapo mbele ya Lakishi, na uwezo wake wote pamoja naye,)
kwa Hezekia, mfalme wa Yuda, na kwa Yuda wote waliokuwako Yerusalemu, kusema,
Senakeribu, mfalme wa Ashuru, asema hivi, Mwatumainia nini hata mkae
mkihusuriwa katika Yerusalemu? Siye Hezekia anayewashawishi, mtolewe kufa kwa
njaa na kwa kiu, akisema, Bwana, Mungu wetu, atatuokoa na mkono wa mfalme wa
Ashuru? Si yeye Hezekia huyo aliyeondoa
mahali pake pa juu, na madhabahu zake, akawaamuru Yuda na Yerusalemu, akisema,
Abuduni mbele ya madhabahu moja, na juu yake mtafukiza uvumba? Je! Ninyi hamjui
mimi na baba zangu tuliyowafanyia watu wote wa nchi? Je! Miungu ya mataifa wa
nchi iliweza kuokoa kwa lo lote nchi zao na mkono wangu? Ni yupi miongoni mwa
miungu ya mataifa wale walioharibiwa kabisa na baba zangu, aliyeweza kuwaokoa
watu wake na mkono wangu, hata Mungu wenu aweze kuwaokoa ninyi na mkono
wangu? Basi sasa asiwadanganye Hezekia,
wala asiwashawishi kwa hayo, wala msimwamini; kwa kuwa hapana mungu wa taifa lo
lote, wala wa ufalme wo wote, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, au
na mkono wa baba zangu; sembuse Mungu wenu atawaokoaje ninyi na mkono wangu? Na
watumishi wake wakazidi kusema juu ya Bwana Mungu, na juu ya Hezekia, mtumishi
wake.Tena akaandika waraka, kumtukana Bwana, Mungu wa Israeli, na kumwambia,
akisema, Kama vile miungu ya mataifa wa nchi isivyowaokoa watu wao na mkono
wangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake na mkono wangu.
Wakawalilia kwa sauti kuu, kwa lugha ya Kiyahudi, watu wa Yerusalemu
waliokuwako ukutani ili kuwaogofisha, na kuwafadhaisha; hata wapate kuutwaa
mji. Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu, kana kwamba kuitaja miungu ya mataifa wa
nchi, iliyo kazi ya mikono ya watu. Na kwa ajili ya hayo Hezekia mfalme, na
Isaya nabii, mwana wa Amozi, wakaomba, wakalia hata mbinguni. Naye Bwana
akatuma malaika aliyewakatia mbali mashujaa wote, na majemadari, na maakida,
matuoni mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake mwenye haya ya uso. Naye
alipoingia nyumbani mwa mungu wake, wale waliotoka viunoni mwake mwenyewe
wakamwangamiza humo kwa upanga. Ndivyo Bwana alivyomwokoa Hezekia, na wenyeji
wa Yerusalemu, na mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na mikononi mwa wote,
akawaongoza pande zote.” Muda hungeweza kutosha kuweza kuonyesha
nguvu ya maombi lakini shuhuda hizi chache katika maandiko na zitutoshe kuweza
kuonyesha kuwa namna pekee ya kushinda vikwazo vya aina yoyote katika ulimwengu
tulio nao ni pamoja na maombi, wakati wowowte tunapokutana na changamoto za
aina yoyote ile na tuliitie jina la Bwana naye atatuokoa narudia tena
changamoto za aina yoyote!
8. Kumbuka unyenyekevu.
Moja
ya njia ya Mungu ya kutuwezesha kushinda vikwazo na kutupatia neema ni
kukumbuka unyenyekevu, Kutembea kwa unyenyekevu kuna faida kubwa sana katika
maisha ya mwanadamu, Tatizo kubwa linaloonekana kwa watu wengi sana leo ni
kujiamini kunakopitiliza kawaida, ni ukweli ulio wazi kuwa kokosa unyenyekevu
kunaleta madhara makubwa sana kuliko unyenyekevu wenyewe, utafiti unaonyesha
kuwa watu wanyenyekevu pia wana kiwango kikubwa sana cha self control yaani
kujidhibiti, Biblia inatuelekeza na kutufundisha faida kadhaa za unyenyekevu.
a. Unyenyekevu
unaifanya neema ya Mungu kuwa kubwa kwetu Mithali
3:34 “Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali
huwapa wanyenyekevu neema.” Kinyume cha unyenyekevu ni kiburi na
tunapokuwa na kiburi na Mungu anatupinga na kuondoa neema yake kwetu
b. Mungu
huwapinga wenye kiburi ona 1Petro 5:5-6
“Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam,
ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu
huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni
chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;”
c. Kiburi
huambatana na fedhea na aibu Mithali
11:2 “Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima
hukaa na wanyenyekevu.”
d. Unyenyekevu
unakufanya uinuliwe juu sana na Mungu Wafilipi
2:6-11 “ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya
Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa
wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa
mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha
mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti
lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila
ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”
Unyenyekevu sio ujinga ni hekima Mungu atatuinua wakati wa vikwazo kama
tutakumbuka kutembea kwa unyenyekvu mbele zake na kujilinda na kiburi.
9. Kumbuka uvumilivu.
Changamoto
nyingine tunazokutana nazo duniani zinahitaji uvumilivu na subira, wakati
mwingine itatuchukua muda mrefu kusubiria kutimizwa kwa ahadi za Mungu wetu
katika maisha yetu kwa msingi huo tutajitaji uvumilivu, wengi wetu tunapenda
kuona mambo yanatokea kwa haraka katika maisha yetu lakini Mungu anazo njia
zake na mojawapo ni kututaka tutembee katika uvumilivu yako mabo mengine
hayatokei kwa haraka mpaka tuwe na subira
neno uvumilivu katika kiingereza linatumika neno Persevearence ambalo maana
yake kwa kiingereza ni doing something
despite of difficulty or delay in achieving success tunaweza kusema kwa
Kiswahili ni hali ya kuendelea kuwa na subira bila kujali muda wala ugumu wa
jambo katika kufikia mafanikio Waebrania
12:1-3 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na
wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi
ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano
yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza
imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili
msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha
Mungu.Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii
ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.”
Unaweza kuona neno la Mungu linatutaka kustahimili yaani kuvumilia wakati
wote tunapopita katika vikwazo, magumu na majaribu ya aina mbalimbali tunapaswa
kumuamini Mungu na kuendelea kuwa na subira bila kupoteza matumaini, Mungu
anamengi ambayo ametuhifadhia na ana mpango wake kwa kila mtihani tunaoupitia
na wakati mwingine kupitia magumu hayo atatokeza mema mbele yetu, Yakobo 5:10-11 “Ndugu,
watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya,
na wa uvumilivu. Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya
subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema,
mwenye huruma.”
10. Kumbuka furaha.
Mojawapo
ya kikwazo kikubwa sana cha mafanikio yetu ni kukubali kuhuzunika, huzuni
inaathiri uwezo wetu wa kufikiri, inatufanya tukate tamaa na kufikiri kuwa
mwisho umefika usikubali kutawaliwa na huzuni wakati wa changamoto
unazozipitia, maandiko yanatutaka tuwe na furaha wakati tunapopitia changamoto
za aina mbalimbali ona Yakobo 1:2-4 “Ndugu zangu,
hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na
kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.”
Endapo una adui usikubali kumuonyesha adui yako machozi, wakati wote
mtegemee Mungu na hakikisha kuwa unafuraha siku zote hili ndio agizo la neno la
Mungu Wafilipi 4:4 “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.”
11. Kumbuka Mapenzi ya Mungu.
Maisha
hayako chini ya udhibiti wetu, kwa hivyo hatupaswi kijisumbua katika jambo
lolote neno la Mungu linasema Mathayo
6:25-27 “Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie
maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si
zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya
kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa
mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye
akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? ” Hatuna
budi kujiachia katika mapenzi ya Mungu yako mambo ambayo hayako chini ya uwezo
wetu yako kwenye mikono ya Mungu hatuwezi kuyadhibiti nsisi wenyewe kwa hiyo ni
muhimu kwetu kumuachia Mungu ayashikilie na hayo ndio mapenzi yake, Mapenzi ya
Mungu ni ngumu kuyatambua wakati mwingine na hayaelezeki wala huwezi kuuliza
kwa nini lakini la msingi ni kuendelea kuamini kuwa Mungu yuko nyuma ya mambo
kutusaidia na kutiokeza mema Warumi
8:28-30 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote
Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale
walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale
aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana
wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale
aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia
haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.” Mungu anajua
makusudi na mapenzi yake kwa nini aruhusu kupitia unachokipitia yeye anajua kwa
undani zaidi, na anajua lililosahihi
pale atakapokuja kukufunulia mapenzi yake utakuja kuelewa ni kwanini aliruhusu
alichokiruhusu katika maisha yako na kwa nini Mungu alikuacha upitie hilo kwa
hivyo ni muhimu kwetu kukubali ilikuwa ni njia ya Mungu kupitia unachokipitia Mwanzo 50:15-20 “Ndugu
zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu
atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. Wakapeleka watu kwa
Yusufu, kunena, Baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake, akasema, Mwambieni
Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana
walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba
yako. Yusufu akalia waliposema naye. Nduguze wakaenda tena, wakamwangukia
miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumwa wako.Yusufu akawaambia, Msiogope, je!
Mimi ni badala ya Mungu? Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu
aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.” Angalia mapito yote ya
Yusufu na kumbuka mapito aliyoyapitia na angalia mwisho wake ilikuwa njia ya
Mungu kumfikisha hapo alipomfikisha kumbe ilikuwa ni njia ya Mungu kumleta
katika ngazi hii japo Mungu alitumia njia mbaya ya ndugu zake kumleta hapo
alipomleta.
12. Kumbuka kuto-kunungu’nika
Manung’uniko
ni moja ya tabia ambayo inafunga Baraka za Mungu, au kuzichelewesha kwetu,
Biblia inatutaka tuache kuning’unikiana sisi kwa sisi Yohana 6:43 “Basi Yesu akajibu,
akawaambia, Msinung'unike ninyi kwa ninyi.” Manunguniko yanaweza
kuleta adhabu kutoka kwa Mungu 1Wakoritho
10:10 “Wala msinung'unike, kama wengine wao
walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu.” Mungu anachukizwa sana na
Manung’uniko, manung’uniko kwa sababu manung’uniko kwake ni sawa na
a.
Kukosa
imani
b.
Kusahahu
matendo ya Mungu
c.
Hayaondoai
tatizo bali yanavunja moyo wengine
d.
Yanaleta
ushuhuda mbaya
e. Yanampa shetani nafasi ya kulaumu
Kwa
kulijua hili neno la Mungu limetuonya tuacha kabisa kunung’unika na badala yake
tumtukuze Mungu na kumshukuru kwa kila jambo, Mitume walikazia sana nyakati za
kanisa la kwanza watu waache kunung’unika manung’uniko ni dhambi
Wafilipi 2:13-15 “Kwa
maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa
kulitimiza kusudi lake jema.Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala
mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio
na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao
mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,”
Yakobo 5:9 “Ndugu,
msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya
milango.”
1Petro 4:8-11 “Zaidi
ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri
wingi wa dhambi. Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung'unika; kila mmoja
kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa
neema mbalimbali za Mungu. Mtu akisema,
na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa
na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na
uweza una yeye hata milele na milele. Amina.” Wana wa Israel mara
kwa mara walijikosesha Baraka za Mungu kwa sababu ya manung’uniko yao,
Manunguniko yanaweza kujibiwa lakini kwa kawaida yanajibiwa vibaya Hesabu 11:1-2 “Kisha
hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa Bwana; Bwana
aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa Bwana ukawaka kati yao,
ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago. Ndipo watu wakamlilia Musa; naye
Musa akamwomba Bwana, na ule moto ukakoma.”
13. Kumbuka Jina la Yesu.
1Samuel 17: 45 “Ndipo
Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na
mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi
ya Israeli uliowatukana.” Moja
ya siri kubwa sana aliyoitumia Daudi kupata ushindi dhidi ya Adui yake na wa
taifa lake ni Jina la Bwana Mungu wa majeshi, Jina hili Nyakati za agano la
kale lilikuwa limefichwa sana na lilikuwa ni siri kubwa mno, lakini katika
nyakati za agano jipya jina hili tumepewa ni jina lanye kifurushi cha wokovu ni
jina pekee linaloweza kumuokoa awaye yote atakayeliitia. Matendo 4:10-12 “ jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa
jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua
katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye
jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la
pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina
jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”Jina
la Yesu ni jina la kipekee sana na Mungu ametupa jina hili ili tuweze kulitumia
kwaajili ya utukufu wake, tunapokutana na magumu na changamoto mbali mbali liko
jina la Yesu, ni jina la pakee sana Marko
16:15-18 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini,
atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa
pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha,
hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”
Unaweza kuona Yesu mwenyewe amatuamuru kwamba kwa jina lake tunaweza kutatua
matatizo na majaribu na changamoto za aina mbalimbali, Jina lake lina nguvu, na
lina mamlaka kubwa sana ya kupambana na hali ngumu za namna yoyote, Jina hili
ni ngome ambalo tunaweza kulitumainia na tukawa Salama Mithali 18:10 “Jina la Bwana ni ngome
imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.” Kwa kuhitimisha ni
muhimu kufahamu kwamba jina la Yesu ni jina lililoinuliwa sana na lina uwezo
mkubwa na kwa sababu hiyo zungumza kwa ujasiri na kwa mamlaka kwani jina hili
ni silaha kubwa na hakuna vita utaishindwa ukilitumia jina la Yesu!
14. Kumbuka kujitenga/kujiepusha (to withdrw)
Ni
muhimu kufahamu kuwa mojawapo ya njia ya kujihami na vikwazo vya aina
mbalimbali ni pamoja na kujitenga au kujitoa au kujiepusha njia kama hii
inaweza wakati mwingine kutuletea amani na njia kama hii ilitumiwa pia na wazee
wetu Abraham na Lutu ona Mwanzo 13:2-13 “Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa
mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu. Akaendelea kusafiri kutoka kusini mpaka
Betheli, mahali pale palipokuwapo hema yake kwanza kati ya Betheli na Ai; napo
ndipo palipokuwa na madhabahu aliyofanya hapo kwanza; naye Abramu akaliitia
jina la BWANA hapo. Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na
makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema. Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae
pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja. Kukawako
ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku
zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi. Abramu akamwambia
Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya
wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu. Je! Nchi hii yote
haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto,
nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande wa kuume, nitakwenda upande wa
kushoto. Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba
lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama
bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari. Basi Lutu
akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki;
wakatengana wao kwa wao. Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa
katika miji ya lile Bonde; akajongeza hema yake mpaka Sodoma.Lakini watu wa
Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya BWANA. BWANA
akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako,
ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki
na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata
milele.” Unaweza kuona sio lazima ung’ang’ane kitu wakati mwingine
kujiepusha kunaweza kuleta suluhu ya kudumu na amani ya kudumu miongoni mwa
pande zenye migogoro, jiepushe, aidha maandiko yanatufunza namna Isaka naye
alivyokuwa mtu mwema na mwenye kujiepusha na migogoro ya mara kwa mara, akiwa
na Abimeleki, walfilistio mara kwa mara walidai kisima alichochimba Isaka ni chao wakagombania lakini yeye alijiepusha
na kuchimba kingine Mungu alimstawisha sana Mwanzo 26:16-22 “Abimeleki akamwambia
Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi.Basi Isaka akatoka
huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko.Isaka akarudi
akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye;
maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye
akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. Watumwa wa Isaka wakachimba
katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. Wachungaji wa
Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo
akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye. Wakachimba
kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. Akaondoka
huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake
Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi
katika nchi.” Tunaweza kuona kuwa
wakati mwingine kujitoa kunaweza kuwa sababu ya kuepuka migogoro na kujiondoa
katika changamoto kadhaaa kwa makusudi mema tu, Hili ni jambo la kawaida
wanapoishi watu na wakati mwingine ikatokea tofauti tunaweza kuamua kujitioa
kwa faida ya pande zote mbili na kwa kusudi la kumpa Mungu utukufu, Jambo hili
halikuwahi kutokea kwa wazee wetu tu bali hata wakati wa mitume tena wenye sifa
kubwa ona Matendo 15:36-40 “Baada ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba, Haya!
Mrejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la
Bwana, wa hali gani.Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja
nao.Bali Paulo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfilia, asiende
nao kazini. Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba
akamchukua Marko akatweka kwenda Kipro. Lakini Paulo akamchagua Sila,
akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana.” Unaona
wakati mwingine hakuna sababu ya kulazimisha mambo, Shamba la Mungu ni pan
asana ni kubwa mmno tunaweza kuamua tu ukielekea kaskazini nitaenda kusini, ili
amani iwepo na Mungu akapate kutukuzwa, hakuna sababu ya kumzunguka mtu wala
kumtesa “make them happy by your absent if your presence makes them not happy”
kama uwepo wako ni tatizo kwako wafanya wenye furaha kwa kuondoka kati yao,
aidha pia yako maeneo mengine ambayo kwayo Biblia inatuonya kujitoa ili
tusiweze kuharibu uhusiano wetu na Mungu Zaburi
1:1 “Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la
wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa
wenye mizaha.” Wakati mwingine ili kujihadhari na vikwazo na
majaribu na mapito mbalimbali njia sahihi inaweza kuwa kujitenga au kujihadhari
au kuondoka Biblia inatutaka tujihadhari na watu wasioendenda kwa utaratibu 2Wathesalonike 3:6-7 “Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo,
jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata
mapokeo mliyoyapokea kwetu. Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa
sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu;” Biblia pia imeagiza
kujitenga na watu wanaoleta mafarakano na wenye kukwaza watu Warumi 16:17 “Ndugu
zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume
cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.” Pia maandiko
yanatutaka tujihadhari na kujiepusha na watu wasiotaka kufanya suluhu wasiotaka
mapatano 2Timotheo 3:2-5 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho
kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe,
wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii
wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,wasiowapenda wa kwao, wasiotaka
kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti,
wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa
utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.” Pia
Biblia inatutaka tujiepushe na jambo lolote lile ambalo haklina faida Tito 3:9 “Lakini
maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya
sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.” Kumbe basi
kujiepusha ni mojawapo ya njia muhimu sana inayoweza kutusaidia kushinda
vikwazo vya aina mbalimbali duniani, sio kila kitu kuwa ni lazima ukabiliane
nacho vingine vinataka ujiepushe tu!
15. Kumbuka kuridhika (To be Content)
Changamoto
kubwa sana inayosumbua watu duniani ni kutokuridhika watu wengi wanasumbuliwa
na tamaa kwa sababu wanataka kuwa zaidi ya kile walichojaaliwa na Mungu, sio
vibaya kunai mambo makubwa lakini ni hatari sana kunai makuu kuliko ikupasavyo
kunia, kuwania kuwa nafasi ya kwanza sio jambo baya, kuwania kupata division
one sio jambo baya lakini kushindana na Mtu, katika maswala ya mali, fedha na
cheo ni tamaa mbaya Warumi 12:1-8 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu,
itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo
ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa
kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya
kumpendeza, na ukamilifu. Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu
aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi,
kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.” Watu wengi sana nyakati za kanisa la
kwanza walitaka kuwa kama Paulo Mtume, lakini yeye aliwaonya kuwa neema
aliyopewa yeye ni tofauti, Mungu humpa kila mmoja karama kwa kadiri ya neema
tama ya kuwa kama Fulani au kutaka kumzidi Fulani inaweza kutuletea mambo
magumu mno kwa hivyo ni muhimu kuridhikana kile ulichonacho Mungu ameahidi
kutokutuacha wala kutupungukia kwa hivyo na tumuombe yeye tuishi maisha ya
kiasi Waebrania 13:5-6 “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo
navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha
kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu
atanitenda nini? ” Kama tutaishi maisha yanayompendeza Mungu na
tukaishai maisha ya kuridhika Biblia inasema kuna faida kubwa sana kuliko watu
wanaotamkani kuwa na mali kwani wengi huangukia katika mitego ya aina
mbalimbali 1Timotheo 6:6-11 “Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. Kwa
maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;ila tukiwa na
chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. Lakini hao watakao kuwa na mali
huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye
kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la
mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo
wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. Bali wewe, mtu wa Mungu,
uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole”.
Ni
muhimu kumsihi Mungu atufundishe kuwa na kiasi, Paulo mtume alifundishwa kuwa
radhi katika hali zote hivyo hakukuwa na aina ya maisha yaliyombabaisha wako
watu wengine hufa kwa sababu ya mali zao mioyo yao iko katika hizo, lakini kama
maandiko yasemavyo hatukuja na kitu duniani wala hatutaondoka na kitu,
tukiwanacho kisitupe kiburi wala mabadiliko wala kuinua mabega na tusipokuwa
nacho tusimkufuru Mungu ona Wafilipi 4:11-13 “Si
kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali
yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo
yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na
vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
0718990796
ikamote@yahoo.com
Amina mtu wa Mungu kwa somo zuri. Ubarikiwe
JibuFutaUbarikiwe sana kwa neno zuri
JibuFutaNashukuru sana kwa hili somo nzuri saaana tena lenye kutuleteya tena faraja katika maisha ya uchristo. Mungu azidi kuwezesha katika kipawa hiki piya akupe maisha marefu.
JibuFuta