1Samuel 16:23 “Ikawa, ile roho mbaya kutoka
kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono
wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.”
Utangulizi:
Moja ya maswala ya msingi sana
katika mafundisho ya Biblia ni pamoja na swala la kusifu na kuabudu, wote
tunafahamu jinsi ibada ya kusifu ilivyo na nguvu kubwa sana, na mara kwa mara
maandiko yameonyesha Muitikio wa Mungu kufanya mambo makubwa sana pale
anaposifiwa kwa njia ya nyimbo na vyombo mbalimbali kama kinanda, gitaa, ngoma
na kwa lugha ya zamani kinubi. Na ndio maana utaweza kuona kuwa kusifu kwa njia
ya vyombio na uimbaji stadi ni moja ya amri za kimaandiko na ushauri unaotolewa
na mfale Daudi ona
Zaburi 33:1-4 “Mpigieni Bwana vigelegele,
enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni Bwana kwa
kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. Mwimbieni wimbo mpya, Pigeni
kwa ustadi kwa sauti ya shangwe. Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, Na kazi yake
yote huitenda kwa uaminifu.”
Ziko sababu kadhaa kwanini
Maandiko yanashauri hivyo na daudi ni
mojawapo ya watu waliokuwa waanzilishi na watu wenye moyo mkubwa wa ujuzi wa
nguvu iliyioko katika sifa, katika maandiko kwa ujumla tunaona wazi nguvu
iliyoko katika kusifu na kuabudu, lakini sio hivyo tu kuna faida kubwa na
nyingi mno katika kumuimbia Mungu kunakoambatana na vifaa vya muziki
1.
Kusifu kunatupa njia ya kumfikia Mungu Zaburi 100:1-5 “Mfanyieni
Bwana shangwe, dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa
kuimba; Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; Kwa kuwa Bwana ndiye
mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.” Kusifu
katika ibada ndio ufunguo wa kuingia katika uwepo wa Mungu, jambo moja la
kusikitisha sana ni kuwa katika makanisa mengi watu hufikiri kuwa ibada ya sifa
ni ufunguzi tu wa ibada na kuwa sio sehemu muhimu ya ibada kwa hivyo utaweza
kuona kuwa Watumishi wengi wa Mungu na wakati mwingine hata wageni wao
hawajitokezi wakati wa sifa katika ibada na hujitiokeza baadaye sana
wanapokaribia kupanda madhabahuni kwaajili ya kuhubiri hili ni tatizo kubwa mno, Kusifu na kuabudu
si sehemu ya kumfungulia mchungaji ibada au kulainisha mioyo ya watu ili neno
la Mungu liingie vizuri ni sehemu kamili nay a muhimu sana ya ibada.
2.
Kusifu kunasambaratisha Kazi za adui Biblia inataja neno kusifu kwa mara ya kwanza mara
baada ya kuzaliwa kwa Yuda katika Mwanzo 29:35 “Akapata
mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita
jina lake Yuda; akaacha kuzaa.” Jina Yuda maana yake Sifa au Kusifu
haiajalishi utalikuta wapi jina hilo vyovyote iwavyo linamaanisha sifa,
Maandiko yanamtaja Yesu kama Simba wa kabiola la Yuda ambaye ameshinda ona
Ufunuo 5:5 “Na
mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya
Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile
muhuri zake saba.” Mara nyingi tunatembea tukiwa na hofu, dhidi ya
shetani, mawazo yako, jirani zako na tunahofu ya kuwa nini kitatokea kwetu, Adui
yetu mkuu ni Shetani yeye anatajwa katika maandiko kama simba aungurumaye ona
katika
1Petro 5: 8 “Mwe
na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye,
huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.”
Hata pamoja na
kutajwa hivyo katika maandiko ni muhimu kwetu kufahamu kuwa shetani pamoja na
majeshi yake yote hayawezi kustahimili kwa simba wa Kabila la Yuda, wakati wana
wa Israel wanataka kuichukua nchi ya kanaani na kupambana na adui zao
walimuuliza Bwana ni nani atatutangulia Mungu aliwajibu Yuda atawatangulia
mbele yenu, kinabii Mungu aklikuwa anaonyesha Sifa zikitangulia hakuna adui
atakayeweza kusimama
Waamuzi 1:1-2 “ Ikawa
baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza Bwana, wakisema, Ni
nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao? Bwana
akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake.”
Hii
inatufundisha wazi tunapokuwa na vita ya kimwili au kiroho sifa itatangulia na
itatuletea ushindi ona
2Nyakati 20:14-24 “Ndipo
Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania,
Mlawi, wa wana wa Asafu, akajiliwa na roho ya Bwana, katikati ya kusanyiko; akasema,
Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana
awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita
si yenu bali ni ya Mungu. Kesho shukeni
juu yao; tazameni, wanakwea kwa kupandia Sisi; nanyi mtawapata penye mwisho wa
bonde, mbele ya jangwa la Yerueli. Hamtahitaji
kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi,
enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa
kuwa Bwana yu pamoja nanyi. Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka
mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana. Na Walawi,
wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana,
Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana. Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje
katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama,
akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana,
Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo
mtakavyofanikiwa. Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale
watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya
jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao
walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu,
na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. Kwani wana wa Amoni na
wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao
walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu
mwenziwe. Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo
jeshi; nao, angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka.”
Kumbe kuna vita
nyingi sana ambazo wala hatukutakiwa kuzipigana kutanguliza sifa mbele ya jeshi
kunatosha, sifa ni silaha kubwa sana katika ulimwengu wa roho inafanya kazi ni
zaidi ya upanga wa adui tunapaswa tu kumuamini simba wa kabila la yuda na kujua
ya kuwa atatupa ushindi, kwa hivyo iko siri kubwa sana katika kumsifu Mungu, adui
atakimbia na kurudi nyuma na kusambaratika endapo tu tutatambua umuhimu wa
kumsifu Mungu kwa nguvu zetu zote, akili zetu zote na ujuzi ufundi na ustadi
wetu wote.
3.
Kusifu kunafungua milango ya vifungo – Matendo 16:24-26
“Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika
chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane
Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na
wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi,
hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo
vya wote vikalegezwa.” Tunaona nguvu kubwa ya sifa kwamba sifa
zinauwezo hata wa kufungua makomeo ya gereza kama ilivyokuwa hapa kwa Paulo na
Sila hii maana yake hata magereza nyingi na vifungo vingi ambavyo tumefungwa na
ibilisi, wachawi, wagananga na watu wenye jicho baya vinaachia ikiwa tu
tutamsifu Mungu, ni wazi kuwa Paulo aliijua siri hii na Daudi aliijua siri hii
na ndio maana maisha yao yote waliyaelekeza katika kumsifu Mungu siku zote
Mapepo yasalimu amri ya mpiga kinubi
Tumetambua kuwa kuna siri kubwa
sana katika kumsifu Mungu, maandiko katika agano jipya yameamuru tuimbe zaburi
pamoja na tenzi za rohoni kwa kadiri ya neema ya Mungu mioyoni mwetu ona Waefeso 5:19 “mkisemezana
kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana
mioyoni mwenu;” na Wakolosai 3:16 “Neno la
Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na
kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa
neema mioyoni mwenu.” Maandiko yanataka tuimbe kwa moyo, kuna siri
ya ajabu katika kumsifu Mungu kwa kuimba kunakoambatana na vyombo, Daudi ni mtu
wa Muhimu na wa msingi aliyekuwa na ujuzi huo, mapema sana katika ujana wake na
utoto wake alikwishakugundua siri inayokaa katika kusifu, Alikuwa na uwezo
mkubwa wa kupiga kinubi mpaka mtu aliyekuwa na mapepo, pepo waliondoka na
kumuacha hivyo mapepo yalisalimu amri ya mpiga kinubi 1Samuel 16:23 “Ikawa, ile roho mbaya kutoka
kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono
wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.”
Hii inatufundisha kuwa ingawa
Mungu alimpeleka Daudi katika kumtumikia Sauli lakini kijana huyu alikaa ikulu
na kujifunza maswala kadhaa ya uongozi, huku akiendelea kupiga kinubi ambacho
kiliondoa msongo wa mawazo kwa Sauli na kusababisha uponyaji hii ni dhahiri pia
kwetu kwamba kumbe tukimsifu Mungu na kuwa na ufahamu kuwa kuna kitu cha ziada
katika kumsifu Mungu, uweza wa Mungu tatatngulia, utafungua milango kwaajili
yetu, utamfukuza mbali adui, uatasababisha adui asambaratike lakini mapepo
yatakimbia roho mbaya zitaondoka, Daudi alikuwa mpiga kinubi hodari mno na
anakumbukwa kwa uandiahi na utunzi wa zaburi nyingi sana na hata leo ukienda Israel
utaweza kuona kuwa amejengeea sanamu yake ambayo inaoneysha wazi akiwa
nameshikilia kinubi, mapepo yasalimu amri ya mpiga kinubi, sisi nasi ni muhimu
kwetu kuwa na ujuzi na ufahamu huu na khakikisha kuwa tunamsifu Mungu na
kumpoigia vigelegele na kumuinua na kusababisha ushindi mkubwa na nguvu za giza
kutoweka hii itatokea na inaendelea kutokea kwa kila mtu anayetambua umuhimu wa
kusifu katika jina la Yesu amen.
Na. Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni