Alhamisi, 5 Agosti 2021

Kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo!


1Timotheo 4:7-8Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.”


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa kufanya mazoezi ni moja ya sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu, Mazoezi yana faida kubwa sana katika maisha haya, Mazoezi yana faida kubwa sana kwa afya zetu, Nyakati za Kanisa la kwanza wakati wa utawala wa kirumi jamii ya watu wa dunia ya wakati ule walifanya sana mazoezi, Michezo ya tamaduni za kiyunani Olympics ilikuwa imeshika kasi sana kwa hivyo watu wengi walifanya mazoezi ya aina mbalimbali, kwa sababu mbalimbali na walikuwa na afya njema, Nyakati za leo wakristo wamepuuzia sana mazoezi, aidha kwa sababu wanafikiri kuwa Biblia haizungumzii mazoezi, ama kwa sababu ya tafasiri mbaya ya Mstari wa msingi niliounukuu hapo juu! Lakini kula utakavyokula, zingatia maelekezo ya aina yoyote ile ya kiafya kama utaweka mazoezi pembeni hutaweza kuwa na afya njema, magonjwa mengi sana yameikumba dunia na watu wengi sana hata wakristo wanaumwa magonjwa ya iana mbalimbali, lakini mengine yanaweza kuepukika, kupunguzwa au hata kujikinga kama kanisa litaelewa umuhimu wa mazoezi, miili yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu, na kwa sababu hiyo Maandiko yanatuagiza kuitunza na namna mojawapo ambayo tunaweza kulitunza hekalu la Roho wa Mungu ni pamoja na kufanya mazoezi kama nitakavyofafanua kwa kina ona 1Wakoritho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

Kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo!

Kama nilivyogusia awali katika utangulizi, kwamba kumekuwa na tatizo kubwa sana la kiafya katika nyakati za leo hata kwa wateule, nchini Marekani kwa mfano watu wamekuwa na tatizo kubwa la uzito unaopitiliza, ulaji wa hovyo, usio wa kiasi na uliokosa nidhamu ikiwa ni mojawapo ya sababu zinazopelekea watu kuwa mabonge na hatimaye baadaye kumlaumu Mungu kana kwamba ndiye aliyewashikia kijiko wale Maandiko yanatuonya dhidi ya ulafi na kututaka tuwe na kiasi wakati wa kula  Mithali 23:2 “ Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi sio hivyo tu lakini ili tuweze kuwa na afya imara, na kuwa wakakamavu kama askari wema wa Yesu Kristo hatuna budi kuwa na wakati wa kufanya mazoezi, Mazoezi yana uwezo mkubwa sana wa kutuimarisha, na kutulinda na magonjwa, yako magonjwa mengi sana ambayo yanaweza kuepukika endapo tutakuwa na tabia ya kufanya mazoezi, magonjwa kama Kisukari, Kansa, Moyo, presha na hata kuondoa mawazo kunaweza kuwa mbali nasi kama tutajali afya zetu na kujihusisha kufanya mazoezi.

 Kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo!

Kuna shida fulani katika tafasiri ya maandiko ya mstari huu 1Timotheo 4:7-8Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.” Watafasiri wengi wa maandiko wamefikiri kwamba labda huenda Paulo mtume amekataza mazoezi, au ameyapuuza mazoezi HAPANA Maandiko haya hayakatazi watu kufanya mazoezi, isipokuwa Paulo mtume anataka kuonyesha kuwa kujitia nidhamu katika kuishi maisha matakatifu kunafaa zaidi kwa maisha haya nay ale ya uzima wa milele! Ilivyo ni kuwa nyakati za Kanisa la kwanza utamaduni wa Kigiriki (Wayunani) ulikuwa umeitawala sana Dunia na kuiathiri hata wakati wa utawala wa kirumi, watu walishika lugha na tamaduni za kigiriki ikiwa ni pamoja na tamaduni za michezo ya aina mbalimbali, zingatia kuwa Michezo ya Olympics ilikuwa imeshika chati ya dunia ya wakati ule, hivyo watu walishiriki michezo ya aina mbali mbali lugha kubwa ya wakati ule ilikuwa ni michezo na hata mifano ya wahubiri wa wakati huo ilitoka kwa wanamichezo ona mfano 1Wakoritho 9:24-27 “Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” Unaona Paulo mtume anatumia mifano ya wanamichezo na nidhamu kubwa waliyo nayo wanamichezo na kuifananisha na namna watu wa Mungu wanavyopaswa kujitia nidhamu ili waweze kupata taji isiyioharibika, Kwa hiyo ulikuwa ni ulimwengu uliotawalaiwa na michezo na lugha nyingi sana zilikuwa za kimichezo ikiwepo mifano hii aliyoitioa Paulo Mtume.

Kwa msingi huo ni wazi kuwa wat wa jamii ya wakati ule  walikuwa wamehamasika sana katika kujishughulisha na michezo au hata mazoezi na wengine wakijitia nidhamu kwaajili ya mazoezi, Mazoezi yalipewa kipaumbele na umuhimu sawa na kuwekwa katika kiwango kimoja na maswala kadhaa yafuatayo

1.       Kujiwekea akiba Mathayo 6:19-21 “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”

 

2.       Kutulia na kutafakari Luka 10:41-42 “Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.”

3.       Kujinyima au kujizuia 1Timotheo 5:6 “Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.”

 

4.       Kufanya kazi Yohana 6:27 “Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.”

 

 

5.       Kujipamba kwa wanawake 1Petro 3:3-6 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.”

 

6.       Kufanya Mazoezi 1Timotheo 4:7-8Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.”         

Unapotafakari Mistari hiyo hapo juu inayokazia mambo yaliyopewa kipaumbele nyakati za Biblia utaweza kuona kuwa wahudumu wa agano jipya waliyatumia mambo yaliyokuwa yamewekewa mkazo na jamii kama somo la kuwekea mkazo jambo lililo la muhimu zaidi kwaajili ya Mungu au kwaajili ya uzima wa milele, Mfano kujiwekea akiba wote tu nafahamu umuhimu wake lakini kujiandaa kwaajili ya maisha milele ni kwa muhimu zaidi kuliko akiba ya kawaida ya dunia hii ambayo ni ya kitambi tu hivyo maandiko hayajakataza kuweka akiba, kutulia miguuni pa Yesu na kumsikiliza au kutafakari ni fungu jema zaidi, kuliko kujitaabisha kwaajili yake, Yesu hakumkataza Martha kufanya kazi, lakini alifurahishwa na kusikilizwa zaidi, kuliko kutumikiwa, kujinyima kuishi maisha ya UTAWA, kutokuoa au kuolewa ni kuzuri, nidhamu wakati wa michezo kampi na kadhalika, kujinyima vyakula Fulani na kujizuai kwa aina yoyote ni kwa muhimu kama mtu anataka lakini kujizuia nafsi ni kwa muhimu zaidi, Kufanya kazi kwaajili ya kupata ridhiki au chakula ni kwa Muhimu na Yesu hazuii hali hiyo lakini kufanyia kazi uzima wa milele ni kwa Munhimu zaidi, kujipamba kwa kusuka nywele na vito vya thamani ni kwa muhimu lakini, kujipamba kwa tabia njema na kujiheshimu ni kwa muhimu zaidi kuliko mapambo yanayoharibika, kufanya mazoezi kwaajili ya afya ni kwa muhimu sana lakini kujizoeza kuishi maisha matakatifu ni kwa muhimu zaidi., kwa msingi huo Lugha ile ya kibiblia hakimumaanisha kuwa mazoezi hayafai, yanafaa kidogo, kidogo hii na maana gani yataimarisha afya zetu, tutakuwa imara, kutakuwa na afya njema lakini mazoezi haya hayazuii mtu kutwaliwa na bwana, wala hayaongezi muda wa maisha yetu duniani, kwa hiyo Lugha inayotumika hapo ni sawa na ile tu kama watu wanatoa kipaumbele kujiwekea akiba Hazina duniani basin a watoe kipaumbele kikubwa kijiwekea akiba au hazina mbinguni, andiko linamaana ya wazi kwamba lolote linalopewa kipaumbele zaidi kuliko mambo ya Mungu, iwe ni TV, iwe ni mpira, Gemu,  na vikachukua nafasi ya Mungu kwa kukosa kiasi hilo haliwezi kuwa jambo jema hata kidogo, Maandiko yanachokitaka hata kama kitu sio dhambi ni muhimu kisipewe kipaumbele kuliko maswala ya ufalme wa Mungu ambayo ndio kwa mujibu wa maandiko ni Muhimu zaidi Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Unaona ndio maana Paulo akasema yanafaa kidogo, kama michezo na mazoezi ynapewa muda mwingi na mkubwa zaidi kuliko kujisomea neno, kuomba au kushuhudia, kutembelea wagonjwa, kuhudhuria ibada, hilo ndio tatizo, kuna faida gani ya kuwa na nguvu na uimara wa kimwili kama roho zetu ni legevu?  Kwa hiyo kimsingi Paulo hajaondoa umuhimu wa Mazoezi, wala mazoezi sio dhambi na yana umuhimu mkubwa sana yatatuweka sawa kiakili, kisaikolojia, kutulinda na magonjwa na kutupa nafasi ya kumtumikia Mungu tukiwa na afya njema lakini yasichukue nafasi kubwa ya kupuuzia mambo ya Mungu, Hilo tu!

Umuhimu wa Mazoezi katika mwili wa mwanadamu:

Kuna faida kubwa nyingi sana za kufanya mazoezi, tafasiri mbaya za kimaandiko, zimewanyima sana wakristo tabia ya kufanya mazoezi kiasi ambacho sasa makanisani kuna magonjwa ambayo yangeweza kudhibitiwa tu na tabia ya kufanya mazoezi, badala ya kufanyiwa maombezi, wakati mwingine Mungu anaweza kutushangaa kwamba unamuombea mtu tatizo ambalo labda amefanya tu uzembe na angeweza kulitunza hekalu la Mungu kwa mazoezi, wakati mwingine mtu anaweza kunenepa sana kumbe sababu yake ni stresses tu,  mtu akifanya mazoezi pia anaongeza uwezo wa kujiamini,  Neema na iongezewe kwako unapozingatia umuhimu wa mazoezi:

a.       Mazoezi yanasaidia kudhibiti uzito usiokuwa wa kawaia

b.      Mazoezi yanasaidia kutukinga na magonjwa ya aina mbalimbali

Mfano:

o   Kupooza au kiharusi

o   Shinikizo la damu

o   Aina zote za kisukari

o   Kupunguza stresses yaani mgandamizo wa mawazo

o   Kutulidha dhidi ya Kansa

o   Kuimarisha misuli ya mwili na kuimarisha viungo vya uzazi

o   Kuuzuia mwili kuchoka haraka uzee 

 

c.       Mazoezi yanasaidia kuongeza nguvu na usambaaji mzuri wa hewa ya oxygen kwenye viungo vya mwili kuweka muonekano mzuri na kuumudu mwili wako vema

d.      Mazoezi yanasaidia kukupa usingizi mzuri

e.      Mazoezi yanasaidia na kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa ubora.

Kwa msingi huo watu wa Mungu, tusipouuzie mazoezi, na kufikiri kuwa wale wanaofanya mazoezi wako wmilini sana na wasiofanya ndio wako kiroho, kumbuka tu kuwa mazoezi yanapaswa kuwa na kiasi, lakini vilevile nia ya kufanya mazoezi kwa mkristo isiwe kubadilisha muonekano wa maumbile yetu bali iwe ni kwaajili ya utukufu wa Mungu, pichani ni mazoezi yanayoitwa squatting ni zoezi zuri kwa wanaume na wanawake, linaweza kufanyika hata ndani, sio lazima uende kiwanjani, linaimarisha miguu, linajenga shepu nzuri, linaimarisha via vya uzani, linakata tumbo, linajenga hips nzuri na kukutioa jasho pamoja na faida kadhaa nilizozianisha hapo juu, Mtangulize Mungu, Muombe Roho Mtakatifu, mwambie hili ni hekalu lako nataka kulitunza na sasa ninapochukua mazoezi nisaidie kufanya haya kwa utukufu wako! Kisha fanya mazoezi.

·         Na Rev. Innocent Kamote

·         Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima


·         0718990796




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni