Jumapili, 25 Oktoba 2020

Na utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake !

 

Mwanzo 27:38-40 “Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.  Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia, Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako, Na penye umande wa mbingu unaotoka juu. Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.

 


Utangulizi:

Wengi wetu tutakuwa tunafahamu habari za Yakobo na Esau kwa sababu tumezisoma mara kadhaa katika Biblia na pengine tumezijadili mara kadhaa na pia kuzihubiri, kwa ujumla watu wengi sana wanaposoma kisa hiki, humsikitikia sana Esau na hata kumuona Esau kama mtu mjinga na aliyedanganywa mara kadhaa na kukandamizwa na Ndugu yake pamoja na mama yake, na tumesahahu kuwa uko upande mwingine ambao Esau ana jambo lake na linaweza kutufundisha kitu.

Kama tunavyoielewa habari hii yenye kusisimua na kusikitisha, Tunasoma kuwa Isaka anamjibu Esau alipouliza kama kuna mbaraka wowote japo mmoja umebaki kwaajili yake, Majibu anayopewa Esau hayaonyeshi kuwa amepata Baraka kwa sababu Isaka alikusudia kumwaga Baraka zote kwa Mwanaye mkubwa na bahati mbaya amebariki Baraka hizo kwa yakobo mwanaye mdogo ambaye alikuja kwa hila baada ya mpango mkakati wa Rebeka ona

Mwanzo 27:1-10 “
Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa. Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu. Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa. Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete. Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, akisema, Angalia, nimemsikia baba yako akisema na Esau, ndugu yako, akinena, Niletee mawindo, ukanifanyie chakula kitamu ili nile, na kukubariki mbele za BWANA kabla ya kufa kwangu. Basi, mwanangu, sikiliza sauti yangu kama nitakavyokuagiza. Enenda sasa kundini ukanitwalie wana-mbuzi wawili walio wema, nami nitawafanya chakula kitamu kwa baba yako, namna ile aipendayo. Kisha utampelekea baba yako, apate kula, ili akubariki kabla ya kufa kwake.

Unaweza kuona kwa njama za
Rebbeka na Yakobo waliweza kuchukua Baraka zote alizokusudiwa Esau, wakati wote wakimfanya Esau kuwa mjinga  na pamoja na baba yake hata kumbariki mtu mwingine 

Mwanzo 27:26-29 “
Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu. Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki BWANA. Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.”


Kulikuwa na tatizo kubwa sana katika familia hii, wazazi walikuwa wamegawanyika mama akiwa na Yakobo na Isaka akiwa na Esau kila mmoja alikuwa na jambo lake moyoni  Isaka alikuwa amekusudia kumbariki Esau kweli kweli na nduguye anngekuwa mtumwa wake tu, na hakukuwa na vinginevyo, Isaka anagundua kuwa amemwaga mibaraka yote kwa Yakobo wakati alikuwa ahajkusudia kumuachia yakobo chochote sasa kumbe amembariki Yakobo na jambo hili lilimpa kutetenmeka san asana Isaka lakini angefanya nini alikuwa amekwisha kutamka

Mwanzo 27:32-33 “
Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza. Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.”Lilikuwa ni tukio la kusikitisha na kutisha sana katika maisha ya Isaka na Esau na Isaka alisema japo mtu huyu amekuja kwa hila atabarikiwa  sasa ni mbaraka gani umebakia Esau alihoji kwa nguvu zake zote kuwa endapo uko mbaraka umebaki tafadhali basi baba unibariki na mimi!

Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika hingo yako!

Ndipo Isaka akatamka mbaraka huu Hebu tuuangalie vizuri Mwanzo 27:38-40 “Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.  Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia, Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako, Na penye umande wa mbingu unaotoka juu. Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.

Esau alipokea mbaraka mmoja tu lakini mbaraka huu ulikuwa na masharti, ni kweli Mungu alimuandalia penye umande na unono, lakini ili aweze kuyapata lazima afanye vita lazima apambane haitakuwa rahisi, na nduguye atamtawala lakini lazima aponyoke na kulivunja kongwa yaani nira ya utumwa na kuwa huru,  

Kongwa ni nini?

Kongwa ni neno la kiswahili lenye jina lingine liitwalo Nira, kwa kiingereza Yoke, chombo hiki huvalishwa wanyama kazi shingoni kwa kusudi la kuwatumikisha na kuwafanyisha kazi kwa lazima, Katika biblia hutumika kama alama ua utumwa, au ukoloni, chombo hiki kinapovalishwa kwa mnyama mnyama huyo hutekeleza matakwa ya Bwana wake tu na kutumikishwa kwa muda na majira na nyakati kama atakavyo bwana wake hivyo mnaya hupoteza uhuru na uwezo wa kufanya mambo yake ayatakayo, Mtu yeyote anayetaka kuwa huru katika jambno lolote linalomtumikisha bila kupenda ni lazima aponyioke na kujivua Kongwa ndipo aweze kuwa Huru! Mbaraka aliopewa Esau na baba yake ulihusisha unono na umande kutoka kwa Mungu lakini ulikuwa unahusisha nguvu zake yaani ilikuwa ili Esau awe huru kutoka kwa nduguye atumie nguvu, apigane akatae kuwa mtumwa kama nchi nyingi za afrika zilivyojipatia uhuru ni chache sana zilipata uhuru bila kumwaga damu, Esau alitamkiwa kuwa mtumwa wa Israel lakini sio milele, alitakiwa kujitetea alitakiwa kupigana alitakiwa kujichomoa na kulivunja kongwa la nduguye ili aweze kuwa huru!

Maandiko haya yalitimizwa kwani wazao wa Yakobo na Esau walikuja kuutimiza unabii huu kwa dhahiri, Wazao wa Esau ambao ndio Edomu walikuja kutawaliwa wakati wa Daudi kupitia jemadari wake Yoabu ambaye aliwatenda vibaya sana na kuwakatilia mbali na kuwapoteza wanaume wote ona  

1Wafalme 11:15-16 “
Kwa maana ikawa, Daudi alipokuwako Edomu, naye Yoabu, mkuu wa jeshi, amepanda awazike waliouawa, akiisha kumpiga kila mwanamume wa Edomu, (kwa kuwa Yoabu alikaa huko miezi sita pamoja na Israeli wote, hata alipompoteza kila mwanamume wa Edomu);”  

Kutokana ana ushindi huu wa Daudi wana wa Esau walikuwa watumwa wa Israel kwa muda Fulani  na walilipa kodi na kutawaliwa, Lakini Biblia inasema baadaye  waklikataaa na kujilipia kisasi na kutangaza uhuru wao na kujitawala ona

2Wafalme 8:20-22 “
Zamani zake, Edomu wakaasi mkononi mwa Yuda, wakajifanyia mfalme. Basi akaenda Yehoramu mpaka Sairi, na magari yake yote pamoja naye. Akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na maakida wa magari; na watu wakakimbilia hemani kwao. Hivyo Edomu wakaasi mkononi mwa Yuda hata leo. Na Libna wakaasi zamani zizo hizo.” 

Biblia inaonyesha kuwa Esau alikataa kuwa mtumwa wa Israel hata leo  na hivyo unabii wa Isaka ulitimizwa, Edomu ukawa ni utawala huru na wakawa watu hatari sana kwa
Yuda na wakati wa utawala wa Ahazi Edomu waliipiga Yuda vibaya sana na kuwachukua Mateka ona

2Nyakati 28:16-17 “
Wakati ule mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa mfalme wa Ashuru ili amsaidie. Kwa kuwa Waedomi walikuwa wamekuja tena, na kuwapiga Yuda, na kuwachukua wafungwa.”

Nisikilize mpendwa ziko haki zako na Baraka zako nyingine huwezi kuzipata hivihivi, huwezi kuzipata kwa maombi pekee huwezi kuzipata kwa kufunga na kuomba ziko Baraka zako zingine zinapatikana kwa kupambana kwa kukataa kuwa mtumwa kwa kuvunja kongwa la nduguyo kongwa ni  chombo anachovalishwa mnyama wa kazi shingoni ili kumtumikisha na kumfanya afanye kazi ngumu tena si kwa hiyari yake mwenyewe. ziko haki nyingine huwezi kuzipata mpaka uende mahakamani. Ziko haki nyingine huwezi kuzipata bila kutumia nguvu au kutumia upanga, waulize wapigania uhuru wengi kama unadhani uhuru luilikuwa jambo rahisi hata kidogo, wazunghu hawangetaka kuachia unono wa rasilimali za Afrika kirahisi au kwa maneno tu, waulize kina Keneth Kaunda, Kwame Nkuruma, Julius Nyerere, Haile Sellasie, Jomo Kenyatta, Abeid Karume, Samora Machel, Martin Luther King na wapoigania haki wa kweli kama ilikuwa rahisi kuwa huru na kuliacha kongwa la kitumwa na kikoloni? Kutokana na upole wetu na ukarimu wetu, Sfrika ilipoteza uhuru wake, rdhi nzuri zilichukuliwa, mashamba mazuri yakawa ya wazungu, Eaafrika waligeuzwa vibarua kwa ujira mdogo, mazao yaliyolimwa walilzazimishwa ya kibiashara, walilipishwa kodi na walipaswa kutumia mamlaka za kifedha za kikoloni Afrika walijikuta wamepotea uhuru wao, Ukombozi wa kweli na uhuru wa kweli ungekuja kwa kupigana tu na si vinginevyo:-

Yako mambo hata kama umeokoka vipi huwezi kuyapata bila mapambano ya dhati Kama hunielewi vizuri Rais wa  sasa wa Malawi anaweza kunielewa vizuri, Yeye alikuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Assemblies of God Malawi kwa miaka 24, kisha aliingia kwenye siasa na chama cha Malawi congress Part, aligombea urais mara kadhaa na mara ya mwisho alipambana na  chama tawala cha DPP ambao walijitangaza kuwa washindi kwa hila  na Rais Peter Mutharika aliapishwa kuwa rais wa malawi haki ikiwa imepotioshwa na uchaguzi ukiwa uimegubikwa na hila na udanganyifu wa kila aina, Askofu huyu Mstaafu haki yake aliipata mahakamani, ambapo mwaka huu 2020 uchaguzi ulipoamuriwa urudiwe na mahakama alishinda kwa asilimia 59% ya kura zote zilizopigwa na kuapishwa kuwa rais wa Malawi akiwa na miaka 65 sasa  lazarous Askofu Chakwera ni rais  wa sita wa Malawi aliyeapishwa mwaka huu june 28 2020, Inawezekana alifunga na kuomba lakini haki yake ilipatikana mahakamani!

Yako mambo mengine ni lazima upambane, yako mambo mengine hayaondoki kwa kuwa mpole yako mambo mengine hayarekebishiki kirahisi, lazima upambane , lazima uvunje kongwa la utumwa, lazima ukatae ushenzi na ujinga na dharau na ukandamizwaji, hivi ndio nchi nyingi za Afrika zilivyojikomboa haikuwa rahisi, shetani hawezi kuruhusu uhuru kwa njia rahisi, hawezi kuruhusu furaha wa njia rahisi, hawezi kuachia mateka kwa njia rahisi  lazima upambane, Isaka akamwambia Esau mwanangu unono upo na umande upo Mungu amekupa lakini wewe utakula kwa upanga  wako na nduguyo amekusudiwa kukutawala lakini ukiponyoka na kulivunja kongwa lake utakuwa huru, Ponyoka kutoka katika ukandamizwaji na maumivu na mateso tangaza uhuru wako mwenyewe  shetani asikuonee tena sio lazima ufie hapo, sio lazima ufie kwenye ndoa hiyo iliyojaaa masimango ugomvi, mikwara ubabe na kutokupatikana kwa suluhu utumwa na udhalilishaji kunyimwa tendo la ndoa, kukosa maamuzi yako, wakeo na ndugu wamekuwa na sauti kuliko wewe mwenye nyumba,  sio lazima ufie kwenye kazi hiyo iliyojaa ukandamizwaji, mateso posho ndogo kuibiwa na kuonewa na kutukanwa, wakati mwingine ili uwe na mbele njema ni lazima upambane, yako mambo ni mpaka ukasirike ndio yanawezekana !, sio lazima ufie kwenye dhehebu hilo unaweza kuanza hata huduma yako, uwezo wa kujikomboa u katika mikono yako wewe mwenyewe jikomboe wewe na ndugu zako! Sio lazima umsamehe mtu aliyedhulumu shamba lako sio kila kitu kinahusu kumuachia Mungu, vingine vinahitaji mapambano pigana weka upanga wako vunja Kongwa la utumwa utakuwa huru na uko sahihi

Wakati wa Uhuru wa zimbabwe Robert Nesta Maley aliimba maneno ya Muhimu sana kwamba wakati mwingine ni sahihi kupigana kwaajili ya Maisha yako yajayo, pata muda sikiliza  maneno yake kuhusu Zimbawe hapa naweka kiasi tu nanukuu

Every man gotta right to decide his own destiny,
And in this judgement there is no partiality.
So arm in arms, with arms, we'll fight this little struggle,
'Cause that's the only way we can overcome our little trouble.

Brother, you're right, you're right,
You're right, you're right, you're so right!
We gon' fight (we gon' fight), we'll have to fight (we gon' fight),
We gonna fight (we gon' fight), fight for our rights!

Natty Dread it in-a (Zimbabwe);
Set it up in (Zimbabwe);
Mash it up-a in-a Zimbabwe (Zimbabwe);
Africans a-liberate (Zimbabwe), yeah.

Na. Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni